Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1813 | 1814 | (Page 1815) | 1816 | 1817 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema mradi wa ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga-Biharamulo yenye urefu wa KM 112 inayojengwa na mkandarasi wa Kampuni ya Synohydro Corporation itakamilika mwishoni mwa mwaka huu.

  Prof. Mbarawa amezungumza hayo mkoani Kagera, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo na kumtaka mkandarasi aongeze kasi ili barabara hiyo iweze kukamilika kwa wakati.

  “Hakikisheni mnaongeza kasi ya ujenzi ili muweze kukamilisha ujenzi huu kwa wakati iwezekanavyo”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.Amemsisitiza mkandarasi kuzingatia viwango vilivyopo katika mkataba kwani mwisho wa siku lazima watanzania wapate barabara inayokidhi mahitaji yao na ubora wake.

  Amewapongeza wasimamizi wa barabara hiyo ambao ni kutoka kwa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kupitia kitengo chake maalum cha wahandisi washauri wazawa (TECU), kwa kuhakikisha wanamsimamia mkandarasi M/S Sinohydro Corporation kwa ukaribu.

  Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Geita Eng. Harun Senkuku amemueleza Waziri Prof. Mbarawa kuwa changamoto ya fidia iliyokuwa inawakabili sasa imemalizika na kiasi cha shilingi milioni 700 zimetumika kukamilisha ulipaji fidia kwa wakazi wote.

  Amemhakikishia Waziri kuwa TANROADS itaendelea kumsimamia mkandarasi huyo ili kuhakikisha thamani halisi ya fedha ya Serikali inapatikana.Mradi wa ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga-Biharamulo KM 112 umehusisha ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga yenye urefu wa KM 45 na barabara ya Bwanga-Biharamulo yenye urefu wa KM 67.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Sinohydro Corporation Ltd anayejenga barabara ya Uyovu-Bwanga KM 45 kwa kiwango cha lami, mkoani Geita.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Bwanga-Biharamulo yenye urefu wa KM 67, mkoani Geita.
  Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Geita Eng. Harun Senkuku akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, kuhusu maendeleo yaliyofikiwa ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga yenye urefu wa KM 45, mkoani Geita. 

  0 0

  Zaidi ya asilimia 80 ya saratani za mlango wa kizazi hutokea katika nchi zinazoendelea, Tanzania ikiwa nchi mojawapo ukilinganisha na Nchi nyingine,kutoka na tatizo hilo maganga mkuu wa mkoa wa ruvuma goziberth mutayhabarwa amewataka wataalamu kuwa na desturi ya kuwa angalia wagonjwa pale wanapokuja kucheki afya zao.Rai hiyo ameitoa wakati wa kufungua mkutano wa siku mbili wa kuhamasisha timu za afya kuhusu saratani ya mlango wa kizazi ,matiti na kifua kikuu.HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE.

  0 0

  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akimueleza jambo Mtaalamu wa kujitegemea kutoka Baraza la Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, liliopo Geneva, Switzerland Ndg. Ikponwosa Ero, nyumbani kwake Mjini Dodoma. katikati ni katibu wa Spika, Ndg. Said Yakubu.
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiwa na ugeni kutoka Baraza la Umoja wa Mataifa lenye Makao Makuu yake Geneva, Switzerland wakiongozwa na Ndg. Ikponwosa Ero (wa pili kushoto) uliomtembelea nyumbani kwake Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akimsikiliza Mtaalamu wa kujitegemea kutoka Baraza la Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Ndg. Ikponwosa Ero ,alipomtembelea nyumbani kwake Mjini Dodoma. katikati ni katibu wa Spika, Ndg. Said Yakubu.

  0 0
  0 0

  Habari zilizonifikia hivi punde zinaeleza kwamba aliyekuwa Jaji wa Mahakama kuu, Jaji Upendo Msuya (pichani), amefariki dunia alfajiri ya leo nyumbani kwake Tegeta jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu. Msiba upo nyumbani kwa marehemu Tegeta.

