Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1777 | 1778 | (Page 1779) | 1780 | 1781 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli (katikati), akimkabidhi Tuzo ya Ushindi wa Kwanza kwa Mashirika yatoayo huduma katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deogratius Kwiyukwa, Viwanja vya Sabasaba, Kilwa Road jijini Dar es Salaam leo, wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo. Kulia anayesaidia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijange.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli (kulia), akimkabidhi Tuzo ya Ushindi wa Kwanza kwa Mashirika yatoayo huduma katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deogratius Kwiyukwa, Viwanja vya Sabasaba, Kilwa Road jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo leo. 
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deogratius Kwiyukwa (katikati), akiwa ameishikilia Tuzo ya Ushindi wa Kwanza kwa Mashirika yatoayo huduma katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Viwanja vya Sabasaba, Kilwa Road jijini Dar es Salaam pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo, mara baada ya kukabidhiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo leo. 
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deogratius Kwiyukwa (wa tatu kushoto), akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Dk. Haruni Kondo (wa tatu kulia), Tuzo ya Ushindi wa Kwanza kwa Mashirika yatoayo huduma katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Viwanja vya Sabasaba, mara baada ya kukabidhiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo, jijini leo. 
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deogratius Kwiyukwa (kushoto), akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Dk. Haruni Kondo (kulia), kwenye banda la shirika katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Viwanja vya Sabasaba, jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia  katika kilele cha  Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani kwenye ukumbi wa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma
   Waziiri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sampuli mbalimbali za korosho katika wakati alipotembelea banda la Ushirika wa Ruangwa, Nachingwea Liwale Cooperative Union (RUNALI) Limited  katika kilele cha  Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani kwenye ukumbi wa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma Julai 30, 2017. Kushoto  kwake ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba na kushoto kwa Waziri ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Convenant, Sabetha Mwambenja
   Bendi ya Jeshi la Kujenga Taifa ikiongoza maandamano katika kilele cha  Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba (katikati) na Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. Tate William Ole- Nasha baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma  kuhutubia katika kilele cha  Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani kwenye ukumbi wa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma

  0 0  0 0

   Msanii wa Muziki wa Kughani Mrisho mpoto akitoa burudani kwa wadau katika Viwanja vya Maonyesho vya Sabasaba kwa kuwakumbusha juu ya Utalii wa ndani kwa kutembelea Hifadhi ya bonde la Ngorongoro hili kuweza kujionea vivutio Mbalimbali
   Mwanamuziki BizMan wa InAfrica Band akipiga Kinanda cha wimbo wa Mrisho Mpoto katika onesho la kuwakaribisha watu katika bonde la Ngorongoro kujionea vivutio vilivyo na maajabu saba ya Dunia


  Waimbaji wa bendi ya Mpoto Theatre ,Ismail na Fery wakiimba wimbo wa waite  katika onesho la kuwakaribisha watu katika bonde la Ngorongoro kujionea vivutio vilivyo na maajabu saba ya Dunia

   Msanii Stara Thomas akiimba pamoja na Mrisho Mpoto katika shoo kuwakaribisha watu katika bonde la Ngorongoro kujionea vivutio vilivyo na maajabu saba ya Dunia iliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba
   Wasanii wa kikundi cha Mpoto Theatre Group wakitoa burudani kwa wadau kuwakaribisha watu katika bonde la Ngorongoro kujionea vivutio vilivyo na maajabu saba ya Dunia iliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba
   Wasanii wa bendi ya In Africa wakimsindikiza Mrisho mpoto kuwakaribisha watu katika bonde la Ngorongoro kujionea vivutio vilivyo na maajabu saba ya Dunia iliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba
   Mpiga Tumba wa InAfrica Band  Ras Pompidou akipiga tumba kuwakaribisha watu katika bonde la Ngorongoro kujionea vivutio vilivyo na maajabu saba ya Dunia iliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba
   Sehemu ya wadau kutoka bonde la Ngorongoro  wakiwa wanafuatilia shoo ya Mrisho Mpoto
   Mpiga gitaa wa InAfrica band Roy Figuiredo ambao wameshirikina a  Mpoto Theatre wakati wa kuwakaribisha watu katika bonde la Ngorongoro kujionea vivutio vilivyo na maajabu saba ya Dunia iliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba
  0 0


