Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110180 articles
Browse latest View live

TTB yageukia utalii wa kimichezo na burudani

$
0
0
BODI ya Utalii Tanzania (TTB), imeaamua kujikita kwenye utalii wa michezo na sanaa ili kuitangaza zaidi Tanzania kimataifa kupitia sekta hiyo inayojumuisha watu wengi ulimwenguni.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Bandari ya Dar es Salaam wakati akiwapokea watalii zaidi ya 50 raia wa Korea Kusini, Ofisa Habari Mkuu wa TTB, Bwana Geofrey  Tengeneza alisema imezoeleka watalii ni wale wanaokuja tu nchini na kutembelea maeneo ya vivutio na kuondoka, lakini hata wasanii na wanamichezo ni watalii wazuri wanaovutia raia wengine kutoka mataifa yao kuja Tanzania.
“Tumeamua kutumia mbinu hii ya kukaribisha watalii wa kimichezo na burudani kwa sababu kupitia wao watu wanaowafuatilia katika mataifa waliyotoka watavutiwa na Tanzania. Tumepoke wachezaji wa Haleluyah kutoka Korea Kusini. Wamewasili Juni 28 kupitia Zanzibar ambako waliweka kituo kwa wiki moja wakacheza mechi mbili na timu ya soka Polisi Zanzibar na Jang’ombe.
“Katika soko hili la Korea Kusini ni miongoni mwa mataifa tuliyoweka juhudi kubwa kupata watalii ikiwemo na China kutokana na idadi ya watu waliokuwepo,” alisema Bw. Tengeneza na kubainisha:
“Kazi yetu kubwa ni kutazama na kubuni mbinu za kuitangaza nchi yetu, wageni hawa zaidi ya 50 watakuwepo hapa kwa wiki moja, watakwenda Mikumi kisha Julai 8 watacheza mechi ya kirafiki na Yanga katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.”
Akizungumzia ujio wao Kocha Mkuu wa Hallelujah FC, Bwana LEE Young Moo alisema wapo hapa kwa ajili ya mechi za kujipima nguvu lakini pia wamevutiwa na utamaduni wa watanzania kutokana na sifa walizopata kutoka kwa watu waliotembelea taifa hili.
“Nafurahi kuwa hapa Tanzania tunataka kucheza na timu za Tanzania ikiwemo Yanga, tunataka kubadili utamaduni na kufanya kazi na wanamichezo wa hapa ili tuwe na uhusiano mzuri. Tumesika mambo mengi kuhusu Tanzania, kumbuka kuna mataifa mengi Afrika lakini utamaduni na watu wa taifa hili vimetuvutia sana,” alisema Bw. LEE.
Kwa upande wake daktari wa timu hiyo inayotajwa kuwa timu ya kwanza soka la kiushindani kuanzishwa Korea Kusini mwaka 1980 ambayo pia inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini humo, Bwana Benjamin Chang amesema anaamini wachezaji wake watakuwa na afya njema kutokana na hali ya hewa tulivu iliyopo Tanzania.
“Hali ya hewa ni nzuri, fukwe za kuvutia na naamini tutakuwa na wakati mzuri katika mbuga za wanyama. Tutakuwa hapa kwa wiki kadhaa tumekuja wachezaji 20 pamoja na maofisa wengine 30 jumla tupo 50, tumeona mambo mengi tuliyokuwa tukiyasikia tu,” alisema Bw. Chang.
Itakumbukwa miezi miwili iliyopita wasanii wa filamu zaidi ya 100 kutoka China walikuja nchini kufanya shughuli za kisanii na kutembelea vivutio ikiwemo fukwe za Zanzibar na mbuga za wanyama ikiwemo Serengeti.
Vilevile wiki iliyopita TTB ilipokea wachezaji 60 wa soka la wanawake kutoka mataifa 20 duniani walikuja kupanda Mlima Kilimanjaro na kucheza soka juu ya kilele cha mlima huo na kuitangaza Tanzania katika ulimwengu wa soka la wanawake.
 Picha ya pamoja ikionyesha kikosi cha timu ya soka ya Hallelujah FC inayoshirki ligi kuu ya Korea Kusini walipowasili Bandari ya Dar es Salaam wakitokea Zanzibar, timu hiyo ni sehemu ya watalii 50 waliotembelea nchini kuangalia vivutio vya kitalii na kucheza mechi za kirafiki ikiwemo na timu ya Yanga ya Dar es Salaam.
 Miongoni mwa watalii kutoka Korea Kaskazini waliowaili na kikosi cha timu ya soka ya Hallelujah FC, akicheza ngoma ya asili na mmoja wa wachezji wa kikundi cha Wanne Star katika bandari ya Dar es Salaam walipopokelewa na maofisa wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) jana. Watalii hao watakuwepo nchni kwa wiki mbili kutembelea mbuga za wanyama na kucheza mechi za kirafiki ikiwemo na timu ya Yanga.
Mwanakikundi kutoka kikundi cha ngoma za asili cha Wanne Star, akicheza na chatu mbele ya watalii kutoka Korea Kusini walipowasili Bandari ya Dar es Salaam kutokea Zanzibar jana. Watalii hao waliopokelewa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) watakuwepo nchini kwa wiki mbili kutembelea mbuga za wanyama na kucheza mechi za kirafiki ikiwemo na timu ya Yanga.
Mwisho

