Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

SAFARI YA MWISHO YA MAREHEMU HASSAN RASHID SHEBUGE, ALIYEKUWA KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI

0
0
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi Jumamosi Julai 6, 2017 ameongoza waombolezaji wakiwemo ndugu, jamaa, marafiki, majirani na wafanyakazi wenzie katika mazishi ya aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge aliyefariki dunia siku ya Alhamisi, Julai 6, 2017 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kupatwa na shinikizo la damu.
Marehemu Shebuge, aliyeagwa siku ya Ijumaa Julai 7, 2017 nyumbani kwake Mbagala Majimatitu Jijini Dar es Salaam amezikwa Jumamosi Julai 8, 2017 katika kijiji cha Funta, Bumbuli, mkoani Tanga.
 Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Rashid Shebuge likiwasili kwenye eneo la makaburi  la kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigella na waombolezaji wengine wakiwa kwenye mazishi ya aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge makaburi  ya kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya  aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge makaburi  ya kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigella  akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya  aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge makaburi  ya kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
Ndugu wa marehemu  akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya  aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge makaburi  ya kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
Msaidizi wa Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Noel Kaganda akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya  aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge makaburi  ya kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga. Kupata habari zaidi BOFYA HAPA

Chuo cha Uhasibu Arusha kinakaribisha maombi ya kujiunga na chuo hicho kwa muhula mpya katika ngazi mbalimbali

0
0
Chuo cha Uhasibu Arusha kinakaribisha maombi ya kujiunga na chuo hicho katika ngazi za Cheti, Diploma, Bachelor, Postgraduate diploma na Masters katika fani zifuatazo:

- Accountancy

- Finance and Banking

- Business Management

- Economics and Finance

-Computer Science na
- Information Technology
Chuo kina kampasi Arusha, Dar es salaam,
Mwanza na Babati mkoani Manyara.

Watumishi wa IAA katika banda lao viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Nyerere (SABASABA) barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam wakiwa tayari kukuhudimia. Banda lao lipo jengo la Wizara ya Fedha na mipango.

MAGAZETI YA JUMATATU LEO JULY 10,2017

TANZIA ; KIFO CHA SETH KATENDE

0
0

Kwa majonzi makubwa, uongozi na wafanyakazi wote wa Efm radio na tv-E , unasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi mwenzetu Seth Katende – maarufu kama bikira wa kisukuma kilichotokea Julai 9 katika hospitali ya taifa Muhimbili.

Ni vigumu sana kuamini na kukubali msiba huu mzito kwetu lakini kwakuwa sisi ni binadamu na kila nafsi lazima ionje umauti, tunamuomba mwenyezi mungu aipumzishe roho ya marehemu mpendwa wetu seth katende mahali pema, Amina.

Uongozi na wafanyakazi wa Efm radio na tv-E unatoa pole kwa familia ya marehemu na wasikilizaji wetu wote walioguswa na msiba huu.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe, Amina.
 Marehemu Seth Katende (Bikira wa Kisukuma) enzi za uhai wake akiwa  studio, Efm redio. 
Kutoka kushoto marehemu Seth Katende akiwa na timu nzima ya kipindi cha ubaoni alichokua akitangaza. 

NEWZ ALERT:MBUNGE HALIMA MDEE AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU HIVI PUNDE.

0
0
Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima mdee, akiwa amehifadhiwa katika ukumbi wa Wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri kusomewa kesi yake.

Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima mdee akisalimiana na Mbunge wa Bunda Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) , Ester Bulaya, akiwa amehifadhiwa katika ukumbi wa Wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri kusomewa kesi yake.

TAARIFA ZAIDI TUTAWALETEA BAADAE KIDOGO.

Tazama matangazo ya moja kwa moja kutoka Chato Mkoani Geita Hivi sasa.

0
0

Tazama matangazo ya moja kwa moja kutoka Chato Mkoani Geita ambapo Mhe. Rais John Pombe Magufuli atashuhudia makabidhiano ya nyumba 50 za watumishi wa afya za mikoa ya Geita, Kagera na Simiyu. 

Pia atashuhudia makabidhiano ya kiwanda cha alizeti za Chato. Sherehe hizo zinahudhuriwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na Balozi wa Japan Mhe. Masaharu Yoshida.

