Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109573 articles
Browse latest View live

TAARIFA KWA UMMA


RAIS WA UMOJA WA WAKUU WA SEKONDARI ATEMBELEA SABASABA

0
0

Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel amesema kuwa katika serikali ya viwanda wakuu wa shule wanaweza kujenga msingi mzuri kwa wanafunzi kwani ni rasilimali katika sekta hiyo.

Mollel aliyasema hayo wakati wa Rais wa Umoja wa Shule za Sekondari nchini (Tahossa)alipotembelea banda la Global Education Link katika maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam, Mollel amesema kuwa wa wakuu wa shule ndio wanaweza kuchukua dhamana ya serikali ya kauli ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwa serikali ya awamu katika dhana ya viwanda.

Mollel amesema kuwa serikali ya viwanda inahitaji watu wa masomo wa sayansi, sanaa na masoko kwa pamoja ndio wanajenga viwanda.

Aidha amesema kuwa Global itaendelea kushirikiana wakuu wa sekondari katika ujenzi wa nchi ya viwanda.

Naye Rais wa Umoja wa Wakuu wa Sekondari Nchini (Tahossa) Mwalimu Vitaris Shija amesema kuwa Global Education Link (GEL) ni chombo ambacho kinafanya wanafunzi wapende masomo ya sayansi ambao ndio watakaotumika katika sekta ya viwanda.

Amesema kuwa sekta ya viwanda inahitaji wataalam wa sayansi, sanaa na biashara ndio mahitaji ya sekta ya viwanda kwa sasa kutokana na kauli ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwa serikali ya awamu ya tano ni serikali ya viwanda.

Shija amesema kuwa Global Education Link imeleta chachu ambapo inatakiwa kuanza kushawishi wanafunzi kusoma sayansi kuanzia shule ya msingi kutokana na mahitaji ya sekta ya viwanda.

Shija amesema kuwa kutokana na mahitaji ya rasilimali katika sekta ya viwanda wakiwa wakuu wa shule za sekondari kuzungumza suala hilo kuanzia kwa wazazi juu ya nchi mahitaji yar rasimali katika sekta yaya viwanda.

Amesema kuwa serikali kulipa wataalam wa nje ni gharama ambao sehemu kubwa watalipwa na kwenda kujenga kwao lakini wanafunzi wa waliokwenda watafanya kazi nchini na kujenga nchi yao.
 Mkurugenzi wa Global Education Link , Abdulmalik Mollel akiwa na Rais wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Nchini (Tahosa) Mwalimu Vitaris Shija katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.
 .Mkuu Idara ya Masoko kwa Njia ya Mtandao, Micky Musa akionesha mfumo wa Taarifa za wanafunzi wanaosoma nje kupitia Global Education Link (GEL) katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.


Picha mbalimbali za mafisa za Global Education Link (GEL) katika katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.

MKURUGENZI APIGA MARUFUKU SHUGHULI ZA KILIMO KWENYE VYAZO VYA MAJI

0
0
Mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya MADABA SHIFII MPENDA ametembelea eneo ambalo limeaharibiwa vibaya na baadhi ya wananchi wanaojishughulisha na kilimo pamoja na ufugaji kwenye vyazo vya maji.Haikuwa rahisi kufikia eneo hilo kwani ilitupasa kutembea kwa mwendo mrefu kuweza kufikia eneo husika ambalo ni chazo cha mto NAMAOVI kijiji cha MWANDE kata ya MATETELEKA halimashauri ya MADABA mkoani RUVUMA HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE. 

