Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

CLOUD AWASILI KUTOKEA SWEDEN APOKEWA KWA SHANGWE NA KUTAMBULISHA FILAMU YAKE MPYA INAITWA 'USIJISAHAU'

$
0
0
--
 Msanii wa Filamu Nchini Issa Mussa 'Cloud'Akipokewa na Rais wa Shirikisho la Filamu nchini ,Simon Mwakifamba, akitokea nchini Swedeni ambako anaishi kwa sasa.  Cloud amekuja nchini kwa ajili ya uzinduzi wa filamu yake ambayo ameifanya huko huko Sweden na kampuni moja inayokwenda kwa jina la Fila(4)
 Msanii wa Filamu Nchini Issa Mussa 'Cloud' akisalimina na mmjoa wa viongozi wa timu ya Bongo Muvi Chick Mchoma mara baada ya kuwasili nchini akitokea nchini Swedeni
 Sehemu ya Mashabiki wa  Msanii wa Filamu Nchini Issa Mussa 'Cloud' wakiwa na mabango katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
  Msanii wa Filamu Nchini Issa Mussa 'Cloud' akizungumza na Waandishi wa Habari  mara baada ya kuwasili nchini akitokea Sweden
  Mke wa Msanii wa Filamu Nchini Issa Mussa 'Cloud' akizungumza na Vyombo vya habari.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Balozi Modest Mero ampongeza Kanali George Itang'ire kwa kupandishwa cheo

$
0
0
Balozi na Mwakilishi Mkazi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Modest Mero akimpongeza Kanali George Itang'ire kwa kupandishwa cheo na Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli kutoka ngazi ya Luteni Kanali na kuwa Kanali wa JWTZ katika ofisi za ubalozi wa Tanzania jijini New York leo.

uhondo wa tanapa wiki hii

BONDIA IBRAHIM KING CLASS AWASILI NCHINI NA UBINGWA AKITOKEA UJERUMANI

$
0
0
 Bondia Ibrahim King Class akiwasili nchini akitokea nchini Ujerumani ambapo alishinda taji la Dunia ubingwa Global Boxig Council  katika uzito wa kati mara baada ya kumchapa Jose Forero wa  wa Panama  kwa Point
  Bondia Ibrahim King Class akinyoosha mkanda wake juu wa ubingwa
  Bondia Ibrahim King Class akiwa na kocha wake Habibu  Kinyogoli  mara baada ya kutaua nchini
  Bondia Ibrahim King Class akiwa na makocha wake Habibu Kinyogoli na Rajabu Muhamila Super D mara baada ya kuwasili nchini
  Bondia Ibrahim King Class akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa ngumi
 Bondia Ibrahim King Class akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa ngumi


TIMU YA TAIFA YA CRICKET YARUDI NCHINI NA VIKOMBE VIWILI NA MEDALI KUTOKEA DUBAI KWENYE MASHINDANO YA DUNIA

$
0
0

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Cricket waliotoka katika mashindano ya Dunia ya mchezo huo wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam wakitokea Dubai ambapo walishiriki mashindano hayo yajulikanayo kama Memon World Cup na kufanikiwa kuchukua nafasi ya tano.
 Wachezaji wa timu ya Taifa ya Cricket wakionesha vikombe walivyopata na Medali katika mashindano ya Dunia ya mchezo huo
 Viongozi na Wachezaji wa mchezo huo wakiwa wanatoka na mizigo ndani ya uwanja wa  Kimataifa wa Ndege wa JK Nyerere wakitokea nchini Dubai kwenye mashindano ya Dunia ya Mchezo wa Cricket ambapo Tanzania imefanikiwa kushika nafasi ya tano.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Miss Kiki afunguka anavyowapagawisha Afrika Kusini

MICHUZI TV: MAPOKEZI YA RAIS DKT MAGUFULI JIJINI MWANZA

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU WA KWANZA RAIS WA SUDAN YA KUSINI MHE. JENERALI TABAN DENG GAI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza Rais wa Sudan ya Kusini Mhe. Jenerali Taban Deng Gai ambapo mazungumzo yao yalihusu kuendelea kudumisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili. Mazungumzo hayo yamefanyika wakati mkutano wa 29 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika ukiendelea, jijini Addis Ababa, Ethiopia. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

BREAKING NYUZZZ...: DC HAPI AIAGIZA POLISI KUMTIA MBARONI MBUNGE HALIMA MDEE

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Hapi ameliagiza jeshi la Polisi Kinondoni kumkamata Mbunge wa Kawe Halima Mdee kwa kosa la kutoa kauli za matusi, dhihaka na uchochezi dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wananchi kwa ujumla.