  0 0

  Imekuwa habari njema kwa wadau wa Efm redio waliopo mikoani ambapo redio haikuweza kuwafikia, sasa Efm redio inasikika katika mikoa mitano ambayo ni Dar es salaam na Pwani kupitia masafa ya 93.7, Mwanza 91.3, Mbeya 103.3 na Mtwara 93.7 na hivi karibuni inatarajia kufikisha masafa yake katika mikoa mingine. Lengo kubwa ni kuhakikisha redio Efm inamfikia kila mtanzania na kuhakikisha jamii inanufaika kupitia matangazo ya vipindi mbalimbali vinavyoenda sambamba na matamasha yanayoendeshwa na redio hii.


  0 0


  Je unajua jinsi TEHAMA inavyoboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma katika Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. Usikose kuangalia kipindi hiki uone jinsi ambavyo TEHAMA inasaidia kuboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma katrina taasisi hiyo

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu (Mb), anatoa pongezi za dhati, kwa wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa kidato cha Sita kwa mwaka 2017, ambapo kiwango cha ufaulu wa matokeo ya kitaifa kimepanda kwa asilimia 0.59 ikilinganishwa na mwaka 2016, huku watoto wa kike wakiongoza kwa ubora mwaka huu.

  Waziri Ummy amempongeza Sophia Juma wa shule ya Sekondari Mazinde juu (Tanga) kwa kushika nafasi ya kwanza, sanjari na Agatha Julius Ninga wa shule ya Wasichana Tabora ambaye ameshika nafasi ya pili kitaifa.

  Kadhalika, Waziri Ummy amewapongeza wanafunzi wote wa kike kwa jitihada walizoonesha na kuweza kufaulu mitihani yao kwa kiwango cha asilimia 97.21 ya waliofanya mtihani; ikilinganishwa na asilimia 95.34 ya wavulana waliofaulu. Waziri ameeleza kufarijika na juhudi ya wanafunzi wa kike, kufuatia ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu kupanda kwa asilimia 94.07 katika madaraja haya ikilinganishwa na wavulana waliofaulu kwa asilimia 93.49. Juhudi hizi sio za kubezwa, na ni ishara thabiti kuwa mtoto wa kike akipewa nafasi hakika anaweza.

  Wizara inatambua ushirikiano wa walimu, wazazi, na jamii ambao wamewezesha kufikiwa kwa ubora wa ufaulu wa watoto wa kike. Juhudi zenu zimesaidia utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kutoa fursa sawa kwa watoto wa kike na wa kiume katika kupata haki ya elimu. Mhe.Ummy amewasa watoto wa kike wa shuleni mbalimbali nchini kutafakari matokeo ya mwaka huu ili kuwa chachu ya kujitambua na kujikinga na mimba shuleni. Kama wanafunzi wa kike watajitambua watasoma kwa ari kubwa kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

  Niwatake watoto wote wa kike waelewe kuwa wamehitimu daraja moja, hata hivyo bado wanalojukumu la kujiendeleza zaidi katika taaluma mbalimbali kama njia ya kumwezesha mtoto wa kike na mwanamke kuchangia katika maendeleo ya taifa kwa umahiri mkubwa.

  0 0

   Rais Dkt John pombe Magufuli mapema leo amefungua barabara ya Kagoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa Kilometa 154. Barabara hii ni muhimu kwa uchumi wa mikoa ya kanda ziwa, kanda ya kati na kanda ya magharibi. Inaunganisha mikoa ya Kagera, Geita, Kigoma, Mwanza, Shinyanga na nchi jirani za Burundi, Uganda na Rwanda
   Rais Dkt John pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya akina Mama waliofika kushuhudia hafla fupi ya ufunguzi wa barabara ya Kagoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa Kilometa 154. Barabara hii ni muhimu kwa uchumi wa mikoa ya kanda ziwa, kanda ya kati na kanda ya magharibi. Inaunganisha mikoa ya Kagera, Geita, Kigoma, Mwanza, Shinyanga na nchi jirani za Burundi, Uganda na Rwanda.

  HABARI ZAIDI TUTAWALETEA BAADAE KIDOGO.

