Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

Lubeleje: Biko imeondoa changamoto zangu za kimaisha

$
0
0
MSHINDI wa droo ya 20 ya Bahati Nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku’ iliyofanyika Jumatano iliyopita, Philipo Lubeleje, amesema kwamba donge nono alilokabidhiwa na Biko limeondoa changamoto zake za kimaisha, kutokana na ugumu wa maisha anaokutana nao kwenye majukumu yake ya kila siku.

Lubeleje anayejishughulisha na ujenzi wa nyumba jijini Dar es Salaam, alikabidhiwa fedha zake jana katika benki ya NMB jijini hapa, huku akisema amekuwa akiishi maisha magumu, hivyo anazitumia fedha zake vizuri ili akuze uchumi wake.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Lubereje ambaye ni mkazi wa Gongolamboto, jijini Dar es Salaam, alisema amepokea ushindi wake kwa shangwe sambamba na kumshukuru Mungu kwa kumuona, akiamini kuwa amefanya hivyo baada ya kubaini kiu yake ya kupata maendeleo ya kiuchumi.

Alisema hata kuamua kucheza bahati nasibu ya Biko kulitokana na kutafuta fursa za kupata mwangaza wa kiuchumi, akisema kuwa shughuli za ujenzi wa nyumba zina changamoto nyingi na uhaba wa kazi mara kwa mara.

“Namshukuru Mungu kwa kuniletea zawadi hii ya Sh Milioni 20 kwa kupitia Biko, hivyo naomba Watanzania wenzangu nao wacheze kwa sababu nao wanaweza kushinda kama mimi kwa kufanya miamala kwenye simu zao za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money, ambapo kama inavyotakiwa, namba ya kampuni ni 505050 na kumbukumbu ni 2456.
Mkazi wa Gongolamboto jijini Dar es Salaam, Philipo Lubeleje, akiwa kwenye furaha baada ya kukabidhiwa Sh Milioni 20 zakw kutoka wa waendeshaji wa bahati nasibu ya Biko. Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa Sh Milioni 20 ambaye ni mkazi wa Gongolamboto jijini Dar es Salaam, Philipo Lubeleje katikati mwenye fulana ya pundamilia akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage wa pili kutoka kulia, wakiwa kwenye tukio la kumkabidhi Sh Milioni 20 mshindi huyo wa droo ya 20. Wengine ni ndugu zake pamoja na afisa wa NMB, jijini Dar es Salaam katika makabidhiano hayo yaliyofanyika jana.
Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, kulia akimkabidhi Sh Milioni 20 mshindi wa droo ya 20 ya bahati nasibu ya Biko, Philipo Lubeleje katikati. Mwingine pichani ni Afisa wa NMB jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Rejista ya Wahisiwa kuwa na Kifua Kikuu(TB) yazinduliwa Mjini Dodoma

$
0
0
Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikari za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene akikata utembe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Rejista mpya ya wanaohisiwa kuwa na Kifua kikuu ambayo itaanza kutumika kwenye vituo vyote vya kutolea huduma, wakati wa Mkutano wa mwaka wa Waganga waWakuu wa Mikoa na Wilaya unaoendelea Mjini Dodoma,Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kigwangwalla
Dkt.Hamisi Kigwangwalla akisoma moja ya Rejista hiyo ambayo imezinduliwa rasmi leo,kulia kwake ni Waziri Simbachawane na aliyesimama kushoto ni Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Zainabu Chaula
Waziri Simbachawene akimkabidhi Rejista hiyo Naibu Katibu Mkuu-TAMISEMI upande wa Afya Dkt. Zainabu Chaula
Baadhi ya Wakurugenzi toka Wizara ya Afya,TAMISEMI pamoja na Taasisi za Wizara ya Afya wakitambulishwa wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya unaofanyika kwenye ukumbi wa LAPF Mjini Dodoma(Picha zote na Wizara ya Afya).

