Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1790 | 1791 | (Page 1792) | 1793 | 1794 | .... | 3353 | newer

  0 0

  MKURUGENZI mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma Shafi Mpenda, amekifungia kituo cha kitengo cha utafiti wa sayansi ya tiba asili na tiba mbadala kinachojishughulisha na kupima afya za binadamu na kutibu magonjwa mbalimbali cha The King Solomon of Sanitarium clinik hadi hapo wataalam wa afya watakapojiridhisha uhalali wake.

  Mbali na kukifungia kituo hicho,Mpenda amesema atawachukulia hatua kali baadhi ya wataalam wake wa idara ya afya walioshiriki kutoa vibali feki vilivyohalalisha kituo hicho kufanya kazi ambayo imeonekana kama kuwatapeli wananchi.

  Kwa mujibu wa Mpenda ni kwamba, kituo hicho kupitia kwa mmiliki wake Selemani Nzaganya kimekuwa kikifanya shughuli zake kinyume na taratibu ambapo hata leseni kutoka kwa baraza la tiba asili kimekwisha muda wake tangu tarehe 1 januari mwaka huu,hata hivyo bado akifanya shughuli zake bila kupata leseni mpya jambo ambalo ni kosa kinyume cha sheria.

  Alisema, amelazimika kufunga kituo hicho kwa ajili ya kuokoa maisha ya wansanchi kwani hata mtu aliyekutwa akihudumia wananchi hana taaluma yoyote inayomwezesha kuhudumia wagonjwa jambo linaloonekana ni hatari kwa afya za watu.

  Kwa mujibu wa Mpenda hii ni mara ya pili kufunga kituo kama hicho na ni kampeni ya kudumu kwa wale wote wanaofanya shughuli za kuwatapeli wananchi wa Madaba ambapo ametoa onyo kwa watu wengine wenye tama ya kupata fedha kwa njia ya ujanja ujanja kutafuta maeneo mengine ya kufanya shughuli zao.

  Hata hivyo kwa mujibu wa majirani ambao hawakutaka kutaja majina yao,wameipongeza serikali kwa uamuzi wa kukifungia kituo hicho kwani wamiliki wake walikuwa wakiwaibia wananchi.

  Walisema, kituo hicho kimekuwa sehemu ya tatizo kwa sababu hata wananchi wanaohitajika kupata ushauri na matibabu hospitalini wamekuwa wakifika katika kituo hicho kwa kuamini kwamba watapata suluhu ya matatizo yao kumbe wanazidisha ukubwa wa matizo waliyonayo.

  Kwa upande wake mtu aliyekutwa akitoa huduma katika kituo hicho Ezakiel Mwakatumbula alisema, wamekuwa wanatoa huduma za matibabu kwa wa magonjwa mbalimbali hasa magonjwa sugu kwa kutumkia dawa za mimea,chakula na matunda.

  Hata hivyo alikanusha kufanya shughuli zao kitapeli na kusisitiza kuwa huduma wanazotoa zimekuwa zikiwasaidia sana wananchi kuokoa maisha yao.


  0 0

  Mwenyekiti wa Klabu ya Gymkhana, Walter Chipeta (kulia) akikabidhi kikombe kwa nahodha wa timu ya mpira wa miguu wa klabu ya Gymkhana Ali Mmandi (mwenye jezi ya kijani) baada ya timu yake kuibuka kidedea katika michuano ya kuelekea katika kilele cha maadhimisho ya miaka 100 ya klabu hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jana jijini Dar es salaam.

  Mwenyekiti wa Klabu ya Gymkhana, Walter Chipeta (kulia) akikabidhi kikombe kwa nahodha wa timu ya mpira wa miguu wa klabu ya Gymkhana Ali Mmandi (mwenye jezi ya kijani) baada ya timu yake kuibuka kidedea katika michuano ya kuelekea katika kilele cha maadhimisho ya miaka 100 ya klabu hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jana jijini Dar es salaam.
  Kapteni wa Mchezo wa Snooker wa Klabu ya Gymkhana, Shaizad Bhanji akishiriki katika mashindano ya kuelekea katika kilele cha maadhimisho ya miaka 100 ya klabu hiyo katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es salaam hivi karibuni.