  0 0  Makamu Mwenyekiti wa Yanga  Clement Sanga pamoja na uteuzi wake wa Mwenyekiti na Wajumbe wapya watakaounda  Kamti ya Mashindano ya Klabu hiyo kwa ajili ya msimu mpya wa 2017/18.
  Makamu Mwenyekiti Clement Sanga amemrejesha Maggid Suleiman ambaye atakuwa Mwenyekiti akisaidiwa na makamu Mustapha Urungu huku wakiteuliwa wajumbe wapya 10.
  Sanga atafanya kikao cha kwanza na  kamati hiyo  siku ya jumamosi Saa 4 asubuhi, Makao Makuu ya klabu,jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  TIMU ya Mpakani imefanikiwa kuingia katika hatua ya robo fainali baada ya kuwafunga mahasimu wao Makuburi kwa mikwahu ya penati 5-4.

  Mchezo huo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Ndondo Cup inayoendelea katika Uwanja wa Kinesi, Sinza, Dar es salaam  ulikuwa ni mchezo wa tatu wa hatua hiyo baada ya timu ya Goms United kuanza kufungua milango ya kuingia hatua ya robo fainali kwa kuifunga Burudani. 

  Mechi hiyo iliyokuwa ya ushindani iliweza kumalizika katika dakika 90 bila timu yoyote kuona mlango wa mwenzio na kwenda katika Mikwaju ya penati.
  Beki kisiki wa timu ya Mpakani (jezi ya njano) Issa Rashid Baba Ubaya akiwania mpira na mchezaji wa Makuburi katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Ndondo Cup ambao ulimalizika kwa Mpakani kuibuka na ushindi wa penati 5-4.
  Beki wa kushoto wa timu ya Makuburi Emmanuel Kichiba akiwa na mpira katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Ndondo Cup ambao ulimalizika kwa Mpakani kuibuka na ushindi wa penati 5-4.
  Wachezaji wa timu ya Mpakani na Makuburi wakiwania mpira hewani katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Ndondo Cup ambao ulimalizika kwa Mpakani kuibuka na ushindi wa penati 5-4.
  Manahodha wa timu ya Makuburi na Mpakani wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Ndondo Cup ambao ulimalizika kwa Mpakani kuibuka na ushindi wa penati 5-4.
  Timu za Makuburi na Mpakani wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Ndondo Cup ambao ulimalizika kwa Mpakani kuibuka na ushindi wa penati 5-4.

  0 0

  Jeneza lenye mwili wa Marehemu Linah George Mwakyembe aliyekuwa Mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, ukiwa nyumbani kwao katika Kijiji cha Ikolo, wilayani Kyela mkoani Mbeya. mwili wa Marehemu Linah George Mwakyembe unatarajiwa kuhifadhiwa kwenye nyumba yake ya Milele mchana huu katika Makaburi ya familia, Kijijini kwao Ikolo, wilayani humo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akilakiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel alipowasili nyumbani kwa Dkt. Harrison Mwakyembe, Kijijini Ikolo, wilayani Kyela, tayari kwa Mazishi ya Marehemu Linah George Mwakyembe aliyekuwa Mke wa Dkt. Mwakyembe.
  Prof. Mark Mwandosya akimfariji Dkt. Harrison Mwakyembe aliyefiwa na Mkewe, Linah George Mwakyembe wakati maandalizi ya mazishi yake, Kijijini kwao Ikolo, wilayani Kyela mkoani Mbeya.  Kushoto ni Mke wa Prof. Mwandosya, Bi. Lucy Mwandosya.
  Wakuu wa Mikoa ya Lindi na Njombe, Godfrey Zambi (kushoto) na Ole Sendeka (kulia) wakiwasili nyumbani kwa  Dkt. Harrison Mwakyembe, Kijijini Ikolo, wilayani Kyela.


  0 0  Kikosi cha timu ya Kagera Sugar kimeweka kambi katika Jiji la Dar es salaam kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi Kuu Vodacom 2017/18 inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Agosti.


  Kocha mkuu wa timu hiyo Mecky Mexime amejumuisha kikosi cha zamani na wale wa watakaoungana na wenzao katika kuimarisha timu hiyo kwa ajili ya msimu mpya.

