Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1771 | 1772 | (Page 1773) | 1774 | 1775 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Na Octavian Kimario-WHUSM Dodoma.

  Wazo la kuwarudisha nchini Dinosaria halina tija kutokana na ugumu wa Kiteknolojia na gharama ikilinganishwa na faida za kuchukua hatua hiyo.

  Akijibu swali la Mbunge wa Mchinga Mhe. Hamidu Hassan Bobali lililo uliza,Ni nini kauli ya mwisho ya Serikali kuhusu faida ambayo wananchi wa Lindi na Tanzania kwa ujumla wananufaika kutokana na mabaki hayo.


  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Ramo Makani amesema Tanzania itaendelea kusisitiza kupata manufaa kutokana na uwepo wa Dinosaria wake huko Berlin-Ujererumani.


  “Kufuatia majadiliano ya kina yaliyohusisha wataalamu wabobezi katika masuala ya Malikale kutoka pande zote mbili imekubalika kuwa Serikali ya Ujerumani itaendesha shughuli za utafiti zaidi huko Tendaguru na katika maeneo jirani ili kuwezesha uchimbaji wa mabaki ya Dinosaria wengine yanayoaminika kuwepo katika maeneo hayo pamoja na kuanzisha Kituo cha Makumbusho ili shughuli za Utalii zifanyike katika eneo hilo na kuvutia watalii kutoka nchini na nje ya nchi” alisisitiza Mhe. Makani.


  Kuhusu Serikali kupunjwa mapato yatokanayo na viingilio katika Makumbusho ya Elimu Viumbe ya Berlin,Mhandisi Makani amesema jambo hilo halina ukweli wowote kwani ni ngumu kufahamu ni kiasi gani hupatikana kama kiingilio kuwaona Mijusi kutoka Tanzania kwakuwa Makumbusho hiyo ina kumbi nyingi zenye masalia kutoka nchi mbali mbali za Afrika na gharama za kuendesha Makumbusho hiyo hutolewa na Serikali ya Ujerumani.

  Ameeleza kuwa Serikali ya Ujerumani itafadhili zoezi la uimarishaji idara inayohusika na Malikale katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuwezesha upatikanaji wa wataalamu wa kutosha wa fani husika ilikuendeleza Utalii wa Malikale nchini.


  Mijusi mikubwa (Dinosaria) ilichimbwa katika Kilima cha Tendaguru,mkoani Lindi kati ya waka 1909 na mwaka 1913 na kupelekwa katika makumbusho ya Elimu Viumbe ya Berlin nchini Ujerumani.


  0 0

   Jengo moja lililopo mtaa wa India jirani na Sabodo Parking Tower jijini Dar es salaam limeshika moto mchana huu ambapo vikosi vya zimamoto vimefika eneo la tukio na kufanikiwa kuuzima. Chanzo na madhara yaliyotokana na moto huo bado kujulikana.


  0 0

  Na Zainab Nyamka-Globu ya Jamii.

  TIMU ya Mtibwa Sugar imewatema wachezaji saba wakikosi hicho waliomaliza mikataba yao na kufanikiwa kusajili chipukizi wawili wapya ambao ni beki wa kati, Hussein Iddi na mshambuliaji Salum Ramadhani kw ajili ya msimu mpya wa mwaka 2017/18. 

  Katika wachezaaji saba walioruhusiwa kuondoka katika timu hiyo ni pamoja na aliyewahi kuwa mshambuliaji wa Yanga Said Bahanuzi baada kumaliza mkataba wake 

  Mkurugenzi wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser amesema kuwa beki Hussein Idd ametokea katika timu ya JKT Oljoro ya Arusha na Salum Ramadhani ametokea Polisi Morogoro na kila mmoja amesaini mkataba wa miaka miwili kila mmoja na ni matumaini ya Mtibwa Sugar watang’ara Manungu. 

