Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

Introducing "Unaionaje" by Young Killer Feat Harmonize


Balozi Seif Ali Iddi akutana na Rais wa Taasisi ya Ushauri wa masuala ya Uhandisi ya Endsight

$
0
0
Taasisi ya Ushauri wa masuala ya Uhandisi ya Endsight iliyo chini ya usimamizi wa Shirika la Changamoto ya Millenia la Marekani (MCC) imeazimia kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha miradi ya Maendeleo kupitia miundombinu ya Mawasiliano na huduma za Kijamii. 
Rais wa Taasisi hiyo Bwana Matthew McLean alitoa kauli hiyo wakati alipofanya mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar. 
Mazungumzo hayo pia yalijumuisha Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mh. Salama Aboud Talib, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usarifishaji Zanzibar Mh. Mohamed Ahmed Salum pamoja na watendaji wakuu wa baadhi ya Taasisi za Serikali. 
Bwana Matthew alisema Endsight imekuwa ikitoa ushauri wa Kitaalamu katika fani ya uhandisi katika kuona kiwango cha miundombinu kinachowekwa kwenye miradi inayohusika zaidi na masuala ya uhandisi inatekelezwa katika hadhi na daraja inayotakiwa kitaalamu. Alisema miundombinu ya bara bara na Mawasiliano, kilimo ikiwemo pia miradi ya huduma za maji safi na salama inahitaji ungalizi sahihi katika uanzishwaji wake ili wakati inapoanza kufanya kazi itoe huduma sahihi iliyokusudiwa kitaalamu. 
Naye Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mh. Salama Aboud Talib pamoja na watendaji wa Serikali walimueleza Bwana Matthew kwamba Zanzibar bado inakabiliwa na changamoto wa upatikanaji wa maji safi na salama katika baadhi ya maeneo.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar akizungumza na Rais wa Taasisi ya Ushauri wa masuala ya Uhandisi  ya Endsight  iliyo chini ya usimamizi wa Shirika la Changamoto ya Milenia la Marekani (MCC)  Bwana Matthew McLean ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar 
Balozi Seif Ali Iddi Kati kati akiwa katika pamoja na Rais wa Taasisi ya Ushauri wa masuala ya Uhandisi  ya Endsight  Bwana Matthew  McLean aliyeko upande wa Kulia yake , Waziri Ardhi Mh. Salama Aboud Talib Kushoto  yake, Naibu Waziri Ujenzi Mh. Mohamed Ahmed Salum wa Pili kutoka Kushoto pamoja na baadhi ya Watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Picha na – OMPR – ZNZ. 

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU TV: Taifa Stars Yaaga Rasmi michuano ya Cosafa kwa kufungwa 4-2 na Zambia