 Matangazo haya yatarushwa moja kwa moja na TBC1, Azam TV, TBC Taifa, Clouds TV na kupitia tovuti rasmi ya Ikulu ambayo niwww.ikulu.go.tz kuanzia saa 4:00 asubuhi hii. 

Karibuni.

BREAKING NEWZZZZ: MHE WILLIAM MGANGA NGELEJA AREJESHA MGAO WA ESCROW

0
0
Mbunge wa Sengerema na Waziri wa Nishati na Madini Mhe, William Ngeleja akiongea na wanahabari leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Habari Bi. Zamaradi Kawawa.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

YAH: KURUDISHA FEDHA (TZS MILIONI 40.4) NILIZOPEWA NA NDUGU JAMES RUGEMALIRA WA KAMPUNI YA VIP ENGINEERING AND MARKETING LTD



1. Kama inavyokumbukwa, kutokana na ukweli kwamba ilisharipotiwa sana kwenye vyombo vya habari,  kwamba tarehe 12/02/2014 nilipokea fedha kiasi cha shilingi milioni 40.4 za kitanzania kutoka kwa Ndugu James Rugemalira, mmiliki wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd. Fedha hizo nilizipokea kupitia akaunti yangu namba 00110102352601 ya Benki ya Mkombozi.

2. Fedha hizo nilizipokea, kwa nia njema, kama msaada/mchango kutoka kwa ndugu Rugemalira ili zinisaidie katika kutimiza majukumu yangu ya kibunge, hususan,kusaidiana na wananchi wa jimbo langu la Sengerema na Taifa kwa ujumla, kutekeleza shughuli za kijamii (mfano ujenzi wa makanisa, misikiti, kusaidia kulipia karo za wanafunzi wasiojiweza, n.k) na shughuli za miradi ya maendeleo ambayo haipo kwenye bajeti ya serikali.



3. Nilipokea Fedha hizo kutoka kwa ndugu Rugemalira bila kujua kwamba fedha hizo zilikuwa zinahusishwa na kashfa ya akaunti ya fedha za Escrow kama ilivyo sasa.
4. Fomu ya Tamko langu kama kiongozi wa umma kuhusu rasilimali na madeni kwa mujibu wa sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 kwa kipindi kilichoishia 31 Desemba, 2014, niliyoiwasilisha ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma tarehe 24/12/2014 ilijumuisha msaada huu wa shilingi milioni 40.4 kutoka kwa ndugu James Rugemalira.
5. Tarehe 15/01/2015 nililipa kodi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kiasi cha Shilingi 13,138,125/= ikiwa ni sawa na asilimia 30 (30%) ya msaada huo niliopewa, kama ilivyoelekezwa na TRA.


SABABU ZA KURUDISHA FEDHA HIZI

i) Nilipokea msaada huu kama wapokeavyo wabunge wengine, kwa nia njema, bila kujua kwamba James Rugemalira baadaye angekuja kuhusishwa na kashfa ya fedha za akaunti ya ESCROW kama ilivyo sasa.



ii) Kwa vile sasa imedhihirika kwamba aliyenipa msaada huu anatuhumiwa kwenye kashfa ya akaunti ya ESCROW, nimepima na kutafakari, na hatimaye nimeamua, kwa hiari yangu mwenyewe, kurejesha serikalini (TRA) fedha zote nilizopewa kama msaada (TZS milioni 40.4) bila kujali kwamba nilishazilipia kodi ya mapato kama nilivyoeleza hapo awali. Risiti ya  ushahidi wa kurejesha fedha hizi serikalini hii hapa.



iii) Nimeamua kurejesha fedha hizi hata kama aliyenipa msaada bado ni mtuhumiwa tu, kwa vile hajathibitika kupatikana  na hatia, kwa sababu sitaki kuwa sehemu ya kashfa/tuhuma hizo.



iiii) Leo nina zaidi ya miaka 12 nikiwa kiongozi wa Umma, na pia niliwahi kuitumikia wizara ya Nishati na Madini kwa takribani miaka mitano na nusu ( Naibu Waziri/Waziri), lakini sijawahi kukumbwa na kashfa ya rushwa au ufisadi. Kwa hiyo nimesononeka na kufadhaika sana kuona kuwa msaada niliopewa sasa unahusishwa na tuhuma.