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MKOANI LINDI KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TANO

0
0
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Mzee Mtopa wakati alipowasili Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi, katika ziara ya kikazi ya siku tano,(katikati) ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfey Zambi, Julai 10, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasili Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne, akiwa mkoani humo Waziri Mkuu ameanza ziara yake katika wilaya ya Liwale kwa ajili ya kukagua shughuli za maendele na jioni ya leo atukuwa na mkutano wa hadhara na kuzungumza na wananchi wa Liwale pamoja na kusikiliza kero zao

Waziri Mkuu ameongozana na Mke wake Mery Majaliwa ambapo walipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi pamoja viongozi wa wilaya za Mkoa wa Lindi ambao walifika katika mapokezi katika uwanja wa ndege wa Nachingwea.Waziri Mkuu hapo kesho anatarajia kuendelea na ziara yake wilayani Ruangwa.

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI JUNI,2017 WAPUNGUA KWA ASIMILIA 5.4

0
0
MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Juni, 2017 umepungua hadi asilimia 5.4 ikilinganishwa na asilimia 6.1 ilivyokuwa mwezi Mei, 2017.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo amesema Mfumuko wa Bei umepungua kutokana na kupungua kwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwezi Juni, 2017 ikilinganishwa na kasi ya upandaji iliyokuwa kwa mwezi Mei, 2017.

“Mfumuko wa Bei wa mwezi Juni, 2017 umepungua hadi kufikia asilimia 5.4 kutoka asilimia 6.1 mwezi Mei, 2017. Hii inatokana na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwezi Juni, 2017,” amesema Kwesigabo.

Amesema Mfumuko wa Bei unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umepungua kwa asilimia 0.1 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 0.2 ilivyokuwa mwezi Mei, 2017.Kwesigabo amesema Fahirisi za Bei zimepungua hadi 109.10 mwezi Juni, 2017 kutoka 109.26 mwezi Mei, 2017. Amesema Kupungua kwa Fahirisi za Bei kumechangiwa hasa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula.

Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa fahirisi ni pamoja na mahindi ambayo yamepungua kwa asilimia 5.1, unga wa mahindi kwa asilimia 2.4, unga wa mihongo kwa asilimia 1.9, machungwa kwa asilimia 2.4, dagaa kwa asilimia 3.2, mbogamboga kwa asilimia 5.7, maharage kwa asilimia 1.8 na viazi mviringo kwa asilimia 6.2.

Aidha Mfumuko wa Bei kwa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani kwa mwezi Juni, 2017 umepungua hadi asilimia 9.8 kutoka asilimia 11.8 mwezi Mei, 2017.

Uwezo wa Shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umeimarika kidogo na kufikia Shilingi 91 na senti 66 mwezi Juni, 2017 ikilinganishwa na Shilingi 91 na senti 53 ilivyokuwa mwezi Mei, 2017.

Hata hivyo, Mfumuko wa Bei nchini Tanzania una mwelekeo unaofanana na baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashariki kwa kuwa Mfumuko wa Bei wa mwezi Juni, 2017 nchini Uganda umepungua hadi asilimia 6.4 kutoka asilimia 7.2 mwezi Mei, 2017; na nchini Kenya, Mfumuko wa Bei wa Mwezi Juni, 2017 umepungua hadi asilimia 9.21 kutoka asilimia 11.70 mwezi Mei, 2017.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigwabo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leokuhusu mfumuko wa bei wa Taifa kwa Mwezi Juni. Kulia ni Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira, Ruth Minja.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Balozi wa Italia atembelea Wizara ya Mambo ya Nje

0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Suzan Kolimba (Mb), akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Roberto Mengoni na ujumbe wake kwa ajili ya kufanya mazungumzo. 
Dtk. Kolimba akisisitiza jambo kwenye mazungumzo na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Roberto Mengoni. Katika mazungumzo hayo alikuwepo pia Makamu wa Rais wa Shirika la Taifa la Reli la Italia, Bw. Giovanni Roca ambaye amekuja nchini kuangalia fursa za uwekezaji katika sekta ya reli baada ya kuhamasishwa na Mhe. Naibu Waziri alipotembelea Italia hivi karibuni. 
Ujumbe wa Italia uliofuatana na Mhe. Balozi ukifuatilia mazungumzo. 
Bw. Charles Faini (kulia), Katibu wa Naibu Waziri na Bw. Salvatory Mbilinyi wa Wizara ya Mambo ya Nje wakinukuu taarifa muhimu 
Picha ya pamoja 

