Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 29/06/2017


MAMIA YA WANANCHI WAMIMINIKA SABASABA KUSAJILIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA

$
0
0
Wananchi kutoka viunga mbalimbali vya Mkoa wa Dar-es-salaam wameendelea kumiminika katika Banda la Maonyesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) lililopo kwenye hema la Jakaya Mrisho Kikwete kuchangamkia Ofa ya Kusajiliwa na kupata Vitambulisho vya Taifa, ndani ya siku za Maonyesho hayo yanayoendelea katika Viwanja ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. 
Mbali na kusajiliwa; baadhi wamejitokeza kupata taarifa za Usajili waliofanya siku za nyuma na kujifunza zaidi kuhusu matumizi na faida za Vitambulisho vya Taifa ambavyo vimeanza kutumika katika huduma mbalimbali nchini zinazotolewa na baadhi ya Taasisi na Mashirika ya Serikali yakiwemo makampuni ya Simu. 
Akizungumza kupitia vyombo mbalimbali vya Habari leo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano (NIDA), Bi. Rose J. Mdami amewataka wananchi kutumia vizuri fursa hii hususani wananchi na wakazi wa mkoa wa Dar-es-salaam ambao hawajasajiliwa Vitambulisho vya Taifa; kwani kwa kipindi hiki cha Sabasaba wametoa kipaumbele kwa wananchi hao ili kupanua wigo wa matumizi mapana ya Vitambulisho hivyo kielektroniki.


“Nasisitiza wananchi wa Dar-es-salaam ambao hawajasajiliwa; wajitokeze wakiwa na viambatisho muhimu vya kuwatambulisha mathalani Cheti cha Kuzaliwa, Vyeti vya Shule, Pasi ya Kusafiria(Passport), Kadi ya Kupigia Kura, TIN namba, Kadi ya Bima ya Afya, Kitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi, Leseni ya Udereva na Kadi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii. Kuwa na Viambatisho vingi zaidi ni kutambulika kwa haraka zaidi” Alisitiza


Kwa mujibu wa Bi. Rose Kitambulisho hicho ni bure; na huduma hii ya kupata Kitambulisho ndani ya siku za maonyesho ni kwa siku saba tu za mwanzo yaani hadi tarehe 07/07/2017, baada ya hapo utaratibu wa kawaida wa kuwasajili wananchi utaendelea. Wananchi pia wameshauriwa kuanza taratibu za kujaza fomu za maombo ya Usajili kwenye Serikali za Mitaa wanakoishi na kugonga mhuri kabla ya kufika kwenye Banda la NIDA ili kurahisisha zoezi. 
NIDA inashiriki kwa mara ya pili maonyesho ya Kimataifa ya Sabasaba ikiwa imekusudia kuwaelimisha wananchi namna gani Mfumo wa Utambuzi na Usajili wa Watu ni ngazi katika kufikia malengo mapana ya Serikali ya Ukuzaji Biashara na Maendeleo ya Viwanda kama Kauli mbiu ya Maonyesho hayo inavyosema Ukuzaji wa Biashara kwa Maendeleo ya Viwanda” .

 Mmoja wa Wananchi akiweka saini ya kielektroniki katika zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa linaloendela katika Banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa – NIDA ndani ya Viwanja Maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara (SABASABA) 

 Afisa usajili Mamalaka ya Vitambulisho vya Taifa - NIDA Ndg. Daniel Katondo akitoa maelekezo ya namna ya kujaza fomu kwa mmoja wa Wananchi waliojitokeza katika zoezi la usajili ndani ya Banda la NIDA katika Maonyesho ya 41 ya kibiashara maarufu kama sabasaba.

 Wananchi wakipatiwa huduma mbalimbali Ndani ya Banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa – NIDA ikiwemo Elimu kuhusu umuhimu wa kitambulisho cha Taifa. Pichani Afisa Uhamiaji Bw. Jamal Kaoneka akimhakiki mmoja wa Wananchi wakati wa kukamilisha Tararibu za Usajili. 