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) YATOA HUDUMA BURE YA UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO, KUTOA USHAURI NA KUELEZA WANANCHI HUDUMA ZA MATIBABU YA MOYO WANAZOZITOA KATIKA MAONYESHO YA SABASABA

$
0
0
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Upendo Mwaipopo akimpima mapigo ya moyo (BP) Lei Jian ambaye alifika katika banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali wanazozitoa.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Aika Nnkya akimpima mapigo ya moyo (BP) Elioth Mgulwa mkazi wa Makambako mkoani Njombe ambaye alitembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo wanazozitoa.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Aika Nnkya akimpa ushauri kuhusu afya ya moyo Kizito Joseph (kushoto) ambaye alitembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo wanazozitoa.
Mama Anastazia Mombeki (kulia) akipimwa urefu na Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rogers Kibula wakati alipotembelea Banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo wanazozitoa.

DC SHINYANGA AKABIDHI SARE ZA SHULE KWA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

$
0
0

Matiro amesema anasikitishwa na wananchi mjini Shinyanga kuwa wa kwanza kuchanga michango ya harusi na wengine kutumia pesa hovyo kwenye vileo na wakati kuna watoto wanahitaji msaada hata wa sare za shule na viatu ili waende shule lakini kutokana na kuishi mazingira magumu watoto wanakwama na hatimaye kufanya vibaya darasani. 

Matiro ametoa rai hiyo leo Alhamis Julai 6,2017 mjini Shinyanga wakati akikabidhi nguzo za shule kwa watoto 164 kati ya 1400 ambao wanaishi katika mazingira magumu katika manispaa ya Shinyanga. 

Matiro ametoa msaada huo kwa kwshirikiana na Shirika la TVMC na PWWCO ambayo yanasaidia watoto na akina mama wanaoishi katika mazingira magumu mjini Shinyanga. 

Matiro alisema lengo kuu la msaada huo kuuonesha umma kuguswa namna ya kusaidia watoto wanaoishi mazingira hayo na siyo kuiachia serikali peke yake zikiwamo NGO's na Wageni kutoka nje ya nchi kuja kuokoa watoto hao na wakati wananchi nao wana uwezo wa kuwatatulia changamoto hizo. 

"Ukipita mchango wa harusi unakuta watu wanakuwa wa kwanza kuchangia tena kwa haraka lakini likija suala la kusaidia watoto wanaoishi mazingira magumu, kila mtu utasikia akisema hana pesa ,wananchi mnatakiwa mbadilike" alisema Matiro. 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amewataka wakazi wa mjini Shinyanga kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili waweze kupata elimu wakiwa katika mazingira rafiki na kupata ufaulu mzuri ambao utawafanya wafikie malengo yao ya maisha. 
Mkurugenzi wa Shirika la TVMC mjini Shinyanga Mussa Jonas Ngangala akisoma taarifa kwa mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro jinsi shirika hilo linavyosaidia watoto wanaoishi katika mazingira Magumu na malengo yao juu ya kusaidia watoto 1,400 wanaoishi katika mazingira magumu katika manispaa ya Shinyanga
Zoezi la kukabidhi sare za shule likiendelea 
Watoto 164 wanaoishi katika mazingira magumu wakiwa wamekaa wakisubiri kupewa msaada wa sare za shule na mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro. 

WATANZANIA WASHINGTON DMV- WAIRUDISHA LABOR DAY WEEKEND REUNION KWA KISHINDO

$
0
0

KAMA ILIVYOKUWA DESTURI YA WATANZANIA  WAISHIO MAREKANI HAPO MIAKA YA NYUMA KUKUTANA WAKATI WA "LABOR DAY WEEKEND" NDANI YA WASHINGTON DC,SASA KUANZIA MWAKA HUU WATANZANIA WAISHIO WASHINGTON DMV WAMEAMUA KUIRUDISHA DESTURI HIYO KWA  KUANDAA  REUNION KABAMBE KWA STYLE YA KIPEKEE,IKIJUMUISHA MICHEZO YA WATOTO,WATU WAZIMA,CHAKULA,PAMOJA NA VIBURUDISHO  KUTOKA KWA WASANII MBALIMBALI KUTOKA TANZANIA NA MAREKANI,HABARI KAMILI NA MPANGO MZIMA KUFUATA ILA KWA SASA WATANZANIA WOTE WAANZE KUJIANDAA NA SAFARI YA WASHINGTON DC SEPTEMBER MOSI HADI TATU.

