Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1812 | 1813 | (Page 1814) | 1815 | 1816 | .... | 3286 | newer

  0 0

   Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustin Kamuzora akiongea na Watumishi wa Baraza   la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) alipokutana nao kuongea mambo mbalimbali ya Kiutumishi,  Ofisi hiyo ambayo iko Chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais.
   Mmoja wa Watumishi wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Injinia Renalda Mukandara akichangia maoni yake wakati wa kikao hiko.
  Sehemu ya Watumishi wa  Baraza   la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustin Kamuzora (hayupo pichani) alipokua akiongea nao alipokutana nao katika Ofisi za Baraza hilo.

  0 0  0 0  0 0


   Airtel Tanzania PLC has embarked on a strategic efficiency enhancement exercise aimed at making the company more flexible and agile and to innovate and respond better to the market demands. 
   
  “This exercise, which shall be completed soon aims to improve organizational efficiency and flexibility by delayering and simplifying the operational structure and thereby enhancing empowerment to its employees. 
   
  This exercise will help Airtel Tanzania to be closer to customers, ensure quicker responses to the customer’s needs, thus, enhancing Airtel Tanzania’ position in the market place”. Said Colaso in a statement issued by Company

  The Managing Director for Airtel Tanzania PLC Mr. Sunil Colaso also said, “The exercise will result in some of the current positions in the current structure becoming redundant. As a responsible corporate, the company shall take all necessary steps to support the impacted employees financially as prescribed by the prevailing laws in Tanzania, while helping them find new opportunities. 
   

  Amongst several other benefits, Airtel Tanzania has engaged a reputed organization to impart skills/ training to the impacted employees, in the endeavor that this will help open up fresh opportunities for such employees. The Company shall bear the full cost of providing this support to the concerned employees”.

  Airtel remains committed to the Tanzanian market. The company has made significant investments in the market to drive innovation, network quality and customer service, and will continue to do so. Through its Corporate Social Responsibility programs, Airtel has supported various secondary schools across Tanzania, touching 58,000 students in over 1,300 schools. Insisted Colaso

  0 0

  Na: Veronica Kazimoto.

  Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania wa awamu ya pili unatarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.

  Akizungumza wakati wa mafunzo ya wadadisi yanayoendelea kufanyika mkoani Dodoma Meneja  wa Shughuli za Kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Wilfred Mwingira amesema  lengo kuu la utafiti huo ni kufuatilia viashiria vilivyowekwa kwenye utafiti wa awamu ya kwanza ili kutathmini na kujua kama kuna athari yoyote iliyotokea.

  "Utafiti huu ni wa kitaifa na utafanyika Tanzania Bara na Zanzibar kwa lengo la kutathmini na kujua kama kuna athari yoyote iliyojitokeza kwenye viashiria vilivyowekwa kwenye utafiti wa awamu ya kwanza", amesema Mwingira.

  Nae Mratibu wa utafiti huo Rainer Kiama amesema kuwa utafiti huu unafanyika ili kutathmini kama mpango unaleta manufaa yaliyokusudiwa katika ngazi ya kaya kwa kutumia viashiria kama vile elimu, afya, kazi na matumizi ya muda, shughuli za kaya zisizo za kilimo, mapato, mikopo, akiba na uhamishaji fedha.

  Viashiria vingine ni  shughuli za kilimo,  makazi ya kaya na upatikanaji wa maji, matumizi na usalama wa chakula katika  kaya, maamuzi katika kaya, ukatili kwa wanawake na matarajio ya vijana, mahusiano ya kaya na jamii pamoja na mtazamo wa kaya kuhusu Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

  Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania wa awamu ya pili utahusisha kaya takribani elfu saba (7,000)  ambazo zilihojiwa katika utafiti wa awamu wa kwanza uliofanyika mwezi Juni, 2015.
   Meneja  wa Shughuli za Kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Wilfred Mwingira akizungumza na wadadisi wakati wa mafunzo ya Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania yanayoendelea kufanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.
   Wadadisi  wakijifunza kwa vitengo namna ya kutumia vifaa vya kielektroniki - tablets vitakavyotumika wakati wa Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu. Mafunzo ya Wadadisi wa utafiti huo yanaendelea kufanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.
   Wadadisi  wakijifunza kwa vitengo namna ya kutumia vifaa vya kielektroniki - tablets vitakavyotumika wakati wa Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu. Mafunzo ya Wadadisi wa utafiti huo yanaendelea kufanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.


