Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110095 articles
Browse latest View live

MWENGE WA UHURU KUPITIA MIRADI YA SHILINGI BILIONI 8 SIMIYU

$
0
0
Mwenge wa Uhuru ukipelekwa eneo la mradi wa maji katika Kijiji cha Bukundi wilayani Meatu kwa ajili ya kufungua mradi huo.

Na Stella Kalinga, Simiyu

MWENGE wa Uhuru umeanza mbio zake rasmi leo katika mkoa wa Simiyu ambapo utapitia jumla ya miradi 43 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 8,450,841,622/=. Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wakati akitoa salamu za Mkoa huo kwa Kiongozi wa kitaifa wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 , Ndg.AmourHamad Amour  katika kijiji cha Bukundi wilaya ya Meatu ukitokea katika mkoa Singida.

Mtaka amesema kati ya fedha hizo shilingi 680,285,524 zinatokana na Nguvu za wananchi ,Serikali Kuu shilingi 4,524,439,388, Halmashauri Shilingi 352,000,875, Washirika wa Maendeleo Shilingi 635,559,935 na Sekta binafsi Shilingi 2,258,555,900/=

Amesema Mwenge wa Uhuru utafungua miradi 14, kuzindua 13, kutembelea na kuona miradi 16 katika sekta ya Elimu,Afya,Maji,Vijana na wanawake, Miundombinu ya barabara, Sekta ya Viwanda, Maliasili, Kilimo, Ushirika na Utawala bora.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe.Anthony Mtaka akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa moja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa leo katika Kijiji cha Bukundi wilayani Meatu.

Aidha, Mtaka amesema katika kutekeleza kwa vitendo ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wa mwaka huu 2017 usemao “SHIRIKI KATIKA KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YANCHI YETU”, Mkoa wa Simiyu umeweza kujipambanua katika utekelezaji wa Sera ya Tanzania ya Viwanda kupitia Kauli Mbiu ya “Wilaya Moja, Bidhaa Moja, Kiwanda Kimoja”

“Katika utekelezaji huu mkoa umefanikiwa kuanzisha kiwanda cha Chaki wilayani Maswa, Kiwanda cha Maziwa wilayani Meatu na Upembuzi yakinifu unaendelea mingine minne ambayo pia itatekelezwa katika Halmashauri zetu nyingine nne” Ameongeza katika miradi kuwa kukamilika kwa viwanda hivyo kutasaidia kutoa ajira kwa vijana wa mkoa wa Simiyu na mikoa jirani kutokana na kuwa malighafi zinazotumika na zitakazotumika katika viwanda hivyo zinazalishwa hapa nchini.

Naye kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru , Ndg. Amour Hamad Amour akifungua jengo la upasuaji kwa wanawake wajawazito katika kituo cha Afya Bukundi wilayani Meatu mbali na kuipongeza wilaya hiyo kwa kujali afya za wananchi wake hususani wanawake wajawazito pia alitaka mradi huo utunzwe na uthaminiwe.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akitoa salamuza Mkoa wakati wa kupokea Mwenge waUhuru kutoka Mkoani Singida katika kijiji cha Bukundi Wilayani Meatu.

“Mradi huu ni mzuri na mimi nimefurahi kuona naanza kuzindua miongoni mwa miradi inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja, hasa akinamama wajawazito hivyo basi nitoe wito kwa wanawake kutumia vizuri jengo hili badala ya kujifungulia majumbani hali inayoweza kuhatarisha afya zenu, vile vile mradi huu utunzwe na kuthaminiwa ili uendelee kutusaidia,”alisema.


“ TUNDURU MPYA INAKUJA,TUPIGE KAZI KWA KUSHIRIKIANA ,HAKUNA KITAKACHOSHINDIKANA” DC TUNDURU

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera
Wilaya ya Tunduru ni moja kati ya Wilaya tano za Mkoa wa Ruvuma, Ni wilaya iliyokuwa nyuma kimaendelea kuanzia miundo mbalimbali japo ni wilaya iliyojaa utajili wa madini. Mkuu wa wilaya hiyo Juma Homera anakuja na na mkakati wa Tunduru Mpya , fuatilia ujue ni upya gani anakuja nao ambao utaiweka tunduru kuwa ya kisasa.

