Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1791 | 1792 | (Page 1793) | 1794 | 1795 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Serikali imerudisha utaratibu wa kugawa vyandarua vyenye viuatilifu kwa akina mama wajawazito na watoto ambao wanapatiwa chanjo ya surua kupitia vituo vya kutolea huduma za afya ya uzazi na mtoto ambapo utaratibu huo utaanza rasmi mwezi Agosti mwaka huu.

  Afisa Muuguzi kutoka Wizara ya Afya Epifania Malingumu amewaambia wajumbe wa mkutano wa uelimishaji juu ya mpango endelevu wa ugawaji vyandarau vyenye viuatilifu vya mda mrefu kuwa kwa sasa vyandarua hivyo havitapatikana katika maduka kama ilivyokuwa kwenye utaratibu wa ‘hati punguzo’ ya zamani.

  Malingumu amesema hapo awali vyandarua vyenye viuatilifu vilikuwa vikitolewa kwa mfumo wa hati punguzo ambapo mama mjamzito alikuwa anatakiwa kutafuta maduka ya mawakala wa vyandarua hivyo mara baada ya kupatiwa hati hiyo katika vituo vya kutolea huduma ya afya ya uzazi.

  “Utaratibu wa hati punguzo wa zamani ulikwisha muda wake mwaka 2014, akina mama walikuwa wanapata changamoto katika kutafuta mawakala wa vyandarua lakini utaratibu mpya ni kwamba mama mjamzito au mwenye mtoto mchanga atapewa chandarua chenye viuatilifu palepale atakapokuwa katika vituo vya kutolea huduma za afya ya uzazi” amesema.

  Ameongeza kuwa mama atapewa chandarua katika hudhurio la kwanza la kliniki ambapo takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 98 ya wajawazito huhudhuria kliniki angalau mara moja pia vyandarua hivyo vitatolewa kwa idadi ya watoto ambao mama atakua amejifungua kwa wakati huo.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza katika mkutano wa uelimishaji juu ya mpango endelevu wa ugawaji vyandarau vyenye viuatilifu vya mda mrefu uliofanyika Mkoani Singida.
  Wajumbe wa mkutano wa uelimishaji juu ya mpango endelevu wa ugawaji vyandarau vyenye viuatilifu vya mda mrefu uliofanyika Mkoani Singida, wa kwanza ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi Pius Shija Luhende pembeni yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida Bravo Lyampembile.
  Maafisa kutoka wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto wakiutambulisha mkoani Singida mpango endelevu wa ugawaji vyandarau vyenye viuatilifu vya mda mrefu.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0  0 0
  0 0


  Watemi wa Kisukuma Kanda ya Ziwa Victoria na viongozi wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania( Tanzania Albinism Society -TAS) wamefanya usafi wa mazingira kisha kula chakula cha pamoja na watoto wenye ualbino wanaolelewa katika kituo cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.

  Watemi hao wakiongozwa na Katibu Watemi wa Kisukuma Kanda ya Ziwa, Mtemi Charles Balele Itale wa Bujashi wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza walitembelea kituo hicho leo Jumamosi Julai 8,2017. 

  Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba alisema chama hicho kimekuwa na ushirikiano mkubwa na machifu wa kanda ya ziwa hicho kuamua kushiriki nao katika kufanya usafi wa mazingira katika kituo cha Buhangija. 

  “Malengo ya kuja hapa kwanza ni kuunga mkono serikali ya awamu ya tano kuhusu masuala ya usafi,pili ni kuwapa ujumbe watoto hawa kuwa wawe na utamaduni wa kufanya usafi hata wanaporudi kwenye familia zao,tatu tumekuja kula chakula cha pamoja na watoto hawa ili kuonesha kuwa tuko pamoja nao”,alieleza Temba. 

  Temba alitumia fursa hiyo kuiomba serikali kuchunguza utitiri wa mashirika yaliyoanzishwa nchini ambapo sasa yapo zaidi ya 10 na kufuatilia vituo mbalimbali vilivyoanzishwa kwa lengo la kuwahudumia watu wenye ualbino hususani watoto kwani sasa vipo takribani 20 lakini wahusika wa vituo hivyo hawasaidii walengwa. 

  Temba alisema mashirika mengi yamekuwa yakijikita katika kupiga vita mauaji ya watu wenye ualbino huku yakisahau kuwa watu wenye ualbino wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa elimu na saratani ya ngozi ambayo imekuwa ikiua watu wengi wenye ualbino. 
  Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba,Mtemi Wenceslaus Seni wa Kanadi mkoani Simiyu na Mtemi Charles Gagambaseni Dogani wa Seke – Kishapu mkoani Shinyanga wakila chakula na watoto kituo cha Buhangija.

