Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

Ripoti Maalum kutoka kwa Mwanakijiji: Watanzania Wasikwazike na Kufedheheka kwa Ulinzi Mkali wa Obama

0
0
 Ulinzi mkali ambao tayari upo na utazidi kuonekana wakati wa Ujio wa Rais wa Marekani umewafanya baadhi ya Watanzania kujihisi wanadunishwa au kuabishwa. Wapo wengine ambao wanaona kuwa hatua mbalimbali za kiusalama zinazochukuliwa kumlinda Obama, Familia yake na ujumbe wake zinaonesha dharau na kutoaminiwa kwa vyombo vyetu vya ulinzi. Wengine wanafika mahali pa kuhisi kuwa Wamarekani wanatudharau sana kiasi kwamba wanatuchagulia nani aonene na Obama (rejea taarifa kwenye gazeti la Mwananchi la leo). Watanzania hawapaswi kujisikia hivyo hata kidogo.
Ulinzi wa Obama ni Mkali iwe ndani ya Marekani au Nje
Wakati wowote Rais wa Marekani anaposafiri iwe ndani ya Marekani au nje ya Marekani ulinzi wake ni mkali na karibu kamili (almost absolute). Kuanzia angalia ambalo anakuwepo (linakuwa no fly zone) na kuwa anaenda na kila kitu kinachoweza kutumika wakati wowote wa dharura yoyote inayoweza kufikirika kutokea. Kuanzia majanga ya moto, maji, maandamano ya kisiasa au hata mapinduzi ya kijeshi ulinzi wa Rais wa Marekani umejiandaa.
Mfano mzuri ni kuwa ikulu ya Rais pale DC – Jumba Jeupe – juu kabisa kuna mzinga wa kutungua ndege – surface to air battery. Lakini kubwa zaidi ni kuwa anga lote linalozunguka Ikulu hiyo ni eneo ambalo ndege haziruhusiwi kuruka (prohibited airspace). Na wakati wowote Rais anaposafiri mahali popote ndege haziruhusiwi kuruka juu yake. Anapotua kwenye uwanja kwa mfano hapa Detroit, hakuna ndege nyingine itakuwa inatua wakati huo huo! Sasa kama hili linatokea Marekani kwa kiasi gani linaweza kutokea Tanzania?
Ripoti hii maalum basi ina lengo la kuwasaidia Watanzania kutokwazika na kiasi cha ulinzi ambao Obama anakuja nao pamoja na usumbufu unaotokana na hilo. Kama msafara wa Rais Kikwete huwa unazusha usumbufu kwa watu basi wa Obama utasababisha kadhia – chukua msafara wa Kikwete zidisha mara 1000!
TEMBELEA LIBENEKE LA MWANAKIJIJI KWA KUSOMA ZAIDI

Libeneke jipya la Mkongwe Jhikoman

0
0
Mwanamuziki wa Reggae nchini Jhikoman afungua mtandao wake www.jhikoman.com mtandao ambao unaweza kusikiliza nyimbo na kusoma mambo mbali mbali ya Jhikoman and Afrikabisa band. Wadau msikose kumpa shavu mtoto wenu Jhikoman Manyika at www.jhikoman.com 

TAARIFA YA MSIBA

0
0
KWA NIABA YA FAMILIA YA NTAMUBANO WA MUGOMA NGARA,
TUNATANGAZA KIFO CHA MAMA YETU MPENDWA
 
 

ANNA GWITABA NTAMUBANO

KILICHOTOKEA  JUMAMOSI DAR ES SALAAM, MSIBA UKO NYUMBANI KWAKE SINZA MUGABE KARIBIA NA CITY STYLE HOTEL.

HABARI ZAIDI KIHUSU MAZISHI ZITAFUATA.

KWA MAELEZO KUHUSU MSIBA HUU WASILIANA

 NA

FLORENCE SSEBUYOYA
+255 786 460 322.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA,.. JINA LAKE LIABUDIWE.

IMETOLEWA NA

FRED ZG SSEBUYOYA.