“ TUNDURU MPYA INAKUJA,TUPIGE KAZI KWA KUSHIRIKIANA ,HAKUNA KITAKACHOSHINDIKANA” DC TUNDURU

KATIBU MKUU WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII ALIPOTEMBELEA MAONYESHO SABASABA

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj.Gen. Gaudence Milanzi wa akifurahia jambo na baadhi ya Wakurugenzi na waoneshaji nje ya banda la Wizara ya Maliasili naUtalii mara baada ya kutembelea banda hilo katika Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, yaliyoanza Juni 28 – Julai 8, 2017 ambapo kwa mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017, yaliyozinduliwa hivi karibuni jijini Dar es salam( Picha na Lusungu Helela- Maliasili na Utalii)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj.Gen. Gaudence Milanzi wa akizungumza jana na baadhi ya Wakurugenzi na waoneshaji nje ya banda la Wizara ya Maliasili naUtalii mara baada ya kutembelea banda hilo katika Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, yaliyoanza Juni 28 – Julai 8, 2017 ambapo kwa mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017, yaliyozinduliwa hivi karibuni jijini Dar es salam( Picha na Lusungu Helela- Maliasili na Utalii)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj.Gen. Gaudence Milanzi wa akizungumza jana na Baadhi ya Wakurugenzi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili naUtalii mara baada ya kutembelea banda hilo katika Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, yaliyoanza Juni 28 – Julai 8, 2017 ambapo kwa mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017, yaliyozinduliwa hivi karibuni jijini Dar es salam( Picha na Lusungu Helela- Maliasili na Utalii).

MKURUGENZI IDARA YA HABARI ATEMBELEA MAONESHO YA 41 YA KIMATAIFA YA BIASHARA

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbasi(katikati) na Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dk. Jimmy Yonaz(kulia) wakijadili jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji (Biashara na Uwekezaji) Prof.Adolf Mkenda walipotembele katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbasi akipata maelezo kutoka kwa Afisa Masoko wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Bw.Ally Mayai alipotembele banda hilo katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbasi(katikati), Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dk. Jimmy Yonaz(kulia) na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari-MAELEZO(Huduma za Habari) Bw.Rodney Thadeus wakipata maelezo kutoka kwa Paul Michael Mkurugenzi wa Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha P.M.Tito’s walipotembelea Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbasi na Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dk. Jimmy Yonaz wakipata maelezo ya namna picha za video za zamani zilivyokuwa zinahifadhiwa alipotembelea banda la Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara leo Jijini Dar es Salaam.
Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dk. Jimmy Yonaz akimpa maelezo Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbasi namna wanavyofanya shughuli zao, alipotembelea banda la hilo katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara leo Jijini Dar es Salaam
1- Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbasi akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Leo Jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jimmy Yonaz.


PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO

MICHUZI TV;UJUE MTO AFRIKA WA MKOANI MBEYA, ULIOPO ENEO LA ILOLO JIJINI MBEYA

ZIFF ANNOUNCES CHIEF GUEST: DEXTER DAVIS

$
0
0
The Zanzibar International Film Festival is excited to announce the 2017 Chief Guest, executive producer, entrepreneur and CEO of D Street Media Group, Dexter Davis.  Dexter will be at ZIFF to host a series of workshops on marketing and distribution, as well as pitching.

Every year ZIFF welcomes a filmmaker as its Chief Guest to celebrate their achievements and contributions to the film industry.  This year, ZIFF is especially excited to welcome Dexter Davis as his visit is just the start of what promises to be a long and important partnership aimed at advancing the develop of the film industry in Africa.

Dexter has a solid and illustrious pedigree within the film industry in the USA and beyond, and has solidified his commitment to the development of African film through a number of initiatives which began in South Africa in 2010. His attendance at ZIFF is further testament to his belief in the future of the African film industry.

Dexter has this to say of his upcoming visit to Zanzibar and ZIFF: “I’m thrilled to be invited to such a beautiful part of the world, and this year’s edition of ZIFF as Chief Guest to host a series of important workshops that speaks to the business of film, which often gets overlooked by independent filmmakers. I can’t thank ZIFF’s team and their CEO Daniel Nyalusi and Festival Director Fabrizio Colombo enough for the invitation to be a part of such an important and much needed festival.  Their commitment to African Cinema and stories from the continent is infectious. I’m looking forward to a long and productive relationship with ZIFF for years to come.”
 Dexter began his career in entertainment at 23 years old when he formed Dexter Davis Productions, a company that specialized in organizing creative fundraising events for nonprofits
in San Francisco, California. In 2000 Davis started the boutique production company StoneCreek Entertainment based in Los Angeles, California. He expanded the company, changed the name to D Street Media Group and relocated to Europe to learn firsthand the global film business. D Street now has offices in Berlin, Buenos Aires, Cape Town and is headquartered in New York City.