OLD SCHOOL REUNION COLUMBUS, OHIO LABOR DAY PATAKUA HAPATOSHI

$
0
0
PAUL RWECHUNGURA, DEO NGASSA YANGA, NICO NA RENATUS NJOHOLE SIMBA

MAMA NGULI WA MITINDO ASYA IDAROUS KHAMSINI NA MISSY TEMEKE KUONYESHA VIVAZI OLD SCHOOL REUNION
Image result for paul rwechungura
Paul Rwechungura kudakia Yanga
Image result for nico renatus
Renatus Njohole na Nico Njohole kuiongza Simba
Jameel Silia na Abui Hamisi kutoka Sweden kucheza mechi ya Simba na Yanga Columbus, Ohio

Wachezaji wa mpira wa kikapu waliowahi chezea Pazi, Vijana, Don Bosco na kwingineko kuonyeshana maujuzi.

PPF YATANGAZA MAJINA YA MADEREVA WALIOCHAGULIWA KWA USAILI AWAMU YA TATU

BEN POL AFURAHISHWA NA UJIO WA MSANII WA MUZIKI WA KIASILI SAIDA KAROLI

$
0
0
Msanii Ben Pol akizungumzia ujio mpya wa msanii wa muziki wa kiasili Saida Karoli katika Tamasha la Rise and Fall ya Saida Karoli iliyofanyika jana usiku kwenye fukwe za EScape One.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Benard Paul 'Ben Pol' amesema amefurahishwa sana na kurejea kwa mwanamuziki wa mziki wa asili Saida Karoli kwani bado ana uwezo mkubwa wa kuimba.

Ben Pol amesema hayo wakati wa tamasha maalumu lililoandaliwa kwa ajili ya kurejea kwa mwanamuziki huyo aliyetamba zamani na nyimbo zenye asili ya kihaya ikiwa ni miaka 15 toka aanze muziki.

Tamasha la Rise and Fall ya Saida Karoli iliyofanyika jana usiku kwenye fukwe za EScape One na lilikutanisha wasanii mbalimbali na viongozi waliojitokeza kumuunga mkono mwanamama huyo ambaye alipotea kimuziki kwa kipindi kirefu.

Amesema kuwa, Saida bado ana uwezo mkubwa sana wa kimuziki na hilo amelithibisha pale alipotoa wimbo wake mpya na watanzania kuukabali kwa asilimia zote na ameendelea kuonyesha uwezo wake katika kuimba.

"Namkubali sana Saida kwani ni mwanamuziki mzuri na ameonyesha uwezo mkubwa katika tasnia ya muziki na amerejea kwa nguvu kubwa sana na nyimbo yake imekubalika,"amesmea Ben Pol.


Saida ametoa wimbo wake mpya ujulikanao kama Urugambo ulio katika mahadhi ya kihaya na umeonekana kushika kasi sana.

Mbali na hilo, Ben Pol aliambatana na msanii wa vichekesho anayejulikana kama Ebitokea ambapo kwa sasa wanahisiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi.

Kwa upande wa Ebitoke alisema kuwa anafurahi sana kuwa na Ben Pol na anafarijika sana kwani 
Msanii Ben Pol akiwa katika picha ya pamoja na msanii wa vichekesho Ebitoke katika Tamasha la Rise and Fall ya Saida Karoli iliyofanyika jana usiku kwenye fukwe za EScape One.


Msanii wa Vichekesho Ebitoke akizungumzia mahusiano yake na Ben Pol.

MAKAMU WA RAIS, SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA WAOMBOLEZAJI MSIBA WA KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI

$
0
0
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasili kwenye Msiba wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi.
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akimfariji Mjane wa Marehemu, Hassan Rashid Shebuge wakati alipofika msibani hapo, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.
  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akishiriki katika Dua ya kumuombea Marehemu Hassan Rashid Shebuge wakati alipofika msibani hapo, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.
 Sehemu ya Waombolezaji wakiwa wamebeba Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge pindi ulipowasili nyumbani kwake, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo tayari kwa maandalizi ya mazishi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi pamoja na Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro wakiwa wamejumuika na waombolezaji wengine kwenye Msiba wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.