 Huduma za Usajili zikiendelea kutolewa kwenye Banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi waishio Mkoa wa Dar-es-Salaam, pamoja na kupatiwa taarifa za hatua za Maombi ya Vitambulisho yalipofikia kwa wale waliokwisha kujisajili. 

Mmoja wa Wananchi waliojitokeza katika Banda la Mamlaka ya Vitambulihso akipatiwa maelezo mbalimbali kuhusu hatua za  Usajili wa Vitambulisho vya Taifa pamoja na Elimu juu ya umuhimu wa Vitambulisho vya Taifa pamoja na Matumizi yake.

ASASI ZA KIRAIA 25 ZAUNGANA KATIKA KUMTETEA MTOTO WA KIKE APATE NAFASI YA PILI KURUDI SHULENI

$
0
0
--
 Rebeca Gumi kutoka tasisi ya Msichana Initiative akizungumza juu ya adha wanazopitia watoto wa kike pindi wanapokuwa katika masomo yao mara tu wanapovunja ungo mpaka kuhitimu mafunzo ya elimu ya juu na kuomba wapewe nafasi ya pekee katika jamii hili waweze kuzifikia ndoto zao.
 Mtafiti kutoka Tasisi isiyo ya Kiserikali ya TWAWEZA ,Richard Temu akizungumzia juu ya matokeo ya tafiti iliyofanyw ana asasi za kiraia kwa kushirikiana na Serikali katika kubaini Changamoto za mtoto wa kike .

 Mkurugenzi wa  chama cha Wanasheria Wanawake nchini (Tawla) Bi.Tike Mwambipile akizungumza masuala ya kisheria yatakayo msaidia mtoto wa kike hili aweze kufanikiw akatika masomo yake.
 Meneja utetezi wa Twaweza ,Annastazia Rugaba akiwasilisha mada juu masuala yanayo mkabili msichana pindi anapokuwa shuleni
 Kaimu Mkurugenzi wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu , Anna Henga akiwasilisha mada juu ya umuhimu wa msichana kupata elimu nchini
 Mhariri mwandamizi wa mtandao wa Jamii Forums Bi. Asha Abinallah akiuliza swali kwa viongozi wa asasi za kiraia
 Sehemu ya washiriki wakiwa katika mkutano huo

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AREHE 29.06.2017.

SIMU TV: Mawakili Wapya 248 Wakubaliwa kuanza kazi

SIMU TV: CRDB imethibitishwa kuwa moja ya taasisi imara ya kifedha hapa nchini

SIMU TV: Serikali imewahakikishia wazabuni malipo baada ya uhakiki

TANZIA: PROFESSOR HENSLAY WILLIAM KABISAMA AFARIKI DUNIA MAREKANI

$
0
0
Familia ya Kabisama  inasikitika kuwaarifu kifo cha marehemu mpendwa  wao Professor  Henslay William Kabisama kilichotokea huko Ontario, Southern  California,  Marekani, tarehe 26 June, 2017
Taratibu za kusafirisha mwili zinafanywa  na tutawaarifu  Karibuni. Kwa ndugu, wafanyakazi wenzake na wanafunzi wake wanaweza kuwasiliana zaidi kwa namba  hizi:
John Matola +255 713 263 321Eddah Mwakale+255 713 274 850Dorcas Membe +255 787915151,
Hellen Nkoma+255 784 604 256

MICHUZI TV: WAFAHAMU AGRICOM AFRICA WENYE SIFA ZA PEKEE KWENYE UUZAJI WA VIFAA NA PEMBEJEO ZA KILIMO

THE 6th EAST AFRICA HEALTHCARE FEDERATION CONFERENCE - SAVE THE DATE!