In 2004 he executive produced his first feature “The Reception,” which premiered at the Tribeca Film Festival in 2005. He continued to produce films, including indie hits like “Rivers Wash Over Me” and “Somewhere Slow” with Jesslyn Gilsig (Glee, Vikings) and David Costabile (Breaking Bad, Billions.) He formed D Street Releasings in 2006 to distribute international films in the U.S., and brokered a first of its kind co-marketing deal with Volkswagen to support specialized cinema in America.

In 2014 Dexter joined the board of Ghana’s National Museum on Slavery and Freedom where he serves with Nobel Peace Prize recipient Kofi Annan and world-renowned architect David Adjaye. Davis has produced four additional films with several films going into production in 2017, including the action-packed heist film “The Blue Mauritius” starring Eric Dane (Grey’s Anatomy, The Last Ship), legendary French actor Gerard Depardieu and South African actress Pearl Thusi and other international stars.

Following is ‘Team Joy,’ which he’s executive producing for Joe Newcomb, the Oscar winning producer of ‘Dallas Buyers Club,’ and ‘Moto Anjos,’ a Brazilian action film set in Sao Paulo, Brazil, directed by Emmy Award winner Joe Tripician. In 2018 D Street will be producing its’ first film set in East Africa called ‘Ballin…On the Other Side of the World,’ and recently announced the casting of Tanzanian personality turned actor Idris Sultan as one of the leads. Aside from film and television production, Davis is building a state-of-the-art film and TV studio in the beautiful town of Port Shepstone. A municipality in the KwaZulu-Natal province of South Africa.

Dexter Davis is committed to producing and distributing films from the African continent to the United States and around the world. Developing content with Africa talent and American talent is key to establishing a star system in Africa and is an important element to how Africa will get out of the shadow of the United States and Europe when it comes to international cinema.

KAMPUNI YA PUMA ENERGY YATOA GAWIO KWA SERIKALI SH. BILIONI 7

$
0
0
SERIKALI imekubali kulifanyia kazi ombi la Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy la kutaka taasisi za umma ziweze kununua mafuta ya kampuni hiyo yenye ubia wa asilimia 50 kwa 50 na Serikali ili faida inayopatikana itumike kwenye kutatua changamoto za Watanzania.

Kauli hiyo imetolewa Mjini Dodoma mapema leo baada ya Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Puma Dk Ben Moshi kutoa ombi hilo kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango wakati wa tukio la kampuni hiyo kutoa gawio la Sh bilioni 7 kwa Serikali ambayo ni faida iliyopatikana kutokana na biashara ya mafuta.

Akikubali ombi hilo Dk.Mpango alisema kuwa watalifanyia kazi ombi hilo hasa kwa kutambua hata mchango wa kampuni ambazo zimewekeza nchini na zina ubia na Serikali, huku akitoa angalizo kuwa pamoja na ombi hilo
kufanyiwa kazi,hakuna sababu ya Puma kubweteka kwani lazima ushindani uwepo ili kupatikana kwa bidhaa bora."Serikali tumefurahi kwa gawio hili ambalo mmelitoa kwani fedha hizi zitakwenda kuhudumia Watanzania masikiniambao wanahitaji kupata huduma muhimu.Hivyo niwahakikishie Puma ombi lenu nimelisikia na tunalifanyia kazi lazima tuendelee kushirikiana ili kuwa na uwekezaji wenye tija kwa nchi yetu,"alisema Dk.Mpango.

Pia alitumia nafasi hiyo kuitaka kampuni ya Puma kuendelea kufanya kazi yao kwa ufanisi zaidi ili mwaka ujao wa fedha, gawio liongezeke zaidi na kuwahakikisha Serikali inalo jicho lake ambalo linaangalia kwa kampuni zote na mashirika ambayo wana ubia nayo.

