Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

RC Rukwa aitahadharisha Manispaa ya Sumbawanga kutumia vizuri Bilioni 1.1 za ukarabati Kantalamba

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amewataka wale wote wanaohusika na usimamizi wa fedha za ukarabati wa moja ya shule Kongwe nchini, kuhakikisha kuwa fedha hizo zinatumika kama zilivyokusudiwa.

Ameyasema hayo baada ya kuzungukia maeneo yote ya shule yanayoendelea kukarabatiwa wakati alipofanya ziara ya kushtukiza ili kujionea hatua waliyofikia katika ujenzi na kutathmini kama thamani ya pesa inakwenda sambamba na ujenzi unaoendelea katika shule hiyo.

Shule ya Sekondari ya Kantalamba ni miongoni mwa shule kongwe 20 nchini ambazo serikali kupitia Wizara ya Elimu imeweka mpango wa kukarabati shule hizo kwa lengo la kutunza hadhi na kuziboresha zaidi. Ambapo shule hiyo imepata mgawo wa shilingi 1,123,353,700/=
“Tafadhalini sana Mwalimu Mkuu, Mkurugenzi, Afisa Elimu na sisi wote tuhakikishe kwamba shule hii imebadilika kwa kuwa hizi pesa si kidogo, bilioni sio hela kidogo, zisichezewe, zifanye kazi iliyokususdiwa na kazi yenyewe ioneshe sura ya bilioni, isijekutokea tukapata kazi nyingine ya kusema kwamba hizi pesa kazi iliyofanyika ni ya hovyo hovyo,” Mh. Zelote Alisisitiza.


Baada ya kuona juhudi zinazoendelea katika ukatabati huo Mh. Zelote amesifu uongozi wa shule wa kuajiri mafundi vijana waliopo mtaani ili kuwa na matumizi mazuri ya fedha hizo tofauti na kuwatumia wakandarasi ambao wangesababisha fedha nyingine zipotee bila ya sababu, na kusisitiza kuwa vijana hao wasimamiwe kwa ukaribu sana na kupewa maelekezo ili wasilipue kazi inayoendelea.  

Pamoja na hayo Mh. Zelote alilisisitiza uwazi kwenye matumizi ya fedha za umma, na kuwataka wakaguzi kuwa makini na kukagua kila hatua ya ujenzi na kuona kuwa kila senti inayotumika inaendana na thamani ya ujenzi inayoonekana. Aidha alizitaka Halmashauri zote Mkoani Rukwa kutenga bajeti kwa kupitia mapato yake ya  ndani ili kuboresha miundombinu ya shule jambo ambalo linaweza kubadilisha muonekano wa shule nyingi mkoani humo.
“Ningependa kuona shule hii inakuwa ya mfano kwakuwa ipo katika makao makuu ya mkoa na pia alishauri kujenga uzio na kuendeleza utunzaji wa mazingira kwa kuweka sharia kali kwa wanafunzi ili waendelee kutunza mazingira ya shule,” Mh. Zelote aliongezea.  

Awali alipokuwa akisoma taarifa fupi ya ukarabati wa shule kongwe Sekondari ya Kantalamba mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Martin Kasansa alitaja changamoto kadhaa zinazorudisha nyuma kasi ya ukarabati wa shule hiyo ikiwemo uchakavu mkubwa wa bwalo uliosababisha kuanza upya ujenzi, upatikanaji wa baadhi ya vifaa mkoani Rukwa kuwa mgumu na kulazimika kuagiza kutoka mkoa wa Mbeya na kutopatikana kwa maji kumechelewesha ujenzi unaoendelea.  

“Kazi ya ukarabati ilianza rasmi mwezi June 2017 na inasimamiwa na mwandisi kutoka Chuo cha Sayansi na teknolojia Mbeya na inategemewa kumalika ndani ya miezi mitatu, lakini upatikanaji wa maji umekuwa ni tatizo katika eneo letu, ” Martin Alisema.
Ukarabati unaoendelea katika shule hiyo unahusisha mabweni 6, vyumba vya madarasa 14, ofisi za walimu, vyoo, mfumo wa maji safi na maji taka, mfumo wa umeme, jiko, bwalo, maabara pamoja na jingo la kilimo. Ambapo mapaka sasa Shilingi 648,051,540.90/= imeshatumika na kufikia asilimia Zaidi ya 58.

Nae Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Bernard Makali aliutaka uongozi wa shule kuangalia maeneo muhimu na kuweaza kuyamalizia ili wanafunzi wasiachwe nyuma na muhula wa mwaka huu na kusisitiza kuwa upishi wa kutumia kuni si mzuri na kuahidi kushikiana nao kutafuta namna ya kupikia kwa kutumia gesi jambo ambalo litatunza mazingira. 

