Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1769 | 1770 | (Page 1771) | 1772 | 1773 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira January Makamba akizungumza wakati wa baraza la Eid lililofanyika kwenye shule ya Sekondari Jumuiya mjini Tanga kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto ni Shehe wa mkoa wa Tanga,Juma Luwuchu.
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akizungumza katika baraza hilo kushoto ni  Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira January Makamba kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa.
  Shehe wa mkoa wa Tanga,Juma Luwuchu akizungumza katika baraza hilo ambapo aliwataka waislamu kuendelea kutenda mambo mema kulia ni Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira January Makamba na mkuu wa mkoa wa Tanga,Martine Shigella.
   Sehemu ya waumini wakimsikiliza Waziri Makamba kwenye Baraza hilo leo
    Sehemu ya waumini wakimsikiliza Waziri Makamba kwenye Baraza hilo leo.


  0 0


  *Ahimiza nyumba za ibada zisaidie vita ya dawa za kulevya 

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepiga marufuku usafirishaji wa chakula kwenda nje ya nchi kuanzia leo. “Kuanzia leo, ni marufuku kwa mtu yoyote kusafirisha mazao ya chakula kwenda nje ya nchi bila ya vibali. Serikali inahamasisha uwekezaji kwenye ujenzi wa viwanda nchini. Kama tutatoa vibali, ni lazima mtu alazimike kusaga nafaka ili kutoa ajira nchini,” amesema. 
  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Juni 26, 2017) wakati akitoa nasaha kwenye Baraza la Eid lililofanyika kitaifa kwenye msikiti wa Masjid Riadha, mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro mara baada ya kuswali sala ya Eid. 
  “Jana nimeona kwenye televisheni taarifa kuhusu malori 10 yaliyokamatwa Tarakea yakiwa na mahindi tayari kuvushwa mpaka. Mheshimiwa RC akasema chakula hicho ni lazima yarudishwe kwa ajili ya usagaji.”

  “Mimi nasema kuanzia leo, yeyote atakayekamatwa akitorosha chakula kwenda nje ya nchi, chakula hicho kitataifishwa na kupelekwa ghala la Taifa na gari lake tutalitaifisha na litaishia Jeshi la Polisi. Tunafanya hayo kwa lengo la kuwalinda Watanzania tusikumbwe na baa la njaa.” 
  Akitoa tahadhari kuhusu uuzwaji wa chakula nje ya nchi, Waziri Mkuu amesema kumekuwa na wimbi kubwa la usafirishaji wa chakula kwenda nje ya nchi bila kibali. “Hilo ni kosa kubwa kwa sababu litasababisha nchi yetu kupata baa la njaa huko mbele,” amesema.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa nasaha kwa waumini (hawapo pichani) waliohudhuria Swala ya Eid el Fitr na Baraza la Eid Kitaifa kwenye msikiti wa Masjid Riadha mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro tarehe 26 Juni, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria Swala ya Eid el Fitr na Baraza la Eid Kitaifa kwenye msikiti wa Masjid Riadha mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akitoa nasaha za Eid, tarehe 26 Juni, 2017. 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally wakati wa stafutahi kwenye Ikulu ndogo ya Moshi, mara baada ya Swala ya Eid el Fitr na Baraza la Eid Kitaifa mkoani Kilimanjaro tarehe 26 Juni, 2017.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally mara baada ya stafutahi kwenye Ikulu ndogo ya Moshi, mkoani Kilimanjaro tarehe 26 Juni, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  Picha mbalimbali zikimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri leo tarehe 26/06/2017 Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

