Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live

Airtel yatoa ofa kabambe katika maonesho ya sabasaba

$
0
0
· Airtel kuuza simu kwa bei nafuu sabasaba
· Simu ya Airtel kuuzwa 16,000 ikiwa na bando la 10,00 mwezi mzima BURE

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imetangaza ofa kabambe wakati wote wa maonyesho ya biashara ya sabasaba mwaka huu zitakazowawezesha wateja wake na wale wapya kuunganishwa na huduma za mtandao kwa gharama nafuu na pia kujipatia simu bomba kwa bei nafuu.


Akiongea na waandishi wa habari katika banda la Airtel lililopo viwanja vya sabasaba Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “dhamira yetu Airtel ni kuendelea kuunganisha jamii kwa bidhaa na huduma, hivyo kwa msimu huu maonesho ya saba saba tutatoa ofa nyingi sana ikiwemo simu aina ya ZTE GS 500, Motorola C113, Motorola F3 na Motorola C117 kwa shilingi 16,000 tu na mteja akishanunua ataunganishwa na bando la shilingi 10,000 litakalodumu kwa muda wa mwezi mmoja”

“Unaweza ukaona hapo gharama ya simu inakuwa nafuu na kisha unaunganishwa na kifurushi cha mwezi mzima BURE kuongea na ndugu, jamaa, na marafiki huku ukifaidi huduma zingine za Airtel” alieleza Mmbando.

Meneja uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando (kulia) na Afisa huduma kwa wateja wa Airtel Bi Veronica Valentine (kushoto) wakionesha simu aina ya ZTE na Motorola katika banda la Airtel lililoko katika viwanja vya maonesho ya biashara maarufu kama sabasaba, simu hizo zitauzwa kwa bei ya ofa ya shilingi 16,000 tu na mteja ataunganishwa na kufurushi cha muda wa maongezi kwa mwezi mzima cha shilingi 10,000 BURE. katikati ni Afisa huduma kwa wateja wa Airtel Tumwidike Michael 
Kutoka kulia ni Afisa huduma kwa wateja wa Airtel Digna Paul na Tumwidike Michael wakitoa huduma katika banda la Airtel lilipo katika vya maonesho ya biashara maarufu kama sabasaba leo. katika banda hilo airtel itauza simu original kwa bei ya shilingi 16,000 ikiwa imeunganishwa na laini ya airtel na bando la mwezi mzima la shilingi 10,000 BURE. 


fisa huduma kwa wateja wa Airtel Tumwidike Michael akionesha baadhi ya simu na vocha zinazouzwa katika banda la Airtel lililoko katika viwanja vya maonesho ya biashara maarufu kama sabasaba, simu hizo zitauzwa kwa bei ya ofa ya shilingi 16,000 tu na mteja ataunganishwa na kufurushi cha muda wa maongezi kwa mwezi mzima cha shilingi 10,000 BURE.



BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA KUWA HISTORIA-WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeadhimia kupambana vilivyo dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya na kuhakikisha inakuwa historia nchini.

Pia ametoa wito kwa wazazi wote nchini waendelee kufuatilia nyendo za watoto ili wasijiingize kwenye mtego wa dawa za kulevya na wala wasisubiri vijana wao waanze kutumia.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Juni 29, 2017) kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani, iliyoadhimishwa mjini Dodoma.

Kufuatia hali hiyo Waziri Mkuu amesema Serikali imejidhatiti kuhakikisha kuwa uzalishaji, usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya unadhibitiwa kikamilifu nchini.

Amesema katika kutimiza azma hiyo, ambayo pia inaelekezwa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Serikali ilifanya mabadiliko ya Sheria ya Dawa za Kulevya kwa kuanzisha chombo cha kisheria cha kupambana na biashara hiyo, ambayo imeongeza adhabu kwa wanaoshiriki.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kwenye uwanja wa Nyerere mjini Dodoma Juni 29, 2017.
Balozi wa Uingereza Nchini, Sarah Cooke akizungumza katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kwenye uwanja wa Nyerere mjini Dodoma Juni 29, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama dawa mbalimbali za kulevya katika maonyesho yaliyokwenda sambamba na Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kwenye uwanja wa Nyerere mjini Dodoma Juni 29, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la Kituo cha Kutoa Huduma kwa Waathirika wa Dawa za Kulevya mjini Dodoma Juni 29, 2017. Kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na kulia ni Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga .

RAIS WA ZANZIBAR DK,SHEIN ATUNUKU NISHANI

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapindizi Dk,Ali Mohammed Shein akimvisha nishani ya Mapinduzi Bwana Aboud Talib Aboud katika hafla ya kutunuku nishani ya Mapinduzi,nishani ya Utumishi uliotukuka na nishani ya Ushujaa iliofanyika katika viwanja vya Ikulu mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapindizi Dk,Ali Mohammed Shein katikati akiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi na waliotunukiwa nishani mbalimbali katika hafla ya kutunuku nishani ya Mapinduzi,nishani ya Utumishi uliotukuka na nishani ya Ushujaa iliofanyika katika viwanja vya Ikulu mjini Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (mbele) pamoja na Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika Sherehe za Kutunuku nishani iliyofanyika leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja 
Baadhi ya waalikwa waliohudhuria katika hafla ya kutunuku nishani ya Mapinduzi,nishani ya Utumishi uliotukuka na nishani ya Ushujaa iliofanyika katika viwanja vya Ikulu mjini Unguja.
Baadhi ya Waheshimiwa waliohudhuria katika hafla ya kutunuku nishani ya Mapinduzi,nishani ya Utumishi uliotukuka na nishani ya Ushujaa iliofanyika katika viwanja vya Ikulu mjini Unguja.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi kulia akipeana mikono na Makamo wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Gharib Mohammed Bilal katika hafla ya kutunuku nishani ya Mapinduzi,nishani ya Utumishi uliotukuka na nishani ya Ushujaa iliofanyika katika viwanja vya Ikulu mjini Unguja.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

MICHUZI TV: MALINZI ,MWESIGWA WARUDISHWA RUMANDE MPAKA JULAI 3

$
0
0
 Rais wa TFF, Jamal Malinzi akiwa na Katibu wake , Celestine Mwesigwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu ambapo walisomewa mashtaka yao kadhaa ya matumizi mabaya ya ofisi ikiwe Kugushi nyaraka za shirikisho hilo pamoja na kutakatisha fedha zaidi ya laki tatu za kimarekani.
  Rais wa TFF, Jamal Malinzi akiwa na Katibu wake , Celestine Mwesigwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu ambapo walisomewa mashtaka ya kadhaa ya matumizi mabaya ya ofisi ikiwa nipamoja na kutakatisha pesa zaidi ya laki tatu za kimarekani. washtakiwa hao wamepelekwa mahabusu Keko kutokana na kesi hiyo kutokuwa na dhamana hivyo wataletwa tena mahakamani  mpaka julai 3.
 Rais wa Simba ,Evance Aveva na Kaimu wake ,Godfrey Nyange(KABURU) wakiongea na aliyekuwa katibu wa Simba Evodius Mutawala katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu ambapo walipandishwa kwa mashtaka tofauti ikiwemo la matumizi mabaya ya ofisi.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA: ZUIO LA USAFIRISHAJI CHAKULA NJE LIKO PALE PALE

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema msimamo wa Serikali wa kuzuia usafirishaji wa chakula kwenda nje ya nchi uko pale pale.

Pia amesema mahindi iliyokamatwa mkoani Kilimanjaro yakisafirishwa kwenda nje ya nchi yataingizwa kwenye Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) na magari yatabaki polisi.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo ( Alhamisi Juni 29, 2017) Bungeni mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mheshimiwa Ritha Kabati (Viti Maalumu) aliyetaka ufafanuzi kuhusu zuio la kusafirisha mazao nje ya nchi kwa mikoa yenye chakula cha ziada.

“Tumedhibiti na kuzuia usafirishaji wa chakula hasa mahindi kwenda nje ya nchi ili kuliepusha Taifa kukumbwa na baa la njaa kutokana na baadhi ya mikoa kutopata mavuno ya kutosha,”

“Kuna maeneo kama ya Sengerema na Geita mahindi yamekauka, hivyo bado tuna upungu wa chakula. Na hata bei ya chakula ipo juu, hatuna namna nyingine zaidi ya kudhibiti utokaji wa chakula kwenda nje na nawasihi wananchi tushirikiane katika jambo hili,” amesema.