KAMPUNI ZA PUMA, TIPPER NA TPB ENERGY ZATOA GAWIO KWA SERIKALI SH. BILIONI 7

$
0
0
SERIKALI imekubali kulifanyia kazi ombi la Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy la kutaka taasisi za umma ziweze kununua mafuta ya kampuni hiyo yenye ubia wa asilimia 50 kwa 50 na Serikali ili faida inayopatikana itumike kwenye kutatua changamoto za Watanzania.
Kauli hiyo imetolewa Mjini Dodoma mapema leo baada ya Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Puma Dk Ben Moshi kutoa ombi hilo kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango wakati wa tukio la kampuni hiyo kutoa gawio la Sh bilioni 7 kwa Serikali ambayo ni faida iliyopatikana kutokana na biashara ya mafuta.
Akikubali ombi hilo Dk.Mpango alisema kuwa watalifanyia kazi ombi hilo hasa kwa kutambua hata mchango wa kampuni ambazo zimewekeza nchini na zina ubia na Serikali, huku akitoa angalizo kuwa pamoja na ombi hilo
kufanyiwa kazi,hakuna sababu ya Puma kubweteka kwani lazima ushindani uwepo ili kupatikana kwa bidhaa bora."Serikali tumefurahi kwa gawio hili ambalo mmelitoa kwani fedha hizi zitakwenda kuhudumia Watanzania masikiniambao wanahitaji kupata huduma muhimu.Hivyo niwahakikishie Puma ombi lenu nimelisikia na tunalifanyia kazi lazima tuendelee kushirikiana ili kuwa na uwekezaji wenye tija kwa nchi yetu,"alisema Dk.Mpango.
Pia alitumia nafasi hiyo kuitaka kampuni ya Puma kuendelea kufanya kazi yao kwa ufanisi zaidi ili mwaka ujao wa fedha, gawio liongezeke zaidi na kuwahakikisha Serikali inalo jicho lake ambalo linaangalia kwa kampuni zote na mashirika ambayo wana ubia nayo.
Awali kabla ya kukabidhi mfano wa hundi ya Sh bilioni 7 kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mwenyekiti wa Bodi yaPuma Dk. Mosha alisema kuwa wanatambua majukumu yao kwenye kufanyabiashara ya mafuta na ndio kampuniambayo inaongoza kwenye soko lakini ombi lao kwa Serikali ni kwamba itoe maelekezo kwa taasisi na mashirika yaumma kununua mafuta kutoka kwao.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kushoto), akipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania Limited, Dk. Ben Moshi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. bilioni 7 ikiwa ni gawio la serikali yenye hisa ya asilimia 50 katika hafla iliyofanyika mjini Dodoma. Anayeshuhudia katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Philippe Corsalettti,anaeshuhudia kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika,Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Dk. Pallangyo pamoja na viongozi waanndamizi kutoka Wizara hiyo wakishuhudia tukio hilo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kushoto), akipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania Limited Dkt.Ben Moshi pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Philippe Corsalettti  mfano wa hundi yenye thamani ya sh. bilioni 7 ikiwa ni gawio la serikali yenye hisa ya asilimia 50 katika hafla iliyofanyika mjini Dodoma. Anayeshuhudia katikati ni ,anaeshuhudia kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika.
Dk Mapango akipongezana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Philippe Corsalettti pamoja na Mwenyekiti wa Puma, Dkt. Moshi
Dk. Mpango akifafanua jambo kwa kusisitiza Taasisi mbalimbali za Serikali kuboresha huduma zao na kuipatia serikali gawio kubwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania Limited, Dk. Ben Moshi (katikati) akijadiliana jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kushoto) pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Puma, Philippe Corsalettti wakati wa hafla ya kampuni hiyo kukabidhi gawio la sh. bilioni 7 kwa serikali mjini Dodoma,pichani kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Dk. Pallangyo na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika.

KUSOMA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MHE. HUSEIN BASHE ATOA UFADHILI WA MASOMO KWA WANAFUNZI WOTE WALIOFAULU NZEGA MJINI

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Mohammed Bashe ametoa ufadhili wa Masomo (Scholarship) kwa jumla ya wanafunzi 42 ndani ya Jimbo la Nzega Mjini ambao wamechaguliwa kujiunga na Masomo ya Kidato cha Tano kwenye  mikoa mbalimbali nchini.
Kabla ya hapo;  mwishoni mwa mwezi  Mei mwaka huu Mhe. Bashe aliwatunuku vijana hawa zawadi katika Tamasha kubwa la *Bashe Annual Academic Awards* ambapo kila mwanafunzi aliyefaulu kwa daraja la kwanza (Division One) alizawadiwa Pesa taslimu Tzs 100,000 huku wale waliopata Daraja la Pili (Division Two) walipatiwa Tzs 60,000 na wale wa daraja la Tatu walipatiwa Tzs 30,000 kwa pamoja na Counterbooks sita(6) kwa kila mwanafunzi kama sehemu ya pongezi na maandalizi yao ya shule; na leo hii amekamilisha kuwalipia ada za mwaka mzima watoto wote.
Hizi ni miongoni mwa jitihada za Mhe. Bashe katika kuwasaidia wadogo zetu na ndugu zetu ndani ya Jimbo la Nzega Mjini kuweza kufikia malengo yao katika Elimu na katika  maisha.
*Mhe. Hussein  Bashe*..... _"Ninafahamu fika kuwa Elimu ndio Ufunguo pekee na silaha muhimu katika maisha ya mwanadamu katika  vita dhidi ya Umasikini na Maradhi; nami nimeamua kuungana na Rais wangu *Dr. John Pombe Magufuli*  katika kuhakikisha tunawasaidia watoto wetu kuweza kupata haki ya msingi ya Elimu kwa ajili ya kuwa na taifa imara na kusaidia jamii nyingi masikini nchini."
Zoezi hili liliongozwa na Afisa Taaluma wa Halmashauri ya Mji wa Nzega Bw. Christopher Wilson Lusinde ambaye alifika kwa ajili ya kuwapongeza na kuwaaga vijana hawa huku akisindikizwa na Mwl. Saidi Uyaga kutoka Shule ya Sekondari Chief Ntinginya huku Ofisi ya Mbunge ikiwakilishwa na Bw. Godfrey Malema ambaye pia ni Afisa Mahusiano katika Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nzega Mjini
 Wanafunzi 42 ndani ya Jimbo la Nzega Mjini ambao wamechaguliwa kujiunga na Masomo ya Kidato cha Tano kwenye  mikoa mbalimbali nchini.