  Katibu Mtendaji wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa,Mussa Mussa akizungumza katika kituo/Shule ya Msingi Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.Kulia ni Katibu wa Umoja wa Watemi wa Kisukuma kanda ya Ziwa, ambaye ni chifu/mtemi wa Bujashi wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza Charles Dotto Balele.Kushoto ni Mwalimu Mlezi wa Shule ya Msingi Buhangija, Frola Kakutebe-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
  Katibu wa Umoja wa Watemi wa Kisukuma kanda ya Ziwa, ambaye ni chifu/mtemi wa Bujashi wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza Charles Dotto Balele Itale akizungumza katika kituo cha Buhangija.Kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba 
  Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba akizungumza katika kituo cha Buhangija ambapo aliiomba serikali kuona umuhimu wa kuwapa nguvu viongozi wa kimila kama zamani kwani wanazungukwa na watu wengi hivyo kuwa na nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko katika jamii.
  Watoto,walimu na maafisa kutoka TAS wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea


  0 0

  Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamini William Mkapa akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo jipya la upasuaji kwenye kituo cha afya cha Nkomo kilichopo kijiji cha Mwalushu,Wilayani Itilima-Simiyu
  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Itilima Dkt. Anold Musiba akitoa maelezo kwa Rais Mstaafu,kulia ni Balaozi wa Japan nchini Tanzania Mhe.Masaharu Yoshida. Jengo hilo limejengwa na Ubalozi wa Japan kupitia Taasisi ya Benjamini Mkapa na kugharimu kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 270.
  Rais Mstaafu akiangalia moja ya vifaa vilivyomo kwenye chumba cha upasuaji .Ujenzi wa jengo hilo kwa asilimia kubwa itawasaidia akina mama wajawazito ambapo awali wananchi wa kijiji hicho walikua wakitembea kilometa arobaini kwenda kupata huduma za namna hiyo.
  Jengo hilo la upasuaji linavyoonekana
  Msimamizi wa ujenzi wa jengo hilo kutoka Taasisi ya Benjamini Mkapa Geofrey Nyaluke (mwenye fulana ya jano) akitoa maelezo kwa Viongozi waliofika kushuhudia ufunguzi wa jengo hilo.


  0 0

  Naibu Spika Dr. Tulia Ackson kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust ameanza ziara ya siku 10 mkoani Mbeya kazi kubwa ikiwa ni kutoa misaada kwa Taasisi mbalimbali zikiwemo shule na hospitali huku akikagua maendeleo ya baadhi ya Taasisi alizozisaidia katika siku za nyuma.

  Dr. Tulia katika ziara yake ya jana alikabidhi misaada vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Tsh. 1.1m kwa Shule ya Msingi Lubwe, Tsh. 2.5m kwa Shule ya Sekondari Nkunga, vitanda 20 kwa Hospitali ya Igongwe pamoja na kukagua ujenzi wa Vyoo na Bafu kwa wajawazito katika Hospitali ya Makandana.
  Naibu Spika Dr. Tulia Akson akiwa amembeba mmoja wa watoto yatima katika Hospitali ya Igogwe
  Naibu Spika Dr. Tulia Akson akivuka Daraja la Nkunga-Lupepo lililopo Rungwe
  Naibu Spika Dr. Tulia Akson akisoma moja ya bango lililowekwa na wananchi wakati wa ziara yake

  Naibu Spika Dr. Tulia Akson akiwa kwenye picha picha ya pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Rungwe
  Naibu Spika Dr. Tulia Akson akisalimiana na wazazi katika Hospitali ya Igogwe ambayo haina eneo la kupumzikia wakinamama baada ya kujifungua

  0 0

   Kamishna wa Vibali na Pasi nchini, Musanga Etimba akitoa maelezo kwa mwananchi Oliver Gabriel, aliyetembelea Banda la Idara ya Uhamiaji katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
   Mwananchi aliyetembelea Banda la Idara ya Uhamiaji, Oliver Albert akiuliza maswali kwa Kamishna wa Vibali na Pasi nchini, Musanga Etimba baada ya kutembelea Banda la Idara hiyo katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mdhibiti wa Pasipoti nchini, Mrakibu Mwandamizi Peter Mwitwa.
   Mkaguzi wa Idara ya Uhamiaji nchini, Mustafa Kipingu (kushoto), akitoa huduma kwa mwananchi aliyetembeleaBanda la Idara hiyo katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
  zi wa Idara ya Uhamiaji, Kitengo cha Uhusiano, Aziz Kirondomara (kushoto), akitoa huduma kwa mwananchi aliyetembeleaBanda la Idara hiyo katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  0 0