Waziri Mkuu amesema kama kunaulazima wa kusafirisha chakula kwenda nje ya nchi wahusika wakaombe kibali katika Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na kibali kiwe cha kusafirisha unga na si mahindi.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema watumishi wote wa iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Mkuu Dodoma (CDA) waliokuwa wanaolalamikiwa na wananchi kutokana na utendaji wao wataondolewa wakati wenzao wakihamishiwa Manispaa ya Dodoma.

Waziri Mkuu amesema kwa sasa wanaendelea na ukaguzi na uhakiki wa kina kwenye masuala ya fedha na utumishi ili waweze kujua CDA ilipovunjwa iliacha fedha kiasi gani na shughuli zake zilifikia hatua gani ili ziendelezwe.

Amesema majukumu yote ya CDA yatafanywa na Manispaa ya Dodoma na baada ya kukamilisha utaratibu huo mpango kazi wote utaendelea kama ulivyopangwa.Kuhusu waliolipia viwanja watakabidhiwa mara baada ya kukamisha utaratibu huo.

Waziri Mkuu alikuwa akijibu swali la Mheshimiwa Matha Malata (Viti Maalumu) aliyetaka kupata tamko la Serikali kuhusu wananchi ambao waliolipia viwanja CDA ambao bado hawajakabidhiwa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
ALHAMISI, JUNI 29, 2017.

Serikali, Wadau wa Habari wakubaliana kujenga uhusiano imara kikazi

$
0
0
Wadau wa Habari nchini wakiongozwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na Wakfu wa Taasisi Huru za Uwazi Afrika (OSIEA) wamefanya semina ya siku moja kwa lengo la kuboresha mahusiano ya utendaji wa kazi iliyoshirikisha Serikali na wadau wa habari nchini.

Semina hiyo pia ilihudhuriwa na maafisa wa Serikali wakiongozwa na Naibu Waiziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Wasanii Bi Annastazia Wambura, Wabunge, wawakilishi wa vyuo vikuu, viongozi wa taasisi za Habari nchini, wahariri na waandishi.

Naibu Waziri, Anastazia Wambura akizungumza kwenye mkutano huo amesema serikali iko bega kwa bega na waandishi wa habari ili kufikia malengo waliyojiwekea katika kuhabarisha umma.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura akizungumza kwenye mkutano wa wadau mbalimbali wa habari waliokutana kujadili namna ya kufanya kazi kwa pamoja na Serikali ili kuleta ustawi wananchi leo kwenye ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Usajili wa Magazeti, Bw. Patrick Kipangula akiwasilisha mada kuhusu sheria ya vyombo vya habari aliyoiwasilisha kwenye mkutano wa wadau wa vyombo vya habari waliokutana na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura.
Mhariri Mtendaji wa The Guardian Ltd, Jesse Kwayu akiwasilisha mada kuhusu namna ya kufanya mahusiano ya kikazi kati ya serikali na wanahabari kwa baadhi ya wabunge, wahariri, Maafisa habari na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Zamaradi Kawawa(kushoto) akitolea ufafanuzi baadhi ya mambo  yanayohusu Idara ya Habari Maelezo yaliyoulizwa na wadau wa habari kwenye mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa habari waliokutana leo kwenye ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma. Katikati ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

CCM YARIDHISHWA NA UCHAPAKAZI WA SERIKALI YA JPM KATIKA KUTEKELEZA ILANI

$
0
0
NA BASHIR NKOROMO

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinaridhishwa sana na kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli kwa kuwa serikali hiyo imejikita ipaswavyo katika kutekeleza ilani ya Chama ikiwemo kuipeleka Tanzania katika nchi ya Uchumi wa Viwanda.

Akizungumza na Waandishi wa habari katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, amesema, CCM imefikia hatua ya kutoa tamko rasmi la kuridhishwa kwake na utendaji kazi wa Serikali hiyo, baada ya Chama kufanya ziara ya uhakiki wa hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa viwanda vikubwa, vya kati na vidogo katika mkoa wa Pwani.