v) Ninarudisha fedha hizi ili kulinda heshima na maslahi mapana ya nchi yangu, chama changu (CCM), Serikali yangu, Jimbo langu la Sengerema, familia yangu na heshima yangu mwenyewe.
HITIMISHO
• Kupokea msaada ni jambo la kawaida, ila ikibainika kuwa msaada unaopewa una harufu ya uchafu hata kama haujathibitishwa na vyombo husika ni vyema kujiepusha nao.
• Ninampongeza, kwa dhati kabisa, Rais wetu mpendwa Dr John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya kwa maslahi ya Taifa letu. Nami naungana na watanzania wenzangu wazalendo kumuombea kwa Mungu na namhakikishia nitaendelea  kumuunga mkono kwa kupigania maendeleo ya nchi yetu.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania
                                                   ________________________



William Mganga Ngeleja (Mb)

Jimbo la Sengerema
10/07/2017

INTRODUCING KIPINDI KIPYA CHA Soga za Diaspora S01E01 - With Jack Massai Marlow.


Airtel na GSMA wandaa mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia simu za mkononi

0
0
Kampuni ya simu za mkoni ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na GSMA wameandaa mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia simu za mkononi ambayo yanafanyika jijini Dar es Salaam kwa mwaka wa pili mfululizo.

Mashindano hayo ambayo yamedhaminiwa na Airtel money na Comviva wakishirikiana na muungano wa mashirika ya simu za mkononi ulimwenguni GSMA yanajumuisha washiriki kutoka Africa. Wajasiriamali wa TEKNOHAMA kutoka Ghana, Kenya, Uganda na Tanzania watachuana kutengeza suluhu kwenye maeneo makuu matatu, yaani malipo kwenye sekta ya usafirishaji, mfumo wa malipo ya jumla (bulk payment )na mfumo wa malipo ya pochi ya Comviva na Airtel yaani ( Airtel Comviva mobile wallet). 

Tanzania imepata fursa ya kuandaa mashindano hayo kwasababu inajulikana kama kiongozi katika sekta ya simu za mkononi inayoongoza katika kujenga mifumo ya malipo ya simu ( mobile money payment) Hivyo ni fursa ya kipekee kwa wajisiriamali wa kitanzania kuweza kutengeneza suluhu za mifumo ya malipo ya simu za mkononi zitakazotumika barani Africa.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo, Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda alisema ushirikiano huu ni muhimu kwa vile unawezesha wajasiriamali wa TEKNOHAMA kuja na suluhu ambayo itaweza kusaidia kufanya malipo kupitia simu za mkononi kwa haraka na hivyo kuokoa kupoteza muda kupanga foleni kusubiria kufanya malipo.

Sisi Airtel Tanzania tumekuwa msitari wa mbele kuwezesha wajasiriamali kwa njia mbali mbali. Kwa kupitia mashindano tunaendeleza uwezeshaji huo kwani kwa kila suluhu itakayopatikana haitaishia hapa mbali itaendelea kuboresha na kuwekwa kwenye mfumo wa malipo ya simu za mkononi, alisema Nchunda.

Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha Teknohama GSMA Gareth Pateman alisema washiriki wa mashindano hayo wanaweza kutengeneza suluhi moja au mbili katika zile tatu huku mshindi akipata ticketi ya kwenda Barcelona, Spain huku akiwa amelipiwa gharama zote.
Mkuu wa Ktengo cha TEKNOHAMA kutoka GSMA Gareth Pateman akitoa mafunzo kwa washiriki kutoka Tanzania wakati mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia simu za mkononi yanayodhaminiwa na Airtel money na Comviva wakishirikiana na muungano wa mashirika ya simu za mkononi ulimwenguni GSMA.
Mkuu wa Ktengo cha TEKNOHAMA kutoka GSMA Gareth Pateman akitoa mafunzo kwa washiriki wa mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia simu za mkononi yanayodhaminiwa na Airtel money na Comviva wakishirikiana na muungano wa mashirika ya simu za mkononi ulimwenguni GSMA
Mkuu wa Ktengo cha TEKNOHAMA kutoka GSMA Gareth Pateman akitoa mafunzo kwa washiriki wa mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia simu za mkononi yanayodhaminiwa na Airtel money na Comviva wakishirikiana na muungano wa mashirika ya simu za mkononi ulimwenguni GSMA
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Isack Nchunda, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana baada ya ufunguzi wa mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia simu za mkononi yanayodhaminiwa na Airtel money na Comviva wakishirikiana na muungano wa mashirika ya simu za mkononi ulimwenguni GSMA.

