Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1789 | 1790 | (Page 1791) | 1792 | 1793 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Kipa wa kimataifa mstaafu wa Taifa Stars Ivo Mapunda ameandaa clinic ya magolikipa siku ya tarehe14  Julai, 2017  itayofanyika katika uwanja wa Karume kuanzia saa mbili asubuhi.  Kituo  cha Ivomapunda Sports Center ndio kimeandaa hii clinic.
  Mgeni rasmi ni mkufunzi anayetoka Taasisi ya michezo ya Keepers Foundation nchini Poland, Marek Dragozs. 
  Hivyo  makipa wote na makocha wa magolikipa wanaalikwa kuhudhuria kwa mchango mdogo wa shilingi 5000 tu. Hii si ya kukosa!


  0 0

   Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwasili katika banda la kampuni  ya Maziwa ya Asas katika Maonesho ya 41 ya Sabasaba
   Meneja Masoko Jimy Kiwelu akitoa Maelezo kwa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan wakati alipotembelea banda la kampuni ya Maziwa la Asas katika  Maonesho ya 41 ya Sabasaba
   Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiasaini katabu cha wageni wakati alipotembelea banda la kampuni ya Maziwa la Asas katika  Maonesho ya 41 ya Sabasaba
  Meneja Masoko Jimy Kiwelu akitoa Maelezo kwa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan wakati alipotembelea banda la kampuni ya Maziwa la Asas katika  Maonesho ya 41 ya Sabasaba.

  0 0


  0 0

  Na Evelyn Mkokoi 
  Kufuatia ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, iliyofanyika Jijini Dar es Salam leo katika Manispaa ya ilala, ilohusisha ukaguzi wa Dampo la Pugu Kinyamwezi, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kupitia Mkaguzi wa Mazingira wa kanda ya Mashariki Bw. Jaffari Chimgege, limeitoza faini Manispaa  ya jiji ya Dar es Salaam kiasi cha shilingi Milioni 25 kwa kosa la uchafuzi wa Mazingira wa kutohudumia Dampo hilo ipasavyo na kupelekea harufu mbaya, vumbi na maji yenye sumu kali  na kuhatarisha afya ya wakazi wa maeneo jirani, viumbe hai na mzingira kwa ujumla.
  Kufuatia malalamiko ya wakazi wa mtaa wa Viwege uliyopo katika kata ya Majoe yaliyowasilishwa na mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Bi Amina Rashid yaliyoeleza kuwa na changamoto mbali mbali katika dampo hilo zikiwemo za vumbi na maji yenye kemikali kwenda katika maeneo ya makazi, Naibu Waziri Mpina, ameitaka Halmashauri ya jiji kuja na mpango mkakati utakaoweza kuupunguzia mzigo dampo la Pugu ambalo kwa sasa linatumika kupokea takataka zote za Halmashauri za jiji la Dar es Salaam na kuonekana kulemewa na mpango huo uwezeshe kila manispaa kuwa na dampo lake.

  Aidha Mpina alibaini kuwepo kwa madhaifu makubwa katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na kuondosha taka katika manispaa za jiji na kuutaka uongozi wa jiji Hususan Mkurugenzi wa Jiji kufuatilia madeni hayo kikamilifu, pamoja na kutoa deadline ya uwasilishwaji wa fedha hizo “ni vyema ghahama za uondoshwaji wa taka zikatokana na taka zenyewe na siyo kutoa fedha za kuhudumia taka kutoka katika vyanzo vingine vya mapato. Alisisitiza Mpina.”

  Mpina pia aliitaka manispaa ya jiji  kutafuta namna bora ya kuondosha taka sumu na kuelekeza taka zote za matairi katika jiji la Dar es Salaam zitafutiwe sehemu tofauti na namna pekee ya kuzitekekeza.

  Akionekana kuongea kwa hasira na msisitizo Naibu Waziri Mpina alisema, “ Hakuna kitu nisichopenda katika utendaji wangu kama kuona taasisi za serikali zikiwa za kwanza katika suala zima la uchafuzi wa mazingira, faini hiyo jiji mtailipa ndani ya siku 14, na kuhakikisha mnarekebisha  matobo yote yanayolalamikiwa kupitisha maji na kupeleka katika makazi ya wananchi pamoja na kujenga mifereji ya maji ya mvua, na maji ya sumu yaende katika mkondo sahihi wa maji hatarishi na bila kusahau kuruhsu maji hayo baada ya kujiridhisha na vipimo vinavyotakiwa.

