Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

WANANCHI WAKIPATA HUDUMA KATIKA MAONESHO YA 41 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA SABASABA

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Nje na  Kikanda,  Dkt Augustine Mahiga akipata maelezo katika banda la TFDA  alipotembelea banda hilo katika maonesho ya 41 ya Kimataifa katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na  Kikanda, Dkt  Augustine Mahiga  akisaini kitabu cha wageni  katika  banda la TFDA  alipotembelea  maonesho ya 41 ya Kimataifa katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. 
 Wananchi wakipata huduma katika banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ajili ya ulipaji wa kodi ya majengo katika  maonesho ya 41 ya Kimataifa katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. 

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI AKUTANA NA TIMU YA WATAALAMU KUTOKA BENKI YA DUNIA KUJADILI MASUALA YA WAKIMBIZI

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza na timu ya wataalamu kutoka Benki ya Dunia wanaosimamia Mpango wa Kuzisaidia Nchi Zilizoathirika na kuhifadhi Wakimbizi, waliofika wizarani kujadili masuala mbalimbali ya wakimbizi.Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza na timu ya wataalamu kutoka Benki ya Dunia wanaosimamia Mpango wa Kuzisaidia Nchi Zilizoathirika na kuhifadhi Wakimbizi, waliofika wizarani kujadili masuala mbalimbali ya wakimbizi.Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke, akizungumza wakati wa kikao na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira,baada ya  timu ya wataalamu kutoka Benki ya Dunia wanaosimamia Mpango wa Kuzisaidia Nchi Zilizoathirika na kuhifadhi Wakimbizi kutembelea  wizara wakiwa na lengo la  kujadili masuala mbalimbali ya wakimbizi.Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

 Mratibu wa Mpango wa Kusaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi,Dk.  John Jingu, akizungumzawakati wa kikao naKatibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira,baada ya  timu ya wataalamu kutoka Benki ya Dunia wanaosimamia Mpango wa Kuzisaidia Nchi Zilizoathirika na kuhifadhi Wakimbizi kutembelea  wizara wakiwa na lengo la  kujadili masuala mbalimbali ya wakimbizi.Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ATEMBELEA BANDA LA PROPERTY INTERNATIONAL, MAONYESHO YA SABASABA

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Property International, Abdul Haleem, kuhusu Ndege ya Kampuni hiyo inayopiga picha za juu kwa muda mfupi wakati wa upimaji wa Viwanja (Unmanned Ariel Vehcle As 1200) wakati Makamu wa Rais alipotembelea Banda la Maonyesho la Kampui hiyo kwenye Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisaini kitabu cha wageni wakati alipowasili kwenye Banda hilo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Property International, Abdul Haleem.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Property International, Abdul Haleem, akiendelea kutoa maelezo kwa Makamu wa Rais kuhusu ujenzi wa nyumba zinazojengwa na Kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na kuuza na kukopesha Viwanja.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Teknolojia ya 'Mega Panel' wa Kampuni ya Property International, Jonathana Kibona, wakati alipotembelea Banda la maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa la Kampuni hiyo ndani ya Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo.

TIB Group yawakaribisha watanzania katika bandalao Sabasaba

VYUO VIKUU VYA NJE YA NCHI VYAENDELEA KUOMBA MIKATABA GLOBAL EDUCATION LINK (GEL)