Awali kabla ya kukabidhi mfano wa hundi ya Sh bilioni 7 kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mwenyekiti wa Bodi yaPuma Dk. Mosha alisema kuwa wanatambua majukumu yao kwenye kufanyabiashara ya mafuta na ndio kampuniambayo inaongoza kwenye soko lakini ombi lao kwa Serikali ni kwamba itoe maelekezo kwa taasisi na mashirika yaumma kununua mafuta kutoka kwao.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kushoto), akipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania Limited, Dk. Ben Moshi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. bilioni 7 ikiwa ni gawio la serikali yenye hisa ya asilimia 50 katika hafla iliyofanyika mjini Dodoma. Anayeshuhudia katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Philippe Corsalettti,anaeshuhudia kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika,Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Dk. Pallangyo pamoja na viongozi waanndamizi kutoka Wizara hiyo wakishuhudia tukio hilo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kushoto), akipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania Limited Dkt.Ben Moshi pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Philippe Corsalettti  mfano wa hundi yenye thamani ya sh. bilioni 7 ikiwa ni gawio la serikali yenye hisa ya asilimia 50 katika hafla iliyofanyika mjini Dodoma. Anayeshuhudia katikati ni ,anaeshuhudia kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika.
Dk Mapango akipongezana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Philippe Corsalettti pamoja na Mwenyekiti wa Puma, Dkt. Moshi
Dk. Mpango akifafanua jambo kwa kusisitiza Taasisi mbalimbali za Serikali kuboresha huduma zao na kuipatia serikali gawio kubwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania Limited, Dk. Ben Moshi (katikati) akijadiliana jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kushoto) pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Puma, Philippe Corsalettti wakati wa hafla ya kampuni hiyo kukabidhi gawio la sh. bilioni 7 kwa serikali mjini Dodoma,pichani kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Dk. Pallangyo na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika.

KUSOMA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Naibu Katibu Mkuu CCM, Mpogolo aipongeza NMB kuanzisha Fanikiwa Account

$
0
0
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo ameipongeza Benki ya NMB kwa kuanzisha akaunti ya Fanikiwa kwani ina lengo la kuwagusa watu wa kipato cha chini ambao ndiyo sehemu kubwa ya wananchi wa Tanzania. Mpogolo ameyasema hayo baada ya kutembelea banda la benki ya NMB kwenye maonesho ya Saba Saba ambapo alipata fursa ya kupata elimu kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zinatolewa na benki hiyo kubwa nchini. 

Aidha, alisema kuwa akaunti hiyo ni nzuri kwa sababu ni mahususi kwa ajili ya wafanya biashara wadogo wadogo wakiwemo mama lishe, wakaanga chips, wauza magenge n.k ambao ni sehemu kubwa ya Watanzania. Akaunti hii pia inamwezesha mfanyabishara kutambulika kama mteja mfanya biashara, atakua mwanachama kweye klabu za biashara za NMB (NMB Business Club), itamwezesha kupata mkopo mpaka milioni thelathini, ina gharama nafuu za uendeshaji na ni rahisi kuifungua kwani haihitaji nyaraka nyingi. 

Lakini pia mteja anaweza kupata huduma katika matawi zaidi ya 200 ya NMB yaliyoenea nchi nzima. “Akaunti ya Fanikiwa inalenga kuwasaidia wafanyabiashara wadogo ili waweze kukuza mitaji na kuendeleza kipato chao; mtu anapopata nafasi ya kupata mkopo ni njia ya kuongeza kipato cha familia na ndivyo uchumi wa taifa unavyoweza kujengwa, Mimi niwapongeze benki ya NMB kwa kuanzisha akaunti hii na niwahamasishe Watanzania watumie fursa hii kuweza kuongeza kipato kwa ajili ya maisha yao na waweze kukuza uchumi wa nchi yetu,” alisema Mpogolo. 

Vilevile, Mpogolo aliwaasa wananchi wasiogope kuchukua mikopo kwenye mabenki ili waweze kuongeza kipato, “Ni jukumu la kila mtu kumuhamasisha mwenzake aone benki ni mahali anapoweza kupata fursa za kujikomboa kiuchumi, kuendeleza ustawi wake kwani mambo kama haya zamani hayakuwepo ambayo yanagusa watu wa hali ya chini.” “Binafsi jambo lililonigusa ni kuanzishwa kwa akaunti ambayo inagusa watu wa kipato cha chini, naona kwamba Benki ya NMB inakwenda kuwa mkombozi wa watu wanyonge kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais na serikali yake ya kuona wananchi wa kawaida na wao wanaboresha uchumi wao.”
 Mkuu wa Kitengo cha 'Trade Finance' wa Benki ya NMB, Linda Teggisa akimweleza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo kuhusu huduma mbalimbali ambazo zinatolewa na Benki ya NMB alipotembelea banda la banki hiyo kwenye maonesho ya 41 ya Saba Saba yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo (kulia) akiuliza jambo kwa Mkuu wa Kitengo cha Trade Finance wa Benki ya NMB, Linda Teggisa (kushoto) wakati alipotembelea banda la Benki ya NMB kwenye maonesho ya 41 ya Saba Saba.