  0 0


  0 0


  0 0


  Imamu Mkuu wa Msikiti wa Buguruni kwa Mnyamani, Sheikh Muhammad Idd Muhammad, akitoa mawaidha wakati wa Swala ya Iddi El Fitri.  
  Waumini wakiswali swala ya Iddi El Fitri kwenye Msikiti wa Buguruni kwa Mnyamani, jijini Dar es Salaam jana. Swala hiyo iliongozwa na Msaidizi wa Imamu Mkuu, Sheikh Ally Bakari, hotuba ikasomwa na msaidizi wa pili wa Imamu, Sheikh Abubakar Khamisi na mawaidha yakatolewa na Imamu Mkuu, Sheikh Muhammad Idd Muhammad.
  Imamu Mkuu wa Msikiti wa Buguruni kwa Mnyamani, Sheikh Muhammad Idd Muhammad, akitakiana heri ya Sikukuu ya Iddi El Fitri na watoto waliofika katika msikiti huo kwa ajili ya swala ya Iddi El Fitri. 
  Imamu Mkuu wa Msikiti wa Buguruni kwa Mnyamani, Sheikh Muhammad Idd Muhammad, akitakiana heri ya Sikukuu ya Iddi El Fitri na waumini. 
  Imamu Mkuu wa Msikiti wa Buguruni kwa Mnyamani, Sheikh Muhammad Idd Muhammad, akitakiana heri ya Sikukuu ya Iddi El Fitri na waumini.  0 0

  Katika hekaheka za  kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitr Uongozi wa Chuo Kikuu Teofilo Kisanji (TEKU) cha Jijini Mbeya kwa kushirikiana na Serikali ya Wanafunzi TEKUSO na mmoja wa wadau wakubwa wa Vijana,Amani Kajuna wamefanya bonanza kubwa la michezo kwa kuzishirikisha Timu mbalimbali kutoka ndani ya Chuo na nje ya Chuo ambapo Timu kutoka Mbozi, Uyole, Madereva Bajaji, Madereva Bodaboda zilishiriki kikamilifu kwenye mpira wa miguu, kikapu, pete na mpira wa wavu.

  Katika mashindano hayo washindi walikabidhiwa zawadi zao na Makamu Mkuu wa Chuo Dkt. Daniel Mosses kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini Mhe. William Ntinika, aliyefungua bonanza hilo na baadaye kuhutubia umati uliokuwepo Chuoni hapo.

  Awali, Makamu Mkuu wa Chuo TEKU-Taaluma Dkt. Daniel Gwakisa alisema "Chuo chetu kimekuwa kikijitambulisha kwa Taaluma yake bora na pia kupitia Michezo, kwani tunaamini vipaji vya Vijana wetu vinapaswa kuendelezwa ili vikue zaidi", alisema na kuongeza kuwa Mhadhiri wa Wanafunzi TEKU Mkufunzi Bi. Stella Seif amesema TEKU wanawalea Vijana (Wanafunzi)  kwa misingi bora kwa kutambua mahusiano ya kada za Cheti, Diploma, Shahada na kada zingine kama za Uzamili.

  Katka ufafanuzi wake alipokuwa akizungumza na Mwandishi wetu ,Rais wa Serikali ya Wanafunzi (TEKUSO) Mhe. Byula Mahona amewaalika wazazi na wanafunzi waliomaliza Elimu za Sekondari na Vyuo kuja kujiunga na Chuo cha TEKU,kwani ni Chuo pekee Jijini Mbeya kinachojali na kukuza vipaji vya wanafunzi huku Taaluma itolewayo ni bora.