  0 0

  Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, iliyokutana leo Jumamosi Julai 01, 2017 kwenye ofisi za TFF, Dar es Salaam imempitisha Wallace Karia (kushoto) kuwa Kaimu Rais wa shirikisho. 
  Kadhalika, Kamati hiyo ya Utendaji ya TFF, imempitisha Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi (kulia) kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF.
  Viongozi hao watakaimu nafasi hizo tajwa hadi hapo mahakama itakavyoamua kuhusu kesi zinazowakabili kwa sasa Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu, Mwesigwa Selestine. 
  Kamati ya Utendaji ya TFF, imekutana kwa dharura kwa mujibu wa Ibara ya 35 (1) inayosomwa pamoja na Ibara ya 35 (6) na kufanya uamuzi huo.

  WAPITISHWA KUWANIA NAFASI MBALIMBALI TWFA
  Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu kwa Wanawake (TWFA), imetangaza majina ya wagombea 11 waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa chama hicho utakaofanyika Agosti 5, mwaka huu mkoani Morogoro.
  Majina ambayo yamepitishwa ni Amina Karuma, Rose Kisiwa, Somoe Ng’itu, Theresia Mung’ong’o, Hilda Masanche, Salma Wajeso, Zena Chande, Triphonia Temba, Mwamvita Kiyogoma, Jasmin Soudy na Chichi Mwidege.
  Nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji.

  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO 
  LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

  0 0

  Benny Mwaipaja, WFM-Dar es Salaam
  BENKI ya Dunia imeipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kusaidia mpango wa Serikali wa miaka 11 wa Elimu bila malipo kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari nchini.
  Kiasi hicho cha fedha ni nyongeza ya Dola milioni 122 zilizotolewa na Benki hiyo katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa maboresho ya elimu kupitia Mpango wa Tekeleza kwa Matokeo Makubwa sasa-BRN, uliolenga kuondoa changamoto za elimu nchini.
  Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bella Bird amesema wakati wa utiaji saini mkataba wa nyongeza ya fedha hizo kati yake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, kuwa nyongeza ya Dola milioni 80 imetokana na Benki hiyo kuridhishwa na namna Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dokt. John Pombe Magufuli, ilivyosimamia kikamilifu mpango huo wa utoaji elimu bure na kuwanufaisha wanafunzi wengi wakiwemo wanaotoka katika familia masikini.
  Amesema kuwa uamuzi huo umesababisha ongezeko kubwa la wanafunzi wanaojiunga na elimu ya msingi, kuongezeka kwa ufaulu, wanafunzi kujua maarifa ya hesabu, kusoma na kuandika, utoaji wa ruzuku  ya elimu kwa wakati, hatua ambayo pia imesababisha kuwepo kwa changamoto za ukosefu wa miundombinu ya shule, changamoto ambazo anaamini zinapungua kupitia mkopo huo wenye masharti nafuu.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James ameishukuru Benki ya Dunia kwa kutoa fedha hizo ambazo amesema zitasaidia kwa kiasi kikubwa mipango ya Serikali ya kuboresha elimu nchini na kuondoa changamoto zinazoukabili mpango huo likiwemo ongezeko hilo kubwa la wanafunzi.
  Bw. James ameeleza kuwa fedha hizo zitasaidia ujenzi wa miundombinu ya madarasa, ubora wa eimu, ukaguzi wa shule, upelekaji wa walimu, na kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu ili waweze kupata haki hiyo ya msingi ya elimu.
  Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila, amesema kuwa katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa elimu wa lipa kulingana na matokeo upitia mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 122 zimetumika kujenga madarasa 1,400, matundu 3,390 ya vyoo, mabweni 261, majengo ya utawala 9, mabwalo ya chakula 9 nyumba za walimu 11, uchimaji wa visima vya maji katika shule nne na kukarabati vyuo vya ualimu.
  Amesema kuwa  mkopo mpya wa dola za Marekani milioni 80 uliotolewa na Benki ya Dunia hata kabla ya awamu ya kwanza ya mradi huo kumalizika hapo mwakani, umeonesha nia ya dhati ya Benki ya Dunia kusaidia maendeleo ya elimu nchini.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (Kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bella Bird, wakitia saini makubaliano ya Benki ya Dunia kuipatia Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na sekondari kupitia mpango wa  lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (Kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bella Bird, wakitia saini makubaliano ya Benki ya Dunia kuipatia Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na sekondari kupitia mpango wa  lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (Kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bella Bird, wakibadilishana hati (mkataba) ya mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na sekondari kupitia mpango wa  lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw, Doto James akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kutia saini makubaliano na Benki ya Dunia ya kuipatia Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na sekondari kupitia mpango wa  lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bi. Bella Bird, akisisitiza jambo mbele ya  waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kusaini makubaliano ya Benki yake ya kuipatia Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na sekondari kupitia mpango wa  lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

