Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

UJUMBE WA TPA WATEMBELEA MAMLAKA YA BANDARI GHANA

$
0
0

Ujumbe wa Tanzania Ports Authority (TPA) ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TPA Prof. Joseph Msambichaka (katikati) unatembelea Mamlaka ya Bandari ya Ghana (GPHA) hapa wakiwa ndani ya chumba cha mawasiliano , wengine katika picha ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Ndg. Kiloyavaha wa pili kulia na Mkurugenzi wa ICT waTPA Ndg. Phares Magesa wa pili kuhoto, na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa ICT wa GPHA na wa kwanza kuhoto ni afisa usalama wa GPHA. TPA hivi karibuni itaanza utekelezaji wa miradi mikubwa ya kuimarisha na kutumia mifumo ya ICT kuongeza ufanisi, kuimarisha ulinzi wa Bandari na kuthibiti usalama wa mizigo ya wateja kuanzia mizigo inapopakiwa kwenye Meli hadi mzigo unapochukuliwa na mteja.

Ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Zanzibar's Maulidi ya Homu Group at Shariah Banking launch in Tanzania mwezi Mei 2010

miondoko ya kumeremeta kwenye mnuso

Mshiriki wa Epic Bongo Star Search Musa Akutana na Vocal Coach Joett

$
0
0

Mshiriki wa Epic Bongo Star Search 2012 akutana na mwalimu wa sauti Joett kwa mawaidha, ushauri na kupokea Jufunze Kuimba na Joett vocal training CD. Blog:http://www.joettmusic.com

KAMA KAWA KAMA DAWA....

OBAMA KARIBU TANZANIA BY DOKII

MKUTANO MKUU WA KNCU WAFANYIKA MJINI MOSHI LEO

$
0
0
Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika mkoa wa Kilimanjaro(KNCU)Maynad Swai akitoa taarifa kwenye mkutano mkuu wa chama hicho unaofanyika katika ukumbi wa Hotel ya KNCU ulioo mjini Moshi.
Kaimu mrajisi wa vyama vya ushirika nchini Bw Peter Rutabanzibwa akizungumza katika mkutano mkuu wa chama cha ushirika mkoa wa Kilimanjaro KNCU.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa chama kikuu cha ushirika mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia kwa makini maelezo ya mwenyekiti(hayupo pichani).
Mjumbe akichangia hoja katika mkutano huo.
Baadhi ya vingozi wa KNCU katika mkutano huo.

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi

Serikali inawasiliana na benki kuu ili kuweka mipango madhubuti ya kuziimarisha na kuziendeleza benki za ushirika nchini ili kuzijengea uwezo wa kuwahudumia wakulima kwa kuvipa mikopo vyama vikuu vya ushirika badala ya kuzitegemea taasisi nyingine za fedha.

Kaimu mrajisi wa vyama vya ushirika nchini Bw Peter Rutabanzibwa amesema hayo katika mkutano mkuu wa chama kikuu cha ushirika mkoani kilimanjaro (KNCU) baada ya wajumbe wake kueleza kutoridhiswha kwake na utendaji wa benki ya ushirika mkoani humo ya kilimanjaro co-operative bank(KCBL).

Bw Rutabanzibwa amesema, lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa benki hizo ikiwemo ya kilimanjaro zinafikiwa kiwango cha juu katika kuwahudumia wakulima hivyo jukumu la wanachama wa vyama vyote vya ushirika nchini na kuziunga mkono benki hizo.

Hata hivyo baadhi ya wajumbe wa mkutano huo walieleza kutoridhishwa kwao na mwenendo wa benki hiyo ambayo imekuwa ikifanya semina za kuvishawishi vyama vya msingi vya ushirika vijitenge na kncu katika biashara ya kahawa na kuuvuruga ushirika.

Kutokana na hali hiyo mwenyekiti wa KNCU Bw Maynard Swai ameutaka mkutano huo utoe tamko juu ya benki hiyo kutaka kuusambaratisha ushirika na kupendekeza wajumbe wawili wa bodi ya wakurugenzi wa KNCU waingie kwenye bodi ya wakurugenzi ya benki hiyo ili kudhiti hali hiyo.

Katika taarifa yake mwenyekiti wa kncu Bw Swai amesema, chama hicho kimeimarisha mtaji wa benki hiyo kwa kuipatia zaidi ya shs. 153.6mil/= kutokana na kilo 1,536,340 za kahawa iliyokusanywa kutoka vyama vya msingi vya ushirika na kuuzwa kwa msimu wa 2009/2010.