TUZO ZA MABALOZI WA USALAMA BARABARANI ZATOLEWA MKOANI DODOMA

0
0
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani,Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,Mohamed Mpinga akionyesha tuzo ya balozi bora wa usalama barabarani, aliyokabidhiwa na Mgeni Rasmi, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Simon Odunga(kushoto) wakati wa hafla ya kutunuku tuzo kwa mabalozi hao,wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani,Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.Hafla hiyo  imefanyika mwishoni mwa wiki  katika Hotel ya Royal,mkoani Dodoma. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Mgeni Rasmi,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Simon Odunga, akimkabidhi  Kamishna Msaidizi wa  Jeshi la Polisi, Fortunatus Musilimu(kulia) cheti cha kutambua mchango wake katika masuala ya  usalama barabarani wakati wa hafla ya kutunuku tuzo kwa Mabalozi wa Usalama Barabarani,wapili kushoto  ni Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani,Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.Hafla hiyo  imefanyika mwishoni mwa wiki  katika Hotel ya Royal,mkoani Dodoma. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Mgeni Rasmi,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Simon Odunga, akimkabidhi  Mkurugenzi wa Barabara wa Mamlaka ya Usimamizi wa Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA), Johansen Kahatano (kulia) cheti cha kutambua mchango wake katika masuala ya  usalama barabarani wakati wa hafla ya kutunuku tuzo kwa Mabalozi wa Usalama Barabarani,wapili kushoto  ni Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani,Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.Hafla hiyo  imefanyika mwishoni mwa wiki  katika Hotel ya Royal,mkoani Dodoma. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mgeni Rasmi,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Simon Odunga (wakwanza  kushoto waliokaa) na Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani,Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto waliokaa), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mabalozi wa Usalama Barabarani mara baada ya kutunukiwa vyeti ikiwa ni utambuzi wa mchango wao katika masuala ya usalama barabarani,iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hotel ya Royal,mkoani Dodoma. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 Mgeni Rasmi, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Simon Odunga, akisindikizwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani,Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) kuingia ukumbini wakati wa hafla ya kutunuku tuzo kwa Mabalozi wa Usalama Barabarani,iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hotel ya Royal,mkoani Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA AKABIDHI NYUMBA 50 ZA WATUMISHI WA AFYA KATIKA MIKOA YA SIMIYU, KAGERA NA GEITA

0
0

 Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akimkabidhi Hati za Umiliki wa nyumba 50 za Watumishi wa Afya kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika uwanja wa michezo wa Mazaina Chato mkoani Geita. 

  Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akizungumza na wananchi wa Mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita kabla ya kukabidhi Hati za umiliki wa nyumba 50 za watumishi wa sekta ya Afya zilizojengwa na Taasisi ya (Mkapa Foundation) katika mikoa hiyo mitatu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita baada ya Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa kukabidhi nyumba 50 kwa wizara ya Afya.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa mara baada ya kukabidhi nyumba hizo 50 zitakazotumika katika Sekta ya Afya katika mikoa ya Kagera, Simiyu na Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa wakati Mbunge wa Chato ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini,  Dkt. Medard Kalemani alipokuwa akihutubia wananchi wa Chato mkoani Geita.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Muhimbili yawezesha watoto kusikia kwa mara ya kwanza

0
0
Watoto watano waliofanyiwa upasuaji na kuwekewa vifaa maalum  vya kusaidia kusikia (Cochlear Implant) leo wamewashiwa vifaa hivyo ili waweze kusikia kwa mara ya kwanza.Zoezi hilo  limefanywa leo na wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na watalaam kutoka MEDEL .