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOA WA MBEYA LAMUAGA KAMANDA ASF A. MANDOFU NA KUMKARIBISHA KAMANDA ACF J.S IKONKO MKOANI MBEYA

0
0
Kamanda muagwa  Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji A. Mwandofu akiwaaga baadhi ya Askari na maafisa wa jeshi la zimamoto na ukoaji mkoa wa mbeya katika hafla fupi ya kumuaga na kumkaribisha kamanda Kamishna msaidizi J.S Ikonko Kuwa kamanda wa jeshi hilo la Zimamoto na Uokoji mkoa wa mbeya.
Kamanda Kamishna msaidizi J.S Ikonko zkizungumza na baadhi ya Askari wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa mbeya (hawapo pichani) Mara baada ya kukaribishwa rasmi kuwa kamanda wa jeshi la zimamoto na Uokoaji  kwa mkoa wa mbeya.

Kulia ni kamanda wa Jeshi la magereza mkoa wa mbeya SACP, Paul Mwankingi (Mgeni Rasmi) akipokea zawadi ya Kifaa cha kuzimia Moto kutoka kwa Askari Poul Kabwogi katika Tafrija fupi ya kumuaga Kamanda muagwa  mrakibu msaidizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji A.Mwandofu na kumkaribisha kamanda Kamishna msaidizi J.S Ikonko Kuwa kamanda wa jeshi hilo la Zimamoto na Uokoji mkoa wa mbeya.
Picha ya Pamoja mgeni rasmi kamanda wa Jeshi la magereza mkoa wa mbeya SACP, Poul Mwankingi, Kamanda muagwa  mrakibu msaidizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji A.Mwandofu, kamanda mpya Kamishna msaidizi J.S Ikonko, Maafisa na Askari wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa mbeya sanjari na wageni waalikwa walio hudhuria hafla hiyo iliyo fanyika katika ukumbi mdogo wa mkapa uliopo jijini mbeya siku ya tarehe 8,07,2017. 
 PICHA ZOTE NA MR.PENGO MBEYA.
MAELEZO NA FC EMMANUEL SPALIKA (PREI MBEYA)

HUDUMA YA MSAADA WA KISHERIA CHINI YA RC MAKONDA WANUFAISHA WAKAZI 80, 000 DAR

0
0
NA LUGENZI KABALE

AKIITIKIA agizo la Rais John Pombe Magufuli alilowataka wateule wake kuwa wabunifu na kujituma ili kuwaondolea wananchi shida mbalimbali , Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ametatua migogoro takribani 8, 000 iliyowahusisha zaidi ya watu 80, 000 ndani ya takribani miezi minane kati ya Disemba mwaka jana na Mwezi Juni mwaka huu.

Makonda ametekeleza jukumu hilo kupitia timu ya wanasheria 35 wanaojitolea kutoa huduma ya msaada wa kisheria bure kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.

Kiongozi wa timu ya Wanasheria hao, Georgia Kamina, aliitaja baadhi ya migogoro ambayo timu yake imekuwa ikisuluhisha kupitia Ofisi za Wakuu wa Wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam kuwa ni ile ya umiliki wa ardhi na michakato ya mirathi mahakamani na katika ngazi ya familia,

Migogoro mingine ambayo timu hiyo ya wanasheria imekuwa ikimsaidia Makonda kuitatua kwa kushirikiana na Wakuu wa wilaya ya Ilala (Sofia Mjema), Kinondoni (Ally Hapi), Temeke ( Felix Lyaniva ), Ubungo (Kisare Makori ) na Kigamboni (_Hashimu Mgandilwa ) ni pamoja na ndoa na matunzo ya watoto kwa ndoa zilizo sambaratika, ajira na mikataba ya ajira, ubakaji, faili kupotea mahakamani, ucheleweshwaji wa kesi mahakamani, umiliki wa nyumba, umiliki au mauziano ya ardhi, mikopo kutoka mabenki ya biashara, uuzwaji mali mbalimbali kwa kukiuka sheria au makubaliano na hata ukosefu wa uaminifu.