  Alisema moja ya mafanikio ya kukuza vipaji vya wanafunzi ni Chuo kumtoa Miss Mbeya 2016 Eunice John Robert ambaye alishiriki Shindano la Miss Tanzania 2016 na kufanikiwa kutwaa taji la Miss Tanzania Personality 2016, aidha kuna vijana wengine wenye vipaji kama Mzee wa Madodoso, Mpoli Daudi (Wachekeshaji), Goliath, D-nax, G-mafic, Ekka da Music, Peff Mc, Ndaki Black (Wanamuziki) nao wakiwa ni miongoni mwa Vipaji kutokea Chuoni hapo.
  Matokeo ya Michezo ya Bonanza yalikuwa kama ifuatavyo: NETBALL:- Teku Queens goli 20 Vs Uyole Queens goli 11 (Mshindi amepata Tshs 50,000/=), BASKETBALL:- Worriers Vikapu 54 Vs Teku Vikapu 50 (Mshindi amepata Tshs 50,000/=), VOLLEYBALL;- Vijana Jiji set 2 Vs Teku set 3 (Mshindi amepata Tshs 50,000/=), Mpira wa miguu kulikua na Timu nne, Bodaboda Fc 2-1 Bajaji Fc,  Unity Fc toka Mbozi 2-1 Home Boys toka Chunya hivyo Fainali ilikuwa kati ya washindi Bodaboda Fc Vs Unity Fc (Dakika 90,Unity Fc 1-1 Bodaboda Fc, mikwaju ya penati Bodaboda Fc 4-5 Unity Fc (Mshindi wa kwanza Tshs 100,000/= wa pili Tshs 50,000/= zilitolewa) 

  Mara baada ya mchezo huo kukamilika ndipo mchezo wa Fainali ya Ligi ya Chuo ulichezwa kati ya Timu ya BAED mwaka wa kwanza Vs Timu ya BEDMATHS mwaka wa pili, Matokeo;- BAED 3-2 BEDMATHS (Mshindi wa kwanza amepata Tshs 400,000/= na wa pili Tshs 100,000/=)

  0 0
  0 0

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii
  Kanda ya Kaskazini.
  Wachezaji 30 wa timu za soka za mataifa mbalimbali wameshiriki kuweka rekodi ya kwanza Duniani kwa kucheza mchezo wa kirafiki katika mlima Kilimanjaro ,umbali mita 5731 kutoka usawa wa bahari.
  Rekodi nyingine iliyowekwa ni ile ya mwamuzi wa kike wa Tanzania anayetambulika na Shirikiho la Soka Duniani (FIFA) Jonesia Rukyaa  kuchezesha mchezo huo  wa dakika 90 uliomalizika kwa sare ya bila kufungana .
  Kundi la Wanamichezo 60 wakiwemo wachezaji 30 wa timu za taifa za wanawake kutoka mataifa zaidi ya 20 walioshiriki kuweka rekodi ya kucheza soka katika eneo la kreta lililopo katika kilele cha Uhuru.
  Wachezaji wa timu za Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Bodi ya utalii pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
  Timu za Gracier fc na Volcano fc zikijiandaa kwa mchezo wa kirafiki katika eneo la Kreta,kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
  Wachezaji wakiweka pozi la picha katika Kreta ya Uhuru katika kilele cha Uhuru juu ya Mlima Kilimanjaro.   0 0

  Airtel yafuturisha wafanyakazi wake siku ya ijumaa kabla ya sikukuu ya Eid

   Wafanyakazi katika kitengo cha mawasilino cha Airtel wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kufuturu . kushoto ni mkurugenzi wa mawasiliano Beatrice Singano, akifatiwa na Afisa uhusiano Jane Matinde, Meneja huduma kwa jamii, Hawa Bayumi pamoja na Afisa uhusiano na matukio, Dangio Kaniki
   Sheikh Hilal Kipoozeo akiongoza wafanyakazi wa Airtel pamoja na baadhi ya wageni kwenye futari
   Wafanyakazi wa Airtel pamoja na baadhi ya wageni kwenye futari
    Wafanyakazi wa Airtel pamoja na baadhi ya wageni kwenye futari
    Wafanyakazi wa Airtel pamoja na baadhi ya wageni kwenye futari.