   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akipeana mkono na Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. LU Youqing, walipokutana katika viwanja vya Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara (sabasaba), Jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) akitoa maelekezo kwa wafanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) kuhusu namna ya kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kukata bima ili kujikinga na majanga, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango lilipo katika viwanja vya maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara (sabasaba), Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Bw. Sam Kamanga.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi wa uendeshaji wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), Naftal Sigwejo baada ya kuulizwa kuhusu ubora wa baadhi ya bidhaa zinazotolewa Serikalini baada ya kutembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) Jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akimpongeza Mzazi wa kijana Msuya Mageta (katikati) aliyejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF kupitia mpango wa Wote Scheme katika Banda la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), Jijini Dar es salaam.

  0 0

  Emirates imewapa baadhi ya familia za kitanzania ladha ya ushindi wa usafiri wa anga wakati walipohudumia kundi la wazazi na watoto wao katika moja ya sinema kali ya Despicable Me 3. 
  Sinema mpya iliyotoka katika anga ya dunia- karibia watoto 30 na wazazi wao na walezi walihudhuria uzinduzi huo uliofanyika Mlimani City Mall IMAX tarehe 8 Julai 2017 kuangalia sinema bora uliyovuta hisia za wengi ikifatiwa na chakula cha mchana sehemu hiyo hiyo iliyoandaliwa na mwenyeji mkurugenzi wa Emirates Tanzania, Rashed Alfajeer. 

  Emirates pia ilipata uzoefu wa familia katika kutangaza ofa ya 50% katika daraja la uchumi kati ya abiria 2 - 8 kusafiri wote katika sehemu 21 zilizopendekezwa kama Uarabuni, Ulaya vile vile Marekani kusini na kaskazini. Hiyo ofa ni kati ya tarehe 6 na 14 julai 2017 na za nje kati ya tarehe 6 julai na 10 Disemba 2017.

  Rashed Alfajeer, Mkurugenzi Mkuu wa Emirates Tanzania alisema: " Emirates ipo kwa ajili ya kutoa thamani kwa pesa na wamejihakikisha kutoa huduma iliyo bora angani mpaka ardhini na hakuna tofauti linapokuja swala la familia katika kusafiri. Kwa watoto, lazima wawekwe huru na waburudike na kuwajali kwa kuwapa wigo mpana katika kuchagua sinema na programu ili kukithi mahitaji yao".

  Ofa hii maalum inatoa nafasi kubwa kwa familia kuwa na likizo ya pamoja sehemu mbali mbali kwa gharama nafuu kwa muda uliowekwa tu na kuongeza wakati wakisafiria na Emirates, familia itarajie kupata wigo mpana wa program za watoto ikiwa na channeli 90 mahususi kwa ajili ya kuwaburudisha watoto ikiwamo pamoja na sinema bora na programu za TV kutoka Disney, Cartoon Network, Cbeebies Na Nickelodon na nyingine nyingi. 

   Chakula pia upewa kipaumbele sana pindi abiria wawapo angani kwenye Emirates. Watoto wenye umri kati ya miaka 2 na 12 hupewa chakula maalum wakihudumiwa katika vyombo vya kisasa wakiwa na staff pamoja na marubani. Wasafiri wenye ugunduzi wachache wanaweza kupata marafiki wapya pindi wawapo safarini, kuna blanketi kwa ajili ya kujifunika na kuweza kujiburudisha na majarida yanayokuja Dar Es Salaam kila siku. Ndege ya EK 0725 inatoka Dubai saa 10:25 na kufika Dar Es Salaam saa 14:50. Ndege inayorudi EK 0726 inatoka Dar Es Salaam saa 16:45 na kufika Dubai saa 23:20.

  0 0

  · Yaanza kuuza makaa hayo kwa kasi
  · Yakiri kuwa na akiba ya makaa ya mawe ardhini ya kuchimba kwa zaidi ya miaka mia moja. 

  Na Koleta Njelekela-STAMICO

  Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeanza rasmi kuuza makaa ya mawe yanayozalishwa katika Mgodi wake wa Kabulo ili kukidhi mahitaji ya watumiaji wakiwemo viwanda vya saruji na nguo na hivyo kukuza Pato la Taifa.

  STAMICO ilianza uzalishaji wa majaribio wa makaa ya mawe katika mgodi wa Kabulo uliopo Kijiji cha Kapeta, Wilaya ya Ileje Mkoa wa Songwe mnamo tarehe 30 Aprili 2017 na mpaka sasa imeweza kuzalisha tani 6,197.