Hivi karibuni CCM ilipata fursa ya kushiriki katika ziara ya Rais Dk. John Magufuli katika mkoa huo wa Pwani, kwa kuwakilishwa na Polepole, ambapo katika ziara hiyo ya siku tatu, Rais alitembelea na kuzindua viwanda kadhaa ambavyo vinaonyesha kuwa vitachangia kwa kasi kuleta mahuisha matumaini ya lengo la Tanzania kuwa nchi ya Uchumi wa Viwanda.

"Katika kipindi cha miaka miwili cha Uongozi Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Magufuli, mkoa wa Pwani pekee, umeweza kuwa na viwanda vikubwa, vya kati na vidogo zaidi ya 370, hii ni hatua kubwa sana inayoonyesha kuwa Serikali hii imedhamiria kuifikisha Tanzania katika Uchumi wa Viwanda", alisema Polepole.

Polepole amesema, kufuatia uhakiki iliofanya CCM katika hivyo viwanda zaidi ya 370, viwanda 87 ni vikubwa ambavyo vina uwezo wa uzalishaji bidhaa hadi za kwenda nje ya nchi na kwenda katika maeneo mbalimbali nchini na kwamba viwanda hivyo vilivyopo mkoa wa Pwani baadhi vimejengwa kwa ubia wa serikali na wadau na vingine wadau wenyewe.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DIAMOND AZINDUA MRADI WA KUUZA KARANGA KATIKA SOKO LA MCHIKICHINI

$
0
0
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) ,akiwa amepiga picha ya pozi na mmoja wa wauza Karanga ambaye ameamua kuuza Karanga za Mwanamuziki huyo na kuachana na Karanga za Kawaida.
Mashabiki wa Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) wakigawana Karanga mara baada ya kuzinunua mara baada ya uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya soko la Mchikichini jijini Dar es Salaam
Mama mzazi wa Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) akiwa anakula Karanga za mtoto wake mara baada ya kuzinduliwa Karume jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) akizungumza na wakazi wa Ilala Mchikichini wakati alipokuwa akifanya shoo ya uzinduzi wa Karanga zake zinazokwenda kwa jina la Diamond Karanga zitakazouzwa madukani kote katika mfumo wa kisasa.


NAIBU KATIBU MKUU CCM ZANZIBAR, AKABIDHI KOMBE KWA MSHINDI WA MASHINDANO YA MASAUNI - JAZEERA CUP

$
0
0
 Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt.Abdulla Juma Saadala, akimkabidhi kombe Nahodha wa timu ya Kundemba FC,Mohamed Haji Shaibu, baada ya kuibuka mshindi katika  mashindano ya Masauni - Jazeera Cup.Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni.Mchezo huo ulimalizika kwa mikwaju ya penati 8-7 iliyopelekea timu ya Kundemba FC  kuibuka bingwa dhidi ya Kilimani Maghorofani.Mchezo huo ulifanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Visiwani Zanzibar. Picha na Abubakari Akida

 Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Abdulla Juma Saadala, akimkabidhi zawadi ya viatu  mchezaji bora wa mashindano ya Masauni - Jazeerah Cup,Shabani Makuka.Kushoto ni Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni, Nassor Saleh Jazeera na watatu ni Mbunge wa jimbo hilo,Mhandisi Hamad Masauni.Mchezo huo ulimalizika kwa mikwaju ya penati 8-7 iliyopelekea timu ya Kundemba FC  kuibuka mshindi  dhidi ya Kilimani Maghorofani, mchezo huo ulifanyika katika viwanja vya Mnazi Mmmoja,Visiwani Zanzibar.Picha na Abubakari Akida

 Mwamuzi Bora wa Mashindano ya Masauni - Jazeera Cup, Ramadhani Khamis Kombo akipokea zawadi kutoka kwa Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt.Abdulla Juma Saadala,b aada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali kati ya timu ya Kundemba FC na Kilimani Maghorofani.Mchezo huo ulifanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja,Visiwani Zanzibar.Picha na Abubakari Akida