$
0
0
 .Mkurugenzi  wa Global Education Link (GEL), ambao ni Mawakala  Wakubwa wa Vyuo Vikuu vya Nje  ya Nchi, Abdulmalik  Mollel akisaini mkataba wa makubaliano  na  Afisa Udahili  wa Chuo cha Sri Venkteswara   cha nchini India cha Uhandisi na Teknolojia  ,  Bheems Neyulu  hafla hiyo ilifanyika katika ofisi za viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam ikiwa ni  sehemu ya kuendelea na kujiandaa katika   maandalizi  ya mahitaji ya rasilmali watu  katika sekta ya viwanda nchini .
 Mkurugenzi  wa Global Education Link (GEL)  Abdulmalik Mollel  akibadilishana hati ya makubaliano  na  Afisa Udahili  wa Chuo cha Sri Venkteswara   cha nchini India ,  Bheems Neyulu  hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za viwanja vya sabasaba jijini  Dar es Salaam.
 Mkurugenzi  wa Global Education Link (GEL)  Abdulmalik Mollel akionesha mfumo wa udahili wa Vyuo Vikuu vya Nje wa Kielektroniki kwa wananchi waliokuwa wakipata  huduma katika ofisi hiyo, katika maonesho ya 41 biashara ya Kimataifa katika viwanja vya sabasaba
 Maafisa wa Global Education Link wakiendelea kutoa huduma katika maonesho ya 41 biashara ya Kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli aridhia maombi ya kustaafu mapema kwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Prof. John Ruhangisa

MAKAMU WA RAIS MHE SAMIA SULUHU HASSAN ATEMBELEA MAONYESHO YA SABASABA DSM

AGPAHI YAKUTANA NA WAGANGA WAKUU WA MIKOA MJINI DODOMA

$
0
0
Shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi nchini Tanzania limekutana na waganga wakuu wa mikoa saba ambako linatekeleza shughuli zake.

AGPAHI imefanya mkutano na waganga wakuu wa mikoa ya Shinyanga,Mwanza,Geita,Simiyu,Tanga,Mara na Manyara siku ya Jumatano, Julai 5,2017 katika ukumbi wa Morena Hotel mjini Dodoma. 

 
Akizungumza katika mkutano huo,Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa alisema lengo ni kujadiliana kuhusu maendeleo, mafanikio na changamoto za miradi na kupanga mikakati ya utekelezaji wa miradi katika mwaka ujao wa miradi.

Dk. Mwakyusa alisema lengo la AGPAHI ni kuboresha afya ya watoto na familia kwa kutokomeza VVU na Ukimwi na kutoa huduma za kinga,matunzo na tiba kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya ikiwemo serikali ili kubuni na kutekeleza mikakati muafaka kwa afya bora.

“Shirika hili lilianzishwa mwaka 2011,kuanzia kipindi hicho tulikuwa tunafanya kazi zetu katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu, lakini kuanzia Oktoba 2016 mikoa ya Mara,Geita,Tanga na Mwanza iliongezeka (tukitekeleza miradi ya Ukimwi) na mkoa wa Manyara uliongezeka ambako tunatekeleza mradi wa kifua kikuu”,alisema Dk. Mwakyusa.

“Tumekuwa tukifanya kazi zetu kwa kushirikiana kwa ukaribu kabisa na serikali. Na wafadhili wetu wakuu ni Watu wa Marekani kupitia shirika la Centres for Disease Control and Preventation (CDC),mfuko wa kusaidia Watoto wenye VVU kwa hisani ya Watu wa Uingereza (CIFF) na Shirika la Development Aid From People to People (ADPP - Mozambique)”, aliongeza Dk. Mwakyusa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa akielezea kuhusu miradi ya Ukimwi inayotekelezwa na shirika hilo katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania. 

 
Meneja Mawasiliano kutoka AGPAHI, Jane Shuma akiwakaribisha waganga wakuu wa mikoa katika ukumbi wa Morena Hotel mjini Dodoma kwa ajili ya kushiriki mkutano ulioandaliwa na shirika hilo. 


Waganga wakuu wa mikoa saba wakimsikiliza Dk. Mwakyusa.