  Akihojiwa na Mwandishi wa Habari hii, mara baada ya zoezi la uuzaji makaa ya mawe kuanza rasmi huko Kabulo jana (6 Julai 2017), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Bwana Hamis Komba, amesema Shirika kupitia mradi wake wa makaa ya mawe wa Kabulo, sasa linaweza kukidhi mahitaji ya watumiaji wote wa makaa ya mawe nchini, katika kipindi cha miaka mia mfululizo kutokana na kuwepo kwa mashapo ya kutosha (mineral resources) na nyenye ubora wa juu katika mgodi huo.

  Bwana Komba amesema matarajio ya Shirika ni kuongeza kiwango cha uchimbaji makaa ya mawe kutoka tani 600 hadi tani 1000 kwa siku, hatua ambayo itaiwezesha STAMICO kuzalisha zaidi ya tani 300,000 kwa mwaka. 

  “Nchi yetu ina rasilimali nyingi za madini yakiwemo makaa ya mawe, hivyo tunapenda kuwahikishia wenye viwanda vinavyotumia makaa hayo hususani viwanda vya Saruji (Cement), kwamba nchi ina makaa ya kutosha hivyo Serikali haitoshindwa kutosheleza mahitaji na makaa yam awe huku ikitekeleza kwa vitendo azma yake kujenga Tanzania yenye viwanda, ili kukuza uchumi wa Taifa" Alifafanua Bwana Komba.
  Kamishna wa Madini Tanzania Mhandisi Benjamin Mchwampaka akiwa katika picha ya pamoja na timu wa wataalam wa STAMICO (wanaotekeleza Mradi wa Uchimbaji Makaa ya Mawe-Kabulo) alipotembelea Mgodi huo hivi karibuni kukagua maendeleo ya mradi huo ambao ulianza rasmi uzalishaji makaa yam awe tarehe 30 Aprili, 2017 na kufanikiwa kuzalisha tani 6197 mpaka sasa. Soko la ndani la makaa hayo linawalenga wazalishaji viwandani hususani wale wa viwanda vya Saruji (Cement) na watengenezaji wa nguo, pamoja na magereza na watumiaji wengine wa majumbani.

  Shughuli za Uchimbaji Makaa ya Mawe zikiendelea katika mgodi wa Kabulo Kiwira, uliopo katika Kijiji cha Kapeta, wilaya ya Ileje, Mkoa wa Songwe. Leseni za Uchimbaji wa Awali wa Madini katika eneo hilo la Kabulo, zina zaidi ya tani milioni 35 zilizothibitishwa za mashapo ya makaa ya mawe, yaliyoko karibu na uso wa ardhi, katika mgodi huo wa Kabulo. Mashapo hayo yanaweza kuchimbwa kwa mfululizo kwa miaka mia moja ijayo.

  Mratibu wa Mradi wa Uzalishaji Mkaa ya Mawe wa Kabulo-Kiwira Bwana Alex Rutagwelela ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji wa STAMICO akielekeza kuhusu zoezi zima la upakiaji makaa ya mawe katika Malori tayari kwa ajili ya kupeleka katika eneo la mauzo lililopo katika kijiji cha Kasumulu, Wilaya ya Kyela, mkoa wa Mbeya. Mgodi huo wa Kabulo-Kiwira uliopo katika kijiji cha Kapeta, Wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe unamilikiwa na kuendeshwa na STAMICO kwa niaba ya Serikali.
  Malori ya Kampuni ya Lake Cement yakipakia Makaa ya Mawe katika eneo la mauzo ya makaa hayo, lililopo umbali wa kilometa mbili kutoka katika barabara kuu ya Mbeya, iendayo nchini Malawi. Eneo hilo la mauzo lipo katika kijiji cha Kasumulu, Wilaya ya Kyela, mkoa wa Mbeya. Makaa hayo ya Mawe yanazalishwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), katika mgodi wake wa Makaa ya Mawe wa Kabulo, ulipo katika kijiji cha Kapeta, Wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe.


