Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

Wasanii wa Tamasha la Filamu Grand Malt watoa msaada wa vyandarua hospitali ya Sekou-toure leo jijini mwanza.

0
0
Wasanii mbalimbali wakiongozwa na Raymond Kigosi  wakikabidhi msaada wa vyandarua kwenye hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou-toure, kwa katibu wa afya wa Hospitali  hiyo Bwa.Daniel Temba ikiwa ni sehemu ya wasanii hao kuwa karibu na wananchi, kisha baadae kuonyesha kazi zao mbalimbali kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
 Sehemu ya vyandarua vilivyotolewa msaada vikiwa tayari vimefungwa na wasanii wa filamu hapa nchini,mara baada ya kutoa msaada wa vyandarua hivyo ndani ya wodi ya wazazi kwenye hospitali ya Mkoa wa jiji la Mwanza-Sekou-toure  mapema leo asubuhi kwa udhamini mkubwa wa kinywaji kisicho na kilevi cha Grandmalt..
 Msanii wa Bongo Movie,Jacline Wolper akiwa katika wodi ya wazazi ,Hospital ya Mkoa wa Mwanza Sekou-toure akifunga chandarua kwenye moja ya vitanda hospitalini hapo,ikiwa ni sehemu ya vyandarua vilivyotolewa na wasanii hao kupitia kinywaji cha Grandmalt
 Wasanii Irine Uwoya na Shamsa Ford wakiwa na mmoja wazazi akiwa amembeba mtoto aliezaliwa kwenye hospitali hiyo ya Mkoa wa Mwanza, Sekou-toure  mara baada ya wasanii hao kutembelea Hospitali hiyo na kutoa vyandarua kwenye wodi Wazazi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza,Halifa Hassan Hida akizungumza machache (mbele ya wasanii wa Bongo Movie (hawapo pichani) ikiwemo na kuwashukuru wasanii hao wa filamu kwa kitendo cha kiungwana kabisa katika suala zima la kuisaidia jamii yao inayowazunguka kwa njia moja ama nyingine na pia amewataka kuwasaidia wasanii wachanga wa jiji la Mwanza na kuwaelekeza njia sahihi za mafanikio katika tasnia hiyo ambayo kwa sasa imezidi kushika kasi siku siku.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA NA HAPA.

MASANJA, SHILOLE WAFIKA ULIPO MJENGO WA UBALOZI WA TANZANIA MAREKANI

0
0
 Juu na chini ni Wasanii Masanja Mkandamizaji na Shilole wakiwa nje ya mjengo wa Ubalozi wa Tanzania, Washington, DC mara walipopita na kupiga picha nje ya mjengo Jumapili June 30, 2013 walipokua wakitokea uwanja wandege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia. Kesho mchana Jumanne April 2, 2013 watatembelea rasmi mjengo huo na kusaini kitabu cha wageni.
 Masanja na Shilole wakiwa na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi wakiangalia menyu tayari kwa kuagiza dinner ya mchana walipokwenda mgahawa wa kijiji cha Swahili uliopo Beltsville, Maryland
 Shilole na Masanja katika picha ya pamoja na mmiliki wa mgahawa wa Swahili Village Bwn.Kelvin.
Masanja na Shilole wakiingia kwenye usafiri wao kuelekea Hotelini walikofikia.

Treni ya 'Mwakyembe yapata jali alfajiri ya leo,kesho kutotoa huduma kabisa

0
0
Leo mnamo saa 11:30 asubuhi vichwa viwili vya treni ya huduma la jiji la Dar es Salaam vilipata ajali ya kugongwa na roli la mizigo aina ya Fusso katika makutano ya reli na barabara ya Kawawa jijini Dar es salaam , katika jali hiyo dereva wa Fusso alifariki duniani papohapo hata hivyo Utingo wake alinusurika.

