Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

MKURUGENZI WA SOKO LA AJIRA VETA ATEMBELEA BANDA LA VETA KATIKA MAONESHO YA SABASABA

$
0
0
Umeonaa! Hivi ni kazi yangu nikimaliza najiajiri. Ndivyo anavyoelekea kusema mwanafunzi Paulina Emmanuel anayejifunza masuala ya ubunifu wa mavazi na mitindo katika chuo cha VETA Chang’ombe Dar es Salaam, akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa soko la ajira, mipango na maendeleo wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Bw. Enock Kibendela alipotembelea banda a VETA kwenye maonyesho ya SabaSaba, Dar es Salaam.
Mwanafunzi Ernest Maranya wa VETA Chang’ombe akitoa maelezo kwa wageni waliotembelea banda la VETA kwenye maonyesho ya Sabasaba Dar es Salaam akionyesha kifaa cha elimu ya mfumo wa jua na sayansi ya anga jinsi kinavyofanya kazi.
Mkufunzi wa masuala ya hoteli na Utalii katika chuo cha VETA Njiro, mkoani Arusha Theonestina Raphael akitoa maelezo kwa askari polisi waliotembelea banda la VETA kwenye maonyesho ya SabaSaba, Dar es Salaam.
Tukiongeza ufundi kidogo tutakuwa tumemaliza kazi! Ndivyo anavyoonekana kusema Mkurugenzi wa soko la ajira, mipango na maendeleo wa VETA, Bw. Enock Kibendela mwenye kofia alipokuwa akikagua bidhaa za Mamlaka hiyo kwenye maonyesho ya sabasaba, Dar es Salaam.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mrtibu wa vyuo vya ufundi stadi kanda ya Dar es Salaam Florence Kapinga na Mwenyekiti wa Kamati ya maonyesho Abdul Mollel na Afisa Uhusiano wa VETA Dorah Tesha.
Mafunzo kwa watu wenye mahitaji maalum yanatolewa hivi! Mwalimu Kintu Kilanga mwenye kofia akimueleza Mkurugenzi wa Soka la ajira, mipango na maendeleo wa VETA Bw. Enock Kibendela kuhusu mbinu wanazotumia kumfundisha mwanafunzi Range Jackson (kushoto) mwenye tatizoo la Hyperactive. Hyperactive ni tatizo ambalo linasababisha mtoto kuwa na uelewa dhaifu wa masuala mbalimbali.
Moja ya bidhaa zilizotengenezwa na Range Jackson mwanafunzi wa VETA Chang’ombe anayesoma mafunzo maalum ya uchomeaji.

Kaskazini Unguja yaongoza kwa ajali barabarani

$
0
0
Na Salum Vuai, Maelezo

WATU 52 wamepoteza maisha na wengine 332 wamejeruhiwa kutokana na ajali 175 za barabarani zilizotokea katika Mkoa wa Kaskazini Unguja kati ya Januari mwaka 2011 hadi katikati ya mwaka 2013.

Takwimu hizo zimetolewa leo na Mkuu wa Usalama Barabarani wa jeshi la Polisi mkoani humo Ali Muhsin, wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya ‘Safiri Salama’, yaliyofanyika katika viwanja vya Mahonda, Wilaya ya Kaskazini B.

Mkuu huyo alisema, ajali za barabarani ni tishio kubwa kwa watumiaji wote wa barabara, wakiwemo madereva, abiria na watembeao kwa miguu, na kwamba tahadhari kubwa inahitaji kuchukuliwa kuziepuka.

Alieleza kuwa, endapo watumiaji wa barabara hawatakuwa waangalifu, majanga ya maafa, ulemavu wa kudumu, majeraha, hasara kwa mali na uharibifu wa miundombinu, vitaendelea kuliandama taifa.