  Pamoja na hayo, Bayser amesema kwamba wanatarajia benchi la Ufundi chini ya Kocha Mkuu Zubeiry Katwila kupandisha baadhi ya wachezaji kutoka katika timu ya vijana ya Mtibwa Sugar. 

  “Uongozi wa Mtibwa Sugar unaendelea kufanyia kazi mapendekezo ya benchi la ufundi, hivyo basi usajili bado unaendelea na nyota wengine wanatarajiwa kuingia makubaliano na Mtibwa Sugar wakati wowote kuanzia sasa,”amesema. 

  Aidha, Bayser amesema kwamba Mtibwa Sugar imeachana na Jaffary Salum Kibaya, Said Mkopi, Maulid Gole ‘Adebayor’, Said Bahanuzi, Vincent Barnabas, Ally Lundenga na Ally Shomary ambao wamemaliza mikataba yao. 

  Mtibwa inasifika mno kwa kuibua wachezaji chipukizi kutoka timu mbalimbali ndogo na wengine kupandisha kutoka kikosi chake cha vijana ambao baadaye hugeuka lulu na kugombewa na timu kubwa, hususan Simba na Yanga.
  Said Bahanuzi akimtoka kwa kasi beki mwingine wa JKT

  0 0

  Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara imewaachia huru Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Lindi Suleiman Mathew  (pichani) na mwenzake Ismail Kupilila ambaye ni Katibu wa CHADEMA Tawi la Nyangamara.. 

  Viongozi hawa walihukumiwa adhabu ya kifungo miezi nane jela bila faini na Mahakama ya Wilaya ya Lindi mnamo 18.01.2017 na kufanikiwa kutoka kwa dhamana baada ya kukata rufaa na kukata hati ya ya dharura kwa ajili ya dhamana. 

  Wakati anasoma hukumu hiyo Jaji Lameck Mlacha alisema kwamba kosa la kusanyiko lisilo halali linatakiwa kufanywa na watu watatu au zaidi sio wawili. Akasema pia kwamba vifungo vyao vimefutwa. Wako huru kwa sababu hawana hatia. 

  Viongozi hao wa Chadema walihukumiwa kifungo cha gerezani tangu Januari mwaka huu, kabla ya kukata rufaa kupinga hukumu ya kesi hiyo iliyofunguliwa februari 8, mwaka jana na kutoka kwa dhamana .

  Machi 7 mwaka huu Wakili wa viongozi hao wa Chadema, Deusdedit Kamalamo alisema kuwa baada ya mahakama kuwahukumu wateja wake kwenda jela miezi minane na kutoa nafasi ya kukata rufaa, walikata rufaa na kukata hati ya dharura kwa ajili ya dhamana. 

  Mahakama Kuu iliwaachia kwa dhamana Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi, Seleman Methew na Katibu wa Tawi wa kata ya Nyangamala, Ismail Kupilila waliokuwa wakitumikia kifungo cha miezi minane kwa kosa la kufanya mikutano bila kibali baada ya kuona kuna kesi ya kusikiliza. 

  Kabla ya kutoa uamuzi wa kesi hiyo namba 1 ya mwaka 2017, Jaji Lameck Mlacha wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mtwara, alisikiliza hoja za pande zote mbili katika shauri hilo na baadaye kuwaachia huru kwa kuwataka waweke dhamana ya sh. 2 milioni kwa kila mmoja.
  Viongozi hao wa Chadema wamekuwa gerezani tangu Januari mwaka huu, kabla ya kukata rufaa kupinga hukumu ya kesi hiyo iliyofunguliwa februari 8, mwaka jana.

  0 0

     Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, pamoja na Mwenyekiti wa Mtandao wa Kuondoa Umasikini Ndg. Mungwe Athuman (kulia) wakimkabidhi  kitabu Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Manghweta Ndg. Elinetha Kimaro (kushoto) wakati wakigawa vitabu Mbali mbali kwa Shule za Sekondari zilizopo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma. 
  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Mtandao wa Kuondoa Umasikini Ndg. Mungwe Athumani (kulia) wakikabidhi vitabu kwa Mwl. Mkuu wa Shule ya sekondari Iduo Ndg. Cathbert Kalindo, Shule iliyopo Wilaya ni Kongwa Mkoani Dodoma.
   