TANZIA: KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI, HASSAN SHEBUGE AFARIKI DUNIA

$
0
0
Katibu Mkuu kiongozi, Balozi John Kijazi anasikitika kutangaza kifo cha Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge (pichani) kilichotokea Julai 06, 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbini Jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Kabla ya kufikwa na Mauti, inaelezwa kuwa Marehemu Shebuge aliugua ghafla akiwa nyumbani kwake, Mbagara Majimatutu mnamo Julai 03, 2017 na kukimbizwa katika Hospitali ya Rangi tatu ili kupatiwa huduma ya dharula na baadae kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbini kwa matibabu zaidi hadi hapo matuti yalipomfika.

Kwa mujibu wa taarifa ya kitaalam iliyotolewa na madaktari, inaelezwa kuwa Maremu Shebuge alipatwa na shinikizo la damu ambalo limepeleka kupoteza kwake maisha.

Tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu, aiweke roho ya Marehemu Hassan Rashid Shebuge mahapa pema peponi, Amin.

Msiba upo nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu.

IFUATAYO NI RATIBA NZIMA YA MSIBA 

WATATU WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI MKOANI TABORA

$
0
0
Na Tiganya Vincent

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora linawashikiria watu watatu kwa tuhuma za mauaji  ya Bwana Mahona Pondamali (50)  mkazi wa Wilaya ya Sikonge yanayosadikiwa kutokea Aprili mwaka huu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Wilbroad Mtafungwa alitoa kauli hiyo jana wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Alisema mnamo tarehe 22 mwezi wa nne mwaka huu mke wa marehemu aliripoti Polisi kupotea kwa mme wake katika mazingira ya kutatanisha na ndipo Jeshi la Polosi ilopoamua kuanza uchunguzi wa tukio hilo na kufanikiwa kubaini kuwa mtu huyo akupotea bali aliwawa.

RPC Mtafungwa alisema kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha tukio kuwa marehemu alipokuwa akinywa pombe alikuwa na tabia ya kumpiga mke wake na watoto na ndipo walipoanda mpango wa kumkodi  mtu wa kumpiga kwa ajili ya ya kumrekebisha tabia hali iliyosababisha mauti yake.

Alisema kuwa baada ya wahusika kubaini kuwa marehemu amekufa ndipo walipoamua kwenda kumtupa katika shimo la wachanaji mbao.

Kamanda Mtafungwa alisema kuwa Polisi kwa kushirikiana na wananchi ndipo walipo gundua kuwa marehemu yuko katika shimo la wachana mbao  na kuamua kulifukua ndipo ndugu wa marehemu waliposema kuwa  ni ndugu yao aliyedaiwa kupotea

Aliwataja wanaotuhumiwa wanaoshikiriwa na Polisi kwa uchunguzi kwa tuhuma za mauaji kuwa Mke wa Marehemu Bibi Tatu Said(30) , mtoto wa marehemu Katambi Mahona (13)na jamii wa kukodi Mwanza Mburuka(31).

Kamanda Mtafungwa aliongeza katika tukioa hilo Polisi walifanikiwa kukamata ng’ombe mmoja  kwa Mburuka ambaye inasadikiwa kuwa ujira kwa mauaji hayo  na jeshi hilo linaendelea kumchunguza kama kuna amekuwa akikodisha ili kutekeleza mauji mablimbali mkoani hapa.

Watuhumiwa wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

BEI YA DAWA ZA SERIKALI YASHUKA NCHINI

$
0
0
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema bei za dawa, vifaa tiba na Vitendanishi vya maabara zinazonunuliwa na kusambazwa Boahari ya Dawa (MSD) zimepungua bei kwa asilimia 15 hadi 80 ukulinganisha na mwaka jana kutokana na hatua ya MSD kuanza utaratibu wa kununua moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, kama alivyo agiza Rais Dk. John Magufuli.

Waziri huyo ameyasema hayo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, alioufanya ofisi za Makao Makuu ya Bohari ya Dawa MSD, Keko, Dar es Salaam leo huku akizielekeza Halmashauri, Hospitali na Vituo vya Afya kutumia bei elekezi ya dawa iliyotolewa ma Wizara ya Afya ambayo ipo kwenye kitabu ya orodha ya bei cha MSD.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa ya kupungua kwa bei za dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kutokana na uamuzi wa serikali wa kununua moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu.