JAFO ATOA AGIZO KWA MAAFISA WA ELIMU KUBORESHA MAZINGIRA YA SHULE

$
0
0

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo ameagiza maafisa elimu nchini kuboresha mazingira ya shule za msingi na sekondari katika halmashauri zao wanazoziongoza ili ziwe na mandhari ya kuvutia.

Jafo ametoa maagizo hayo alipokuwa akitembelea ujenzi wa madarasa, vyoo, na mabweni katika wilaya ya Kisarawe.

Katika ziara yake, Jafo amefurahishwa sana na ujenzi unavyo endelea wilayani humo kwa ulazaji wa matofali katika majengo yote kutokana na ujengaji wa aina hiyo unayafanya majengo kuwa na ubora mkubwa.

Naibu Waziri Jafo ametaka mazingira ya shule zote nchini yawe safi kwa kupanga mawe pembeni na barabara, kupanda majani, maua na miti ili shule ziwe kivutio kwa watoto.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Maneromongo katika mkutano wa kuhamasisha maendeleo. 
Ujenzi wa madarasa na mabweni unaoendelea katika shule ya sekondari Maneromango 
Wananchi wa kata ya Maneromango wakiwa katika mkutano wa pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akishuhudia upangaji wa mawe katika moja ya majengo yanayojengwa wilayani Kisarawe. 


MASTER MIYAZATO WA OKINAWA GOJU RYU KARATE AMPANDISHA NGAZI SENSEI FUNDI RUMADHA.

$
0
0
Sensei Fundi Rumadha amefanya na kufaulu vizuri mitihani wake wa kupanda ngazi toka Dan ya tatu "Sandan" kwenda ngazi ya nne "Yondan" chini ya waamuzi (masters) toka Okinawa wakiongozwa na Sensei Yoshihiro Kancho Miyazato, ambaye ni Master au mwalimu mkuu wa Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu Karate-Do.
Hilo limejiri katika semina (Gasshuku) ya Masensei toka Ujerumani, Ureno, Uingereza, Japan, na Tanzania katika semina "Gasshuku" iliyofanyika jijini Warsaw, Poland, mwishoni mwa juma liliopita.
Sensei  Rumadha sasa ana mamlaka ya kuwasaidia wanafunzi wake wa Tanzania na kuwafanyia mitihani na kuwapa "Dan" hadi ngazi ya pili " Nidan" sababu katika Goju Ryu Karate  kuanzia Dan ya 3 na kuendelea hutolewa na Master Miyazato pekee.
"Ni matumai yetu wanachama wa Jundokan So Honbu Tanzania kujiwajibisha kimafunzo, na kuimarisha umadhubuti wa mbinu (techniques)  kuliko kulenga sana ngazi bila msingi mzuri kimafunzo, hasa katika kufanya "Kata" na "Bunkai". anasema Sensei Fundi Rumadha.
Sensei Rumadha, ambaye  sasa anashikilia ngazi ya daraja la nne  (Yondan) na mwenye uzoefu na umahili  wa Goju Ryu Karate kwa zaidi ya miaka 38, alitoa Shukran zake kwa mlezi wake wa mafunzo tokea utotoni, Mwalimu "Sensei Magoma Nyamuko Sarya chini ya uongozi wake "Bomani Brigade" kama ilivyojilikana "BB" na mwanzilishi mwanzilishi wa Okinawa Goju Ryu Tanzania mwaka 1973,  hayati Sensei Nantambu Camara Bomani. 
Tanzania na Angola zinatarajiwa kuhudhuria maadhimisho ya miaka 65 tangu kuanzishwa kwa chama cha "Jundokan" na Master Eiichi Miyazato Sensei huko Naha City, Okinawa, mwezi wa Novemba 1918. Chama hicho kwa sasa kinaongozwa na mwanawe Yoshihiro Kancho Miyazato, ambaye pia ni Mwenyekiti mkuu dunia wa chama hicho na mwanae Master Eiichi Miyazato.
Sensei Miyazato amewafanyia mitihani ya mikanda myeusi zaidi ya walimu 15 toka ngazi ya pili" Nidan" hadi ngazi ya saba "Nanadan". Ngazi hizi zote kwa utamaduni wa mtindo huu wa Okinawa Goju Ryu huchukua miaka mingi sana kupandishwa ngazi ambapo ni tofauti na mitindo mingine. 
Kongamano la Karate mtindo wa Goju Ryu la Jundokan So Honbu hufanyika kila mwaka nchi za Ulaya kwa kutembelewa na wakuu wake toka katika visiwa vya Okinawa ili kuwasahihisha mbinu za mafunzo na mikakati mipya ya chama, na  walimu toka nje ya bara la Ulaya kwa muda wa miaka zaidi ya miwili sasa ikiwemo Tanzania na Angola hualikwa. 
 Mwaka huu mitihani imefanyika kwa usimamizi wa walimu wakuu (Masters) watano chini ya mwenye kiti sensei Yoshihiro "Kancho" Miyazato, Tetsu Gima sensei, Tsuneo Kinjo sensei na Miyazaki sensei na mjumbe mwingine pia. 
Wakuu hao wa Okinawa Goju Karate  wametilia mkazo na msisitizo mkubwa sana kuzimudu mbinu kwa kina na matumizi yake, na pia kuandaa watoto wadogo kwani ndio walimu wa kesho. 
 Mengine  juu la misafara hii ni kuwajumuisha masensei wote wa chama cha Jundokan So Honbu, kuwasahihisha na kuwafundisha mbinu za kupanda ngazi mbalimbali  ili kupunguza  gharama za kwenda Okinawa, Japan. kimafunzo.
 Sensei Fundi Rumadha akikabidhiwa hati baada ya  kufaulu vizuri mitihani wake wa kupanda ngazi toka Dan ya tatu "Sandan" kwenda ngazi ya nne "Yondan" toka kwa   Sensei Yoshihiro Kancho Miyazato, ambaye ni Master au mwalimu mkuu wa Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu Karate-Do ya Okinawa, Japan.
 Sensei Fundi Rumadha akipongezwa kwan kupanda ngazi toka Dan ya tatu "Sandan" kwenda ngazi ya nne "Yondan" chini ya waamuzi (masters) toka Okinawa wakiongozwa na Sensei Yoshihiro Kancho Miyazato, ambaye ni Master au mwalimu mkuu wa Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu Karate-Do.
Sensei Fundi Rumadha akiw na waamuzi  toka Okinawa wakiongozwa na Sensei Yoshihiro Kancho Miyazato (katikati), ambaye ni Master au mwalimu mkuu wa Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu Karate-Do.
Masensei toka Ujerumani, Ureno, Uingereza, Japan, na Tanzania katika semina "Gasshuku" wakiwa na furaha nyingi baada ya kupandishwa daraja.