  Awali akitoa taarifa ya hali ya mazingira  na usimamizi wa taka katika Dampo  la Pugu Kinyamwezi , Mkuu wa Idara ya usimamizi taka wa jiji la hilo Bw. Shedrack Maximillian alimueleza Mpina kuwa jiji linakabiliana na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja dampo kupata moto, dampo kutokuwa la kisasa na maji yenye sumu kwenda katika makazi ya wananchi.

  Hata hivyo Manispaa ya ilala imetenga kiasi cha fedha shilingi Bilioni moja za kitanzania kwa mwaka wa fedha ulioisha pamoja na kuzungumza na wadau wa maendeleo ikiwa ni mkakati madhubuti wa kuweza kuboresha Dampo hilo kinalotumika kwa kiasi kikubwa na manispaa zote za jiji la Dar es Salaam. 
   Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina (kulia) akionyesha jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema wakati wa ziara yake aliyoifanya mapema hii leo jijini Dar es salaam ya kukagua uchafuzi wa mazingira katika Dampo la Pugu Kinyamwezi lililopo Wilaya ya ILala.   
   Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina (kulia) akiwa ameambatana na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe. Isaya Mwita (kushoto) wakati wa ziara ya kukagua uchafuzi wa mazingira katika Dampo la Pugu Kinyamwezi ambap ameipiga faini ya milioni 25 Manispaa ya Ilala kwa uchafu wa mazingira kwa wakazi wa Pugu.       
   Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina akizumgumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara hiyo aliyoifanya katika Dampo la Pugu Kinyamwezi lililopo Ilala jijini Dar es salaam.   
  Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina (kulia) akibadiishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema(katikati), Sophia Mjema na kushoto ni Mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam Mhe. Isaya Mwita wakati wa ziara ya ukaguzi wa uchafuzi wa mazingira uliofanyia katika dampo la Pugu KInyamwezi jijini Dar es salaam.  

  0 0
  0 0

  Timu ya wataalam kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme  Tanzania (TANESCO) wameanza maandalizi ya uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji wa Umeme Umeme Vijijini Awamu yaTatu (REA III) katika mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza na Simiyu. Uzinduzi huo unatarajiwa kufanywa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani mapema wiki ijayo. Sambamba na uzinduzi huo, wakandarasi watakaotekeleza mradi huo watatambulishwa kwa wabunge, madiwani na wanakijiji kutoka katika mikoa husika ambapo miradi itatekelezwa.

   Mkurugenzi wa Utawala na Fedha kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), George Nchwali (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwenye eneo la jiwe la msingi kwa ajili ya uzinduzi wa Mradi wa REA Awamu ya Tatu ambalo liko katika hatua za mwisho wa ukamilishwaji wake.

   Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Mhe. Diwani Athuman (mbele) akizungumza na timu  ya watendaji kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme  Tanzania (TANESCO) na wakandarasi ofisini kwake kuhusiana na maandalizi ya uzinduzi huo.

   Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Kanali Mstaafu, Shaban Lissu (katikati) akisalimiana na Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Masoko na Teknolojia kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Elineema Mkumbo (kulia) mara baada ya  timu ya maandalizi kuwasili katika eneo la Rwabigaga wilayani Kyerwa ambapo kutafanyika uzinduzi huo kwa mkoa wa Kagera

  Mkurugenzi wa Utawala na Fedha kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), George Nchwali (kushoto) akielezea miradi ya umeme vijijini  inayotekelezwa na Wakala huo. Kulia ni Meneja Mipango Miradi na  Tafiti kutoka wakala huo,  Mhandisi Jones Olotu.


  0 0

      Na Haji Nassor (OUT), Pemba
  Kiasi cha  shilingi bilioni 39.7 kati ya shilingi bilioni 42 zilizotolewa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu Zanzibar ‘BMEJZ’ kwa ajili ya kuwakopesha wanafunzi waliosoma elimu ya juu, ziko mikononi mwa wadaiwa hao, kuanzia mwaka 2006 hadi mwezi Juni mwaka huu.