  0 0

  Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda amewataka wananchi, taasisi  na viongozi mbalimbali wenye uwezo kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwa lengo la kuwakwamua na hali ya kiuchumi iliyopo kwa sasa.
  Mwenda ameyasema hayo Jijini Dar es salaam jana katika hafla ya Idd aliyoindaa nyumbani kwake na kusheherekea na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha  Umra kilichopo Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni.
  Alisema pamoja na mambo mengine,kufanya hivyo ni kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli katika harakati zake za kimaendeleo anazozifanya.
  Alisema viongozi wananchi pamoja na jamii kwa ujumla haina budi kuendana na dhamira aliyonayo Rais Magufuli ya Taifa kujikwamua kiuchumi hususani kipindi hiki anapofanya mambo mbalimbali ya kuliletea maendeleo.
   Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda akizungumza wakati wa  hafla ya Idd aliyoindaa  nyumbani kwake jijini Dar es Salaam. na kusheherekea na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha  Umra kilichopo Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni .
   Mratibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Imra James Gabon akitoa neno la shukrani mara baada ya kupokea msaada.
   Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda akiwakabidhi  watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha  Umra kilichopo Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni .baadhi ya zawadi aliyowaandalia (kushoto) Mratibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Imra James Gabon.
   Mke wa Meya Mama Tausi Yusufu Mwenda (mwenye nguo ya bluu) akimkabidhi moja ya zawadi Bi.Nuhimu Iddi anayetoka katika kituo hicho.
   Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda akiwakabidhi zawadi watoto. Kwa habari kiamili BOFYA HAPA  0 0

  Watanzania  wameshauriwa kuchangamkia fursa ya kutembelea  maeneo matakatifu nchini Israel kwa gharama nafuu inayokadiriwa kuwa kati ya nafuu inayokadiriwa kuwa kati ya Dola za Kimarekani 1700 na 1800. 
   Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bibi Devota Mdachi,  amesema jijini jana kuwa wadau wa utalii wa Israel wangependa kuona Watanzania wanatembelea Israel. 


  Bibi Mdachi akiongozana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki ambaye alikuwa kiongozi wa msafara,  walitembelea Israel kwa siku tatu, walikutana na na wadau wa sekta ya utalii na kuwaeleza  vivutio vilivyopo nchini.

  “Tumetembelea maeneo mengi ya kiroho ikiwemo miji ya Nazareth na Jerusalem, wenyeji wetu wamenipa ujumbe kuwa wanahitaji Watanzania waende wakahiji katika maeneo hayo kwa bei nafuu inayokadiriwa kuwa kati ya Dola za Kimarekani 1700 na 1800. 
  “Fursa hii ni nzuri tafadhali tusiiache kwa sababu mbali ya hija lakini kuna mambo mengi mengine.  Watakaokwenda watakutana na raia wa mataifa mengine watawauliza kuhusiana na Tanzania,  maana yake mtageuka mabalozi wetu na kuvutia watalii wengi zaidi,” alisema Bibi. Mdachi. 
  Alibainisha kuwa kiasi hicho cha Dola 1700 au 1800 kinahusisha nauli ya kwenda na kurudi, malazi pamoja na ziara ya maeneo matakatifu ndani ya miji husika. 
  “Kampuni ya Another World imeahidi ifikapo Agosti mwaka huu wataleta watalii kutoka Israel watakaotembelea maeneo ya Hifadhi ya Katavi, Mahale, Ngorongoro na Zanzibar. 
  Mmiliki wa kampuni ya Another World, Bw Shlomo Carmel ameahidi kuleta watalii zaidi ya 2000 kati ya Agosti na Disemba mwaka huu.


  Vilevile kuna wawekezaji katika sekta ya hoteli za viwango vya kimataifa wameahidi kuja kuwekeza nchini, kifupi imekuwa ni ziara yenye tija kwetu sote,” alibainisha Bibi. Mdachi.

  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Balozi Emmanuel Nchimbi (kulia) akiwasilisha hati ya utambulisho kwa Rais wa Brazil, Michel Temer wakati alipofika kujitambulisha katika Ikulu ya Palácio do Planalto Jijini Brasilia, nchini humo, hivi karibuni.
   Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Balozi Emmanuel Nchimbi (kulia) akisalimiana na Rais wa Brazil, Michel Temer wakati alifika kujitambulisha katika Ikulu ya Palácio do Planalto Jijini Brasilia, nchini humo, hivi karibuni.
  Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Balozi Emmanuel Nchimbi (wa pili kulia) akiwa ameambatana na Mkewe (kulia kwake) wakiwasili katika Ikulu ya Palácio do Planalto Jijini Brasilia, alipokwenda kujitambulisha kwa Rais Michel Temer.