  Michuano ya mpira wa miguu ikiendelea

  Mchezaji wa mpira wa Golf  Mwanaidi Ibrahim akishiriki katika michuano ya kuelekea katika kilele cha maadhimisho ya miaka 100 ya klabu hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jana jijini Dar es salaam.

  0 0

   Kaimu Afisa Habari wa Jeshi La Kujenga Taifa (JKT),Kanal Separatus Lubinga  akitoa maelezo kwa Waziri wa kazi, Uwezeshaji, Wazee ,Vijana na Maendeleo kwa watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maudline Cyrus Castico alipotembelea Maonesho ya 41 ya Sabasaba
   SSGT. Faustine Mabata kutoka Suma JKT Furniture akitoa maelezo kwa Waziri wa kazi, Uwezeshaji, Wazee ,Vijana na Maendeleo kwa watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maudline Cyrus Castico alipotembelea Maonesho ya 41 ya Sabasaba
    SSGT. Faustine Mabata kutoka Suma JKT Furniture akitoa maelezo kwa Waziri wa kazi, Uwezeshaji, Wazee ,Vijana na Maendeleo kwa watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maudline Cyrus Castico alipotembelea Maonesho ya 41 ya Sabasaba.


  0 0
  Jenerali Joseph Ole Nkaissery enzi za Uhai wake.
   
  Waziri huyo amefariki dunia saa chache baada yake kulazwa katika hospitali ya kibinafsi ya Karen kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu. 
  Taarifa za kifo chake zimetangazwa na mkuu wa utumishi wa umma Bw Joseph Kinyua mwendo wa saa kumi na moja alfajiri. 

  “Ni kwa huzuni kubwa na mshangao kwamba tunatangaza kifo cha ghafla cha Waziri wa Usalama wa Ndani Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery,” taarifa ya Bw Kinyua imesema. 

  “Taifa litaendelea kupashwa habari zaidi punde maelezo yatakapopatikana.”
  Jenerali Nkaissery amefariki siku chache baada ya mwanasiasa mkongwe G.G Gitahi aliyekuwa seneta wa jimbo la Laikipia kufariki dunia.

  Waziri wa elimu nchini Kenya Dkt Fred Matiang'i (pichani) ameteuliwa kuwa kaimu waziri wa usalama wa ndani kufuatia kifo cha aliyekuwa waziri Meja Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery.


  0 0  0 0


  · ‘App’ hii imelenga kuwasaidia watumiaji wake kupata taarifa muhimu kuhusu hoteli, usafiri, sehemu za vivutio, klabu, kasino, maduka makubwa, ubalozi na hospitali.

  Kampuni ya simu za mkononi Zantel ambao wanaongoza katika utoaji wa huduma bora za data, leo imezindua application ya simu inayojulikana kama ‘Discover Tanzania Mobile App” ambayo lengo lake ni kuhimiza utalii wa ndani na nje kwa lengo la kuwapatia watalii taarifa sahihi za maeneo ya utalii yanayopatikana na hapa nchini Tanzania.

  App hiyo itakuwa na taarifa zote za muhimu zinazopatikana hapa nchini zikiwamo kuhusu hoteli, usafiri, maeneo ya vivutio, kumbi za starehe, maduka makubwa, ubalozi na hospitali ambapo huduma hiyo itapatikana na kwenye Google Play Store kwa gharama nafuu ya Shilingi 500 tu.

  Akizungumzia huduma hiyo jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Zantel, Gasper Mbowa alisema, “Tunayofuraha kubwa kuzindua App hii ni kwa ajili ya wateja wetu, lakini jambo kubwa zaidi ni kuwa Zantel ndio Kampuni ya kwanza ya Mawasiliano kuanzisha huduma hii hapa nchini.” ‘Discover Tanzania mobile App’ ni rahisi kutumia na pia ni huduma ya bei nafuu kwa watu wote, kwa wageni na wenyeji. 