  0 0

  Na Ofisa Habari Mufindi
  Serikali Wilayani Mufindi, amewataka vijana waliohitimu mafunzo ya awali ya kujitolea ya Jeshi la kujenga Taifa JKT kikosi cha 841 Mafinga, kuwa walinzi namba moja wa amani katika jamii zao, kwa kuwafichua waharifu watakao jaribu kuhatarisha amani na utulivu uliopo nchini kwa sasa .
  Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh. Jamhuri William, wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana waliokuwa wakihudhuria mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa kutoka kikosi cha 841 kilichopo Mjini Mafinga Wilayani Mufindi.
   “ kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na maadui wa nje na ndani ya nchi wanaojaribu kuvunja Amani na utulivu uliostawi kwa muda mrefu hapa nchini, hivyo, nawaagiza  Mkalinde  kiapo chenu cha utii nauadilifu kwa Taifa na Mkuu wa nchi kwa kutekeleza sera ya Taifa inayotanabaisha kuwa  kila raia wa Tanzania ni Mlinzi wa nchi yake”
  Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amewaasa vijana watakao pata fursa ya kuajiriwa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama mara baada ya kuhitimu mafunzo, wakafanye kazi kwa nidhamu, uadilifu na uaminifu na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kuajiri vijana wa JKT pekee kwenye sekta zote zinazohusika na ulinzi na usalama wa nchi.
  Jumla ya vijana (846) wavulana wakiwa (612 ) na wasichana (234) wenye elimu za Msingi mpaka chuo kikuu, wamehitumu mafunzo ya awali ya kijeshi ya miezi (06) na kufuzu kuingia hatua ya pili ya mafunzo ya Malezi na stadi za kazi katika Jeshi la kujenga Taifa JKT.
  Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William, akitunuku zawadi kwa mmoja kati ya wanafunzi waliofanya vizuri wakati wa mafunzo.


  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Profesa Riziki Shemdoe, akiwasili kwenye Ofisi za kambi ya 841 Mafinga kushiriki mahafali hayo
  Vijana wa JKT wanaohitimu mafunzo ya awali, wakipita mbele ya Mgeni wa heshima kutoa heshima ya kijeshi

  0 0

  Maafisa wa Mfuko wa PSPF kulia Faidha Khatau na Hazina Konde wakimkabidhi mashukaka Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Dr Ali Salum Ali anayefutia ni Mkurugenzi Utawala na Uendeshaji Dr. Abubakar Khamis Hamadi, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa jengo jipya wa Hospitali ya Watoto Mnazi mmoja PSPF imekabidhi mashuka 75 kwa ajili ya wodi za watoto katika hospitali hiyo Kuu Zanzibar ikiwa ni moja ya kusaidia Jamii.  
  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar Dr. Ali Salum Ali akipokea mashuka kutoka kwa Maafisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Hazina Konde (katikati) na Afisa Mkuu wa Tawi la Zanzibar PSPF Bi. Faidha Thatau wakikabidhi mashuka hayo kwa ajili ya matumizi ya Wodi ya Watoto katika hospitali ya Taifa ya Mnazi Mmoja Zanzibar hafla hiyo imefanyika katika majengo mapya wa hospitali hiyo Zanzibar. 
  Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Faidha Thatau akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi mashuka kwa Uongozi wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar. Mfuko wa PSPF hutowa huduma za mafao mbalimbali kwa Wanachama wake Bima ya Afya kwa wateja wao.  