Akiiongea kwa niaba ya Makonda, Kamina aliliambia Habari LEO katika mahojiano maalum yaliyofanyika hivi karibuni katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa, Ilala Boma Jijini Dar es Salaam hivi karibuni, alitaja migogoro wanayopokea na inayotia fora katika mkoa wa Dar es Salaam kuwa ni ile inayohusisha masuala ya mirathi, umiliki wa ardhi, ajira na mikataba kati ya waajiri na waajiriwa, ndoa na matunzo ya watoto kwa ndoa zilizo sambaratika na baadhi ya wananchi kuingia mikataba mibovu na mabenki katika harakati za kupata mitaji ya biashara.

"Mheshimiwa Paul Makonda alichukua jukumu la kuanzisha huduma ya msaada wa kisheria bure kwa wananchi kutokana na uzoefu alioupata katika ziara ya kukutana na wananchi aliyofanya mkoa mzima mwezi Novemba mwaka jana," alibainisha Kamina na kuongeza kuwa ili kuwaepusha wananchi na mchakato mrefu na unaoumiza wa kumaliza migogoro yao mahakamani aliamua kuunda timu ya wanasheria wa kujitolea ili kutekeleza dhamira hiyo ya kuwasaidia wananchi wenye migogoro mbalimbali ya kisheria.
Kiongozi wa timu ya wanasheria hao aliongeza kwa kusema kuwa Mkuu wa Mkoa aliguswa na namna baadhi ya wananchi walivyokuwa wakipoteza mashamba, nyumba, mali na hata kufukuzwa kazi kwa uonevu kwa kukosa uelewa wa sheria.

Kesi ya Shambulio inayomkabili Adam Kighoma Malima kuanza kusikilizwa mwezi Ujao

0
0
Na Karama Kenyunko, blog ya jamii.

Kesi ya shambulio inayomkabili aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mbunge mstaafu wa Mkuranga, Mhe. Adam Kighoma Malima na mwenzake kuanza kusikilizwa Agosti 9, mwaka huu.

Hatua hii imekuja baada ya upande wa mashtaka kukamilisha upelekezi na kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali (PH).

Katika hali hiyo, Malima anashtakiwa pamoja na Ramadhani Mohamed.Wamesomewa PH, na Wakili wa Serikali, Ester Martin mapema Leo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage.

Katika maelezo hayo, Malima na Mohammed wamekubali maelezo yao binafsi, siku ya tukio kuwa walikuwepo Masaki, walikamatwa na kushtakiwa na wamekanusha tuhuma zote zinazowakabili.

Katika kesi hiyo, Malima anadaiwa kuwa Mei 15,2017 katika eneo la Masaki kwa makusudi alimzuia ofisa wa polisi H.7818 PC ABDU kufanya kazi yake halali.Malima anadaiwa kumzuia afisa huyo kufanya kazi yake ya kumkamata Ramadhani Kigwande kwa kosa la kumshambulia Mwita Joseph.
Kwa upande wa mshtakiwa wa kwanza, Ramadhani Mohammed Kigwande Naye anakabiliwa na shtaka la kumshambulia Mwita Joseph.
Ilidaiwa, Mei 15,2017 huko huko Masaki mshtakiwa Ramadhani akiwa na nia ya kumzuia Mwita Joseph ambaye ni afisa oparesheni wa kampuni ya Priscane Business Enterprises wakati alipokuwa akimkamata kwa kupaki vibaya gari namba T 587 DDL alimshambulia na kumsababishia maumivu.
Washtakiwa wote wapo nje kwa dhamana hadi Agosti 9, mwaka huu.

WANANCHI WAHAMASISHWA KUFANYA KAZI KWA AJILI YA MAENDELEO

0
0
 Mkazi wa kijiji cha Mwande kata ya Mateteleka halmashauri ya wilaya ya Madaba,mkoani Ruvuma Thobias Ngulungula akitoa malalamiko yake ya ahadi ya Rais Dkt John Magufuri ya kutoa shilingi milioni 50 kwa kijiji mbele ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Madaba Shafi Mpenda(hayupo pichani)wakati wa mkutano wa hadhara kijijini hapo jana. ambapo ameiomba serikali kuharakisha ukutekeleza ahadi hiyo ili iwasaidie wananchi kuanzisha vikundi vya kiuchumi katika vijiji vyao.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Madaba, mkoani Ruvuma Shafi Mpenda akizungumza jana  na wakazi wa kijiji cha Mwande kataya Mateteleka wilayani Songea katika mkutano wa hadhara uliolenga kuhamasisha kazi za maendeleo kijijini hapo baada ya serikali kuanzisha kijiji hicho kwa  lengo la kusogeza huduma mbalimbali za kijamii karibu na wananchi wa kijiji hicho.