   Spika wa Bunge Mhe Job  Ndugai (wa pili kushoto) akizungumza na Wazazi wa Wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Sekondari Laikala iliyopo Wilayani Kongwa, Dodoma wakati wa zoezi la kugawa Vitabu shuleni hapo  vilivyotolewa na Mtandao Kuondoa Umasikini, kushoto ni Meneja wa Mtandao huo Ndg. Peter Yobwa.
     Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (wa tatu kulia) akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ibwaga iliyopo Wilayani Kongwa, Dodoma baada ya kugawa vitabu shuleni hapo, vitabu hivyo  vimetolewa na Mtandao wa kuondoa Umasikini. Kulia kwa Spika ni Mweyekiti wa Mtandao huo Ndg. Mungwe Athuman  na kushoto kwake ni Meneja wa Mtandao huo Ndg. Peter Yobwa. Zoezi la ugwaji wa vitabu hivyo lilianza  toka wiki iliyopita ambapo takribani shule thelathini za Sekondari zilizopo Wilaya ya Kogwa, Dodoma zimenufaika na msaada huo. (Picha na Ofisi ya Bunge).


  0 0

  Waziri  Mkuu Kassim  Majaliwa  akisikiliza jambo kutoka  kwa  Mbunge  wa Kigoma  Kaskazini  Peter  Serukamba  (CCM).  walipo kutana katika viwanja vya Bunge  Mjini Dododma  leo June 28, 2017.


  0 0

   Watanzania wenye asili ya kihindi wakiwa kwenye kifaa kinachotumika na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, baada ya jengo lililopo Mtaa wa Indira Ghandhi,jijini Dar es Salaam, kushika moto ambao ulifanikiwa kuzimwa na askari wa jeshi hilo kabla ya kuleta madhara.Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

   Askari wa  Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakiwa katika shughuli za uzimaji moto baada ya jengo lililopo Mtaa wa Indira Ghandhi,jijini Dar es Salaam,kushika moto ambao ulifanikiwa kuzimwa na askari wa jeshi hilo kabla haujaleta madhara.Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

   Askari wa  Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakijiandaa kupokea waathirika wa janga la moto  katika shughuli za uzimaji moto baada ya jengo lililopo Mtaa wa Indira Ghandhi,jijini Dar es Salaam,kushika moto ambao ulifanikiwa kuzimwa na askari wa jeshi hilo kabla haujaleta madhara.Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

   Jengo la ghorofa 12 lililopo Mtaa wa Indira Ghandhi lililoshika moto na kufanikiwa kuzimwa na askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,leo jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji

  Kifaa kinachotumika na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  kuzima moto,kuokolea watu na mali kwenye majengo marefu, kikisaidia uokoaji  katika  jengo lililopo Mtaa wa Indira Ghandhi,jijini Dar es Salaam, baada ya kushika moto ambao ulifanikiwa kuzimwa na askari wa jeshi hilo kabla haujaleta madhara.Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI


  0 0


  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

  MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka waendesha mashitaka, polisi na wapelelezi wa kesi za wanyamapori na misitu kubadilika katika kazi zao ili kulinda rasilimali hizo kwa vizazi vya sasa na vijavyo.Aidha, ameitaka mahakama kutoa muongozo kwa watumishi wake kuhusu namna ya kuendesha kesi zinazohusiana na nyara za serikali kwa lengo la kuwa na uwiano sawa katika utoaji amri.

  Samia amesema hayo leo mjini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mwongozo kwa wapelelezi, waendesha mashitaka na Polisi wa kesi za wanyamapori na misitu ulioandaliwa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP).

  Amesema wote hao wanatakiwa kufanya kazi zao ipasavyo kuhakikisha usalama wa wanyamapori na misitu kwani kwa kupoteza maloiasili hizo kunafanya uchumi wa nchi kushuka na kwamba wasifanye kazi hiyo kwa kuweka mazingira ya rushwa.

