Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live

ROSE TWEVE AENDELEA KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI MKOA WA IRINGA

$
0
0
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (CCM) amepanga kutumia zaidi ya Sh Milioni 60 kutoka katika mshahara wake kuwawezesha wanawake katika kata 107 za mkoa wa Iringa kuanzisha mifuko maalumu ya kuwezeshana kiuchumi.

Zaidi ya kata 40 za wilaya ya Iringa, Kilolo na Mufindi zimekwishanufaika na mpango huo unaokiwezesha kikundi cha wanawake katika kila kata kupata Sh 600,000 ambazo hazirudishwi. Akikabidhi kiasi hicho cha fedha kwa vikundi vya kata za Nyololo na Malangali, Tweve alisema zoezi hilo litaendelea katika kata zingine zote zilizobaki zitakazokamilisha taratibu mbalimbali ikiwemo ya kuunda uongozi wake na kufungua akaunti benki.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (CCM) akifurahi pamoja na wananchi wa kata ya Nyololo wakati wa muendelezo wa ziara yake kata 107 ya kuwahamisha wanawake wajiinue kiuchumi kwa kutumia vikundi pamoja na kuwawezesha kwa kuwapatia kiasi cha shilingi laki sita (600,000) kwa ajili ya kujiendeleza.

Tweve alisema kwa kupitia mifuko hiyo itakayojulikana kama mifuko ya Rose Tweve ya kila kata wanawake watajiwekea utaratibu wa kuweka na kukopa, kuinuana kimaendeleo na kubuni mambo mengine yatakayowazidishia kasi ya maendeleo yao. “Wanawake tupo wengi sana, lakini tunakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazoturudisha nyuma. Huu ndio muda wa kujipanga upya na kubadili maisha yetu kwa kutumia kauli mbiu ya rais wetu Dk John Magufuli ya Hapa Kazi tu,” alisema.

Alisema kutakuwepo na utaratibu wa kuvifanyia tathimini vikundi hivyo na vile vitakavyofanya vizuri vitapata nyongeza ya fedha kila mwaka kwa kupitia mpango huo na matokeo chanya yatakayojitokeza katika vikundi hivyo yatamshawishi atafute wafadhili wengine wa ndani na nje ili wasaidie zaidi.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (CCM) akizungumza na wananchi wa kata ya Nyololo wakati wa muendelezo wa ziara yake kata 107 ya kuwahamisha wanawake wajiinue kiuchumi kwa kutumia vikundi pamoja na kuwawezesha kwa kuwapatia kiasi cha shilingi laki sita (600,000) kwa ajili ya kujiendeleza.

“Nimeanzisha mpango huu kwa kutumia rasilimali zangu mwenyewe na kwangu mimi naona hili la kusaidia wanawake wenzangu kwa kutumia rasilimali zangu linawezekana, sitoi fedha hizi ili mgawane kwa matumizi yasiofaa, natoa kama jitihada zangu za kuwahamasisheni kuona haja ya kuwekeza kwa pamoja na kwa manufaa ya wote,” alisema.

Akishukuru kwa mchango huo, mmoja wa viongozi wa kikundi cha wanawake wa mfuko wa Rose Tweve wa kata ya Malangali, Judith Kisinini alisema wako katika mchakato wa kuanzisha duka la kuuza pembejeo za kilimo, hatua itakayowawezesha wanawake wakulima wa kata hiyo kupata huduma hiyo kwa gharama nafuu.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (CCM akikabidhiwa zawadi ya kitenge na wanawake wa kata ya Malangali Mkoa wa Iringa wakati wa muendelezo wa ziara yake kata 107 ya kuwahamisha wanawake wajiinue kiuchumi kwa kutumia vikundi pamoja na kuwawezesha kwa kuwapatia kiasi cha shilingi laki sita (600,000) kwa ajili ya kujiendeleza.

Kisinini alisema kikundi chao chenye wanachama zaidi ya 200 hadi sasa kimejiwekea taratibu mbalimbali za kufikia malengo yao na kila mwaka kila mwanachama atalazimika kuchangia sh 50,000 kama hisa. “Fedha hizo pamoja na michango ukiwemo wa mheshimiwa mbunge na faida tutakayokuwa tunapata kutoka katika shughuli tutakazokubaliana kufanya zitatumika kuendeleza wanachama wote bila ubaguzi wowote,” alisema.

Diwani wa kata ya Malangali ambaye pia ni katibu wa mbunge huyo, Shakila Salim aliunga mkono juhudi za mbunge huyo kwa kuvichangia vikundi hivyo Sh 100,000 kila kimoja na Tweve alikipongeza kikundi cha kata ya Mtitu wilayani Kilolo ambacho mapema mwaka huu alikipatia kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kutunisha mfuko wake ambao sasa una zaidi ya Sh Milioni 1.8.

