Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

Dk.Shein Akutana na Uongozi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Biashara la Taifa la Zanzibar (ZSTC)

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko na Uongozi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Biashara la Taifa la Zanzibar (ZSTC)pamoja na Uongozi wa Shirika la Biashara la Taifa la Zanzibar (ZSTC) katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Biashara la Taifa la Zanzibar (ZSTC)Bw.Kassim Malik Suleiman (kushoto) na Wajumbe wengine wa Bodi hiyo wakiwa katika kikao sha siku moja na Uongozi wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko pamoja na Uongozi waShirika la Biashara la Taifa la Zanzibar (ZSTC) chini Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) kilichofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko na Uongozi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Biashara la Taifa la Zanzibar (ZSTC)pamoja na Uongozi wa Shirika la Biashara la Taifa la Zanzibar (ZSTC) katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Biashara la Taifa la Zanzibar (ZSTC) Bw.Kassim Malik Suleiman (kulia) alipokuwa akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati wa kikao cha siku moja kilizungumzia masuala mbali mbali kuhusu Shirika la Biashara la Taifa la Zanzibar (ZSTC) katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,(kushoto) Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe.Amina Salum Ali,[Picha na Ikulu. 04/07/2017.

Muonekano Uwanja wa Taifa Kuelekea Mechi na Everton Julai 13 2017.

$
0
0
unnamed
Muonekano wa Uwanja wa Taifa kuelekea Mechi ya Everton Julai 13 2017 (Picha na Hassan Silayo-IDARA YA HABARI-MAELEZO)
12

ANKAL MICHUZI ATEMBELEA WADAU KATIKA MAONESHO YA SABASABA

$
0
0
 Ankal Michuzi akizungumza na Wadau Abdul Malik wa Globala Education Link na Pascala Mayala wa PPR Katika Maonesho ya Sabasaba
  Ankal Michuzi akizungumza na Wafanyakazi wa kampuni ya Magazeti ya Serikali DailyNews na Habari Leo katika Maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Ankal Michuzi  akisalimiana na wafanyakazi wa kampuni ya Magazeti ya Serikali DailyNews na  Habari leo
Habari Leo katika Maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam katika picha ya pamoja na wafanyakazi  wafanyakazi wa kampuni ya Magazeti ya Serikali DailyNews na Habari leo

SPIKA NDUGAI APATA UGENI KUTOKA CRDB BENKI LEO OFISINI KWAKE MJINI DODOMA.

$
0
0
unnamed
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akizungumza wakati alipotembelewa na ugeni kutoka CRDB Benki Tawi la Dodoma, Katikati ni Meneja wa CRDB Benki Tawi la Dodoma Ndg. Rehema Hamisi na kulia ni Meneja Biashara Ndg. Danny Shemdoe, katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

TASWIRA MBALIMBLI YA MAONESHO YA SABA SABA

$
0
0
Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob akitazama noti bandia katika banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika maonesho ya 41 biashara katika viwanja vya saba saba leo.
Mkurugenzi wa Uangalizi wa Benki wa BoT, Kanuti akimpa maelezo Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, juu ya usimamizi wa maduka ya kubadishia fedha za kigeni na za ndani katika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link , Abdulmaalik Mollel akimpa maelezo mteja wakati maonesho ya 41 ya biashara kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakiwa katika Banda la Global Education Link
Wananchi wakiwa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

WATUMISHI WAWILI WA HOSPITALI YA KITETE MKOANI TABORA WAKAMATWA NA DAWA NA VIFAA TIBA WALIVYOKUWA WAMEFICHA KATIKA MIKOBA YAO

$
0
0
Na Tiganya Vincent-RS-TABORA

Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara amemtaka Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Kitete kuwakama mara moja na kuwafikisha Polisi watumishi wawili wa Hospitali hiyo wanaotuhumiwa kukutwa na dawa na vifaa tiba katika mikoba yao.

Dkt. Ntara alitoa kauli hiyo jana(leo) mjini Tabora baada ya watumishi hao kukamatwa na vifaa hivyo katika mikoba yao kinyume na utaratibu wa hospitali na ambazo dawa hizo na vifaa wanatuhumiwa walikuwa wakitaka kwenda kuziuza katika hospitali binafsi.