Hata hivyo vichwa hivyo vya treni vilipata mkosi tena wa ajali ambapo viligongwa na basi dogo la Daladala aina ya Isuzu katika makutano ya reli eneo la Kamata. Tukio hilo lilisababisha majeruhi kadhaa katika basi hilo la daladala ambapo majeruhi  wamelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbil wakiwemo askari wawili Polisi kutoka Kikosi cha Reli  mmojawapo akiwa  mahututi.
 
Vichwa hivyo viifanikiwa kufika stehesheni kwa wakati na kuanza kutoa huduma ya usafiri wa treni jijini  kutoka Dar Stesheni kwenda Ubungo Maziwa hadi saa 5 asubuhi hata hivyo huduma ya leo  jioni Julai 01, 2013, imesogezwa mbele na itaanza saa 12 jioni badala ya saa 10:30 alasiri. 

mabadiliko haya yamebidi yafanyike   kufuatia Jiji la Dar es Salaam kuwa na hekaheka ya kumpokea Raisi wa Marekani Barack Obama.
 
Aidha uongozi wa  TRL unawataarifu wakazi wa jiji kuwa kesho Julai 02, 2013, huduma za treni ya jiji hazitakuwepo hadi keshokutwa Julai 03, 2013, ambapo zitaendelea kama kawaida.
 
Imtolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
 Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu.
 
Makao Makuu ya TRL
Dar es Salaam.
Julai 01, 2013.

WAUGUZI WA AFRIKA MASHARIKI WAFANYA MKUTANO ZANZIBAR

0
0
Wazira wa Afya Juma Duni Haji, akifungua Mkutano wa Wauguzi wa Afrika Mashariki kulia Clavery Mpandana Muguzi Mkuu Tanzania ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi Afrika Mashariki kushoto Katibu Mkuu Wizara ya Afya Muhamed Saleh Jidawi. Mkutano huo uliofanyika Hoteli ya Oceanview nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Badhi ya Wajumbe wa Mkutano wa Wauguzi wa Afrika Mashariki wakifuatilia hutuba ya ufunguzi iliyotolewa na Waziri wa Afya Juma Duni Haji, huko Hoteli ya Ocean view nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Waziri wa Afya Juma Duni, katikati waliokaa akiwa katika Picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano wa Wauguzi wa Afrika Mashariki uliofanyika katika Hoteli ya Ocean view nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar.

USIKU WA MATUMAINI J'PILI HII: SAA 16 ZA MAAJABU

0
0

Na Mwandishi Wetu
SIYO siri, Julai 7, mwaka huu (Siku ya Sabasaba), anga lote la Jiji la Dar es Salaam litasimama kwa muda wa saa 16. Burudani mfululizo pamoja na matukio ambayo hayajawahi kushuhudiwa, mengine ni adimu sana, yatachukua nafasi pana siku hiyo kwenye Uwanja wa Taifa.

Diamond.
Ni saa 16 za maajabu! Tafakari Mbunge wa Kigoma Mjini (Chadema), Zitto Kabwe, ataonesha uwezo wake wa kucheza masumbwi na kuchapana na staa wa filamu Tanzania, Vincent Kigosi ‘Ray’. Je, ni vigumu kuamini? 
Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, atakuwa na kibarua chake katika mchezo wa ndondi, atakapopanda ulingoni kuzipiga na malkia wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper. Uheshimiwa na usupastaa kando, zitapigwa ngumi tu kwa raundi nne.

MAPOKEZI YA RAIS OBAMA IKULU, NA MKUTANO WAKE NA WANAHABARI JIJINI DAR LEO

0
0
Rais Barack Obama wa Marekani na mkewe Michelle Obama wakipokewa kwa Shangwe Ikulu,Jijini Dar es salaam mchana wa leo.
Rais Barack Obama wa Marekani na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakipokewa kwa Shangwe Ikulu,Jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na mgeni wake,Rais Barack Obama wa Marekani wakati walipokuwa wakielekea sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kukutana na kuzungumza na Waandishi wa habari Ikulu,Jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa maelezo ya mti wa mpingo anaotaka kuupanda katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais Barack Obama wa Marekani na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakizungumza na waandishi wahabari Ikulu,Jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa maelezo ya mti wa mpingo aliotaka kuupanda Rais wa Marekani,Barack Obama katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo
Rais Obama akipanda mti aina ya mpingo katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho kikwete akimsindikiza mgeni wake baada ya kumpatia mapokezi ya kihistoria leo Ikulu. PICHA NA IKULU