TANGAZO LA MSIBA WA KEIZA MAMBOSASA

$
0
0
image
Familia ya Bw. na Bi Ramadhan Mambosasa wanasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao mpendwa Keiza Mambosasa kilichiotokea tarehe 27 Alhamisi huko Mbezi Beach, Dar es salaam.


Sala ya marehemu itafanyika katika msikiti wa Mzimuni, Kawe, saa saba alasiri, na baada ya hapo mazishi yatafanyika huko Mwanakilenga  Bagamoyo.

 Sisi tulikupenda lakini Mungu alikupenda zaidi
Mungu akulaze mahali pema peponi…
AMINA




JK akifungua mkutano wa Global Smart 2013 Smart Partnership Dialogue

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU YAONGEZA MUDA WA MAOMBI YA MIKOPO KWA MWAKA WA MASOMO 2013/2014

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawafahamisha waombaji wa mikopo kwa mara ya kwanza, Wanafunzi wanaondelea na masomo na Umma kwa ujumla kuwa muda wa maombi ya mikopo umeongezwa kwa mwezi mmoja hadi Julai 31, 2013.
 
Pamoja na nyongeza hii ya muda, Bodi inasisitiza waombaji kujaza fomu za maombi ya kwa njia ya mtandao (OLAS) kwa usahihi na kuzingatia muda wa maombi uliowekwa ili kuepuka usumbufu usio wa lazima. Waombaji wa mara ya kwanza wahakikishe wanajaza kwa ufasaha na kuweka viambatanisho vyote muhimu ili kufanikisha mchakato wa uchambuzi na upangaji wa mikopo.  
 
Kundi la kwanza la wanafunzi waliopangwa kulitumikia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambao wamemaliza mafunzo hayo mwezi Juni, 2013 wanapaswa kutumia fursa hii kujaza fomu za maombi ya mikopo bila kukosa. Aidha, kundi la pili la wanafunzi wanaotegemea kuanza mafunzo hayo mwezi Julai, 2013 walitakiwa wawe wameshaomba mikopo kati ya tarehe 1 Mei, 2013 na 30 Juni, 2013 lakini endapo kuna wachache ambao hawakuweza kufanya hivyo basi nao watumie muda huu wa nyongeza kujaza fomu za maombi kwa njia ya mtandao wakiwa huko huko JKT.
 
Endapo mwombaji yeyote atakabiliana na matatizo wakati wa kujaza fomu yake anashauriwa kupiga simu kwenye dawati la huduma kwa wateja kwa namba 022 550 7910 kati ya saa 2.00 asubuhi na saa 2.00 usiku siku za Jumatatu hadi Ijumaa, na kati ya saa 2.00 asubuhi na saa 10.00 jioni siku za Jumamosi.
 
Ikumbukwe kwamba Bodi haitaongeza muda wa ziada baada ya Julai 31, 2013 ili kutoa nafasi kwa Bodi kuendelea na mchakato wa uchambuzi na upangaji mikopo.
 
IMETOLEWA NA:
BODI YA WAKURUGENZI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

Twanga Pepeta kuzindua albam yao ya 10 kesho Leaders Club

$
0
0
BENDI ya African Stars “Wana Twanga Pepeta” kesho Jumapili itazindua albamu yake 10 ijulikanyo kwa jina la Nyumbani Ni Nyumbani kwenye viwanja vya Leaders Club huku ikisherehekea miaka 15 tokea kuanzishwa kwake.

Uzinduzi huo utapambwa na michezo mbali mbali kuanzia saa 3.00 asubuhi ambapo timu nane za mpira wa miguu zitawania zawadi mbali mbali katikamichuano ijulikanalo kwa jina la ASET Bonanza. Timu hizo zitaongozwa na ile ya waandishi wa habari za michezo, Taswa FC na nyingine kama Brake Point, Mango, Namanga, Kivukoni, Camp Combine, Wagadau na Kunduchi.

Mbali a burudani kutoka kwa Twanga Pepeta, siku hiyo pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wanamuziki wa kizazi kipya, Linex, Barnaba, bila kusahau, wakongwe wa muziki wa dansi nchini, bendi ya Mlimani Park maarufu kwa mtindo wa Sikinde Ngoma ya Ukae.