PROF. MBARAWA: FIDIA ZITALIPWA KWA WANAOSTAHILI KISHERIA

$
0
0

Serikali imesema itawalipa fidia kwa mujibu wa sheria wananchi wote waliopisha ujenzi wa barabara katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Amesema hayo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati akizungumza na wananchi wa Mwigumbi mkoani Shinyanga alipokagua ujenzi wa barabara ya Mwigumbi – Maswa yenye urefu wa KM 50.3 inayojengwa kwa kiwango cha lami na mkandarasi wa Kampuni ya CHICO na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wake ambao unagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 61.

“Kila anayestahili kulipwa fidia atalipwa kama sheria inavyoelekeza na endapo akatokea yeyote mwenye malalamiko Serikali ipo itamsikiliza”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi na Viongozi wa Wakala wa Barabara (TANROADS), wa mkoa ili kuhakikisha barabara hiyo inakamilika kwa wakati na spidi inayotakiwa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akipokea taarifa kutoka kwa Mkandarasi wa Kampuni ya CHICO (katikati), anayejenga barabara ya Mwigumbi-Maswa KM 50.3 inayojegwa kwa kiwango cha lami ambao ujenzi wake umefikia takribani asilimia 77. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Mwigumbi, wakati alipokagua ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa KM 50.3 inayojengwa kwa kiwango cha lami. 
Muonekano wa sehemu ya Barabara ya Mwigumbi-Maswa KM 50.3 inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Shinyanga. 
Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mwanza Eng. Marwa Rubirya (kushoto), akitoa taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), kuhusu maendeleo yaliyofikiwa ya ujenzi wa barabara ya Usagara-Kisesa KM 16.135 inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani humo 

Muonekano wa sehemu ya Barabara ya Usagara-Kisesa KM 16.135 inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Mwanza. 

MICHUZI TV: BAR YA VAMPONJI FOREST JIJINI MBEYA YANUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO

BANK OF AFRICA YAKABIDHI GREDA KWA MTEJA WAKE

$
0
0
BANK OF AFRICA imekabidhi rasmi mtambo wa ujenzi (Greda jipya aina ya JCB) lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 300 kwa kampuni ya Dezo Civil Contactors Limited, kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo kandarasi ya ujenzi wa kuta kwenye Pwani ya Bahari ya Hindi.

Makabidhiano ya mtambo huu ni sehemu ya mpango endelevu wa benki wa kununua na kukodisha mitambo (lease finance), ambayo inawawezesha wateja kujiongeza kiutendaji kwa kupata vifaa vya kisasa bila ya kulazimika kuwa na pesa taslimu za manunuzi ya vifaa hivyo.