  Kwa muda wa siku tatu mteja wa Zantel atatumia kiasi cha shilingi 500, kwa siku saba mteja atatozwa shilingi 2000 na kwa mwezi mzima mteja atatozwa 3,000. Aliongeza kuwa alama ya siri kwa ajili ya kupata huduma hiyo kupitia sms au sauti kwa wateja wa Zantel ni 15582 ambapo watatozwa Tsh. 1 tu kwa sekunde.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Wananchi wakiwa katika shamba lililopo ndani ya Viwanja vya Sabasaba wakiambiwa namna ya kulima aina mbalimbali za mbogamboga Kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es salaam.

  Mkurugenzi wa Maendeleo wa kampuni ya Agri Must Lead Peter Mkufya akimuonesha mpiga picha wa Globu ya Jamii mbogamboga aina ya bilinganya inayolimwa ndani va viwanja vya Sabasaba.


  Wananchi wakiwa nadani ya shamba liliopo ndani ya Viwanja vya Sabasaba walipotembelea  Kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es salaam. Picha na Emanuel Massaka.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  Ikiwa ni katika kuboresha mazingira na kuepukana kutaka miti zipo njia nyingi sana za kuhakikisha mazingira yanaendelea kutunzwa na kuboreshwa, Kampuni ya Afri Tea and Coffee Blenders imekuja na suluhisho la kuachana na masuala ya ukataji miti ovyo.
  Watanzania wametakiwa kubadilika kwa kuacha kukata miti ovyo kwa ajili ya mkaa bali watumie nishati mbadala ambayo itasaidia katika kutunza mazingira.
  Hayo yamesemwa wakati akizungumza na Globu ya Jamii, Mkuu wa Masoko na Biashara wa Afri Tea and Coffee Blenders (ATCB)Zachy Mbenna amesema wamekuja na njia mbadala ya kuepukana na matumizi ya mkaa kwa kutengeneza nishati mbadala inayotengenezwa kwa mabaki ya miti (magome) aina ya miwati.
  Mbenna amesema, utumiaji wa magome hayo katika utengenezaji wa nishati mbadala umechukua nafasi ya ukataji miti hai ambapo watu wanatumia kutengeneza mkaa na kupelekea kuharibu mazingira.

  "Nishati hiyo mbadala ambayo inajulikana kama Briquets inatengenezwa kwa magome ya mabaki ya miti ya miwati ambayo inatumika kwa ajili ya kutengenezea ngozi, tulifikia hatua hii ya kutengeneza hizi baada ya kuona tunatumia zaidi ya tani nyingi zaidi za kuni ndani ya mwezi mmoja kitu ambacho kilikuwa kinatugharimu sana,"amesema Mbenna.

  "Baada ya kuona tumefanikiwa katika kupunguza gharama pamoja na ukataji wa miti kwa ajili ya kuni, baadhi ya viwanda navyo kutumia bidhaa hizi tukaamua kupeleka kwa wananchi kwa matumizi ya nyumbani ikiwemo pamoja na kuja na majiko yao maalumu kwani Briquets zinahitaji hewa ili kuweza kufanya kazi kwa uharaka zaidi, "amesema Mbenna.
  Ametoa wito kwa makampuni, taasisi na watu wengine watambue wao ndiyo watu wa kwanza wa kulinda mazingira na njia nzuri ni kutumia nishati mbadala ambayo ni njia bora ya kuhifadhi mazingira.
  Mkuu wa Masoko na Biashara wa kampuni ya Afri Tea and Coffee Blenders (ATCB) akielezea mkaa na aina ya majiko yanayotumika kwa nishati mbadala (Briquets) zinazotengenezwa kampuni ambapo yanapatikana kwenye maonesho ya 41 ya kimataifa ya biashara ya sabasaba yanayoendela Jijini Dar es salaam.
  Mkuu wa Masoko na Biashara wa kampuni ya Afri Tea and Coffee Blenders (ATCB) akionyesha  mkaa na aina ya majiko yanayotumika kwa nishati mbadala (Briquets) zinazotengenezwa kampuni ambapo yanapatikana kwenye maonesho ya 41 ya kimataifa ya biashara ya sabasaba yanayoendela Jijini Dar es salaam.
  Fundi wa majiko yanayojulikana kama Simba Stones akielezea namna nishati mbadala ya mkaa wa magome ya miti (Briquets) inavyofanya kazi kwnye majiko hayo yanayopatikana  kwenye maonesho ya 41 ya kimataifa ya biashara ya sabasaba yanayoendela Jijini Dar es salaam.
  Fundi wa majiko yanayojulikana kama Simba Stones akielezea kwa wananchi waliojitokeza katika banda lao namna nishati mbadala ya mkaa wa magome ya miti (Briquets) inavyofanya kazi kwnye majiko hayo yanayopatikana  kwenye maonesho ya 41 ya kimataifa ya biashara ya sabasaba yanayoendela Jijini Dar es salaam.