  Wadadisi  wakijifunza kwa vitengo namna ya kutumia vifaa vya kielektroniki - tablets vitakavyotumika wakati wa Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu. Mafunzo ya Wadadisi wa utafiti huo yanaendelea kufanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.

  0 0

  Kampuni ya Coca-Cola leo imezindua katika soko la Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla, soda mpya ya “Coca-Cola Bila Sukari”. Uzinduzi wa soda hii mpya umefanyika katika kiwanda cha Nyanza Bottlers mkoani Mwanza, ambapo pia baadaye utafanyika katika mikoa Dar es Salaam na Mbeya ambapo awali ulifanyika mjini Moshi .

  Soda mpya ya ‘Coca-Cola Bila Sukari’ ladha yake imeboreshwa zaidi kutokana na soda isiyo na sukari iliyokuwa inatengenezwa hapo awali ya Coca-Cola Zero ambapo soda mpya ladha yake inashabihiana na soda ya Coca-Cola asilia lakini haina sukari kabisa.

  Tangia mwaka 2006 wakati soda ya Coke Zero imeingia kwenye masoko, kampuni ya Coca-Cola imekuwa ikifanya jitihada kuhakikisha inatengeneza soda mpya ya Coca-Cola isiyo na sukari lakini yenye ladha sambamba na Coca-Cola asilia na imefanikiwa kuja na soda mpya ya ‘Coca-Cola Bila Sukari’ kinywaji ambacho kitawezesha watumiaji wa Coca-Cola kuipata kwa ladha asilia hata kama watachagua kuipata isiyotengenezwa kwa sukari.

  “Soda ya Coca-Cola Zero ina ladha nzuri pia, lakini pamoja na ubora wake timu ya Coca-Cola imekuwa ikifanyia kazi kuhakikisha inapatikana soda isiyo na sukari lakini yenye ladha inayoshabiana na Coca-Cola asilia”. Alisema Meneja Mauzo Mwandamizi wa Nyanza Bottlers, Deus Kadico.

  Kadico aliongeza kuwa; “Ubunifu wa wataalamu wetu umewezesha kupatikana soda mpya ya ‘Coca Cola Bila Sukari’ ambayo inatoa wigo kwa wateja kuwa na chaguo la kupata kinywaji cha Coca-Cola kwa radha asilia kwa kadri wanavyotaka,ikiwa na ladha ya sukari ama isiyo na sukari”. 

  Pamoja na hayo, Kadico alisisitiza kuwa lengo kubwa ni kuhakikisha watumiaji wa soda ya Coca-Cola wanafurahia ladha yake halisi na asilia wanapokunywa soda yenye sukari au ‘Coca-Cola Bila Sukari’.

  Soda za ‘Coca Cola Bila Sukari’ zimeanza kuwa kwenye soko la Tanzania kuanzia mwezi uliopita katika sehemu zote zinapouzwa soda na bei yake ni sawa na soda aina nyingine zote zinazotengenezwa na kusambazwa na kampuni ya Coca-Cola.
  Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini Tanzania, Sia-Louise Shayo akizungumza na umati wa wasambazaji na mawakala wa soda ya Coca-Cola jijini Mwanza wakati wa hafla maalumu ya uzinduzi wa kinywaji kipya cha ‘Coca-Cola Bila Sukari’. Uzinduzi wa soda hii mpya umefanyika katika kiwanda cha Nyanza Bottlers mkoani Mwanza, ambapo pia baadaye utafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam na Mbeya.