Note Verbale on the Passing of Dr. Tonia Kandiero

WANANCHI JIJINI MWANZA WAFURIKA OFISI YA TRA KULIPIA KODI YA ARDHI

$
0
0
 Wananchi wa Jiji la Mwanza wakiwa wamefanya foleni nje ya Jengo la Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania Kanda ya Mwanza, kusubiri muda wao wa kwenda kulipia Kodi ya Ardhi ambayo leo Juni 30 ndio mwisho wa kulipia kwa wale ambao bado. hii ni kufuatia agizo la Serikali la kuhakikisha kila mmiliki wa nyumba analipia kodi hiyo na kwa wakati

WASHIRIKI WA SHINDANO LA BONGO STYLE WAENDESHEWA SEMINA KUHUSU PICHA,MITINDO NA UANDISHI WA FILAMU

$
0
0
Joyce Msigwa ambaye ni Mratibu wa Faru Arts and Sports Development Organization (FASDO) akitoa maelezo kwa washiriki wa 'Bongo Style Competition' 2017, kuhusiana na asasi ya FASDO.
Mwezeshaji Erick Chrispin akitoa semina kwa washiriki wa Bongo Style namna ya kujiongoza wenyewe katika maswala ya Fedha,Muda na uongozi.

Baadhi ya washiriki wa shindano la Bongo Style 2017, wakiwemo wapiga picha,waandishi wa miswada ya Filamu na wabunifu wa mitindo upande wa mavazi wakiwa wanafanya zoezi waliopewa na mwezeshaji Bw. Erick Chrispin (ambaye hayupo pichani)

Megawati 5000 kupatikana 2021, Ni baada ya kukamilika kwa mradi wa Stieglers Gorge

$
0
0
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani ( wa pili kulia mbele) akimwongoza Waziri wa Maji, Nishati na Umwagiliaji kutoka Ethiopia, Dk. Seleshi Bekele (katikati mbele) kwenye ziara ya kukagua eneo la ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za maji la Stiegler’s Gorge, Rufiji mkoani Pwani katika ziara hiyo.
Na Greyson Mwase, Rufiji.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani amesema Tanzania inatarajia kupata umeme wa uhakika wa Megawati 5000 ifikapo mwaka 2021, mara baada ya kukamilika kwa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia  nguvu za maji katika maporomoko ya maji ya Mto Rufiji kwenye  eneo la Stiegler’s Gorge  lililopo  Rufiji mkoani Pwani ambao utaongeza umeme wa kiasi cha Megawati 2100 katika  gridi ya taifa.

Dk. Kalemani aliyasema hayo jana tarehe 29 Juni, 2017 katika ziara ya Waziri wa Maji, Nishati na Umwagiliaji kutoka  Ethiopia, Dk. Seleshi Bekele aliyeambatana na wataalam wa masuala ya ujenzi wa mitambo  ya kuzalisha umeme kwa kutumia maji kutoka  Ethiopia kwenye eneo  la mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji ya Stieglers Gorge wilyani  Rufiji mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani akishuka kwenye boti kwa ajili ya kuelekea kwenye eneo la Stieglers Gorge kutakapojengwa mradi huo.

Wengine walioshiriki katika ziara hiyo ni pamoja na wataalam wa masuala ya  umeme na ujenzi wa mabwawa kutoka Tanzania,  Shirika la Umeme  Tanzania (TANESCO) na Wizara ya Nishati na Madini.  Ziara  hiyo inafuatia maombi ya  Rais John Magufuli kwa Waziri Mkuu wa Ethiopia ya kutuma wataalam wa masuala ya ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za maji kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na  wataalam wa masuala ya umeme na ujenzi wa mabwawa kutoka Tanzania.

Dk Kalemani alisema kuwa kupatikana kwa umeme wa uhakika ifikapo mwaka 2021 kutachochea ongezeko la viwanda hivyo kuongezeka kwa fursa za ajira na biashara na kukuza uchumi wa nchi.
Alisema mradi huo mkubwa ni moja ya mikakati ya Serikali  kuhakikisha nishati inakuwa na mchango mkubwa katika  kufikia malengo  ya  Dira ya Maendeleo ya Taifa yenye lengo la kuhakikisha kuwa nchi inatoka katika orodha ya nchi maskini duniani na kuingia katika orodha ya nchi zenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Waziri wa Maji, Nishati na Umwagiliaji kutoka Ethiopia, Dk. Seleshi Bekele (kushoto) akieleza jambo kwa Mhaidrolojia Mwandamizi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Stanislaus Kizzy (kulia) katika ziara hiyo. Anayesikiliza katikati ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani.