 Nahodha wa timu ya Kundemba FC, Mohamed Haji Shaibu, akipokea zawadi ya mshindi wa kwanza  wa mashindano ya Masauni-Jazeera Cup  kutoka kwa Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar , Dkt.Abdulla Juma Saadala.Kushoto ni Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni, Nassor Saleh Jazeera na watatu ni Mbunge wa jimbo hilo, Mhandisi Hamad Masauni .Picha na Abubakari Akida

 Nahodha wa timu ya Kundemba FC, Mohamed Haji Shaibu, akipokea zawadi ya mshindi wa kwanza  wa mashindano ya Masauni-Jazeera Cup  kutoka kwa Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar , Dkt.Abdulla Juma Saadala.Kushoto ni Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni, Nassor Saleh Jazeera na watatu ni Mbunge wa jimbo hilo, Mhandisi Hamad Masauni .Picha na Abubakari Akida

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Dkt. Tonia Kandiero

ZANTEL YAFUTURISHA WATEJA NA WAFANYAKAZI WAKE ZANZIBAR

$
0
0

Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohamed Khamis Mussa maarufu kwa jina la Baucha (Kulia) na Mkuu wa huduma za Ezypesa Zantel, Shinuna Kassim (katikati) wakifurahia jambo na mteja wa Zantel katika hafla ya kupata futari iliyoandaliwa na Kampuni hiyo mwishoni mwa juma mjini Unguja-Zanzibar.
Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohamed Khamis Mussa maarufu kwa jina la Baucha (Katikati) akipata futari na baadhi ya wateja wa Kampuni hiyo katika hafla iliyoandaliwa na Kampuni hiyo mwishoni mwa juma mjini Unguja-Zanzibar.
Wafanyakazi wa Zantel kwa upande wa Zanzibar wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Benoit Janin (hayupo pichani) wakati wa kupata futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wafanyakazi wa Zantel mwishoni mwa juma mjini Unguja-Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni hiyo wa upande wa Zanzibar wakati wa kupata futari iliyoandaliwa kwa ajili yao mwishoni mwa juma mjini Unguja-Zanzibar.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

DKT KIGWANGALLA AFUNGUA MKUTANO WA TANO WA MADAKTARI NA WANASAYANSI WA SIKU MBILI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee, Dk Khamisi Kigwangalla akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa tano wa Madaktari uliofanyika katika ukumbi wa Kisenga Makumbusho jijini Dar es Salaam .
Sehemu ya madaktari na wanasayansi walioshiriki mkutano huo ambao unajadili masuala mbalimbali ya tiba katika bara la Afrika na hapa nchini 
Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee, Dkt Khamisi Kigwangalla akikagua maonyesho ya Dawa yaliyopo nje ya mkutano huo
Sehemu ya madaktari na Wanasayansi walioshiriki mkutano huo ambao unajadili masula mbalimbali ya tiba katika bara la afrika na hapa nchini
Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee, Dk Khamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa meza kuu na washirika wa Maendeleo nchini

Mkuu wa Wilaya ya Temeke kufanya oparesheni maalum kwa wadaiwa sugu

$
0
0
Kufuatia wafanyabishara kutokulipa kodi kwa wakati na wengine kuwa wadaiwa sugu na kupelekea baadhi ya halmashauri kukwama katika kuendeleza miradi ya maendeleo na kujitegemea hatimaye Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva kufanya oparesheni maalum kwa wadaiwa sugu.

Akizungumza mapema leo DC Lyaniva ameeleza kuwa zoezi hilo litalenga kukusanya kodi kwa wale wadaiwa sugu ambao wamekuwa wakidaiwa na Halmashauri hiyo kwa muda mrefu.

DC Lyaniva ametaja idadi ya wadaiwa sugu kuwa ni 142 ambapo wadaiwa wa leseni za biashara wakiongoza kwa idadi kubwa ya wadaiwa 69, ushuru wa huduma 52 na wadaiwa sugu kwa upande wa masoko wakiwa ni 21.

Jambo ambalo limepelekea halimashauri hiyo ya wilaya ya Temeke kutofikia malengo ya makusanyo ya kodi ya shilingi bilioni 29 ambapo wamefanikiwa kukusanya bilioni 23 pekee huku zaidi ya bilioni 6 zikibakia kwa wadaiwa sugu.