  0 0

  Benki ya KCB Tanzania inaendelea kuwapatia wanawake wajasiriamali waliopitia mafunzo ya ujasiriamali ya KCB 2jiajiri ushauri wa kibiashara kwa vitendo ofisini kwa wafaidika wa 2jiajiri. 

  Maafisa watatu ambao ni; afisa fedha, sheria na masoko wanawatembelea wafaidika hao wajasiriamali waliomaliza mafunzo ya KCB 2jiajiri katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Moshi, Morogoro na Zanzibar.

  KCB 2jiajiri ni programu inayolenga kumkomboa mwanamke mjasiriamali kutoka katika matatizo yanayosababisha biashara yake ishindwe kukua na kuwa endelevu. Matatizo yanayolengwa kutatuliwa kutoka kwa wanawake wajasiriamali hawa ni elimu ya kifedha, kufikiwa na huduma za kifedha, ukosefu wa dhamana, kutokujua vizuri masuala ya kisheria, uelewa finyu wa sera za serikali na kiuchumi, njia hafifu za kuendesha biashara endelevu, ukosefu wa mtaji, utaalamu wa kuanzisha biashara kubwa n.k.

  “Programu hii ilizinduliwa rasmi Desemba, 2016, ambapo hadi sasa tumewapa stadi za biashara endelevu wanawake wajasiriamlai 258 kutoka mikoa 6 ya Tanzania.” Alisema Christine Manyenye, Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB.

  Akielezea kuhusiana na programu ya KCB 2jiajiri Bi. Manyenye alieleza kuwa, wafaidika wa KCB 2jiajiri baada ya kumaliza mafunzo ya siku tatu darasani, kwa sasa wananufaika kwa kupata ushauri wa kibiashara na kitaalamu kutoka kwa washauri watatu katika nyanja za Kifedha Kisheria na Masoko.
  Afisa Sheria Bi. Doris Mugarula (wakwaza kushoto) na Afisa Fedha Bi. Happiness Kisanga (wapili kushoto) wa Benki ya KCB wakimsikiliza mjasiriamali Bi. Batula akielezea maendeleo ya biashara yake ya nguo mkoani Arusha. 
  Afisa Sheria, Bi. Doris Mugarula (wakwanza kulia) na Afisa Fedha Bi. Happiness Kisanga (wapili kulia) wa Benki ya KCB wakimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Shamsa Ally (kushoto) katika duka lake la vifaa vya magari makubwa mkoani Morogoro.
  Afisa Masoko, wa Benki ya KCB, Bi. Ghati Muhere (kulia), akimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Jac Bazaar (kushoto) katika duka lake la vifaa vya umeme mkoani Morogoro.
  Afisa Masoko Bi. Ghati Muhere (aliyechuchumaa) na Afisa Fedha Bi. Happiness Kisanga (aliyesimama) wa Benki ya KCB wakimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Violeth (aliyeinama) katika biashara yake ya kilimo mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
  Afisa Masoko, Bi. Ghati Muhere (wakwanza kulia), Afisa Sheria, Bi. Doris Mugarula (watatu kushoto) na Afisa Fedha, Bi Happiness Kisanga (wapili kushoto) wa Benki ya KCB wakimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Mercy (wakwanza kushoto) katika biashara yake ya huduma za Interneti mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.


  0 0

  Baraza la ulamaa limetoa wito kwa vyombo vya dola kumchukulia hatua stahiki mtu aliyejitokeza katika mkoa wa pwani na kudai yeye ni Mtume. 

  Akisoma wito huo, kwa niaba ya Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Ally, Mwenyekiti wa Halmashauri kuu Bakwata Sheikh Hamisi Said Mataka amesema, anachodai mtu huyo aliyetajwa kwa jina la Hamza Issa kuwa yeye ni nabii hayako kabisa katika mafundisho ya kiislamu.

  Amesema kauli ya Issa kudai yeye ni mtume na kisha kwamba ni Muislamu kwa kutumia maandiko ya Uislamu, ni upotoshaji mkubwa ambao ukiachwa bila kudhibitiwa ni kuruhusu fujo na uvunjifu wa amani. 