Mwandishi na Muongozaji wa filamu Amil Shivji aelezea filamu ya T-Junction iliyofungua pazia tamasha la ZIFF 2017

0
0
Mwandishi na Muongozaji wa filamu katika kampuni ya KIJIWENI Production, Amil Shivji akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau wa masuala ya filamu (hawapo pichani) mapema leo Julai 9,2017 wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.
Mwandishi na Muongozaji wa filamu katika kampuni ya KIJIWENI Production, Amil Shivji akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau wa masuala ya filamu mapema leo Julai 9,2017 wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.
Muigizaji mpya Hawa Ally alietumia jina la Fatuma akielezea namna alivyoweza kuucheza uhusika kwenye filamu ya T-junction. Kushoto ni Mwandishi na Muongozaji wa filamu katika kampuni ya KIJIWENI Production, Amil Shivji mapema leo Julai 9,2017 wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.
Mwandishi na Muongozaji wa filamu katika kampuni ya KIJIWENI Production, Amil Shivji akiwatambulisha Hawa Ally (Fatima) na Magdalena Christopher (Maria) mapema leo Julai 9,2017 wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.
Amil Shivji (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) na baba yake mzazi  Profesa Issa Shivji mara baada ya uzinduzi huo wa tamasha la 20 la ZIFF 2017. (PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE).

TAARIFA MUHIMU KWA WARUFANI WA UHALALI WA VYETI


BREAKING NEWZZZZ: Uteuzi wa Mwenyekiti pamoja na wajumbe wote wa Baraza la Michezo Tanzania wasitishwa.

0
0
Na Shamimu Nyaki WHUSM.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe, amesitisha uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Baraza la Michezo la Taifa kuanzia leo Julai 10 2017 kufuatia Baraza hilo kushindwa kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Michezo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo Dkt Mwakyembe ameeleza kuwa, amelivunja Baraza hilo kwa mamlaka aliyopewa na Sheria ya BMT Na.12 ya mwaka 1967 iliyofanyiwa marekebisho na Sheria Na.6 ya mwaka 1971 pamoja na kanuni zake za mwaka 1999. 

Waziri Mwakyembe amechukua uamuzi huo kutokana na maagizo aliyopewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika hotuba yake ya kuahirirsha Bunge Mjini Dododma Julai 5 mwaka huu, ya kufanya mapitio na kulitathmini upya Baraza hilo.

“Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliniagiza nilifanyie mapitio na kulitathmini upya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ili kujiridhisha na usimamizi wake wa shughuli za michezo nchini, na kwamba ikidhihirika kwamba usimamizi wa BMT wa michezo nchini si imara basi ninaweza kulivunja Baraza lililopo na kuunda upya.” Alisema Waziri Mwakyembe.

Aidha Waziri Mwakyembe ameeleza kuwa Baraza hilo limeshindwa kutafuta njia bora za kuondoa changamoto ambazo zilikua zinahitaji utashi na dhamira ya kujituma, ikiwemo Viongozi wa michezo kushika nafasi zaidi ya moja, kushindwa kusimamia ushiriki wa wanamichezo wa Tanzania na wa nje katika michezo mbalimbali.

Pia Waziri Mwakyembe alizitaja sababu nyingine za kuvunjwa kwa BMT kuwa ni Uchaguzi wa vyama vya michezo nchini kugubikwa na ubabe na rushwa, mapromota wa mchezo wa ngumi nchini kuendesha shughuli zao bila kusajiliwa, pamoja na kanuni za vyama vya michezo kukosa uhakiki wa kubaini upungufu kuhusu masuala ya fedha.