Makubaliano haya ya ukodishaji wa mitambo yanaakisi katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi, usafirishaji, teknolojia ya habari na mawasiliano, utalii, madini, mafuta na gesi.

BANK OF AFRICA imebaini huu ni mpango ambao una tija kubwa kwa wajasiriamali wakubwa kwa wadogo, kwa ajili ya kufanikisha uendeshaji wa biashara zao ambao utaongeza uzalishaji na faida kubwa. Mteja kupitia mpango huu anapewa fursa pana ya kufanya chaguo lake bila kikwazo chochote na bila ya uhitaji wa amana ya awali au dhamana nyingine. Marejesho ni malipo ya ukodishaji ya kila mwezi na mteja ana uwezo wa kuchagua kua mmiliki wa mali husika pindi ifikapo mwisho wa mkataba wa ukodishaji.

Benki humsaidia mteja kuhakiki chombo anachotaka kuingianacho mkataba kama kina ubora ili kuweza kuinua uchumi wake na uchumi wataifa kwa ujumla.
Naibu Mkurugenzi mtendaji wa BANK OF AFRICA TANZANIA Bw. Wasia Mushi akikabidhi mfano wa funguo kuashiria makabidhiano ya Greda kwa Mteja Bw. T Hitesh Vishram ambae ni Project Supervisor wa Kampuni ya Dezo Civil Contractors Limited, Katikati ni meneja wa masoko, Utafiti na maendeleo wa BANK OF AFRICA TANZANIA Bw. Muganyizi Bisheko.

ESRF YAANDAA MKUTANO KUJADILI BIASHARA NA UWEKAZAJI KATI YA TANZANIA NA CHINA

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango akisoma hotuba kwa niaba ya Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanachama wa Chama cha Wanafunzi walisomea China (CAAT), Linas Kahisha akielezea uzoefu wake katika fursa za kibiashara nchini humo katika mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Tanzania nchini China, Mh. Mbelwa Kairuki akizungumzia namna ambavyo watanzania wanaweza wakafaidika na fursa za biashara na uwekezaji nchini China wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA


TAHMEF YATOA HUDUMA BURE YA UPIMAJI WA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI WILAYANI KONDOA KATIKA KUADHIMISHA MWAKA MMOJA TANGU KUANZISHWA KWAKE

$
0
0
TAHMEF (Tanzania Health and Medical Education Foundation) ni shirika lisilo la kiserikali (NGO), lililozinduliwa rasmi tarehe 8 Julai 2016 na Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, watoto na wazee Mhe Dr. Hamisi Kigwangalla.

Tarehe 8 Julai 2017 TAHMEF ilitimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake, na katika maadhimisho hayo TAHMEF imetoa huduma bure ya upimaji wa Saratani ya shingo ya kizazi, wilayani Kondoa, mkoani Dodoma katika viwanja vya hospitali ya Wilaya.

Zoezi hilo liliendeshwa kwa Muda wa siku mbili (8-9 julai 2017) zaidi ya wanawake 500 Wilayani kondoa walijiandikisha na kupata huduma bure ya elimu na upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi.

Hivi sasa TAHMEF inaendesha mradi uitwao NURU YA AFYA unaolenga kuwezesha wanawake wasio na ajira rasmi na kuendelezwa harakati za kumfikia kila mtanzania kupitia utoaji wa huduma za afya bure kwa wale wenye kipato cha chini pia kuchangia vifaa na mahitaji mengineyo ya hospitali katika vijiji mbalimbali, kuongeza uelewa na ufahamu wa watanzania juu ya changamoto mbalimbali za afya na jinsi ya kukabili changamoto hizo mapema.

TAHMEF inatoa Shukrani za dhati kwa PSI na uongozi wote wa Mkoani Dodoma kwa ushirikiano mkubwa ulioleta mwitikio mzuri kwa wakazi wa kondoa na kufanikisha zoezi zima
 Wanawake wakazi wa Kondoa  wakipewa elimu juu ya Saratani ya shingo ya kizazi kabla ya kupewa huduma ya upimaji wa saratani ya shingo ya Kizazi.
Wanawake wakazi wa Kondoa  wakisubiri kupewa huduma ya upimaji wa saratani ya shingo ya Kizazi.

BENKI YA NMB YASHINDA TUZO YA BENKI BORA YA MAENDELEO AFRIKA 2017

$
0
0
BENKI ya NMB PLC imeshinda tuzo mbili katika sherehe za utoaji wa tuzo wa benki bora duniani zilizofanyika Jijini London, Uingereza. NMB Imetajwa kwa mara ya kwanza kuwa ni Benki Bora ya Maendeleo Barani Afrika huku tuzo ya pili ikiwa ni Benki Bora Tanzania 2017 hii ni mara ya Tano Mfululizo.