VICE PRESIDENT SAMIA SULUHU HASSAN OPENS THE SADC DEVELOPMENT FINANCE INSTITUTIONS NETWORK CHIEF EXECUTIVE OFFICERS' FORUM IN DAR

$
0
0
 K-VIS BLOG/Khalfan Said
 Tanzania Vice President Her Excellency Samia Suluhu Hassan today opened the SADC Development Finance Institutions Network Chief Executive Officer's Forum at Julius Nyerere Convention Centre in Dar es Salaam.
The  Forum will focus on the theme, "Towards Industrialization for Sustainable and Inclusive Development-Role of DFIs in SADC." an official said adding that this was in recognition of prioritisation of industrialisat
ion by SADC-Heads os State as a key element towards the achievement of sustainable economic growth and development in the SADC region and enhancing  the welfare of it's peoples. The Official further stated that  the successful  implementation of the regional industrialisation strategy will require massive  investment across verious industrial sectors.

Vice President Her Excellency Samia Suluhu Hassan, (L), shakes hands with the Chief Executive Officer SADC Development Finance Resource Centre, Mr. Stuart Kufeni, as she leaves the Convention Centre. Cenctre in  Chair of the SADC DFI Network and Group Managing Director for FINCORP in Swaziland, Mr.Dumisani Msibi
Chairperson of the Board of Directors of Tanzania Agricultural Development Bank, (TADB), Mrs.Rosebud V.Kurwijila, makes a vote of thanks
 Tanzania Vice President Her Excellency Samia Suluhu Hassan, makes her opening remarks during the SADC Development Finance Institutions Network Chief Executive Officer's Forum at Julius Nyerere Convention Centre in Dar es Salaam Thursday July 6, 2017.
 Chair of the SADC DFI Network and Group Managing Director for FINCORP in Swaziland, Mr.Dumisani Msibi

 Vice President Hon. Samia Suluhu Hassan, (L), shakes hands with the Chair of the SADC DFI Network and Group Managing Director for FINCORP in Swaziland, Mr.Dumisani Msibi, after she had delivered her opening remarks.


Tanzania’s Central Bank, Deputy Governor, Dr, Bernard Y Kibese, (L), shakes hands with the Managing Director, Tanzania’s Export Processing Zones Authority, Col. (rtd), Joseph Simbakalia, as the Acting Managing Director of Tanzania Agricultural Development Bank, (TADVB), Mr. Francis Assenga, looks on, during the SADC Development Finance Institutions Network Chief Executive Officer’s Forum, at Julius Nyerere Convention Centre in Dar es Salaam.

Rais wa Zanzibar Dk.Shein aelekea Uingereza kwa ziara maalumu ya wiki mbili leo

$
0
0
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (kushoto) alipokuwa akiagana na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud alipokuwa akiondoka chini leo akifuatana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)  kuelekea Nchini Uingereza kwa ziara maalum ya wiki mbili
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na 
​Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi pamoja ​
Viongozi mbali mbali 
​ 
 alipokuwa akiondoka 
​n
chini leo na Ujumbe wake kuelekea Nchini Uingereza kwa ziara 
​maalum 
ya wiki
​ mbili

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali alipokuwa akiondoka nchini leo na Ujumbe wake kuelekea Nchini Uingereza kwa ziara maalum  ya wiki mbili. Picha na IKULU

7 of 9 Print all In new window MASHEHA WAPYA WAAPISHWA ZANZIBAR

$
0
0
 Baadhi ya Masheha walioteuliwa kushika nafasi hizo katika Wilaya mbalimbali za Mjini Magharibi wakiwa wanasubiri kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud hafla iliofanyika Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni mjini Unguja.
 Baadhi ya Masheha walioteuliwa kushika nafasi hizo katika Wilaya mbalimbali za Mjini Magharibi wakiwa wanasubiri kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud hafla iliofanyika Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni mjini Unguja.
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud kushoto akimuapisha ndugu Elvis Victor Luanda kuwa sheha wa shehia ya Binti Amrani katika hafla ya kuwaapisha masheha  iliofanyika Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni mjini Unguja.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud kushoto akimuapisha ndugu Ali Silima Shauri  kuwa sheha wa shehia ya Mkele katika hafla ya kuwaapisha masheha  iliofanyika Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni mjini Unguja. PICHA NA YUSSUF SIAMI/MAELEZO ZANZIBAR

Mahojiano maalumu kuhusu Maana Ya Utakatishaji Fedha

Wizara Ya Ardhi Yahamia rasmi Dodoma

Usaili wa kuwasaka warembo wa Miss Grand Tanzania wiki ijayo

$
0
0
Usaili wa kuwatafuta washiriki wa mashindano ya kumtafuta mrembo wa Miss Grand Tanzania utafanyika Julai 10, mwaka huu katika ukumbi wa Dar es salaam Convention Centre, jijini Dar es Salaam.

Zoezi za usaili litakalosimamiwa na wadau wa urembo nchini litaanza saa 4.00 asubuhi na kufikia tamati saa 11.00 jioni.

Mratibu wa mashindano hayo nchini Abraham Mahimbo amewataka warembo wenye vigezo kuichangamkia fursa hiyo kwani ni mashindano yanayokuja kuleta mapinduzi katika fani ya urembo nchini.