  0 0

  IDARA ya Uhamiaji Mkoani Tanga imeanza mikakati ya kukabiliana kwa vitendo na wimbi la wahamiaji haramu kuingia mkoani hapa kwa kuanzisha kizuizi eneo la Mkata wilayani Handeni kwa muda wa saa 24. 

  Hayo yalibainishwa na Afisa Uhamiaji Mkoani Tanga DCI, Crispin Ngonyani wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mipango waliojiwekea kuzibiti vitendo vya namna hiyo. 

  Alisema wameamua kuanzisha mpango huo kutokana na asilimia kubwa ya wahamiaji haramu hao wanapokuwa wamefika kwenye eneo hilo la kizuizi wanashushwa na kupakia pikipiki maarufu kama bodaboda na kuingia mkoani Tanga. 

  “Kutokana na hali hiyo ndio maana tumeamua kuweka kizuizi hicho ambacho kimekuwa ni eneo ambalo linatumika kuwafaulisha wahamiaji haramu kwenye pikipiki maarufu kama bodaboda kwa lengo la kuzibiti suala hilo kwa vitendo “Alisema. 

  Aidha pia alisema hivi sasa wamejipanga kuhakikisha wanadhibiti maeneo yote ambayo yamekuwa na mianya ya kutumia kwa ajili ya kupitia ili kuweza kuhakikisha hawaingii mkoani Tanga. 

  “Lakini pia tuwatake wananchi kuhakikisha wanawafichua wahamiaji haramu pindi wanapokuwa wakiwaona kwenye maeneo yao kwani wamekuwa na madhara makubwa hivyo wanapaswa kutoa taarifa kwa mamlaka husika “Alisema. 

  Hata hivyo aliwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa iwapo watabaini kuwepo kwa watu wasiowaelewa kwenye maeneo yao ili hatua kali ziweze kuchukuliwa.


  Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0


  VICTOR MASANGU, KIBAHA

  VIJANA wa dini ya kiislmamu hapa nchini wametakiwa kuachana na vitendo vya kushinda vijiweni na kujiingiza katika wimbi la uhalifu na utumiaji wa madawa ya kulevya ambayo yanachgangia kwa kisi kikubwa kupoteza nguvu kazi ya Taifa na badala yake sasa wawe wazalendo kwa kuhakikisha wanazilinda kwa hali na mali rasilimali zote pamoja na kutunza amani iliyopo

  Kauli hiyo imetolewa na Naibu Sheikh wa Mkoa wa Pwani Hamisi Mtupa wakati wa sherehe za baraza kuu la waislamu la Iddy ngazi ya Wilaya ya Kibaha ambalo limefanyika katika viwanja vya mwendapole na kuhudhuliwa na viongozi wa ngazi mbali mbali wa dini pamoja na serikali kutoka katika Mkoa wa Pwani.

  Sheikh Mtupa mbaye pia ni Kadhi wa Mkoa wa Pwani alibainisha kuwa kwa sasa watanzania wote wanapaswa kubadilika na kuhakikisha kwamba wanakuwa walinzi wa rasilimali zote zilizopo nchini kwa lengo la kuweza kuwathibiti baadhi ya watu ambao wamekuwa wakijinufaisha wao wenyewe kwa maslani yao binafsi bila ya kujali wananchi wa hali ya chini.

  Hama kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo amewaasa wananchi wote kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Dk John Magufuli pamoja na kuchapa kazi kwa bidii ili kuweza kupambana na janga la umasikini na kuachana na kuwa tegemezi ambapo pia amechangia kiais cha shilingi milioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya waislmau ya Wilaya.