Welcoming Ramadhan Conference​- 1434

0
0
Dear Brothers & Sisters in Islam,
Peace and Blessing of Allah be with you, Alhamdulillah , all is set for another Welcoming Ramadhan Conference. Like the people in the Government busy preparing welcoming Visitor  US President Baraka Obama, The TAMPRO Welcoming Ramadhan organising Committee is busy ensuring we appropriately prepare welcoming our holy visitor, the Holy Month of Ramadhan 1434 on Sunday of July 07th, 2013 In shaa Allah.
• The Venue is Accomodating 400 people only with the Prayer Space, that is we have limited sits that are not exceeding 80 as of July 29th, 2013.
• The 1434 Muslim Community awards have been organised in better improved version into the following groups: ◦ Islamic Education Impact Award: ◦ Islamic Books & Research Writing Award: ◦ Islamic Media Award: ◦ Islamic Women Role Model Award ◦ Islamic Scholars (Sheikh, Imam, Ustaadh) Award
• The names to present the above mentioned groups has been approved where each nominee will be awarded Trophy, Certificate and TZS 500,000. Hopeful more improvement in the future in shaa allah. • • The communication language will be in Swahili (80%) while the rest can be Arabic & or English,
• The theme is “WOMEN, the power behind Community Prosperity” To show case how Islam embrace women in a Qur'anic & prophetic ways. This has nothing to do with World first ladies & Popular Females Meeting and our theme was set back during last year (1433) WRC after opinions from female participants, but we are lucky it collided with what is happening to first ladies.
• We will have some english video from the International Speakers like Dr. Bilal Philips, Dr. Abdullah Hakim Quick, Dr. Zakir Naik, Sheikh Khaled Yasin, Imam Siraj Wahhaj, Sheikh Abdul Rahim Green and many morethat if you come with your storage divice can get them FREE to boost your Iman in shaa allah We did our best to invite most major islamic organizations and Muslims Professionals regardless of their status through various media. Get your ticket soon, be there
May allah bless you in all that you are doing in the service of
Ummah-Alwaahumma Amiyn.
Wabillaah tawfiiq.
+255 715 670 714 / +255 789 100 000

Mazishi ya Marehemu Mzee Constantine Munishi Kyara mjini Moshi

0
0
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa Marehemu Mzee Constantine Munishi Kyara wakitoa heshima za mwisho kwenye ibada ya mazishi iliyofanyika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro adre wa Kanisa Katoliki Parokia ya Moshi Mjini, akiongoza ibada ya mazishi ya Marehemu Mzee Constantine Munishi Kyara iliyofanyika eneo la Rau, nje kidogo ya mji wa Moshi, Kilimanjaro juziIbada ya mazishi ikiendelea. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Article 17

WAZIRI CHIKAWE AKIKABIDHI CHETI KWA WAHITIMU

0
0
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, akimkabidhi Stashahada mmoja wa wahitimu wa Shule ya Biashara ya Aseki iliyoko Dodoma, ambapo jumla ya wahitimu 158 walihitimu kwa ngazi ya Stashahada na Astashahada.

TFDA JOB VACANCIES,POST 26 JUNE 2013.!


TAARIFA YA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA SEKRETARIETI YA MKOA WA DODOMA

0
0
Sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma mwishoni mwa wiki ilifanya kikao cha pili cha baraza la wafanyakazi wake ambapo kwa mujibu wa katibu wa baraza hilo Ndugu Paul Masanja wajumbe wa baraza hilo ni pamoja na wawakilishi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Ofisi zote za Wakuu wa Wilaya Mkoa wa Dodoma, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na Uongozi wa chama cha wafanyakazi wa serikali kuu na Afya TUGHE Mkoa.

Masuala muhimu katika kikao hiko cha baraza la wafanyakazi yalijumuisha Nafasi ya vyama vya wafanyakazi ndani ya baraza hilo, masuala ya mafao kwa watumishi wa Umma. Vilevile mapitio ya bajeti ya mwaka 2012/13, bajeti ijayo ya 2013/14 na kupitia mtiririko wa bajeti kwa kipindi cha kuanzia 2009/10 hadi 2013/14.