Alitaja sababu mbalimbali zinazochangia ajali hizo, kuwa ni uhaba wa miundombinu imara, ubovu wa vyombo vya moto, mabadiliko ya hali ya hewa, utendaji mbaya wa wasimamizi wa sheria za usalama barabarani na kasoro za kibinadamu.

MAMA SALMA KIKWETE NA WAKE WA MARAIS WALIOKUWA KWENYE MKUTANO WA SMART PARTNERSHIP WATEMBELEA MAONESHO

$
0
0
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiandamana na Mheshimiwa Inagosi Bulo kutoka DRC (kushoto) na Inkhosikati Lambikiza wa Swaziland na Mama Charlotte Scott wa Zambia wakiwa nje ya banda la Zanzibar mara baada ya kutembelea banda hilo.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Maendeleo Mama Salma Kikwete akiangalia bidhaa mbalimbali za aina ya shanga zilizokuwa zikionyeshwa kwenye banda la SIDO wakati walipotembelea maonesho hayo tarehe 30.6.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na wageni wake wakiangalia mashine ya kutengeneza nguo aina ya vikoi kwenye banda la SIDO wakati walipotembelea banda hilo tarehe 30.6.2013.
Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na Mke wa Makamu wa Rais wa Zambia Mama Charlotte Scott ambaye aliondoka uwanjani hapo kwenda uwanja wa ndege kuungana na mume wake kwa ajili ya safari bya kurudi nchini Zambia.

HUDUMA ZA NSSF ZAVUTIA WENGI SABASABA

$
0
0
Banda la NSSF linavyoonekana kwa nje.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya maofisa waandamizi wa NSSF katika Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Uendeshaji wa Masuala ya Kompyuta, Kassim Mwandoro akitoa ufafanuazi kuhusu huuma wanazotoa kwa watu waliotembelea banda la NSSF. 
Mapokezi
Mtoto, Suleiman Mohamed Salum (15), ambaye ni mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Ufundi Mtwara akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Amina Mbaga.
Watu mbalimbali wakipata huduma.
Maelekezo.
Ofisa wa Wakala wa Bima wa NSSF, Issac Peter akitoa maelezo ya huduma wanazotoa.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (kulia) akiwa na Ofisa Uhusiano Mwandamizi (NSSF), Theopista Muheta.
Mwanachama wa Orwinda Saccos, Rosemery Mulamula akionesha mali mpya walizoleta katika Monesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa. Saccos hiyo imeweza kushiriki maonesho hayo baada ya kupata mkopo kutoka NSSF.
Ofisa Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Salvatory Hinju (kulia), akifafanua jambo kwa mteja George Robert aliyetembelea banda la shirika hilo lililoko katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume, akitoa maelezo kwa Leonard Chacha Kitoka (kushoto) kuhusu miradi mbalimbali ya ujenzi inayofanywa na NSSF wakati mteja huyo alipotembelea banda la shirika hilo kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba. Katikati ni Mhandisi wa NSSF, John Ndazi.
Ofisa Matekelezo Sekta Binafsi wa NSSF, Ally Mkulemba akimuonesha mmiliki wa Nkoromo Blog, Bashir Nkoromo jinsi ya kujaza fomu za kujiunga Uanachama wa Hiari wa NSSF.

Article 23

Article 22

SHILOLE NA MASANJA WAHUDHURIA TAMCO FAMILY DAY DMV

$
0
0
Shilole (kati) akipata picha ya pamoja na Bwn. Idd Sandaly(kushoto) Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV na mjumbe wa kamati ya maandalizi ya sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na Tamasha la Utamaduni wa kiswahili Marekani litakalofanyika Jumamosi July 6, 2013 Capitol Heights, Maryland. Kulia ni mwenyekiti wa kamati hiyo ya maandalizi, Bwn. Baraka Daudi.
Katibu wa kamati ya maandalizi ya sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili Marekani, Bi. Asha Nyang'anyi katika picha ya pamoja na Shilole kwenye TAMCO famuly day iliyofanyika Jumapili June 30, 2013.
Halima Ali (kati) akipata picha ya pamoja na Masanja Mkandamizaji na Shilole.
Wadau wa DMV wakipata picha ya pamoja na Shilole na Masanja.
Muhtar akipata picha ya pamoja na Masanja. 
Mrs Haward katika picha ya pamoja na Masanja na Shilole.
Wadau katika picha ya pamoja na Shilole.
Mr & Mrs Sebo wakipata Ukodak moment na Shilole.