Mahimbo amesema mashindano ya Miss Grand Tanzania ambayo yatakuwa chini ya Miss Grand International yanakuja kuleta mapinduzi na kuyapa heshima mashindano ya urembo nchini.

“Warembo wanaojiamini na waliotayari kwa mapinduzi ninawakaribisha katika usaili kwani nafasi hii ni adhimu ambayo hutokea mara moja tu katika maisha,” alisema Mahimbo.

Amevitaja vigezo vya kushiriki mashindano hayo ni umri wa kati ya miaka 18-27, urefu sentimita 168, ambaye hajaoelwa, hajawahi kupata mtoto, ajue utamaduni na matukio yanayoendelea nchini, kisiasa, uchumi, mazingira, matatizo, awe na tabia njema na hajawahi kujihusisha na vitendo vya aibu kama biashara ya ngono.

Alisema siku ya usaili washiriki watatakiwa kuwasilisha vyeti vya kuzaliwa na fomu zinapatikana Swahili Studios- Magomeni, Merry Bright Beauty Point-Tabata, City Star Boutique- Namanga na Infinity Lounge Mbezi Beach.

“Kwa mawasiliano kuhusu ushiriki wa mashindano hayo wawasiliane nami kwa namba ya simu  0717 653 653.”

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZITAKA TAASISI ZA MAENDELEO YA FEDHA NA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA (SADC),KUIMARISHA USHIRIKIANO

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amezitaka Taasisi za Maendeleo ya Fedha za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuimarisha ushirikiano na kubadilisha uzoefu katika utendaji wao wa kazi ili kuhakikisha kazi zinazofanywa na Taasisi hizo zinakuwa na manufaa kwa wananchi wa Jumuiya hiyo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati anafungua Mkutano wa mwaka wa Taasisi za Maendeleo ya Fedha za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kama taasisi hizo za kifedha zitafanya kazi kwa kuzingatia ubunifu na uaminifu ana uhakika kuwa malengo waliyojiwekeza yatafikiwa kwa wakati hasa katika uwekezaji katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ameeleza kuwa bado upo umuhimu mkubwa kwa Taasisi hizo za Kifedha katika nchi za SADC kuendelea kutumia ipasavyo wataalamu wa vyuo vikuu na taasisi za utafiti kwa lengo la kukuza uchumi unaotokana na ujuzi kupitia ubunifu.

Makamu wa Rais pia amehimiza nchi wanachama wa SADC kupitia taasisi za kifedha za nchi hizo kushirikiana katika kuchangia fedha katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo katika nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji amesema anaimani kubwa kuwa mkutano utasaidia kwa kiasi kikubwa uimarishaji wa utendaji wa kazi katika Taasisi hizo za Maendeleo ya Fedha katika nchi za SADC.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji.


WCS YATOA MSAADAWA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 936 KWA UHIFADHI WA WANYAMAPORI

$
0
0
Katibu mkuu (mwenye koti nyeusi) akikata utepe wa uzinduzi wa ofisi ya pori la piti kulia kwake ni kaimu mkurugenzi mkuu wa tawa bw.martin loibooki na kushoto nimeneja wa pori la rukwa/piti bw.ambrose mungo’ng’o .

Na Mwandishi wetu Songwe

Taasisi ya Kimataifa ya kijamii ya uhifadhi wa wanyamapori ya World Concervation Society- WCS imetoa msaada wa zaidi ya shilingi milioni 936 kwa mapori ya akiba ya Lukwati- Piti ambazo zimetumika kujenga jengo la kisasa la ofisi, ununuzi wa magari matatu ya doria na kuendesha mafunzo ya askari wa wanyamapori wa mapori hayo yaliyoko mkoani Songwe.

Akiongea katika halfa ya kukabidhi miradi hiyo kwa serikali ya Tanzania, Mkurugenzi wa WCS Aaron Nicholaus amesema taaisisi hiyo inajivunia kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuendeleza shughuli za uhifadhi wa wanayamapori wakiwemo tembo ambao ni maliasili muhimu kitaifa na kimataifa ambapo shirika la misaada la watu wa Marekani USAID nalo ni mdau mkubwa katika ufadhili huo.
katibu mkuu akipokea magari 3 aina ya toyota l/cruiser pickup toka kwa mratibu wa mradi wa cws bw. Aaron nicholaus.

Bwana Nicholaus alisema msaada huo umetilia mkazo suala la mafuzo ambayo yatawaongezea askari ujuzi na weledi wa kukabiliana na majangili ambao wamekuwa wakiua tembo na wanyamapori wengine kwa maslahi yao binafsi na kusababisha hasara kwa serikali ambayo inawategemea wanyamapori kwa maendeleo ya jamii na taifa.

“Tunapofikiria uhifadhi, tuangalie pia masuala ya mapito ya wanyamapori kama tembo ambayo yamekuwa yakitoweka kutokana na kuongezeka kwa shughuli za binadamu na hivyo kuathiri uhifadhi maana tembo huhitaji eneo kubwa kwa malisho” alisme abwana Nicholaus.

