Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1772 | 1773 | (Page 1774) | 1775 | 1776 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Rais Mstaafu Mhe Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim wakiwa na Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Armando Emilio Gwebuza wakiwa kwenye misa ya Kitaifa kuomboleza kifo cha Rais mstaafu wa Botswana Sir Ketumire Masire katika ukumbi wa Sports Centre wa Chuo Kikuu cha Botswana mjini Gaborone leo. Marehemu Masire anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwake Kanye, kilomita 80 kutoka Gaborone. Mhe Mkapa amemuwakilisha Rais Dkt John Magufuli kwenye msiba huo.
  Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim na Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Armando Emilio Gwebuza wakiwa kwenye misa ya Kitaifa kuomboleza kifo cha Rais mstaafu wa Botswana Sir Ketumire Masire katika ukumbi wa Sports Centre wa Chuo Kikuu cha Botswana mjini Gaborone leo. Marehemu Masire anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwake Kanye, kilomita 80 kutoka Gaborone
  Rais Mstaafu Mhe Benjamin William Mkapa akihojiwa na kituo cha TV cha Afrika Kusini cha SABC kwenye misa ya Kitaifa kuomboleza kifo cha Rais mstaafu wa Botswana Sir Ketumire Masire katika ukumbi wa Sports Centre wa Chuo Kikuu cha Botswana mjini Gaborone leo. Marehemu Masire anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwake Kanye, kilomita 80 kutoka Gaborone.
  Rais Ian Khama wa Botswana akiongoza wakati wa nyimbo ya Taifa ikipigwa
  Rais Mstaafu Mhe Benjamin William Mkapa na Mama Anna Mkapa na viongozi wengine wakitoka ukumbini baada ya  misa ya Kitaifa kuomboleza kifo cha Rais mstaafu wa Botswana Sir Ketumire Masire katika ukumbi wa Sports Centre wa Chuo Kikuu cha Botswana mjini Gaborone leo. Marehemu Masire anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwake Kanye, kilomita 80 kutoka Gaborone. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wajumbe wa Kamati mbili alizoziteua za Uchunguzi wa Mchanga wa  Madini (Makinikia) Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 28, 2017.PICHA NA IKULU
   Katibu Mkuu kiongozi Balozi John Kijazi (kulia) akiongea na Waziri wa Maji, Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele anayaongoza ujumbe kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo iliyopo nchini kusaidia mchakato wa ujenzi wa Dam (bwawa la kuzalisha umeme)  la Steigler’s Gorge kabla ya kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2017. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Maji, Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele anayaongoza ujumbe kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo iliyopo nchini kusaidia mchakato wa ujenzi wa Dam (bwawa la kuzalisha umeme)  la Steigler’s Gorge  Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri wa Maji, Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele na ujumbe kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo iliyopo nchini kusaidia mchakato wa ujenzi wa Dam (bwawa la kuzalisha umeme)  la Steigler’s Gorge  Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2017 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Waziri wa Maji, Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele na ujumbe kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo iliyopo nchini kusaidia mchakato wa ujenzi wa Dam (bwawa la kuzalisha umeme)  la Steigler’s Gorge  pamoja na jopo la wataalamu wa Tanzania wanaosimamia mradi huo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono  na Waziri wa Maji, Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele baada ya kupata picha ya pamoja na ujumbe wake kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo iliyopo nchini kusaidia mchakato wa ujenzi wa Dam (bwawa la kuzalisha umeme)  la Steigler’s Gorge  pamoja na jopo la wataalamu wa Tanzania wanaosimamia mradi huo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2017

  0 0


  0 0  0 0
  0 0


  0 0

  IYK Columbus inawakaribisha wote kwenye mkesha wa mafundisho ya neno la Mungu utakaofanyika Ijumaa hii 6/30 kuanzia saa tano usiku katika kanisa la Gethsemane. Anwani ni 35 E Stanton Avenue, Columbus OH.
  Karibuni wote.
  Mbarikiwe

  0 0


  0 0

  Hatimaye kamati ya huru ya uchaguzi ya klabu ya MAJIMAJI imejitokeza mbele ya waandishi wa habari na kutangaza tarehe rasimi ya uchaguzi huo baada ya wanachama kushinikiza kufanyika kwa uchaguzi, ambapo nafasi zinazowania ni mwenyekiti wa klabu,makamu mwnyekiti wa klabu na mjumbe wa bodi .