Daktari Bingwa wa magonjwa ya Masikio, Pua na Koo Edwin  Liyombo amesema Juni   5 na 6 mwaka huu watoto hao walifanyiwa upasuaji huo kwa mara ya kwanza na kuwekewa vifaa maalum kwa ajili ya kusikia (Internal complete) lakini leo wamekuja kuwekewa na  kuwashiwa  vifaa vya nje(External complete) ili waweze kusikia.

Kwa upande wake mtaalam wa vifaa vya usikivu Fayaz Jaffer amesema baada ya kuwekewa kifaa hivyo watoto hao wanapaswa kurudi kila baada ya wiki mbili kwa miezi mitatu na baada ya hapo  watarudi  wiki mbili kwa miezi sita ili kufanyiwa mazoezi.

‘’Baada ya hapo wanaanza kuwafanyia mazoezi ya kuongea ( speech therapy) ndani ya mwaka mmoja na kadiri umri unavyozidi kwenda watakuwa wameshaanza kusikia na kujifunza kuongea na kupelekwa kujifunza zaidi katika shule za kawaida na si shule maalum kama ilivyozoeleka” amesema mtaalam huyo.

Juni 7 mwaka huu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alizindua huduma ya upasuaji wa kupandikizaji wa vifaa vya usikivu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili , ambapo katika Hospitali za Umma Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kutoa huduma hiyo  na ya pili katika nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki ikitanguliwa na Kenya.
 Muwakilishi wa Medel Afrika Mohamed El Disouky akimfanyia mazoezi ya kuzungumza mtoto Asma Athuman Mwinyi ambaye alipata matatizo ya kusikia akiwa na miaka sita.
Mtaalam Mohamed El Disouky akimfanyia majaribio ya kifaa cha usikivu mtoto Silas Machaku ( 3 ) ambaye aliwekewa kifaa maalum cha usikivu kwa ndani (Internal complete) lakini leo amewekewa kifaa kwa nje (External complete) ili aweze kusikia . zoezi hilo limefanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

WIZARA YA AFYA YAZINDUA MPANGO WA KUTEMBELEA HOSPITALI ZA UMMA NCHINI

0
0
Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezitaka hospitali nchini kutumia miongozo katika kutekeleza shughuli mbalimbali za huduma za afya  pamoja na kuimarisha mifumo ya TEHAMA ili kuwapo kwa mawasiliano kati ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na hospitali nyingine za rufaa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa wizara hiyo Dk. Mpoki Ulisubisya wakati akizindua mpango wa kufuatilia utoaji wa huduma za afya yakiwamo mafanikio na changamoto katika hospitali za umma nchini.

Dk Ulisubisya amesema mpango wa wizara yake ni kuzitembelea hospitali za umma nchini utaanzia kwenye hospitali za kibingwa ili ziwe kitovu cha kutoa mafunzo kwa hospitali nyingine nchini.

“ Malalamiko ni mengi yanapaswa kushughulikiwa kwa kuwekwa mifumo imara ya utekelezaji wa shughuli za huduma za afya kwa lengo la kuzuia kushuka kwa ubora wa huduma. Pia, hali hii itasaidia kuimarisha maadili miongoni mwa watumishi,” amesema Dk Ulisubisya wakati akizindua mpango huo leo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya akizungumza katika mkutano wa kuzindua mpango wa kuzitembelea hospitali za umma nchini ili kujua mafanikio na changamoto zilizopo kwenye hospitali hizo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tiba, Dk. Dorothy Gwajima wa wizara hiyo. Mpango huo umeandaliwa na wizara ya afya na ziara hiyo imeanza rasmi leo Muhimbili.
 Baadhi ya wataalamu wa afya kutoka Muhimbili na taasisi nyingine wakimsikiliza Katibu Mkuu, Dk Ulisubisya katika mkutano wa uzinduzi uliofanyika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
 Kaimu Mkurugenzi wa Tiba, Dk. Dorothy Gwajima (kushoto) wa wizara hiyo pamoja na wataalamu wengine wakifuatilia mkutano huo leo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza kabla ya kuzinduliwa kwa mpango wa kutembelea hospitali za umma ili kujua mafanikio na changamoto  zilizopo kwenye hospitali hizo.
 Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dk Juma Mfinanga wa Muhimbili akimwelekeza jambo Kaimu Mkurugenzi wa Tiba, Dk. Dorothy Gwajima (kushoto) wa wizara ya Afya wakati wa ziara ya kutembelea hospitali hiyo leo. Wengine ni maofisa kutoka wizara ya afya na hospitali ya Muhimbili.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Uzinduzi Rock City Marathon; RT yazitangaza rasmi kuwa ni mbio za kimataifa