Hapi ameagiza mbunge huyo kukamatwa, kukaa korokoroni kwa saa 48, kuhojiwa na kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria kwa maneno aliyoyatoa jana akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya Chadema mtaa wa ufipa. 

Hapi amesema kuwa maneno aliyoyatoa Mdee ni matusi yenye lengo la kuleta uchochezi unaoweza kuhatarisha amani na utulivu.
"Sitamvumilia mwanasiasa yeyote atakayethubutu kutoa kauli za matusi dhidi ya Mh. Rais, au zenye kutaka kuleta uchochezi katika wilaya yangu."
Alisema DC Hapi.

TEHAMA yaongeza ufanisi a kazi katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC)

$
0
0
Je unajua jinsi TEHAMA inavyoboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Usikose kuangalia kipindi hiki.

Airtel na DTB wazindua maabara ya kompyuta kwa wanafunzi wa Dar kujifunza kutengeneza programu

$
0
0
 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) leo imezundua maabara ya kompyuta ilijulikanayo kama  “Airtel Fursa Lab” katika shule ya msingi ya kijitonyama wilaya ya Kinondoni kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata ujuzi katika masomo ya Tehama na kukuza ujuzi katika maswala ya kitechnologia
  
Maabara hiyo ya “Airtel Fursa Lab” itatoa mafunzo ya msingi ya kompyuta kwa hatua ya awali  na mafunzo ya hatua ya juu zaidi kwa  wanafunzi wa shule za msingi, sekondari, chuo kikuu na jamii nzima kwa ujumla. Walimu pia watapata mafunzo ya kompyuta yatakayowawezesha kutoa msaada kwa wanafunzi watakaotumia maabara hiyo

Akizindua maabara hiyo mgeni rasmi ambaye ni  Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu, Prof. Faustin Kamuzora aliwapongeza Airtel na DTBi kwa kuweka nguvu pamoja  katika ushirikiano huu ambao utachochea mapinduzi kwa vijana wa kitanzania katika sekta ya habari namawasiliano (ICT).  Hii itasaidi kujenga jamii yenye msukumo wa kutafuta masuluhisho na kujiongezea wigo katika ujasiliamalia ambayo utasaidia kukuza uchumi wa viwanda kwa taifa”

Pia alitoa wito kwa wadau wengine kuunganisha nguvu katika ushirikiano kama huo ili kuleta maendeleo zaidi”

Akiongea katika uzinduzi huo pia, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya alisema “ wakati Tanzania imejipanga kufikia uchumi wa viwanda mahitaji ya wafanyakazi wenye ueledi katika teknologia wanahitajika sana ili kufikia malengo haya. Hivyo ni muhimu kujenga vijana wenye ujuzi  na ueledi wakiwa katika umri mdogo na hivyo tunajisikia fahari kuwa sehemu ya kutoa ujuzi na kukuza maendeleo ya watanzania katika Teknologia ya Tehama kupitia maabara ya Airtel Fursa  tunayozindua leo.

Maabara ya Airtel Fursa ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kutumia teknologia ya mawasiliano ya simu pamoja na Tehama katika kustawisha biashara na kukuza ujuzi katika teknologia  na hivyo kuwa na nguvukazi yenye ueledi zaidi.  Natoa wito kwa vijana na jamii nzima kuchangamkia fursa hii na kuitumia maabara hii ya kompyuta ipasavyo. Aliongeza Mallya

  Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais , Prof. Faustin Kamuzora (katikati) akiongea wakati wa uzinduzi wa maabara ya Kompyuta itakayojulikana kama“Airtel Fursa Lab” ili kufundisha watoto na vijana mafunzo ya TEHAMA chini ya usimamizi na ushirikiano kati ya Airtel na Dar Teknohama Bussiness Incubator (DTBI)  kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano na Mkurugenzi Mkuu wa DTBI Eng. George Mulamula (kushoto). “Airtel Fursa Lab” imezinduliawa leo kwenye shule ya msingi ya kijitonyama iliyoko wilaya ya Kinondoni.
 Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais , Prof. Faustin Kamuzora (wapili kulia) akikata utepe ili kuzinduzia  maabara ya Kompyuta ya “Airtel Fursa Lab” ili kufundisha watoto na vijana mafunzo ya TEHAMA chini ya usimamizi na ushirikiano kati ya Airtel na Dar Teknohama Bussiness Incubator (DTBI)  kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano na Mkurugenzi na kushoto kwake ni Mkuu wa DTBI Eng. George Mulamula na Mwenyekiti wa kamisheni ya ICT Tanzania Maharage Chande na Mweyekiti wa Bodi ya Shule ya msingi Kijitonyama John Mutajwaha “Airtel Fursa Lab” imezinduliawa leo kwenye shule ya msingi ya kijitonyama iliyoko wilaya ya Kinondoni.
 kushoto ni Mwanafunzi wa shule ya msingi  Aghakan Serira Telerico akielezea jinsi alivyotengeneza program ya Robot  kwa Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais , Prof. Faustin Kamuzora wakati alipozindua Maabara hiyo  kwenye shule ya msingi ya kijitonyama wilaya ya kinondoni, wanaoshudia ni Mkuu wa DTBI Eng. George Mulamula na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano ambao ndio wasimamizi na wadhamini wa  Maabara hiyo. “Airtel Fursa Lab” imezinduliwa leo kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata ujuzi katika masomo ya Tehama na kukuza ujuzi katika maswala ya kitechnolojia
Mwanafunzi wa shule ya msingi  Aghakan mzizima Brayan Basimaki (wakwanza kushoto) akielezea jinsi anavyotengeneza program zake za kompyuta  kwa Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais , Prof. Faustin Kamuzora wakati alipozindua Maabara hiyo  kwenye shule ya msingi ya kijitonyama wilaya ya kinondoni, Maabara hiyo. “Airtel Fursa Lab” imezinduliwa leo kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata ujuzi katika masomo ya Tehama na kukuza ujuzi katika maswala ya kitechnologia.