Alisisitiza kuwa mbali na mradi huo mkubwa, serikali imeweka mikakati ya kutumia vyanzo vingine vya nishati kama vile Gesi, Makaa ya Mawe, Jotoardhi, Upepo ili kuhakikisha kuwa nchi inapata umeme wa uhakika. Akielezea mafanikio ya mradi huo mbali na upatikanaji wa umeme wa uhakika, Dk. Kalemani alisema kuwa mradi huo utachochea ukuaji wa shughuli za uvuvi katika mkoa wa Pwani.

KIZIMBANI KWA KUMDANGANYA MCHUNGUZI WA TAKUKURU NA KUJIPATIA 105 MILIONI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Othman Mzange maarufu kama Julius Lyimo ama Anthony Mathew Hakalu amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kumdanganya mchunguzi wa Takukuru na kujipatia milioni 105 kwa njia ya udanganyifu.

Mshtakiwa amesomewa mashtaka yake na Wakili wa Serikali Mwandamizi Vitals Peter mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Godfrey Mwambapa.

Katika shtaka la kwanza imedaiwa kuwa,  tarehe  tofauti tofauti 2011, katika ofisi ya Takukuru Dar es salaam, wakiwa kwenye uchunguzi wa kesi namba PCCB/HQ/ENQ/07/2016 kwa mshtakiwa alimdanganya afisa uchunguzi wa Takukuru kwa kujitambulisha kwake kuwa yeye ni Antony Mathew Hakalu kwa nia ya kuficha uhalisia wake.

Imedaiwa kuwa, January 28,2009 katika Manispaa ya Kinondoni mshtakiwa kwa makusudi, aliwasilisha katika ofisi ya ardhi Manispaa ya Kinondoni barua yenye namba TIB/ORG/59/1/A ya Januari 2009 kwa madhumuni ya kuonyesha benki ya TIB ikiwa  kama mfilisi wa Tanzania Housing Bank(THB) imeuza ploti namba 596 iliyopo Mikocheni kwa Julius Lyimo.

Aidha, mshtakiwa anadaiwa siku na mahali hapo aliandika barua ya uongo kwa afisa ardhi wa Manispaa ya Kinondoni kwa madhumuni ya kuonesha Benki ya TIB ikiwa kama mfilisi wa THB imeuza ploti namba 596 iliyopo Mikocheni kwa Julius Lyimo.

Mshtakiwa huyo pia anadaiwa kuwasilisha hati ya kiapo ya uongo katika Manispaa hiyo kwa madhumuni ya kuonesha kiapo hicho kimeapwa na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kinondoni, M. Mriam ambayo ilikuwa ikisema Julius Lyimo amezaliwa mwaka 1952.

Mshtakiwa huyo kwa njia ya udanganyifu, alijipatia milioni 105 kutoka kwa Josia William Masonu kwa kujifanya yeye ni mmiliki wa hizo ploti namba 596 yenye hati namba 82320 L.O namba 350982 KMC/LD/5487 iliyopo Mikocheni Manispaa ya Kinondoni na kwamba alikuwa na uwezo wa kuiuza  kwa Josia, huku akijua kuwa siyo kweli.

Mshtakiwa amekana mashtaka hayo na amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka, upelelezi umekamilika na kesi hiyo itatajwa Julai 4, mwaka huu.

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 57 MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO JUNI 30, 2017

$
0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiongoza kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(TAMISEMI) Mhe,Selemani Jafo akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.

Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), wafanyika Dar.

$
0
0


Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Mh Charles Mwijage (kushoto), akizungumza na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Mh. Almas Maige (kulia), huku Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dk. Aggrey Mlimuka akisikiliza wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama hicho jijini Dar es Salaam jana.
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (wa pili kushoto) akilakiwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Almas Maige (kushoto), na Mratibu wa Mradi wa Mwanamke wa Wakati Ujao, Lilian Machera (kulia) alipokuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama hicho, Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Mama Jayne Nyimbo (wa pili kushoto), akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo wakati wa Mkutano Mkuuu wa Mwaka wa chama hicho jijini Dar es Salaam jana. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dk. Aggrey Mlimuka, aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Mhe. Almas Maige na Makamu Mwenyekiti mpya, Felix Kagisa.
Mkurugenzi​Mtendaji ​ wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Dk. Aggrey Mlimuka (kushoto), akiwa na baadhi ya maofisa wa chama hicho wakati zoezi la kuhesabu kura likiendelea. 


DC MKURANGA AZINDUA JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE WA WILAYA HIYO

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbert Sanga amewataka wanawake wa Wilaya hiyo kuachana na masuala ya utegemezi kwa wanaume na zaidi wajikite katika kujiendeleza kiuchumi kwa kuanzisha miradi midogo midogo ikiwemo kuanzisha vikundi vya ujasiriamali  ikiwa ni katika kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ya kila Wilaya kuwa na vikundi vya kujiinua kiuchumi..

Amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji wanawake lililofanyika jana na kuvikutanisha zaidi ya vikundi 30 kutoka Wilaya ya Mkuranga na kuelezea matatizo wanayokumbana katika vikundi vyao.