  0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.  Mtaalamu na mshauri wa masuala ya urembo na Ngozi Irene Moshi ametoa ushauri kwa kina mama hususani wasichana kutumia vipodozi vyenye vimea asilia ili kuepukana na kuharibu ngozi zao.

  Amesema hayo wakati akiongea na globu ya Jamii, Irene amesema kupitia saluni ya Timeless wameweza kuwasaidia watu wengi na kuwapatia tiba kuhusiana na masuala ya ngozi na hasa katika usahihi wa kutumia vipodozi vinavyoendana na ngozi ya muhusika.


  "Tunatoa ushauri wa kitaalamu kuhusiana na matumizi sahihi ya vipodozi kulingana na aina ya ngozi ya muhusika pia kutoa malekezo ya kutumia vitu sahihi kwa wakati sahihi kama vile kulingana na hali ya hewa kipindi cha joto na baridi,"amesema Irene.

  Amesema kuwa, anatoa ushauri kwa vijana hususani wa kike kujifunza zaidi masuala ya urembo kwani inaweza kusaidia katika kuboresha ngozi zao na wanaweza kutumia vipodozi sahihi na kutokuharibu ngozi zao.

  Mbali na kutoa tiba, Timeless walianza kutoa mafunzo rasmi mwaka 2016 Irene amesema kuwa wanatoa mafunzo kwa vijana wanaopendelea kufahamu shughuli mbalimbali za urembo ikiwemo tiba ya ngozi, upambaji ambapo wameweza kutoa vijana wengi kwa kipindi cha mwaka mmoja na tayari wengine wameshajiajiri katika sehemu zao na pia Timeless wanajishughulisha na masuala ya kupamba maharusi, nywele na kucha na mapambo ya maharusi ikwemo kadi.

  Mtaalamu na mshauri wa masuala ya urembo na Ngozi Irene Moshi akimuhudumia mteja aliyetembelea katika banda lao la Timeless Hair and Beauty Saloon kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es salaam.

   Mtaalamu na mshauri wa masuala ya urembo na Ngozi Irene Moshi akizungumza na Globu ya Jamii kuhusiana na masuala ya urembo wa ngozi na kuonyesha baadhi ya mapambo ya maharusi yanayopatikana kwenye saluni yao ya Timeless.
  Wateja wakiwa wanapata maelezo kutoka kwa  mfanyakazi wa Timeless Hair and Beauty Saloon katika banda laokwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es salaam.Picha na Emanuel Massaka,

  0 0

  --

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS), Profesa Dos  Santos Silayo  akiwa katika banda la TFS na Familia yake katika Maonesho ya 41 ya Sabasaba jijini Dar es Salaam ambapo aliweza kukagua namna ya shughuli za Tasisi hiyo zinavyofanywa .

  Afisa  Ufugaji Nyuki kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Mwanahamisi Mapolu   akizungumza na wawekezaji kutoka Oman waliofika katika  banda la TFS cujus ni aina gani ya Asali zinapatikana niching
  Mjumbe wa Bodi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)  Bi Sauda Simba akipata maelezo kutoka kwa Afisa Ufugaji Nyuki kutoka TFS, Mwanahamis Mapolu wakati alipotembelea Banda hilo katika maonesho ya 41 ya Sabasaba jijini Dar es Salaam
  Mjasiliamali kutoka Viana Kushoba wanaotengeneza Mashine ya makaa Mbadala akiwapa makaawakazi wa jiji waliomtembelea katika Maonesho ya 41 ya Sabasaba na kununua mkaa huo ambao ni rafiki wa mazingira na unazuia ukataji miti hivyo kusaidia katika kulinda misitu yetu.
  Afisa ufugaji Nyuki wa Shamba la miti la serikali la Sao Hill linalomilikiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS),Said Abubakary  akionesha waandishi wa habari moja ya malighafi inayotokana na misitu katika kutengeneza vipodozi vya aina mbalimbali