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dkt. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya tuzo ya Benki kinara wa ubunifu Afrika Mashariki “East African Most Innovative Bank of the year” ambayo Benki hiyo imepewa na jarida la utafiti wa biashara la The Business Year hivi, Katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Benki hiyo, Azikiwe Jijini Dar es salaam Juni 29, 2017.
  Baadhi ya Tuzo walizopata Benki ya CRDB.

  0 0

   Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Mangwi, kata ya mchukwi wilayani kibiti jana alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji na afisa mtendaji wa kijiji. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la polisi.

  Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na wananchi wa kijiji cha mangwi, kata ya mchukwi wilayani kibiti jana alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji na afisa mtendaji wa kijiji hicho. IGP Sirro alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi kijijini hapo kutowafumbia macho wahalifu wanaotenda mauaji hayo na kuwataka kuwa na kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu hao.  picha na hassan mndeme-jeshi la polisi.

   Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro akitoa rambirambi ya msiba kwa wananchi wa kijiji cha mangwi, kata ya mchukwi wilayani kibiti jana alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji ya Mwenyekiti wa kitongoji na Afisa Mtendaji wa kijiji hicho. picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akikagua nyumba iliyochomwa moto na wahalifu waliofanya mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji na afisa mtendaji wa kijiji cha mangwi, kata ya mchukwi wilayani kibiti jana alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji  hayo. picha na hassan mndeme-jeshi la polisi.
  0 0

   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akisisitiza jambo katika kikao cha Kamati ya Uongozi kilichokutana jana usiku katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma, kulia ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama
   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akiongoza kikao cha Kamati ya Uongozi kilichokutana jana usiku katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma, kulia ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama.
   Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge wakiwa tayari kwa ajili ya kuanza kwa kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika jana usiku katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akiongoza kikao cha Kamati ya Uongozi kilichokutana jana usiku katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma, kulia ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama.

  0 0

  Jovina Bujulu-MAELEZO.

  Tanzania ni miongoni mwa nchi 193 zilizosaini mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na kuenea hali ya jangwa duniani (UNCCD). Mkataba huu unalenga kupambana na tatizo la uharibifu wa ardhi katika maeneo yenye ukame na kufanya juhudi za kuyahifadhi.

  Mkataba huu ni muhimu kwa nchi yetu ambayo uchumi wake unategemea ardhi kwa ajili ya kilimo ambacho kinachochea maendeleo na ajira kwa wananchi walio wengi.

  Hivi karibuni dunia iliadhimisha siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame ambayo ilikiongozwa na kauli mbiu isemayo “Ardhi ni makazi yetu tuitunze kwa manufaa ya baadaye”. Kauli mbiu hii inahamasisha jamii kutunza ardhi kwa kuwa ndiyo makazi yetu.

  Akiongea hivi karibuni mjini Dodoma, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba alisema kuwa kauli mbiu hii inahimiza jamii kuongeza juhudi za kutunza ardhi, na kuzingatia maendeleo endelevu ya rasilimali tulizo nazo kwa ajili ya maendeleo ya sasa na kwa vizazi vijavyo.

  Madhumuni ya kuadhimisha siku hii ni pamoja na kuongeza uelewa miongoni mwa jamii na kujua athari za jangwa na ukame katika maisha ya kila siku ya binadamu na jinsi ya kuthibiti hali hiyo.