  Amesema, kazi za kupeleleza na kuendesha kesi za wanyamapori zimekuwa na ushawishi mkubwa wa rushwa kutoka kwa wahusika na kuwataka kufikiria maslahi mapana ya nchi na sio wao binafsi.

  "Jamani, msiogope kufa, kifo kipo na kila mmoja wetu atakufa hata mnyama ikiwemo huyo FaruJohn, muhumu ni namna ya kujua aina ya kifo utakachokufa, lakini Jambo la kusikitisha mmekuwa mkiponzwa na fedha, wahenga walisema 'fedha ni sabuni ya roho lakini pia walisema fedha ni fedheha," amesema Samia.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akikata utepe kuashiria Uzinduzi Kitabu cha Mwongozo kwa Wapelelezi na Waendesha Mashitaka wa Kesi za Wanyamapori na Misitu kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wengine pichani ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (kulia),Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw.  Alvaro Rodrigues na kushoto ni Muendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali Biswalo Mganga na Naibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais - Ikulu) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Naibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni Kitabu cha Mwongozo kwa Wapelelezi na Waendesha Mashitaka wa Kesi za Wanyamapori na Misitu kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, katikati ni Muendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali Biswalo Mganga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais - Ikulu)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Mwongozo kwa Wapelelezi na Waendesha Mashitaka wa Kesi za Wanyamapori na Misitu kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais - Ikulu).


  0 0


  0 0

  Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akimkaribisha Ofisini kwake, Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza (UK), Kangoma Kapinga, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Mwenyekiti huyo ambaye alifuatana na Katibu wa CCM wa tawi hilo Leybab Mdegela alifanya mazungumzo na Kanali Lubinga ikiwemo haja ya kuimarishwa matawi ya CCM yaliyopo nchi za nje.
  Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza Kangoma Kapinga akisaini kitabu cha wageni Ofisini kwa Kanali Ngemela (katikati), kabla ya mazungumzo yao kuanza. Kushoto ni Katibu wa CCM Tawi la Uingereza Leybab Mdegela.
  Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akifafanua jambo wakati akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza Kangoma Kapinga (kulia), katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Katibu wa CCM wa tawi hilo Laybab Mdegela. PICHA: BASHIR NKOROMO-CCM Blog.


  0 0

   Na Rhoda Ezekiel Kigoma, 

  BARAZA la madiwani halmashauri ya Wilayani Buhigwe limemuondoa rasmi Madarakani aliekuwa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Elisha Bagwanya kufuatia kuthibitishwa kwa tuhuma mbili kati ya saba zilizokuwa zimewasilishwa kwa tume hiyo zikimkabili Mwenyekiti huyo, moja ikiwa ni kutumia vibaya madaraka na kuisababishia hasara halmashauri .

  Uamuzi huo umetolewa leo katika viwanja vya Shule ya msingi Buhigwe mara baada ya madiwani wa baraza hilo kupiga kura ya ndio kuunga mkono taarifa ya kamati ya Mkuu wa Mkoa kigoma Brigedia Jeneral Emanuel Maganga, iliyokuwa imebaini ukweli wa tuhuma mbili kati ya saba zilizo wasilishwa na madiwani hao na kumtaka mkurugenzi na Baraza kumuondoa Mwenyekiti huyo.

  Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Anosta Nyamoga, alithibutisha kumuondoa mwenywkiti huyo kwa kutangaza matokeo ya kura 20 za ndio na saba za hapana zilizo pigwa na Madiwani wa Halmashauri hiyo .

  Nyamoga alisema mnamo tarehe 25 machi alipokea barua kutoka kwa madiwani 20 wa halmashauri hiyo ya kutokuwa na imani na mwenyekiti wa halmashauri na kwa mujibu wa kanuni Na 4(3) ya kanuni za kudumu za Halmashauri,  wajumbe wa Mkutano wasiopungua theluthi mbili wanaweza kuomba kuitishwa kwa mkutano kwa lengo la kujadili agenda ya kumuondoa madarakani mwenyekiti wa halmashauri kutokana na sababu zinazotajwa.

