Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

Waziri Mwijage aipongeza serikali ya Norway

$
0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza na wadau mbalimbali wa maswala ya Gesi kwenye warsha iliyoandaliwa na kampuni ya Satoil yenye makao yake makuu nchini Norway, iliyoyangika kwenye Hotel Hyatt Regency jijini Dar es Salaam leo. Waziri Mwijage ameipongeza serikali ya Norway kwa kuona umuhimu wa kuwekeza kwenye GAS hapa nchini, kwani wao wamekuwa ni wakongwe kwenye sekta hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Borge Brende akizungumza na wadau mbalimbali wa maswala ya Gesi  kwenye warsha iliyoandaliwa na kampuni ya Satoil jijini Dar Es Salaam leo.
Meneja Mkazi wa Statoil Tanzania, Oystein Michelsen akizungumza na wadau mbalimbali wa maswala ya Gesi  kwenye warsha lililoandaliwa na kampuni ya Satoil jijini Dar Es Salaam leo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Statoil Tanzania , Genevieve Kasanga akizungumza katika warsha hiyo.


MICHUZI TV: DKT. KALEMANI AMEMFUTA KAZI MENEJA ANAYESIMAMIA MIRADI YA TEDAP

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 30/06/2017

MASAUNI ATANGAZA MAJINA YA WATUHUMIWA 16 WA MAUAJI YANAYOENDELEA KIBITI, MKURANGA NA IKWIRIRI

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Simon Sirro, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), baada ya kufanya kikao kuhusiana na uhalifu katika maeneo ya Kibiti,Mkuranga na Ikwiriri,mkoani Pwani, ambapo Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto),alitangaza kutafutwa kwa watu 16 wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu huo.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa polisi makao makuu,jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), baada ya kufanya kikao na viongozi wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi kuhusiana na uhalifu katika maeneo ya Kibiti,Mkuranga na Ikwiriri,mkoani Pwani, ambapo alitangaza kutafutwa kwa watu 16 wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu huo.Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Simon Sirro.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa polisi makao makuu,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akionyesha baadhi ya picha za watuhumiwa wa uhalifu katika maeneo ya Kibiti,Mkuranga na Ikwiriri kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), baada ya kufanya kikao na viongozi wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi ambapo alitangaza kutafutwa kwa watu 16 wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu huo.Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP),Simon Sirro.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa polisi makao makuu,jijini Dar es Salaam.

MAVUNDE ASHIRIKI UJENZI WA MIUNDOMBINU YA SHULE YA MSINGI NZASA

$
0
0
MBUNGE wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde leo ameshirikiana na wananchi wa Kijiji cha Nzasa,Kata ya Chihanga katika ujenzi wa nyumba za walimu, madarasa na matundu ya vyoo. 

Ujenzi huo unahusisha nyumba tatu za walimu, ,madarasa matatu na matundu ya vyoo 7.

Katika ujenzi huo, unatarajiwa kugharimu Sh.205,500,000 ambazo zinazotokana na mradi wa ‘Pay 4 Results’(P4R) uliopo chini ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia.

Akizungumza na wananchi hao, Mavunde ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, aliwapongeza kwa kujitolea kuhakikisha mradi unafanikiwa.

Alibainisha kuwa changamoto zilizokuwa zikiikabili shule hiyo ni kukosekana kwa nyumba za walimu na hivyo kuwafanya walimu kuishi umbali wa kilomita zaidi ya 25.

Mbali na hilo alisema kulikuwa na upungufu wa madarasa pamoja na uchakavu wa vyoo.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akichanganya zege kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule ya msingi Nzasa. 
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akichanganya zege kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule ya msingi Nzasa. 

Wananchi wa Nzasa wakishiriki katika ujenzi wa miundombinu ya shule ya msingi ya Nzasa wakiwa na Mbunge wao Anthony Mavunde 
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akimsikiliza mmoja wa wazee wa kijiji cha Nzasa. 