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA AKABIDHIWA GARI AINA YA WINGLE 5 NA KAMPUNI YA GREAT WALL MOTORS

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amekabidhiwa gari aina ya Wingle 5 na Kampuni ya Great Wall Motors ya nchini China kwa kushirikiana na kampuni ya wazawa ya Kifaru Motors (T).

Akielezea sababu ya kukabidhi gari hiyo kwa serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam, Meneja Mwandamizi wa Kampuni hiyo nchini Afrika Kusini Jianguo Liu ameeleza kuwa ni kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli.

Meneja Liu ameeleza kuwa gari hiyo inathamani ya shilingi milioni 55, hivyo itumike kutatua changamoto mbalimbali za Wananchi.

Kwa upande wake RC Makonda amewashukuru wahisani hao kwa msaada huo na kuahidi kuutumia msaada huo kama ilivyokusudiwa, huku akieleza kuwa utaratibu wa kulitumia gari hilo utatokana na maoni ya wananchi ambapo watapiga kura kupitia namba maalumu na kueleza gari hilo liende kwenye idara ipi, kwa mfano idara ya elimu, afya, polisi nakadhalika, zoezi hilo litachukua siku kumi.

RC Makonda ameongeza kuwa serikali yake itaendelea na utaratibu huo wa kupigia kura magari yaende kwenye idara ipi ili kuchochea ufanisi wa kazi na wanachi ndiyo watakao kuwa waamuzi wa hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikabidhiwa gari na Meneja Mwandamizi wa Kampuni hiyo GWM ya nchi ya Afrika Kusini Jianguo Liu leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akilikagua gari hilo
Muonekano wa gari hilo. Picha na Emmauel Massaka,Globu ya Jamii.
Meneja Mwandamizi wa Kampuni hiyo GWM ya nchi ya Afrika Kusini Jianguo Liu kakizungumza machache kabla ya kukabidhi gali hilo leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuwashukuru wahisani Kampuni ya Great Wall Motors ya nchini China kwa kushirikiana na kampuni ya wazawa ya Kifaru Motors (T).kwa kukabidhi gari leo jijini Dar es Salaam.

RC MAKONDA AMEKABIDHIWA GARI AINA YA WINGLE 5 NA KAMPUNI YA GREAT WALL MOTORS

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amekabidhiwa gari aina ya Wingle 5 na Kampuni ya Great Wall Motors ya nchini China kwa kushirikiana na kampuni ya wazawa ya Kifaru Motors (T).

Akielezea sababu ya kukabidhi gari hiyo kwa serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam Meneja Mwandamizi wa Kampuni hiyo nchini Afrika Kusini Jianguo Liu ameeleza kuwa ni kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli.

Meneja Liu ameeleza kuwa gari hiyo inathamani ya shilingi milioni 55, hivyo itumike kutatua changamoto mbalimbali.

Kwa upande wake RC Makonda amewashukuru wahisani hao kwa msaada huo na kuahidi kuutumia msaada huo kama ilivyokusudiwa, huku akieleza kuwa utaratibu wa kulitumia gari hilo utatokana na maoni ya wananchi ambapo watapiga kura kupitia namba maalumu na kueleza gari hilo liende kwenye idara ipi, kwa mfano idara ya elimu, afya, polisi nakadhalika, zoezi hilo litachukua siku kumi.

RC Makonda ameongeza kuwa serikali yake itaendelea na utaratibu huo wa kupigia kura magari yaende kwenye idara ipi ili kuchochea ufanisi wa kazi na wanachi ndiyo watakao kuwa waamuzi wa hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikabidhiwa gari na Meneja Mwandamizi wa Kampuni hiyo GWM ya nchi ya Afrika Kusini Jianguo Liu leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akilikagua gari hilo.
Muonekano wa gari hilo. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuwashukuru wahisani Kampuni ya Great Wall Motors ya nchini China kwa kushirikiana na kampuni ya wazawa ya Kifaru Motors (T).kwa kukabidhi gari leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Mwandamizi wa Kampuni hiyo GWM ya nchi ya Afrika Kusini Jianguo Liu kakizungumza machache kabla ya kukabidhi gali hilo leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmauel Massaka,Globu ya Jamii.