TECNO YAAMSHA DUDE KWA BEI CHEE SABASABA

$
0
0

Inline image 1




2
KWA msimu huu wa maonyesho ya Sabasaba, kampuni maarufu ya simu za mkononi nchini Tanzania, Tecno, inazidi kuendelea kuwajali wateja wake bila ya kujali vipato vyao.
Tecno imetambulisha sokoni simu mpya maarufu kama TECNO DUDE, simu hiyo imekuja kama mkombozi kwa Watanzania wenye kipato cha chini waliokuwa hawana uwezo wa kumiliki simu zenye teknolojia ya kisasa ya kimtandao na zenye kasi ta 4G (fourth generation).
1 (2)
Tecno imekuletea simu hiyo ambayo utaipata kwa Sh 180,000. Simu hiyo ambayo mbali na kupatikana madukani mbalimbali hapa nchini, pia ukifika kwenye Viwanja vya SabaSaba inapatikana.

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof.Ibrahim Hamis Juma atembelea maonesho ya sabasaba

$
0
0
 Mkurugenzi Msaidizi wa TEHAMA wa Mahakama ya Tanzania, Machumu Essaba akimuelezea Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof.Ibrahim Hamis Juma kuhusu Mfumo wa Takwimu za Mahakama (JSDS)alipotembelea Banda la Mahakama hivi karibuni katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Sabasaba.

 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Majaji, watumishi wa Mahakama pamoja na watumishi kutoka Taasisi ambazo ni wadau wa Mahakamawanaoshiriki kwenye Maenesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Sabasaba. 

 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akipata maelezo kuhusu utengenezaji wa samani za nyumbani na maofisini alipotembelea banda la Maonesho la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelesa jijini Dar es salaam.

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitembelea sehemu mbalimbali katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam. Aliyefuatana naye ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Tanzania (TANTRADE), Bw. Edwin  Rutageruka. 

MATOKEO CHANYA KATIKA ELIMU

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 06.07.2017

TANZANIA YATEULIWA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA 37 WA SHIRIKA LA MAKAZI AFRIKA 2018

$
0
0

● Kunufaika na kuvutia  watalii
● Ni mkutano unaovuta wawekezaji na wafanyabiashara
● Mkutano huo huhuzisha nchi wanachama 44 wa Afrika

Na Muungano Saguya, Victoria Falls, Zimbabwe
Tanzania imeteuliwa kwa kauli moja na wajumbe wa Mkutano wa 36 wa Makazi Afrika(Shelter Afrique) kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 37 ambao utafanyika mwezi Julai 2018 Jijini Dar es Salaam. 


Mkutano huo ambao una wanachama kutoka nchi 44 za Afrika walikutana katika Mji wa Kitalii wa Victoria Falls nchini Zimbabwe ili kujadili changamoto za hali ya makazi kwa watu wa nchi hizo ili kuona namna ya kutatua changamoto hizo kwa kutumia uzoefu wa kila nchi mwanachama.