RC KILIMANJARO, ANNA NGWIRA, AIPONGEZA PSPF KWA KUENDESHA MAFUNZO KW WASTAAFU WATARAJIWA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira, (kulia), akipokea kadi ya uanachama wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, kupitia mpango wa hiari, (PSS), kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, wakati wa semina ya wastaafu watarajiwa mkoani Kilimanjaro Juni 30, 2017.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira,akiagana na wanachama wasitaafu watarajiwa,wa mfuko wa pesheni wa PSPF,mara baada ya kufungua semina hiyo Mkoa wa Kilimanjaro Juni 30, 2017
Baadhi ya wastaafu watarajiwa wakiwa kwenye semina ya mafunzo iliyoandaliwa na PSPF mkoani Kilimanjaro.

NORWAY YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA DOLA MILIONI 10.5 KUBORESHA ELIMU

$
0
0

Benny Mwaipaja, WFM, DAR ES SALAAM

SERIKALI ya Norway imeipatia Tanzania msaada wa Dola Milioni 10.5 za Marekani kupitia programu ya miaka mitatu ya maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, inayotarajiwa kuanza Mwaka Mpya wa Fedha- Julai Mosi mwaka huu.

Mpango huo pamoja na uzinduzi wa Awamu ya Pili ya Program ya Maendeleo ya Sekta ya Mafuta, umezinduliwa Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo kwa niaba ya Serikali zao.

Dkt. Mpango ameishukuru Serikali ya Norway kwa msaada huo mkubwa utakaochangia kuboresha utendajikazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kuijengea uwezo zaidi wa kitaalamu, miundombinu na vitendeakazi vingine vitakavyo changia kuongeza uwezo wa Mamlaka hiyo wa kukusanya mapato ya Serikali.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo amesema kuwa hatua ya Serikali ya Norway kuendelea kufadhili programu ya pili ya Mpango wa kuendeleza Sekta ya Mafuta utaiwezesha Serikali kubobea katika masuala ya utaalamu wa masuala ya sheria na usimamizi wa sekta hiyo.

Nae Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Mhe. Borge Brende amesifu utendaji kazi mahili wa Mhe. Rais Dokta John Pombe Magufuli wa kupambana na ufisadi na vitendo vya rushwa pamoja na kuimarisha ukusanyaji kodi, hatua ambayo itaifanya nchi ipige hatua za maendeleo haraka.

Amesema kuwa hajawahi kuona nchi yoyote duniani ikiendelea bila kuweka nidhamu na uwajibikaji serikali pamoja na kutokusanya mapato yake ipasavyo na kuahidi kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na serikali ya awamu ya tano kufanikisha mipango yake ya kuwaletea wananchi wake maendeleo.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Borge Brende wakielezana jambo kabla ya kuzindua rasmi Mpango wa miaka mitatu wa Maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya Program ya Maendeleo ya Sekta ya Mafuta, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Borge Brende akielezea kuhusu kuendelea kwa ushirikiano wenye tija na Tanzania wakati wa kuzindua rasmi Mpango wa Maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya program ya maendeleo ya Sekta za Mafuta jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza jambo wakati wa kuzindua rasmi Mpango wa miaka mitatu wa Maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya Program ya Maendeleo ya Sekta za Mafuta, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Borge Brende (katikati) na Balozi wa Norway nchini Tanzania Hanne Marie Kaarstad wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo (hayupo pichani) wakati akielezea umuhimu wa Program ya Maendeleo ya Sekta za Mafuta, Jijini Dar es Salaam.

UWT YAPULIZA KIPYENGA CHA KUCHUKUA FOMU KUOMBA UONGOZI, YAMUUNGA MKONO JPM KUHUSU MIMBA SHULENI

$
0
0
NA BASHIR NKOROMO, DAR.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Amina Makilagi leo ametangaza rami tarehe ya Wanachama wa Jumuia hiyo kuanza kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi tangu ngazi ya Kata hadi Taifa, na kusema fomu zinatolewa bure, huku akionya kuwa atakayejaribu kutumia rushwa kuomba nafasi yoyote atakatwa.

Pia ametumia ameaema UWT inaunga mkono tamko la Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Magufuli alilolitoa hvi kribuni kwamba, ni marufuku kwa msichana atakayepata ujauzito akiwa shuleni katika mfumo rasmi kurudi masomoni katika mfumo huo rasmi.

