Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

MKUU WA MAJESHI WA TANZANIA ZIARANI NCHINI OMAN

0
0
Mkuu wa majeshi ya Tanzania Mheshimiwa Kaimu Davis Mwamunyange, alifanya ziara ya Kikazi nchini Oman kuanzia tarehe 23 hadi 27 Juni 2013 kwa Mwaliko wa mwenyeji wake Luteni Jenerali Ahmed bin Harith Al Nabhani.

Ziara hii ilikuwa na madhumuni makuu ya kuimarisha uhusiano wa kindungu uliopo baina ya Oman na Tanzania kupitia sekta ya ulinzi na kuanzisha uhusiano wa karibu na ushirikiano baina ya vyombo hivi vya ulinzi kati ya Tanzania na Oman.

Katika ziara hii Mhe. Jenerali Mwamunyange alikutana na kufanya mazungumzo na Mwenyeji wake Luteni Jenerali Ahmed bin Harith Al Nabhani na pia kukutana na Waziri katika Ofisi ya Mfalme Mheshimiwa Luteni Jenerali Sultan bin Mohamed Al Nuamani .

Mbali na kukutana na viongozi hawa wa Oman, Mkuu wa majeshi alipata nafasi kutembelea maeneo kadhaa kujonea shughuli mbalimbali za Jeshi la Oman, alitembelea makumbusho ya Jeshi la Oman, Chuo cha Uongozi na kamandi cha Oman, Chuo cha Jeshi la Anga, Hospital ya Jeshi , Makao makuu ya Jeshi la Askari wa Miguu pamoja Makao makuu ya Jeshi la Majini.

Katika maeneo yote aliyotembelea Mheshimiwa Mkuu wa Majeshi alifurahishwa sana na shughuli za jeshi la Oman na kuridhika na hatua iliyopigwa na Jeshi la Oman. Mkuu wa majeshi pia alitembelea ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Oman kujionea shughuli mbalimbali za Ubalozi na pia kuhudhuria hafla ya chakula cha Usiku kilichoandaliwa kwa heshima yake nyumbani kwa Mheshimiwa Balozi
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akikagua Gwaride la Mapokezi mara alipowasili katika Makao makuu ya Jeshi la Oman kuanza Ziara ya kikazi nchini Oman, kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Oman Luteni Jeneral Ahmed bin Harith Al Nabhani.


MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA SEKRETARIETI YA MKOA WA DODOMA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akitoa salamu zake za ufunguzi kwa wajumbe wa baraza la wafanyakazi la sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma (hawapo pichani) wakati wa kikao cha pili cha baraza hilo.
Wajumbe wa baraza la wafanyakazi la sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma wakisikiliza kwa makini salamu za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakati wa ufunguzi wa kikao cha pili cha baraza hilo.
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rhehema Nchimbi (katikati waliokaa) na wajumbe wa baraza la wafanyakazi la sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma. Kutoka kushoto waliokaa, katibu wa baraza Ndg. Paul Masanja, Katibu wa TUGHE Mkoa Ndg. Mchenya John; kushoto kwa Mkuu wa Mkoa ni Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge na mwisho ni katibu msaidizi wa baraza Ndg. Pili Juma.

Mbaspo watawazwa kuwa mabingwa wa Airtel Rising Stars Mbeya

0
0
Mshambuliaji wa Msimamo Youth Educator’s,Saimon Kizito (kulia) akipiga mpira huku beki wa Buguruni Youth Center,Mzee Bazil akijaribu kumzuiya katika mashindano ya vijana U-17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa Ilala,kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam juzi.
Mshambuliaji wa Msimamo Youth Educator’s,Adeus Kizito akijaribu kumpiga chenga beki wa Buguruni Youth Center,Husein Hamza katika mashindano ya vijana U- 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa Ilala,kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam juzi.
Kiungo wa timu ya Buguruni Youth Center,Razak Abdalah (wapili kulia) akiwania mpira na beki wa Msimamo Youth Educator’s, Adam Zogombwa (kulia) katika mashindano ya vijana U- 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa Ilala, kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam, jezi namba tatu ni Mzee Bazil akijiandaa kutoa msaada kwa mwenzake.
Kiungo wa Msimamo Youth Educator’s,Rajabu Mohamed (katikati) akiwania mpira na wachezaji wa Buguruni Youth Center,Karim Matola (kushoto) na Razak Abdalah katika mashindano ya vijana U- 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa Ilala,kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam,jezi namba tatu ni Mzee Bazil akijiandaa kutoa msaada kwa mwenzake.