  Maafisa Wafawidhi wa PSPF Tawi la Zanzibar wakitandika kitanda katika moja ya vitanda katika Wodi ya Watoto Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar baada ya kukabidhi mashuka hayo 75 kwa ajili ya hospitali hiyo ya Watoto Zanzibar.Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amemtumia salamu za rambi rambi Rais wa Benki ya Maendelea ya Afrika (AfDB) Dk. Akinwumi Adesina,kufutia kifo cha Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo Kanda ya Afrika Kusini, Dk. Tonia Kandiero,kilichotokea Juni 28, 2017 huko mjini Pretoria nchini Afrika Kusini.

  Katika salamu hizo za rambi rambi, Dk. Shein alieleza kuwa ameshtushwa sana na kifo cha hafla cha Mkurugenzi huyo wa (AfDB) katika Kanda ya Afrika ya Kusini Dk. Tonia Kandiero ambacho kimeigusa sana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na jamii mbali mbali za Bara la Afrika.  Dk. Shein alisema kuwa kwa niaba yake binafsi, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wananchi wote wa Zanzibar, wanatoa mkono wa pole kwa Rais Adesina, kwa Benki ya  AfDB, wafanyakazi wote wa Benki hiyo pamoja na ndugu na familia ya marehemu Tonia kutokana na msiba huo. 
  Salamu hizo za Dk. Shein zilieleza kuwa wananchi wa Zanzibar pamoa na Serikali yao wanaendelea kumkumbuka marehemu kwa mapenzi makubwa aliyonayo kwa Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuitembelea mara kwa mara kwa ajili ya kujumuika pamoja katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo katika sekta muhimu za kiuchumi na kijamii hasa miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege, elimu na miradi ya maji. 
  “Daima tutaendelea kutoa shukrani zetu kwake kwa kurahisisha shughuli za uratibu na majadiliano baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)  pamoja na wahusika wengine muhimu wa maendeleo kwani alikuwa mchapakazi mzuri na aliyetoa mchango mkubwa katika nchi hii” zilieleza salamu hizo za rambi rambi alizotuma DK. Shein. 
  Aidha, salamu hizo za rambirambi zilieleza kuwa hikma zake, busara zake na mapenzi yake makubwa vyote kwa pamoja vitaendelea kukumbukwa sio kwa watu wa Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee bali zitakumbukwa na wapenda maendeleo wote duniani kutokana na mchango wake mkubwa. 
  Sambamba na hayo, Dk. Shein katika salamu hizo za rambi rambi alimuomba Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dk. Adesina,  kupokea salamu hizo kwa msiba huo mkubwa uliotokea na kumuhakikishia kuwa mawazo, fikra na majonzi ya Wazanzibari na Watanzania wote kwa jumla bado yataendelea katika kumkumbuka kiongozi huyo 
  Dk. Shein alimuomba  Rais huyo wa (AfDB) kuzifikisha salamu hizo za rambirambi kwa Wanafamilia, Wafanyakazi na viongozi wote wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). 
  Pamoja na hayo, salamu hizo zilimuomba Mwenyezi Mungu awape moyo wa subira ndugu, jamaa na marafiki wa Marehemu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huku akimuomba Mwenyezi Mungu kumlaza mahala pema kiongozi huyo. 
  Marehemu Dk. Tonia kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu wa AfDB katika Ofisi za Kanda ya Afrika ya Kusini mwishoni mwa mwaka 2016, alikuwa Mwakilishi wa Benki hiyo hapa nchini Tanzania ambaye alifanya kazi zake hapa nchini kwa takriban miaka sita. 