  Alisema tume ya mkuu wa mkoa baada ya kupitia tuhuma zote saba zilizotajwa katika barua hiyo ilibaini tuhuma mbili ni za ukweli na zinamnyima Mwenyekiti huyo sifa za kuwa kiongozi, tuhuma hizo ni pamoja na kufanya kazi ya ukandarasi na halmashauri kwa kutumia kampuni yake inayoitwa BUYENZI GENERAL SUPPLIES kwa kazi ya mradi wa maji Nyamugali ambao ni mbovu ,mradi wa Barabara ya Kijiji cha Kigogwe Mrungu,kujenga mradi huo kwa kutumia kampuni ya NGELUKE CONSTRUCTIONS kwa kutumia uwezo wake kama mwenyekiti wa halmashauri na kuzuia miradi hiyo isikaguliwe.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Elisha Bagwanya alievaa suti ya rangi ya Blue 
  Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya  ya Buhigwe Anosta Nyamoga akiwasilisha taarifa ya tume ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma dhidi ya Mwenyekiti wa halmashauri hiyo

  Baadhi ya Madiwani.  0 0

  Na Zainab Nyamka-Globu ya Jamii.
  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imethibitisha kuwashikilia Rais wa TFF Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake Selestine Mwesigwa kwa mahojiano.
  Afisa uhusiano wa TAKUKURU Musa Misalaba amesema, ni kweli wanawashikilia viongozi wa TFF kwa ajili ya mahojiano ambapo wamekuwa wakifanya uchunguzi kwa muda mrefu kabla ya kuamua kuwashikilia kwa ajili ya mahojiano.
  “Ni kweli kwamba tunaendelea na uchunguzi dhidi ya viongozi mbalimbali wa TFF na uchunguzi huo tumekuwa nao kwa muda mrefu lakini kuhusu kuwashikilia kwa nini, bado ni siri yetu upande wa uchunguzi, katika uchunguzi tunaongozwa na misingi ya sheria, kanuni na taratibu hatuwezi tukaweka wazi kila jambo.”

  Misalaba amesema kuwa Jambo la msingi ambalo wananchi wanatakiwa kuelewa ni kwamba, kuna uchunguzi ambao wanaendelea nao ambao umekuwa ukifanywa kwa muda mrefu na kuhusiana kuwashikilia Malinzi na Mwesigwa wamesema muda wa uchunguzi ukikamilika watawapeleka mahakamani.
  “Tunawashikilia na bado tuko nao chini ya ulinzi wetu , tunaongozwa na sheria tutakapomaliza uchunguzi wetu tutaweka wazi kama ni kuwaachia ila ushahidi ndio utakaoamua lakini ni lini ni swala kiuchiunguzi, lakini ni siri ya uchunguzi.”
  Hivi karibuni gazeti la Nipashe liliandika mfululizo wa makala zilizokuwa zikielezea tuhuma za ufisadi zilielekezwa kwa Malinzi na viongozi wenzake wa TFF.

  Rais wa TFF Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake Selestine Mwesigwa.

  0 0

   Naibu Mhifadhi (Huduma za Shirika) wa Mamlaka ya  Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Asangye N. Bangu (kushoto), akipeana mkono na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa TFF wa Maendeleo ya Soka (TFDF), Derek Murusuri. Bw Bangu alizitembelea ofisi za TFDF ili kujadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano kati ya Mamlaka yake na Mfuko huo. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi za TFDF zilizoko Mikocheni jijini Dar Es Salaam leo (28 June 2017).
  Katika mazungumzo hayo, Bw Bangu ameahidi kushirikiana na Mfuko huo katika kuendeleza soka la Tanzania.
  Timu ya Taifa ya vijana walio chini ya miaka 20 (U-20), Ngorongoro Heroes, inatumia jina la Mamlaka hiyo ya Taifa ambayo pia ni mojawapo ya maajabu saba ya dunia.