  Katika sura mpya za kikosi cha Kagera Sugar ni Juma Nyoso aliyekuwa anatumikia adhabu ya kufungiwa miaka miwili kutokujihusisha na soka, Omary Daga na Abdala Mguhi kutoka African Lyon iliyoshuka daraja.   Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar wakiwa katika mazoezi ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi Kuu Vodacom 2017/18 .
  Dakatri wa timu ya Kagera Sugar akiganga mchezaji aliyeumia katika  mazoezi ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi Kuu Vodacom 2017/18 .

  Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar wakiwa katika mazoezi ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi Kuu Vodacom 2017/18 .

  Kocha wa timu ya Kagera Sugar Mecky Mexime akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wanaoendelea na mazoezi katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es salaam.Picha na Globu ya Jamii


  0 0

  Serikali haijafuta mafunzo kwa watumishi wa umma ambapo Taasisi za Serikali zimeelekezwa kuandaa Mpango wa Mafunzo kwa watumishi kwa njia ya uwazi na shirikishi ili kuepuka malalamiko kutoka kwa baadhi ya watumishi wa umma.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam.

  Mhe. Kairuki amesema mwajiri anapoandaa Mpango wa Mafunzo kwa watumishi wake ni vyema mpango huo ukawa shirikisha kwa watumishi wote ili kujua mpangilio wake, ikiwa ni pamoja na kuandaa orodha ya ziada ya watumishi watakaochukua nafasi za wale waliopangwa kushiriki mafunzo lakini wakashindwa.

  “Napokea malalamiko mengi sana kuhusiana na upendeleo katika suala la mafunzo, napenda kuwasisitiza waajiri tuandae Mpango wa Mafunzo ambao ni shirikishi kwa watumishi wote kuepuka haya, wengine wanapangwa na hawashiriki mafunzo,” Mhe. Kairuki amesema na kuongeza baadhi ya watumishi wa umma wanapangwa kushiriki mafunzo na hawaendi kwa sababu mbalimbali, lakini fursa ya nafasi hizo hawapangiwi wengine ili kuendana na mpango.

  Mhe. Kairuki ameongeza kuwa Mpango wa Mafunzo shirikishi pamoja na kuondoa malalamiko, utasaidia pia kutorudisha fedha zilizobaki kwa watumishi wa umma ambao walipangwa lakini wakashindwa kuhudhuria mafunzo kwa sababu mbalimbali.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala alipofanya ziara ya kikazi  katika Manispaa hiyo ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema akitoa hotuba ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuzungumza na watumishi wa umma katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Manispaa hiyo Jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Bw, Msongela Palela akiwasilisha taarifa ya manispaa anayoiongoza kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika Manispaa hiyo ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (Hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

  Mthibiti Mkuu Ubora wa Shule – Manispaa ya Ilala, Bi. Juliana Mhonyiwa akiwasilisha hoja wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha watumishi wa umma Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) leo Jijini Dar es Salaam.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

  Na Editha Karlo, Globu ya Jamii-Kigoma
  SHIRIKA la Kimataifa lisilo la kiserikali la EngenderHealth limetoa msaada wa vifaa tiba chini ya ufadhili wa Bloomberg kwa Mkoa wa Kigoma ili kuboresha huduma za afya ya uzazi.
  Akiongea wakati wakukabidhi vifaa hivyo muwakilishi wa shirika la EngenderHealth kutoka makao makuu Dar es Salaam Dkt.Godson Maro alisema kuwa lengo lao ni kuendelea kuboresha huduma za uzazi,ikiwa ni sambamba na kupunguza vifo vya mama na mtoto.
  Dkt Maro alivitaja vifaa walivyotoa msaada kuwa ni pamoja na vitanda vya kujifungulia,mashine za kupima mapigo ya moyo ya mtoto,mzani wa kupima uzito,vitanda vya kupumzikia akina mama baada ya kujifungu,mashine ya kupima mapigo ya moyo ya mtoto akiwa tumboni na drip stand vyote vina thamani ya zaidi ya shilingi milioni 374.
  "Vifaa hivi vitapelekwa katika zahanati mbalimbali zilizopo Mkoani hapa zenye upungufu wa vifaa tiba pia tutaendelea kushirikiana na serekali kuboresha huduma za afya ili kufikia malengo makubwa ya kupunguza vifo vya mama na mtoto"alisema.
  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt Paul Chawote alishukuru kwa msaada huo wa vifaa tiba kwani utawasaidia kutatua changamoto mbalimbali walizokuwa wanakutana nazo katika utoaji wa huduma.