0
0
SHIRIKISHO la Riadha la Taifa (RT) limezitangaza rasmi mbio za Rock City Marathon kuwa mbio za kimataifa baada ya kukidhi vigezo vyote ikiwa ni pamoja na kuhusisha mbio za km 42 kwa mara ya kwanza. Hatua ambayo imepongezwa na wakuu wa mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, na Kagera kwa kuwa itachochea ukuaji wa utalii katika kanda hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw John Mongella kwenye hafla ya uzinduzi wa mbio hizo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza, Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Bi Mary Tesha mbali na kupongeza hatua hiyo alisema uwepo wa mbio hizo katika kalenda ya Riadha kimataifa itawavutia watalii wengi katika ukanda huo pia na hivyo kufungua fursa zaidi kupitia utalii.

“Tunatarajia kwamba sasa mbio hizi zitafahamika zaidi duniani na kuvutia washiriki wa kimataifa ambao tunatarajia pia watakuja kama watalii na pia watapata kufahamu fursa za kiuwekezaji,’’ alisema.

Alitoa wito kwa washiriki wa ndani hususani wa mikoa ya Kanda ya Ziwa pamoja na wadhamini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Octoba 29 mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba jijini humo kwa uratibu wa kampuni ya Capital Plus International.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainabu Telack alisema Mkoa wake unaenda kujipanga kuhakikisha kwamba unatoa washiri bora katika mbio hizo huku akitoa wito kwa waandaaji wa mbio hizo kwa kushirikiana na viongozi wa riadha nchini kuhakikisha wanazitangaza kimataifa mbio hizo ili zivutie washiriki wengi wa kimataifa watakaokuja na fursa nyingine za kiuchumi ikiwemo sekta ya utalii na uwekezaji.


Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Bi Mary Tesha (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Rock City marathon mwaka 2017 wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Butiama Bi Annarose Nyamubi (kulia) aliemuwakilisha mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mbio hizo Bw Zenno Ngowi (wa pili kushoto) na Makamu wa pili wa Shirikisho la Riadha Taifa (RT), Dk Hamad Ndee. Bi Tesha alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw John Mongella.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainabu Telack akitoa nasaa zake kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa Rock City Marathon uliofanyika jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Alitoa wito kwa washiriki wa ndani hususani wa mikoa ya Kanda ya Ziwa pamoja na wadhamini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Octoba 29 mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba  jijini Mwanza kwa uratibu wa kampuni ya Capital Plus International.
Mpimaji wa njia wa njia za riadha anayetambulika kimataifa Bw John Bayo akimuonyesha mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa njia zitakazotumika katika mbio hizo baada ya kupimwa kitaalamu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mbio hizo Bw Zenno Ngowi akizungumza kwenye uzinduzi huo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UFUTA KUUZWA KWA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI-MAJALIWA

0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imemuagiza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba akutane na Bodi ya mazao mchanganyiko kwa ajili ya kuliondoa zao la ufuta na kuliingiza katika mfumo wa stakabadhi ghalani.