TGGA YATOA SOMO JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI KISARAWE

$
0
0

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Mtera Mwampamba (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Kamishna wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA) Makao Makuu, Rose Majuva kuhusu kazi zinazofanywa na chama hicho ikiwemo kuwapa uwezo wanawake wa kujitambua na kujiamini alipokwenda kuzindua Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi wilayani humo.

Majuva aliwaasa wanawaje kuacha kutumia mikopo ya benki kuchezea ngoma bali waitumie kujiendeleza kibiashara na kuwa na tabia ya kulipa kwa wakati mikopo hiyo. Pia aliwaeleza mbinu mbalimbali za kufanya biashara na miiko yake. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDAKAMANDA WA MATUKIO BLOG.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Mtera Mwampamba (kulia), akiangalia kiroba cha mkaa uliotengenezwa kiasili kwa kutumia taka mbalimbali alipokuwa akitembelea mabanda ya wajasiriamali kabla ya kuzindua Jukwaa hilo. Kushoto ni Gifti Mbaraka wa banda hilo la Vijana Wasiriamali Wakulima Kisarawe. Katikati ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kisarawe, Mussa Gama.
 
Viongozi wa TGGA wakiwa kwenye banda lao wakati wa maonesho yaliyofanyika wakati wa uzinduzi wa Jukwaa hilo mjini Kisarawe
Mwampamba akiangalia bidhaa mbalimbali za wajasiriamali.

MKUTANO WA KITAIFA WA WADAU WA ELIMU NA CHAMA CHA WALIMU WAFANYIKA JIJINI DAR

$
0
0
Shirika la ActionAid-Tanzania, Mtandao wa Elimu Tanzania, Shirika la Maendeleo ya Elimu Singida-MEDO na Mtandao wa Asasi za Kiraia-KINGONET  kwa pamoja wanatekeleza mradi wa uhamasishaji utoaji elimu bora kupitia rasilmali zetu wenyewe ( PROMOTING QUALITY EDUCATION THROUGH PROGRESSIVE DOMESTIC RESOURCE MOBILIZATION) unaotekelezwa huko Kilwa na Singida Vijijini kwa ngazi ya wilaya kwa kufanya kazi na kamati za shule na klabu za haki za watoto shuleni.

 Kitaifa MRADI Huo unalenga kufanya  utetezi wa mabadiliko ya kisera na sheria  hasa suala la ulipaji kodi, ukusanyaji kodi kwa haki (tax Justice), uzibaji wa mianya ya uvujaji wa kodi  ili makusanyo yaongezeke na yagharimie huduma bora kwa wananchi wa Tanzania hususani kuboresha utoaji wa Elimu bora Nchini.

Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania Bi. Cathleen Sekwao akifungua mkutano huo aligusia pia kuhusu “utoaji wa huduma za jamii hapa nchini unakabiliwa na ufinyu wa fedha, wote tu mashahidi kuwa hadi kufikia mwezi Machi, 2017 serikali ilikuwa imetoa asilimia 34 tu ya bajeti yote ya 2016/2017. 

 Jambo hili lina madhara makubwa katika utoaji wa huduma za jamii hasa elimu msingi yenye ubora  hasakwa mtoto wa kike”.
Aliongelea pia serikali kushindwa kutoa asilimia mia moja ya fedha za kutekeleza bajeti ya 2016/2017 tafiti zinaonyesha kuwa Tanzania inapoteza fedha nyingi kupitia misamaha ya kodi.
Mwakilishi kutoka Mtandao wa Kodi Tanzania (TTJC), Grace Masalakulangwa akiwasilisha ripoti ya utafiti ya One Billion Question iliyotafitiwa na shirika la ISCEJIE katika Mkutano uliowakutanisha wadau wa Elimu na Wenyeviti wa Chama cha Walimu ngazi ya mikoa ya Tanzania Bara  iliyofanyika jijini  Dar es Salaam. 
Afisa Mradi wa Elimu kutoka TENMET, Alistidia Kamugisha akifungua mkutano na kuwaelezea malengo ya mkutano huo wa siku mbili kwa wadau wa elimu na Chama cha Walimu Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET), Cathleen Sekwao akitoa mada kuhusu umuhimu wa ukusanyaji wa rasilimali za ndani na kuwekeza katika kuboresha sekta ya elimu hususani kwa mtoto wa kike na maslahi ya walimu katika mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ANNA MGHWIRA ,ASHUHUDIA MAGARI 103 YAKIWA NA SHEHENA YA MAHINDI NJIA PANDA YA HIMO.