Taarifa ya miradi hiyo iliyotolewa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi ilieleza kuwa miradi hiyo ina thamani kubwa kwa uhifadhi wa mapori hayo yenye ukubwa wa zaidi ya kilomita za mraba 6,119 ambayo yanapakana na Hifadhi ya taifa ya Ruaha na pori la akiba la Rungwa.
Katibu mkuu akiongea na baadhi ya kikosi cha askari waliyopata mafunzo ya kukabiliana na ujangili. 

Meneja wa Mapori ya Lukwati Piti Bwana Alphonce Ambroce Mung’ong’o akitoa ufafanuzo na mchanganuo wa gharama za miradi hiyo alisema jengo la kisasa la ofisi limegharimu zaidi ya shilingi milioni 227, magari matatu kwaajili ya doria yana thamni ya dola 255,000 za kimarekani boti na mfumo wa radio call una thamani ya zaidi ya shilingi milioni 234.

NSSF YAZINDUA MIKOPO KWA WANACHAMA WAKE KUPITIA BENKI YA AZANIA

$
0
0
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lazindua utoaji wa mikopo kwa SACCOS na kupitia Benki ya Azania. Mikopo hii ni mahususi kwa ajili ya kuwasaidia wanachama wa NSSF kuweza kujikwamua kiuchumi hususan kuweza kutekeleza sera ya Viwanda ya awamu ya tano kwa kutumia mikopo hiyo kufungua Viwanda vidogo vidogo.

Mikopo hiyo itatolewa hadi kiwango cha juu kisichozidi fedha taslimu za kitanzania 300,000,000 kwa SACCOS au AMCOS. Vile vile mwanachama wa NSSF anaweza kukopa hadi shilingi 20,000,000 kupitia SACCOS au AMCOS aliyojiunga nayo na mikopo hiyo italipwa ndani ya miezi 24.

Alipokuwa akizindua mpango huo, Makamu wa Rais Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan aliwaasa wanachama wa NSSF kuchangamkia fursa hiyo ya mikopo na kuwaomba waitumie mikopo hiyo kama chachu ya kujikwamua kiuchumi na kuwaasa kuwa na nidhamu ya hali ya juu katika kuendeleza biashara zao.

Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa mpango huo Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof Godius Kahyarara alisema SACCOS na AMCOS zote zitakaoomba mikopo hiyo ni lazima ziwasilishe taarifa sahihi za fedha zilizokaguliwa kwa miaka mitatu na kuhakikiwa na COASCO na mwanachama anaruhusiwa kukopa hadi mara tatu ya Amana zake alizijiwekea ndani ya SACCOS au AMCOS ambayo yeye ni mwanachama.
Makamu wa Rais wa Jammhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mikopo ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Kupitia Benki ya Azania alipotembelea banda la NSSF katika maonesho ya Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu Nyerere.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kuhusu dawa ya kuangamiza viuadudu vinavyosababisha ugonjwa wa malaria alipotembelea banda la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika maonesho ya Sabasaba, viwanja vya Mwalimu Nyerere. NSSF ni mdau wa kiwanda hicho cha Viuadudu kilichopo mkoani Pwani.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara akitoa ufafanuzi kuhusu mikopo ya NSSF kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe Mama Samia Suluhu Hassan kabla ya  kuzindua rasmi mikopo hiyo katika viwanja vya Sabasaba.

UCHAGUZI TWFA KUFANYIKA DAR ES SALAAM

$
0
0
Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu kwa Wanawake (TWFA), sasa utafanyika Dar es Salaam badala ya Dodoma na Morogoro - mikoa iliyotangazwa awali.

Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Msomi Wakili George Mushumba, amesema kwamba taratibu zote zimekamilika na kwamba siku ya uchaguzi ni Jumamosi Julai 8, mwaka huu.

Wakili Mushumba ametoa wito kwa wajumbe wote kufika Dar es Salaam Ijumaa Julai 7, mwaka huu kwa ajili ya kufahamu tararibu za awali za uchaguzi.

Tayari Kamati ya Mushumba ilitangaza majina ya wagombea 11 waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu.

Majina ambayo yamepitishwa ni Amina Karuma, Rose Kisiwa, Somoe Ng’itu, Theresia Mung’ong’o, Hilda Masanche, Salma Wajeso, Zena Chande, Triphonia Temba, Mwamvita Kiyogoma, Jasmine Soudy na Chichi Mwidege.

Nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji.

FOMU ZA KUWANIA UONGOZI TAFCA

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA), Ramadhani Mambosasa ametoa wito wa walimu wa soka kujitokeza kwa wingi kuchukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi - ngazi ya taifa.

Mambosasa ametoa wito huo ikiwa zimebaki siku mbili tu kwa mujibu wa kanuni kukamilisha hatua hiyo. Fomu hizo zinazopatikana ofisi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam, zilianza kutolewa juzi Julai 3, 2017 na mwisho ni Julai 7, mwaka huu.

“Wanaojitokeza wachache. Wengine wanadai hawafahamu zilizo ofisi za DRFA. Tunatoa wito wajitokeze kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali,” amesema Mambosasa.

Nafasi zilizotangazwa kuwaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina ambao fomu zao zinapatikana kwa Sh 200,000 wakati nafasi za wajumbe wa Mkutano Mkuu TFF na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji fomu zao zinapatikana kwa Sh 100,000.