MSD kwasasa inaagiza dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji wanchizipatazo 20 ambazonipamojana Kenya, Uganda, Afrika Kusini, India, Bangladesh, Pakistan, Jamuhuri ya Watu wa Korea, China, Ujerumani, Uingereza, Uswisi, Denmark, Ufaransa, Ubelgiji, Italia, Romania, Marekani, Cyprus, Falme za Kiarabu, na Tanzania. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu amesema tayari wametoa mikataba 73 kwa wazalishaji ambapo kati ya hiyo 46 ni ya wazalishaji wa dawa ambao wanatoka nchi za Uganda, Denmark, Ufaransa, Ujerumani, China, Afrika Kusini, Nchi za Falme za Kiarabu,Bangladesh, India, Kenya na Tanzania ambao wanazalishia aina 178 za dawa.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu akisisitiza jambo katika mkutano huo.

Baadhi ya dawa hizo ni pamoja na dawa ya chanjo ya homa ya ini (hepatitis B Vaccine ) awali ilikuwa ikiuzwa shilingi 22,000 sasa inauzwa shilingi 5,300, Dawa ya sindano ya Diclofenac kwa ajili ya maumivu (vichupa 10) awali ilikuwa ikiuzwa shilingi 2,000 sasa inauzwa shilingi 800 na Dawa ya kupambana na maambukizi ya bacteria (Amoxicillin/Clavulanic Acid Potassium 625mg) yenye Vidonge 15 awali iliuzwa shilingi 9,800 sasa inauzwa shilingi 4,000.

Kwa upande wa vifaa tiba amesema jumla ya wazalishaji 18 wamepata mikataba ambao wanatoka Uingereza, Ujerumani, India, Kenya na Tanzania, kwa ajili ya aina 195 za vifaa tiba.Aidha, kwa upande wa vitendanishi vya maabara, jumla ya wazalishaji 9 kutoka nchi za Uingereza, Ujerumani, Ubelgiji, Romania, China, India na Kenya wamepata mikataba kwa ajili ya aina 178 za vitendanishi vya maabara. 
Sehemu ya Washiriki.

Kwa mujibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Serikali ya awamu ya tano imeboresha kwa kiasi kikubwa hali ya upatikanaji wa dawa nchini ambapo bajeti ya dawa,vifaa tiba, vitendanishi vya maabara na chanjo kwa mwaka huu wa fedha 2017/2018 ni shilingi Bilioni 269 kutoka Bilioni 251 ya mwaka jana wa fedha 92016/2017.
Picha ya pamoja. Na Dotto Mwaibale

MICHUZI TV: MWANAMUZIKI SHAABAN DEDE AZIKWA LEO JIJINI DAR

$
0
0
Sehemu ya Waumini wa Kiislam pamoja na waombolezaji wengine, wakishiriki kwenye Mazishi ya Marehemu Shaaban Dede, katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam leo.

Baadhi ya ndugu, Jamaa na Marafiki wa karibu wa Marehemu Shaaban Dede wakielekea katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhwan Kikwete akizungumza na Waandishi wa Habari katika Mazishi hayo yaliyofanyika katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo. 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza akitoa Salamu za Rambirambi kwa niaba ya Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, katika Mazishi hayo yaliyofanyika katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

MAMA JANETH MAGUFULI AZUNGUMZA NA KUTOA MISAADA MBALIMBALI KWA WAZEE WASIOJIWEZA 400 CHATO MKOANI GEITA

$
0
0
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwakabidhi kwa pamoja mafuta waakilishi wa Wazee kutoka kata ya Kasenga AnatoryBisate (64) kulia pamoja na Bi. Winfrida Lawrent(65) kushoto mara baada ya kuzungumza na wazee 400 katika Ukumbi wa Mshikamano SACCOS Chato mkoani Geita.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiimba pamoja na wanakwaya wa Mwagazege mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mshikamano SACCOS Chato mkoani Geita.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akizungumza na Wazee wasiojiweza zaidi ya 400 kutoka Wilaya ya Chato katika Ukumbi wa Mshikamano Saccos. 