Mkurugenzi wa kampuni ya ASET inayomili bendi hiyo, Asha Baraka alisema kuwa bendi inayoundwa na wanamuziki chipukizi au Yosso, Aset Academia nayo itatoa burudani ya utangulizi katika uzinduzi huo uliodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, Clouds Media Group, Radio One na CXC Africa.

Asha alisema kuwa wamejipanga kukoga nyoyo za mashabiki siku hiyo kwani wameandaa shoo mbali mbali zijulikanazo kwa jina la Twanga 2013 na nyimbo zao mpya zilizomo kwenye albamu hiyo ambazo ni Nyumbani ni Nyumbani uliyotungwa na Kalala Junior, Ngumu Kumeza (Ibrahim Mpoyo), Mwenda Pole (Badi Bakule), Kila Nifanyalo (Jumanne Saidi), Shamba la Twanga (Greyson Semsekwa na Twanga 2013 ambao ni utunzi wa wanamuziki wote wa bendi hiyo.

Albamu nyingine za bendi hiyo ni Kisa Cha Mpemba iliyozinduliwa mwaka 1999, Jirani (2000), Fainali Uzeeni (2001), Chuki Binafsi (2002), Ukubwa Jiwe (2003), Mtu Pesa (2004), Safari (2005),Password (2006), Mtaa wa Kwanza (2007), Mwana Dar es Salaam (2009) na Dunia Daraja iliyozinduliwa mwaka 2011.

Asha alisema kuwa wameamua kufanya hivyo ili kuwakumbusha mashabiki wao wapi walipoanzia (tokea) na wapi wanapokwenda katika muziki wa dansi. Alisema kuwa kimuziki wamepata mafanikio makubwa sana kutokana na kupata mialiko ya kimataifa kama nchi za Ulaya mama Uingereza, Ujerumani, Uholanzi, Finland, Norway na nyingine nyingi.

WABUNGE WA CCM WAKUTANA MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma kuhudhuria kikao cha wabunge wa CCM Juni 29, 2013. Kulia ni Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye.
Mkurugenzi wa Idara ya mambo ya Nje ya CCM, Dr.Asha Rose Migiro akikaribishwa na Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma kuhudhuria kikao cha wabunge wa CCm Juni 29, 2013. Katikati ni Mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa.
Washiriki wa Mkutano wa Wabunge wa CCM wakiimba wimbo wa CCM kabla ya kuanza kwa kikao chao kwenye ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma Juni 29, 2013. Kutoka kulia ni Spika wa Bunge Anne makinda, Waziri Mkuu Mizengo Pinda (mwenyekiti) Katibu Mkuu wa CCm, Abdulrahman Kinana na Jenista Mhagama ambaye ni Katibu.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

RAIS MAHINDA RAJAPAKSA WA SRI LANKA ATEMBELEA MBUGA YA SERENGETI

$
0
0
Rais wa Sri Lanka Mahinda Rajapaksa ambaye yuko nchini kuhudhuria Mkutano wa Global Smart Partneship jana alitembelea Hifadhi ya Taifa Serengeti na kuvutiwa na mandhari nzuri ya Serengeti iliyosheheni wanyama mbalimbali. Rais Rajapaksa aliwasili asubuhi jana na kufanya safari ya utalii wa siku (day trip) akiwa amefuatana na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki. Katika muda mfupi aliotembelea Serengeti aliweza kujionea wanyama mbali mbali kama vile Simba, Tembo, Twiga na makundi makubwa ya pundamilia na nyumbu.

Aidha, kufuatia kuvutiwa na uzuri wa Serengeti Rais Rajapaksa aliahidi kutembelea tena hifadhi hiyo mwezi ujao akiwa na familia yake ili waweze kujionea uzuri wa hifadhi hiyo akiwa na muda wa kutosha pamoja na familia yake.
Rais Mahinda Rajapaksa (katikati) akiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki (kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Butiama Anjelina Mabula mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa Serengeti.
Rais Mahinda Rajapaksa akiaga mara baada ya kutembelea Hifadhi ya Serengeti tayari kwa safari ya kurejea Dar es Salaam.