$
0
0

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

ENEO la njia Panda linalounganisha barabara za Moshi/Arusha,Tanga/Dar es Salaam na ile ya Holili mpakani mwa nchi jirani ya Kenya linatajwa kama kituo kikuu cha Malori yanayosafirisha Nafaka kwenda nchi jirani ya Kenya.

Uchunguzi uliofanywa na Globu ya Jamii umebaini kuwepo kwa maeneo yasiyo rasmi ya kuegesha Malori hayo ,mengine yakiwa na Matela yake ,ambako shughuli za kupakua mahindi na kupakia katika Magari Madogo aina ya fuso zinazotoka nchi jirani ya Kenya hufanyika.

Maeneo mengine yanayotajwa kuwepo na Magulio ya Mahindi ni katika sehemu za maegesho ya magari zilizopo katika vituo mbalimbali vya kuuza Mafuta ,pamoja na baadhi ya nyumba za wageni ambazo zimegeuzwa Maghala ya kuhifadhia Mahindi.

Magari zaidi ya 103 yanashikiiwa katika maeneo ya Njia Panda na Himo yakiwa yamebeba Shehena ya Mahindi tayari kusafirishwa huku baadhi ya madereva wakiyatelekeza Malori yao kwa siku ya tano sasa na kwenda kusiko julikana .

Hatua iliwasukuma Wafanyabiashara wa Mahindi pamoja na Madereva kufika ofisi za Mkuu wa mkoa kuwasilisha malalamiko yao juu ya kukamatwa kwa Malori hayo yakiwa Njia Panda badala ya mpakani kama alivyo agiza Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa.

Wakizungumza nje ya jingo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa,Wafanyabiashara hao ,Laurance Kanyota,Nuru Madai na Mariam Ramadhan walisema wameshangazwa na hatua ya jeshi la Polisi kushikilia magari yao yalikuwa na Mahindi yakisafirishwa kuelekea mikoa ya Arusha na Moshi.

“Magari yetu yapo pale Sheli Maount Meru,yalitokea Tunduma kwenda Arusha,yalipofika pale siku ya Jumamosi madereva walienda kula siku kuu ya Idd,jana (Juzi) asubuhi Matandiboi wakapiga simu kwamba tumezungukwa na Polisi ,tukaenda pale tukaonana na OCD tukaliza kwanini mnatushikia magari ambayo yako Njia Panda yanayoenda Arusha au Moshi ,wakajibu tumetumwa kushika magari yote ya Mahindi.”alisema Mfanyabiashara Mariam.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akiwa ameongozana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kilimanjaro wakiwemo Kamanda wa Polisi ,Hamis Issah na Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba wakitembelea maeneo ambayo yameshikiliwa magari yaliyobeba shehena ya Mahindi .
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiangalia magari yaliyobeba shehena ya Mahindi yanayoshikiliwa katika eneo la Njia Panda ya Himo.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akizungumza na baadhi ya madereva na Wafanyabaisahara ambao Mahindi yao yanashikiliwa eneo la Njia Panda ya Himo.

FUKUTO LA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA KLABU YA MAJIMAJI LA PAMBA MOTO.

$
0
0
Klabu ya MAJIMAJI inatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi agust 5 mwaka huu ,ambao watakuwa na lengo la kuiongoza klabu hiyo na kuiletea maendeleo mkoa wa ruvuma kwa ujumla. Uchaguzi huo unafanyika baada ya viongozi wa awali kufikia kikomo wa kuiongoza klabu ya majimaji

WANANCHI WA KIJICHI WAOMBA UKARABATI WA BARABARA YA KIJICHI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jmaii.