Kila Mwaka, Jarida la Euromoney huandaa hafla ya kuyatambua zaidi ya Makundi 20 ya bidhaa za kitaasisi za kifedha zikiwemo benki kote duniani kwa kuagalia benki bora na ya kiwango cha juu kwa kila bara na benki bora katika nchi takribani 100 duniani kote. Tuzo hii huzitambua taasisi za kifedha duniani kote ambazo zimepata mafanikio ya hali ya juu katika maeneo yao, kwa kuonyesha ugunduzi na kupata mafanikio ya kifedha kila mwaka.

Jarida ya Euromoney liliandika kuwa,“NMB siyo benki iliyo hai bali ni benki inayofanya kazi. Maamuzi makubwa yanafanyika kwenye maeneo ya mtaji, biashara na watu yamekuwa yanafanyika. Katika maboresho hayo, bado benki imeweza kutoa gawio zuri kwa wanahisa kuliko taasisi yoyote ya fedha nchini.”

Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker alisema kuwa ubunifu katika huduma, tekinolojia na uwekezaji katika fedha za kielektroniki kwa msaada wa mtandao mpana wa matawi na ATM imechangia kuiboresha benki na kuifanya taasisi bora ya kifedha nchini.

“Kutatua changamoto za jamii ya watu wasiotumia huduma za kibenki nchini inachukua uwekezaji, ubunifu na uwezo wa kuwaleta wadau katika malipo na huduma zingine za kifedha,” alisema bi Ineke

Bi Ineke alisema “kuwa ushindi wa tuzo mbili kwa mpigo za benki ya maendeleo Afrika na benki Bora Tanzania ni kielelezo tosha kuwa juhudi zetu zinaonekana situ Tanzania bali Afrika nzima.”

“Tunatoa shukrani zetu wa wateja, wafanyakazi na washika dau wote kwa kuwa sehemu ya mafanikio haya makubwa kwa benk, “ alisema Bi Ineke na kuongeza kuwa NMB itaendelea na ahadi yake ya kuwapa huduma bora wateja wake sasa na siku za mbeleni.

Akizungumza kwenye hafla, Mhariri wa jarida la euromoney Bwana Clive Horwood alisema “mchuano wa kupata tuzo mwaka huu ulikuwa wa ushindani sana katika taasisi zilizoshiriki na hivyo kufanya uamuzi kuwa mgumu sana Benki zilizoshinda na kujipatia tuzo zetu zimechukua hatua kubwa katika mipango yao ya kibenki. Mabenki huko miaka ya mbele yatakuwa yanaangalia nini unafanya na pia nini ambacho hukifanyi. Mwaka huu, benki zilizong’ara zimetafsiri kwa unaga ubaga ni wapi kwenye nguvu Zaidi na kuzingatia maeneo hayo.”

RC Gambo awataka watendaji kutatua kero za wananchi

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho M. Gambo awaagiza viongozi wa serikali ya kijiji , kata, tarafa, Halmashauri na wilaya  kuhakikisha wanatenga muda wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua ikiwa ni sambamba na kutekeleza  majukumu yao kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo ili kuleta tija kwa serikali na wananchi, aidha mkuu huyo wa mkoa ameeleza hayo alipokua kwenye ziara yake ya siku tano kwenye halmashauri ya Meru alipokua kwenye kikao chake na  watumishi wa Halmshauri makao makuu,maafisa watendaji wa kata,maafisa tarafa pamoja na madiwani.
Sehemu ya Wananchi wa Halmashauri ya Meru Jijini Arusha wakiwa kwenye Mkutano wa pamoja na Mkuu wa Mkoa wao pamoja na watendaji.

IGP SIRRO AFANYA MABADIRIKO YA KAWAIDA KWA MAKAMANDA WA POLISI

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Saimon Sirro,  amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni pamoja na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga.

Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kamishna  Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Suzan Salome Kaganda amekuwa Mkuu wa kitengo cha Mafao na Fidia  Makao Makuu ya Polisi, na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Murilo Jumanne Murilo ambaye alikuwa kamanda Polisi Mkoa wa Shinyanga.

Aidha, Nafasi ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Simon Sylverius Haule, ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu  wa Polisi wa Mkoa wa Mara.

Uhamisho huo ni mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya  Jeshi la Polisi katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.

Imetolewa na:
Barnabus D. Mwakalukwa - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.