Pia amewaagiza wakuu wa mikoa yote inayolima zao la ufuta kukutana na Dkt. Tizeba kwa ajili ya kupanga mfumo mzuri wa uuzaji katika msimu wa mwaka 2016/2017 wakati Serikali ikijipanga kuliingiza zao hilo katika mfumo wa stakabadhi ghalani.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Julai 10, 2017) wakati akisalimiana na wananchi katika vijiji vya Nangano, Kibutuka na Kiangara alipowasili katika wilaya ya Liwale kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Lindi.

Ametoa kauli hiyo baada ya mbunge wa jimbo la Liwale, Mheshimiwa Kuchauka pamoja na wananchi kuiomba Serikali iwasaidie kuboresha bei ya zao la ufuta ambayo imekuwa ikiyumba.

Waziri Mkuu amesema “tatizo lipo kwenye mfumo wa  uuzaji zao la ufuta, unauzwa kwa bei ya rejareja, wanunuzi wako huru. Serikali imemuagiza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuliondoa zao katika bodi ya mazao mchanganyiko na kuliingiza katika mfumo wa stakabadhi ghalani ili kuboresha bei yake.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Bw. Justine Monko kuhakikisha anamaliza tatizo la maji katika vijiji vya Nangano,Kibutuka na Kiangara.

Amesema  Serikali imedhamiria kuondoa tatizo la maji kwa kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400. “Ndio maana Serikali imekuja na Kampeni inayosema mtue mama ndoo kichwani.”

Pia amemtaka Mhandisi wa Maji Bw. Andrew Kilembe kuandika barua ya kufuatilia fedha za maji sh. milioni 76 kwa ajili ya kijiji cha Kiangara walizopangiwa katika bajeti ya mwaka 2016/2017 kwa Waziri wa Maji ili waweze kukamilisha uchimbaji wa kisima.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwaeleza   wananchi wa Kijiji cha Kiangala  jinsi serekali ya awamu ya tano inavyo shughulikia kero za za wananchi Nchini Wananchi hao   walijitokeza July 10, 2017  ili waweze kumueleza kero  zinazo wasumbua  Waziri  yupo Wilayani Liwale Mkoa wa Lindi kwa ziara ya Kikazi ya siku Nne.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  na Mkewe Mery Majaliwa wametembelea Hospitali  ya Wilaya ya Liwale July 10, 2017 na kuwapa zawadi  Watoto Mapacha wenye Siku Mbili  waliozaliwa katika Hospital ya  Liwale, Waziri Mkuu yupo wilayani Liwale Mkoani Lindi kwa ziara ya Kikazi katika Mkoa  wa Lindi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akihutubia umati wa wananchi wa  wilaya ya Liwale waliojitokeza kuja kumsikliza  Michezo wa  wilaya ya Liwale July 10, 2017 Waziri Mkuu yupo wilayani Liwale Mkoani Lindi kwa ziara ya Kikazi katika Mkoa wa Lindi.

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI WAKABIDHIWA GARI

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza ambaye ni Mgeni rasmi akikata utepe ikiwa ni ishara ya kukabidhi rasmi gari la kuzimia moto kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, tukio ambalo limeshuhudiwa na Kamaishna Jenerali wa Jeshi hilo, Viongozi mbalimbali wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani humo, Mdau aliyetoa msaada huo Ndugu, Zacharia Hanspoppe, Maafisa na Askari wa Jeshi hilo pamoja na wananchi. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji akionesha funguo ya gari hilo mara baada ya tukio la kukata utepe na kukabidhiwa rasmi na Mkuu wa Mkoa Bi. Amina Masenza ambaye alikuwa ni Mgeni rasmi katika makabidhiano hayo. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza mwenye kitambaa cheupe katikati, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye wa kwanza mbele, Mdau ndugu Zachalia Hanspope wa pili kutoka kushoto, pamoja na Viongozi wa kamati ya vyombo vya ulinzi na usalama Mkoani Iringa wakifurahi tukio la makabidhiano. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Gari lililokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoro na Uokoaji Thobias Andengenye. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza (kushoto) akiagana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kulia) mara baada ya kuhitimisha shughuli ya makabidhiano ya gari la kuzimia moto lililotolewa msaada na mdau Ndugu, Zacharia Hanspoppe. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WALIOKULA FEDHA ZA USHIRIKA WATAZILIPA-MAJALIWA

0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitahusika na ulipaji wa deni la fedha za Ushirika na badala yake kila aliyekula fedha hizo atazilipa mwenyewe.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Julai 10, 2017), wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Liwale katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa wilaya.