  Na Mnamo Disemba 21 mwaka 2016 maremu Dk. Tonia, alifika Ikulu mjini Zanzibar kumuaga Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwa anaelekea katika kituo chake kipya cha kazi huko Afrika ya Kusini, baada ya kupewa majukumu ya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika katika Kanda ya Afrika ya Kusini.


  0 0

  Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pension wa LAPF Bwana James Mlowe akipokea tuzo kutoka kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli baada ya LAPF kuwa mshindi wa Kwanza katika maonyesho ya 41 ya sabasaba katika kategori ya mifuko ya Hifadhi ya jamii, Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage Mapema leo Jijini Dar es salaam. 
  Meneja masoko na mawasiliano wa Mfuko wa Pension wa LAPF Bwana James Mlowe Akipokea tuzo kutoka kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli baada ya LAPF kuwa mshindi wa kwanza katika maonyesho ya 41 ya sabasaba Mapema leo Jijini Dar es salaam. 
  Tuzo ya Mshindi wa kwanza katika maonyesho ya 41 ya sabasaba katika viwanja vya Mwl JK Nyerere barabara ya Kilwa DSM. Tuzo hii ilikabidhiwa kwa Mfuko wa Pensheni wa LAPF na Raisi Dr. John Pombe Magufuli Mapema leo Jijini Dar es salaam.
  Rehema Mkamba afisa mwandamizi masoko na mawalisiliano Bi Rehema mkamba akoionyesha tuzo baada ya LAPF Kuibuka mshindi wa kwanza katika kategori ua mifuko ya hifadhi ya jamii na bima kwenye maonyesho ya 41 ya sabasaba 2017 Mapema leo Jijini Dar es salaam. 
  Wafanyakazi wa LAPF nje ya banda lao wakifurahia tuzo yao ya kuwa mshindi wa kwanza kategori ya mifuko ya Pensheni na Bima katika maonyesho ya 41 ya sabasaba waliyokabidhiwa na Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk John Pombe . Magufuli mapema leo. 


  0 0

   Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage, (kulia), akipeana mikono na Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, leo Julai 1, 2017.
   Waziri Mwijage a,kizungumza na wafanyakazi wa PPF kwenye banda la Mfuko huo.
   Waziri Mwijage akipeana mikono na Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa PPF, Bi. Pauline Msanga
   Waziri Mwijage akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa PPF baada ya kutembelea banda lao
   Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele, (kushoto), akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), Bw. Richard Kayombo alipotembela banda la Mfuko huo
   Wafanyakazi wa PPF wakiwahudumia wananchi waliotembela banda hilo
    Wafanyakazi wa PPF wakiwahudumia wananchi waliotembela banda hilo
  Waziri Mwijage, akiagana na wafanyakazi wa PPF baada ya kutembelea banda hilo. Kulia ni Mkuu Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Ben Mwaipaja.