  0 0


  Mwenyekiti wa kampuni ya Upimaji na Upangaji wa Makazi (HUSEA), Renny Chiwa akitoa maelezo machache juu ya mradi wa 'Ardhi Clinic' katika uzinduzi wa uliofanyika Kata ya Msigani-Mbezi wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam. Bw. Chiwa alisema kuwa lengo la mradi huo ni kusaidia juhudi za serikali za kupanga, kupima na kumilikisha kila kipande cha ardhi nchini nzima na pia kuboresha maisha ya mamilioni ya watanzania kupitia ushauri na utoaji elimu kwa wananchi katika masuala yote ya ardhu kwa nia ya kutengeneza makazi bora yaliyopangwa na kupimwa kwa ajili ya kizazi cha sasa na baadae.
  Mkurugenzi wa kampuni ya Upimaji na Upangaji wa Makazi (HUSEA), Pamela Maro akiwafafanua machache mbele ya waandishi wa habari juu ya Mradi wa 'Ardhi Clinic' katika uzinduzi uliofanyika katika Kata ya Msigani, Mbezi jijini Dar es Salaam. Alisema kuwa malengo makuu ya mradi wa 'Ardhi Clinic' ni tiba mbadala kwa changamoto mbali mbali za masuala ya ardhi baada ya kugundua kuwa changamoto nyingi zinatokana na masuala ua ardhi hapa Tanzania kama migogoro ya wafugaji na wakulima, wananchi kuuziwa maeneo ya wazi, utapelikwenye masuala ya ardhi, uendelezaji wa makazi usiofuata mipango, ukosefu wa maadili katika taaluma za upangaji na upimaji, ukosefu wa hati miliki, ukosefu wa huduma za jamii n.k hazina tofauti na magonjwa ambayo wanahitaji tiba haraka kuyakabili.
  Wananchi wakiendelea kupata elimu ya ardhi. 
  Vifaa vya kisasa vinavyotumika katika upimaji wa ardhi. 


  0 0


  0 0

  Na Judith Mhina - MAELEZO

  Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni muasisi aliyeenzi lugha adhimu na tamu ya Kiswahili na anastahili tuzo maalum kwa kutambua umuhimu wa lugha  hiyo katika kuleta umoja, mshikamano, na maendeleo barani Afrika.

  Mwalimu kwa kutambua umuhimu wa lugha ya Kiswahili, alianza kuweka mfumo wa matumizi ya lugha hiyo katika utendaji wa serikali, jamii nzima ya Tanzania na Umoja wa Afrika. Aidha, sera za Tanzania za kushiriki katika kupigania Uhuru wa nchi kadhaa za Afrika na uwepo wa wakimbizi nchini kwa idadi kubwa imewezesha lugha hii kuvuka mipaka na kuenea kote kusini mwa Afrika.

  Mwalimu amepata wapiganaji mahiri wa lugha ya Kiswahili ambao wapo wengi, lakini kwa uchache makala yangu itaangazia viongozi yaani, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi, na Rais mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano, Marais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, Rwanda, Paul Kagame, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila na Jemedari wa kuenzi lugha ya Kiswahili anayeifanya lugha hii kuwa Lulu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli. 

  Mtakubaliana nami mchango wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi katika kutumia lugha ya Kiswahili fasaha, katika shughuli zote za Serikali na za kijamii zilisukuma mwamko wa gurudumu la kiswahili kusonga mbele haswa kwa wale wanaodhani lugha za kigeni ni bora kuliko lugha yao.


  0 0


  Klabu ya Dar es Salaam Gymkhana (DGC) ambayo ni miongoni mwa klabu kongwe za michezo hapa nchini Tanzania, leo imeadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake kwa mtindo wa aina yake uliowakutanisha wadau mbalimbali wa klabu hiyo kupitia chakula cha jioni jijini Dar es Salaam.

  Tangu wiki iliyopita, kumekuwa na shughuli mbalimbali za kimichezo ambazo zilianza kufanyika tangu 3 Julai na kilele chake kuwa siku ya leo ya tarehe (08/07/2017). Shughuli hizo ziliandaliwa kwa lengo la kupamba tukio hili muhimu.

  Miongoni mwa michezo iliyokuwa ikifanyika ni pamoja na tenisi, kriketi, squash, mashindano ya gofu na michezo mingine mingi.

  Mgeni rasmi aliyehudhuria sherehe ya kilele cha maadhimisho hayo wakati wa kufunga michezo hiyo, alikuwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ambaye alizungumiza shamrashamra za kuadhimisha miaka 100 ya klabu hii mkongwe.

  “Binafsi nimefurahishwa sana kusikia kwamba michezo yote iliyohusishwa kwenye maadhimisho ya tukio hili kubwa na muhimu ambalo imefanyika na kuisha salama kwa kipindi chote cha wiki moja, jambo ambalo linaonyesha waandaaji walijapanga vyema. Ni imani yangu kwamba udhamini wa wadau mbalimbali umewezesha kufanikisha kufanyika michezo yote hii muhimu,” alisema Waziri Dk Mwakyembe.