Eneo la Barabara  ya Mtoni Kijichi yenye urefu wa Kilo
mita 0.9 ikiwa imeharibiwa na mvua na kusababisha kufungwa kwa barabara hiyo kwa muda wa mwezi mmoja sasa.

Barabara hiyo ni njia kuu ya wapita kwa miguu na magari  pia kutokana na njia hiyo kuunganisha maeneo ya Kota za Benki, Nasako, Kota za Polisi na Jeshi  na Polisi na shule ya Sekondari Neluka na Shule ya Sekondariu ya Mbagala Kuu.

Wananchi wa eneo hilo wamesema kuwa barabara hiyo inahatarisha sana kwani watoto wao wamapokuwa wanapita katika  njia hiyo wanaweza wakajisahau na kutaka kuchungulia ili kuona ndani kuna nini na kuweza kuanguka pia, pia kuna baadhi ya watoto ambao ni watundu huamua kuingia ndani ya shimo na wengine kushindwa kutoka.

Wameiomba serikali kuikarabati barabara hiyo ambayo inaunganisha maeneo makubwa ya kata ya Kijichi.
 Picha mbalimbali zikionesha jinsi barabara ya Mtoni Kijichi inayounganisha maeneo ya Kata ya Kijichi na kusababisha baadhi ya mahitaji muhimu kukosekana kwa takribani mwezi mmoja.

WANAHABARI MBEYA WAJITOSA KUJILIPIA BIMA YA AFYA YA TAIFA (NHIF), RC MAKALLA AKABIDHI KADI ZA BIMA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Gabriel Makalla, amewapongeza waandishi wa habari mkoa wa Mbeya kwa uamuzi wao wa kuhamasishana kuchangia na kupatiwa kadi za bima ya Afya ya Taifa (NHIF).
Pongezi hizo zimetolewa katika ukumbi wa Coffee Garden mjini Mbeya alipokuwa akikabidhi kadi za bima ya Afya kwa baadhi ya waandishi wa habari Jijini Mbeya.
Makalla amesema waandishi wa habari wanafanya kazi kubwa katika Taifa na waandishi wa mkoa wa Mbeya wameamua kujitambua zaidi na kutambua kuwa matatizo hayaji kwa kupenda ikiwemo Kifo, Kuugua na uzee.
“Niwakumbushe wamiliki wa vyombo vya habari kuwawekea mazingira mazuri waandishi wao na kwamba kuna msemo unaosema kuwa ukondefu wa mbwa ni aibu kwa mwenye mbwa hivyo kutapatapa kwa waandishi wa habari ni aibu kwa wamiliki” alisema Makalla.
Aliomba waandishi kuendeleza uzalendo wao ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi kujiunga na bima za afya ikiwemo mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF).
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya Hoseah Cheyo alimwambia Mkuu wa mkoa kuwa pamoja na mambo mengine, waandishi wa habari wanampongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi kubwa anazoendelea kuzifanya kwa ajili ya Taifa.
Katibu Mkuu wa chama hicho alisema kuwa waandishi wa habari wamehamasishana wenyewe katika kupata michango na kulipia kadi hizo.
Mwakilishi wa Mganga mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dr. Agness Buchwa, 
alisema kwa sasa Hospitali za mkoa wa Mbeya hususani Hospitali ya Mkoa na Rufaa, wametenga maeneo maalum kwa ajili ya watu wanaotibiwa kwa njia za kadi za bima ya Afya.
Mwakilishi wa Meneja wa mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa, Haji Mpeta alisema kuwa matibabu ni ghali hivyo waandishi waliolipia kadi za bima ya Afya wataweza kupata matibabu katika vituo 6500 kote nchini kwa gharama ya Tsh. 76,800 kwa mwaka.
 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Gabriel Makalla
 makamu Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya Hoseah Cheyo, akizungumza kwa niaba ya waandishi wa habari wa mkoa huo.
 Mwakilishi wa Mganga mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dr. Agness Buchwa, akizungumza na waandishi wa habari katika hafla fupi ya kuwakabidhi kadi za bima ya afya ya Taifa baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya hawapo pichani..
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akimkabidhi kadi ya bima ya Afya  mwandishi wa habari Aines Thobias katika ukumbi wa Coffee Garden  uliopo Jijini Mbeya.
 Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa mbeya wakiendelea kudodosa matukio katika hafra fupi ya kupokea kadi za uwanachama wabima ya Afya 
PICHA ZOTE NA MR.PENGO MICHUZI MEDIA MBEYA.
MAELEZO NA GORDON KALULUNGA WA KALULUNGA BLOG