UCHAGUZI CHAMA CHA WATAALAMU WA TIBA ZA MICHEZO

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Wataalamu wa Tiba za Michezo (TASMA), kimetangaza Uchaguzi Mkuu wa chama hicho kwamba utafanyika Agosti 5, mwaka huu katika Ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam.

“Wanachama wote wanakaribishwa kushiriki kwa namna moja au nyingine katika zoezi hili muhimu sana,” amesema Mwenyekiti wa kamati hiyo, Leslie Liunda alipokuwa anatangaza ramani ya mchakato wa uchaguzi huo leo Alhamis Julai 06, 2017.

Amesema: Mwanachama ye yote anayependa kukiongoza chama hiki anaombwa kuchukua fomu katika ofisi za Olimpiki Maalumu, zilizoko jirani na Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kwa ajili ya kugombea nafasi anayoona kuwa anaweza kuimudu.”

Nafasi zinazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina ambao fomu zao zinapatikana kwa Sh 200,000 wakati nafasi za wajumbe wa Mkutano Mkuu TFF na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji fomu zao zinapatikana kwa Sh 100,000.

MAMLAKA YA UDHIBITI NA MANUNUZI YADHAMIRIA KATIKA KUBORESHA MANUNUZI YA ZABUNI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MAMLAKA  wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA)imejizatiti katika kufanya marekebisho ya sheria ikiwa ni katika kuboresha zaidi manunuzi ya zabuni kwa serikali.

Akizungumza wakati akitembelea banda la PPRA lililopo kwenye jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dkt Laurent Shirima amesema kuwa maboresho hayo yatalenga katika sehemu tano ambazo zitaboresha manunuzi ya zabuni katika nyanja mbalimbali.

Dkt Shirima amesema kuwa wataboresha manunuzi katika kupunguza gharama za ununuaji wa zabuni, serikali kununua kwa bei za sokoni wakimaanisha bei halisi ya zabuni pia watatoa upendeleo kwa makampuni ya ndani ikiwemo makundi maalumu kama vile wanawake, wazee na vijana.

Ameongezea kuwa, katika maboresho mengine yatakuwa ni katika kuendeleza viwanda kama serikali ya awamu ya tano inavyosisitiza ukuaji wa viwanda huku PPRA ikiangalia zaidi wataalamu wa manunuzi kutoka ndani pia wapo katika hatua za mwisho za kuhamia katika mfumo wa kieletroniki wa ununuzi wa zabuni.

PPRA ni mamlaka inayohusiana na udhibiti wa manunuzi ya Umma ambapo kupitia kwa Mtendaji Mkuu Dkt Shirima amewaondoa hofu wananchi kuwa waiamini taasisi yao kwani mambo mengi ya msingi yameshawekwa wazi na fedha za umma zinahitaji uwajibikaji.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma  PPRA Dkt Laurent Shirima akizungumza na wanahabari wakati alipotembelea banda la Mamlaka wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma PPRA lililopo kwenye jengo la Wizara ya Fedha na Mipango na kuelezea namna wanavyojizatiti katika kuboresha ununuaji wa zabuni kwa serikali.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Dkt Laurent Shirima akimuhudumia mwananchi aliyetembelea banda lao na katika maadhimisho ya 41 ya Monesho ya kimataifa ya Sabasaba leo Jijini Dar es salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Dkt Laurent Shirima akipata maelezo kutoka kwa  mfanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa Taifa (PPF) wakati alipotembelea banda hilo lilipo katika Jengo la Wizara ya Fedha na Mipango  katika maadhimisho ya  41 ya Monesho ya kimataifa ya Sabasaba leo Jijini Dar es salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MWIJAGE:WATANZANIA PENDENI BIDHAA ZA NGOZI ZINAZOZALISHWA TANZANIA.

$
0
0
 .Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji , Charles Mwijage  akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Biashara na Uhusiano wa Kiwanda cha Bora  Sylivery  Buyaga (wa pili kulia)  juu ya kiwanda  hicho kinavyofanya kazi.jijini Dar es Salaam.
 .Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji , Charles Mwijage akionyesha ubora wa kiatu kinachotengenezwa na kiwanda cha Bora.jijini Dares Salaam.
Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji , Charles Mwijage akitembelea kiwanda cha Cha Bora ambacho kilibinafsishwa  na sasa kimeanza uzalishaji wa bidhaa ya ngozi utaokafanya kozi kupata soko.jijini Dar es Salaam.

UPDATE MSIBA WA MKONGWE WA MUZIKI MAREHEMU SHAABAN DEDE

$
0
0
Msiba upo nyumbani kwa marehemu Mtaa wa Congo na Msimbazi hapa Dar es salaam. Kwa mujibu wa mwanae Hamad Dede mazishi yatafanyika kesho saa saba katika makaburi ya Kisutu. 

Mwili utaswaliwa msikiti wa Makonde mtaa wa Msimbazi na Nyamwezi baada ya swalat Jumaa.

JUMIA TRAVEL YAZINDUA RIPOTI YA UTALII TANZANIA 2017 JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Na Dotto Mwaibale

 SERIKALI imeahidi kuendelea kuwashirikisha wadau mbalimbali katika sekta ya utalii hususani kwenye utungaji wa sera pamoja na kutengeneza mazingira mazuri ya uendeshwaji wa shughuli hizo nchini Tanzania.