Sanga amewaambia kuwa wanawake bila kuwezeshwa wanaweza wakajiendeleza wenyewe kwani utakapomuelimisha mwanamk mmoja utakuwa umeelimisha watu wnegi sana.

"wanawake mkijiwezesha wenyewe mnaweza sio lazima muwezeshwe kwani tunachoamini ni kuwa ukimuelimisha mwanamke umeelimisha dunia kwani nyinyi ndiyo msingi mkubwa wa familia katika jamii zinazotuzunguka mtakapoamua kukaa na kutokujishughulisha basi hakutakuwa na msingi mzuri wa kizazi kijacho,"amesem Sanga.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji  WanawakeWilaya ya Mkuranga Mariam Ulega alisema kuwa anashukuru sana kwa Mkuu wa Wilaya kuja kuwazindulia jukwaa lao na cha zaidi kwa kuwa wameshapatikana viongozi wa Jukwaa hilo kwa wilaya ya Mkuranga na zaidi anaomba umoja na ushirikiano kutoka kwa wakina mama kutoka kata mbalimbali ili kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.

Kabla ya kuzinduliwa kwa jukwaa hilo ulifanyika uchaguzi na kupatikana kwa Mwenyekiti Mariam Ulega. 
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbert Sanga akizindua Jukwaa la Uwezeshaji wanawake lililofanyika jana na kuwasihi wanawake kuachana na masuala ya utegemezi zaidi wanatakiwa kujiendeleza ili kujiinua kiuchumi na pia kuviendeleza vikundi vyao na kuvisajili ikiwa ni katika kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ya kila Wilaya kuwa na vikundi vya kujiinua kiuchumi.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Wilaya ya Mkuranga Mariam Ulega akizungumza na wakina mama wa wilaya hiyo kutoka kata mbalimbali kuhusiana na kuviendeleza vikundi vyao kwa ajili ya kuacha kuwa tegemezi kwa wanaume ikiwa ni katika kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ya kila Wilaya kuwa na vikundi vya kujiinua kiuchumi.


 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbert Sanga akipokea maandamano ya wakina mama wa Mkuranga wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji wanawake lililofanyika jana na kuwasihi wanawake kuachana na masuala ya utegemezi zaidi wanatakiwa kujiendeleza ili kujiinua kiuchumi na pia kuviendeleza vikundi vyao na kuvisajili ikiwa ni katika kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ya kila Wilaya kuwa na vikundi vya kujiinua kiuchumi.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAHALIFU WANNE WAUWAWA KATIKA MAPAMBANO NA POLISI KIBITI

$
0
0
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua wahalifu wanne wanaosadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji katika mapambano yaliyodumu kwa zaidi ya nusu saa katika kijiji cha Pagae wilayani Kibiti mkoani Pwani.

Akielezea tukio hilo Mkuu wa Oparesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema tukio hilo lilitokea siku ya Alhamisi juni 29 majira ya saa tatu usiku kwenye barabara ya vumbi itokayo Pagae kuelekea Nyambunda ambapo Askari Polisi wakiwa doria walikutana na kikundi cha watu kinachokadiriwa kuwa na watu sita ambapo wahalifu hao baada ya kuona gari la Polisi walikimbilia vichakani na kuanza kuwarushia risasi Polisi.

Sabas alisema baada ya hali hiyo kutokea Askari nao kwa ujasiri walijibu na mapambano hayo yalidumu kwa zaidi ya nusu saa ambapo Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu wanne kwa risasi ambao baadaye walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali.

“Katika tukio hilo tumefanikiwa kupata silaha mbili aina ya SMG na magazine mbili pamoja na risasi 17 zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao na hii ni dalili kuwa tunaendelea vizuri na oparesheni yetu ambayo inashirikisha vyombo vingine vya ulinzi na Usalama katika wilaya hizi tatu za Mkuranga, Kibiti, na Rufiji” Alisema Sabas.

Aidha Sabas ametoa wito kwa wahalifu wengine kuacha mara moja kufanya vitendo hivyo kwa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kufanya jitihada zote za kuhakikisha kuwa maeneo hayo yanakuwa salama na wananchi wanaishi katika hali ya amani na usalama.