Kaimu Jaji Mkuu atembelea banda la Tume ya Kurekebisha sheria

$
0
0
Kaimu Jaji Mkuu Prof Ibrahim Juma akipata maelezo kutoka kwa Katibu Msaidizi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Agnes Mgeyekwa, kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Husein Katanga.
Kaimu Jaji akisaini kitabu cha wageni katika banda la Tume ya Kurekebisha Sheria wakati alipotembelea banda hilo leo.
Kaimu Jaji Mkuu Prof Ibrahim juma akiingia kutembelea banda la Tume

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA NYANGAO WATEMBELEA BUNGE NA KUKUTANA NA MAJALIWA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyangao iliyopo Jimbo la Mtama mkoani Lindi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. Kushoto kwake ni Mbunge wa Kuteuliwa, Mama Salma Kikwete na wapili kushoto kwake ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye  wakisalimiana na wananfunzi wa Shule ya Sekondari ya Nyangao mkoani Lindi kwenye viwanja vya Bunge jini Dodoma Julai 4, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Nyangao iliyopo katika Jimbo la Mtama Mkoani Lindi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. Wapili kushoto kwake ni Mbunge wa Kuteuliwa, Mama Salma Kikwete na kulia ni Mbunge wa Mtama Nape Nnauye.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Nyangao iliyopo katika Jimbo la Mtama Mkoani Lindi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. Wapili kushoto kwake ni Mbunge wa Mtama Nape Nnauye.

JOKATE ,MPOTO NA INSPECTOR WAWA KIVUTIO BANDA LA NGORONGORO

$
0
0
 Msanii wa Muziki wa Kughani Mrisho Mpoto akiimba mbele ya mashabiki waliomzunguka katika kituo cha taharifa cha Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro kilichopo katika banda la Maonyesho ya 41 ya Saba saba jijini Dar es Salaam
 Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana CCM,Jokate Mwegelo akicheza na wamasai katika kituo cha taharifa cha Ngorongoro kinachoongozwa na Mrisho  Mpoto katika Viwanja vya Maonyesho Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana CCM,Jokate Mwegelo akicheza na wamasai katika kituo cha taharifa cha Ngorongoro kinachoongozwa na Mrisho  Mpoto katika Viwanja vya Maonyesho Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Msanii wa Muziki wa Bongofleva Nchini Haroun Kahena 'Inspector Haroun' Akizungumza na wadau     taharifa cha Ngorongoro kinachoongozwa na Mrisho  Mpoto katika Viwanja vya Maonyesho Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Sehemu ya Wamasai waliofika katika kituo cha taharifa cha Ngorongoro kinachoongozwa na Mrisho  Mpoto katika Viwanja vya Maonyesho Sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya Wamasai waliofika katika kituo cha taharifa cha Ngorongoro kinachoongozwa na Mrisho  Mpoto katika Viwanja vya Maonyesho Sabasaba jijini Dar es Salaam.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA MSHINDI WA TUZO YA UINGEREZA