Kama ilivyotarajiwa, timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Mbaspo jana ilitawazwa kuwa mabingwa wa Airtel Rising Stars mkoa wa Mbeya baada ya kukusanya pointi nne sawa na mahasimu wao Mbosa lakini wakiwa na magoli mengi ya kufunga. Timu ya Mbeya Secondari haikupata hata pointi moja katika mtanange huo wa kusaka vipaji

Mbaspo walianza mbio zao za kutwaa ubingwa kwa kutoshana nguvu ya 3-3 dhidi ya Mbosa siku ya Jumatatu Juni 24 kabla ya kufanya mauaji makubwa ya 6-0 dhidi ya timu dhaifu ya Mbeya Sekondari siku ya Jumanne. Michezo yote imefanyika kwenye uwanja wa Magereza jijini Mbeya.

Mbosa walifikisha point nne juzi Jumatano walipoitandika Mbeya Sekondari 3-0 hivyo kumaliza wakiwa na point nne na magoli sita wakati wapinzani wao Mbaspo wakifikisha jumla ya magoli tisa ya kufunga. Katika mechi ya juzi, magoli ya Mbosa yalitiwa kwenye kamba na Michael Mwashilanga, Riziki Juma na Julius Landa. Wakati huo huo, chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mbeya kimetangaza kikosi cha wachezaji 18 kuuwakilisha mkoa huo kwenye michuano ya Taifa ya Airtel Rising Stars inayoanza kutimua vumbi kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 2.

Wachezaji hao ni Ismail Yesaya, Emmanuel Alex, Gift Sanga, Jackson Mwaibambe, Boaz Mwangole, Costa Sanga, Seif Zubery, Stanley Angelo, Enock Sikaonga, Kaunda Malata, Joel Kasimila, Hamprey Nyeo, Elia Salengo, Peter Noah, Emmaneul Mtimbi, Michael Bosco, Richard Kalinga na Zamoyoni Mwashambwa.

Katika mkoa wa Morogoro, mji kasoro bahari, timu ya Moro Kids imetoka sare ya bila kufungana na Techfort katika mchezo wa kushambuliana kwa zamu uliopigwa kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya Morogoro juzi Jumatano na kushuhudiwa na mashabiki wengi wa mji huo.

Airtel Rising Stars vile vile imeanza kutimua vumbi katika jiji la Mwanza ambapo timu ya Marsh Athletical imedhihirisha umwambe wake katika soka baada ya kuifunga Nyamagana United 2-0 kwenye uwanja mkongwe wa Nyamagana.

Timu za mikoa zimepangwa kuanza kuwasili jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki tayari kwa ajili ya kindumbwe ndumbwe cha Airtel Rising Stars ngazi ya taifa katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Wachezaji 16 watachaguliwa wakati wa mashindano hayo ili kuunda timu itakayoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars. Nchi mwenyeji wa michuano hiyo itatangazwa baadaye mwezi ujao.

EBONY LIFE TV DEBUTS ON DStv!

0
0

Ebony Life TV, the brainchild of dynamic African talk show star Mo Abudu, debuts on DStv on July 1 and promises to deliver a fresh new energy and perspective to audiences across East, West and Central Africa.

Fusing exclusive African original programming, featuring some of the continent’s biggest names, with relevant international urban movie and series programming, Ebony Life TV will be available on DStv channel 165 to DStv Premium, Compact Plus (where available) and Compact viewers.

With the tagline “Live the Ebony Life”, the channel is both inspirational and aspirational, celebrating style and success while simultaneously motivating audiences to dream and dream big. Glossy, polished and sophisticated, the EL experience puts African superstars such as Kate Henshaw-Nuttal, Uche Jombo Rita Dominic, Funke Akindele, Tiwa Savage and Banky W. on a line-up that also features Latoya Jackson, Taye Diggs, Damon Wayons and Sherri Shepherd.