Vilevile amewataka wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana wahalifu wengine ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anaishi kwa usalama ambapo kwa ambaye atakayetoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa wahalifu hao kiasi cha shilingi milioni kumi kitatolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro.
MKUU WA OPERESHENI ZA POLISI, NAIBU KAMISHNA DCP LIBERATUS SABAS, AKIONYESHA BUNDUKI AINA YA SMG ZILIZOPATIKANA JUZI USIKU WAKATI WA MAPAMBANO YA KURUSHIANA RISASI BAINA YA WAHALIFU NA POLISI KATIKA KIJIJI CHA PAGAE WILAYANI KIBITI MKOANI PWANI. BUNDUKI 2 AINA YA SMG ZILIPATIKANA PAMOJA NA MAGAZINI 2 NA RISASI 17. PICHA NA HASSAN MNDEME-JESHI LA POLISI.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA NORWAY BORGE BRENDE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende wanne kutoka (kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga wanne kutoka (kulia)pamoja na vingozi wengine wa Tanzania na Norway mara baada ya mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwatazama Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende wakati akizungumza jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

TANGAZO KWA UMMA

$
0
0

Menejimenti ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF inapenda kuwafahamisha Wanachama na Umma kwa ujumla kuwa Ofisi ya Kanda ya Dar es Salaam iliyopo Mtaa wa Mkwepu, Jengo la Diplomatic House, katikati ya jiji la Dar es Salaam itahamia rasmi kwenye jengo la LAPF Millenium Towers, ghorofa ya tatu, lililopo barabara ya Ali Hassan mwinyi eneo la Makumbusho kuanzia tarehe 01/07/2017. Hivyo wanachama na wadau wote wa Mfuko wataendelea kupata huduma kulingana na matarajio yao katika mazingira yaliyoboreshwa zaidi. Karibuni sana tuwahudumie.




“Ishi na Staafu kwa Ufahari na LAPF”

MAEGESHO YA KIVUKO LINDI KUKAMILIKA MWEZI NOVEMBA MWAKA HUU

$
0
0
Serikali imesema ujenzi wa maegesho ya kivuko Mkoani Lindi utakamilika mwezi Novemba mwaka huu ili kurahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo kwa wakazi wa eneo la Kitunda Mkoani Lindi.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alipokagua maendeleo ya ujenzi wa maegesho hayo na kusema ujenzi huo umegharimu kiasi cha Tsh, bilioni 1.8 ambazo zitahusisha maegesho ya Kivuko na kujenga barabara ya kiwango cha lami mita 150 upande wa Kitunda Mkoani Lindi.

‘Tuliahidi na sasa tunatekeleza, nimefurahi kuona ujenzi unaendelea vizuri na ninawahakikishia mwezi Novemba tutakuja kuzindua kivuko’ alisema WazirI Profesa Mbarawa.

Aidha,Waziri Mbarawa amemtaka Mkandarasi anaejenga magesho hayo kuzingatia thamani ya fedha wakati wa ujenzi wake ili mradi huo uweze kudumu kwa muda mrefu.

‘hakikisha unajenga maegesho haya kwa kuzingatia viwango tulivyokubaliana, hatutaki kuona kasoro mara tu baada ya mwezi mmoja, hizi ni fedha za walipa kodi na tunategemea miundombinu hii ikae muda mrefu’ alisisitiza Waziri Prof. MBARAWA.

Kwa upande wake Msimamizi wa Mradi huo, Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), mkoa wa Lindi, Eng. Issack Mwanawima amemuhakikishia Waziri Profesa Mbarawa kuwa watasimamia mradi kwa kuzingatia viwango katika ujenzi huo na kuhakikisha unakamilika kama mkataba unavyosema.
Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS). Mkoa wa Lindi,Eng. Issack Mwanawima (mwenye koti la draft), akimweleza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa maegesho hayo, Mkoani humo, wakati Waziri huyo alipotembelea mradi huo hivi karibuni.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), akiangalia ujenzi wa wa maegesho ya kivuko unaojengwa katika mkoa wa Lindi alipotembelea mradi huo hivi karibuni. Mradi huo utahusisha maegesho ya kivuko na ujenzi wa mita 150 za barabara ya lami upande wa Kitunda.
Tinga Tinga likiendelea na ujenzi wa maegesho ya kivuko Mkoani lindi. Ujenzi wa maegesho hayo unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu.
Meneja wa Bandari ya Mtwara, Eng. Juma Kijavara (katikati), akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), eneo la gati ya Lindi ambalo litatakiwa kuchimbwa ili kuongeza kina cha gati hilo, alipotembelea gati hiyo hivi karibuni.

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA UMOJA WA WANAMICHEZO WA MPIRA WA MIGUU KUTOKA FC GRACE UNITED STATES LEO OFISINI KWAKE MJINI DODOMA.