Mgeni rasmi katika kikao hiko alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi ambapo miongoni mwa masuala aliyoyapa msisitizo katika salamu zake za ufunguzi wa kikao hiko ni pamoja na yafuatayo:


·        Sera ya “Tenda kwa matokeo makubwa sasa” (Big Result Now). Dr. Nchimbi aliwataka watumishi wa umma kwa nafasi zao kwenye ofisi za serikali na shughuli mbalimbali lazima wajiwekee vipaumbele vya majukumu yao na kuweka mkakati mzuri wa utekelezaji utakaoleta ufanisi mkubwa na kasha kuweka utaratibu wa kupima matokeo ya utendaji.

Alifafanua kuwa lazima wafanyakazi waweke vipaumbele vinavyolenga kuleta mabadiliko makubwa katika kutatua kero na changamoto za wananchi mfano kwenye sekta ya utunzaji kumbukumbu/masijala, Afya na sekta zingine za huduma na uzalishaji.


·        Dr. Nchimbi aliwataka watumishi/wafanyakazi hususani wataalamu wa kilimo kujadili na kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa tatizo la muda mrefu la upungufu wa uzalishaji wa chakula ndani ya mkoa unaoleta tatizo la upungufu wa chakula mara kwa mara mkoani Dodoma ukilinganisha na mahitaji ya chakula yaliyopo kwa hivi sasa.


·        Vilevile aligusia tatizo/changamoto ya Mkoa wa Dodoma kuwa na matokeo yasiyoridhisha katika sekta ya elimu hususani ngazi ya msingi na sekondari. Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa Dr. Nchimbi, wafanyakazi wanaujuzi na utaalamu katika nyanja mbalimbali kulingana na mahitaji hivyo hawana budi kutumia utaalamu na ujuzi wao wote kusaidia Mkoa wa Dodoma kuondokana na tatizo lao la kufanya vibaya kwenye sekta ya elimu.


·        Msisitizo mwingine uliwekwa kwenye suala la kuboresha hali ya makazi ya wananchi/ujenzi wa nyumba bora za makazi za wananchi na uondoshaji wa Tembe. Wataalamu wawasaidie wananchi kuboresha shughuli zao za uzalishaji na kujiwekea utaratibu wa kufanya mavuno kwenye shughuli zao hususani kuvuna mifugo na mazao na kuwekeza kwenye kuboresha makazi yao kuanzia ngazi za vijijini hadi mijini.

  
·        Dr. Nchimbi aliwatahadharisha watumishi wa Umma wenye tabia ya kuhujumu serikali wawe makini, aidha alikemea mahubiri hasa ya siasa yenye  viashiria vya uvunjifu wa amani, utulivu na mshikamano, vurugu na umwagaji damu; aliwaasa watumishi/wafanyakazi wasikubali kujihusisha na suala hili. Badala yake watumishi wa umma wanatakiwa kuzingatia maadili mema ya kazi zao, kuzingatia taratibu, kanuni na sheria ili kuboresha utoaji wa huduma katika sekta zote.

·        Vilevile Dr. Nchimbi aliwasisitiza wafanyakazi waone umuhimu wa kijiendeleza kielimu ili kuzidi kuboresha utoaji wa huduma zao na utendaji wao kwa ujumla. Aliwataka wafanyakazi watumie fursa zilizopo kama vile vyuo kujiendeleza. Aliwaagiza waajiri (Katibu Tawala Mkoa) kutoa kipaumbele cha ruhusa kwa ya kusoma kwa watumishi wa serikali wanaotaka kujiendeleza kielimu kupitia chuo kikuu huria cha Tanzania tawi la Dodoma kwa kuwa hawaaribu ratiba ya kazi kwani wanaweza kusoma huku wanafanya kazi kuitumikia serikali.


Alikemea tabia ya watumishi/wafanyakazi wasiopenda kujiendeleza kielimu kwa kubakia kwenye daraja moja la elimu kwa muda mrefu bila kujiendeleza na kusema kuwa inazorotesha utendaji na ufanisi.


Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza hilo la wafanyakazi wa sekretarieti ya Mkao wa Dodoma  ambaye pia ni Katibu Tawala wa Mkoa Dodoma Ndugu Rehema Madenge alitoa Rai kwa wafanyakazi wa serikali wawe na desturi ya kubadilika kuanzia sasa na kusisitiza alichokieleza mkuu wa mkoa hususani sera ya Tenda kwa Matokeo Makubwa Sasa (Big Result Now).


Imetolewa na:

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma


Idara ya Habari

Mshindi wa Cheka Nao Akabidhiwa Kitita Chake-Morogoro

0
0
 Mshindi wa droo kubwa ya Promosheni ya Cheka Nao Bw.Mkude Iddi, mkazi wa Morogoro, (kushoto) akioneshwa ujumbe wa M-Pesa wenye  Tsh milioni 2 na Meneja Mauzo wa Vodacom Kanda ya Morogoro, Kamanda Kasapila, alizotumiwa kwa kushinda katika promosheni hiyo inayoendeshwa na Vodacom Tanzania. Mshindi huyo ni kati ya washindi 5 waliojishindia shilingi Milioni 2 kila mmoja kwenye Promosheni hiyo  inayowawezesha  wateja kuongea na mitandao yote kwa bei nafuu. Ili kujiunga wateja wanatakiwa kupiga *149*01#.
Meneje Mauzo wa Vodacom Tanzania Kanda ya Morogoro, Bw. Kamanda Kasapila (kushoto) akimshuhudia mshindi wa droo kubwa ya Promosheni ya Cheka Nao, Bw.Mkude Iddi, akisaini baada ya kutoa fedha zake kwa njia ya M-Pesa alizotumiwa baada ya kushinda katika promosheni hiyo. Mshindi huyo ni kati ya washindi 5 waliojishindia shilingi Milioni 2 kila mmoja kwenye Promosheni hiyo  inayowawezesha wateja kuongea na mitandao yote kwa bei nafuu. Ili kujiunga wateja wanatakiwa kupiga *149*01#.
 Mshindi wa droo kubwa ya Promosheni ya Cheka Nao Bw.Mkude Iddi, mkazi wa Morogoro (kulia) akihesabu fedha zake baada ya kukabidhiwa na Mejena Mauzo wa Vodacom Tanzania Kanda ya Morogoro, Bw. Kamanda Kasapila. Mshindi huyo ni kati ya washindi 5 waliojishindia shilingi Milioni 2 kila mmoja kwenye Promosheni hiyo  inayowawezesha  wateja kuongea na mitandao yote kwa bei nafuu. Ili kujiunga wateja wanatakiwa kupiga *149*01#.


Baadhi ya waandishi wa habari wakimfanyia mahojiano mshindi wa droo kubwa ya promosheni ya Cheka Nao Bw.Mkude Iddi, mkazi wa Morogoro (kulia) baada ya kukabodhiwa shilingi milioni mbili alizojishindia kupitia promosheni ya Cheka Nao hiyo  inayowawezesha  wateja kuongea na mitandao yote kwa bei nafuu. Ili kujiunga wateja wanatakiwa kupiga *149*01#.

wapiganaji walipokutana na mpiganaji mwenzao..!

0
0
Wapiganaji walipokutana na mpiganaji mwenzao hivi karibuni katika harakati za kusaka taswira,pichani kulia ni Bashir Nkoromo na kushoto ni Richard Mwaikenda (na pichani kati ni Mwanadada mpiganaji akiwa ameshikiria makini kifaa chake cha kazi,la ajabu hakutaka jina lake lijulikane),lakini alionekana kivutio kikubwa katika utafutaji wa taswira za tukio husika (Picha na Mdau.).

Global 2013 Smart Partnership Dialogue

Spika wa Bunge la Oman na Ujumbe wake watembelea Hifadhi ya Ngorongoro

0
0
Naibu Waziri wa Maliasiri na Utalii Mhe. Lazaro Nyarandu akimpatia briefing Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheihk Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maalawi kabla ya kuanza kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro leo.
Mhe. Nyarandu akimuongoza Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheihk Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maalawi kuingia lango kuu la Hifadhi ya Ngorongoro leo.
Naibu Waziri wa Maliasiri na Utalii Mhe. Lazaro Nyarandu akiongea na waandishi kuhusu ugeni wa Bunge la Oman uliongozwa na Spika wa Bunge lao Mhe. Sheihk Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maalawi (kushoto) kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro leo.
Msafara wa Magari yaliobeba ugeni huo kutoka Bunge la Oman ukiwa Ngorongoro.
Mhe. Spika akipata Taswirazz Mbungani.