Homegrown programming on the channel includes the glamourous flagship talk-show Moments with Mo. This time round, the always engaging Mo is joined by two brand new co-hosts, whose selection during an intense search is also chronicled on the dramatic, must-watch reality show Mo’s Search.

Article 8

HII IMEKAAJE WADAU??

0
0

Hizo pichani ni nguo za Dereva na Kondakta wa wa Basi hili zikiwa zimeanikwa hapo.

MAONYESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA YAANZA RASMI LEO, BIDHAA ZINAZOTENGEZWA NA WAFUNGWA CHINI YA USIMAMIZI WA ASKARI MAGEREZA

0
0
Lango Kuu la kuingilia Banda la Jeshi la Magereza ambapo kuna bidhaa mbalimbali zinapatikana zikiwemo Samani za Ndani, Vifaa vya Ushonaji na Ufumaji, Majiko, Viatu, Vifaa vilivyotengenezwa kwa Mkonge, Mianzi na Henzerani, Vinyago vya aina mbalimbali, Mazao ya Kilimo pamoja na Chumvi. Bidhaa hizo zote zimetengenezwa katika ubora wa hali ya juu na Wafungwa kwa kushirikiana na Askari wa Jeshi la Magereza ndio waliotengeneza bidhaa hizo ambazo zinauzwa kwa bei inayomjali mlaji. Wananchi na Wadau mbalimbali hamna budi kutembelea Banda hili ili kuweza kujionea bidhaa hizo zenye ubora pamoja na kuliunga Mkono Jeshi letu la Magereza katika shughuli na kazi hizo za Mikono ambazo Wafungwa kupitia Programu ya Urekebishaji wa Wafungwa Magerezani Wafungwa hupata ujuzi mbalimbali ukiwa mo ufundi stadi ambao matokeo yake ni bidhaa hizo zilizopo katika Banda la Magereza katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa, Saba Saba, Dar es Salaam.
Jiko la Mkaa (Plate mbili) la kuoka Mikate, kuchoma nyama, mishikaki, samaki pamoja na kupikia vyakula mbalimbali. Jiko hili limetengenezwa na Wafungwa wa Gereza Mtego wa Simba , Morogoro kwa kushirikiana na Askari wa Jeshi la Magereza ikiwa ni utekelezaji wa Programu mbalimbali za Urekebishaji wa Wafungwa wanapokuwa wakitumikia vifungo vyao Magerezani kwa kuwapa ujuzi mbalimbali wa ufundi stadi.
Bao la Mchezo wa Jadi ambalo lipo katika Banda la Jeshi la Magereza ambalo lina viti viwili lenye Thamani ya Tsh. 950,000/= bao hilo limetengenezwa na Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga kwa kushirikiana na Askari wa Jeshi la Magereza. Mchezo wa Bao la Jadi ni Maarufu hapa nchini kwani hata Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere wakati wa uhai wake alipenda Mchezo huo wa Bao la Jadi.
Kitanda cha kulalia chenye ukubwa wa 5 x 6 kikiwa na kiti cha watu wawili na meza havipo pichani. Kitanda hicho kimetengenezwa na Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga kwa kushirikiana na Maofisa Magereza ikiwa ni utekelezaji wa Programu ya Urekebishaji wa Wahalifu Magerezani ili waweze kuwa na ujuzi wanapotoka Magerezani.
Meza ya kujipodolea(Dressing Table) ikiwa na Stuli moja ambayo imetengenezwa kwa kutumia mbao za Mti wa Mkongo yenye Thamani ya Tsh. 1,450,000/= ambayo imetengenezwa na Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga kwa kushirikiana na Maofisa Magereza katika utekelezaji wa Programu ya Urekebishaji wa Wahalifu Magerezani.
Viatu vya aina mbalimbali vinavyotengenezwa kwa kutumia ngozi za wanyama. Viatu hivyo vinatengenezwa katika Kiwanda cha Karanga Moshi cha Jeshi la Magereza pia Wafungwa wa Gereza Karanga kwa kushirikiana na Maofisa wa Magereza wametengeneza Viatu hivyo vyenye ubora wa hali ya juu kama vinavyoonekana.
Muonekano wa Bustani ya mbogamboga iliyopo katika Banda la Jeshi la Magereza lillilopo katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ambayo yameanza leo. Bustani hii inahudumiwa na Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga kwa kushirikiana na Wataalam wa Kilimo wa Jeshi la Magereza ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa programu ya Urekebishaji wa Wahalifu.
Muonekano wa nje wa Banda la Jeshi la Magereza katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yaliyopo katika Viwanja vya Sabasaba Jijini, Dar es Salaam ambayo yameanza leo (Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI (TFF) LEO