DC Lyaniva amesisitiza kuwa kwa wasiolipa kabla ya tarehe mosi ya mwezi Julai mwaka huu watachukuliwa hatua kali za kisheria, hivyo ni vyema wakatimiza wajibu huo haraka iwezekanavyo na kufafanua kuwa kwa umuhimu wa jambo hilo ofisi zitakuwa wazi mpaka siku ya jumapili.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva.

RAIS DKT. MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA DKT. TONIA KANDIERO

$
0
0
Dkt. Tonia Kandiero 

“Kwa mshituko na masikitiko makubwa nimepokea taarifa za kifo cha Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika Kanda ya Afrika Kusini Dkt. Tonia Kandiero aliyefariki dunia ghafla jana usiku tarehe 28 Juni, 2017 akiwa ofisini kwake huko Pretoria Afrika Kusini”

Hii ni kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa leo tarehe 29 Juni, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kupokea taarifa za kifo cha Dkt. Tonia Kandiero ambaye kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu wa AfDB katika Ofisi za Kanda ya Afrika Kusini mwishoni mwa mwaka 2016 alikuwa Mwakilishi wa AfDB Tanzania.

“Nitamkumbuka Dkt. Tonia Kandiero kama mchapakazi hodari aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi yetu, nikiwa Waziri wa Ujenzi nimeshirikiana nae kwa karibu kufanikisha utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo kwa nchi yetu ambayo imefadhiliwa na AfDB, ametoa mchango mkubwa kufanikisha ujenzi wa madaraja na barabara za Dodoma – Iringa, Dodoma – Babati, Namtumbo – Tunduru – Mtambaswala, Arusha – Taveta – Voi na pia alitoa mchango mkubwa katika kufanikisha miradi mingine ambayo ipo mbioni kutekelezwa ikiwemo ujenzi wa barabara ya Bagamoyo – Tanga – Mombasa, Mbinga – Mbambabay na Tabora - Katavi”.

Kufuatia kifo cha Dkt. Tonia Kandiero Mhe. Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais wa AfDB Dkt. Akinwumi Adesina, familia ya Dkt. Tonia Kandiero, wafanyakazi wote wa AfDB, ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu.

Dkt. Magufuli amemuombea marehemu Dkt. Tonia Kandiero apumzishwe mahali pema peponi, Amina.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
29 Juni, 2017

MICHUZI TV: Kampuni ya Agricom Afrika na World Group Machine ya China zaingia makubaliano katika sekta ya kilimo

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Agricom Afrika, Angelina Ngalula (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya World Group Machine ya nchini China, Buxin Wang wakati wakitambulisha mashine za kisasa za kuvunia mpunga, baada ya kuingia makubaliano ya kuwa wauzaji wa mashine hizo hapa nchini. Kampuni ya Agricom ni Kampuni ya kizalendo inayojihusisha na uagizani na uuzaji wa pembejeo za kilimo ikiwa ni zile za kulimia, kuvunia. Makubaliano hayo yamefikiwa leo Juni 29, 2017 katika ofisi zao zilizopo Mivinjeni, Kilwa Road jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Agricom Afrika, Angelina Ngalula (katikati) na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo na ujumbe wa  Kampuni ya World Group Machine ya nchini China ulioongozwa na Mkurugenzi wake, Buxin Wang, uliofanyika leo Juni 29, 2017 katika ofisi zao zilizopo Mivinjeni, Kilwa Road jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja baada ya mkutano wao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Agricom Afrika, Angelina Ngalula (wa tatu kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya World Group Machine ya nchini China, Buxin Wang wakati wakitambulisha mashine za kisasa za kuvunia mpunga, baada ya kuingia makubaliano ya kuwa wauzaji wa mashine hizo hapa nchini. Kampuni ya Agricom ni Kampuni ya kizalendo inayojihusisha na uagizani na uuzaji wa pembejeo za kilimo ikiwa ni zile za kulimia, kuvunia. Makubaliano hayo yamefikiwa leo Juni 29, 2017 katika ofisi zao zilizopo Mivinjeni, Kilwa Road jijini Dar es salaam. Wengine pichani toka kushoto ni Meneja Mipango wa Kampuni ya Agricom Afrika, Eric Mwidunda, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa Kampuni ya World Group Machine ya nchini China, Jiayin Xu, Mtaalam wa Mashine hizo kutoka Kampuni ya World Group Machine ya nchini China, Yonghong Yu pamona na Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Agricom Afrika, Bernadetha Mariki.