  "Kwa mujibu wa maelezo yaliyoenea katika mitandao ya kijamii na ya kutoka baraza za Masheikh wa Mkoa wa Pwani chini ya kiongozi wake Sheikh na Qadhi wa Mkoa wa Pwani, amedai kuwa yeye ni Nabii Ilyasa kwa maana ya kwamba roho ya Nabii Ilyasa imemuingia yeye Hamza Issa na kwa hiyo yeye amekuwa Nabii Ilyasa" amesema Sheikh 

  Ameongeza maelekezo na mafundisho ya uislamu yako wazi kuwa hakuna Mtume mwingine katika Uislamu baada ya Mtume Muhammad (S.A.W) na kwamba upatikanaji wa MTU ndani ya uislamu na kudai kuwa yeye ni Mtume ni kutaka kuamsha hisia Kali za waislamu nchini.

  "Baraza la Ulamaa linapenda kuwafahamisha waislamu kwamba, yeyote atakayemfuata mpotoshaji huyu atakuwa ametoka ndani ya uislamu" amesema Sheikh Mataka. 

  Pia Baraza limetoa wito kwa Masheikh wa Mikoa, Wilaya na viongozi wa taasisi mbali mbali za Kiislam kutotoa fursa ya aina yoyote kwa huyo anayejiita Nabii ( Hamza Issa), ili kuzuia kuipotosha jamii.
  Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu Bakwata ,Sheikh Khamis Said akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, juu ya Vyombo vya Dola kuchukua hatua stashiki kwa mtu mmoja mkazi wa Mkoa wa Pwani, Hamza Issa anaejiita Nabii IIyasa .
  Waandishi wa Habari wakimsilikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu Bakwata, Sheikh Khamis Said, leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.


  0 0

  Na Karama Kenyunko, blog ya jamii.

  Mlalamikaji katika kesi ya madai iliyofunguliwa na Dk.William Morris dhidi ya Mchungaji Joseph Mwingira na Philis Nyimbi amewasilisha maombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akiomba, mkewe, Mwingira na Mtoto wake (9) wafanyiwe kipimo cha DNA.

  Maombi hayo ya Dr. Morris yamewasilishwa mahakamani hapo leo na wakili wake Respicious Ishengoma mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba, kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.

  Katika Maombi hayo Dr. Morris ambae ni mume wa (mdaiwa wa Pili, Philis Nyimbi) anaiomba mahakama itoe amri ya mkewe Mwingira na mtoto wakafanyiwe kipimo hicho cha DNA ili aweze kujua wazazi halisi wa mtoto aliyezaa na mkewe.

  Katika madai yake, Dkt. Morris anadai mchungaji Mwingira alizini na mkewe na hatimaye kuzaa naye mtoto wa kiume( 9).Mapema mahakamani hapo, wakili Ishengoma aliomba mahakama ianze kusikiliza maombi hayo kabla ya kuingia kwenye kesi ya msingi lakini Wakili wa Mchungaji Mwingira na Dk. Phillis waliomba kupatiwa muda ili waweze kuwasilisha majibu yao.

  Kesi hiyo itatajwa tena Agosti 2, mwaka huu. 

  Katika maombi, yake Dk. Morris, anaiomba mahakama itoe amri kwake yeye, walalamikiwa Mchungaji Mwingira na Dk. Phillis pamoja na mtoto waende kupimwa DNA.

  Desemba 28, 2011 Dk. Morris na Phillis walifunga ndoa katika Kanisa la Anglican, Upanga na wakati wa ndoa yao (Mchungaji Mwingira na Phillis) waliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na kubahatika kupata mtoto mwenye miaka tisa na matatizo mbalimbali ya kiafya kwa mkewe.

  Mlalamikaji huyo anadai alitoa taarifa polisi katika kituo cha Kibaha, ambapo aliambiwa ni suala la uzinzi au udhalilishaji ambalo haliwezi kuwa la kijinai na kushauriwa afungue kesi ya madai.