MAGAZETI YA JUMANNE LEO JULAI 18,2017

Ratiba ya msiba wa marehemu Professor Henslay William Kabisama

$
0
0

Ndugu, Jamaa, Marafiki, wanafamilia na wote  tuliopatwa na msiba huu wa marehemu Professor  Henslay William Kabisama uliyotokea huko Ontario, California, Marekani, mnaarifiwa kwamba familia itawasili siku ya Jumatano Julai 19, 2017 usiku na maombolezo yataanza siku hiyo hiyo  nyumbani kwa marehemu Ursino  Victoria nyuma ya Ofisi za Halotel.

Siku ya Ijumaa  Julai 21, 2017 Mwili wa mpendwa wetu Prof Henslay Kabisama utawasili  uwanja wa ndege wa Julius Nyerere saa tisa mchana.
Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi Julai 22, 2017  katika makaburi ya Kinondoni, yakitanguliwa na ibada ambayo itafanyika  katika kanisa la   St Alban Upanga saa saba kamili mchana.
 Bwana alitoa na bwana ametwaa jina bwana libarikiwe - AMEN.

BADO WIKI 6 TU KWA ILE BASH YA OLD SCHOOL REUNION KUBAMBA COLUMBUS OHIO

$
0
0

HOTELS IN COLUMBUS

Hampton Inn Columbus I-70 E/Hamilton Road
2093 S Hamilton Rd, Columbus, OH 43232
hamptoninn3.hilton.com
(614) 552-2400

Holiday Inn Express & Suites Columbus Southeast
4041 Hamilton Square, Groveport, OH 43125
ihg.com
(614) 920-2400

Hawthorn Suites by Wyndham Airport Columbus East
2084 S Hamilton Rd, Columbus, OH 43232
wyndhamhotels.com
(614) 864-8844

La Quinta Inn Columbus Airport Area
2447 Brice Rd, Reynoldsburg, OH 43068
laquintacolumbusairport.com
(614) 866-6456

Comfort Suites Columbus
5944 Scarborough Blvd, Columbus, OH 43232
choicehotels.com
(614) 552-2525

Days Inn & Suites Columbus East Airport
2100 Brice Rd, Reynoldsburg, OH 43068
wyndhamhotels.com
(614) 864-1280

Courtyard by Marriott Columbus Airport
2901 Airport Dr, Columbus, OH 43219
marriott.com
(614) 475-8530

MWALIMU COMMERCIAL BANK (MCB) YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA "WEKA AKIBA NA USHINDE"

$
0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

WATEJA wanne wa Mwalimu Commercial Bank PLC wamejishindia zawadi za IPAD na vocha za manunuzi baada ya kuibuka washindi kwenye Droo iliyochezeshwa na benki hiyo kufuatia kweney promosheni ya “Weka Akiba na Ushinde” kwa Wateja wake na wananchi kwa ujumla.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 18, 2017 wakati wa kukabidhi zawadi za washindi, Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko cha benki hiyo, Bw. Valence Luteganya, (pichani juu), alisema, Droo hiyo ilikuwa wazi kwa wateja wote waliopo na watakaojiunga na benki kwa kufungua akaunti kwa kuweka akiba ya Shilingi 50, 000 au zaidi.

Akifafanua zaidi Bw. Lutenganya alisema, kampeni hiyo ilizinduliwa Mei 18, 2017 na wamepokea wateja wengi ambao walishiriki kwenye Droo hiyo iliyochezeshwa chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha, (Gaming Board of Tanzania).

Aliwaja washindi hao kuwa ni pamoja na Bw. Shukuru Sanga, kutoka Waning’ombe mkoani Njombe ambaye alijinyakulia IPAD, wakati Bw. Benester Lazaro, na Grace Machemba kutoka Dar es Salaam, walijinyakulia vocha za manunuzi kama ilivyo kwa Bi. Joyce Sangusangu kutoka mkoani Dodoma.
Meneja wa Tawi la Samora la Benki ya Mwalimu, (Mwalimu Commercial Bank, Plc), Leticia Ndongole, (kushoto), akimkabidhi IPAD, Bw. Shukuru Sanga kutoka Waning’ombe mkoani Njombe, wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni ya “Weka akiba na ushinde” inayoendeshwa na benki hiyo.Hafla hiyo imefanyika leo Julai 18, 2017 kwenye tawi lam benki hiyo Mtaa wa Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam. Wengine ni washindi kutoka kulia, ni Bw. Benester Lazaro na Bi. Grace Machemba wote kutoka Dar es Salaam.
Bw. Lutenganya akiwa na maafisa wa benki hiyo wakati akizungumzia zawadi hizo
Mshindi wa IPAD, Bw. Shukuru Sanga kutoka Waning’ombe mkoani Njombe, akiongea kwa niaba ya washindi wenzake.