Waziri Mkuu ambaye yuko katika na ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, amesema Serikali haiwezi kukubali Ushirika ukafa nchini kwa ajili ya watu wachache wasiokuwa waaminifu.

Amesema watu wote waliopewa dhamana ya kuongoza Vyama vya Ushirika na kuamua kujinufaisha kwa kula fedha za vyama watazilipa.

Waziri Mkuu amewaagiza Viongozi wa Mkoa wa Lindi kufanya ukaguzi katika Vyama vyote vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) ili kubaini ni wakulima wangapi wanadai.

Amesema baada ya kufanya uchunguzi na kubaini idadi ya wakulima wanaodai na kiasi cha fedha wawachukulie hatua wahusika wote kwa mujibu wa sheria.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO ZANZIBAR AZUNGUMZA NA WAANDISHI KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA IDADI YA WATU DUNIANI

0
0
Na Maelezo Zanzibar 
Wakati dunia inaungana kuadhimisha siku ya Idadi ya Watu duniani bado uzazi wa Mpango unaonekana ni changamoto katika baadhi ya maeneo ya Zanzibar.

Hali hiyo hupelekea ongezeko la idadi ya watu lisiloendana na kasi ya ukuaji wa uchumi na upatikanaji wa huduma za jamii katika maeneo mbalimbali nchini.Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Khalid Salum wakati akitoa taarifa yake kwa Vyombo vya habari kuelekea maadhimisho hayo hapo kesho.

Amesema ni vyema jamii kujenga mwamko juu ya umuhimu wa suala la uzazi wa Mpango ili kujenga jamii bora, iliyoimara na chachu katika kuongeza kasi ya maendeleo.

Dkt. Khalid amesisitiza jamii kuendelea kutumia njia za asili za uzazi wa mpango ambazo ni salama kwa afya ya mama na kuhudhuria katika Vituo vya afya kupata taaluma ya matumizi ya njia za kisasa pale inapohitajika.
Ameongeza kuwa suala la uzazi wa Mpango limesisitizwa hata katika Vitabu vya Dini ili kumpa nafasi Mama mzazi kurudisha afya na nguvu anazozitumia wakati wa kubeba mimba na kujifungua.

Kila ifikapo July 11, Zanzibar huungana na nchi zingine duniani kuadhimisha Siku ya Idadi ya Watu duniani ambapo kwa mwaka huu Kauli mbiu ni “Uzazi wa Mpango:Kuwawezesha Watu,kuendeleza Mataifa”
 Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na maadhimisho ya siku ya Idadi ya Watu duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo July,11. Kulia yake ni Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Zanzibar Juma Hassan Reli.
 Baadhi ya wandishi wa habari wakifuatilia mkutano wao na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed hayupo pichani uliofanyika wizarani kwake Mjini Zanzibar.
 Mwandishi wa habari wa Idara ya Habari Maelezo Faki Mjaka akiuliza swali kwa Waziri wa Fedha na Mipango juu ya siku ya Idadi ya Watu duniani katika mkutano uliofanyika Wizarani kwake Vuga.
 Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed akitoa ufafanuzi wa maswali alioulizwa na wandishi wa habari.
Picha na Makame Mshenga.