$
0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Samuel Mwanyika, mshindi wa tuzo ya Stephen Thomas iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Watu wenye Mtindio wa Ubongo (Down's Syndrome Association) ya Uingereza kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. Katikati ni Mama wa mtoto huyo Sophie Mshangama.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Sophie Mshangama ambaye ni mama yake Samuel Mwanyika aliyeshinda tuzo ya Stephen Thomas iliyotolewa Juni 8, 2017 na Taasisi ya Kimataifa ya Watu wenye Mtindio wa Ubongo (Down's Syndrome Association) ya Uingereza kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Samuel Mwanyika (wa pili kushoto), mshindi wa tuzo ya Stephen Thomas iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Watu wenye Mtindio wa Ubongo (Down's Syndrome Association) ya Uingereza kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. Wa kwanza kushoto ni Elias Mwanyika (kaka yake Samuel) akiwa na picha iliyoshinda tuzo hiyo na wa kwanza kulia ni Sophie Mshangama ambaye ni mama yake Samuel. 
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akiwa na Samuel Mwanyika (wa pili kushoto), mshindi wa tuzo ya Stephen Thomas iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Watu wenye Mtindio wa Ubongo ya Uingereza kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. Wa kwanza kushoto ni Elias Mwanyika (kaka yake Samuel) akiwa na picha iliyoshinda tuzo hiyo na wa kwanza kulia ni Sophie Mshangama ambaye ni mama yake Samuel. 

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 59 MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO JULAI 4, 2017.

$
0
0
  Naibu Spika  wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk.Tulia Ackson  akiongoza    kikao cha hamsini na tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Julai 4, 2017.
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Prof Palamagamba Kabudi akisoma maelezo kuhusu Sheria ya marekebisho ya Sheria mbalimbali wa Mwaka 2017  kikao cha hamsini na tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Julai 4, 2017.
 Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza  jambo na Mbunge wa Mtama Mhe.Nape Nnauye  katika kikao cha hamsini na tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Julai 4, 2017.
 Walimu na wanafunzi kutoka Sekondari ya Nyangao kutoka Mtama Mkoani Lindi wakiwa Bungeni kujifunza shughuli mbalimbali katika kikao cha hamsini na tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Julai 4, 2017.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA MRADI MKUBWA WA MAJI SENGEREMA MKOANI MWANZA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine  akifungua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyamazugo Wilayani Sengerema. Mradi huo unatarajiwa kuhudumia wakazi wa Sengereza kwa asilimia 100 tofauti na asilimia 33 ya awali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo ya mradi huo mkubwa wa maji kutoka kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Antony Sanga wakati alipoanza ukaguzi wa mradi huo kabla ya kuufungua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Maji Eng. Gerson Lwenge wakati akielekea kukagua mradi wa maji katika kijiji cha Nyamazugo Wilayani Sengerema. Mradi huo unatarajiwa kuhudumia wakazi wa Sengereza kwa asilimia 100 tofauti na asilimia 33 ya awali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza Mwanachama mpya wa CCM ambaye alikuwa Kada maarufu wa CHADEMA kanda ya Ziwa Hamis Tabasamu mara baada ya kuzindua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyamazugo, Sengerema mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na waandishi wa habari  mbalimbali wa mkoani Mwanza ambao walishiriki katika kazi ya ufunguzi wa mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyamazugo, Sengerema mkoani Mwanza.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI YAAHIDI KUBORESHA MIUNDOMBINU KUVUTIA WAWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA FEDHA VIJIJINI

$
0
0

Na Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma

Serikali imeeleza kuwa inajitahidi kuboresha miundombinu kama vile teknolojia ya Mawasiliano, Barabara, Ulinzi, Maji na Umeme katika maeneo ya vijijini ili kuweka mazingira bora yatakayovutia wawekezaji kutoka sekta binafsi kuwekeza katika sekta ya fedha ili kupanua huduma hiyo katika maeneo ya mijini na vijijini.

Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Josephine Chagulla (CCM), aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kuwapa wanawake elimu kuhusu mikopo pamoja na kufikisha huduma za kibenki maeneo ya vijijini ili waweze kufikiwa na huduma za kifedha.

Mhe. Josephine Chagulla ameeleza kuwa wanawake wengi wa vijijini hawakopesheki kwa sababu benki haziwafikii, pia hawana mafunzo maalumu ya kuwasaidia ujuzi wa namna ya kuzifikia huduma hiyo ya kukopeshwa

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa, elimu ya fedha inahusisha wadau mbalimbali ikiwemo Serikali na Taasisi zake, ambapo kwa upande wa Serikali, Benki Kuu inaratibu uanzishwaji wa taasisi ya kitaifa itakayokuwa na jukumu la kuratibu, kuwezesha na kusimamia utoaji wa elimu ya fedha kwa jamii.

“Serikali kupitia Benki Kuu imetoa mwongozo wa Uwakala wa Huduma za Kibenki ili kupanua wigo wa huduma za kibenki kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi na kwa gharama nafuu hasa katika maeneo ya vijijini”. Alisema Dkt. Kijaji.

JARIDA LA NCHI YETU LA MWEZI JUNI

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images