Hayo yalisemwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Utalii Tanzania, Denis Simkoko katika hafla fupi ya uwasilishwaji wa Ripoti ya Utalii Tanzania kwa mwaka 2017 kutoka kwa Jumia Travel, kampuni inayojishughulisha na huduma za hoteli na usafiri mtandaoni tukio lililofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip katikati ya jiji la Dar es Salaam leo asubuhi.

“Bila shaka mafanikio tuliyonayo kwa sasa katika sekta ya Utalii nchini ni matokeo mazuri ya ushirikiano wa karibu baina ya serikali na wadau wengine. Shirikisho la Utalii Tanzania lipo kama daraja katika kuwaunganisha wadau mbalimbali wa sekta hii nchini kote na wizara husika yenye mamlaka kwa mujibu wa serikali. 

Huwa tunakutana na wadau wa utalii ambapo ni takribani vyama 12 nchini kote ndani ya kipindi maalumu cha mwaka na kujadili masuala mbalimbali yanayotukabili. Baada ya hapo sasa ndiyo sisi kama shirikisho huwa tunayawasilisha maoni hayo kwa serikali ili kupata ufumbuzi na pia kutengeneza fursa ambazo zitatukutanisha pamoja wadau katika meza moja ya majadiliano, “ alisema  Simkoko.  

“Mbali na mchango wetu kwenye kupendekeza maboresho ya kodi na sera, pia tunao watu wetu kwenye vikosi kazi na kamati mbalimbali ambao hufanya kazi kwa ukaribu na serikali. Ingawa bado kuna changamoto katika kupata ushirikiano kamili au wa moja kwa moja baina ya serikali na sekta binafsi, bado tunaimani juu ya mifumo thabiti na ya uwazi katika uandaaji na ufanyikaji wa mikutano, majadiliano na mafunzo. 
 Meneja Mkaazi wa Kampuni ya Jumia Travel Tanzania, Fatema Dharsee, akizungumza katika hafla fupi ya uwasilishwaji wa Ripoti ya Utalii Tanzania kwa mwaka 2017 kutoka katika kampuni hiyo inayojishughulisha na huduma za hoteli na usafiri mtandaoni tukio lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip katikati ya jiji la Dar es Salaam leo asubuhi.
 Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Geofrey Kijangwa akizungumza kwenye hafla hiyo.

Maofisa wa Shirikisho la Utalii Tanzania (TCT),  wakiwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kulia ni Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho hilo, Denis Simkoko, Meneja Mkuu wa Mauzo wa Hoteli ya Ramada Resort Dar es Salaam, Amina Kapya na Ofisa Tawala wa Chama cha Wamiliki wa Hoteli  Tanzania (HAT), Jeniffer Abel.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



Mkurugenzi wa kampuni ya Golden Shark Mining Ltd Kizimbani kwa tuhuma za kutapeli na kutakatisha zaidi ya bilioni nne.

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blog ya jamii.

Mkurugenzi wa kampuni ya Golden Shark Mining Ltd, Cuthbert Kishululi amepandishwa katika kizimbani cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu likiwemo la kutakatisha zaidi ya USD milioni mbili, ambazo ni sawa na zaidi ya bilioni nne

Kishululi (48) anayeishi Salasala, wamesomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Respicious Mwijage wa mahakama hiyo.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa serikali, Pius Hilla amesema, January 4 mwaka 2013 jijini Dar wa Salaam, mshtakiwa kwa nia ya kudanganya alitengeneza nyaraka ya uongo ambayo ni cheti cha kumbukumbu kuonyesha kuwa hajawahi kufanya uhalifu ( Non- Criminal Certificate) cha 17 August 2015.

Imedaiwa kuwa, cheti hicho kilikuwa na nia ya kuonyesha kuwa, kimetolewa na Munusco United Nations Organization Stabilization Mission in the Democratic Republic of Congo kwenda kwa M/S Delicore Metals Company Ltd, huku akijua kuwa siyo kweli.

Hilla ameendelea kudai kuwa, kati ya Julai Mosi na Agosti 30 mwaka juzi,mshtakiwa kwa nia ya kudanganya, alijipatia USD 2,405,000, ambazo ni zaidi ya milioni nne, kutoka Holism Group Ltd kwa uongo baada ya kujifanya angewapatia kilo 500 za dhahabu kutoka kwenye kampuni hiyo ya Holism kupitia kampuni yake ya Golden Shark Mining Ltd

Katika shtaka la tatu imdaiwa kuwa, kati ya Julai 22 na Agosti 27 mwaka juzi, mshtakiwa alitakatisha fedha hizo kwa kujihusisha kwenye muamala wa USD 2,405,000 na kuelekeza fedha hizo zipelekwe kwenye account namba 010095361111 iliyopo katika bank ya I and M bank kwa jina la Delicore Metals Kampuni.

Aidha imedaiwa kuwa, mshtakiwa alizitoa fedha hizo huku akijua kuwa ni zao la uhalifu wa kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.Hata hivyo, mshtakiwa amekana mashtaka yote, na amerudishwa rumande kwa kuwa shtaka la utakatishaji wa fedha halina dhamana.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika, imeahirishwa hadi Julai 14 ambapo upande wa mashtaka unatarajia kuongeza washtakiwa wengine katika kesi hiyo.