  0 0

   .Meneja Mradi wa Simba Motor, Brig Jenerali (Mstaafu), Michael Luwongo akizungumza katika utambulisho wa magari mpya ya Foton Motor leo jijini Dar es Salaam,kulia ni Meneja Mkuu Foton Motor Kenya Ltd, Apple Sun.
   .Kamishina wa Jeshi la Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Mstaafu, Suleman kova kushoto aliyefika katika utambulisho wa Magari ya kisasa ya Foton Motor jijini Dar es Salaaam, Kulia ni Rahma Kova.

  Muonekano wa magari mapya ya kampuni Foton Motor leo jijini Dar s es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelea gereji inayotengeneza  Magari ya RSA Limited  ya mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro kukagua maendeleo ya ukarabati na ubadilishaji mwonekano wa Magari mabovu 26 ya Jeshi la Polisi yaliyosafirishwa kwenda huko hivi karibuni.
  Akiwa katika gereji  hiyo Mhe. Makonda amejionea magari hayo yakiwa katika hatua mbalimbali za utengenezaji ambapo ameomba uongozi wa kampuni hiyo kukamilisha ukarabati wa magari hayo kwa wakati iliyaweze kuongezea ulinzi na usalama jijini Dar es salaam.
  Aidha RC Makonda amesema kuwa anataka kubadili mwonekano wa jeshi la polisi Mkoa wa Dar es salaam kwa kuhakikisha magari ya polisi yanakuwa na hali nzuri itakayowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa uufanisi kwa kuyabadili magari hayo kuwa kama yale ya Askari wa umoja wa mataifa.

  ”Hakuna kitu kinachoninyima usingizi kama pale mwananchi anapohitaji polisi wafike mahala pa tukio na polisi hawafiki, na kufanya hali ya amani kutoweka na wakati huohuo polisi wanataka kufanya kazi yao ila wanashindwa kutokana na uhaba wa vifaa.
  "Hii ndiyo sababu ninahangaika ili siku moja Dar es Salam iwe na amani hata kufikia hatua ya watu kufanya biashara zao kwa masaa 24 na kutembea kwa amani muda wote", alisema  RC Makonda.
  "Nimepata Pikipiki 200, baiskeli 500 na  kutengeneza magari haya 56 kuwa na viwango vya kimataifa kama magari ya Umoja wa Mataifa yanavyoonekana
  "Yaani kwenye gari ya doria itaweza kuwa na maafisa wa polisi tisa kwa nyuma, ambao watatu watakuwa kushoto na watatu kulia mwa gari hiyo huku wawili wakiwa nyuma ya gari hiyo na mmoja akiwa amesimama mbele na silaha kubwa", aliongeza  RC Makonda.
  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akikagua moja ya magari 26 ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es salaam yaliyopelekwa katika gereji  ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani Kilimanjaro kwa ukarabati ili yaendane na kazi ya jeshi la p0lisi
  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akijadiliana jamabo na uongozi wa gereji  ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani Kilimanjaro wakati alipokagua magari ya polisi yanayofanyiwa ukarabati mkubwa.
  Mkuu wa mkoa wa DEar es salaam Mh. Paul Makonda akiakizungumza na uongozi wa gereji  ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani Kilimanjaro
  Mkuu wa mkoa wa Dear es salaam Mhe. Paul Makonda akikagua moja ya magari 26 ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es salaam yaliyopelekwa katika Garage ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani Kilimanjaro.

  0 0


  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango,(pichani) amejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari na kuhimiza wananchi kufanya hivyo kwani moja ya faida kubwa ni kujihakikishia kuwa na bima ya Afya.

  Waziri aliyasema hayo leo Julai 8, 2017, wakati alipotembelea banda la PSPF lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, maarufu Sabasabawakati wa Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea.