  “Malengo hayo yanadhihirisha umuhimu wa utunzaji wa ardhi na udongo kwa matumizi endelevu hasa kwa ajili ya kilimo, mifugo, na huduma nyingine kama utalii wa wanyama pori na uwindaji.” Aliongeza Mhe. Makamba.


  0 0

  Afisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Amani Marcel (kuli) akimueleza jambo mmoja wa wateja kuhusu kituo cha Huduma kwa Wateja katika Banda lao kwenye maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa Dar es salaam (Sabasaba) yaliyoanza rasmi jana  Juni 28, 2017 katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam. Kushoto ni Kaimu Meneja Kiongozi wa Masoko na Uhusian wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Salim Kimaro.
  Askari Polisi akipata huduma ya Upimaji afya Bure inayotolewa na NSSF Katika maonyesho ya Sabasaba yaliyoanza jana 
  Afisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Aisha Sango akimsikiliza Mteja katika maonyesho ya Sabasaba yanayondelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa
  Maafisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Nora Mwidunda na Grace Japhet wakizungumza na wageni wakati wa Manyesho ya Sabasaba.

  0 0


  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

  Kaimu Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma amewaasa mawakili kutokuwa mawakala wa kupeleka rushwa mahakamani badala yake wawe mawakala wa kutenda haki na kufuata maadili ya sheria.

  Aidha, amewaasa mawakili hao wasome zaidi sheria za nje ya Tanzania ili pindi wanapotayarisha mikataba iwe mizuri kwa kuwa mikataba mingi inayoingiwa haitegemei sheria ya hapa nchini pekee.

  Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akiwaapisha mawakili 248 kutoka vyuo mbalimbali nchini, ambao wameingizwa katika orodha ya mawakili waliopo Tanzania.

  Profesa Juma amesema Tanzania inaingia mikataba mingi ambayo haitegemei sheria zilizopo nchini, hivyo wanapaswa kusoma zaidi ili wanapoandaa mikataba hiyo iwe kwa maslahi ya taifa.Ameongeza kuwa, wananchi wengi wamekuwa wakitoa maoni yao kwamba kuna tatizo la rushwa mahakamani ambalo halipaswi kufumbiwa macho.

  Amesema ni vema mawakili wakafuata sheria na kuwa na maadili ya kufanya kazi kwa weredi na na siyo kupeleka rushwa mahakamani.

  Aidha amewaambia mawakili hao kuwa, karne ya hii ya sasa inawataka mawakili kutumia ujuzi wao wa sheria sio kutafsiri na kuelewa sheria za Tanzania pekee bali na za Kimataifa pamoja na kupambana na changamoto zinazoikabili nchi.

  Profesa Juma amesema mapambano yao yanatakiwa kulenga kuondoa umasikini kwa kuwa wanasheria wa wanyonge na kuisaidia nchi kufikia malengo yanayotakiwa.

  Pia amewaasa mawakili hao kuangalia gharama walizotumia wazazi wao hadi walipokubaliwa ili wawasaidie na kuisaidia serikali kutoka ilipo.

  Hata hivyo, aliwatoa hofu mawakili hao kwamba Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS), hakiwezi kufutwa kwa kuwa imependekezwa kuwepo kwa mabadiliko ya sheria ambayo hayalengi mtu wala taasisi binafsi bali inaangalia sheria kwa upana wake.

  Alisema wanataka kuangalia mawakili wenye viwango, vyuo vinavyotoa sheria vinakidhi viwango hivyo hawapaswi kuwa na hofu.

  "Tunatarajia vijana hawa wadogo walioapishwa leo wataweza kulitumikia taifa kwa zaidi ya miaka 30, katika umri wa kustaafu wa miaka hivyo tunategemea matokeo chanya kutoka kwao," ameeleza Kaimu Jaji.

  Naye, Rais wa TLS, Tundu Lissu amesema mawakili hao ni wasaidizi wa mahakama katika kutenda haki na kwamba wanatakiwa kuielekeza jamii njia ya utawala wa sheria, haki za binadamu na demokrasia.