$
0
0
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akizungumza pale ugeni kutoka Umoja wa Wanamichezo wa Mpira wa Miguu kutoka FC GRACE UNITED STATES ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. wa pili kulia ni Mwenyeji na kiongozi wa Msafara Bishop Oscar John.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikat) akimsikiliza Mheshimiwa William Ngeleja akizungumza wakati Umoja wa Wanamichezo wa Mpira wa Miguu kutoka FC GRACE UNITED STATES ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akimsikiliza Bishop Oscar John (aliesimama) akizungumza, pale ugeni kutoka Umoja wa Wanamichezo wa Mpira wa Miguu kutoka FC GRACE UNITED STATES ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akizungumza na ugeni kutoka Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania ulioongozwa na Rais wa Chama hicho Ndg. Mwadini Jecha (katikati) na Mratibu wa Mawasiliano Ndg. Anne kilimo (kushoto) uliomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Washindi wa Medali za Dhahabu katika Mashindano ya kimataifa ya Mazingira na Sayansi yaliyofanyika hivi karibuni nchini Marekani. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shule ya Wavulana ya Feza Ndg. Ibrahim Rashid, anaefuata ni Ndg. Rashid Kikwete, kulia ni Mhe. Hawa Ghasia, wa pili kulia ni Ndg. Kassi Nkamia na watatu kulia ni Ndg. Abdallah Rubeya, waliotembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.

TANZANIA NA NORWAY KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA SIASA NA DIPLOMASIA

$
0
0
 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ameeleza kuwa kusainiwa kwa Mkataba wa Makubaliano (MoU) kuhusu kushirikiana katika Mashauriano ya Kisiasa na Kidiplomasia kati ya Tanzania na Norway kumefungua sura mpya ya mahusiano kati ya nchi hizo mbili. 

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar Es Salaam wakati anaongea na waandishi wa habari baada ya shughuli ya uwekaji saini wa makubaliano hayo aliyoifanya kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Mhe. Borge Brende kukamilika.

Alisema kusainiwa kwa MoU hiyo kutazifanya nchi hizo kuwa na mahusiano ya karibu zaidi katika kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya kisiasa na kidiplomasia ambayo kimsingi yalikuwepo tokea zamani lakini leo yamerasimishwa. 

Mhe. Mahiga amewambia wanahabari kuwa Tanzania na Norway zimekuwa zikishirikiana kiuchumi, kiteknolojia na kijamii kwa takribani miaka 55 sasa. Baadhi ya maeneo aliyoyataja ambayo nchi hizo zimekuwa zikishirikiana katika kipindi hicho ni pamoja na uzalishaji wa nishati ya umeme hususan vijijini, afya, elimu, kilimo na utunzaji wa misitu. 

Mhe. Mahiga aliendelea kueleza kuwa katika kikao chao, wamejadili maeneo mapya ya ushirikiano yakiwemo utunzaji wa mazingira na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa sekta binafsi za nchi hizo mbili kinyume na awali mahusiano zaidi yalikuwa baina ya Serikali mbili.

Waziri Mahiga ameishukuru Norway kwa jitihada zake ziliozasaidia uvumbuzi na uchimbaji wa gesi asilia nchini kupitia kampuni ya Statoil ambayo imewekeza nchini mtaji mkubwa kuliko mahali popote Afrika.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufalme wa Norway, Mhe. Borge Brende wakiweka saini Mkataba wa Makubaliano kuhusu kushirikiana katika Mashauriano ya Kisiasa na Kidiplomasia kati ya Tanzania na Norway.Ttukio hilo lilifanyika jijini Dar Es Salaam kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere na kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Norway mwenye makazi yake nchini Sweden, Mhe. Dora Msechu, Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne Marie Kaarstad, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya, Bi. Mary Matari, pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga (hawapo pichani). 
Waheshimiwa Mawaziri wakibadilishana mikataba mara baada ya kuweka saini.


JNIA TBIII Kuanza Kutumika Dec 2018-Mhe. Mbarawa

$
0
0
Prof. Ninatubu Lema, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, (aliyenyoosha mikono) akimweleza jambo Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kutoka kulia), leo wakati akianza ziara ya kutembelea jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA_TBIII).
Meneja wa Mradi wa Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), Bw. Ray Blumrick (kushoto) akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwenye ujenzi wa jengo hilo, ambapo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbarawa (wa tatu kutoka kushoto) akimsikiliza kwa makini.
Mhandisi Simba Charles (aliyenyoosha mkono) akionesha eneo la maegesho ya magari kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati), leo alipofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Bw. Ray Blumrick, Meneja Mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII) akimwelekeza namna paa lilivyo imara, Prof. Makame Mbarawa (Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano) aliyetazama juu katikati wakati wa ziara yake kwenye jengo hilo leo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri (MAB) ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Prof Ninatubu Lema akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (wa pili kutoka kushoto) leo alipofanya ziara ya kutembelea jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa TAA, Bw. Richard Malulu.

Viongozi wa Dini kanda ya Ziwa Wabebeshwa mzigo, Utunzaji wa Mazingira Ziwa Victoria

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt. Charles Mlingwa, akifungua kikao hicho, pembeni kulia ni Mratibu wa LVEMP Bw. Omari Myanza.
Na Atley Kuni,  Mwanza.