  “Mimi nitoe wito kwa wananchi kujiunga zaidi na mpango huu kwani watafaidika na huduma ya afya na nyinyi muongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi ili wajiunge zaidi.” Alisema Mhe. Dkt. Mpango.

  Dkt. Mpango pia alikabidhiwa kadi yake ya uanachama muda mfupi baada ya kujiunga.

  “Mheshimiwa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari una faida nyingi na tumewalenga hasa watu wa kawaida kama vile wajasiriamali, wakulima, mama lishe, bodaboda, na machinga, na tumekuwa tukipata watu wengi wanaokuja kujisajili na Mpango huu na wengi wao wamevutiwa na hii Bima ya Afya ambayo ni moja ya faida azipatazo mwananchama” Alisema Afisa Uhusoano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi wakati akimkabidhi Mhe. Waziri akdi yake ya uanachama.

  Bw. Njaidi pia alimwambia Mhe. Waziri kuwa, kwa kujiunga kwake na Mpango huo wa uchangiaji wa Hiari, kutasaidia pia kuwakadia bima ya afya wasaidizi wake katika miradi kama vile ya shambani na ufugaji.

  “ Hawa wote wanawezakuingia kwenye mpango huu wa bima kupitia uanachama wako katika Mfuko.” Alimuhakikishia Mhe. Waziri.


  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, (kulia), akikabidhiwa kadi ya uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi, muda mfupi baada ya Mhe. Waziri kujiunga na Mpango huo leo Julai 8, 2017, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere kunakofanyika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, ambapo PSPF inatoa huduma zote kwenye Maonesho hayo.
  Waziri Dkt. Mpango, (kulia), akimsikilizia kwa makini Bw. Njaidi kuhusu faida zitokanazo na kujiunga na Mpango wa PSS

  Waziri Dkt. Mpango(kulia), akipokea fomu ya kujiunga na PSS, kutoka wka Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Msanii maarufu, Mrisho Mpoto. Katikati ni Afisa Habari Mwanamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi.

  Waziri Mpango (kulia), akiuliza maswali kwa maafisa wa PSPF.


  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  *Asema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi ya kuzalisha umeme wa Kinyerezi II na kusema kwamba ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wake.

  Amesema hayo leo (Jumamosi, Julai 08, 2017) alipotembelea mradi huo wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia unaojengwa eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam.

  Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa mradi huo kutaliwezesha Taifa kuwa na umeme wa uhakika, utakaowezesha kuendesha viwanda.

  Amesema mkakati wa Serikali ni kuongeza kiwango cha uzalishaji wa umeme ili Watanzania wapate umeme mwingi utakaosambazwa hadi vijijini kwa gharama nafuu.

  “Tunataka tupate umeme wa kutosha ili viwanda vitakavyojengwa viwe na nishati ya uhakika na ya gharama nafuu. Ni wajibu wetu kuendelea kuimarisha utekelezaji wa miradi hii.” Amesema.

  Naye, Meneja wa Mradi wa kuzalisha umeme wa Kinyerezi, Mhandisi Stephen Manda amesema gharama za mradi wa Kinyerezi II ni dola milioni 344.

  Meneja huyo amesema tayari mradi huo umefikia asilimia 66.32 ya ujenzi wake na sasa wako katika hatua mbalimbali za kukamilisha, ikiwemo ujenzi wa misingi ya mitambo na jengo la kuendeshea mitambo.

  “Pia tunaendelea na ujenzi wa nguzo za kupokelea laini ya msongo wa kilovoti 220 kutoka Kinyerezi I hadi Kinyerezi II, ambapo mtambo wa kwanza wa megawati 30 utawashwa ifikapo Desemba 2017 na kila mwezi tutaingiza megawati 30 katika gridi ya Taifa.”

  Amesema miradi iliyoko katika eneo hilo ambayo iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji ni Kinyerezi 1 (150MW), Kinyerezi I Extension (185MW ) na Kinyerezi II (240MW).