  "Idadi ya mawakili Tanzania ni ya pili katika Afrika Mashariki ikiongozwa na Kenya na mwisho Uganda. Kuapishwa kwa mawakili hawa ni jambo jema ambalo Tanzania inajipanua katika utoaji wa huduma," alisema Lissu.

  Mgeni Rasmi Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akifuatilia jambo wakati wa sherehe za 56 za kuwakubali na kuwasajiri, Mawakili wapya 248 mapema hii leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya ndugu wa Mawakili wapya wakisubiri zoezi la kuapishwa kwa ndugu zao mapema hii leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Mawakili wapya wakisubiri zoezi la kuapishwa mapema hii leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
  Mgeni Rasmi Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma (wanne toka kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Majaji na Mawakili wapya mara baada ya kuwaapisha mapema hii leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.Picha na Eliphace Marwa -Maelezo

  0 0

  MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), imejivunia kujenga shule ya kisasa ya msingi ya Tumaini iliyopo kata ya Mafumbo, wilaya ya Bukoba Mjini ili iwe mbadala wa shule ya Tumaini iliyopo eneo la karibu na uzio wa Kiwanja cha ndege.

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Salim Msangi amesema shule hiyo inamajengo tisa yenye madarasa 24 kati ya hayo 21 ni ya watoto wasio na mahitaji maalum na matatu ni ya watoto wenye mahitaji maalum; zipo ofisi za walimu, vyoo vya shule na vya walimu, na nyumba ya kukaa mwalimu mmoja.

  “Ninaona fahari kubwa na nimefarijika sana kuona shule imekamilika kwa kiwango kikubwa na sasa watoto wetu watasoma katika mazingira ya ya utulivu na amani tofauti na awali katika shule ya Tumaini kulikuwa na kelele za ndege kila zinapotua na zinaporuka,” amesema bw. Msangi.

  Pia Bw. Msangi amesema shule ya zamani ilikuwa katika maeneo hatarishi ya karibu na barabara ya kutua na kuruka kwa ndege, jambo ambalo lingeweza kuleta maafa makubwa endapo kungetokea ajali maeneo hayo.

  Naye mkandarasi wa mradi huo kutoka kampuni ya ujenzi ya CMG ya Mwanza, Mhandisi Jumanne Warema amesema pia madarasa hayo yatawekewa madawadi 315, meza na viti 16 za walimu na madarasa ya watoto wenye mahitaji yatawekwa viti maalumu 48.

  Mkuu wa shule ya Tumaini, Bw. Theophil Ndyakowa ameishukuru TAA kwa msaada huo mkubwa walioutoa kwa ujenzi wa shule ya kisasa, ambapo sasa wanafunzi watasoma kwa bidii zaidi.

  Hata hivyo mradi huo wa shule umedhaminiwa na Benki ya Dunia, ambapo pia wamefanikisha ujenzi wa jengo la kisasa la abiria, jengo la kuhifadhi umeme na kukarabati barabara ya kutua na kuruka kwa ndege.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dr. Leonard Chamuriho (watatu kushoto) akiwafafanulia jambo wahandisi Diana Munubi na Mbila Mdemu (kushoto) huku Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi (mwenye suti nyeusi) akisikiliza mara baada ya kukagua shule mpya ya msingi ya kisasa ya Tumaini iliyopo Bukoba.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wa shule ya kisasa ya msingi ya Tumaini iliyopo kata ya Mafumbo, wilaya ya Bukoba Mjini.
  Wanafunzi waliohamishiwa kutoka katika shule ya msingi Tumaini iliyokuwa maeneo ya karibu na kiwanja cha ndege cha Bukoba, sasa wakiwa mapumziko kwenye shule mpya iliyojengwa maeneo ya Mafumbo kwa usimamizi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA


  0 0

   Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Congo, Ferre Gola, (wa pili kulia) Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Ltd, Teddy Mapunda (kulia) na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru mchanganyiko, Anna Mshana, kwa pamoja wakipaka rangi katika ukuta wa chumba cha darasa la Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, wakati walipofika shuleni hapo kwa ajili ya kujionea mazingira ya shule hiyo, baada ya kuomba kusaidiwa mahitaji hayo, ambapo msaada huo umetokana na mauzo ya meza za Onyesho maalumu la mwanamuziki huyo linalofanyika leo Alhamisi kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
   Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Congo, Ferre Gola, (kushoto) na Christian Bella,  kwa pamoja wakipaka rangi katika ukuta wa chumba cha darasa la Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, wakati walipofika shuleni hapo kwa ajili ya kujionea mazingira ya shule hiyo, baada ya kuomba kusaidiwa mahitaji hayo, ambapo msaada huo umetokana na mauzo ya meza za Onyesho maalumu la mwanamuziki huyo linalofanyika leo Alhamisi kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Ltd, Teddy Mapunda, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya mwanamuziki wa kimataifa kutoka Congo, Ferre Gola (wa pili kulia) na Christian Bella (kulia) walipofika SHule ya Uhuru Mchanganyiko kwa ajili ya kukabidhi na kupaka rangi katika baadhi ya vyumba vya madarasa ya shule hiyo. msaada huo umetokana na mauzo ya meza za Onyesho maalumu la mwanamuziki huyo linalofanyika leo Alhamisi kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
   Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Anna Mshana, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya mwanamuziki wa kimataifa kutoka Congo, Ferre Gola (wa pili kulia) na Christian Bella (kulia) walipofika Shule ya Uhuru Mchanganyiko kwa ajili ya kukabidhi na kupaka rangi katika baadhi ya vyumba vya madarasa ya shule hiyo. msaada huo umetokana na mauzo ya meza za Onyesho maalumu la mwanamuziki huyo linalofanyika leo Alhamisi kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  WAZIRI wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba amewataka viongozi wa miradi ya kilimo inayofadhiliwa na serikalipamoja na mashirika ya misaada kuzingatia malengo ya kuanzishwa miradi hiyo ili kuongeza uzalishaji wa chakula nchini.

  Akizungumza katika skimu ya umwagiliaji ya Dakawa mkoani Morogoro hivi karibuni Dkt. Tizeba alisema wakulima hawana sababu ya kuwa na hiyari kwani fedha zinazotolewa ni nyingi na wahisani pamoja na serikali wanataka kuona matokeo ya misaada hiyo.

  “Naomba unisikilize ndugu mwenyekiti, waliopewa pesa kwa ajili ya kilimo wasiwe na hiyari ya kulima, hatuwezi kuendelea kusikia tu wenzetu wanavuna tani nyingi katika mataifa mengine ikiwa sisi bado tunaendelea hivi hivi,” alisema Dkt. Tizeba na kusisitiza:“Anayetaka kukaa hapa kwenye skimu akae kwa kufuata masharti na asiyetaka aondoke apishe wengine. 

  USAID (Shirika la misaada la watu wa Marekani) kiasi walichotoa kinafikia Sh bilioni 29, tukizigawa kila mmoja anapata Sh milioni 60. Naombeni make halafu mkubaliane kuwa suala la kufanya kilimo cha hiyari katika maeneo tuliyofadhili hatutaki kusikia. Msimu ujao tunataka tuvune tani 12 katika skimu hii.”

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo, Dkt. Filimini Mizambwa amesema ili taasisi zinazosaidia wakulima ziendelee kuwepo lazima wakulima hasa wadogo waonyeshe tija katika shughuli wanazofanya ikiwemo kuonyesha matokeo mazuri wakati wa mavuno.

  “Ili sisi tuendelee kuwepo lazima wakulima hasa mkulima mdogo fanikiwe, wito wangu wakulima wajifunze kilimo chenye tija na kufanya kazi kwa juhudi ili kuwaonyesha wafadhili fedha zao hazipotei bure kwa uzembe.