MASANJA NA SHILOLE WAELEKEA WASHINGTON,DC KWENYE SHEREHE YA MIAKA 3 YA VIJIMAMBO NA TAMASHA LA UTAMADUNI WA KISWAHILI

$
0
0
Wasanii Masanja Mkandamizaji na Shilole wakikwea pipa kuelekea Washington, DC kwenye sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili Marekani litakalofanyika July 6, 2013 kuanzia saa 4 asubuhi (10:00 am) na Rais Mustaafu Ali Hassan Mwinyi ndiye atakayekua mgeni wa rasmi. Mhe. Ali Hassan Mwinyi anatarajiwa kufika Washington, DC siku ya Alhamisi July 4, 2013.

VETA YA MWAGA TEKNOLOJIA SABASABA

$
0
0
Mhandisi Adrian Kashula wa VETA Kipawa jijini Dar es Salaam, akitoa maelezo kuhusu teknolojia ya kisasa ya umeme wa viwandani ambayo inatumia eneo dogo na kutoa taarifa pale panapotokea hitilafu, akitoa maelezo kwa wageni waliotembelea banda hilo.
Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu wa VETA Chang’ombe Dar es Salaam, fani ya uchoraji ramani na usanifu majengo, Fatma Mohamedi akitoa maelezo kuhusu mafunzo ya taaluma hiyo yanayotolewa na chuo hicho katika ngazi mbalimbali.
Baadhi ya mashine na mitambo inayozalishwa na vyuo mbalimbali vya VETA nchini, ambayo ikitumika vema inaweza kulikomboa taifa kiuchumi kwa kuepuka utegemezi wa mashine na mitambo kutoka nje.


MEYA JERRY SILAA AWATAKA WATANZANIA KUTUNZA NA KULINDA AFYA ZAO ILI KUJENGA FAMILIA NA JAMII YENYE AFYA BORA

$
0
0
IMG_2846
Wananchi wa Tanzania wameelezwa kuwa kazi ya kuboresha huduma za afya na afya ya mazingira na maji ni ngumu na kuwa inahitaji nguvu za pamoja kati ya jamii, halimashauri na wadau mbalimbali ili kupata mafanikio yaliyokusudiwa hasa ya uzuiaji wa magonjwa.
Akitoa nasaha wakati wa kufunga wa zoezi la utoaji wa huduma za afya kwa uwiano katika jamii kata ya Gombo la Mboto, Mgeni rasmi Mh. Jerry Silaa, Mstahiki Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Ilala amesema huduma za afya na afya ya mazingira ni muhimu katika maisha ya kila siku ya binadamu.
Ameongeza kwa kuwapongeza sana wakazi wa Gomngo la mboto Markaz pamoja na viongozi wao kwa juhudi kubwa walioifanya katika kuhakikisha uwepo wa kituo cha tiba karibu na jamii na kuwa wanastahili kuwa mfano wa kuigwa na jamii zingine.
Aidha amesema hilo ni moja wapo katika utekelezaji wa agizo la Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika lengo lake la kupeleka huduma za tiba zikiwamo zile za zinazohitaji madaktari bingwa karibu na wananchi.
IMG_2798
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Dr. Asha Mahita akielezea dhamira ya Idara katika kuendeleza Afya ya Jamii kwa kusogeza Huduma za Afya karibu na Jamii, Huduma hizo zinahusisha matibabu kwa magonjwa mbalimbali kama Magonjwa ya Moyo, Kisukari, Malaria, Macho, Meno, Afya ya Akili, Ushauri na kupima VVU kwa hiari, Elimu juu ya Uzazi wa Mpango na Afya ya Uzazi, Afya ya Mazingira, Lishe, na Jinsia, pia ametoa tathmini ya wakazi wa Kata ya Gongo la Mboto Markaz waliopatiwa huduma za Afya bure kwa zoezi lililofanyika kwa muda wa siku tatu ikiwemo Afya ya Akili, Kifua Kikuu na matibabu ya Ujumla.
IMG_2869
Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akipima Presha wakati wa kufunga zoezi la Utoaji wa Huduma za Afya kwa Uwiano katika jamii ikiwa ni ishara ya kuhamasisha watu kujenga utamaduni wa kupima Afya zao.
IMG_2882
Wakazi wa Kata ya Gongo la Mboto wakipatiwa dawa za bure baada ya kufanyiwa vipimo wakati wa kutoa Huduma ya Upimaji Afya Bure kwa wakazi wa kata hiyo iliendehshwa kwa siku tatu.
IMG_2900
Mtaalamu wa Magonjwa ya Kisukari kutoka Kituo cha Afya Amana Dkt. Abushiri Rajabu akitoa maelezo kwa Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa kuhusu Elimu anayotoa kwa jamii kuhusiana na Ugonjwa huo.
IMG_2792
wakazi wa Gongo la Mboto wakimsikiliza Diwani wao ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa wakati wa kufunga zoezi la utoaji wa Huduma za Afya kwa Uwiano katika Jamii kata ya Gongo la Mboto.