WAZIRI MKUU APIGA MARUFUKU KUSAFIRISHA MAHINDI NJE YA NCHI BILA KIBALI

UFADHILI WA MASOMO KWA WANAFUNZI WALIOFAULU NZEGA MJINI

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Mohammed Bashe ametoa ufadhili wa Masomo (Scholarship) kwa jumla ya wanafunzi 42 ndani ya Jimbo la Nzega Mjini ambao wamechaguliwa kujiunga na Masomo ya Kidato cha Tano kwenye  mikoa mbalimbali nchini.
Kabla ya hapo;  mwishoni mwa mwezi  Mei mwaka huu Mhe. Bashe aliwatunuku vijana hawa zawadi katika Tamasha kubwa la *Bashe Annual Academic Awards* ambapo kila mwanafunzi aliyefaulu kwa daraja la kwanza (Division One) alizawadiwa Pesa taslimu Tzs 100,000 huku wale waliopata Daraja la Pili (Division Two) walipatiwa Tzs 60,000 na wale wa daraja la Tatu walipatiwa Tzs 30,000 kwa pamoja na Counterbooks sita(6) kwa kila mwanafunzi kama sehemu ya pongezi na maandalizi yao ya shule; na leo hii amekamilisha kuwalipia ada za mwaka mzima watoto wote.
Hizi ni miongoni mwa jitihada za Mhe. Bashe katika kuwasaidia wadogo zetu na ndugu zetu ndani ya Jimbo la Nzega Mjini kuweza kufikia malengo yao katika Elimu na katika  maisha.
*Mhe. Hussein  Bashe*..... _"Ninafahamu fika kuwa Elimu ndio Ufunguo pekee na silaha muhimu katika maisha ya mwanadamu katika  vita dhidi ya Umasikini na Maradhi; nami nimeamua kuungana na Rais wangu *Dr. John Pombe Magufuli*  katika kuhakikisha tunawasaidia watoto wetu kuweza kupata haki ya msingi ya Elimu kwa ajili ya kuwa na taifa imara na kusaidia jamii nyingi masikini nchini."
Zoezi hili liliongozwa na Afisa Taaluma wa Halmashauri ya Mji wa Nzega Bw. Christopher Wilson Lusinde ambaye alifika kwa ajili ya kuwapongeza na kuwaaga vijana hawa huku akisindikizwa na Mwl. Saidi Uyaga kutoka Shule ya Sekondari Chief Ntinginya huku Ofisi ya Mbunge ikiwakilishwa na Bw. Godfrey Malema ambaye pia ni Afisa Mahusiano katika Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nzega Mjini
 Wanafunzi 42 ndani ya Jimbo la Nzega Mjini ambao wamechaguliwa kujiunga na Masomo ya Kidato cha Tano kwenye  mikoa mbalimbali nchini.





WAGOMBEA WAANZA KUJINADI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA CHAMA CHA SOKA CHA WANAWAKE JULAI 08.

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KUELEKEA uchaguzi Mkuu wa Chama cha Soka la Wanawake unaotarajiwa kufanyika Jumamosi ya Julai 08  wagombea wa nafasi mbalimbali wameanza kujinadi sera zao wakiahidi kuendeleza vyema soka la wanawake linaloanza kushika kasi kwa sasa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wagombea hao wanaotetea nafasi zao wamesema kuwa wanatarajiwa kuendeleza pale walipoishia katika awamu waliyotoka kwani wanaamini kuwa wakirejea katika nafasi zao maendeleo ya soka la wanawake yatazidi kukua.

Mwenyekiti anayetetea nafasi yake, Amina Kaluma amesema kuwa atahakikisha anazidisha mahusiano mazuri na mashirikisho mengine ya soka kutoka nchi tofauti ikiwemo kujitangaza zaidi kwenye soka la wanawake.

Amina amesema kuwa, atatumia nafasi yake kama Mwenyekiti kuwashawishi wakina mama kuwaruhusu watoto wao kucheza mpira wa miguu ikiwemo kuwahamasisha wao kama wanawake kusaidia katika kuinua soka la wanawake kwani asilimia kubwa nao ni mashabiki wa mpira.