MKURUGENZI MKUU WA MFUKO WA PENSHENI LAPF BW.ELIUDI SANGA ATEMBELEA MAONESHO YA SABASABA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa Serika za Mitaa LAPF Bw. Eliudi Sanga akimsikiliza Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe wakati alipotembelea katika banda la Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwenye viwanja vya maonyesho ya biashara vya Mwalimu J.K. Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa Serika za Mitaa LAPF Bw. Eliudi Sanga akifurahia jambo na Varerian Mablanketi Mkurugenzi wa Huduma kwa wanachama LAPF kulia katikati ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe na kushoto ni mmoja wa wafanyakazi wa mfuko huo. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa Serika za Mitaa LAPF Bw. Eliudi Sanga akimsikiliza Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe wakati alipotembelea katika banda hilo kutoka kulia ni Rehema Mkamba Afisa Mawasiliano Mwandamizi LAPF na wa pili ni Varerian Mablanketi Mkrugenzi wa Huduma kwa wanachama LAPF. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa Serika za Mitaa LAPF Bw. Eliudi Sanga akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea banda hilo. 
Baadhi ya wananchi waliofika katika banda hilo wakiendelea kupata huduma kutoka kwa wafanyakazi wa mfuko huo. 

POLISI WAWASHAMBULIA NA KUWAUA WAHALIFU WAWILI IKWIRIRI.

$
0
0
 Na. Frank Geofray -Jeshi la Polisi. 

Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua wahalifu wawili ambao ni miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika Kanda maalumu ya Polisi Rufiji kufuatia operesheni kali inayoendelea katika Wilaya ya Mkuranga, Kibiti na Rufiji mkoani Pwani.

Akielezea tukio hilo, Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas alisema tukio hilo lilitokea siku ya Jumatano Julai 5 majira ya saa nne usiku katika msitu wa Ngomboroni kata ya Ikwiriri, Wilaya ya Ikwiriri Kanda maalumu ya Rufiji ambapo askari wa operesheni maalum wakiwa katika doria za ufuatiliaji wahalifu sugu wanaojihusisha na mauaji yanayoendelea katika Kanda hiyo ya kipolisi.

Sabas alisema Askari wakiwa na mtuhumiwa mmoja muhimu anayeshiriki katika mauaji hayo ambaye alikuwa amekamatwa na baada ya mahojiano alikubali kwenda kuwaonesha Polisi mahali ambapo ni maficho ya wenzake.

Sabas alieleza kuwa, baada ya kufika eneo la msitu wa Ngomboroni kikundi cha watu wanaokadiriwa kufikia watano walikurupuka kutoka kwenye kichaka na kuanza kukimbia ndipo askari Polisi kwa tahadhari kubwa walianzisha mashambulizi na kufanikiwa kumjeruhi mhalifu mmoja kwa risasi, katika mashambulizi hayo mtuhumiwa aliyekuwa mkononi mwa polisi naye alijaribu kutoroka na hivyo kupelekea kumjeruhi kwa risasi hivyo idadi yao kufikia wawili. 

Majeruhi hao wawili walifariki dunia njiani wakati wakipelekwa hospitali kwa matibabu kutokana na kuvuja damu nyingi iliyosababishwa na majeraha ya risasi waliyoyapata. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Katika tukio hilo tumefanikiwa kupata silaha mbili aina ya SMG na shot gun moja pamoja na risasi tisa za SMG zilizokuwa kwenye Magazine.” Alisema Sabas. 


Aidha, mkuu huyo wa Operesheni maalum za Jeshi la Polisi Naibu kamishina Sabas ameendelea kuwasisitiza wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa wahalifu wengine waliosalia na kwamba zawadi nono bado ipo pale pale na itatolewa kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa sahihi kuhusiana na wahalifu wanaojihusisha na mauaji katika kanda maalumu ya Rufiji.
Mkuu wa Oparesheni Maalumu za Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas (Kushoto) na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Rufiji, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Onesmo Lyanga wakionyesha kwa Waandishi wa habari silaha mbili zilizopatikana baada ya mapambano katika msitu wa Ngomboroni Tarafa ya Ikwiriri ambapo katika tukio hilo waliuwawa wahalifu wawili wanaojihusisha na mauaji katika wilaya ya Mkuranga, Kibiti na Rufiji. 
Mkuu wa Oparesheni Maalumu za Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas akionyesha kwa Waandishi wa habari silaha mbili aina ya SMG na Shot Gun zilizopatikana baada ya mapambano katika msitu wa Ngomboroni Tarafa ya Ikwiriri ambapo katika tukio hilo waliuwawa wahalifu wawili wanaojihusisha na mauaji katika wilaya ya Mkuranga, Kibiti na Rufiji. Kulia kwake ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Rufiji, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Onesmo Lyanga.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi) 

KARIMJEE JIVANJE YADHAMINI WANAFUNZI KATIKA KOZI YA UZAMILI YA UHIFADHI WA MAZINGIRA YA WANYAMAPORI

$
0
0
 Taasisi ya Karimjee Jivanje (KJF) imeongeza nguvu zaidi katika kuhifadhi na kusimamia mazingira ya bara la Afrika kwa kudhamini wanafunzi kutoka Tanzania kuendelea na masomo yaliyopendekezwa ya shahada ya uzamili katika eneo hilo. 