 Aidha, katika Mkutano huo ambapo Tanzania iliwakilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu, kwa niaba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi, iliteuliwa kuwa Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano huo wa 36.
Mambo mbalimbali yalijadiliwa na kukubalika ikiwa ni pamoja na kuondoa changamoto ya Rasilimali Fedha  inayozikabili nchi nyingi wanachama wa Umoja huo na kushindwa kuwapatia wananchi wa Afrika makazi bora na nafuu. Katika kuondoa changamoto hiyo Mkutano huo umeazimia kuongeza Daraja C la wanachama wa umoja huo ambalo litahusisha mashirika, taasisi za kifedha  na nchi za nje ya bara la Afrika ili kupata fedha au kuwa na ubia wa pamoja wa kusaidia kuwapatia wananchi wan chi wanachama makazi bora na nafuu. Kadhalika, nchi hizo za kiafrika zimekubaliana kuhakikisha kila nchi inakamilisha michango yake inayodaiwa ili kuwezesha umoja huo kuendelea kusaidia mikopo kwa nchi wanachama ya kugharamia miradi ya ujenzi wa nyumba. Kundi A la Umoja huo huhusisha nchi 44 za Afrika na Kundi B huhusisha Benki ya Afrika(ADB).
Kuteuliwa kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 37 kumechangiwa na Wajumbe wengi kufurahishwa na mabadiliko yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano na Rais Dkt John Pombe Magufuli amekuwa gumzo kubwa kwa Wajumbe wa Mkutano huo wa Makazi kila walizungumzia changamoto zinazolikabili Bara la Afrika.
Faida zitakazopatikana katika Mkutano huo kufanyika nchini Tanzania ni pamoja na kukuza utalii wa Tanzania kwa Wajumbe hao kuelezwa fursa za utalii na kujionea kazi mbalimbali za wajasiriamali hususan wa sekta ya nyumba ambao hualikwa katika Mkutano huo. Aidha, ni fursa kubwa kwa nchi kujitangaza kibiashara na kuvutia wawekezaji kutoka Bara la Afrika.
Tanzania ilijiunga na Shelter Afrique mwaka 2003 na Mkutano wa 32 wa Shelter - Afrique uliofanyika N’djamena, Chad mwaka 2013 ulipitisha Azimio Namba GM/2013/005 la kuongeza Hisa kwa kila nchi mwanachama kwa lengo la kukuza mtaji wa kampuni hiyo na kuiwezesha kuweka nguvu zaidi katika masuala ya uendelezaji nyumba barani Afrika.
Shirika la Nyumba la Taifa limenufaika na mtaji huo ambapo mwaka 2002 lilikopeshwa Dola za Kimarekani 1.5 milioni na kuzitumia kujenga nyumba 212 eneo la Boko Jijini Dar es Salaam na mwaka 2011 lilikopeshwa fedha kiasi cha Dola za Kimarekani 14.5 milioni mkopo uliotakiwa kurejeshwa katika kipindi cha miaka 10 na mkopo huo ulitumika kujenga nyumba za gharama nafuu zipatazo 558 katika maeneo mbalimbali nchini. Pamoja na kuikopesha NHC, Shelter Afrique imewekeza kiasi cha Dola za Kimarekani 27,500,000/= katika miradi mbalimbali ya ujenzi wa nyumba nchini Tanzania.
Mkutano huo wa 36 umefanyika katika Mji wa Kitalii wa Victoria Falls nchini Zimbabwe zamani ikiitwa Southern Rhodesia, ambapo wajumbe walipata pia fursa ya kutembezwa kwenye vivutio vya kitalii vilivyopo katika Mji huo unaopakana na nchi ya Zambia, zamani ikiitwa Nothern Rhodesia.

MASHAIRI YA NASRI IBRAHIM: "EWE MOYO"

TRA YAENDELEA KUWABAMBA WAFANYABIASHARA WASIOTOA RISITI ZA MACHINE ZA KIELEKRONIKI

$
0
0
Meneja Elimu kwa Mlipa kodi wa Mamlaka ya mapato Nchini (TRA), Bi. Dayana Masala ameongoza operesheni ya kuwakamata wafanyabiashara wa vituo vya mafuta wanaohudumia pasipo kutoa risiti na kusababishia serikali kutokusanya mapato stahiki kwa huduma wanazotoa  jijini Dar es Salaam. 
Operesheni hiyo ilifanyika mapema jijini humo na baadhi ya vituo vya mafuta kubambwa baadhi ya watoa huduma ya uuzaji wa nishati ya petroli na diseli wakitoa huduma ya kwa vyombo vya moto bila kutoa risiti kwa wateja jambo ambalo ni kinyume cha sheria za nchi jambo linalosababishia serikali kupoteza mapato. 
Bi Msala amewaonya wafanyabiashara wenye tabia ya kutopenda kuwapa wateja risiti kwani kwa kufanya hivyo watalazimika watakapobainika watalipa faini ya shilingi milioni nne na nusu. Pia amewasisitiza wananchi kudai risiti wanapopata huduma za bidhaa mbalimbali kwani kwa kutokufanya hivyo pia ni kosa na wakikutwa wamenunua bidhaa bila kudai risiti watalazimika kulipa fidia ya shilingi milioni moja na nusu.
Imeandaliwa na Robert Okanda Blog