TAMASHA LA TISA LA MUZIKI LA CHAMWINO KUUNGURUMA MJINI DODOMA JULAI 21 HADI 23, 2017

TANZANIA KUONESHA NGUVU YAKE YA UCHUMI WA VIWANDA DESEMBA MWAKA HUU KATIKA MAONESHO MAALUM

Wasomi WAACHE KULALAMIKA NA KUJIKITA KWENYE TAFITI ZAIDI - MHE BENJAMIN MKAPA

mafunzo ya kutambulisha kazi za wasaidizi wa sheria, kwa masheha na madiwani wa Mkoa wa kusini Pemba

0
0
 MRATIBU wa mafunzo ya kutambulisha kazi za wasaidizi wa sheria, kutoka Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Safia Saleh Sultan, akielezea lengo la mafunzo hayo, kwa masheha na madiwani wa Mkoa wa kusini Pemba, yaliofanyika ofisi ya ZLSC mjini Chakechake
 MRATIBU wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Fatma Khamis Hemed, akielezea kazi na mikakati ya kituo, kwenye mafunzo ya kutambulisha kazi za wasaidizi wa sheria, kwa masheha na madiwani wa Mkoa wa kusini Pemba, kwenye mafunzo yalifanyika Kituoni kwao Chakechake
 Katibu tawala wilaya ya Chakechake, Sheha Mpate Mtumwa, akifungua mafunzo ya kutambulisha kazi za wasaidizi wa sheria, kwa masheha na madiwani wa Mkoa wa kusini Pemba, kwenye mafunzo hayo yaliofanyika Kituoni kwao Chakechake
 MTOA mada ya Ugatuzi wa madaraka Said Makame Said, akielezea maana ya ugatuzi, kwa madiwani na msheha wa Mkoa wa kusini Pemba, kwenye mafunzo hayo yaliotayarisha na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, na kufanyika osifini kwao mjini Chakechake Pemba
 AFISA Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Khalfan Amour Mohamed, akigusia kipengele cha mamlaka ya masheha kisheria, kwenye mafunzo ya kutambulisha kazi za wasaidizi wa sheria, kwa masheha na madiwani wa Mkoa wa kusini Pemba, yaliofanyika Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC mjini Chakechake
MASHEHA na Madiwani wa mkoa wa kusini Pemba, wakifuatilia mafunzo ya kutambulisha kazi za wasaidizi wa sheria, kwenye mafunzo yaliotayarishwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, na kufanyika ofisini kwao mjini Chakechake. (Picha na Haji Nassor, Pemba).

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango afanya ziara ya kushitukiza Ofisi za TRA na vituo vya mafuta Kigamboni

0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt. Philip Isdor  Mpango  (Mb)  akiongea na mmoja wa wananchi (anayemuonesha karatasi ) waliofika kulipa kodi ya majengo katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) – Kigamboni, ambapo alieleza kuridhishwa na utendaji wa watumishi katika mamlaka hiyo.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), aliyevaa miwani na kukunja mikono, akiwa amejichanganya katika kundi la wakazi wa mji wa Kigamboni waliojitokeza kulipa kodi ya majengo katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania-Kigamboni, akiwa na lengo la kuchunguza namna wananchi wanavyopata huduma. 

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt. Philip Isdor Mpango  (Mb) (kulia) akisalimiana na mmoja wa wakazi wa Mji wa Kigamboni waliojitokeza kulipa kodi katika Ofisi za mamlaka ya mapato Tanzania TRA-Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt. Philip Isdor  Mpango  (Mb), akiwapongeza na kuwashukuru wananchi wa Kigamboni waliojitokeza kulipa kodi ya majengo na kutoa rai kwa wananchi kujenga utamaduni wa kulipa kodi kwa hiari ili kufikia uchumi wa viwanda na kuendesha huduma za jamii.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiamuru Kituo cha Mafuta cha Mjimwema Kigamboni kifungwe, baada ya kubaini kuwa wamiliki wamekiuka masharti kwa kutotumia mashine maalumu za kielektroniki ya kutolea risiti hatua inayoikosesha Serikali mapato ya kodi.


Viewing all 109573 articles
Browse latest View live




Latest Images