  Amedai kitendo cha mkewe kuwa na uhusiano na Mwingira kimeharibu mipango yake ya mbele kiasi cha kumfanya apoteze matumaini ya kuishi.
  Aidha, kitendo hicho kimemuaibisha na kushusha hadhi yake ndani na nje ya nchi ya Tanzania.

  0 0

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Harisson Mwakyembe akilia juu ya jeneza la Mke wake Marehemu Linah Mwakyembe wakati wa kuaga mwili huo nyumbani kwake Kunduchi, Jijini Dar es Salaam mapema leo  ambapo baadaye mwili huo ulisafirishwa kwenda Kyela, Mbeya kwa ajili ya mazishi. 
   Ibada ya kuombea mwili wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Harisson Mwakyembe, Marehemu Linah Mwakyembe ikiendelea katika kanisa la KKKT Kunduchi, Dar es Salaam kabla ya mwili huo kusafirishwa kwenda kyela, Mbeya kwa ajili ya mazishi.

  Picha na Ofisi ya Bunge

  0 0  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amezindua huduma mpya ya fedha mtandao ijulikanayo kama TTCL PESA ya Kampuni ya Simu Tanzania TTCL. Uzinduzi huo umefanyika katika Makao Makuu ya TTCL barabara ya Samora jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mheshimiwa Omari Nundu ambaye ni Mwenyeketi wa Bodi ya TTCL, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujezi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Anjelina Madete, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bwana Waziri Kindamba, Wajumbe wa Bodi na wafanyakazi wa TTCL.

  Akizungumza katika hafla hiyo Makamu wa Rais alisema uzinduzi wa huduma ya TTCL PESA ni mwendelezo wa jitihada za Kampuni hiyo kurejea katika nafasi yake ya awali ya kuwa suluhisho la kweli la utoaji huduma za Mawasiliano hapa nchini.

  “Kuzinduliwa kwa huduma hii ni uthibitisho mwingine kwamba, TTCL inatekeleza kikamilifu maagizo ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais wetu mpendwa Dkt John Pombe Magufuli ambaye ameelekeza kuwa, Mashirika yote ya Umma yajiendeshe kwa faida, yatoe gawio Serikalini, yawahudumie wananchi kwa kiwango cha juu kabisa cha ubora na kwa gharama nafuu” alisema Makamu wa Rais.

  Aidha, Makamu wa Rais alisisitiza kwamba TTCL PESA itawezesha wananchi kutuma na kutoa pesa kwa viwango vya chini kabisa kupita mitandao yote, pia itawezesha wananchi kulipia Bill za Umeme (LUKU), Maji, Ving’amuzi na kuwezesha wateja kununua muda wa maongezi na vifurushi vya data vya TTCL. Aliwataka TTCL kuendelea kuwa wabunifu zaidi ili waweze kuongeza huduma nyingine kadiri mahitaji na siku zinavyokwenda.

  Akijibu kuhusu changamoto zilizotajwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Makamu wa Rais alisema Serikali inazijua na itaendelea kuzipatia majawabu. Hatahivyo aliwataka watumie vyema rasilimali walizopewa ikiwamo Mkongo wa Taifa na Kituo cha Kuhifadhia Kumbukumbu za kimtandao kupata pesa za kujiendeshea.

  Makamu wa Rais pia aliipongeza menejimenti ya TTCL kwa wazo lao la kufikiria kuanzisha kiwanda cha simu hapa nchini. Alisema “msisitizo wa serikali yetu kwa sasa ni ujenzi wa uchumi wa kipato cha kati ifikapo 2025 kupitia uwekezaji katika viwanda hivyo wazo lenu la ujenzi wa kiwanda cha simu limekuja wakati muafaka”.