IGP SIRRO AWAFARIJI WAFIWA KIBITI

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Mangwi, kata ya mchukwi wilayani kibiti jana alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji na afisa mtendaji wa kijiji. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la polisi.

Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na wananchi wa kijiji cha mangwi, kata ya mchukwi wilayani kibiti jana alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji na afisa mtendaji wa kijiji hicho. IGP Sirro alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi kijijini hapo kutowafumbia macho wahalifu wanaotenda mauaji hayo na kuwataka kuwa na kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu hao.  picha na hassan mndeme-jeshi la polisi.

 Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro akitoa rambirambi ya msiba kwa wananchi wa kijiji cha mangwi, kata ya mchukwi wilayani kibiti jana alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji ya Mwenyekiti wa kitongoji na Afisa Mtendaji wa kijiji hicho. picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akikagua nyumba iliyochomwa moto na wahalifu waliofanya mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji na afisa mtendaji wa kijiji cha mangwi, kata ya mchukwi wilayani kibiti jana alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji  hayo. picha na hassan mndeme-jeshi la polisi.



Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway kuzuru Tanzania

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufalme wa Norway, Mhe. Borge Brende (pichani) atafanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini (tarehe 29 na 30 Juni 2017).
 Madhumuni ya ziara ya Mhe. Brende ambaye atawasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tarehe 29  saa tatu usiku ni kuimarisha mahusiano kati ya Norway na Tanzania.
Wakati wa ziara yake, Mhe. Waziri Brende pamoja na mambo mengine atafanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 30 Juni 2017.


Aidha, siku hiyo hiyo asubuhi, mgeni huyo atafanya mazungumzo na mwenyeji wake, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere na baadaye wataweka saini Mkataba wa Makubaliano (MoU) kuhusu Ushirikiano wa Mashauriano ya Kisiasa na Kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.


Mhe. Borge pia atakutana na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Philip Mpango (Mb.) ambapo kwa pamoja watashiriki katika uzinduzi wa programu ya kushirikiana katika masuala ya kodi na uzinduzi wa awamu ya pili ya programu ya kuendeleza mafuta(oil for development program) utakaofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro tarehe 30 Juni 2017.  
Uzinduzi wa programu hizo pia utahudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Dkt. Medard Kalemani (Mb.) na Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dkt. Charles Kichere.

Ratiba ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway inaonesha pia kwa kushirikiana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (Mb.) na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Dkt. Medard Kalemani watashiriki katika shughuli za kufunga semina ya Mradi wa Kusindika Gesi asilia (LNG) iliyoandaliwa na kampuni ya mafuta ya kutoka Norway inayoitwa Statoil ambayo pia inaendesha shughuli zake hapa nchini. Semina hiyo inafanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Mhe. Waziri baada ya kukamilisha ratiba yake nchini atarejea Norway siku ya Ijumaa tarehe 30 Juni 2017 saa nne usiku.

 Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,


Dar es Salaam, 29 Juni 2017

AZAM FC WAANZA KUJIFUA TAYARI KWA MSIMU MPYA WA 2017/18

$
0
0
Golikipa wa Azam aliyesajiliwa kutoka timu ya Mbao Fc Benedict Haule akiwa ameanza mazoezi na klabu yake ya zamani.

Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC imeanza  rasmi mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao (2017-2018) huku ikiwa imepata mwaliko maalum nchini Rwanda kutoka kwa mabingwa wa nchi hiyo, Rayon Sports.
Awali Azam FC ilipanga kuanza maandalizi ya msimu mpya Jumatatu ijayo Julai 3, lakini kutokana na mwaliko huo imeamua kuanza mazoezi mapema, ambapo Rayon imealika kwa ajili ya kucheza nao mchezo wa kirafiki Julai 8 ikiwa ni sehemu ya kusherehesha ubingwa walioutwaa.
Wachezaji waliofanikiwa kuhudhuria kwenye mazoezi hayo ya kwanza ni pamoja na makipa Mwadini Ally, Benedict Haule, aliyerejea Azam FC kwenye usajili huu akitokea Mbao FC, Metacha Mnata na mabeki Bruce Kangwa, Abbas Kapombe, Ramadhan Mohamed, Abdul Omary.