Mama Kikwete awataka watanzania kuthamini bidhaa zinazozalishwa nchini

$
0
0

Watanzania wametakiwa kujifunza kuthamini vitu vya kwao na kuona kuwa ni bora zaidi kwa kufanya hivyo hata wageni watavipenda kwani bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi hazitapandishwa thamani na watu kutoka nje. 

Mwito huo umetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kutembelea maonyesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika uwanja wa Mwalimu Nyerere uliopo barabara ya Kilwa wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.

Mama Kikwete aliambatana na Mke wa Mfalme Mswati wa Swaziland Inkhosikati Lambikiza, Mke wa Makamu wa Rais wa Zambia Mama Charlotte Scott na Mwakilishi wa Mke wa Rais Joseph Kabila wa Jamuhuri ya watu wa Congo ambaye ni Waziri wa Jinsia, Watoto na Familia Inagosi Bulo.

Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kuwa walitembelea maonyesho hayo ili kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa ndani na nje ya nchi kuanzia ngazi ya juu hadi chini.

“Tumeona bidhaa za aina mbalimbali zinazozalishwa ndani na nje ya nchi na jinsi watu wanavyoweza kubadilishana uzoefu wa biashara hakika kadri siku zinavyozidi kwenda kuna maboresho makubwa juu ya utengenezaji wa bidhaa zinazozalishwa nchini”, alisema Mama Kikwete.

Aliwashukuru wageni alioambatana nao kwa kuzipenda bidhaa zilizopo kwenye mabada ya watanzania na kuwaomba wananchi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Dar es Salaam kutembelea maonyesho hayo kwani kuona ni kujifunza.

Pia aliwapongeza na kuwashukuru wanawake kwa kazi kubwa wanazozifanya za kuzalisha bidhaa na kufanya biashara mbalimbali ambazo zimewasaidia kujiletea maendeleo yao na jamii inayowazunguka.

Imeandikwa na Anna Nkinda – Maelezo

MNEC Magesa akutana na mjumbe wa NEC ya chama tawala cha Ghana mjini Accra

$
0
0
Mjumbe wa NEC Ndg. Phares Magesa akisalimiana na Mjumbe wa NEC ya Chama tawala Cha Ghana Mhe. Mensah ambaye ni Mbunge wa Greater Accra na Waziri wa Serikali ya Ghana walipokutana katika mazungumzo binafsi mjini Accra, Ghana jana.

WATU HAWA WANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI KOKOTE WALIPO

$
0
0
Jeshi la Polisi linazo taarifa za kuaminika kuhusu watu hawa, wanaoonekana katika hizo picha hapo chini, ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vikubwa vya kihalifu hapa nchini na katika maeneo mbalimbali nje ya nchi yetu.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wote wazalendo na wenye mapenzi mema na nchi yetu, kutoa taarifa za watu hawa popote watakapoonekana katika kituo chochote cha Polisi kilicho caribú, ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye mkondo wa sheria.

Ndugu mwananchi, hata kama ni ndugu yako, usisite kutoa taarifa za watu hawa kwa sababu ni watu hatari sana. Zawadi nono itatolewa kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa watu hao.

Kwa taarifa unaweza pia kupiga Makao Makuu ya Polisi kwa kutumia simu namba 0754 78 55 57.