  Mwisho, Makamu wa Rais alisema TTCL PESA itatoa fursa kubwa ya ajira kwa wananchi kuwa mawakala na itarahisisha shughuli za kiuchumi hasa biashara na hivyo aliwasihi wananchi kuonesha uzalendo wao kwa kutumia huduma za TTCL.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta pazia kuashiria uzinduzi wa huduma ya TTCL Pesa uliofanyika Makamu Makuu ya TTCL barabara ya Samora jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Ndugu Wazir W. Kindamba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta pazia kuashiria uzinduzi wa huduma ya TTCL Pesa uliofanyika Makamu Makuu ya TTCL barabara ya Samora jijini Dar es Salaam. 
  Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Ndugu Wazir W. Kindamba (kulia) akimuonesha namna ya kutumia huduma ya TTCL Pesa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kukamilika kwa uzinduzi wa TTCL Pesa uliofanyika Makamo Makuu ya TTCL barabara ya Samora jijini Dar Es Salaam. 
  Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Ndugu Wazir W. Kindamba (katikati) pamoja na Mwenyekiti ya Bodi ya TTCL Mhe. Omari Nundu wakimuonesha kwa vitendo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jinsi pesa inavyotumwa na kupokelewa kupitia huduma ya TTCL Pesa mara baada ya kukamilika kwa uzinduzi wa TTCL Pesa uliofanyika Makamo Makuu ya TTCL barabara ya Samora jijini Dar Es Salaam.

  0 0

  Wilayani Chamwino mkoani Dodoma maeneo karibu na Ikulu kunatarajia kuwa na burudani ya aina yake kwa wakazi wa kijiji hicho na maeneo yanayokizunguka, ambapo linatarajia kufanyika Tamasha la 9 la muziki wa asili ya Cigogo 'Chamwino Music Festival'.
  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Dk. Kedmon Mapana mipangilio ya maandalizi kuelekea tamasha hilo yamekamilika kwa kiasi kikubwa yakiwemo makundi na kamati nzima ya maandalizi imekamilisha asilimia kubwa ya matakwa ya tamasha hilo.
  Dk. Mapana anasema mipangilio imekamilika katika maeneo kama ukusanyaji wa fedha zitakazofanikisha tamasha hilo, maandalizi kwa washiriki na wageni waalikwa katika tamasha hilo.
  Dk. Mapana anasema kwa upande wa bajeti ya tamasha hilo ambayo ilikuwa ni shilingi milioni 32 lakini zimepatikana milioni 18 kwa sababu kwamba wafadhili wakubwa ni watu binafsi wanaoamini urithi wetu ni muhimu sisi kama binaadam sababu utu wetu umejengeka katika mila na desturi.
  "Ukitaka kupata utambuzi kwa wanachofikiria Wagogo jinsi wanavyokula, mahusiano yao ya kijamii na kwa ujumla kwa yote yanabebwa katika nyimbo na ngoma zao, hivyo tumeonelea tuyaweke wazi, ndipo tukaasisi tamasha hilo," alisema Dk. Mapana.
  Anasema kwamba ufadhili wa tamasha hilo wameupata kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Chamwino Connect lenye makazi yake nchini Marekani huku wafadhili wengine ni serikali ya kijiji cha Chamwino ambacho kinatoa maeneo ya kufanyia tamasha hilo huku wafadhili wengine ni wasanii wenyewe ambao hujitolea kwa kiasi kikubwa ili kukuza utamaduni wao.
   Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Dk. Kedmon Mapana akimuonesha Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson matangazo ya tamasha
   Katibu Mtendaji wa Basata, Mngereza na Dk. Mapana wakiimba kwa pamoja mojawapo ya ngoma  katika tamasha la  Chamwino
  Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Dk. Kedmon Mapana akipiga ngoma ya Kigogo. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0

  Mtanzania Augustino  Mponzi anayeishi jijini Dallas, Texas, Marekani, amebuni mchezo marufu wa karata uitwao ALBASTINI kwa njia ya mtandao. Mchezo huu unaweza kuchezwa kwa kutumia simu ya mkononi pamoja, tablet pamoja na iPad, na iPad Touch.
  Hivi sasa Tino Bw. Mponzi ameandaa mashindano ya ALBASTINI ambayo anasema watu wote duniani kuliko na internet wanaweza kucheza kwa kutumia simu za mkononi. Tayari ameshatengeneza Application zinazomwezesha mtu mwenye simu za Android  pamoja na tablet zenye kutumia Google play hali kadhalika wenye kutumia iPhone,  iPad na iPad Touch wanaweza kushiriki kwani App ya iOS inawezesha mchezo huo kupakuliwa na kuwekwa (install) kwenye vifaa hivyo.