Makilangi amesema, UWT inaunga mkono tamko hilo kwa sababu ndiyo maelekezo yaliyomo katika Ilaniya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020, na pia ndiyo Sera ya Serikali katika kusimamia utoaji elimu katika mfumo rasmi hapa nchini.

"Tafiti mbalimbali za Jumuia na Taasisi nyingine hapa nchini na za Kimataifa likiwemo Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataida (UNICEF), Mwanafunzi mjamzito au aliyejifungua ni vigumu kuendelea na masomo katika mfumo ambao umeandaliwa kulingana na Saikolojia ya akili ya mtoto asiye na majukumu ya malezi na ndiyo maana upomfumo uliopendekezwa na sera na ilani ya CCM kwamba anayekatiza masomo katika mfumo rasmi anaweza kuendelea katika mfumo usio rasmi, Mifumo isyo rasmi kwa ajili ya wanafunzi wa aina hiyo na wengine waliokosa masomo katika mfumo wa kawaida ni  kama MEMKWA na QT" , alisema Makilagi.

Alisema UWT inatambua na kuheshimu mapendekezo  ya tafiti hizo kuhusu watoto na pia inakubaliana na sera ya Serikali na Ilani ya CCM kuweka utaratibu bora na wenye manufaa  zaidi wa kuwazuia wajawazito na wazazi  kuendelea na masomo katika mfumo rasmi na badala yake kutengeneza mfumo mbadala wa kupata elimu kwa kuwa kufanya hivyo kumaimarisha nidhamu, na uwezo wa kitaaluma wa watoto.


MRADI WA UMEME STIEGLER’S GORGE HAUTAATHIRI MAZINGIRA YA PORI LA SELOUS

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Katavi

Wizara ya Maliasili na utalii imewataka wadau wa uhifadhi kote nchini kuunga mkono mpango wa Serikali wa kujenga mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme katika mto Rufiji kwenye pori la akiba la Selous ambao ukikamilika unatarajiwa kuzalisha zaidi ya megawati 2,100.

Katibu Mkuu wizara ya Maliasili na utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi amesema utekelezaji wa mradi huo wa umeme ni wa muhimu kwa taifa kwani utasaidia kuharakisha maendeleo ya taifa kuelekea azima yake ya Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati.

Akiongea wakati akifunga mafunzo ya askari wa wanyamapaori kutoka Mamlaka ya wanayamapori Tanzania -TAWA na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Katibu mkuu Meja Jenerali Gudance Milanzi amesema mradi huo wa umeme pamoja na mradi wa bwawa la maji la Kidunda utachukua eneo dogo tu la pori la akiba la Selou lenye ukubwa wa zaidi ya kilomita za mraba elfu 50.

Amesema pori hilo ndilo kubwa miongoni mwa mapori ya aina hiyo ulimwenguni na ukubwa wake ni zaidi ya nchi za Rwanda na Burundi zikiunganishwa kwa pamoja.

Katibu Mkuu amesema ujenzi wa miradi hiyo hauna tafsiri kwamba Tanzania haithamini masuala ya uhifadhi bali unazingatia uhifadhi wenye manufaa kwa jamii na maendeleo ya taifa na hasa dhamira ya serikali ya rais Dk John Pombe Magufuli kuelekea Tanzania ya viwanda ambayo inahitaji nishati ya umeme itakayoyotosheleza mahitaji ya taifa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu –TAWA Bw. Martin Loibooki akisoma risala mbele ya mgeni Rasmi
katibu mkuu akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu wa jinsia ya kike 10 kati ya 97 waliyohitimu, wa tatu kutoka kushoto waliyokaa ni kaimu mkurugenzi mkuu-tawa
wahitimu wakitoa heshima mbele ya mgeni rasmi.

MAGAZETI YA JUMAMOSI LEO JULY MOSI,2017

HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE YAFUNGA MWAKA WA FEDHA 2016/2017 KWA KUTOA MISAADA KWA VITUO VYA WATOTO YATIMA COMPASSION NA UWEMBA MISSION

$
0
0


HYASINTA KISSIMA-NJOMBE

Halmashauri ya Mji Njombe imetoa misaada yenye thamani ya shilingi milioni mbili laki moja na arobaini kwa vituo viwili vya watoto yatima Compassion na Uwemba Mission ikiwa ni sehemu ya mapato ya ndani ya Halmashauri yaliyokusanywa katika robo ya nne ya mwaka wa fedha 2016/2017.