KAMATI HURU YA UCHAGUZI WA KLABU YA MAJIMAJI YAKETI KWA DHARURA

$
0
0
Kamati huru ya uchaguzi ya klabu ya Majimaji ya mjini Songea imefanya kikao cha dharura  ili kupitia mapendekezo ya wanachama na wakereketwa wa klabu hiyo kuhusu kuangali upya namna ya kupunguza gharama za uchukuaji fomu kwani umekuwa ukiwaumiza wengi. Endelea kuangalia video

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 05.07.2017


MEYA WA JIJI NA MEYA WA KINONDONI WATEMBELEA BANDA LA (LAPF) MAONYESHO YA SABASABA

$
0
0
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mh. Isaya Mwita akizungumza na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe wakati alipotembelea katika banda la Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwenye viwanja vya maonyesho ya biashara vya Mwalimu J.K. Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.

Mfuko wa LAPF na Jiji la Dar es salaam wana Mpango kabambe wa kutekeleza ujenzi wa kituo kipya cha mabasi ya kwenda mikoani jijini Dar es salaam utakaogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 30.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe akitoa maelezo kwa Meya wa Jiji na Meya wa Kinondoni Mh. Benjamin Sitta wakati mameya hao walipotembelea katika banda la mfuko huo leo
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mh. Isaya Mwita na Meya wa Kinondoni Mh. Benjamin Sitta wakisaini kitabu cha wageni wakati walipowasili katika banda hilo kulia ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe.
Matukio mbalimbali ya picha yakiontesha baadhi ya wafanyakazi wa LAPF wakiwahudumia wananchi waliofika kwenye banda la mfuko wa Pensheni wa LAPF kwenye Maonyesho ya Sabasaba barabara ya Kilwa leo.

KHERI YA SIKU YA KUZALIWA MDAU

$
0
0
Dj Tony kutoka Arusha, Tanzania
Michuzi Blog inakutakia kheri ya siku ya kuzaliwa

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS JULY 6, 2017

WAZIRI KINDAMBA ATEULIWA KUWA AFISA MTENDAJI MKUU WA TTCL

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) 
Bw. Waziri Waziri Kindamba.