  0 0


  Mafunzo special ya Urembo, kutoka kwa Mwanadada mwenye Vyeti vyenye Uthibitisho wa Kimataifa wa MakeUp Artistry & Beauty Influence (DYF Certified/MakeUpByMario Certified)

  Njoo ujifunze kutumia MakeUp, Ujanja wa kitaalamu, Siri za upakaji wanazotumia professionals, Reviews za bidhaa mbalimbali za Urembo, kipengele cha Maswali na Majibu kuhusu Urembo na Bidhaa zake, na pia Zawadi mbali mbali (goodie bags) zitatolewa kwa washiriki.

  Kama wewe ndio kwanza unaanza kujifunza au tayari ni MakeUp Artist (MUA) na unataka kuongeza ujuzi, basi fanya booking maana hii ni kwaajili yenu na wote mnakaribishwa. Itakuwa ni Regency Hotel (Mikocheni) tarehe 8 na 9 za Mwezi wa Saba (July). Kwa Booking na Maelezo zaidi wasiliana kwa namba 0685219111 au follow @cherie_mals !! HII SIO YA KUKOSA (wahi maana nafasi ni chache)
  #101BeautyClass #CherieMals #CherieOnTheBeat #SharingIsCaring #MakeUpArt
  #2DayClass #WaremboNaUrembo

  0 0

  Na Dotto Mwaibale
  CHAMA cha Wananchi (CUF), kinatarajia kumfikisha mahakamani  Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) 
   kwa kukiuka taratibu za sheria ya wadhamini kwa kutojiridhisha juu ya uhalali wa majina ya Bodi ya Wadhamini yaliyofikishwa kwake kama yalipitishwa na kikao halali cha chama kwa mujibu wa katiba.
  Kauli hiyo ameitoa Katibu  Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seifjijini Dar es Salaam leo wakati akizungumza na waandishi wa habari.
  Alisema wanachukua hautua hiyo kutokana RITA kushindwa kutumia mwongozo na weledi katika kutekeleza majukumu yao na badala yake wamesukumwa na utashi binafsi kwa ajili ya hujuma dhidi ya chama hicho.
  “Chama chetu kimepatwa na mshituko mkubwa sana, kuona taasisi kubwa nan yeti yenye dhamana kubwa katika nchi inaweza kufanya vitendo vya ovyo. RITA ni taasisi inayobeba maisha ya watu ya kila siku. Licha ya kusajili Bodi za Wadhamini, inasajili vizazi na vifo, ndoa, talaka na inatunza wosia kwa ajili ya mirathi,” alisema Maalim.
  Alisema michakato wa kufungua kesi hiyo inaanza leo ambapo alieleza kuwa tayari wamekwisha agiza mwawakili kulishughulikia. Kutokana na matarajio ya ufunguzi wa kesi hiyo watawasilisha maombi mbele ya Mahakama Kuu kuitaka isimamishe kesi nyingine zote walizofungua kuhusiana na kadhia hiyo hadi hapo shauri linalohusu uhalali wa maamuzi ya RITA  litakapoamuliwa.
  Maalim alisema kusajiliwa kwa bodi hiyo ambayo aliiita kuwa ni bodi feki, alieleza kwamba ni mwendelezo wa kukihujumu na kukidhoofisha chama kunakofanywa dola kupitia kwa Msajili wa Vyama vya Siasa pamoja na Profesa Ibrahim Lipumba na kundi lake.
  Alitaja mambo manne ambayo yalikuwa msukumo wa kusajiliwa kwa bodi hiyo. Alisema kuwa ni kwa ajili ya kufuta kesi zote zilizofunguliwa na ambazo zinawaelemea licha ya kutumia nguvu kubwa ya dola, kufungua akaunti mpya ya benki ili kumwezesha Profesa Lipumba kupata ruzuku.
  Aliongeza mengine kuwa ni Bodi hiyo kuwezesha udhibiti wa Ofisi za Makao Makuu, Zanzibar pamoaja na kumwondoa madarakani Katibu Mkuu Maalim Seif Hamad na hivyo kufanikisha njama za kuwapokonya haki Wazanzibar kwa maamuzi yao ya Oktoba 25 mwaka 2015.
  Hamadi alisema kamwe  haki ya Wazanzibar haitapotea na kuahidi kuwa ndani ya miezi mitatu haki hiyo itakuwa imepatikana.
  Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi(CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu madai ya muendelezo wa hujuma dhidi ya chama hicho zinazofanywa na ofisi ya msaji wa vyama vya siasa nchini. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu wa chama hicho, Seveline Mwijage.
   Maofisa wa Chama hicho wakiwa meza kuu wakati wa mkutano na wanahabari.
   Wabunge wa chama hicho wakiwa kwenye mkutano huo.
   Baadhi ya wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
   Wapiga picha kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.