"Nitatumia nafasi yangu kuwahamasisha wakina mama kujiwekeza zaidi katika soka la wanawake kwani asilimia kubwa wao ni mashabiki na pia waweze kuwaruhusu watoto wao wa kike kucheza mpira wa miguu kwani
hauna uhuni kama wengi wanavyosema,"amesema Amina.

Kwa upande wa Mgombe wa nafasi ya Katibu Mkuu anayetetea nafasi yake Somoe Ng'itu amesema kuwa katika kipindi chao cha miaka minne iliyopita wameweza kuhakikisha ligi ya wanawake inachezwa na ikiwa katika ubora wa hali ya juu pamoja na kupata udhamini.

Mbali ba hilo wameweza kushiriki katika Kombe la Afrika Mashariki na Kati na kufanikiwa kutwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza, TWFA imeweza kuwa na timu za vijana za Taifa kwa upande wa wanawake kwa umri wa miaka 17 na 20 huku kwa mara ya kwanza ikijumuisha wachezaji kutoka nchi nzima.

Uchaguzi wa wanawake utafanyika Jumamosi huku kampeni za Uchaguzi zikiwa zimeanza Julai 4 mwaka huu.
Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha soka la Wanawake Amina Kaluma akinadi sera zake mbele ya wanahabari.

WATEJA WA VODACOM WAICHANGAMKIA RED RLX KATIKA MAONESHO YA SABASABA

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza nchini, Vodacom Tanzania inashiriki Maonesho ya 41 ya Viwanda na Biashara maarufu kama “Sabasaba” ambapo mamia ya wateja wameoneshwa kufurahishwa na kujiunga na huduma mpya inayojulikana kama “RED RLX” ikiwa ni miongoni mwa huduma nyingi zinatolewa bandani hapo. 
Huduma hii ni mpango unaojumuisha vifurushi na kulipa kadri mteja atumiavyo na lengo ni kuwafanya wateja wa Vodacom waishi bila wasiwasi linapokuja suala la mawasiliano. 
Vifurushi hivi vina dakika nyingi, MB za intaneti nyingi, SMS nyingi na pia dakika za kupiga simu nje ya nchi. Wakati mteja anaponunua kifurushi cha RED, anaweza kuchagua huduma ya kifurushi cha kujirudia (kujinunua tena) kila kinapoisha muda wake au kununua mara moja tu. Mteja wa Vodacom akinunua bando ya RED, atapata nafasi na kipaumbele ya kuhudumiwa bila kukaa kwenye foleni wakati akitembelea duka lolote la kampuni hiyo, atapata huduma ya SOKONI App BURE, taarifa fupi ya M-Pesa BURE pindi anapohitaji na huduma ya kipekee pindi atakapowasiliana na huduma kwa wateja. Ili mteja ajiunge na kunufaika na kifurushi hiki anatakiwa kupiga *149*01# na Chagua RED na ataona vifurushi hivi vya RED. Kifurushi cha Silver • TZS 30,000 • 600 Dakika (Mitandao Yote) • 3GB Data • 3,000 SMS Kifurushi cha Gold • TZS 50,000 • 1,000 Dakika (Mitandao Yote) • 7GB Data • 7,000 SMS Kifurushi cha Platinum • TZS 95,000 • 2,500 Dakika (Mitandao Yote) • 30 Dakika (Kimataifa) • 20GB Data • 15,000 SMS

Nyimbo mpya "MAJIBU" kutoka Kwa Kabouk Mtanzaniano Msanii wa Kitanzania anaeishi Gothenborg. Sweden

RAIS MSTAAFU MHE. ALLI HASSAN MWINYI ATEMBELEA BANDA LA ZANTEL KATIKA MAONESHO YA KIMATAIFA YA SABASABA YA 2017 JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0