  Koka alisesema kwamba nia yake kubwa ni kushirikiana na wananchi wa jimbo lake katika kuleta maendeleo hivyo amewaomba waislamu waendelee kujenga upendo na ushirikiano wa hali na mali katika kuakikisha kwamba ujenzi wa ofisi hiyo ya wilaya inakamilika ili iweze kuanza kufanya kazi kwa jili ya kutoa huduma.

  “Mimi kama mbunge wenu katika hili kwa kuanzia nitachangia kiais cha shilingi milioni tatu lakini sio kwamba ndio nitaishia hapo hapana nataka kuona na nyinyi wenzangu tunashirikiana kwa pamoja ili kuweza kukamilisha ujenzi wa ofisi ya Wilaya na nikiona kwamba tupo pamoja na mimi tena nitaongezea kiasi cha shilingi milioni mbili lengo ikiwa ni kuona tunakuwa na sehemu sahihi ya kuweza kukutana na kufanya shughuli zenu,”alisema Koka.

  Awali akisoma risala katika sherehe hizo Katibu wa kamati ya maandalizi ya Baraza la Iddi Wilaya ya Kibaha Hoseni Ibrahimu ameiomba serikali ya awamu ya tano kuongeza vipindi vya dini mashuleni kwa lengo la kuweza kutoa huduma za kiroho kwa wanafunzi wa kiislamu

  “sisi kama baraza kuu la waislmamu Bakwata Wilaya ya Kibaha kikubwa tunachoiomba serikali ni kuongeza vipindi vingi vya dini katika mashule ili wanafunzi waweze kupata fursa ya kujifunza zaidi mafundisho ya kiroho na tuna imani itaweza kusaidia kuwaongezea uwezo mkubwa katika kujifunza mambo mbali mbali yanayohusina na dini ya kiislamu,”alisema Ibrahimu.


  BARAZA kuu la waislamu (BAKWATA) Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani kwa sasa licha ya kukabiliwa na changamoto mbali mbali linahitaji kiasi cha shilingi milioni 15 kwa ajili ya kuanza maandalizi ya ujenzi wa ofisi ya wilaya.
  Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akizungumza na waumini wa dini ya kiislamu hawapo pichani wakati wa sherehe za Baraza kuu la waislamu (BAKWATA) Wilaya ya Kibaha kwenye viwanja wa Mwendapole Wilayani Kibaha (PICHA NA VICTOR MASANGU) Caption-4 Naibu Sheikh wa Mkoa wa Pwani Hamisi Mtupa akizungumza jambo wakati wa sherehe hizo za baraza kuu la waislamu Wilaya ya Kibaha.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

  0 0


  Na. Catherine Sungura na Benson Mwaisaka,WAMJW- Kibaha

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amempongeza na kumshukuru Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuongeza chachu katika mapambano dhidi ya malaria kwa kununua lita laki moja na kusambazwa kote nchini.

  Ameyasema hayo wakati wa ugawaji wa Viuadudu vya kutokomeza mbu wa malaria kwa halmashauri kumi na moja zilizofika katika kiwanda cha kuzalisha Viuadudu hivyo kilichpo Mjini Kibaha

  Aidha ,Waziri Ummy alisema anamshukuru Mhe. Rais kwa kumruhusu kuanza zoezi hilo kwa awamu ambapo kwa awamu ya kwanza Viuadudu hivyo vitagawiwa kwa Halmashuri 14 nchini ambazo zina viwango vikubwa vya maambukizi ya ugonjwa wa malaria,“hii ametupa nguvu na ari sisi tuliopo kwenye dhamana ya kusimamia sekta ya afya katika kupambana na Malaria.

  Hata hivyo alisema kwa mujibu wa takwimu toka ofisi ya Takwimu nchini zinaonyesha kwamba kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria nchini ni asilimia 14 ambapo katika kila watoto walio chini ya miaka mitano kati ya watoto 100 watoto 14 wamekutwa na maambukizi ya Malaria

  “Maelekezo yangu hasa kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya ni kuhakikisha dawa hii mnapulizia kuzingatia miongozo iliyotolewa na Wizara ya Afya,Muangalie ukubwa wa eneo la mazalia ya mbu,na kiasi kinachotakiwa kupulizia”.