RC NCHIMBI : WATUMISHI PUNGUZENI KULALAMIKA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amewataka watumishi kupunguza malalamiko na kuelekeza nguvu zao katika kuhudumia wananchi kwa mambo yanayoonekana kwa macho.

Dkt Nchimbi ameyasema hayo katika baraza maalumu la madiwani wa halmashauri ya Itigi ambapo amewataka watumishi na watendaji kupunguza muda wa vikao ili waende kuwatumikia wananchi.

Amesema kumekuwa na tabia ya kulalamika ambayo pia inaambukiza kwa watumishi na watendaji wengine badala ya kutoa suluhisho kwa changamoto ambazo zitawasaidia wananchi.

Dkt Nchimbi ameongeza kuwa watendaji na madiwani wasitumie muda mwingi ofisini pamoja na kusubiria taarifa za makaratsi ambazo hazina uhalisia wa matukio na hali halisi inayoendelea kwa wananchi.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akimkabidhi Mwenyekiti wa halmashauri ya itigi Ally Minja cheti cha mafunzo ya usimamizi wa miradi ya serikali.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na watumishi, watendaji na madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Itigi (hawapo pichani).
 Baadhi ya watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Itigi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi.
Mkaguzi wa Nje wa Hesabu za Serikali  Anna Kakunguru akizungumza katika baraza maalumu la halmashauri ya Wilaya ya Itigi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DARAJA LA FURAHISHA MWANZA LAKAMILIKA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema ujenzi wa Daraja la waenda kwa miguu lililopo eneo la Furahisha na barabara ya kutoka Furahisha hadi Pasiansi yenye urefu wa KM 2.7, imekamilka kwa asilimia 99 Mkoani Mwanza.

Prof. Mbarawa amesema hayo wakati alipokuwa akikagua maendeleo ya ujezi wa daraja hilo katika ziara yake ya kikazi mkoani humo na kuridhishwa na ukamilishwaji wa ujenzi wake. “Daraja hili litaondoa changamoto kwa wananchi wanaotembea kwa miguu na litapunguza au kuondoa adha ya msongamano wanaovuka kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine”, amesema Prof. Mbarawa. 

Prof. Mbarawa amewataka wananchi kutunza daraja hilo na miundombinu yake ili liweze kutumika kwa muda mrefu kwani limekuwa nembo ya Mkoa wa Mwanza. 

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongela, ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kujenga Daraja la Furahisha kwa kuwa limebadilisha mandhari ya Jiji hilo. “Jiji la Mwanza ni kitovu cha Kanda ya Ziwa, wananchi wameguswa moja kwa moja na mradi wa ujenzi wa daraja hili”, amesema Bw. Mongela. 


Muonekano wa daraja la waenda kwa miguu lililopo eneo la Furahisha, mkoani Mwanza. Ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99 na limejengwa na kampuni ya Nyanza Roads Works. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongela (kulia), wakishuka ngazi za daraja la waenda kwa miguu lililojengwa eneo la Furahisha, alipokagua ujenzi wake mkoani Mwanza. 
Mhandisi Mkazi anayesimamia uboreshaji wa kiwanja cha ndege cha Mwanza Bw. Geofrey Asulumenye, akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, upanuzi wa njia za kurukia ndege katika kiwanja hicho mkoani humo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mkazi Bw. Geofrey Asulumenye (kulia), kuhusu uboreshaji wa kiwanja cha ndege cha Mwanza, alipokuwa akikagua uwanja huo. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA MAMIA KUAGA MWILI MAREHEMU LINAH MWAKYEMBE JIJINI DAR LEO

$
0
0
Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan akiongoza Viongozi mbalimbali wa Serikali,ndugu jamaa na Marafiki katika kutoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa Marehemu Linah George Mwakyembe,mapema leo katika kanisa la KKKT Kunduchi,jijini Dar.Marehemu Linah Mwakyembe aliyefariki mwisho mwa wiki anatarajiwa kusafirishwa leo jioni kwenda wilayani Kyela mkoani Mbeya kwa mazishi.
Pichani wa tatu kulia ni Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo,Dkt Harisson Mwakyembe akiwa sambamba na Familia yake ndani ya kanisa la KKKT Kunduchi wakishiriki kwa pamoja misa ya kuaga mwili wa Marehemu Linah Mwakyembe aliyefariki mwishoni mwa wiki.
Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan akimpa mkono wa pole kwa Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo,Dkt Harisson Mwakyembe,kufuatia kifo cha mke wake mpendwa Linah Mwakyembe,kilichotokea mwishoni wa wiki jijini Dar. 
Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan akitoa salamu za pole wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Linah George Mwakyembe,mapema leo katika kanisa la KKKT Kunduchi,jijini Dar.Marehemu Linah Mwakyembe aliyefariki mwisho mwa wiki anatarajiwa kusafirishwa leo jioni kwenda wilayani Kyela mkoani Mbeya kwa mazishi.
Misa ya kuaga mwili wa Marehemu Linah George Mwakyembe ikiendelea mapema leo katika kanisa la KKKT Kunduchi,jijini Dar.Marehemu Linah Mwakyembe aliyefariki mwisho mwa wiki anatarajiwa kusafirishwa leo jioni kwenda wilayani Kyela mkoani Mbeya kwa mazishi.
Baadhi ya Viongozi wa chama na Serikali wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kuaga mwili wa Marehemu Linah George Mwakyembe,mapema leo katika kanisa la KKKT Kunduchi,jijini Dar.Marehemu Linah Mwakyembe aliyefariki mwisho mwa wiki anatarajiwa kusafirishwa leo jioni kwenda wilayani Kyela mkoani Mbeya kwa mazishi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimfariji Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo,Dkt Harisson Mwakyembe kufuatia kuondokewa na mke wake Linah Mwakyembe mwishoni mwa wiki.