  Wakati fedha hizo zikiwa mikononi mwa wadaiwa, tayari shilingi bilioni 2.3 ndizo pekee, zilizokwisharejeshwa na wakopaji, ambapo kati ya hizo shilingi bilioni 42, shilingi bilioni 7.7 Bodi hiyo ilizirithi kutoka kwa uliokuwa mfuko wa elimu ya juu Zanzibar, ambao ulikoma kufanya kazi zake mwaka 2011.

  Bodi hiyo ya mikopo ya elimu ya juu, kila mwezi hukusanya wastani wa shilingi milioni 100, kutoka kwa wakopaji ambao ni wanafunzi kila mwezi hadi mwezi Juni mwaka huu wa 2017.

  0 0


  0 0

  KAMA ILIVYOKUWA DESTURI YA WATANZANIA  WAISHIO MAREKANI HAPO MIAKA YA NYUMA KUKUTANA WAKATI WA "LABOR DAY WEEKEND" NDANI YA WASHINGTON DC,SASA KUANZIA MWAKA HUU WATANZANIA WAISHIO WASHINGTON DMV WAMEAMUA KUIRUDISHA DESTURI HIYO KWA  KUANDAA  REUNION KABAMBE KWA STYLE YA KIPEKEE,IKIJUMUISHA MICHEZO YA WATOTO,WATU WAZIMA,CHAKULA,PAMOJA NA VIBURUDISHO  KUTOKA KWA WASANII MBALIMBALI KUTOKA TANZANIA NA MAREKANI,HABARI KAMILI NA MPANGO MZIMA KUFUATA ILA KWA SASA WATANZANIA WOTE WAANZE KUJIANDAA NA SAFARI YA WASHINGTON DC SEPTEMBER MOSI HADI TATU.
  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akipokelewa na Msani Mrisho Mpoto katika banda la Elimu kwa Umma la Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro katika Maonesho ya Sabasaba ambapo kupita banda hilo mkuu wa mkoa amehahidi kuwapeleka wanafunzi 50 wa mkoa wa Dar es Salaam bonde la hifadhi ya Ngorongoro
    Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akiasalimaina na Watendaji wa Ngorongoro  katika banda la Elimu kwa Umma la Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro katika Maonesho ya Sabasaba
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda, akikabidhi zawadi kwa watoto waliojibu maswali vizuri juu ya hifadhi ya Ngorongoro
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makondaakikabidhi zawadi kwa watoto waliojibu maswali vizuri juu ya hifadhi ya Ngorongoro
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akizungumza na wakazi wa jiji la Dar es Salaaam waliofika katika banda la Elimu kwa Umma la Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro katika Maonesho ya Sabasaba. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Duka la My Wedding Solutions, Anna Lema akishirikiana na Mama yake Mzazi pamoja na Mtoto wake Doreen kukaka keki maalum ya Sherehe za kuamisha ya Miaka 10 ya Duka la My Wedding Solutions, iliyofanyika katika Hoteli ya Sea Scape, Mbezi Beach Jijini Dar es salaam usiku wa Julai 7, 2017.
  Mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa Duka la My Wedding Solutions, Anna Lema (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya wageni waliofika katika Sherehe ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Duka la My Wedding Solutions, iliyofanyika katika Hoteli ya Sea Scape, Mbezi Beach Jijini Dar es salaam usiku wa Julai 7, 2017.
  Mmoja wa ma MC wa shughuli hiyo, Salma Msangi akizungumza wakati akiweka sawa mambo katika Sherehe hiyo ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Duka la My Wedding Solutions, iliyofanyika katika Hoteli ya Sea Scape, Mbezi Beach Jijini Dar es salaam usiku wa Julai 7, 2017.
  Sakina Lyoka ambaye ni MC pia akisikiliza jibu baada ya kumuuliza swali, Mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa Duka la My Wedding Solutions, Anna Lema, katika Sherehe hiyo ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Duka la My Wedding Solutions, iliyofanyika katika Hoteli ya Sea Scape, Mbezi Beach Jijini Dar es salaam usiku wa Julai 7, 2017.