Akizungumza wakati akikabidhi misaada hiyo katika kituo cha watoto Yatima Compassion, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda amesema kuwa Halmashauri yake imejiwekea utaratibu wa kuhakikisha kuwa katika kila robo ya mwaka wa fedha inatenga fedha kwa ajili ya kusaidia jamii ya wenye uhitaji wakiwemo watoto yatima ili kuonesha upendo lakini pia kuijengea jamii tabia ya kuonesha upendo na kusaidia wale wote wenye mahitaji mbalimbali.

“Kila tunapokusanya mapato imekua ni utaratibu wa Halmashauri kwa kushirikiana na idara ya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa jamii kuangalia makundi yenye uhitaji na kuona ni kwa namna gani tunayaongezea nguvu zaidi ili nao waweze kujikwamua kimaisha na kuona kuwa wao pia ni sehemu ya jamii inayotambulika na kuheshimika. 
Tumekua tukifanya hivi mara kwa mara na leo tunapofunga mwaka na kuanza mwaka mpya wa fedha tumeona kwa kile kidogo tulichokipata tuweze pia kugawana na watoto hawa na furaha yangu imeongezeka kwani mpaka sasa Halmashauri yangu tumefanikiwa kukusanya mapato kwa asilimia mia na kuvuka lengo .”Alisema Mwenda.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda wa kwanza kulia akiwa amembeba mtoto anayelelewa katika kituo cha watoto Uwemba Mission.Kulia kwake ni Afisa Maendeleo na Afisa Ustawi wa Jamii Hosea yusto
Mtoto Imelda Msola kutoka kituo cha watoto Compassion akitoa mkono wa asante kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda mara baada ya kukabidhiwa misaada mbalimbali katika kituo hicho
Misaada iliyokabidhiwa katika kituo cha watoto Uwemba Mission.

Jeshi la Polisi na Mapambano yake dhidi ya Mauaji yanayoendelea Kibiti

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA RASMI MAONYESHO YA 41 YA SABASABA JIJINI DAR LEO

$
0
0


Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyabiashara mbalimbali waliokuwa katika Ukumbi wa Mikutano wakati wa Ufunguzi wa Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, yaliyoanza Juni 28 - Julai 8, 2017 ambapo kwa mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017, katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkabishi tuzo Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Rwekaza Mukandala ambao wameibuka washindi wa jumla katika Maonyesho ya Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, yaliyoanza Juni 28 - Julai 8, 2017 ambapo kwa mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017, Maonesho hayo yamezinduliwa rasmi leo jijini Dar es salaam.Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi tuzo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Kindamba baada ya Kampuni yake kuibuka washindi sekta ya mawasiliano, katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, yaliyoanza Juni 28 - Julai 8, 2017 ambapo kwa mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017,Maonesho hayo yamezinduliwa rasmi leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi tuzo kwa mwakilishi wa TPDC.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi tuzo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi kwa niaba ya moja ya taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi tuzo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Property International Bw. A. Haleem  ambao waliibuka washindi wa tatu wa jumla katika Maonyesho ya Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, yaliyoanza Juni 28 - Julai 8, 2017 ambapo kwa mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017, yaliyozinduliwa rasmi leo jijini Dar es salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Jeshi la Magereza Kutoa Elimu ya Namna ya kuanzisha Kilimo cha Kisasa kwa kutumia Maeneo Yenye Ufinyu wa Nafasi

$
0
0

Na Christina Mwangosi, MOHA

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Dk. Juma Malewa amesema Jeshi la Magereza nchini litatoa elimu ya namna kila Mtanzania hata aishie kwenye nyumba za ghorofa ama maeneo yenye nafasi ndogo ya kuanzisha kilimo cha mbogamboga, anavyoweza kutumia eneo dogo kuendeshea shughuli za kilimo cha mbogamboga wakati huu Maonyesho ya SabaSaba yanayoendelea katika Viwanja vya SabaSaba jijini Dar es salaam.