  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini,Profesa James Mdoe, wakati alipoenda kukagua mradi wa kuzalisha umeme Kinyerezi II, Julai 8, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea maelezo ya maendeleo ya mradi kutoka kwa Meneja mradi Stephen Manda, wakati akikagua mradi wa kuzalisha umeme Kinyerezi II, Julai 8, 2017. 
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Tito Esau, wakati alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme Kinyerezi II, Julai 8, 2017. 
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiongea na Wananchi wakati alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme Kinyerezi II, Julai 8, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala wakati alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme Kinyerezi II, Julai 8, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tanesco Balozi Dkt. James Nzagi, wakati alipoenda kukagua mradi wa kuzalisha umeme Kinyerezi II, Julai 8, 2017.

  0 0

  Timu ya soka ya TPB Bank FC imefanikiwa kulipiza kisasi kwa timu ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC baada ya kuifunga kwa mabao 3-2 katika mchezo huo maalum uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Sheria (Law School)  uliopo maeneo ya kituo cha mabasi cha Mawasiliano jijini Dar es salaam.
  Katika mchezo wa kwanza, Taswa FC iliifunga TPB Bank FC kwa mabao 4-0 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja  huo huo.
  TPB Bank FC ilitumia  idadi pungufu ya wachezaji wa Taswa FC kufunga mabao yote katika mchezo huo ambao pia ulikuwa wa maandalizi kwa timu hiyo ya benki kuelekea katika mashindano ya soka ya taasisi za kibenki yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni. Taswa FC ilianza mechi hiyo ikiwa na wachezaji nane tu.
  Bao la kwanza la TPB Bank FC lilifungwa na nahodha wa timu hiyo, Baraka Kyomo  katika dakika ya 10 ya mchezo  baada ya kuwashinda kasi mabeki wa Taswa FC na kufunga kirahisi.
   Wakati Taswa FC ikijiuliza, Kyomo alifunga bao la pili katika dakika ya 17 kabla ya Ojo Ajali kufunga la tatu katika dakika ya 35 ya mchezo.
  Taswa FC ilianza harakati za kusawazisha mabao hayo kuanzia kipindi cha pili baada ya kutimia wachezaji wote 11. Bao la kwanza la Taswa FC lilifungwa na Fred Pastory baada ya kupokea pasi safi ya Zahoro Mlanzi kabla ya Shedrack Kilasi kufunga la pili kufutia mpira wa kona wa Juma Ramadhani.
  Kiongozi wa timu hiyo Chichi Banda alisema kuwa wamefuraishwa na ushindi huo na kuwaomba Taswa FC kujipanga kwa ajili ya mchezo unaofuata
   TPB bank FC
  Taswa FC

  0 0


  0 0


  Na Ripota wa Mafoto Blog, Kibaha

  MBUNGE wa Kibaha mjini, Silyvestry Koka (kulia) na Diwani wa Kata ya Sofu, Yusuf Mbonde, wakishirikiana na wananchi wa kata hiyo Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani, kusafisha eneo lililo na majani kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa Zahanati. Mhe. Mbunge leo asubuhi alifanya ziara ya kushitukiza katika eneo hilo baada ya kupata tetesi kuwa eneo hilo limeuzwa.

  Aidha imeelezwa kuwa tetesi za kuuzwa kwa eneo hilo zilimfikia Diwani wa Kata hiyo, Bw.Mbonde, aliyeamua kumfuata Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Kibaha, Jenifer Ommolo, ambaye 'eti' alikiri kuwa jambo hilo nalitambua na kumwahidi kuwa wangepewa eneo mbadala wa hilo, jambo ambalo Diwani hakukubariana nalo na kuamua kulifikisha kwa Mhe.Mbunge wake.

  Mbunge huyo, alifika eneo hilo na kukutana na wapiga kura wake na kuamua kushiriki nao zoezi la kusafisha baada ya baadhi ya wananchi kukumbwa na hofu wakidai kuwa eneo hilo lilibadilishwa lengo la matumizi kwa kumgawia mtu aliyejulikana kwa jina la Mchome, ili kuliendeleza, ambaye pia hadi Mbunge anafika leo alikuwa bado hajaanza ujenzi wa aina yeyote.