  0 0
  0 0

  Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dr. Pindi Chana akisalimiana na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe alipotembelea banda la LAPF katika maonyesho ya biashara ya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam,mapema jana.
  Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya LAPF Prof. Faustine Bee (katikati aliyeshika tuzo ya ushindi wa Lapf )akiwa katika picha ya pamoja na Meneja masoko wa LAPF Bw.James Mlowe pamoja na wafanyakazi wa mfuko huo wakati alipotembelea banda la mfuko wa Pensheni wa LAPF katika viwanja vya Sabasaba mapema jana . 
  Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dr. Pindi Chana akipokea zawadi kutoka kwa mtumishi wa LAPF Simboninsia Ndosi alipotembelea banda la LAPF katika maonyesho ya biashara ya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, kulia anayeshuhudia tukio hilo ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe mapema jana 
  Wanachama wapya wa LAPF wakielekezwa kujaza fomu ya kujiunga na mfuko huo mapema jana katika viwanja vya sabasaba mapema jana. 
  Mtumishi wa LAPF akimsajili mmoja wa wanachama wa LAPF alietembelea banda hilo. 
  Wateja wakiwa wanasubiri kupata kadi zao za uanachama mara baada ya kujiunga na mfuko huo mapema jana katika maonesho ya sabasaba.
  Maafisa wa LAPF wakitoa maelezo kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam waliofurika kwenye banda la LAPF na kujiunga na uanachama kwenye mfuko katika maonesho ya SabaSaba mapema jana.

  0 0  Mfanyakazi wa Finca Microfinance Bank Bi ;Irene Kijangwa akimpa maelezo mteja aliyetembelea banda lao kuhusu hatua jinsi ya kufungua akaunti za Finca .mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es salaam.
  Mfanyakazi wa Finca Microfinance Bank Bi ;Irene Kijangwa akimpa maelezo mteja aliyetembelea banda lao kuhusu hatua jinsi ya kufungua akaunti za Finca .mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es salaam.
  Wafanyakazi wa Finca Microfinance Bank wakitoa maelezo kwa mteja aliyefika katika banda la FINCA kufungua akaunti Mapema jana katika maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es salaam.


  0 0

  Ujenzi wa Daraja la Kavuu lenye urefu wa Mita 89 linalounganisha Halmashauri ya Wilaya ya Mlele na Halmashauri ya Wilaya ya Mpwimbwe Mkoani Katavi ujenzi wake umekamilika na litaanza kutumika ifikapo mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu.

  Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa Daraja hilo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amesema kukamilika kwa ujenzi huo kutarahisisha usafirishaji wa abiria na Mizigo kutoka Mkoa wa katavi kwenda mikoa ya jirani.

  “Serikali iliona kero kubwa wanazozipata wananchi wa mkoa huu hasa kwenye usafirishaji wa abiria na mizigo kwenye kipindi cha mavuno, hivyo baada ya kukamilisha Daraja hili wananchi wataweza kupita vipindi vyote vya Mwaka,” alisema Naibu Waziri Eng. Ngonyani.

  Aidha, Eng. Ngonyani amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Katavi Eng. Abdon Maregesi Kuhakikisha Mzani unaohamishika unawekwa ili kudhibiti magari yatakayozidisha Tani 36.

  Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Katavi Eng. Abdon Maregesi amemuhakikisha Naibu Waziri, Eng. Ngonyani kuwa wakala utaweka mzani huo ili kutoruhusu magari yaliyozidisha Uzito wa Mzigo kupita kwenye Daraja hilo.
   Naibu Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa kwanza kushoto), akikagua ujenzi wa Nyumba za viongozi zinazojengwa na Wakala Wa Majengo nchini (TBA) Mkoani Katavi, Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mlele Bi. Rachel Kassanda.
   Meneja Wa Wakala Wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Abdon Maregesi (kulia), akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Katikati) juu ya hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Daraja la Kivuu wakati Naibu Waziri huyo alipokagua, Mkoani Katavi.

   Muonekano wa Daraja la Kavuu lenye urefu wa Mita 89 linalounganisha Halmashauri ya  Wilaya ya Mlele na Halmashauri ya Wilaya ya Mpwimbwe Mkoani Katavi ambalo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99.


  0 0

  Wamiliki wa bendi ya FM Academia “Wazee wa Ngwasuma” wametoa ufafanuzi juu ya kile kilichopelekea Nyoshi el Saadat kuvuliwa cheo cha urais wa bendi.