  0 0

  Na Robert Hokororo


  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack amefanya ziara wilayani Kishapu kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

  Katika ziara hiyo Telack alikagua mradi wa huduma ya maji kutoka Ziwa Victoria uliopo kata ya Maganzo na maendeleo ya ujenzi wa zahanati kata ya Shagihilu.

  Mradi mwingine ni wa mjasiriamali wa kusindika alizeti na kukoboa nafaka za mpunga na mahindi ambao unatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.Kwenye kata ya Kishapu eneo la Mhunze alitembelea mradi mwingine wa ghala la kuhifadhi nafaka na mashine za kukoboa nafaka za mahindi na mpunga.

  Katika ziara hiyo kiongozi huyo aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Albert Msovela na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa akiwemo Kamanda wa Polisi Mkoa was Shinyanga, Muliro Jumanne Muliro.

  Alikaribishwa na mwenyeji wake, Mkuu wa wilaya, Nyabaganga Talaba, Katibu Tawala Wilaya, Shadrack Kangese, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga, Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya na wakuu wa idara katika halmashauri hiyo.
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto) akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga wakati wa ziara yake wilayani humo. Wengine pichani kulia ni Kamanda wa Polisi mkoa huo, Muliro Jumanne Muliro.
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akiangalia mashine za kukoboa na kusaga nafaka pamoja na kusindika alizeti kutoka mjasiriamali Mzee Nassoro alipokuwa kata ya Mwamamalasa.
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kulia) akiwa na Katibu Tawala Mkoa, Albert Msovela (katikati) pamoja na Katibu Tawala Wilaya, Shadrack Kangese (kushoto) wakati wa ziara.


  0 0

  Benny Mwaipaja, WFM - Dodoma

  Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO), inakamilisha majaribio ya utafiti wa hali ya umasikini katika mikoa ya Dodoma na Kilimanjaro kabla ya kuanza utafiti huo nchi nzima mwezi Agosti, mwaka huu.

  Hayo yamesemwa mjini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa wakati Ujumbe kutoka Benki ya Dunia ulipotembelea na kukagua ujenzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu mjini humo.

  Amesema kuwa ana matarajio kwamba mchakato wa taarifa za utafiti huo zitafanywa mjini Dodoma baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Ofisi hiyo inayojengwa kwa gharama ya shilingi 11.6 bilioni, zikiwa ni fedha za mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia.

  Dkt. Chuwa ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa wakusanya taarifa za utafiti huo ili Serikali iweze kupata takwimu sahihi za hali ya umasikini nchini kwa ajili ya kutathmini programu mbalimbali na kupanga mipango ya maendeleo ya wananchi wake.
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina chuwa (wa pili kushoto) akingalia kitofali kinachotengezwa na mkandarasi anayejenga jengo la Taasisi hiyo wakati Ujumbe kutoka Benki ya Dunia ulipotembelea na kukagua ujenzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu linalojengwa mkoani Dodoma.
  Mshauri wa Masuala ya Kitakwimu kutoka Benki ya Dunia nchini Tanzania, Elizabeth Talbert (kushoto) akisisitiza jambo wakati Ujumbe kutoka Benki hiyo ulipotembelea na kukagua ujenzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu linalojengwa mkoani Dodoma.
  Mkandarasi Msanifu Majengo, Mhandisi Shomvi (aliyevaa sweta kulia) anayesimamia ujenzi wa jengo la ofisi ya Taifa ya Takwimu linalojengwa Mkoani Dodoma akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo wakati Ujumbe kutoka Benki ya Dunia ulipotembelea na kukagua ujenzi wa Jengo hilo mjini Dodoma.
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina chuwa (wa pili kushoto) akifurahia jambo na timu ya wataalamu wa ujenzi na ujumbe kutoka Benki ya Dunia ulipotembelea na kukagua ujenzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu linalojengwa mkoani Dodoma.
  (Picha: Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM).


older | 1 | .... | 1772 | 1773 | (Page 1774) | 1775 | 1776 | .... | 3272 | newer