Serikali mkoani hapa, imewapa jukumu kubwa viongozi wa dini kutoka baadhi ya mikoa ya kanda ya ziwa kuhakikisha wanakuwa bega kwa bega katika kulitunza ziwa Viktoria na Maliasili zake ili liweze kuwa tegemeo kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Akifungua Semina ya siku moja mkoani hapa Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, na risala yake kusomwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt. Charles Mlingwa, Mongella amesema, viongozi wa dini wanalo jukumu kubwa kwani wao husimamia imani za watu.
Baba Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo katoliki Musoma Mkoani Mara akiongea na Waandishi wa habari nje ya Mkutano huo kuelezea umuhimu wa mazingira.

“Ninyi Viongozi wa dini dhima mliyonayo ndani ya jamii ni kubwa sana na chochote mtakacho waelekeza waumini wenu lazima waweze kukitekeleza, hivyo niwaombe sana viongozi wangu tulilinde ziwa viktoria kwa jitihada zetu zote’’ alisema Mongella.

Aidha Mongella amesema kuwa, kuwepo kwa Ziwa Victoria ni fursa ya uendelezaji ya kauli mbiu ya “Tanzania ya Viwanda” ambayo Serikali ya awamu ya Tano inasisitiza, “Ziwa hili linasaidia upatikanaji wa rasilimali zinazotumika kwa matumizi ya nyumbani na viwandani, usafiri na usafirishaji na uzalishaji wa nishati ya umeme Hivyo basi hatuna budi kuhifadhi mazingira ya Ziwa na Bonde lake” amesisitiza Mkuu huyo wa mkoa.

Kwa upande wao, viongozi wa dini wakiongea wamesema, wao wanatambua na hata vitabu vya dini vinaelekeza juu ya mwanadamu anachopaswa kufanya katika kulinda mazingira ikiwepo ziwa Viktoria.
Sheik Hassan Kabeke, akiafafnua jambo kwa waandishi wa habari nje ya Warsha hiyo namna suala la mazingira linavyo tajwa katika Kuran tukufu.

Mwenyekiti mwenza wa Kamati ya amani ya madhehebu ya dini katika Mkoa wa Mwanza, Sheik Hassan Kabeke, amesema katika Uislam na hususan ni katika mafundisho ya Mtume Muhama S.A.W, inafafanua juu ya mito miwili yaani mto Nile na Furabu ambayo mtume aliipitia huku akisema kwamba, Mto Nile ambao unafungamanishwa na Ziwa Viktoria Mtume amesisitiza kuyatunza mazingira, “Katika kupanda miti kwenye uislamu mtu hupata thawabu, tunaimani kabisa kwamba kila mmoja wetu akitunza mazingira ni sehemu ya Ibada, amesema Kabeke. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Mwanafunzi wa TEKU mkoani Mbeya ang’arishwa na Milioni 20 za Biko

$
0
0
WAENDESHAJI wa bahati nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku’, leo wamemkabidhi Sh Milioni 20 mshindi wao wa droo ya 18, Linda Mhewa, ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji University (TEKU), kilichopo jijini Mbeya.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mhewa aliyetangazwa kuwa mshindi wa donge nono la Milioni 20, alisema kwamba ni furaha yake kuona Mungu amemchagua katika bahati nasibu hiyo inayotikisa hapa nchini tangu kuanzishwa kwake.

Alisema amekuwa mchezaji mzuri wa Biko, huku akiamini kuwa kushinda kwake ni sehemu ya kubadilisha maisha yake kiuchumi jambo ambalo ndilo alilokusudia kiasi cha kuamua kucheza Biko.

“Wakati napigiwa simu na Kajala sijaamini kabisa, nikaamini baada ya kuona ni kweli hususan baada ya kukabidhiwa fedha zangu ikiwa ni matokeo ya kucheza kwangu Biko, huku ukiwa mchezo rahisi kwa sababu kwa kutumia simu za mikononi za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kwa kuingiza namba ya kampuni 505050 na ile ya kumbukumbu 2456, huku kianzio cha kucheza kikianzia Sh 1,000 na kuendelea,” Alisema Mhewa.

Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alimpongeza mshindi wao wa jijini Mbeya, huku akimtaka ahakikishe kuwa uchumi wake unakua kwa kuhakikisha kwamba anazitumia vyema fedha alizoshinda kutoka kwenye bahati nasibu yao.

“Ni jambo zuri kuinuka kiuchumi kwa kupitia mchezo huu wa kubahatisha wa Biko, ambapo tumeshuhudia mamia ya Watanzania wakiibuka kidedea katika droo za wiki pamoja na ushindi wa papo kwa hapo unaotoka kila dakika,” Alisema.

Kwa mwezi Mei pekee, zaidi ya Sh Milioni 500 zimetolewa kwa washindi, huku donge nono la Sh Milioni 20 likienda kwa washindi wawili kwa droo ya Jumatano na Jumapili.