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNE 30, 2017

JARIDA LA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU - MEI, 2017

WAHANDISI WAZAWA KUHUSISHWA UJENZI BANDARI YA MTWARA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameuagiza Uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kupeleka wahandisi wa kutosha katika ujenzi wa Gati ya Mtwara ili kupata uzoefu katika kazi za ujenzi.

Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Bandari hiyo Waziri Prof. Mbarawa amesema ushiriki wa wahandisi hao utasaidia kuwajengea uzoefu mkubwa na hivyo kuokoa fedha nyingi ambazo zitatumika kwa kuwatumia wahandisi wa kigeni.

“Mradi huu unagharimu fedha nyingi hivyo ni muhimu wahandisi wa TPA wakaja kujifunza kwa vitendo ili mradi utakapokamilika wahandisi wetu watumike kufanya ukarabati na matengenezo badala ya kusubiri kuwaleta tena wahandisi kutoka nje”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Amesisitiza uongozi wa TPA kutafuta wahandisi waliomaliza vyuo nchini ili waweze kujifunza kwa vitendo kupitia mradi huo kama sehemu ya mafunzo kwa vitendo ili kupata uzoefu.

Kwa upande wake, Meneja wa bandari ya Mtwara, Eng. Juma Kijavara, amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa tayari utekelezaji wa agizo la kutafuta wahandisi hao umeshaanza na hatua inayofata ni kuwasili kwa wahandisi hao eneo la madi.

Upanuzi wa bandari ya Mtwara utahusisha awamu nne na awamu ya kwanza ambayo itagharimu kiasi cha Tsh. bilioni 137 na inatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 22, kukamilika kwa gati hiyo kutaiwezesha bandari hiyo kuhudumia meli ya ukubwa wa mita 300 na kukuza uchumi wa mkoa huo kupitia usafirishaji wa gesi, saruji, korosho pamoja na makaa mawe.
Meneja wa Bandari ya Mtwara, Eng. Juma Kijavara (kulia), akimuonyesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, eneo ambalo ujenzi wa gati ya pili ya bandari hiyo utakapoanza kujengwa wakati Waziri huyo alipokagua vifaa vya Mkandarasi vilivyowasili katika eneo la mradi hivi karibuni.
Baadhi ya Vifaa ambavyo vitatumika katika ujenzi wa gati ya pili ya bandari ya Mtwara vikiwa vimeshawekwa site tayari kwa kuanza ujenzi. Ujenzi huo unakadiriwa kukamilika ndani y amiezi 22.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (mwenye suti ya Blue), akiangalia vifaa vitakavyotumiwa na Kampuni ya M/S China Railways Construction Engineering Group (CRCEG) na M/S China Railways Major Bridge Engineering Group Co. ltd (CRMBEG) katika ujenzi wa gati ya pili ya bandari ya Mtwara, mkoani humo hivi karibuni.

PPF YATANGAZA MAJINA YA WATU WALIOCHAGULIWA KWA AJILI YA USAILI NAFASI ZA UDEREVA

Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images