Fahamu miundombinu ya serikali mtandao

WATEJA WA VODACOM WAICHANGAMKIA RED RLX KATIKA MAONESHO YA SABASABA

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza nchini, Vodacom Tanzania inashiriki Maonesho ya 41 ya Viwanda na Biashara maarufu kama “Sabasaba” ambapo mamia ya wateja wameoneshwa kufurahishwa na kujiunga na huduma mpya inayojulikana kama “RED RLX” ikiwa ni miongoni mwa huduma nyingi zinatolewa bandani hapo. 
Huduma hii ni mpango unaojumuisha vifurushi na kulipa kadri mteja atumiavyo na lengo ni kuwafanya wateja wa Vodacom waishi bila wasiwasi linapokuja suala la mawasiliano. 
Vifurushi hivi vina dakika nyingi, MB za intaneti nyingi, SMS nyingi na pia dakika za kupiga simu nje ya nchi. Wakati mteja anaponunua kifurushi cha RED, anaweza kuchagua huduma ya kifurushi cha kujirudia (kujinunua tena) kila kinapoisha muda wake au kununua mara moja tu. Mteja wa Vodacom akinunua bando ya RED, atapata nafasi na kipaumbele ya kuhudumiwa bila kukaa kwenye foleni wakati akitembelea duka lolote la kampuni hiyo, atapata huduma ya SOKONI App BURE, taarifa fupi ya M-Pesa BURE pindi anapohitaji na huduma ya kipekee pindi atakapowasiliana na huduma kwa wateja. Ili mteja ajiunge na kunufaika na kifurushi hiki anatakiwa kupiga *149*01# na Chagua RED na ataona vifurushi hivi vya RED. Kifurushi cha Silver • TZS 30,000 • 600 Dakika (Mitandao Yote) • 3GB Data • 3,000 SMS Kifurushi cha Gold • TZS 50,000 • 1,000 Dakika (Mitandao Yote) • 7GB Data • 7,000 SMS Kifurushi cha Platinum • TZS 95,000 • 2,500 Dakika (Mitandao Yote) • 30 Dakika (Kimataifa) • 20GB Data • 15,000 SMS

Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira katika ziara ya kikazi wilayani Rombo

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira Jumatano hii amefanya ziara ya kikazi wilayani Rombo. Aliianza kwa kukutana na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya hiyo na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama kabla ya kufika kituo cha uhamiaji kati ya Kenya na Tanzania upande wa Holili. 
 Aliendelea na ziara ndani ya wilaya kupitia eneo la mpaka wa Kenya na Tanzania linalotajwa kama njia ya panya ya kutorosha magendo na mahindi toka Tanzania kwenda Kenya. Ziara yake ilifikia kituo kingine cha uhamiaji kati ya Kenya na Tanzania cha Tarakea na kisha kumalizia ziara yake eneo la msitu wa miti ya kupandwa wa Rongai eneo la Kamwanga.
 Ziara ilianza saa tatu asubuhi na kumalizika sa kumi na mbili jioni. Mhe Mkuu wa Mkoa alisisitiza kila Mtumishi kutimiza wajibu wake kwa kuwa na UTU NA UZALENDO. "...Lazima tumpime mtumishi kwa kila siku amefanya kazi gani katika ofisi yake - tangu mlinzi, mfagizi hadi afisa wa juu. Ni lazima tuwajibike. Watumishi lazima mtambue nafasi zenu, mziheshimu na kujua kuwa kazi na nafasi yako ni kiungo cha nafasi na kazi ya mwenzako..."alisema Mhe. Mghwira.
 Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akilakiwa na watumishi akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Rombo 
 Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akiongea na watumishi alipowasili kuanza ziara ya kikazi wilayani Rombo.
 Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akioneshwa maeneo na Katibu Tawala Bw. Abubakar Asenga wakati wa  ziara ya kikazi wilayani Rombo
 Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akitembezwa maeneo mbalimbali katika  ziara ya kikazi wilayani Rombo.




NIDA WAONGEZA MASHINE ZA KUTOLEA VITAMBULISHO SABASABA KUKIDHI MAHITAJI YA MAELFU YA WANANCHI WANAOMIMINIKA BANDANI KATIKA MAONESHO YA SABASABA