Mshindi wa droo ya 18 ya Biko, Linda Mhewa, akiwa anazishangaa fedha zake kiasi cha Sh Milioni 20 alizokabidhiwa na waendeshaji wa bahati nasibu hiyo ya Biko Tanzania, leo jijini Mbeya.
Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Paul William Ntinika mwenye suti, akimpongeza mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko, Linda Mhewa, aliyeibuka kidedea katika droo ya 18 iliyochezeshwa Jumatano iliyopita. Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Mbeya. Kushoto aliyeshika kipaza sauti ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven. Kulia ni Afisa wa Benki ya NMB, jijini Mbeya. Picha na Mpigapicha wetu Mbeya.

Mwanafunzi huyo ambaye ni msichana wa pili kufanikiwa kuzoa mamilioni ya Biko kupitia bahati nasibu ya Biko, aling’ara katika droo ya Jumatano iliyopita, ikiwa ni mwendelezo wa bahati nasibu hiyo kumwaga mamilioni kwa kupitia mchezo wao unaotoa zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, bila kusahau droo kubwa ya Jumatano na Jumapili ya Sh Milioni 20.
Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven kushoto, akimkabidhi hundi ya Sh Milioni 20 mshindi wao Linda Mhewa wa pili kutoka kushoto.

SPIKA WA BUNGE NDUGAI AKIFATILIA KWA UMAKINI MISWADA YA MALIASILI

$
0
0

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akifuatilia mjadala katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Pamoja iliyokuwa ikijadili miswada miwili ya sheria kuhusiana na usimamizi wa maliasili za Nchi.kikao hicho kilifanyika Mjini Dodoma jana Katika Ukumbi wa Msekwa.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akifuatilia mjadala katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Pamoja iliyokuwa ikijadili miswada miwili ya sheria kuhusiana na usimamizi wa maliasili za Nchi.kikao hicho kilifanyika Mjini Dodoma jana Katika Ukumbi wa Msekwa.

Wazazi wachangamkia Toto Afya Kadi ya NHIF

$
0
0
Wananchi mbalimbali wakipata huduma kwenye banda la NHIF ambapo kampeni ya usajili wa Toto Afya Kadi unafanyika. 

Na Mwandishi Wetu

KAMPENI ya usajili wa watoto chini ya Umri wa miaka 18 unaofanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwenye maonesho ya 41 ya Sabasaba, umekuwa kivutio kikubwa ambapo wazazi na walezi wamepongeza mpango huo.

NHIF inaendesha kampeni hiyo chini ya mpango wa Toto Afya Kadi ambapo wazazi na walezi wanawasajili watoto wao kwa gharama ya shilingi 50,400 na kupatiwa kitambulisho cha matibabu kitakachomwezesha kupata huduma hizo ndani ya nchi.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Ushauri wa Kiufundi Dr. Aifena Mramba akitoa maelezo kwa wananchi waliofika bandani hapo. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti bandani hapo, Mkazi wa Kinondoni Bw. Ally Raymond amepongeza Mfuko kwa kuja na mpango huo ambao umekuwa ni wa nafuaa kwa wazazi na walezi ambao hawakuwa na fursa ya kupata huduma hizo.

“Kwa kweli hii ni hatua kubwa lazima tuwapongeze hasa kwa kuwajali watoto hawa chini ya umri wa miaka 18 ambao hasa ndio wana uhitaji mkubwa wa matibabu hivyo name nitoe wito kwa wazazi wengine kutumia fursa hii ili kuwa na uhakika wa matibabu wa watoto wao,” alisema Bw. Raymond.

Mzazi mwingine alipongeza hatua ya NHIF ya kusajili na kutoa vitambulisho hivyo baada ya siku moja hatua ambayo imeondoa usumbufu kwa wanaohitaji kusajili watoto wao.
Usajili wa Toto Afya Kadi ukiendelea. 

Akizungumza bandani hapo Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti, Bi. Angela Mziray alisema kuwa hii ni fursa nzuri kwa wazazi na walezi ya kupata vitambulisho vya matibabu na kuwa na uhakika wa kupata matibabu wakati wowote na kuondokana na usumbufu ambao wangeweza kuupata.

Alisema kuwa NHIF imeanzisha mpango huo kutokana na umuhimu wa kundi la watoto ambao wameonekana kuwa na uhitaji mkubwa wa kulindwa kwa kuhakikishiwa huduma za matibabu. Jumla ya watoto 150 wameshasajiliwa na kupatiwa vitambulisho vyao.

Mbali na huduma ya usajili wa watoto, Mfuko pia unatoa huduma ya elimu kwa juu ya huduma za Bima ya Afya lakini pia kushughulikia kero mbalimbali za wanachama.
Wananchi wakilipia gharama za usajili wa Toto Afya Kadi kwa Maofisa wa Benki ya NMB.

Viewing all 110029 articles
Browse latest View live




Latest Images