Mwenyekiti wa heshima wa kundi la makampuni ya Karimjee Jivanjee nchini Tanzania, Hatim Karimjee alisema mpango huo wa masomo uliundwa na taasisi na mpaka sasa imejitolea kudhamini wanafunzi wawili mwaka 2016 na wanne mwaka huu.

 Alisema Taasisi imetoa msaada wa dola 105,000 sawa na ( 236.2Millioni Tzs) mwaka jana ambapo wanafunzi wawili walichukua kozi ya shahada ya uzamili, na mwaka huu wanafunzi wanne wamedhaminiwa na taasisi ambapo imetoa msaada wa dola 210,000 sawa na (472.5 Miilioni Tzs) na ina mpango wa kutoa dola 180,000 sawa na (405Million Tzs) kwa ajili ya kudhamini nafasi za masomo mwaka ujao “Karimjee Jivanjee imefurahi kuzindua nafasi za masomo ya uhifadhi wa mazingira. 

Wanafunzi hawa watajifunza masomo yalipondekezwa ya shahada ya uzamili ya usimamizi wa uhifadhi wa mazingira ya wanyamapori katika bara la Afrika. Tunapenda kushirikiana na chuo kikuu cha Glasgow nchini Scotland na chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela kilichopo Arusha kuanzisha masomo ya shahada ya uzamili ambapo wanafunzi watasoma mwaka mmoja Glasgow na mwaka mmoja Mkoani Arusha. Wanafunzi hao watatambulika kama wanafunzi kutoka Karimjee,” 
Mwenyekiti wa kundi la makampuni ya Karimjee Jivanjee, Hatim Karimjee (kulia) akimkabidhi kifaa cha kusomea mmoja wa mwanafunzi aliyepata udhamini wa kusoma shahada ya uzamili katika uhifadhi wa mazingira ya wanyamapori katika bara la Afrika Zabibu Kabalika (kushoto) katika hafla iliyofanyika mkoani Arusha. 
Mwenyekiti wa kundi la makampuni ya Karimjee Jivanjee akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuzindua masomo yaliyopendekezwa ya kozi ya uzamili katika uhifadhi wa mazingira ya wanyamapori mkoani Arusha, Nyuma Kulia ni Dr. Haydon wa chuo kikuu Glasgow kilichopo Scotland, akifuatiwa na Prof, Karoli Njau wa chuo cha sayansi na teknolojia cha Nelson Mandela, wengine ni wanafunzi waliopata nafasi ya masomo, Zabibu Kabalika (wa tatu kulia) na Evaline Munisi. 
Mwenyekiti wa Kundi la makampuni ya Karimjee Jivanjee akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuzindua kozi ya uzamili iliyopendekezwa katika uhifadhi wa mazingira ya wanyamapori mkoani Arusha. kulia ni wanafunzi waliopata nafasi ya masomo ya shahada ya uzamili katika uhifadhi wa mazingira ya wanyamapori Evaline Munisi ( kwanza kulia) na Zabibu Kabalika.


SPIKA WA BUNGE APOKEA MSAADA WA MIFUKO 200 YA SEMENTI NA HUNDI YA SH. MILIONI 15 KUTOKA BENKI YA CRDB TAWI LA DODOMA KWA AJILI YA UJENZI WA NYUMBA ZA WALIMU, WILAYANI KOGWA, DODOMA.

$
0
0


Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (katikati) akipokea hudi ya shilingi milioni 15 na msaada wa Mifuko mia mbili (200) ya sementi kutoka kwa Mkurugenzi wa CRDB Benki Tawi la Dodoma Ndg. Rehema Hamisi (kushoto) waliotoa ili kusaidia ujenzi wa nyumba za Walimu wa Shule ya sekondari Laikala iliyopo Wilayani Kogwa, Dodoma. Wengine katika picha ni wafanyakazi wa Benki hiyo tawi la Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (katikati) akionyesha hudi ya shilingi milioni 15 aliyokabidhiwa na Mkurugenzi wa CRDB Benki Tawi la Dodoma Ndg. Rehema Hamisi (kushoto) alipokuwa wanatoa msaada wa ujenzi wa nyumba za Walimu wa Shule ya sekondari Laikala iliyopo Kogwa, Dodoma kulia ni Mkuu wa Shule hiyo Ndg. Msafiri Simon.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza mara baada ya kukabidhiwa hudi ya shilingi milioni 15 na Mkurugenzi wa CRDB Benki Tawi la Dodoma Ndg. Rehema Hamisi alipokuwa wanatoa msaada wa ujenzi wa nyumba za Walimu wa Shule ya sekondari Laikala, Kogwa, Dodoma. Walioshikilia hundi hiyo ni Wanafunzi wa shule hiyo.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Walimu, Wanafunzi wa shule ya Laikala iliyopo Kogwa, Dodoma na wakazi Kata ya Saranga (hawapo pichani), mara baada ya kupokea msaada huo kushoto ni Mkurugenzi wa CRDB Benki Tawi la Dodoma Ndg. Rehema Hamisi na kulia Diwani wa kata ya Sagara Ndg. Simon Kamando.

(Picha na Ofisi ya Bunge)
Viewing all 110180 articles
Browse latest View live




Latest Images