  0 0

  Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto ameteuliwa kuwa balozi wa hifadhi ya wanyama ya Ngorongoro kwaajili ya kuwahamasisha watanzania kutembelea kivutio hicho na kujionea ufahari wake.
  Mshairi huyo ameteuliwa na Wizara ya Utalii baada ya kuonyesha jitihada mbalimbali anazozifanya katika hatua ya kuitangaza nchi ya Tanzania katika nyanja mbalimbali.
  Akiongea na mwandishi wetu Jumamosi hii akiwa katika viwanja vya Sabasaba ndani ya banda la Ngorongoro, Kaimu Mhifadhi wa Mamlaka ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Samson Mtunga amesema wameona Mrisho Mpoto ni mtu sahihi ambaye ataweza kuitangaza nchini katika mambo ya kitalii.
  “Tumemteua Mrisho Mpoto kuwa balozi wetu wa utalii, tumeona ni mtu ambaye anaweza kufanya kazi hiyo vizuri kwa sababu tayari kuna baadhi ya juhudi zake binafsi tumekuwa tukiziona katika shughuli zake mbalimbali. Kwahiyo kama mnavyojua wizara ina bidhaa nyingi Mpoto anaanza na Ngorongoro lakini baadaye anaweza kuongezewa majukumu kwa sababu tuna vitu vingi sana tunahitaji vitangazwe,” alisema Samson Mtunga.
  Kwa upande wa Mpoto amesema ataitumia nafasi hiyo kuwahamasicha Watanzania juu ya ufahari wa hifadhi hiyo pamoja na kuvitangaza vitu pekee vinavyopatikana.
  “Kazi iliyopo mbele yangu kwa sasa ni kuhakikisha Watanzania wanatembelea vivutio vyetu, tukiizungumzia Ngorongoro ni hifadhi ambayo ndani yake pia kuna binadamu wanaishi, kuna wanyama wengi. Kwahiyo huu ndio wakati ya kuthamini vya nyumbani na kuvitumia ipasavyo. Kwa mfano umechukua likizo ya mwezi mmoja tembelea kule ukiwa na familia yako ukaone mambo mazuri ambayo huwenda hayapatikani duniani kote,” alisema Mpoto.Mpoto amewataka Watanzania ambao wanatembelea maonyesho ya Sabasaba wasiache kutembelea banda hilo ili kujifunza mambo mbalimbali kuhusu hifadhi ya Ngorongoro.
  “Kwa sasa hivi nipo kwenye banda la Ngorongoro kwahiyo ukifika hapa tunaweza kuongea mengi kuhusu hifadhi hii ili na wewe ukirudi nyumbani ukawaeleze wengine kwamba Ngorongoro sio sehemu ya mchezo mchezo,”
  Alisema Watanzania wakitembelea hifadhi hiyo kwa wingi kwanza watafurahia upekee wa hifadhi hiyo pia wataweza kuchangia kuongeza pato la taifa hela ambazo zinaenda kutatua kero mbalimbali za watanzania iliwemo maji, barabara na huduma ya afya.

  0 0


  Shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi nchini Tanzania limeendesha Kampeni ya Upimaji wa Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi kwa watoto na vijana katika halmashauri ya Msalala na Manispaa ya Shinyanga katika mkoa wa Shinyanga. 

  Zoezi la kupima watoto na vijana limefanyika Juni 30,2017 na Julai 1,2017 katika zanahati ya Buluma iliyopo katika kijiji cha Buuma kata ya Jana katika halmashauri ya Msalala na zanahati ya kijiji cha Galamba katika kata ya Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga.

  Zaidi ya watoto na vijana 760 walipata fursa ya kupima afya zao.

  Akizungumza wakati wa zoezi hilo la upimaji,Afisa Mradi, Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Charles Simon, alisema kampeni ya Upimaji VVU kwa vijana na watoto yenye kauli mbiu ya “Ijue Afya ya Mwanao” inalenga kuwafikia vijana na watoto wengi zaidi ili kujua afya zao.

  “Hili ni zoezi endelevu,AGPAHI kwa kushirikiana na serikali tumekuwa tukipima afya za watoto na vijana na pale inapobainika wamepata maambukizi ya VVU huwa tunawaanzishia huduma ya tiba na matunzo”,alieleza Simon.

  Ijumaa Juni 30,2017: Hapa ni katika Zahanati ya Buluma iliyopo katika kijiji cha Buluma kata ya Jana halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoa wa Shinyanga .

  Afisa Mradi, Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Charles Simon akiwaeleza wazazi na walezi walioleta watoto na vijana katika zahanati ya Buluma kuhusu lengo la Kampeni ya Upimaji wa Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi kwa Watoto na Vijana.

  Wazazi,vijana na watoto wakimsikiliza Afisa Mradi, Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Charles Simonwakati akitolea ufafanuzi juu ya kampeni ya Upimaji VVU.