Naibu Waziri Ole Nasha awaasa watanzania kula korosho

$
0
0

Na Chalila Kibuda , Gobu ya Jamii 

Naibu Waziri wa Kilimo , Uvuvi na Mifugo, William Ole Nasha amewasaa watanzania kula korosho kwa wingi ili kuweza kuepukana na magonjwa mbalimbali ambayo yanagharimu na kukosa nguvu kazi ya taif. 

Nasha ameyasema hayo leo katika Siku ya Korosho katika maonesho ya 41 biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba), amesema kuwa korosho inasaidia kuepukana na mafuta mwilini ambayo yanasababisha magojwa ya moyo kwa kiasi kikubwa. 

Amesema kuwa katika utumiaji wa kurosho kwa kula inafanya kuongezeka kwa pato la taifa na kuwafanya wananchi kuwa nguvu kazi yenye kuzalisha kwa tija kwa maendeleo uchumi hasa katika kuelekea uchumi wa viwanda. 

Nasha amesema kuwa kilimo cha korosho kimeboreshwa na kuwataka wakulima kulima mbegu za kisasa pamoja na kufuata ushauri wa watalaam wa kilimo katika maeneo yao. 

Aidha amesema kuwa katika maonesho hayo watu watumie fursa ya kujifunza kilimo cha kurosho katika kujenga uchumi wa viwanda wa adhima ya serikali ya awamu ya tano ya Dk. John Pombe Magufuli. 

Makamu Mwenyekiti Bodi ya Korosho, Makola Majogo amesema kuwa wanaendelea katika utoaji wa ulimaji wa kilimo cha kisasa cha kurosho katika kuwa ni zao kuleta maendeleo uchumi wa nchi pamoja na mkulima kunufaika na kilimo hicho.
 Naibu Waziri wa Kilimo , Uvuvi na Mifugo, William Ole Nasha akizungumza katika siku ya Korosho katika maonesho ya 41 ya biashara Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mwenyekiti  wa Bodi ya Korosho, Makola Majogo akizungumza na waandishi wa habari juu umuhimu wa zao la korosho katika maonesho ya 41 ya biashara Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

 Naibu Waziri wa Kilimo , Uvuvi na Mifugo, William Ole Nasha akiwa katika picha ya pamoja na mifuko ya korosho katika maonesho ya 41 ya biashara Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wadau wa waliofika katika Siku Korosho katika maonesho ya 41 ya biashara Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

WANANCHI WAJITOKEZA KWA WINGI KATIKA MAADHIMISHO YA 41 YA MAONESHO YA SABASABA

$
0
0

 Wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye maadhimisho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika Viwanja vya Sabasaba leo Jijini Dar es salaam
Farasi awa kivutio kwa watoto wengi wajitokeza kupiga picha.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mpakani wakiwa wamekuja kutembelea maadhimisho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika Viwanja vya Sabasaba leo Jijini Dar es salaam

 Wananchi wakiwa wametembelea banda la Mifugo na uvuvi na kuangalia namna samaki aina ya kambale wanavyofugwa maadhimisho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika Viwanja vya Sabasaba leo Jijini Dar es salaam.Picha  na Team Michuzi Sabasaba.

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) yakaribisha wananchi kupima afya bure sabasaba

$
0
0
Na Frank Mvungi- Maelezo

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete imewataka Wananchi  kujitokeza kwa wingi kupima afya zao hasa magonjwa ya moyo katika msimu huu wa maonesho ya Kimataifa ya 41 ya Biashara ya Dar es Salaam yanayofanyika katika viwanja vya JK Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika viwanja vya maonesho hayo Mkurugenzi Mkuu  wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi amesema kumekuwa na muitikio mkubwa sana kwa wananchi kutembelea banda lao ambapo amesema kuwa kwa siku takribani watu 700 wanafika katika banda hilo kwa ajili ya kupata huduma na ushauri.

“Ni vizuri watanzania wakatumia fursa hii kufika hapa  na watapatiwa baadhi ya vipimo na ushauri  bure katika banda  letu lililopo ndani ya viwanja vya sabasaba kwa kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuwahudumia wananchi wake kwa kuhakikisha kuwa wanapata huduma zote za msingi zenye kiwango na ubora,” Alisisitiza Prof. Janabi

Akifafanua  Prof. Janabi amesema  Taasisi hiyo imedhamiria kuwahudumia wananchi wakati wote wa maonesho na hata baada ya hapo wapo tayari kuwahudumia wale wanaohitaji huduma katika taasisi hiyo.