  Waziri Ummy amewataka wahakikishe wanapulizia Viuadudu hivyo angalau mara nne kwa mwezi kwa maana kila baada ya siku saba,hivyo ni lazima wanunue vifaa vya kupulizia dawa hii pamoja na kutoa mafunzo kwa watumishi watakaenda kufanya zoezi hilo.

  Pamoja na hayo Waziri Ummy aliwataka ifikapo mwisho wa mwezi huu kila Mkurugenzi wa Halmshauri awe ampelekee mahitaji halisi ili kuona ni jinsi gani watatekeleza kazi hiyo “Lazima nipate mahitaji halisi toka Halmashauri kwa kuwa Mhe. Rais ameshatuonyesha njia na ametuelekeza badala ya kununua dawa pia tununue na viuadudu hivi”

  Naye Mkurugenzi Msaidi toka Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhandisi Elli Pallangyo alisema leo hii Halmashauri kumi na moja sawa na Mikoa sita ndizo zilizofika katika uzinduzi huo wa ugawaji wa Viuaduddu kwa awamu ya kwanza,alizitaka Halmashauri hizo na mgawanyo wa lita kwenye mabano

  Liwale(1,200), Tarime (384), Misungwi(1,296), Kasulu(540), Songea(816),Kakonko(660), Kisarawe(720), Kyerwa(1,080), Rufiji(5,088), Geita(2,100), Kilombero(1,140)
  Matukio mbaljmbali zikionyesha matukio wakati wa ugawaji Viuadudu vya kutokomeza Mbu wa Malaria Mjini kibaha.Pichani ni Waziri Ummy Mwalimu akigawa Viuadudu hivyo kwa Halmashauri kumi na moja


  0 0

  SERIKALI wilayani Korogwe Mkoani Tanga imepania kuhakikisha wanakomesha vitendo vya mimba za utotoni kwa kuwachukulia hatua kali watakaobinika kuhusika na matukio hayo ili kuweza kuondosha hali hiyo kwenye jamii.

  Lakini pia imesema watakaohusika kuwa kichocheo cha ndoa hizo zifanyike wakiwemo wazazi kutoka pande zote mbili watafikishwa mahakamani ili sheria zichukue mkondo wake zaidi kwa lengo la kukomesha vitendo vya namna hiyo kwenye jamii.

  Hayo yalibainishwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe ,Mhandisi,Robert Gabriel wakati makabidhiano ya vyumba vya madarasa vitano na vyoo ishirini na nne,mradi maji na uzio wa shule ya msingi jitengeni iliyopo Mji mdogo wa Mombo uliofanywa na taasisi isiyo ya kiserikali A better World ya Canada ikishirikiana na Vuga development Initiative
  .
  Alisema hatua hiyo ina lengo la kuhakikisha wanakomesha vitendo vinavyofanya na baadhi ya vijana vya kuwa sha wishi wananfunzi wa kike na kuwapatia ujauzito hivyo kupelekea wasichana hao kukatisha masomo yao.

  Mkuu huyo wa wilaya alisema hivi sasa lazima wawe wakali na watu wanaocheza na maisha ya watoto ya wanafunzi ambao asilimia kubwa masomo yao yana haribiwa mara tu baada ya kushawishiwa na kupewa ujauzito.
  MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Mhandisi
  Robert Gabriel akizungumza wakati makabidhiano ya vyumba vya madarasa vitano na vyoo ishirini na nne,mradi maji na uzio wa shule ya msingi jitengeni iliyopo Mji mdogo wa Mombo uliofanywa na taasisi isiyo ya kisherikali A better World ya Canada ikishirikiana na Vuga development Initiative kulia ni Founder wa A Better World Canada Eric Rajabu na Mkurugenzi wa Taasisi ya A Better Worild Canada
  nchini Tanzania,Aizidi Kaoneka 
  Founder wa A Better World Canada Eric Rajabu kushoto akizungumza katika halfa hiyo kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya A Better Worild Canada nchini Tanzania,Aizidi Kaoneka 
  Mkurugenzi wa Taasisi ya A Better Worild Canada nchini Tanzania,Aizidi Kaoneka akizungumza katika halfa hiyo 