  “Kuingia kwenye mashindano ni bure na mshidndi atapata Apple iPad”, anasema Bw. Mponzi, akiongezea kwamba baada ya kupakua (install) application hiyo mdau utapata maelekezo yote ya namna ya kucheza. Link za mchezo huo ni hizi hapa chini. KAZI KWAKO mpenzi wa ALBASTINI>
  0 0
 • 07/18/17--21:36: DRAFTI


 • 0 0


  0 0

  Kituo Kikuu cha Mabasi, Dodoma
  Bw. Justin Kisoka, Mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye amebobea katika masuala ya uchumi akitoa somo namna vijana wa Kitanzania watakavyoweza kuuza bidhaa zao ndani ya soko la Afrika Mashariki lenye nchi sita na idadi ya watu wanaofikia milioni 165. 
  Mfanyabiashara akielezwa namna bidhaa zake ambazo amezibeba kichwani atakavyoweza kuziuza katika nchi za Afrika Mashariki na kupata faida kubwa.

  Ujumbe wa kutaka vijana na Watanzania kwa ujumla wazinduke ili wanufaike na soko la Afrika Mashariki ulifikishwa kwa njia tofauti ikiwemo sanaa ya maigizo.

  Baadhi ya watu waliojitokeza kupata mbinu za kufanya biashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hapa ilikuwa Kituo Kikuu cha Mabasi mjini Dodoma.


  Gandhi Hall , Mwanza 

  Bw. Justin Kisoka akiwa kwenye bustani ya Gandhi Hall mjini Mwanza akitoa somo namna Wanamwanza watakavyoweza kuuza Sato, Sangara na bidhaa nyingine katika soko la Afrika Mashariki.
  Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  Wananchi wametakiwa kutumia Gesi Bayogesi kwani inapunguza gharama za watumiaji wa vyanzo vingine vya nishati ,pia gesi hii inasaida kutunza mazingira .

  Hayo yamebainishwa leo na Mratibu wa Ubunifu kutoka ECHO Harold
  Msanya wakati akitoa mada katika semina ya wadau mbalimbali wanaotumia Teknologia ya biogas , wamiliki wa mitambo hiyo pamoja na mafundi wanaofunga na kutengeneza mitambo hiyo .

  Alisema kuwa gharama za nishati ya umeme na gesi asilia ni ghali sana hasa kwa mtumiaji atakayedhamiria kutumia jiko la umeme au jiko la gesi lakini kwa gesi hii ya  samadi mtumiaji au mabaki ya nyasi aina mbalimbali zitamgharimu muda wake tu kujaza samadi na maji kila siku na atakuwa
  hana malipo ya pesa kila mwezi kama itakavyomlazimu kulipia umeme na gesi asilia kila mwezi, na hata kuni ambazo watumiaji wengine hununua

  Alibainisha kuwa njia hii imeweza kuwasaidia na kuwapa
  faida baadhi ya wananchi ambao wameanza kutumia teknoligia hii na pia wengi wao wameshanufaika na huduma hii .

  Aidha Bayogesi ambayo aghalabu hutokana na kinyesi cha wanyama, masalia ya mimea na kinyesi cha binadamu inaweza kuzalishwa na kutumika kupikia na hata matumizi mengine kama vile kuendeshea
  mitambo mbalimbali.

  Mkufunzi wa semina ya wadau mbalimbali wanaotumia Teknologia ya biogas ,pamoja na wamiliki wa mitambo hiyo pamoja na fundi Rowah Spear akiendelea kutoa elimu katika semina hiyo inayofanyika leo jiji hapa

  wakwanza kulia ni Mratibu wa Ubunifu kutoka ECHO Harold Msanya akiwa anafafanua jambo mbele ya wakufunzi hao .