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete imekuwa ikitoa huduma za upasuaji wa moyo tangu kuanzishwa kwake hali inayosaidia kupunguza gharama zilizokuwa zinatumika kusafirisha wagonjwa kwenda nje ya nchi kwa matibabu kwa kipindi kirefu sasa.

 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi akiteta jambo na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi yake alipotembelea Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam leo. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo Bi. Anna Nkinda.
 Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Bashir Nyangasa akielezea namna upasuaji wa moyo unavyofanywa kwa mmoja wa mwananchi aliyetembelea banda la taasisi hiyo katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) leo.
 Wananchi wakipata huduma ya vipimo katika banda la Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) leo.
Wananchi wakipata huduma ya vipimo katika banda la Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) leo.


Picha na: Frank Shija – MAELEZO.

Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Zanzibar atembelea banda la Global Education Link

$
0
0
Mkurugenzi wa Udahili wa Global Education Link Ltd Zakia Nassor akimuelezea jambo Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Zanzibar Moudline Castico wakati alipotembelea banda Global Eductaion Link katika maonesho ya biashara ya 41 ya kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba Jijini Dar es salaam.
Mtaalamu wa Udahili wa Global Education Link Medadi Sota akimuelezea  Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Zanzibar Moudline namna ya kuwasaidia wanafunzi kudahili wanafunzi katika nchi mbalimbali wakati alipotembelea banda la Global Link katika maonesho ya biashara ya 41 ya kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba Jijini Dar es salaam.

Wanafunzi wakiendelea kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupata mwongozo wa wa namna ya kujiunga na vyuo vya nje ya nchi kupitia Global Education Link katika maonesho ya biashara ya 41 ya kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba Jijini Dar es salaam.

NHIF YAWAPONGEZA WANANCHI WANAOENDELEA KUJITOKEZA KUPATA KADI ZA BIMA YA AFYA

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bw. Mpoki Alisubisya akipata maelezo ya jinsi wanachama wa NHIF wanavyohakikiwa wakati wakienda kupata huduma katika vituo vya afya. Maelezo yanatolewa na Afisa mtaalam wa mambo ya Tehama wa NHIF Bw. Maleko katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea huku Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa NHIF Bw. Muganga akifuatilia.
 Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Angela Mziray akimuelekeza mwananchi aliyejitokeza kwenye banda la Bima ya Afya kwa ajili ya kujipatia kadi ya Bima katika maadhimisho ya maonesho ya 41 ya kimataifa ya biashara Sabasaba leo Jijini Dar es salaam.

 Wananchi wakiendelea kuoata huduma ya Bima ya Afya katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika maadhimisho ya maonesho ya 41 ya kimataifa ya biashara Sabasaba leo Jijini Dar es salaam.
Maafisa wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya (NHIF) wakiwa wanendelea na kazi ya kusajili wananchi wanaojitokeza kupata kadi za bima ya Afya katika maadhimisho ya maonesho ya 41 ya kimataifa ya biashara Sabasaba leo Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Zanzibar atembelea banda la Global Education Link

$
0
0
Mkurugenzi wa Udahili wa Global Education Link Ltd Zakia Nassor akimuelezea jambo Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Zanzibar Moudline Castico wakati alipotembelea banda Global Eductaion Link katika maonesho ya biashara ya 41 ya kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba Jijini Dar es salaam.
Mtaalamu wa Udahili wa Global Education Link Medadi Sota akimuelezea  Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Zanzibar Moudline namna ya kuwasaidia wanafunzi kudahili wanafunzi katika nchi mbalimbali wakati alipotembelea banda la Global Link katika maonesho ya biashara ya 41 ya kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba Jijini Dar es salaam.

Wanafunzi wakiendelea kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupata mwongozo wa wa namna ya kujiunga na vyuo vya nje ya nchi kupitia Global Education Link katika maonesho ya biashara ya 41 ya kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba Jijini Dar es salaam.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images