  Mratibu wa Wahudumu wa afya ngazi ya Jamii na Upimaji VVU wilaya ya Kahama, Peter Shimba akizungumza kabla ya zoezi la upimaji VVU halijaanza ambapo alilishukuru shirika la AGPAHI katika harakati zake za mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi na kwamba serikali itaendelea kushirikiana nalo katika mapambano hayo.


  0 0
  0 0  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT)  Brigedia Jenerali Charo Yateri amesema kuwa jitihada na juhudi zinazofanywa na vijana wake ndicho kitu kikubwa kilichopelekea kupata tuzo ya  masuala ya Kilimo na ufugaji.

  Tuzo hiyo walikabidhiwa  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli katika ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.

  Brigedia Jenerali Yateri alisema kuwa, mbali na kujihusisha na masuala ya ufugaji na kilimo amvapo wana dhana mbalimbali wanazozitumia ikiwemo Kilimo cha umwagiliaji pia wanajihusisha na ufugaji wa samaki kwa njia ya kisasa ya kuwaweka.

  Pmaoja na hilo,  SUMA JKT wamejikita zaidi katika utengenezaji wa samani za ndani kama makabati, vitanda, samani za maofisini na vitu mbalimbali pia wanatengeneza nguo mbalimbali.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT)  Brigedia Jenerali Charo Yateri akizungumza na Globu ya Jamii mara baada ya kupata tuzo katika masuala ya Kilimo na ufugaji waliyokabidhiwa  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli katika ufunguzin wa maadhimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.

  Dhana mbalimbali za Kilimo zinazotumika kwa Kilimo cha Umwagiliaji vinavyotumika na Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT), dhana hizo ziliweza kuwekwa wakati wa ufunguzi  maadhimimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.


   Baadhi ya wananchi wakiangalia Mabwawa ya Samaki yanayotumiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) kwa ajili ya ufugaji ambapo kila tenki moja linachukua samaki 100 wakati wa ufunguzi  maadhimimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.


  Wananchi wakiangalia mabanda ya kuku wanaofugwa na Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) wakati wa ufunguzi  maadhimimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.
  Samani zinazotengenezwa na Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) zikiwa katika banda lao wakati wa ufunguzi  maadhimimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.


  0 0  Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa pili kulia pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Kinondon ndg:Said Masanga wakionja bidhaa ya dagaa zinazookwa na wajasilia mali wadogowadogo wilaya ya Ubungo

  Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa pili kulia akionyeshwa shati la batiki moja ya bidhaa zinazotengenezwa wajasilia mali wadogowadogo wilaya ya Ubungo

  Katibu wa UVCCM Wilaya ya Ubungo Leah Mbeke akizungumza

  Baadhi ya Vijana walioudhuria Mafunzo ya Ujasilia Mali UVCCM Ubungo
  yalio fungulia na Ndg:Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka katikUkumbi wa Texaz Manzese

  ”Viongozi wa UVCCM Wilaya zote nchini fuatilieni Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015-2020,Hakikisheni asilimia 5 inayotolewa na kila Halmashauri nchini zinawafikia Vijana”Aliyasema Ndg:Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wakati akifungua Semina ya Mafunzo ya Ujasiliamali kwa Vijana wa Wilaya Ya Ubungo Katika Ukumbu wa Texaz Manzese.


  0 0

  Katibu wa chama Cha MAPINDUZI CCM mkoa RUVUMA AMINA IMBO amewataka wale wote watakaochukua fomu za kugombea katika ngazi za wilaya na mkoa kuachana na tabia za kupiga kampeni kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria za chama cha mapinduzi.HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE.

  0 0

  Msimu wa tatu wa tamasha la MAJIMAJI SEREBUKA linaloandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali Songea Mississipi, linatarajia kuanza julai 22 mwaka huu,Huku mishezo mbalimbali itahusishwa ikiwemo riadha,ngoma za asili,maonyesho ya kiabiahara na mdahalo,na nini hasa lengo la tamasha hilo huyu hapa mwenyekiti wa tamasha DAMASI NDUMBARO anabainisha. HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE

older | 1 | .... | 1777 | 1778 | (Page 1779) | 1780 | 1781 | .... | 3282 | newer