MAMLAKA ZA AJIRA NCHINI ZAAGIZWA KUREKEBISHA TAARIFA ZA WATUMISHI WA UMMA WANAOTARAJIA KUSTAAFU ILI WAPATE STAHILI ZAO KWA WAKATI

$
0
0

Mamlaka za ajira katika utumishi wa umma nchini zimeelekezwa kufanya marekebisho ya taarifa za watumishi wa umma wanaotarajiwa kustaafu ili waweze kupata stahili zao kwa wakati kama inavyostahili.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo - Kata ya Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Mhe. Kairuki amesema wapo watumishi wa umma ambao walipandishwa vyeo lakini muda wao wa kustaafu umekaribia na bado hawajafanyiwa mabadiliko yoyote katika taarifa zao.

“Natumia fursa hii kuwaelekeza waajiri wote katika utumishi wa umma warekebishe taarifa za watumishi hawa wanaokaribia kustaafu ili waweze kupata haki na stahili zao,” Mhe. Kairuki amesema serikali inawajali watumishi wa umma na kuongeza wale ambao tayari wameshastaafu, watafutwe na wajaze fomu maalum za madai kupitia kwa waajiri wao ili serikali iwalipe stahili zao kadri inavyostahili.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo - Kata ya Ubungo alipofanya ziara ya kikazi katika Kata hiyo ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Maji (Water Institute), Dkt. Shija Kazumba akiwasilisha hoja mbalimbali zinazowahusu watumishi wa umma kutoka taasisi anayoiongoza wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo - Kata ya Ubungo kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Afisa TEHAMA wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Dotto Namkaa akiwasilisha mada kuhusu namna ya kujisajili katika Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal) wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo -Kata ya Ubungo kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam. 


BENKI YA NMB YAWALETEA WATEJA WAKE HUDUMA YA TRADE FINANCE ILI KUENDELEZA UCHUMI WA VIWANDA

$
0
0
Benki ya NMB imekuja na huduma yake ijulikanayo kama Trade Finance yenye lengo lakuendana na mabadiliko na kuendeleza Uchumi wa Viwanda nchini.

Trade Finance ni utaratibu wa Benki ambao unamwezesha Mteja kama Mkandarasi, Wazalishaji na Wasambazaji kupata bidhaa na huduma za Kibiashara ndani na nje ya nchi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Warsha fupi iliyoandaliwa na Benki hiyo, Mkurugenzi Mtendaji - NMB, Bi. Ineke Bussemaker amesema kuwa huduma hiyo inahusika na Manunuzi pamoja na kuleta vifaa mbalimbali kutoka nje ya nchi, Usafirishaji wa Vifaa na bidhaa mbalimbali.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo hiko cha Trade Finance, Bi. Linda Mtango Teggisa amesema kuwa Kitengo hiko kinahusika pia katika udhamini kwa Mteja endapo atashindwa kulipia huduma hiyo.

Pia amesema kuwa Benki italazimika kufanya mapitio ya taarifa za Mteja pale inapotokea Mteja huyo kuhitaji dhamana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker akizungumza katika Warsha iliyoandaliwa na Benki hiyo katika kuhusu huduma ya Trade Finance.
Mkuu wa Kitengo cha Trade Finance, Bi. Linda Mtango Teggisa akizungumzia juu ya Kitengo hiko kinahusika pia katika udhamini kwa Mteja endapo atashindwa kulipia huduma hiyo.
Mmoja wa Wataalamu wa huduma hiyo ya Trade Finance katika Benki ya NMB akitoa ufafanuzi kuhusu huduma hiyo inavyofanya kazi kwa Wateja.
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images