Hata hivyo Sektretarieti ya Baraza itaendelea kufanya kazi katika kipindi hiki kwa kushirikiana kwaukaribu na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakati taratibu za kumpata mwenyekiti na wajumbe wapya zikiendelea kufanyika kwa mujibu wa Sheria.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akisitisha uteuzi wa Mwenyekiti pamoja na wajumbe wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Michezo Yusuph Singo na kushoto ni Msajili wa Vyama vya Michezo nchini Bw. Ibrahim Sapi Mkwawa. Picha na Eliphace Mrawa - Maelezo

Efm radio na TV-E zaomboleza kifo cha mfanyakazi mwenzao Seth Katende aka bikira wa kisukuma

0
0
Kwa majonzi makubwa, uongozi na wafanyakazi wote  wa Efm radio na TV-E , unasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi mwenzetu Seth Katende – maarufu kama Bikira wa Kisukuma kilichotokea Julai 9, 2017  katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.

Uongozi na wafanyakazi wa Efm radio na TV-E unatoa pole kwa familia ya marehemu na wasikilizaji wetu wote walioguswa na msiba huu.

Ni vigumu sana kuamini na kukubali msiba huu mzito kwetu lakini kwa kuwa sisi ni binadamu na kila nafsi lazima ionje umauti, tunamuomba Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu mpendwa wetu Seth Katende mahali pema peponi.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe 
Amina

INTRODUCING NEW AUDIO "Mtoto Mbichi" by Kayumba Ft. Aslay from Mkubwa na Wanawe

ZOEZI LA KUORODHESHA KAYA KWA AJILI YA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI KUANZA KESHO

0
0
Na Veronica Kazimoto 

WADADISI wa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 wameaswa kuzingatia maadili ya kazi wakati wa zoezi la kuorozesha kaya linalotarajia kuanza kesho ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya utafiti huo.

Akizungumza wakati wa mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa wadadisi hao, Meneja wa Takwimu za Jamii na Watu, Sylvia Meku kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu amesema ili kufanikisha zoezi la uorodheshaji wa kaya, ni lazima wadadisi hao wakazingatia maadili ya kazi pamoja na kufuata taratibu zote za Utumishi wa Umma.

“Ofisi ya Taifa ya Takwimu inawaagiza kwenda kwenye jamii kwa ajili ya kuorodhesha kaya zitakazofanyiwa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Natumaini mtatii na kuheshimu maadili ya Utumishi wa Umma ili muweze kufanikisha kazi hii kwa ufanisi,” amesema Slyvia Meku.

Amesema Zoezi la Uorodheshaji wa Kaya litafanyika mikoa yote ya Tanzania Bara kwa takribani siku 15 kuanzia kesho Julai 11, 2017 na baadae kufuatiwa na utafiti wenyewe unaotarajia kuanza mwezi Desemba, 2017.

Sylvia Meku amesema utafiti huu unafanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango na baadhi ya Wadau wa Maendeleo kwa lengo la kuangalia kiwango cha umasikini nchini. 
 Meneja wa Takwimu za Jamii na Watu Bi. Sylvia Meku akizungumza wakati wa mafunzo ya Wadadisi watakaokwenda kuorozesha kaya mikoa yote kwa ajili ya maandalizi ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya litafanyika kwa muda wa siku kumi na tano (15) kuanzia kesho tarehe 11 Julai, 2017.
  Baadhi ya Wadadisi wakimsikiliza kwa makini Meneja wa Takwimu za Jamii na Watu Bi. Sylvia Meku (hayupo Pichani) wakati wa mafunzo ya Wadadisi watakaokwenda kuorozesha kaya mikoa yote kwa ajili ya maandalizi ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya litafanyika kwa muda wa siku kumi na tano (15) kuanzia kesho tarehe 11 Julai, 2017.
Baadhi ya Wadadisi wakiwa kwenye gari wakielekea Kata ya Mchikichini, Ilala na Kawe jijini Dar es Salaam kufanya mazoezi ya kuorozesha kaya kwa vitendo kwa ajili ya maandalizi ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya litafanyika kwa muda wa siku kumi na tano (15) kuanzia kesho tarehe 11 Julai, 2017.
 Baadhi ya Wadadisi wakielekezwa namna ya kutumia ramani wakati wa kufanya mazoezi ya kuorozesha kaya kwa vitendo na Mtalaam wa Ramani Jumanne Msuya wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (katikati) kwa ajili ya maandalizi ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya litafanyika kwa muda wa siku kumi na tano (15) kuanzia kesho tarehe 11 Julai, 2017.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL GHULA)

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU WAKAZI WA MAHENGE NA LINDI KULIPWA FIDIA YA MRADI WA MADINI YA GRAPHITE

Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images