Introducing Wimbo Mpya wa Fatma

MAGAZETI YA IJUMAA LEO JULY 7,2017

KIONGOZI MKUU WA KANISA LA LIBERATION CITY MINISTRIES AND MIRACLES DUNIAI NABII DKT. CHRIS OKAFOR APATA MAPOKEZI MAKUBWA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Kiongozi Mkuu wa Liberation City Ministries and Miracles Duniani Dkt. Chris Okafor akipokea shada ya maua baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jana tayari kwa Kongamano kubwa la WAKATI WA UTULIZO 2017 
 Kiongozi Mkuu wa Liberation City Ministries and Miracles Duniani Dkt. Chris Okafor akilakiwa kwa shangwe na waumini baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jana tayari kwa Kongamano kubwa la WAKATI WA UTULIZO 2017 

MZUNGU KICHAA ON "TOGETHER AS ONE" TOUR 2017!

$
0
0

MZUNGU KICHAA, the famous  Danish singer and musician born in Denmark but grew up in Tanzania, has started his whirlwind tour on the 6th of July with concerts in Dar es salaam and Zanzibar, and he hopes to see you all there! 

 He will also be launching his new video "TOGETHER AS ONE" featuring Bongo Fleva King Juma Nature and Karen Mukupa.... Says Mzungu Kichaa; "Who knows, they might even join me on stage. I'm crossing my fingers ✌ and guarantee  that you WILL enjoy".

CHECK OUT HIS ITINERARY UP THERE↑

MAONESHO YA SABASABA 2017; PSPF YAWAAMBIA WANACHAMA NA WANANCHI WAENDELEE KUTEMBELEA BANDA LAO ILI KUPATA HUDUMA ZOTE WANAZOHITAJI

$
0
0


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MFUKO wa Pensheni wa PSPF umewaahidi wananchi wanaojitokeza kwenye banda la Mfuko huo, lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu kama Sabasaba, kuwa wataendelea kupatiwa huduma zote kama ambazo wamezoea kuzipata kwenye ofisi za Mfuko huo kote nchini.

Ahadi hiyo imetolewa leo Julai 6, 2017 na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi, baada ya kuona umati mkubwa wa wananchi waliofika kupatiwa huduma mbalimbali zikiwemo zile za wanachama kujua michango yao, wananchi kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari, (PSS), ambapo mtu aliyejiunga na mpango huo husajiliwa na kupatiwa kitambulisho papo kwa hapo.

"Leo idadi ya watu imeongezeka sana bila shaka wamevutiwa na huduma zetu na tunawahakikishia tutaendelea kutoa huduma bora na za haraka hadi tarehe ambayo maonesho haya yatafikia kilele kama alivyoagiza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa siku za maonesho zimeongezeka hadi Julai 13, 2017 badala ya Julai 8." Alifafanua Bw. Njaidi.

Idadi kubwa ya wananchi waliofika kwenye banda hilo ni wale wajasiriamali ambao wengi wamejiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari ambapo moja ya faida kubwa ya kujiunga na mpango huo ni kupata fao la bima ya afya inayomuwezesha mwanachama kupatiwa matibabu yeye na wategemezi wake kwenye hospitali zilizoaishwa kote nchini.

Win-God Simon, (kushoto), Afisa wa PSPF akiwahudumia wananchi na wanachama wa Mfuko huo waliotembelea banda la PSPF leo Julai 6, 2017

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw.Erick Shitindi(kulia), akipokea vipeperushi vyenye taarifa mbalimbali za Mfuko wa Pensehni wa PSPF kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi wakati alipotembelea banda la Mfuko huo leo Julai 6, 2017.

Wananchi waliofurika wkenye banda la PSPF, leo Julai 6, 2017
Bw. Costa wa PSPF, (kushoto), akifafanua jambo kwa wananchi hawa waliofika kwenye banda la PSPF.

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images