WWF Praises President Obama For Major Pledge During Africa Visit To Tackle Illegal Wildlife Trade

USIKU WA TUDD THOMAS WAFANA NDANI YA DAR LIVE

0
0
Wasanii mbalimbali wakiwemo Marlaw, Izzo B, Chegge, Tundaman, Mhe. Temba, Amin, Queen Darleen, Quick Lacka, Baghdad, Scorpion Girls, Makomandoo na wengineo usiku wa kuamkia leo walifanya makamuzi ya nguvu katika Tamasha la Usiku wa Prodyuza Tudd Thomas lililofanyika kwenye Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo pande za Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam.
Chegge akiwadatisha wapenzi wa burudani wa Dar Live katika Usiku wa Tudd Thomas.
Izzo B akiongea na Mshua ndani ya Dar Live.
Mwanamuziki Marlaw akiwabembeleza mashabiki wa Dar Live.


MAADHIMISHO YA SIKU YA SERIKALI ZA MITAA YAFANA IRINGA MANISPAA YA IRINGA

0
0
Mbunge Msigwa na  mkuu  wa  wilaya ya  Iringa  wakitazama  ndizi aina ya Jamaica inayolimwa Mtwivila Iringa iliyoletwa katika maonyesho ya  serikali za mitaa mjini Iringa
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini akiwasili jukwaa kuu na kusalimiana na mkuu wa wilaya ya Iringa Dr Leticia Warioba.
Mkuu  wa wilaya ya  Iringa Dr Leticia  Warioba akimtazama  kwa makini  askari wa kikosi cha  zimamoto mjini Iringa akionyesha jinsi  ya kuzima  moto
Watangazaji  wa kituo  bora  cha matangazo  cha  televisheni ya  Manispaa ya  Iringa (IMTV) wakiwa katika banda lao la maonyesho leo katika  viwanja vya Mwembetogwa mjini Iringa (picha zote na Francisgodwin Blog -mzee wa matukio  daima)

Makamu wa Rais,Dkt. Bilal afunga Mkutano wa siku tatu wa Viongozi wa Kimataifa wenye lengo la kutokomeza njaa Barani Afrika,Jijini Addis Ababa

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mommmed Gharib Bilal, akifunga Mkutano wa siku tatu wa Viongozi wa Kimataifa wenye lengo la kutokomeza njaa Barani Afrika .Mkutano huo ulimazika jana jioni mjini Addis Ababa Ethiopia.
Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiongoza Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Kimataifa kuzungumzi juu ya kutokomeza tatizo la njaa Barani Afrika uliomalizika mjini Addis Ababa Ethiopia leo.
Ujumbe wa Tanzania uliofuatana na Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal wakifuatilia kwa makini mkutano wa Afrika uliozungumzia juu ya kutokomeza tatizo la njaa Barani Afrika . Mkutano huo ulimalizika jana jioni July 01-2013 mjini Addis Ababa Ethiopia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal wa pili kushoto akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Viongozi wa kimataifa waliohudhuria Mkutano wa Kimataifa uliozungumzia juu ya kutokomeza tatizo la njaa Barani Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia July 01-2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mommmed Gharib Bilal na ujumbe wake, wakiingia kwenye ukumbi wa mkutano wa Viongozi wa kimataifa uliozungumzia juu ya kutokomeza tatizo la njaa Barani Afrika . Mkutano huo ulimalizika jana jioni mjini Addis Ababa Ethiopia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mwenyekiti wa AUC Dk. Nkosazana Dlamina Zuma, kwenye ukumbi wa Mikutano wa umoja huo baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Viongozi wa Kimataifa uliozungumzia juu ya kutokomeza tatizo la njaa Barani Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia jana jioni July 01-2013.(Picha na OMR).