  Dk Mwakyembe alisema matarajio ya serikali ya awamu ya tano ni kuona wadau wanaongeza nguvu kujihusisha zaidi kwenye shughuli za michezo jambo ambalo linaweza kuibua vipaji zaidi kwa Watanzania wote.

  Waziri Mwakyembe alimwaga pongezi kwa wanachama wote wa klabu hiyo wa sasa na wale waliopita pamoja na kila mtu ambaye alishiriki kwa nafasi yake kuhakikisha klabu ya Dar Gymkhana inafanikiwa zaidi.

  “Ninatambua fikaumuhimu wa klabu hii kwa ngazi ya taifa letu kwani imekuwa miongoni mwa taasisi ambayo imekuwa ikihamasisha kukuza michezo, utalii na kuwakutanisha pamoja watu kwenye matukio ya kijamii,” alisema.

  Waziri Mwakyembe aliwataka Watanzania kujenga utamaduni wa kushiriki michezo mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha afya zao na kuwahamasisha wananchi kujiunga na klabu hii ambayo ina michezo mbalimbali. Alisema klabu hii imekuwa ikiwakutanisha wageni kutoka mataifa mbalimbali na Watanzania.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akikabidhi kikombe kwa Nahodha wa mpira wa miguu wa Klabu ya Gymkhana Aliabid Mamdani (kulia) baada ya timu yake kuibuka washindi wa jumla katika michuano iliyofanyika hivi karibuni katika kuadhimisha ya miaka 100 ya klabu ya Gymkhana. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jana wakati wa kilele cha maadhimisho hayo jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Mwenyekiti wa klabu ya Gymkhana Walter Chipeta.
  Mwenyekiti wa klabu ya Dar es salaam Gymkhana, Walter Chipeta akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 100 ya Klabu ya Dar es salaam Gymkhana yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam. 
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakeyembe akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 100 ya Klabu ya Dar es salaam Gymkhana yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam. 
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Dar Gymkhana, George Kritsos wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 100 ya Klabu ya Dar es salaam Gymkhana yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam.   0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa Chato mkoani Geita. Rais Mstaafu Mkapa katika siku ya kesho anatarajiwa kukabidhi nyumba 50 za watumishi wa sekta ya Afya zilizojengwa na Taasisi ya (Mkapa Foundation) katika mikoa ya Simiyu, Kagera na Geita.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa Chato mkoani Geita. Rais Mstaafu Mkapa katika siku ya kesho anatarajiwa kukabidhi nyumba 50 za watumishi wa sekta ya Afya zilizojengwa na Taasisi ya (Mkapa Foundation) katika mikoa ya Simiyu, Kagera na Geita. Kushoto ni Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida mara baada ya kuwasili Chato mkoani Geita. Balozi huyo wa Japan katika siku ya kesho anatarajiwa kukabidhi mtambo wa kukamua Mafuta ya Alizeti (Double Refine) uliojengwa Chato mkoani Geita kwa Msaada wa Serikali ya Japan.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Kampuni  ya Moovn Technologies kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania PLC, wamezindua ushirikiano mpya utakaowarahisishia wateja wao kupata huduma ya usafiri na kuwafikishia huduma za simu watu zaidi ya milioni 12 barani Afrika.


  Moovn ni teknalojia inayomwezesha mtu anayetaka usafiri kuupata kwa haraka akiwa sehemu alipo kwa kutumia simu yake ya mkononi au kompyuta. Teknalojia hii pia inawawezesha watu kufikishiwa bidhaa kutoka sehemu mbali mbali na madereva.


  Ushirikiano huu kati ya Vodacom ambayo ni moja kati ya makampuni makubwa ya simu za mkononi Afrika pamoja na Moovn, utawawezesha watu zaidi ya milioni 12 kujiunga kwenye huduma hiyo ya Moovn app kwa kupitia simu zao za mkononi.