  Dkt Chawote alisema kuwa vifaa hivyo watavitunza vizuri ili visaidie wananchi wengi na kudumu kwa muda mrefu.
  Alisema Mkoa wa Kigoma unachangamoto ya watumishi katika zahanati nyingi na sababu kubwa ni mbiundombinu hasa ya. barabara hali inayofanya watumishi wengi wakipangiwa kazi huwa hawafiki.

  Muwakilishi wa shirika la kimataifa lisilo la kiserekali la EngenderHealth Dkt Godson Maro kutoka makao makuu Dar es Salaam akimkabidhi Mganga mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt Paul Chawote vifaa tiba vilivyotolewa na shirika hilo ili kuboresha huduma ya uzazi kwa mama na mtoto

  Kikosi cha wafanyakazi wa shirika lisilo la kiserekali la kimataifa la EngenderHealth kutoka Dar es salaam na Kigomawakiwa katika picha ya pamoja baada ya makabidhino ya vifaa tiba.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Globu  ya jamii
  Watu wawili, Safina Kassim Rupia na David Faustine Chimomo, wamepandishwa katika kizimba cha mahakama ya hakimu mkazi kisutu na kusomewa mashtaka ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya bilioni 12.7 huku wakikwepa kulipa kodi ya kiasi hicho cha fedha.

  Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa Serikali Mwandamizi Nassoro Katuga amedai mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa, kuwa, kati ya Julai 11 na Oktoba 28,2015 washtakiwa hao wakiwa Azam ICD Sokota walitenda makosa hayo.
  Imedaiwa, siku hiyo washtakiwa walisababisha hasara ya Sh 12,618,970,229 kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa kutoa makontena 329 bila ya kulipiwa kodi.
  Katuga ameendelea kudai kuwa,siku hiyo katika bandari Kavu ya Azam ICD iliyopo Sokota katika wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam washtakiwa hao walisaidia kukwepa kodi ya makontena 329 ambayo kodi yake ilikuwa na thamani ya sh. 12,618,970,229.
  Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote kwa sababu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi ya uhujumu uchumi hadi Mahakama Kuu.
  Kwa mujibu wa wakili Katuga, Upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na washtakiwa wamepelekwa rumande hadi 27,2017 itakapokuja kwa kutajwa.

  Mtuhumiwa David Faustine Chimomo akiwa anatoka  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kusomewa mashtaka ua uhujumu uchumi  na kuisababishia serikali hasara ya bilioni 12.6 huku wakikwepa kulipa kodi ya kiasi hicho cha fedha.


  Mtuhumiwa Safina Kassim Rupia akiwa anatoka  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kusomewa mashtaka ua uhujumu uchumi  na kuisababishia serikali hasara ya bilioni 12.6 huku wakikwepa kulipa kodi ya kiasi hicho cha fedha.


  0 0

  Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

  RAIS Dkt John Pombe Magufuli anatarajia kuanza ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani Kigoma ambapo pamoja na mambo mengine atazindua barabara zenye kiwango cha lami na mradi wa maji.

  Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emanuel Maganga alisema kuwa Rais atawasili mkoani Kigoma kupitia Wilaya ya Kakonko tarehe July 21 akitokea Mkoani Kagera ambapo atafanya uzinduzi wa barabara iliyojengwa kwa kiwango cha lami kutokea Nyakanazi hadi Kibondo yenye kilometa 50.

  Mkuu wa Mkoa alisema pia siku hiyo Rais atafanya mkutano wa hadhara na wananchi katika Wilaya ya Kakonko ili kusikiliza kero zao mbali mbali,pia Rais ataelekea Wilayani Kasulu ambapo pia atazindua barabara kidahwe mpaka kasulu iliyojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 63.

  Maganga alisema July 22 Rais ataweka jiwe la msingi mradi wa maji uliopo Manispaa ya Kigoma Ujiji na kisha atafanya mkutano wa hadhara na wananchi katika uwanja wa Lake Tanganyika.