  Imeelezwa kuwa eneo hilo baada ya kutolewa kwa ajili ya kujengwa Zahanati ambayo kwa kiasi kikubwa ilitakiwa kujengwa kwa ushirikiano mkubwa na wananchi ambao wengi wao walipigwa na butwaa na kurudi nyuma baada ya kusikia eneo hilo amegaiwa Mchome, aliyetakiwa kuliendeleza.

  Baada ya Mbunge Koka kuwasili eneo hilo hii leo asubuhi, wananchi wajitokeza na kuonyesha ushirikiano huo kwa kushirikiana na viongozi wao, na baadaye kubaki na matumaini ya kuona kinajengwa kile walichokikusudia baada ya Mbunge kutoa tamko kwa kusema eneo hilo linatakiwa kujengwa Zahanati ya wananchi na si kitu kingine.
  Mbunge wa Kibaha mjini, Silyvestry Koka, akizungumza na wananchi wa Kata ya Sofu Wilayani Kibaha, wakati wa zoezi la kufyeka na kusafisha eneo la kujenga Zahanati,ambapo alilaani kitendo hicho cha uuzwaji wa eneo la wananchi alichokiita cha kitapeli.
  Wananchi wakimsikiliza kwa makini mbunge wao, baada ya zoezi hilo.

  0 0


  0 0

  Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akipewa Maelezo kuhusu huduma zinazotolewa na Mahakama ya Tanzania katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi Mhe. Joachim Tiganga alipotembelea banda hilo sehemu ya Mahakama Kuu.
  Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akizungumza jambo na watumishi wa Mahakama alipotembelea banda la Mahakama ya Tanzanaia sehemu ya Mahakama Kuu Divisheni ya kazi leo jijini Dar es salaam.
  Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akizungumza jambo na watumishi wa Mahakama alipotembelea banda la Mahakama ya Tanzanaia sehemu ya Mahakama Kuu Divisheni ya kazi leo jijini Dar es Saalaam.
  Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akiangalia ukuta uliojegwa kwa kutumia Teknolojia ya Moladi alipotembelea banda la wadau wa Mahakama (Moladi Tanzania). Mahakama ya ya Tanzania inatumia Teknolojia ya Moladi kujenga baadhi ya Mahakama zake.
  Fundi Mchundo wa Mahakama ya Tanzania, Hassan Dunia akimuelezea Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu kuhusu ujenzi wa majengo ya Mahakama kwa kutumia teknolojia ya Moladi leo alipotembelea banda la wadau wa Mahakama (Moladi Tanzania).
  Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi Mhe. Joachim Tiganga akimsindikiza Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu baada ya kumaliza kutembelea banda la Mahakama ya Tanzania

  0 0

  Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiongoza maandamano ya Mabalozi wa Usalama Barabarani kuingia Uwanja wa Mashujaa, wakiadhimisha siku yao iliyofanyika kitaifa mkoani Dodoma leo.Kulia ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo,Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,DCP Mohamed Mpinga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani ambapo aliwaasa madereva kufuata sheria ili kuweza kupunguza tatizo la ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na kuacha idadi kubwa ya wahanga wa ajali hizo.Wapili kushoto ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo,Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,DCP Mohamed Mpinga na anayefuatia ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma,Lazaro Mambosasa. Maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa Uwanja wa Mashujaa,leo mkoani Dodoma.
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambae pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,DCP Mohamed Mpinga, akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani ambapo aliwaasa askari wa usalama barabarani kusimamia sheria ili kuweza kupunguza tatizo la ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na kuacha idadi kubwa ya wahanga wa ajali hizo.Kulia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na kulia ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma,Lazaro Mambosasa. Maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa Uwanja wa Mashujaa,leo mkoani Dodoma.
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma,Lazaro Mambosasa akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani ambapo aliwashukuru mabalozi hao kuchagua mkoa wa Dodoma kufanyia maadhimisho hayo na kuahidi kuelimisha watumiaji wa vyombo vya moto sheria na kanuni za usalama barabarani ikiwa anaongoza mkoa ambao ni Makao Makuu ya nchi .Wakwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambae pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,DCP Mohamed Mpinga.Maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa Uwanja wa Mashujaa,leo mkoani Dodoma.


older | 1 | .... | 1790 | 1791 | (Page 1792) | 1793 | 1794 | .... | 3353 | newer