Alisema kuwa baada ya kukamatwa na kupekuliwa katika mikoba yao ndipo walikuwa na dawa na vifaa tiba ambavyo havitakiwa kutoka nje ya hospitali na havikuwa na maelekezo ya Mganga.Kufuatia kazi hiyo ilifanywa na walinzi hao Katibu Tawala huyo wa Mkoa aliwapongeza na kuwaagiza kuongeza kupekua watu wote wanaokwenda kuona wagonjwa kwa sababu yawezekana watumishi wengine ambao sio waadilifu wakatumia nafasi hiyo kutorosha dawa na vifaa tiba.

Alimwagiza Mganga Mfawaidhi wa Hospitali hiyo kuhakikisha watuhumiwa hao wanakamatwa mara moja na kufikishwa Polisi wakati hatua nyingine za kiutumishi zinaendelea.Watumishi waliokamatwa kwa tuhuma za kukutwa na dawa na vifaa tiba katika mikoba yao ni Petronila Mbipa Bundala ambaye ni Mhudumu na Monica Alexanda Rugeinamu ambaye ni Muuguzi.

Aidha ameagiza watumishi hao waandikiwe mara moja barua za kusimamishwa kazi kutokana na tuhuma za kukutwa na mali ya mwajiri wao kinyume na sheria.Vifaa na dawa vilivyokamatwa ni Cannula, Surgical gloves, Syringesa, Urinal bag, IV giving set, Blood giving set,Brainded silk number, water injection, powder, soap, examination grolve, gentamyacin injection ampule, ascorbic acid.

Hivi karibuni Hospitali hiyo imekumbana na wizi wa mara kwa mara hatua iliyopelekea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kusimamisha Kampuni iliyokuwa imepewa jukumu la kulinda na kulazimika kuweka Kampuni nyingine wakati taratibu za kuichukulia hatua Kampuni ya awali zikiendelea.

Kuanza kwa Kampuni mpya tayari watuhumiwa hao wamekamatwa na ulinzi umeimarishwa.

PROF. KABUDI:UPUNGUFU KATIKA MFUMO WA KISHERIA WA USIMAMIZI WA SEKTA YA MADINI

NIDA YAFURIKA WANANCHI WANAOHITAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA SABASABA

$
0
0


Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano na Hifadhi  hati  kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa 'NIDA' ,Rose Mdami  akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam aliyefika kupata huduma ya Kitambulisho cha Taifa katika banda lao lililopo  katika Viwanja vya Maonyesho Sabasaba
 Afisa Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)  Agnes Gerald  akiwa amezungukwa na wateja mbalimbali  waliofika kupata vitambulisho vya Taifa. katika viwanja vya Maonesho Sabasaba
 baadhi ya wakazi wa jiji wakisubiri kupigwa picha hili waweze kupatiwa Vitambulisho vyao
 Afisa Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA),Said Said akiwa amezungukwa na wateja mbalimbali  waliofika kupata vitambulisho vya Taifa. katika viwanja vya Maonesho Sabasaba
 Afisa kutoka Uhamiaji ,Elias Chipolo akikagua nyaraka  na viambatanisho vinavytakiwa katika fomu ya kuomba vitambulisho vya Taifa.
Sehemu ya watu waliofurika katika Maonyesho ya Sabasaba kufuata vitambulisho vya Taifa