MFALME MSWATI WA SWAZILAND AAONDOKA NCHINI

0
0
Mfalme Mswati wa Swaziland akisindikizwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipoondoka kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam kurejea nyumbani baada ya kufungua maonyesho ya Biashara ya Kimataifa kwenye uwanja wa Mwalimu Nyerere Julai 1,2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na mfalme Mswati wa Swaziland ambaye aliondoka nchini baada ya kufungua maonyesho ya Kiataifa ya Biashara kwenye uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Julai 1, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WINDHOEK SABA SABA PAVILION

0
0
Come visit our completely renovated Windhoek Pavilion & VIP Lounge! Air conditioning, restrooms, a new stage & sound system added for 2013! Arrive early and beat the traffic, as this pavilion opens an hour before everyone and stays open until late. The Windhoek Pavilion is the only place to offer your favorite beer along with shows & entertainment, giant screen, pool tables and a VIP lounge all in a truelly premium setting. Watch out for the Green Party we are hosting this weekend!!!
Traditional dancers, acrobats and so much more exciting entertainment exclusively at the Windhoek Pavilion...
Our friendly Windhoek Hostesses are an elite team of premium hostesses whose job is to welcome, delight, and help co-ordinate our visitors in our super premium pavilion. Please be sure to visit us and experience the only 100% PURE BEER in Tanzania.

KUMBUKUMBU

0
0
KUMBUKUMBU YA MWAKA MMOJA YA MAREHEMU MAMA OSITHA JOHN JAKA

Hatimaye siku , miezi imepita hadi hii leo ambapo imetimia mwaka mmoja (1) tangu ulipofariki mchana ule wa siku ya Jumatatu, JULAY, 2, 2012.

Japokuwa haupo nasi hapa duniani lakini tupo nawe Kiroho kwa kuendeleza mema yote uliyotufundisha na kutuasa.Tunakukumbuka kwa Upole, Upendo, Busara, na Ukarimu uliokuwa nao kwa familia na marafiki.

Daima unakumbukwa sana na watoto wako wapendwa

TAASISI YA ACOT IMEWEZA KUTWAA UBINGWA WA EAST AFRICA CUP 2013

0
0
KATIKA MASHINDANO HAYA YA EAST AFRICAN CUP HUJUMUISHA VIJANA MBALIMBALI WENYE UMRI KATI YA MIAKA 13 HADI 16, KUTOKA NCHI ZOTE ZA AFRIKA MASHARIKI. TIMU ZILIZOSHIRIKI MWAKA HUU ZILITOKA TANZANIA,KENYA,UGANDA,BURUNDI,ZAMBIA. JUMALA YA TIMU NI 85 NA JUMLA YA WASHIRIKI WOTE WALIKUWA 1175.

ACOT ILIWEZA KUFANYA VYEMA KUANZIA HATUA YA MAKUNDI,ROBO,NUSU NA BAADAYE FAINALI. FAINALI ILIFANYIKA KATIKA UWANJA WA MEMORIAL MJINI MOSHI. ACOT-TEMEKE--DAR ES SALAAM ILIPAMBANA NA CHRISC ZANZIBAR. MPAKA FILIMBI YA MWISHO ACOT ILIWEZA KUWANYESHWA VIKOMBE VIWILI TU VYA UROJO KWA BILA NA KUTAWAZWA KUWA MABINGWA WAPYA KWA MWAKA 2013.
WACHEZAJI WAKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA.
UPANDE WA KUSHOTO NI MKURUGENZI MKUU WA MASHINDANO HAYA NDUGU.BJARTE ØEN AKIWA NA MKURUGENZI MSAIDIZI WA MICHEZO TANZANIA NDUGU JULIANA YASODA AKIWAVESHA WACHEZAJI WA ACOT MEDANI YA DHAHABU.
BAADHI YA VIONGOZI WA ACOT WAKIWA WAMEFURAHI PAMOJA NA KUSHIKIRIA KOMBE HILO KUTOKA KUSHOTO ELIPINA, EMMANUEL, TIMOTH, CAROLINE.