Kamishna Jenerali Dk. Malewa amesema kuwa pamoja na kuandaa Shamba Darasa kwa ajili ya kutoa elimu ya shughuli mbalimbali za kilimo, Jeshi la Magereza limeandaa bidhaa mbalimbali ambazo zitaonyeshwa wakati wote wa Maonyesho pamoja na kuuzwa wakati wote wa Maonyesho hayo.

Dk. Malewa amesema miongoni mwa bidhaa hizo ambazo ziko kwenye Banda la Magereza ni samani mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya ofisi na nyumbani ikiwemo makabati ya vyombo na nguo, meza na viti, madawati kwa ajili ya shule za msingi na sekondari, vitanda, sofa, ‘dressing table’ pamoja na viatu vya ngozi vya kike na kiume.

Amesema Jeshi la Magereza pia litauza pia majiko sanifu yanayotumia kuni kidogo, mashuka, foronya, vikoi pamoja na sabuni zenye ubora kwa ajili ya kufua nguo ambazo zinatengenezwa katika Kiwanda cha Sabuni kilichopo Mkoa wa Mbeya.

Amesema Jeshi la Magereza katika kipindi hiki cha Maonyesho litatoa elimu ya shughuli za kilimo cha kisasa bure na kwa wale wananchi ambao maeneo yao yanafikika Wataalamu wa Magereza wanaweza kuwatembelea wananchi kwenye maeneo yao na kuwafundisha namna ya kuanzisha kilimo hicho kinachojulikana kama ‘kilimo cha jikoni’.

Azam TV kuzindua app za televisheni leo

$
0
0

Kampuni ya Azam Media inazindua app za kisasa kwa ajili ya habari, michezo na matangazo ya televisheni. App hizo za aina yake katika mifumo ya Android na iOS, zinaanza kupatika leo Jumamosi kupitia Play Store ya Google na App Store ya Apple – unatakiwa kupakua app yenye rangi ya njano iliyoandikwa Azam Pay TV. 
Kupitia app hizo zilizosanifiwa kwa kuzingatia mahitaji ya wateja wa ndani na nje ya Tanzania zitakuwa na chaneli saba kwa kuanzia, ikitarajiwa chaneli nyingine zitaendelea kuongezwa.Chaneli hizo ni Azam One, Azam TWO, Sinema Zetu, Azam Sports HD, UTV, ZBC2 na Real Madrid.

CEO wa Azam Media, Tido Mhando, amesema app hizo zinatarajiwa kuleta mageuzi makubwa katika utoaji wa huduma za televesheni na kuendana na teknolojia ya kisasa katika soko. 
“Hatua hii tuliyofikia leo ni kielelezo tosha kuwa tunasikiliza wateja wetu wanataka nini na tunafanya jitihada kutoa huduma zilizo bora na zenye kukidhi viwango vinavyoendana na chapa Azam inayojulikana kote Afrika Mashariki kwa ubora,” ameeleza Mhando. 
Mhariri wa Masuala ya Mitandao wa Azam TV, Hassan Mhelela, amesema app hizo zimesanifiwa kuwa rahisi kuzitumia kwa kuzingatia umuhimu wa upatikanaji wa huduma za habari na televisheni kupitia vifaa vya mkononi. 
“Mfumo huu wa Azam TV app utawawezesha watu wengi zaidi kupata taarifa na kufuatilia vipindi vya kwenye televisheni kwa kutumia vifaa vya mkononi kama simu au tablet. Kinachotakiwa ni mtandao wenye nguvu unaokuwezesha kucheza video au kuangalia televisheni yaani streaming,” amesema Mhelela. 
Kwa kuanzia app hizo zinapatikana bure kwa yoyote mwenye kifaa chenye internet kinachotumia mfumo wa Android au iOS. 

Azam Media ni kampuni tanzu ya Bakhresa Group.