  Mkufunzi wa semina ya wadau mbalimbali wanaotumia Teknologia ya biogas ndugu Rowah Spear akiwa anawaelekeza baadhi ya wadau waliouthuria semina jinsi biogas inaweza kufanya kazi

  wadau wakiendelea kufuatilia mada iliokuwa inaendelea .

  Mkurugenzi wa ECHO Erwin Kinsey akiwa anaonyesha wakulima na wadau walioshiriki semina hiyo mmea aina ya gugukaroti ambalo ,alisema kuwa gugu ilo kwa asilimia 90% huku asilimia 10% ni gugu ambalo linaweza kutumika kutengeneza biogas(na woinde shizza,Arusha)

  wadau wakiendelea na majadiliano katika makundi yao ikiwa ni sehemu ya kujifunza njia mbalimbali na matumizi ya biogas .Habari picha na Woinde Shizza,Arusha .  0 0

   Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na wafanyabiashara wa Stendi ya Mabasi Ubungo,wajumbe wa Kamati ya Fedha na uchumi ya Halmashauri ya Jiji alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha mabasi ubungo jana,kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji.
   Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akiwasikiliza Askari Polisi wa Ubungo alipofanya ziara ya kushtukiza jana katika kituo cha mabasi yaendoyo mikoani. katikati Mwenye Shati jeupe ni Diwani wa kata ya segerea ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya fedha na uchumi ya Halmashauri ya Jiji, Patrick Asenga.wa kwanza kushoto ni Meneja wa Kituo cha mabasi ubungo Iman Kasagara.
    Meneja wa Kituo cha mabasi Ubungo , Iman Kasagara akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita na Kamati ya fedha na Uchumi walipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha mabasi Ubungo.
   Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na waandishi wa habari jana alipofanya ziara ya kushtukiza ya kutembelea kituo cha mabasi ubungo. 
   Mbunge wa Jimbo la Ubungo, ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ziara iliyofanywa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Kamati ya fedha ya jiji.

  0 0

  Watendaji wa halmashauri za wilaya na manispaa wamekuwa ni kiwanda cha kutengeneza hoja za mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa hesabu za Serikali kwa kukosa umakini, uaminifu, uwajibikaji na kutokuzingata sheria, kanuni na maadili ya utumishi wa umma.

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema ameyasema hayo mapema leo katika baraza maalumu la madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakati wa kujadili hoja 80 za Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2015/16 licha ya halmashauri hiyo kupata hati safi.

  Dkt Nchimbi amesema wamekuwa ndio wazalishaji wakubwa wa hoja tena hoja zenyewe zikionyesha udhaifu wao wa kutotimiza wajibu wao huku akiwaeleza kuwa hoja hizo zinaonyesha kuwa kuna udhaifu katika utendaji wao.

  “Hoja hazitengenezwi na madiwani, ni nyinyi watendaji kwa uvivu, mnashindwa kufuata taratibu hadi mnazalisha hoja, mmekuwa ni kiwanda na kiwanda chenyewe kibaya cha kuzalisha hoja, badilikeni”, amesisitiza Dkt Nchimbi.

  Aidha amewataka madiwani kuwa wasimamizi wa miradi na shughuli za serikali pamoja utendaji wa watumishi ili wasiendelee kuzalisha hoja kwakuwa utendaji ukilega lega unawaathiri wananchi ambao ndio wamewaamini ili wawakilishe.
   Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza katika baraza maalumu la madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakati wa kujadili hoja za Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu na Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally Mwanga.
   Watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi katika baraza maalumu la madiwani la kujadili hoja za Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.
   Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Rustika Turuka akizungumza katika baraza maalumu la madiwani la kujadili hoja za Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.
  Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi katika baraza maalumu la madiwani la kujadili hoja za Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


older | 1 | .... | 1812 | 1813 | (Page 1814) | 1815 | 1816 | .... | 3286 | newer