  0 0

  Baadhi ya wanachama wa majimaji wameutuhumu uongozi uliopo madarakani kwa ubadhilifu wa mali za klabu hiyo na kudai ndio chanzo cha kuchelewesha uchaguzi wa viongozi wapya.

  0 0
 • 06/28/17--10:24: Article 8


 • 0 0
  0 0

  Na Chalila Kibuda, Dodoma
  Vijana wengi wanaangamia kutokana na kutumia dawa za kulevya na kufanya taifa kukosa nguvu kazi ya kufanya uzalishaji.
  Hayo ameyasema leo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square mkoani hapa, amesema kuwa vijana kuwa na familia wameshindwa kuwa wazalishaji kwa kuishia katika matumizi ya dawa za kulevya.
  Amesema vita ya dawa za kulevya ilishatangazwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli na wengine ni kufanya utekelezaji kuhakikisha linafanikiwa dhidi vita ya dawa za kulevya.
  Rugimbana amesema kuwa Dodoma inalengwa na kuwindwa kutokana na vyuo vingi kuwepo hali ambayo vijana wanaweza kungeuka na kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya.Katika maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa amepiga marufuku matumizi ya shisha katika hoteli zilizopo katika mkoa wake kutokana na kuwa sehemu ya dawa za kulevya.
  Aidha amemuomba Mkurugenzi wa Life and Hope Sober House ya Bagamoyo, Al- Karim Bhanji kujenga sober house katika mkoa wa Dodoma kutokana na kuwepo kwa kundi la vijana ambao wameathrika na matumizi ya dawa za kulevya.
  Bhanji amesema kuwa wanaangalia uwezo katika kuweza kujenga kituo ili kuweza kuwarudisha vijana kutoka katika matumizi ya dawa za kulevya na kuwa wazalishaji katika taifa lao.Amesema kuwa vijana wanaathirika sana na matumizi dawa za kulevya na kufanya familia zao kuwa na mzigo wa kuwategemea wazazi wakati wazazi hao walitakiwa kusaidiwa na vijana wao.
  Katika maonesho hayo yameshirikisha umoja wa vituo vya kuhudumia walioathirika na dawa za kulevya Voice of Sober Houses (VOS).
  Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Rogers Sianga akipeana mkono na Mkurugenzi wa Life and Hope Sober House ya Bagamoyo Bw. Al- Karim Bhanji jana wakati maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Jana.

  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Jordan Rugimbana akipeana mkono na Mkurugenzi wa Life and Hope, Sober House ya Bagamoyo, Al- Karim Bhanji wakati alipotembelea banda la Life and Hope, Sober House ya Bagamoyo katika maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.

  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Jordan Rugimbana akipata maelezo katika banda la Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya kutoka kwa Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya, Anastazia Sauli katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.

  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Jordan Rugimbana akizungumza na katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma .


  0 0


older | 1 | .... | 1771 | 1772 | (Page 1773) | 1774 | 1775 | .... | 3285 | newer