Rais Mstaafu wa awamu ya Pili wa Tanzania Mhe. Ally Hassan Mwinyi (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Data na Vifaa vya intaneti wa Zantel, Hamza Zuheri (wa tatu kushoto) juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel jana jijini Dar es salaam baada ya kiongozi huyo kutembelea banda la Kampuni hiyo katika maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea hivi sasa katika viwanja vya Mwl J.K Nyerere.
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili wa Tanzania Mhe. Ally Hassan Mwinyi (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Data na Vifaa vya intaneti wa Zantel, Hamza Zuheri (wa pili kushoto) juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel jana jijini Dar es salaam baada ya kiongozi huyo kutembelea banda la Kampuni hiyo katika maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl J.K Nyerere. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji Mhe. Charles Mwijage na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo na Biashara nchini Christopher Chiza (wa pili kulia).
Msanifu Maabara kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Sebastian Magulu (kushoto) akizungumza wakati wa kumtoa damu Mkazi wa Mbagala, Husna Hamisi (katikati) katika banda la Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel alipotembelea banda hilo jana jijini Dar es salaam ili kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni hiyo. Zantel kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa damu Salama wameandaa utaratibu wa uchangiaji damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji wa huduma hiyo katika kipindi hiki cha maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl J.K Nyerere. Kulia ni Meneja wa Chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia Mtingwa.
Mkazi wa mkoa wa Morogoro, Peter Albano akichangia damu katika banda la Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel alipotembelea banda hilo jana jijini Dar es salaam ili kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni hiyo. Zantel kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa damu Salama wameandaa utaratibu wa uchangiaji damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji wa huduma hiyo katika kipindi hiki cha maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl J.K Nyerere. Anayetoa damu ni Msanifu Maabara kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Sebastian Magulu. 

INTRODUCING "HAKUNA TV" BY Hamaguy Ft Ommy G

KAIMU JAJI MKUU ASEMA MAHAKAMA YA TANZANIA KUANZA KUSIKILIZA KESI ZA KIBENKI.

$
0
0

Na Magreth Kinabo – Mahakama ya Tanzania.

5/07/2017

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma, amesema kwamba Mahakama ya Tanzania imejipanga kusikiliza kesi zilizokwama zinazohusu mabenki kwamba ili ziweze kwenda kwa haraka na kulingana na sera ya, ikiwemo kuwezesha ukuzaji wa uchumi wa nchi .

Kauli hiyo ilitolewa na jana Kaimu Jaji Mkuu huyo , wakati alipotembelea Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyoko, Barabara ya Kilwa Road jijini Dar es Salaam, ambapo alizungumzia kuhusu mlundikano wa kesi mahakamani alisema Mahakama ya Tanzania inafanya mikakati ya kuweza kuzipunguza.

“ Tunahitaji majaji zaidi ya 30 ili kuweza kupunguza mlundikano uliopo wa kesi zilizopo Mahakamani,” alisema Profesa .

Profesa Juma alisema hayo, baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya maonesho, ambapo alisema Mahakama ya Tanzania, imepiga hatua katika mabadiliko ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA), akitolea mfano Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara, ambapo alishauri kwamba mahakama zingine za chini ziweze kujifunza.

Profesa Juma pia alitoa ushauri kwa watu wenye viwanda nchini kufuata sheria na taratibu, waweze kusajiliwa kwa kuwa kufanya hivyo kutawafanya washiriki kuongeza pato la Taifa na kukuza uchumi wa nchi .

“ Nimetembelea Banda la Mkemia Mkuu wa Serikali nimeona mazao na bidhaa mbalimbali,hivyo ni vema watu wanaotengeneza bidhaa wakasajiliwa ili waweze kufuata sheria na taratibu za nchi, kwa kuwa kufanya hivyo kutawezesha bidhaa zao kuwa bora na wataweza kuiwezesha nchi kushiriki katika uchumi wa kisasa,” alisema Profesa Juma.

Katika maonesho hayo, Kaimu Jaji Mkuu huyo, miongoni mwa mabanda aliyoyatembelea banda la Mahakama ya Tanzania, Jeshi la Magereza , Banda la Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM),banda la Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikal(GCLA)i, banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA). Banda la Wakala wa Usajili , Ufilisi na Udhamini (RITA) Mamlaka ya Reli Tanzania, na Mabanda la Mamlaka ya Reli Tanzania, Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) ,Shirika la Maendeleo ya Petrol nchini (TPDC .
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akisaini kitabu cha wageni katika katika banda la Mahakama sehemu ya Mahakama Kuu ya Tanzania. Aliyesimama mwenye miwani ni Jaji wa Mahakama Kuu
Mhe. Edson Mkasimongwa.

INTRODUCING NEW SINGLE "MTIHANI" BY NEY LEE

Viewing all 110095 articles
Browse latest View live




Latest Images