Imetolewa na:- 
 Advera Senso - SSP 
 Msemaji wa Jeshi la Polisi(T)

NIPO TAYARI KUUTUMIKIA UMOJA WA MATAIFA –LUTENI JENERALI MELLA

$
0
0
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akiwa na Mkuu mpya ya UNAMID Luteni Jenerali Paul Ignace Mella na kulia ni Luteni Jenerali Wynjones Mathew Kisamba Naibu Kamanda na ambaye pia alikuwa akikaimu nafasi ya Kamanda Mkuu UNAMID. Luteni Jenerali Mella na Luteni Jenerali Kisamba walikuwa hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kwa ziara ya Kikazi na mafunzo. Lt. Jenerali Mella anasema yupo tayari kulitekeleza jukumu alilokabidhiwa na Umoja wa Mataifa na kwamba uteuzi wake katika wadhifa huo ni heshima kubwa wa Tanzania, Afrika, kwake yeye binfasi na zaidi kwa JWTZ ambayo mwaka itakuwa inatimizia miaka 50 tangu kuanzishwa kwake
Mkuu Mpya wa UNAMID Luteni Jenerali Mella akiwa katika picha ya pamoja na waambata wa kijeshi kutoka nchi za Afrika na kwingineko wakati alipotambulishwa kwao katika hafla fupi iliyoandawali na Uwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa. kutoka kushoto ni Naibu Mwakilishi Balozi Ramadhan Mwinyi, Lt. Jenerali Wynjones Kisamba, Balozi Tuvako Manongi, Lt. Jenerali Paul Mella na Maj. Jenerali Ngodi Mkuu wa jeshi la kulinda amani huko Lebano (UNFIL).
Mkuu mpya wa UNAMID, Luteni Jenerali Paul Mella akibadilishana mawazo na Kanali Mike Redmond ambaye ni Mwambata Jeshi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa.
Luteni Jenerali Mella akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Uwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa mataifa, wamo pia Balozi Tuvako Manoni, na Luteni Jenerali Kisamba.

MFALUME MSWATI III WA SWAZILAND AZINDUA RASMI MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA LEO JIJINI DAR

$
0
0
Mfalume Mswati III wa Swaziland akitoa hotuba yake wakati wa Uzinduzi Rasmi wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Sabasaba, Jijini Dares Salaam(Kushoto kwa King Mswati III) ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Pinda.
Mfalume Mswati III wa Swaziland(katikati) akiwa amesimama na Meza Kuu wakiimba Wimbo wa Taifa la Swaziland leo katika Uzinduzi wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa, Jijini Dar es Salaam(wa pili kulia)ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Pinda.
Mfalume Mswati III wa Swaziland akiingia katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimayaifa tayari kwa Uzinduzi Rasmi akiwa ameongozana na Mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda.(Picha na Lucas Mboje)

Article 15

Wajasiliamali wa Safari Wezeshwa jijini Mwanza,wakabidhiwa vifaa vyao

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Mwanza,Amina Masenza(wa pili kushoto) akimkabidhi mjasiliamali Trekta(Power Tiller) na tela lake ,Shingi Jumanne wakati wa hafla ya kukabidhi ruzuku kwa wajasiliamali waliofuzu katika program ya Safari Wezeshwa iliyofanyikakwenye Uwanja wa Furahisha mwishoni mwa wiki.Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager Oscar Shelukindo na Meneja Matukio wa Kanda ya Ziwa TBL,Eric Mwayella.
Mjasiliamali,Shingi Jumanne akitoa shukrani kwa Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo wakati wa hafla ya kukabidhi ruzuku kwa wajasiliamali waliofuzu katika program ya Safari Wezeshwa iliyofanyikakwenye Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza,mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Wilaya ya Mwanza,Amina Masenza(kulia) akimkabidhi mjasiliamali Mashine na kufua umeme na ya kuranda na kuchana mbao,Simon Shija wakati wa hafla ya kukabidhi ruzuku kwa wajasiliamali waliofuzu katika program ya Safari Wezeshwa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Furahisha mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager Oscar Shelukindo.
Mkuu wa Wilaya ya Mwanza,Amina Masenza(katikati) akimkabidhi mjasiliamali Mashine ya kusaga,Depdatus Mtalemwa wakati wa hafla ya kukabidhi ruzuku kwa wajasiliamali waliofuzu katika program ya Safari Wezeshwa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Furahisha mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager Oscar Shelukindo.