PUNDA WAKIWA MALISHONI JIJINI TANGA LEO

0
0
Kamera ya Globu ya Jamii,mchana huu imewanasa Punda hawa wakipata msosi (wakila majani) katika moja ya Bustani ndani ya Jiji la Tanga.

USIKU WA TUDD THOMAS KUFANYIKA JUNI 30 DAR LIVE

Taswirazz ya eneo la Tegeta jijini Dar leo

0
0
 Muonekani wa eneo la Tegeta leo ukitokea katikati ya Mji wa Dar.
Daladala zimepaki pembeni na ilihali njia inayotumia ni moja na kupelekea magari mengine kupita kwa shida.

Wami Mkoani Pwani ionekanavyo sasa

0
0
 Pichani ni Daraja la Mto Wami Mkoani Pwani ambapo kuna moja ya vyanzo vikuu vya Maji hapa nchini.
 Huu ndio Upana halisi wa Daraja la Mto Wami ambalo haliwezi pitisha gari zaidi ya moja.
 Kitu cha Air Force One kikipandisha mliwa wa Wami.
Malori na Mabasi katika kona za Milima ya Wami.
Huu ndio Mto Wami wenyewe.

EU Celebrates Croatia's Accession

0
0
TODAY the Head of the Delegation of the European Union to Tanzania and the East African Community, Ambassador Filiberto Ceriani Sebregondi, hosted an event to mark the accession of Croatia to the European Union effective July 1 Croatia will then become the 28 Speaking at the occasion, Ambassador Sebregondi said that the EU was delighted to welcome Croatia to become part of the unique economic and political partnership between European countries.

"Croatia’s accession is a result of ten years of rigorous negotiations and it brings with it benefits to the country's people and for the rest of Europe, even though it is a small - but very beautiful- country," Ambassador Sebregondi said.

Ambassador Sebregondi saluted the success of Croatia's accession, as well as the consistent efforts displayed by the EU, and the valuable support of the rest of the EU Member States.


"We look forward to Croatia's participation in the EU, and we expect it to also be a success story – to the benefit of the EU, of Croatian people, and of the Western Balkans region," he said adding: "Work in the region is not finished, but Croatia's example shows that the EU's doors remain open for countries committed to European democratic agenda.


Croatia's accession on the 1 The function was attended by members of the Croatian community in Dar es Salaam, EU Heads of Mission in Tanzania, senior officials from the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation together with members of staff of the EU Delegation to Tanzania.

Background

Croatia applied for membership in 2003 and the European Commission's Opinion was made in 2004 before it was granted candidate status in 2004. Accession negotiations started in 2005 and concluded in 2011.

The Treaty on European Union states that any European country may apply to join the EU if it respects the Union’s democratic values and is committed to promoting them. More specific criteria are known as the Copenhagen Criteria.

They state that a country may only join the EU if:

• Politically – it has stable institutions guaranteeing democracy, the rule of law and human rights;

• Economically – it has a functioning market economy and is able to cope with competitive pressure and market

forces within the EU;

• Legally – it accepts established EU law and practice, particularly the major goals of political, economic and monetary union.

The accession process has a number of stages, all of which must be approved by all existing EU member states for a country to be accepted as a member. A country is first granted the prospect of membership. It then becomes an official candidate for membership, before finally moving on to official membership negotiations. When negotiations and accompanying reforms have been completed, the country may join the EU.

th European country to join the world's most ambitious regional integration model.

st of July demonstrates that EU membership remains an attractive and valuable prospect. "

Spika wa Bunge la Oman na ujumbe wake wawasili Dodoma, asaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano baina ya Bunge la Tanzania na Bunge la Oman