  0 0


  Na Dotto Mwaibale

  JAMII imetakiwa kujenga moyo wa kusaidia watu waliopo katika makundi yenye uhitaji ili nao wajisikie kama watu wengine waliopo katika familia.

  Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark inayojishughulisha na uwezeshaji jamii, Agnes Mgongo wakati kampuni hiyo ilipokuwa ikitoa zawadi ya Sikukuu ya Eid El-Fitr katika Kituo cha watoto Yatima cha Mtoto Wetu Tanzania kilichopo Kimara Suca jijini Dar es Salaam leo hii.

  "Ni vizuri jamii ikajenga tabia ya kuwakumbuka watoto na watu wengine waliopo katika makundi maalumu kwa kuwafariji badala ya kuiachia serikali ambayo ina mambo mengi ya kufanya" alisema Mgongo.

  Alisema kampuni yake iliguswa na changamoto walizonazo watoto waishio katika kituo hicho ikaona ni vizuri katika kipindi hiki cha sikukuu ya Eid El-Fitr wakajumuike nao kwa kula na kucheza pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali.

  Mgongo alitaja zawadi walizotoa kupitia wadau wengine marafiki wa taasisi hiyo kuwa ni nguo, vinywaji na chakula ambacho kilipikwa katika kituo hicho.

  Akizungumzia changamoto wanazokumbana nazo watoto waliopo katika makundi yenye uhitaji, Wanswekula Zacharia alisema ni pamoja na vitabu, karo, sare za shule na mahitaji mengine.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo akizungumza na wanahabari wakati wa kutoa zawadi kwa watoto Yatima wa Kituo cha Mtoto Wetu Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo akiwa amekaa na watoto wa kituo hicho.
  Mratibu wa Miradi wa Kampuni hiyo, Gasparino Haule akiongoza kucheza katika hafla hiyo.


  0 0


  0 0   Sheikh Shariff Majini kutoka Dar es salaam Siku ya Eid Pili akiwa Arusha ameendesha Dua maalum ya kuaga Mwezi mtukufu wa Ramadhani. Sheikh aliifanya Dua hiyo katika viwanja vya soko la Kilombero stendi ya Hiace.
  Dua ya Sheikh ilianza saa nane na kumalizika saa kumi na mbili jioni na kuhudhuriwa na wakazi wengi wa Jiji la Arusha. Pia Sheikh alipata nafasi ya kusikiliza shida mbalimbali za watu waliojitokeza katika Dua. Sheikh anataraji kuendelea na Dua Jijini Arusha siku ya Eid Tatu (Jumatano tarehe 28-06-2017) katika viwanja vya Soko la Kilombero stendi ya Hiace.
  Sheikh Shariff Majini akiwasili kuendesha Dua maalum ya kuaga Mwezi mtukufu wa Ramadhani katika viwanja vya soko la Kilombero stendi ya Hiace jijini Arusha.
  Sehemu ya umati wakati wa dua  hiyo katika viwanja vya soko la Kilombero stendi ya Hiace jijini Arusha.
   Sheikh Shariff Majini akiendesha Dua maalum ya kuaga Mwezi mtukufu wa Ramadhani. katika viwanja vya soko la Kilombero stendi ya Hiace jijini Arusha.
  Sehemu ya umati wakati wa dua  hiyo katika viwanja vya soko la Kilombero stendi ya Hiace jijini Arusha.

older | 1 | .... | 1769 | 1770 | (Page 1771) | 1772 | 1773 | .... | 3348 | newer