  Na July 23 Rais ataelekea Wilayani Uvinza kwaajili ya kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji uliopo katika Kata ya Nguruka eneo la amani na baadae mkutano wa hadhara na wananchi.

  Maganga amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais kwani hii ni ziara yake ya kwanza tokea uchaguzi Mkuu ufanyike.
  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia mstaafu Emanuel Maganga akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya ziara ya Rais Dkt John Pombe Magufuli Mkoani Kigoma.

  0 0

  Selemani Jaffo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi) akisikiliza maelezo kutoka kwa mama Abia Magembe kuhusu bidhaa zinazotokana na zao la muhogo. Kushoto kabisa ni Mratibu wa Mradi wa Green Voices kutoka Hispania, Alicia Cebada na kulia ni Mratibu wa mradi huo nchini Tanzania, Secelela Balisidya.

  NAIBU Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jaffo, amesema halmashauri zinawajibu wa kuunga mkono jitihada za utunzaji wa mazingira na kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

  Kutokana na hali hiyo, ameonya mtu yeyote asikwamishe jitihada zinazofanywa na akinamama washiriki wa mradi wa Green Voices Tanzania huku akiahidi kuwa serikali iko nao bega kwa bega. Alisema kwamba, endapo kuna mtu katika idara zilizo chini ya wizara yake atakwamisha jitihada zao, basi akinamama hao wawasiliane naye moja kwa moja.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi wa Green Voices nchini Tanzania uliofanyika kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri Jaffo alisema kwamba, wizara yake ndiyo yenye jukumu kubwa la kuwawekea mazingira mazuri akinamama hao kutekeleza miradi yao chini ya halmashauri husika, hivyo akawaahidi kuwapatia ushirikiano wa kutosha kuhakikisha miradi hiyo inakuwa endelevu na suala la mazingira linapewa kipaumbele.

  Mradi wa Green Voices unatekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Kigoma, Mwanza na Kilimanjaro, kukiwa na miradi 10 ikiwemo ya kilimo cha mihogo, kilimo cha matunda, uyoga, ufugaji wa nyuki, ukaushaji wa mbogamboga na utengenezaji wa majiko rafiki wa mazingira.

  Bidhaa za mbogamboga zilizokaushwa kutoka Morogoro.


  0 0

   Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisaini kitabu cha Maombolezo wakati wa mazishi ya Mke wa Waziri Wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Dkt Harisson Mwakyembe, Marehemu Linah Mwakyembe Wilayani Kyela, Jijini Mbeya.
    Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsabai Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Dkt Harisson Mwakyembe wakati mazishi ya Mke wake, Marehemu Linah Mwakyembe Wilayani Kyela, Jijini Mbeya.
   Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Naibu Spika Dkt Tulia Ackson wakati wa mazishi ya Mke wa Waziri Wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Dkt Harisson Mwakyembe, Marehemu Linah Mwakyembe Wilayani Kyela, Jijini Mbeya.
    Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akitoa Salamu za heshima kwa mwili wa Mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Dkt Harisson Mwakyembe, Marehemu Linah Mwakyembe wakati wa mazishi yake nyumbani kwake Wilayani Kyela, Jijini Mbeya.
   Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa (wa kwanza toka kushoto)Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai, Naibu Spika Dkt Tulia Ackson wakifuatilia misa ya mazishi ya Mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Dkt Harisson Mwakyembe, Marehemu Linah Mwakyembe wakati wa mazishi yake nyumbani kwake Wilayani Kyela, Jijini Mbeya
  Mweyekiti wa Wabunge wa Chuma cha Mapinduzi kutoka Mkoa wa Mbeya Mhe Victor Mwambalasu akizungumza kwa niaba ya Wabunge wa Mkoa huo wakati wa mazishi ya Mke wa Waziri Wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Dkt Harisson Mwakyembe, Marehemu Linah Mwakyembe Wilayani Kyela, Jijini Mbeya. Wengine katika picha ni Wabunge wa Chama cha Mapinduzi kutoka Mkoa wa Mbeya.

  Picha na Ofisi ya Bunge

  0 0
 • 07/19/17--06:54: TAARIFA KWA UMMA


older | 1 | .... | 1813 | 1814 | (Page 1815) | 1816 | 1817 | .... | 3272 | newer