President Kikwete Hosted Smartpartner Dinner

0
0
The Host patron and adviser to the Global 2013 Smart Partners Dr.Jakaya Mrisho Kikwete presents Commonwealth Partnership for Technology and Management(CPTM) Companion award to Sir Martin Laing (Malta) during a dinner he hosted for Smart partner participants held at Mwalim Nyerere International Conference Centre in Dar es Salaam yesterday evening.
President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete presents CPTM Award to Sir.Charles Masefield UK yesterday evening during the Smart partnership Dinner hosted for participants in Dar es Salaam yesterday evening.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete pose for a photograph with the recipients of Commonwealth Partnership for Technology and management(CPTM) awards.On the lest is Sir.Martin Laing of Malta and on the right is Sir.Charles Masefield United Kingdom.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and his guest King Mswati III of Swaziland admire a lion trophy on display at Mwalimu Nyerere conference Centre yesterday during a dinner hosted for participants to Smart Partnership International Dialogue held at Mwalimu Nyerere International Conference Centre in Dar es Salaam yesterday evening.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete gives description of a lion trophy to Malaysian Prime Minister Najib Razak (second left) and King Mswati III of Swaziland at Mwalimu Nyerere Conference Centre during a dinner he hosted to the participants of of Smart Partnership International Dialogue yesterday evening.(photos by Freddy Maro).

Minister Membe bids farewell to former Prime Minister of Malaysia

0
0
Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation receives Tun Dr Mahathir Mohamad, former Prime Minister of Malaysia, who is also a Commonwealth Partnership for Technology Management (CPTM) Fellow Emeritus and Companion.  Tun Dr. Mohamad has cooperated with a number of African leaders to articulate the aims of the movement in achieving national visions, inclusivity through financial inclusion, quality and standards as well as innovation.   

Tun Dr. Mohamad is received by Mr. Omary Mjenga, Assistant Director of the Department of Asia and Australasia in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation. 
Hon. Minister Membe (2nd left), walks former Prime Minister of Malaysia Dr. Mahathir Mohamad to the VIP Room at the Julius Nyerere International Airport in Dar es Salaam.   Dr. Mohamad has been participating in the 2013 Global Smart Partnership Dialogue held from June 28, 2013 at the Mwalimu Nyerere Convention Centre in Dar es Salaam.


Vacancy Announcement 2013/14

WADAU WA ZAO LA ZABIBU MKOA WA DODOMA WAZUNGUMZIA UMUHIMU WA ZAO HILO

0
0
Wakulima wa zabibu Mkoani Dodoma wametakiwa kutambua kuwa zao la zabibu lina thamani ya kimataifa na siyo ya kimkoa wala kitaifa na hivyo bei yake inatakiwa kuwa ya kimataifa kulingana na masoko ya kimataifa.

Wakulima hao wameshauriwa wasikubali mtu yeyote awapangie bei ya zabibu kimkoa au kitaifa kwa kuwa bei ya zabibu ya hapa nchini inatakiwa kushabihiana na kushindana na bei ya zabibu inayolimwa na kuuzwa kwenye nchi nyingine Duniani kama vile Afrika kusini na Italia.

Ushauri huu ulitolewa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi alipokuwa akifungua kikao cha wadau wa zao la zabibu kilichofanyika mjini Dodoma ambapo kiliwajumuisha wakulima wa zabibu kutoka vijiji vinavyolima zabibu hapa Mkoani Dodoma.

Wadau wengine walikuwa umoja wa wafanyabiashara, wakulima na wenyeviwanda TCCIA, Bank ya NMB, Wataalamu wa masuala ya Ushirika kutoka Idara ya Ushirika na Maafisa kilimo wa Wilaya zinazolima zabibu.