TANAPA WIKI HII

Dr. Mengi ataka wasambazaji kushawishi uwekezaji

$
0
0
Makampuni ya Tanzania ya uwakala wa usambazaji wa bidhaa za kutoka nje ya nchi, wameshauriwa kuyashawishi makampuni ya nje kujenga viwanda vya kuzalisha bidhaa hapa hapa nchini. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi ametoa ushauri huo jijini Dar es salaam wakati akitembelea mabanda ya maonyesho ya Kimataifa ya Biashara, na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wanaunga mkono kwa vitendo jitihada za Rais John Pombe Magufuli za kutaka kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
 Akifuatana na Mkurugenzi wa TPSF Bw. Louis Accaro, Afisa Biashara wa Tan-Trade Bw. Mohamed Mkadara, na Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wajasiriamali Bi. Jacquiline Maleko, Dr Mengi ametembelea mabanda mbalimbali, yakiwemo yaliyopo chini ya mwamvuli wa Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda, na Kilimo – TCCIA, Mfuko wa Fursa sawa kwa wote-EOTF, na Banda la Kampuni ya Agricom, ambayo Mkurugenzi wake Mtendaji Bi. Angelina Ngalula alielezea jinsi ilivyojipanga kusambaza zana za kisasa za kilimo ili kumpunguzia mkulima gharama za uzalishaji. Katika majumuisho yake Dr Mengi alishauri Tan-Trade na TPSF washirikiane katika kuangalia namna ya kuboresha zaidi maonyesho hayo, hususan katika kuboresha mabanda ya maonyesho ili yalingane na hadhi halisi ya kimataifa. 
Meneja Mkakati wa Kampuni ya Agricom Afrika, Eric Mwidunda (kushoto) akitoa maelezo kuhusu ubora wa matrekta hayo kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi (wa pili kushoto) alipotembelea kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Agricom, Bi. Angelina Ngalula (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi alipotembelea banda la kampuni hiyo kujionea huduma zao kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha juu na chini ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi akifurahia jambo na wanawake wafanyabiashara kwenye banda la TWCC katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha ya juu kulia ni Noreed Mawalla wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC). Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akisalimiana na wanawake wajasiriamali wanaofadhiliwa na EOTF akiendelea kutembelea wajasiriamali katika maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Anayemuongoza ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akipata maelezo ya huduma mbalimbali za mikopo riba nafuu kwa wanawake kutoka kwa Afisa Huduma kwa Wateja wa Tanzania Women's Bank, Renita Michael (kulia) ndani banda la EOTF wakati alipotembelea maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa na Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Jacqueline Maleko.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA


KAIMU JAJI MKUU, WAZIRI MWIJAGE WATEMBELEA BANDA LA WCF

$
0
0

 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.Profesa Ibrahim Hamisi Juma, (kushoto), akikaribishwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Sebera Fulgence, alipotembela banda hilo kwenye hema la Jakaya Kikwete viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu kama Sabasaba, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kunakofanyika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam Julai 4, 2017. Mhe Profesa Hamisi  alitumia kwa uchache dakika 15 akiwa na shauku ya kupata taarifa zaidi kuhusu kazi na majukumu ya Mfuko huo. 

Mhe Profesa Hamisi alielezwa kuwa Mfuo huo umeundwa mahsusi kwa ajili ya kutoa fidia stahiki kwa Mfanyakazi aliyepata ugojnwa au kuumia mahala pa kazi. Hali kadhalika, alielezwa kuwa pamoja na kwamba Mfuko huo  ni wa Hifadhi ya Jamii, namna ya uchangiaji wake unatofautiana na Mifuko mingine, ambapo Mwajiri ndiye anawajibika kisheria kumchangia mfanyakazi wake kila mwezi wakati Mifuko mingine, wachangiaji ni wote, mwajiri na mwajiriwa. 

Wakati hyuo huo, Waziri anayehusika na sekta ya Viwanda na Biashara, sekta ambayo inatoa ajira kubwa kwa wafanyakazi, naye alipata fursa ya kutembelea banda hilo ambapo kama ilivyokuwa kwa Kaimu Jaji Mkuu naye alielezwa majukumu yanayotekelezwa na Mfuko ambapo Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Sebera Fulgence, alimueleza kuwa sekta ya viwanda na biashara ni miongoni mwa sekta zinazotoa wanachama wengi kwenye Mfuko huo, ukiachilia elimu na afya na kwamba Mfuko umekuwa ukiendelea kutoa elimu zaidi kwa waajiri kuhusu umuhimu wa kuchangia wafanyakazi wao kwa manufaa ya mwajiri na mwajiriwa pindi yanapotokea madhara. 