  Kupitia mpango huo, kampuni ya Vodacom itatoa bure au kwa punguzo huduma za data kwa wateja wa Moovn pamoja na madereva ili waweze kupata huduma hiyo kwa urahisi zaidi.  Wateja wa huduma hiyo wataweza  kuchagua usafiri wa aina mbali mbali kama vile boda boda, bajaji pamoja na taxi kulingana na mahitaji yao kwa kutumia Moovn app. Pamoja na kulipa kwa fedha taslimu, wataweza pia kulipa kwa kutumia huduma ya kifedha ya M-Pesa  Huduma hii ya aina yake inalenga kuboresha maisha ya wateja wa kampuni zote mbili zilizo kwenye ushirikiano. Ushirikiano huu pia unalenga kutengeneza ajira pamoja na kuboresha hali ya kiuchumi kwa jamii za Kitanzania na Afrika kwa ujumla.  “Tunayo furaha kuungana na mshirika mwenzetu katika kutoa huduma hii muhimu tukilenga kwa pamoja  kubadili maisha ya watu,” anasema Godwin Gabriel ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Moovn  Kumhakikisha mteja usalama wake, mtumiaji wa huduma hii anaweza kubonyeza batani inyoitwa ‘panic button’ na ujumbe mfupi wa maandishi utatumwa kwa mtu wake wa karibu ukieleza sehemu alipo na utambulisho wa dereva muda wowote wakati akiwa kwenye chombo cha usafiri.  Kipengele hiki cha usalama ni muhimu kwa kuwa kwa siku za hivi karibuni kumekuwa  na matukio ya abiria kufanyiwa uhalifu na baadhi ya madereva wasio waaminifu. Mteja pia anaweza kuwafamisha ndugu jamaa na marafiki zake kinachoendelea kuanzia mwanzo hadi mwisho wa safari yake.  Pamoja na mambo mengine, huduma hii itawawezesha wafanyabiashara kufuatilia bidhaa na huduma wanazowapelekea wateja wao kuanzia wanapomkabidhi dereva hadi zinapomfikia mteja.  Madereva  watakuwa wakipata malipo yasiyobadilika (Flat commission) kwa kila safari watakokuwa wakifanya na  kwa upande wao wateja watafurahia gharama zisizopanda.  Naye Mkurugenzi wa kitengo cha biashara wa Vodacom Hisham Hendi alisema “M-Pesa inawawezesha watu wote kuweza kufikiwa na huduma ya kifedha kwa urahisi katika sehemu walipo. Wakati tukifanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa watanzania wengi wanafikiwa na huduma za gharama nafuu za kifedha, tunaendelea pia kuwaletea wateja wetu huduma zenye ubunifu zinawezesha Serikali na biashara kuwasiliana huku tukitoa malipo mazuri kwa mawakala wetu,”  Aliwashauri watumiaji wa mtandao huo kwa kufanya malipo kwa njia ya simu kwani ni salama zaidi kuliko kubeba fedha taslimu. Kupitia huduma ya LIPA KWA M-PESA alisema malipo katika huduma nyingi na bidhaa yamerahisihwa kupitia App mpya ya M-Pesa

  0 0

   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masaunia kizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Kondoa na Chemba mkoani Dodoma. Masauni amefanya ziara ya kikazi katika wilaya hizo. Wa kwanza kushoto  ni Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Sezaria Makota, na wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simoni Odunga.Wa kwanza Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani humo, SSP Mohamed Kitia.
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma, Sezaria Makota wakati alipokua akitoa taarifa yake ya Wilaya kwa kiongozi huyo ambaye yupo ziarani katika Wilaya ya Kondoa na Chemba. 
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Chemba, mkoani Dodoma, Simon Odunga,wakati alipokua akitoa taarifa yake ya Wilaya kwa kiongozi huyo ambaye yupo ziarani katika Wilaya ya Kondoa na Chemba. 
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kondoa, SSP Mohamed Kitia wakati alipokua akitoa taarifa yake ya Ulinzi na Usalama wilayani humo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Sezaria Makota, na Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga. Masauni yupo ziara ya kikazi katika Wilaya hizo ambapo alizitembelea Taasisi zilizopo ndani ya Wizara yake. 

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Karama Kenyunko-Globu ya Jamii

  , Mjasiliamali anayejihusisha na utengenezaji wa extension za Umeme kwa kutumia mbao, anaiomba Serikali izitambue bidhaa za mbao ili apate kiwanda kikubwa ambacho kitamuwezesha kutoa ajira kwa vijana na bidhaa hizo kufika hadi nje ya nchi.

  Charles Antoni Sanga, ambaye ni mwafrica wa kwaza kugundua ujuzi wa kupitisha umeme kwenye mbao, ameongea hayo katika maonyesho ya 41 ya biashara (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

  Amesema, upitishaji wa Umeme kwenye mbao ni bora na siyo rahisi kusababisha shoti ya Umeme, pia ujuzi huo unatoa fursa kwa kuwainua wajasiliamali wanaochaji simu vibandani.

  "Ninahamasidha kauli mbiu ya Mh.Rais kuwa Tanzania ya viwanda inawezekana sababu kuna vitu tunavyobuni watanzania ambayo ni imara kuliko vile vya kutoka nje ya nchi".