Ushauri huo umetolewa kufuatia kuwepo kwa malalamiko ya wakulima kuonewa, kunyanyaswa na kuhujumiwa hasa kwenye soko la zabibu na baadhi ya wanunuzi kwa bei isiyolingana na hadhi ya kimataifa ya zao la zabibu wakati wanunuzi wenyewe wanauza zabibu hizo kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi kwa bei kubwa hadi kufikia zaidi ya mara sita ya bei wanayonunua kwa wakulima.

Dr. Nchimbi alifafanua kuwa kwa Mkoa wa Dodoma, zao la zabibu ni mojawapo kati ya mazao ya msingi, nguzo na mhimili kwa maendeleo ya Mkoa na Taifa, hivyo ni lazima lilindwe kwa masoko na bei za uhakika. Wataalamu wasaidie kutengenezwa na kupatikana kwa bei na masoko hayo. Vilevile Dr. Nchimbi aliwaagiza Halmashauri za Wilaya Mkoani Dodoma na CDA kuhakikisha wanakuwa na mpango kabambe wa miradi na mashamba ya zabibu na kuhakikisha wanayatolea hati miliki.

Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa wakulima wa zabibu Mkoa wa Dodoma (DOGCO Ltd) ndugu Omary Ramadhani alisema kwa sasa umoja huo unaundwa na AMCOS sita na bado wakulima kwenye vyama vyao vya msingi wanaendelea kujiunga.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa Agenda za Msingi zilizopo mezani kwa DOGCO ltd kwa sasa ni pamoja na uanzishaji wa kiwanda cha kuongeza thamani ya zao la zabibu na kusindika mchuzi wa zabibu na tayari wameshafanya mazungumzo na na Benki ya Uwekezaji TIB.

Vilevile ni pamoja na kujadili juu ya upatikanaji wa bei elekezi ya zabibu kitaifa ambayo wanapendekeza serikali itangaze bei hiyo kama ilivyo bei ya mazao mengine kama kahawa, chai, korosho, pamba na tumbaku.

British Council yatoa mafunzo ya uongozi na biashara kwa viongozi wa taasisi za sanaa na sanaa za maonesho

0
0
 Washiriki katika mafunzo ya uongozi na biashara yananofanyika kwenye Ukumbi wa Nafasi Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mafunzo hayo, washiriki hao wametoka katika taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na sanaa na sanaa za maonesho.
Mafunzo haya yanatolewa na Britishi Council, na mwezeshaji ni Faisal Kiwewa kutoka shirika la Bayimba la nchini Uganda.

Kili Music Tour 2013 ilivyofana ndani ya jijini Tanga

0
0
 Msanii wa Muziki wa Hip Hop,Roma Mkatoliki akipanga na kupangua vina vyake wakati wa Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika usiku wa Kuamkia leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani,jijini Tanga.
 Mkali wa Hip Hop,Prof. Jay a.k.a a.ka The Heavy Weight  MC akikamua vilivyo mbele ya Wakazi lukuki waliofika kwenye viwanja vya Mkwakwani kuona Onyesho la Muziki linaloongozwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia yake ya Kilimanjaro maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013.
Mwana FA a.k.a Binamu akiimba wimbo wake wa Yalaiti na Mwanadada aliepanda jukwaani kuimba badala ya Msanii alieimba nae wimbo huo.

Binamu akikamua huku shangwe zikitawala.
Msanii wa Muziki wa Taratibu,Maarufu kwa jina la Recho akiimba nyimbo zake mbali mbali wakati wa Onyesho la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika usiku wa Kuamkia leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani,jijini Tanga.
Mamaa wa Majanga aitwae Snura akiwapagawisha wakazi wa Tanga na goma lake lililoshika hatamu sana hapa nchini (MAJANGA).
Ali Kiba na madansa wake wakitoa Burudani kwenye Onyesho hilo.
Mkali wa Hip Hop hapa nchini kwa Mwaka 2012/13,Kala Jeremier akifanya mambo yake mbele ya Mashabiki wake Lukuki waliofika ndani ya Uwanja wa Mkwakwani,Jijini Tanga usiku wa kuamkia leo.

MDAU NA MBAO BEGANI

Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images