  Wiki mbili zilizopita Nyoshi alivuliwa cheo hicho alichokitumikia kwa takriban miaka 20 na nafasi yeke kuchukuliwa na Patcho Mwamba, hatua ambayo imezua fikra tofauti miongoni mwa mashabiki wa muziki wa dansi – wengine wakiona Nyoshi kaonewa na wengine wakiunga mkono mabadiliko.

  Blake Mwambona ambaye amejitambulisha kama mdogo wa aliyekuwa mmiliki wa FM Academia (Marehemu Martin Kasyanju), amesema kwamba kwa zaidi miezi sita iliyopita, maendeleo ya bendi yamekuwa yakididimia kwa kasi kuwa, ikiwa ni pamoja kukosekana ari kwa wanamuziki wengi.

  Mwambona amesema wanaamini mfumo wa kubadilishana uongozi, ndio bora zaidi badala kumsimika mtu uongozi kwa miaka mingi na mwisho wa siku anageuka kuwa mtawala. 

  Naye Nsajigwa Martin Kasyanju ambaye ni mtoto wa marehemu Martin Kasyanju, amesema kuwa wao hawajamfukuza Nyoshi, ila akiamua kuondoka hawana kizuizi.Tayari imedaiwa kuwa Nyoshi yuko chimbo akisuka bendi yake mpya na hajakanyaga show za FM tangu avuliwe urais wa bendi.

  Katika mahojiano yake na Jembe FM ya Mwanza wiki mbili ziliyopita, Nyoshi alifunguka kuwa ameachana na FM Academia na ataibuka na bendi mpya. 

  “Hatujamfukuza, tumebadili uongozi wa bendi kwa manufaa ya biashara yetu, kama yeye hawezi kuishi FM bila cheo cha urais, hatutakuwa na namna ya kumsaidia. Kwetu sisi biashara kwanza halafu mambo mengine baadae", Japo yanasemwa mengi, hata hivyo sisi tunatambua Nyoshi bado ni muajiliwa wa FM Academia kama mikataba inavyojieleza na taratibu za kazi zilivyo, anaeleza Nsajigwa.

  “Tunathamini sana mchango wa Nyoshi, lakini ni lazima ifahamike kuwa FM Academia inafanya biashara, kuna wakati maamuzi magumu lazima yachukuliwe kwaajili kulinda biashara” aliongeza Nsajigwa na kufichua kuwa mabadiliko hayo yameongeza furaha, amani na ari kwa wanamuziki wa FM Academia.

  0 0

  Wafanyakazi kampuni ya Uber Godfrey Mabula na Ibrahimu Kunguya wakitoa maelezo kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam waliofurika katika banda kujua jinsi Program ya Uber inayorahisisha usafiri wa kutumia teknolojia ya kisasa na gharama nafuu pia wateja wote waliopakua Program hiyo walipata punguzo la kiasi cha 8200Tsh kwa safari yao ya kwanza.Mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es salaam. 
  Wateja waliofika katika banda la uber wakipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa Uber Jinsi ya kupakua na kutumia Progamu ya Uber ambayo inarahisisha usafiri na kwa gharama nafuu,Mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es salaam. 
  Balozi wa Uber akitoa maelekezo kwa mteja aliyefika katika banda lao ambapo pia wateja walijipatia punguzo la kiasi cha 8200 Tsh mara baada ya kupakua na kutumia program ya uber katika kuagiza usafiri kwa bei nafuu na kwa teknolojia ya kisasa mapema jana katika maonesho ya saba saba. 


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaeleza viongozi mbalimbali waliotembelea viwanja vya maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jinsi Taasisi yake inavyofanya kazi za kutibu magonjwa ya Moyo na umuhimu wa kupima afya mara kwa mara japo mara moja kwa mwaka.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea jambo na Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa Tan Trade Fidelis Mugenyi wakati alipotembelea maonyesho ya Kimataifa ya biashara yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam. 
  Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akiwaonyesha wananchi waliotembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jinsi upasuaji wa Moyo unavyofanyika.
  Wananchi wakiwa katika mstari wa kupima magonjwa ya Moyo bure na kupata ushauri katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi (kushoto) akibadilishana mawazo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tan trade Edwin Rutageruka (kulia) na Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa Tan Trade Fidelis Mugenyi (katikati) alipotembelea maonyesho ya Kimataifa ya biashara yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam. 


older | 1 | .... | 1789 | 1790 | (Page 1791) | 1792 | 1793 | .... | 3348 | newer