Mfuko wa WCF ni Taasisi ya Hifadhi ya Jamii iliyoundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi (sura 263 marejeo ya mwaka 2015).
 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Sebera Fulgence(kulia), akimpatia maeelzo Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamisi Juma (kushoto) na ujumbe wake kuhusu shughuli zifanywazo na WCF.
  Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Sebera Fulgence(kulia), akimpatia maelezo Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamisi Juma (kushoto) na ujumbe wake kuhusu shughuli zifanywazo na WCF.
 Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage, (kulia), akizungumza jambo na Maafisa wa WCF, Bw. Sebera Fulgence (wapili kushoto) ambaye ni Afisa Uhusiano Mwandamizi na Bi.Bi.Inocencia William

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

CHAMA CHA UOKOAJI MAJINI TANZANZIA, CHAMA CHA MAKOCHA WA KUOGELEA NA KIKOSI CHA KMKM WANDAA MAFUNZO YA USALAMA MAJINI ZANZIBAR

$
0
0
Katibu Mkuu chama cha uokoaji majini Tanzania Bwa. Alexander Mwaipasi akitoa maelezo ya mafunzo ya usalama majini yatayofundishwa kwa muda wa wiki katika Skuli ya kimataifa iliyopo Mazizini Mjini Zanzibar.
Kapten Khatibu Khamis wa Kikosi cha KMKM Zanzibar akifungua mafunzo ya usalama majini kwa vikundi mbalimbali vinavyojishuhulisha na uokoaji Afika Mashariki pamoja na skari wa jeshi hilo katika Skuli ya kimataifa Mazizini Mjini Zanzibar. (kulia) Katibu Mkuu chama cha uokoaji majini Tanzania Bwa. Alexander Mwaipasi na (kushoto) ni Katibu wa KMKM Sports Club luteni Sheha Mouhammed Khamis.
Mkufunzi Job Kania kutoka chama cha uokoaji cha Dunia (ILS) akifafanua jambo kwa baadhi ya wanafunzi wa mafunzo ya usalama majini yaliyofanyika Skuli ya kimataifa Mazizini Mjini Zanzibar.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya usalama majini akimunyesha mgeni rasmin jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtu alieza na kuokolewa katika mafunzo hayo.

Picha na Makame Mshenga.

VIONGOZI WA KIMILA MKOANI MBEYA WAUNGA MKONO KAULI MBIU YA HAPA KAZI TU.

$
0
0
Na Zawadi Msalla-WHUSM

Viongozi wa kimila Mkoani Mbeya waunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hatua mbalimbali za kuhakikisha Tanzania inafika katika uchumi wa kati wa Viwanda .

Wameyasema hayo walipokuwa wakizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel katika ziara yake Mkoani humo na kuongeza kuwa ni vema Watanzania waungane kwa pamoja kufanikisha nia njema ya Rais, Dkt. Magufuli.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi hao ,Chifu Rocket Mwashinga kutoka Igawilo alisema kuwa Rais anasisitiza wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kuondokana na umaskini na kulijenga taifa.

“Tufikishie ujumbe huu kwa Mhe. Rais ili hao vijana wetu wanaokimbilia mijini badala ya kukaa na sisi wazee kulima nchi isiwe na njaa warudishwe vijijini waje walime na kwa maendeleo yao binafsi na taifa” 

“Inasikitisha sana kuona siku hizi vijana wakilalamikia Serikali kuwa maisha ni magumu wakati wameacha mashamba na wao ndiyo watu wenye nguvu ambapo magenge makubwa ya ujambazi, wabakaji na walevi waliopitiliza yaliyopo huko mijini yanatokana na vijana wasio na ajira” Alisema Chifu Mwashinga.

Aidha Wakuu hao wa kimila walieleza kuwa ili kauli mbiu ya Hapa Kazi tu iweze kutekelezeka wameiomba Serikali iangalie utaratibu wa kuwarudisha vijijini vijana wasio na ajira waliopo mijini kwa kuwa wao ndio nguvu kazi na chachu ya maendeleo. 

Pia viongozi hao waliishauri Serikali kufufua kilimo shuleni ambapo hapo awali watoto walifundishwa elimu ya kujitegemea kwa kulima mashamba na kujenga majengo ya shuleni mambo ambayo kwa sasa hayafanyiki.

“Tulifundishwa kupenda kilimo tukiwa shuleni ,watoto wa siku hizi hata jembe hawajui kulishika” Alieleza Chifu Joseph Mwalawa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel aliiomba ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuwatambua wakuu hao wa kimila ili kwa pamoja waweze kusukuma gurudumu la Maendeleo ya taifa.