MAANDALIZI YA MAPOKEZI YA OBAMA YAKAMILIKA, TASWIRA ZA IKULU ASUBUHI HII

$
0
0
Taswira mbalimbali zinazoonesha maandalizi ya mapokezi makubwa ya Rais wa Marekani Barack Obama atapowasili Ikulu jijini Dar es salaam mchana huu. Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama ilivyo kawaida yake amepita kila mahali kuangalia kwamba mambo yanaenda mswano, ikiwa ni pamoja na kusaliamiana na makundi ya wananchi wa Dar es salaam walioko katika lango kuu la Mashariki. 
Bendera zikiwa zimepangwa na kupangika katika upande wa lango kuu la Mashariki,Ikulu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaliamiana na makundi ya wananchi wa Dar es salaam walioko katika lango kuu la Mashariki.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia Kibao cha Barabara wa Barack Obama.


Mapitio ya magazeti leo

UCHOKOZI WA KING KINYA

Morogoro, Mwanza, Temeke wapata mabingwa ARS

$
0
0
Kiungo wa timu ya Garden, Juma Masoud (kulia) akiwania mpira na beki wa Mapambano, Said Ally katika mchezo wa fainali mashindano ya Vijana U-17 Airtel Rising Stars,kwenye Uwanja wa Tualipo Dar es Salaam,Garden waliibuka mabingwa wa Mkoa ya Temeke kwa ushindi wa goli 4-1.
Mshambuliaji wa timu ya Garden, Roma David (kulia) akiwania mpira na mshambuliaji wa Mapambano, Jacobo Widon katika mchezo wa fainali mashindano ya Vijana U-17 Airtel Rising Stars, kwenye Uwanja wa Tualipo Dar es Salaam, Garden waliibuka mabingwa wa Mkoa wa Temeke kwa ushindi wa goli 4-1.
Alliance Schools Academy ikiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabithiwa kombe na kuibuka washindi wa Airtel Rising stars katika mkoa wa Mwanza.

Mashindano ya vijana chini ya umri wa mika 17 ya Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa yamefikia tamati mwishoni mwa wiki kwa timu za Moro Kids, Alliance Schools Academy na Garden kutangazwa mabingwa katika mikoa ya Morogoro, Mwanza na Temeke.

Moro Kids imetwaa uchampioni baada ya kujikusanyia pointi nne sawa na wapinzani wao wakubwa timu ya Techfort lakini Moro Kids wakatangazwa washindi kwa kuwa na magoli mengi ya kufunga. Techfort walihitimisha michuano hiyo kwa kuifunga timu dhaifu ya Anglikana 2-1 katika uwanja wa shule ya sekondari Morogoro. Magoli yao yalipatikana kupitia kwa washambuliaji Alobogast Mtalemwa na Octatus Lupekenya wakati Anglikana walifunga goli lao pekee kupitia kwa Kessy Khamis.

Hadithi ya mkoani Morogoro vile vile ilitokea huko jijini Mwanza ambapo timu ya Mwanza Alliance Schools Academy ilimemaliza ligi ikiwa na pointi nne sawa na timu ya Marsh Athletical lakini Alliance wakanyakuwa ubingwa wa mkoa kwa kuwa na magoli mengi ya kufunga.