PPF YAKARIBISHA WADAU KUTEMBELEA BANDA LAO SABASABA

$
0
0
Mfuko wa pensheni wa PPF unapenda kuwakaribisha wadau wote kutembelea katika banda la PPF kwenye maonyesho ya kimataifa ya biashara ili kuweza kujua shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko wa pensheni wa PPF kama vile Taarifa za michango, Usajili, mafao , uwekezaji ikiwemo mikopo ya SACCOS kwa wanachama wa PPF.
Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. Juma Mwita akitoa maelezo kuhusu michango kwa mwanachama wa PPF, mara baada ya kumkabidhi taarifa ya michango yake katika banda la PPF kwenye maonyesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya mwalimu JK Nyerere jijini Dar es Salaam.
Afisa wa Idara ya Mifumo ya Habari wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi. Hawa Kimaro akitoa maelezo kuhusu michango kwa mwanachama wa PPF, Bw. Walter Vasolela mara baada ya kumkabidhi taarifa ya michango yake katika banda la PPF kwenye maonyesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya mwalimu JK Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mdau wa PPF akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi wa kanda ya kusini ya PPF, Bw. Thomas Chisanga alipotembelea banda la PPF.

MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA) YATWAA TUZO GHANA

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Thomas William akionyesha Tuzo ya Ushindi wa Ubunifu iliyoshinda NIDA katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Afrika yaliyofikia kilele chake tarehe 23 Juni, 2013, Accra Ghana.

Video Mixer 8 Camera inauzwa

$
0
0
Kaka Michuzi Assalam Alaykum pole na mihangaiko najua hukosi kwenye Pertnership inayoendelea, Nilikuwa nauza Video mixer ingesaidia sana kwenye mikutano hiii

Roland V8 video mixer ina 8 INPUT CAMERAS na 8 OUTPUT professional imeshinda award ya Olympics 2008.
Panasonic Video mixer -MX50 4 INPUTS CAMERAS
CIMA-YCP -9 Ina 2 IPUTS CAMERAS
Zimejaaa lots of effects ukigoole au youtube hayo majina basi utaziona function zake Nimeona kwenye Partnership unahangaika na Camera moja tu sasa ukiweza kuunga camera 8 ingekusaidia.

Maelezo zaidi wasiliana na nuramoboy@yahoo.com

JK AWAANDALIA MARAIS DHIFA YA KITAIFA YA CHAKULA CHA USIKU

$
0
0
 Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mfalme wa Swaziland, King Mswati katika hafla ya chakula cha usiku alichokiandaa kwenye viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam jana usiku, kwa waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufaa ya Wote (Global Smart Partinership Dialogue). TBL ni moja kati kampuni zilizofadhli hafla hiyo.
 Rais wa zamani wa Msumbiji, Joachim Chisano (kushoto) akikaribishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernald Membe katika hafla ya chakula cha usiku.
 JK akiwa na Museveni wa Uganda (kushoto), Kingi Mswati wa Swaziland na Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi
 Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Alnold Kilewo (kushoto), akiwa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Chibuku cha Dar Brew, Kilowi Suma (wa pili kushoto), katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Rais Jakaya Kikwete  kwa marais na viongozi mbalimbali waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufaa ya Wote (Global Smart Partinership Dialogue). Kutoka kulia ni Kiongozi wa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, Halfan Mpango na Mkurugenzi wa Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Esther Mkwizu. Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ni kati ya kampuni zilizofadhili hafla ya chakula hicho.
 Rais Jakaya Kikwete akiwaongoza baadhi ya marais na viongozi wengine kucheza muziki uliokuwa ukiporomoshwa na kikundi cha sanaa cha Tanzania House of Talent (THT), wakati wa hafla ya chakula cha usiku alichokiandaa viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam jana usiku, kwa marais na viongozi waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufa ya Wote (Global Smart Partinership Dialogue). Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ilikuwa kati ya kampuni zilizofadhili hafla ya chakula hicho.

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images