MKUTANO MKUU WA TANO WA WADAU WA MFUKO WA GEPF WAFANA MJINI ARUSHA

0
0


Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka akifungua Mkutano Mkuu wa tano wa wadau wa mfuko huo ulifanyika jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa GEPF, Daudi Msangi akifafanua jambo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa tano wa Mwaka wa wadau wa Mfuko wa akiba ya Wafanyakazi Serikalini (GEPF), jijini Arusha.
 Mkurugenzi Masoko na Uendeshaji wa GEPF, Anselim Peter akitoa mada.
 Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Wiliam Erio akifuatilia mada wakati wa mkutano huo. 
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka akimsikili kwa makini Meneja Masoko na Utekeleza wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini (GEPF), Aloyce Ntukamazina mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa tano wa wadau wa mfuko huo ulifanyika jijini Arusha. 

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

KONGAMANO LA WAZI NA UZINDUZI WA MPANGO WA KULETA MATOKEOMAKUBWA SASA KWA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

NHIF yatoa ngao kwa washindi wa Mashindano ya TIKA

0
0
Naibu Waziri wa Elimu katika Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Kassim Majaliwa akikabidhi ngao iliyotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa mshindi wa mashindano ya TIKA yaliyofanyika mjini Morogoro kwa Kiongozi wa timu ya Garage FC Jumanne Wida baada ya kuibuka washindi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Emanuel Humba akikabidhi ngao kwa Shaaban Mrisho kwa kuibuka washindi katika mashindano ya TIKA yaliyodhaminiwa na NHIF.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emanuel Humba akipeana mkono wa pongezi na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera baada ya kupokea cheti cha ushiriki na mchango wa NHIF uliotolewa kufanikisha maadhimisho ya Serikali za Mtaa.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emanuel Humba akionesha cheti kilichotambua mchango wa NHIF katika maadhimisho hayo.
Kikosi cha Timu ya Garage FC ambacho kiliibuka mshindi katika mashindano ya TIKA wakiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Mfuko uliodhamini mashindano hayo.

RATIBA YA MAZISHI YA MAREHEMU ANNA BWENDA NTAMUBANO

0
0
MAREHEMU ANNA BWENDA NTAMUBANO.


FAMILIA YA NTAMUBANO WA MUGOMA,NGARA INAWATANGAZIA RATIBA YA MAZISHI YA MPENDWA WETU ANNA BWENDA NTAMUBANO YANAYOTARAJIA KUFANYIKA SIKU YA JUMATANO TAREHE 3 JULAI.

SAA TANO ASUBUHI KUTAKUWA NA CHAKULA CHA PAMOJA

IKIFUATIWA NA

KUAGA MWILI KUANZIA SAA SITA MCHANA
(NYUMBANI KWA MAREHEMU SINZA MUGABE).

SAA SABA KAMILI KUTAKUWA NA MISA YA KUMUOMBEA MAREHEMU KWENYE

KANISA LA KKKT SINZA KUMEKUCHA.

BAADA YA HAPO TUTAKUSANYIKA KWENYE MAKABULI YA KINONDONI KUANZIA SAA TISA KWA AJILI YA

MAZISHI.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIBARIKIWE.
IMETOLEWA NA FRED ZG SSEBUYOYA.

mapokezi ya rais barack obama wa marekani

RAIS BARACK OBAMA WA MAREKANI AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU MBILI HAPA NCHINI

0
0

Rais Barack Obama wa Marekani ameondoka nchini mchana huu kurudi nchini Marekani,baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini iliyoanza jana.Rais Obama na mwenyezi wake Rais Jakaya Kikwete, leo walifanya ziara ya kutembelea mitambo ya kuzalisha umeme ya Symbion iliopo Ubungo jijini Dar es Salaam ambako Rais Obama alizindua rasmi mpango wa nchi yake kusaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa nchi saba za Afrika, ikiwemo Tanzania.

PICHA ZA MATUKIO MBALI MBALI ZITAWAJIA BAADAE KIDOGO 
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images