Katika mchezo wa kufunga dimba uliopigwa kwenye uwanja mkongwa wa Nyamagana Ijumaa jioni, Alliance Schools Academy na Marsh Athletical walipambana vikali katika mchezo uliovuta hisia za watazamaji wengi ambapo wachezaji wa pande zote mbili walionyesha vipaji vya hali ya juu ya kusakata kabumbu.

Mchezo mwingine wa kufunga dimba ulipigwa katika uwanja wa Twalipo katika mkoa wa kisoka wa Temeke jijini Dar es Salaam, ambapo timu ya Garden wallibukwa mabingwa baada ya kuiadhibu bila huruma timu ya Mapambano 4-1. Washindi walipata magoli yao kupitia kwa Badili Salum, Bona David, Juma Masudi na Said Mohamed wakati Mapambano walipaga goli lao la kufutia machozi kupitia kwa Said Hassan.

Wakati huo huo, chama cha soka mkoa wa Morogoro kimetangaza kikosi chake kitakacho uwakilisha mkoa huo katika fainali za taifa za Airtel Rising Stars zinazotarajiwa kuanza kutimua vumbi katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 2 hadi Julai 7.

Kikosi chao kinajumuisha washambuliaji mapacha Evance na Robert Roshan. Wengine ni Fadhili Kamwenda, Juma Shaban, Boniface Myowela, Majid Musisi, Ramadhani Kondo, Rotan Nkamwa, Dickson Mwesa, Alphonce Lukani, Octatus Lupekenya, George Chota, Salum Kiibwa, Shafii Ngesa na Petro Mgaya.

Mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya taifa mwaka huu yanashirikisha timu za wasichana na wavulana kutoka mikoa tisa – Kinondoni, Ilala, na Temeke itakayoleta timu za wasichana na wavulana wakati Tanga, Kigoma na Ruvuma zitashirikisha wasichana pekee huku mikoa ya Morogoro, Mwanza na Mbeya ikiwa na timu za wavulana tu.

Maandalizi kwa ajili ya mtanange huo wa taifa yamekamilika na timu kutoka mikoani zinatarajiwa kuanza kuwasili jijini Dar es Salaam mwishoni wa wiki tayari kwa mashindano hayo. Fainali za ARS Taifa vile vile zilifanyika katika uwanja huo mwaka jana ambapo Temeke waliibuka washindi.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UGONJWA WA HOMA YA DENGUE “DENGUEFEVER”

RAIS BARACK OBAMA AWASILI NCHINI MCHANA HUU

$
0
0
 Rais Barack Obama wa nchini Marekani na Mkewe Michelle Obama wakiwa sambamba na watoto zao,wakiwasili chana huu kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,jijini Dar es Salaam mchana huu kwa ziara ya siku mbili hapa nchini.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Barrack Obama wa Marekani muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mchana wa leo. Kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Barrack Obama wa Marekani muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana.nyuma ya Rais na mgeni wake ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mke wa Rais wa Marekani Mama Michelle Obama.
Rais Barrack Obama akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ).
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa Marekani Rais wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana.Huku Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama Wakiangalia.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa Marekani makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi muda mfupi baada ya Rais huyo wa Marekani kuwasili nchini kwa Ziara ya kikazi ya siku mbili.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa Marekani makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi muda mfupi baada ya Rais huyo wa Marekani kuwasili nchini kwa Ziara ya kikazi ya siku mbili.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange akisalimiana na Rais Barrack Obama katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
RaisDkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwaongoza wageni wao Rais Barrack Obama wa Marekani na mkewe Michelle kuangalia ngoma mbalimbali za utamaduni muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere kwa ziara ya siku mbili nchini.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Barrack Obama wa Marekani wakifurahia na kufuata mapigo ya ngoma za utamaduni katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu jijini Dar es Salaam leo mchana wakati wa mapokezi ya kiongozi huyo wa Marekani na ujumbe wake.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akiwatambulisha baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali kwa Rais Barrack Obama na mkewe katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Picha na Freddy Maro,Ikulu.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images