Viungo ni Frank Domayo, Masoud Abdallah, Stanslaus Ladislaus na mshambuliaji Yahaya Zaidi, huku wachezaji wengine wakiwa na udhuru na baadhi wakiwemo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachoshiriki michuano ya COSAFA, Nahodha Msaidizi Himid Mao ‘Ninja’, kiungo Salmin Hoza na mshambuliaji Mbaraka Yussuf.

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Nassor Cheche, alisema kuwa mbali na mwaliko huo kupelekea kuanza mapema mazoezi, pia sababu nyingine ni kuwaweka fiti zaidi wachezaji ambao hawakuchaguliwa timu ya Taifa ili watakapoungana na wale walioitwa waweze kwenda sawa.
“Tukapokwenda Rwanda kati ya tarehe 5 hadi 6, tunaweza kupata siku kadhaa za kufanya maandalizi yetu pamoja na kucheza mechi kadhaa kabla ya kurejea nyumbani tayari kabisa kufanya maandalizi ya mwisho kwa ajili ya ligi ya msimu ujao,” alisema.
Cheche alisema amefurahishwa sana na namna alivyowaona wachezaji kwenye mazoezi hayo ya kwanza huku akieleza kufurahishwa na usajili unaoendelea kufanywa na timu hiyo mpaka sasa na sera ya klabu ya kupandisha wachezaji kutoka Azam Academy.
“Maingizo ni mazuri na kilichobakia hivi sasa ni kufanya mazoezi kwa pamoja na kuelewana na wenzao, wajuane kitabia nje na ndani ya uwanja ili waweze kushirikiana ma kubwa kuweza kulisukuma mbele gurudumu hili la Azam FC,” alisema.
Azam FC inayodhaminiwa na Benki bora ya NMB na kinywaji safi cha Azam Cola, itaendelea tena na mazoezi kesho saa 10 jioni.


WITO KWA WADAU KUTOA MAONI KUHUSU MISWADA MITATU YA SHERIA

MAFUNZO YA UANZISHWAJI MATUMIZI YA MASHINE ZA KIELETRONIC (EFD) YATOLEWA ZANZIBAR.

$
0
0
 Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika mafunzo kuhusiana na Uanzishwaji wa matumizi ya Mashine za kieletroniki (EFD)yaliofanyika katika ukumbi wa ZRB Mazizini mjini Unguja
 Kamishna wa Bodi ya mapato Zanzibar Amour Hamil Bakari akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kwa waandishi wa Habari kuhusiana na Uanzishwaji  wa matumizi ya Mashine za kieletroniki (EFD)yaliofanyika katika ukumbi wa ZRB Mazizini mjini Unguja.
 Mwandishi wa Habari wa Hits Fm Jazaa Kombo akiuliza maswali katika mafunzo kwa waandishi wa Habari kuhusiana na Uanzishwaji  wa matumizi ya Mashine za kieletroniki (EFD)yaliofanyika katika ukumbi wa ZRB Mazizini mjini Unguja.
 Mwandishi wa Habari wa Habari Leo Khatib Suleiman akiuliza maswali katika mafunzo kwa waandishi wa Habari kuhusiana na Uanzishwaji  wa matumizi ya Mashine za kieletroniki (EFD)yaliofanyika katika ukumbi wa ZRB Mazizini mjini Unguja.
Meneja wa Sera ,Utafiti na Mipango Z R B Ahmed Haji Saadati akitoa ufafanuzi wa  maswali mbalimbali yalioulizwa  katika mafunzo kwa waandishi wa Habari kuhusiana na Uanzishwaji  wa matumizi ya Mashine za kieletroniki (EFD)yaliofanyika katika ukumbi wa ZRB Mazizini mjini Unguja.
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live




Latest Images