DUKA LA KADI ZA KISASA ZA MIALIKO MBALIMBALI YA SHEREHE LAZINDULIWA MWENGE

$
0
0
Duka la kadi mbalilmbali za mialiko ya sherehe limezinduliwa Mwenge,jana jijini Dar, ambapo kila mtu anaweza kumudu gharama.

Akizungumza baada ya kufunguliwa duka hilo Mkurugenzi Mtendaji wa R Plus , Rehema Moses amesema kuwa wameweka kadi zinazoendana na wakati katika sherehe na hafla  mbalimbali.

Amesema Kadi za mialiko walizo nazo ni Send off ,KitchenParty , Harusi pamoja na mialiko ya Kiofisi zinazokwenda kisasa na wakati zaidi.

Rehema amesema katika biashara hiyo wajasirimali wengine wanaweza kununua hapo kwa bei ya jumla kutokana na mahitaji yao.

Amesema kadi zinazopatikana  za aina zote za kumfanya kila mtu kuweza kumudu kwa gharama nafuu kutokana na uwezo wake.
Mgeni Maalum wa Ufunguzi wa Duka la Kadi Mwenge, Doris Mollel Foundation, Doris Mollel akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka la kadi Mwenge.
Mkurugenzi Mtendaji R Plus na Mmiliki wa Duka la Kadi za Mialiko, Rehema Moses akimuonesha kadi mbalimba mgeni maalum wa ufunguzi wa Duka, Doris Mollel katika hafla iliyofanyika Mwenge.
Mkurugenzi Mtendaji R Plus na Mmiliki wa Duka la Kadi za Mialiko, Rehema Moses akiwa na Mwenza wake wakikata keki mara baada ya duka hilo kufunguliwa.
Mgeni Maalum, Doris Mollel akiwa na Mmiliki wa Duka, Rehema Moses na wadau mbalimbali waliofika katika duka hilo wakibadilishana mawazo mara baada ya uzinduzi
Picha ya Pamoja.

KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA KUMI YA DUKA LA MY WEDDING SOLUTIONS


MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS SUDAN KUSINI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudani Kusini Mhe. Jenerali Taban Deng Gai ambapo mazungumzo yao yalihusu kuendelea kudumisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili.Mazungumzo hayo yamefanyika wakati mkutano wa 29 wa wakuu wa nchi na serikali wa Umoja wa Afrika, jijini Addis Ababa ukihitimishwa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JULY 5, 2017

Tecno Dude Mkombozi Wa Watanzania inapatikana sabasaba na nchi nzima

INTRODUCING: MAJIBU BY KABOUK

Phillip Luberege wa Dar es Salaam azoa Sh Milioni 20 za Biko

$
0
0
FUNDI ujenzi Phillip Luberege mwenye maskani yake Gongolamboto jijini Dar es Salaam, ametangazwa kuwa mshindi wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, akipatikana katika droo ya 20 ya kuwania Sh Milioni 20.

Luberege ametangazwa mshindi leo jijini Dar es Salaam katika droo ya 20 iliyochezeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja, akishirikiana na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe.

Akizungumza katika droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema mshindi huyo amepatikana baada ya kupatikana kwa washindi wa mikoani kiasi cha kuashiria kwamba kumekuwa na mwamko mkubwa kutoka kona zote za Tanzania kuchangamkia mchezo wao kwa watu kuchangamkia fursa ya ushindi wa papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja.

Alisema kwamba mchezo wao wa Biko ni rahisi kucheza pamoja na kushinda, kwa sababu unachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo namba ya kampuni yao ni 505050 na kumbukumbu yao ni 2456, huku kiasi cha kuanzia kucheza kikiwa ni Sh 1000 na kuendelea.

“Sh 1000 ya kucheza Biko inampa mshiriki wetu nafasi mbili ya ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 20 ambapo hufanyika Jumatano na Jumapili, huku mpaka sasa Biko ikitoa zaidi ya Sh Bilioni moja kwa miezi miwili ya Mei na Juni pekee,” Alisema.

Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akionyesha namba ya mshindi wa Sh Milioni 20 aliyopata mkazi wa Gongolamboto, Phillip Luberege. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe.
Kajala Masanja kulia akiwa na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe.

Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images