$
0
0
 Wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakiwa wanawaandaa watu kupiga picha katika eneo la Nje mara baada ya watu kujaa ndani na kulazimika  kuongeza mashine ndani ya maonesho ya Sabasaba ambapo hitaji la watu kupata vitambulisho vya Taifa limekuwa kubwa
 Msululu wa watu wakiwa katika eneo la nje ya banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakisubiri kupatiwa huduma kwa ajili ya kupata vitambulisho ndani ya Viwanja vya Maonesho ya Sabasaba
Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano na Hifadhi  hati  kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa 'NIDA' Bi. Rose Mdami  akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam aliyefika kupata huduma ya Kitambulisho cha Taifa katika banda lao lililopo  katika Viwanja vya Maonyesho Sabasaba
Foleni ya kupata vitambulisho katika banda la ndani la NIDA ikiwa imeshika kasi kuliko kawaida hali iliyowalazimu kuongeza vifaa na watumishi wa kufanyakazi katika Viwanja vya Sabasaba
Afisa Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA), Bw. Said Said akiwa amezungukwa na wananchi waliofika kupata vitambulisho vya Taifa katika viwanja vya Maonesho Sabasaba katika eneo la nje na kuwapa maelzo namna ya kupata Vitambulisho vya Taifa
Sehemu ya wananchi wakiwa wamekaa chini wakisubiri foleni yao ifike ili waweze kuchukua Vitambulisho vya Taifa kutoka NIDA
Maofisa  kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) wakiwa Wamezungukwa na wananchi waliofika kupata vitambulisho vya Taifa. katika viwanja vya Maonesho Sabasaba.
Picha na Humphrey Shayo, Gobu ya Jamii

OSHA WAJIKITA KATIKA KUTOA ELIMU KATIKA MAONESHO YA SABASABA

$
0
0
 Afisa Takwimu kutoka Wakala wa Usalama na Afya  Kazini (OSHA)  akimsaidia mmoja wa wakaazi wa Jiji la Dar es Salaam ambao wamefika katika banda hilo kujifunza namna Wakala huo unavyofanya kazi
 Mkaguzi Uslama wa Umeme kutoka OSHA Bi. Maria Ndaskoy akimuelewesha mmoja wa wadau wa Mamlaka hiyo waliofika katika Banda la Maonesho Sabasaba kulipia masula mbalimbali
 Mkaguzi wa Mazingira Mahala pa kazi kutoka OSHA akitoa elimu nmana ya watu wanavyotakiwa kukaa katika maeneo ya viwandani wakiwa salama na kuwaeleza kazi za OSHA 
Mkaguzi wa Afya  kutoka OSHA Dkt Edwin Senguo akitoa huduma ya upimaji Macho kwa wadau waliofika katika banda hilo

Fahamu miundombino ya serikali mtandao

TANZIA: MWANAMUZIKI SHAABAN DEDE AFARIKI DUNIA LEO

$
0
0
Mwanamuziki mkongwe Shaaban Dede amefariki dunia leo saa mbili asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu kwa takriban wiki mbili, mwanae Hamad Dede amethibitisha. 

Hamad Dede amesema mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Mbagala jijini Dar es salaam, na kwamba ratiba na taratibu zote zitatangazwa mara zitapokamilika kupangwa.

Marehemu Dede atakumbukwa kama mmoja wa wanamuziki nguli kutokea nchini Tanzania kwa sauti yake tamu na utunzi wa nyimbo mbalimbali zilizoshika chati akiwa na bendi mbalimbali zikiwemo Tabora Jazz, Bima Lee, Mlimani Park na Mondo Ngoma ambako alikuwa anatumikia hadi mauti yanamkuta.

Globu ya Jamii inatoa mkono wa rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na mashabiki wa Shaaban  Dede kwa kuondokewa na mkongwe huyu wa muziki.



Mola aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi - AMIN

Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un


WATU WAZIDI KUPATA VITU KEMKEM NDANI YA SABASABA

$
0
0
 Wakazi wa mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam wakiwa wamebeba bidhaa mbalimbali  ambazo wamenunua ndani ya maonesho ya 41  Sabasaba
  Wakazi wa mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam wakiwa wamebeba bidhaa mbalimbali  ambazo wamenunua ndani ya maonesho ya 41  Sabasaba
 Makatuni ya kucheza na watoto ndani ya Viwnaj vya Maonesho ya Sabasaba

 Mussa Manyoka akicheza na Nyoka ndani ya Viwanja vya Saba Saba katika banda la Maonesho ya Hifadhi ya Taifa ya Bonde la Ngorongoro

In Africa Band wakitoa burudani ndani ya Viwanja vya Saba Saba Maonesho ya Hifadhi ya Taifa ya Bonde la Ngorongoro
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images