INVITATION TO SOKO FILAM MARKET

$
0
0

The SOKO FILAM market is a place for content producers, distributors, broadcasters and aggregators to network, do business and connect. 
For three days at the Park Hyatt Zanzibar there will be an exhibition with stands and meeting spaces, and at the Maru Maru Hotel there will be a conference programme of panel discussions and presentations. 
It is free to participate as a delegate, and you and your team can sign up here: http://www.ziff.or.tz/soko-filam/ 
A host of top industry names and experts have already confirmed their attendance and participation at the event, including: ShowMax, iflix video on demand, Citizen TV, Clouds TV, The Kenya Film and Classification Board, Riverwood, Uganda Film Commission, the African Film Consortium, Trace Mziki, RongaTV and Aya Distribution (UK) Udada Film Festival, Rotterdam Film Festival, African Voices Dubbing Company, MychoiceTV, Tibaz Productions, and Ubongo Productions amongst others. 
Top international speakers will also be attending, including well respected film industry expert, author and founder of the Africa in Motion Film Festival, Lizelle Bisschoff, Mykel Parish, President of the African Film Consortium, Dr. Ezekiel Mutua, from the Kenya Film Classification Board, Judd Ehrlich, Emmy Award winning documentary filmmaker, Priscilla Mlay, a filmmaker who has been working in the Tanzania film/TV industry since 2012, and Debra Zimmerman, the Executive Director of Women Make Movies, a non-profit NY based film organization that supports women filmmakers. CONFERENCE Panel discussions are free to attend and open to all REGISTERED SOKO FILAM DELEGATES. Registration MUST be one via the website: http://www.ziff.or.tz/soko-filam/

MICHUZI TV: RAIS DKT. MAGUFULI AISHAURI TANTRADE KUWEKEZA KATIKA VIWANDA

DIASPORA TALENT SHOW

LAPF WANG'ARA KATIKA UFUNGUZI WA MAONESHO YA SABASABA

$
0
0

 Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa hifadhi ya Jamii wa LAPF Bw. James Mlowe akizungumza na Mkurugenzi wa Afri Tea Blenders  Bw. Abdulhakim Mulla alipotembelea banda la maonyesho lililopo kaika maonesho ya Sabasba jijini Dar es Salaam
 Afisa Matekelezo wa LAPF Emmanuel Meisha akizungumza na mmoja wa Wateja wa LAPF ambae ameweza kufika katika banda la mfuko huo wa hifasdhi ya jami hili aweze kujiunga
 Afisa Matekelezo wa LAPF, Juma Venerando akitoa hudama kwa wateja waliofik katika banda la LAPF, Kupata huduma hili waweze kujiunga na mfuko huo


Wafanyakazi wa mfuko wa Pensheni wa LAPF wakiwa katika picha ya pamoja na tuzo ya ushindi wa kuwa mfuko bora wa hifadhi ya jamii katika maonesho ya Sabasba 2017

YALIYOJIRI KATIKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI LEO July 1, 2017

$
0
0

Serikali imesema itawachukulia hatua kali kwa wananchama wa vyama vya ushirika watakaobainika kutumia vibaya nafasi zao; https://youtu.be/EaFfpndBx5Y

Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kuanza kutumia mufumo mpya ulioboreshwa wa ukusanyaji tozo kwa njia ya kieletroniki; https://youtu.be/2nJ6snIRTh0?t=1

Wadau wa elimu kutoka mtandao wa elimu Tanzania wakuutana jijini Dar es Salaam kujadili namna ya kutoa elimu bora kwa watoto wa kike; https://youtu.be/lw08f-SnGCM

Mamlaka ya mapato Tanzania TRA yaongeza muda wa kulipia kodi ya majengo  kwa wadaiwa hadi July 15 mwaka huu. https://youtu.be/ii77cWnrRyM?t=1

Taasisi ya kupambana na rushwa Geita imemfikisha mahakamani  aliyekuwa afisa ugavi wa halmashauri ya Geita kwa matumizi mabaya ya ofisi. http://simu.tv/rhGNKRg

Waziri Prof.Makame Mbarawa afanya ziara katika ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage https://youtu.be/VLPCE01p5Hc

Chama cha wafanyabiashara wa Ujerumani kinatarajia kufungua ofisi zake nchini Tanzania katika kudumuisha urafiki na wafanyabiashara nchini; https://youtu.be/4bnjMRR8ym4?t=1
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images