  Aidha ameiomba Serikali na wadau mbali mbali wanaopenda bidhaa hizo za mbao kujitokeza na kumuinua kwani anafanya kazi katika mazingira magumu kwani hata TBS walimuagiza kuwa awe na karakana na machine Au hata jengo lakini hana chochote kwani hana fedha za kumuwezesha kuwa na vifaa hivyo.

   Mgunduzi wa Soketi ya Mbao Charles Sanga akieleza Kwa Makini jinsi alivoweza kutengeneza Soketi hizo
   Charles Sanga akionesha moja ya Soketi aliyoitengeneza


  0 0

  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.  Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa hotuba yake wakati wa fainali za shindano la Bongo Style, lililofanyika makumbusho ya Taifa Jijini Dar ,linalohusisha fani za ubunifu wa mavazi,upigaji picha na uandishi wa miswada ya filamu ambapo aliipongeza Taasisi isiyo ya kiserikali ya Faru Arts and Development Organization(FASDO) kwa kuandaa mashindano hayo, alisema kuwa Serikali inalojukumu la kusaidia Asasi kama FASDO ambazo zinaingia katika maswala ambayo Serikali hawakuyawekea msingi mkubwa. "Naomba niagize na kuwa kuna watendaji wetu wa wizara katika sherehe hii mkae chini na watu wa FASDO ili mwaka kesho zoezi hili lifanyikie Bungeni Dodoma" Alisema Dkt. Mwakyembe.
   Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.  Dkt. Harrison Mwakyembe (wa tatu kutoka kulia) akimkabidhi Agnes Nyahonga  tuzo na zawadi ya mfano wa Hundi yenye thamani ya Tsh 1,000,000 aliyeshinda   shindano la Bongo Style katika kipengele cha ubunifu wa mavazi.
   Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.  Dkt. Harrison Mwakyembe(wa pili kutoka kulia) akimkabidhi Goodhope Elieskia maarufu kwa jina la Zagamba  tuzo na zawadi ya mfano wa Hundi yenye thamani ya Tsh 1,000,000 aliyeshinda   shindano la Bongo Style katika kipengele cha uandishi wa miswada ya Filamu
   Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na MichezoMh.  Dkt. Harrison Mwakyembe(wa kutoka kulia) akimkabidhi Masoud Masoud  tuzo na zawadi ya mfano wa Hundi yenye thamani ya Tsh 1,000,000 aliyeshinda   shindano la Bongo Style katika kipengele cha ubunifu wa mavazi.
   Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na MichezoMh.  Dkt. Harrison Mwakyembe(wa pili kutoka kulia) akimkabidhi Philip Florian  tuzo ya Best Personality aliyopokea kwa niaba ya Kelvin Mwanasoko ambaye hakuweza fika katika Mashindano hayo.


  0 0


  *Asema nchi ina utulivu wa kisiasa na uchumi unaokuwa kwa kasi

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewahakikishia uwekezaji wenye tija wawekezaji watakaokuja nchini kwa kuwa Tanzania ni nchi yenye amani, utulivu wa kisiasa na uchumi wenye kukua kwa kasi.

  Ameyasema hayo leo (Jumapili, Julai 09, 2017) alipomuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Aga Khan alipochaguliwa kuwa Imamu Mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani.

  Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua na kuthamini shughuli mbalimbali zinazofanywa na mtandao wa taasisi za Aga Khan zilizopo hapa nchini, hivyo Serikali itaendelea kushirikiana nao.

  Ameupongeza mtandao wa taasisi za Aga Khan kwa kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli katika kutoa kipaumbele cha kuwapa fursa watu wenye kipato cha chini kushiriki katika uzalishaji ili waweze kujikwamua kiuchumi.

  “Nawahakikishia kwamba uwekezaji wenu hapa nchini utakuwa na baraka kwa sababu nchi imetulia kisiasa na uchumi wake unakua kwa kasi. Nawaomba muendelee kuwaalika wanajumuia wa madhehebu ya Shia Ismailia popote walipo duniani waje kuwekeza nchini fursa bado zipo.”
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi waiyo hudhuria katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi waiyo hudhuria katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na mama Zakia Megji wakati wa maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, (kushoto) ni Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia Amin Lakhani Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia Amin Lakhani wakati wa maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, (katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sofia Mjema Julai 9, 2017.
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na Muwakilishi wa AKD resident Amin Kurji katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli,(katikati) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Aga Khan Suleiman Shabbudin Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


older | 1 | .... | 1791 | 1792 | (Page 1793) | 1794 | 1795 | .... | 3348 | newer