0
0
Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali akiwa na ujumbe wa Wabunge toka Oman yupo hapa nchini kwa ziara ya kikazi ya siku sita ambapo pamoja na mambo mengine amesaini mkataba wa uanzishwaji wa ushirikiano wa Bunge la Tanzania na Bunge la Oman katika Maswala mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi akimkaribisha Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Dodoma jana.
Kaminisha wa Tume ya Utumishi ya Bunge Mhe. Abdulkarim Shah akimkaribisha Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Dodoma jana.
Naibu Spika Mhe. Job Ndugai akimtambulisha Katibu wa Bunge. Dkt. Thomas Kashililah kwa Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali alipowasili Dodoma jana.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkaribisha Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge Dodoma ambapo anafanya ziara ya kibunge ikiwa ni pamoja na kusaini makubaliano ya ushirikiano baina ya mabunge haya mawili.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda pamoja na Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali wakisaini mikataba ya makubaliano ya ushirikiano baina ya mabunge haya mawili.
Wakibadilishana mikataba ya Makubaliano.
Picha ya Pamoja Ujumbe wa Spika wa Bunge la Oman na Wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge la Tanzania. Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge

Rais Kikwete Azungumzia Ziara ya Rais Obama nchini Tanzania

0
0
Ubalozi wa Tanzania London ukishirikiana na Urban Pulse na Freddy Macha wakuletea video fupi ya Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete akizungumzia ziara ya Rais Barack Obama, alipokuwa Uingereza karibuni.

Mafunzo kwa Maafisa Habari Kuhusu Namna ya kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi

0
0
Mafunzo ya kuwajengea Uelewa Maafisa Habari kutoka katika Wizara zinazohusika moja kwa moja na masuala ya mazingira kuhusu Namna ya Kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi . Vilevile Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na Ukataji Miti ovyo na Uharibifu wa Mazingira. Mafunzo haya yametolewa na Regalia Media kwa ufadhili wa REDD.
Baadhi ya Maafisa Habari katika mafunzo ya vitendo kuhusu namna ya  kupima urefu wa mti ili kuweza kujua kiwango cha kaboni iliyomo katika miti. Zoezi hili limefanyika katika msitu wa kupandwa Morogoro.
Dr. Zahabu akitoa maelekezo ya namna ya zoezi zima la kupima upana wa misitu linavyofanyika.
Washiriki wakijaribu kutumia kipimo kupima kipenyo cha mti katika mafunzo hayo
Picha zote na Asteria Muhozya, Afisa Habari  Wizara ya  Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto 

Spectacular Opening of the Global 2013....

0
0
The 2013 Global Smart Partnership Dialogue was launched in spectacular fashion Friday in Dar es Salaam. The Smart 29ers got the Dialogue off to a great start, sharing their experiences, insights and visions with the Dialogue Host Patron, 
His Excellency Dr Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania, alongside numerous Heads of State and a selection of CPTM Fellows. Over 800 people then filled the auditorium to hear Joint Dialogue Conveners Ambassador Ombeni Sefue and Dr Mihaela Smith set the tone for the coming days, celebrating the ability of Smart Partners' Dialogues to unite such a diverse and interesting range of people. 
His Excellency Dr Kikwete proceeded to evoke the power that technology can have when leveraged effectively, improving people's lives and achieving socio-economic transformation. 
 His Excellency's speech was followed by the launch of the Technology Gallery and the CPTM Smart Partners' Hub at the Convention Centre with a video showcasing high impact technologies. The day's events were rounded off with a spectacular Opening Dinner at the Gymkhana Club grounds featuring music, dancing and speeches from His Excellency President Yoweri Kiguta Museveni, President of the Republic of Tanzania CPTM Fellow and Companion, Chair of the Smart Partnership Movement.


kipanya

PRESIDENT OBAMA'S TRIP TO AFRICA

0
0
President Obama and the First Lady travel to Senegal, South Africa, and Tanzania to meet with leaders from government, business, and civil society, and to reinforce U.S. commitment to expanding economic growth, investment, and trade; strengthening democratic institutions; and investing in the next generation of African leaders. White House video

wanatafuta riziki...

0
0
 Watoto wanaojihusisha na Biashara mbali mbali katika Barabara kuu itokayo Chalinze - Segera mkoani Tanga,wakikimbilia moja ya Gari ambalo lilikuwa nimesimama ili kuweza kuuza bidhaa zao kwa abiria waliopo kwenye Gari hilo.
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images