Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1768 | 1769 | (Page 1770) | 1771 | 1772 | .... | 3348 | newer

  0 0

   

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira mara baada ya kuwasili Mkoani hapo kwa ajili ya kuhudhuria ibada ya Eid Elfitr itakayo fanyika Kitaifa Mkoani Moshi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  ​Kituo cha redio cha EFM Jumapili ya leo tarehe 25/6/2017 kimehitimisha mchezo wake uitwao sakasaka ambao ulianza mnamo tarehe 28 Mei na kuchezeshwa katika wilaya tano ambazo ni Kigamboni, Ubungo, Ilala, Temeke, na Bagamoyo. Ni mwaka wa tatu sasa tangu mchezo huu wa sakasaka uanze kuchezeshwa.
  Mchezo huu huchezeshwa kwa kuficha vitu katika uwanja fulani na vitu hivyo huwa na thamani ya pesa iliyoandikwa katika karatasi yenye muhuri wa kituo cha redio, ambapo dondoo za kitu kilichofichwa na mahali kilipofichwa hutajwa katika redio hivyo msikilizaji atakae weza kuunganisha dondoo hizo na kukipata kitu hicho ndio atakuwa mshindi.
  Efm redio imetoa kiasi cha shilingi milioni saba na laki tano katika mchezo huu wa sakasaka kwa washindi 40 katika wilaya zote tano ambapo katika kila wilaya wanapatikana washindi nane, thamani ya mshindi wa kwanza ni shilingi milioni moja, na washindi wengine ni wa laki moja, elfu hamsini n.k.
  Imekua ni kawaida kama redio kuja na vitu mbalimbali ambavyo vitashirikisha wasikilizaji wetu ikiwa ni namna moja ya kuwashukuru na kuwawezesha katika biashara zao pamoja na familia zao kiujumla.
   Baadhi ya mashabiki wa EFM wakishuhudia zoezi zima na washindi kukabidhiwa pesa zao.
   Mtangazaji wa kipindi cha Uhondo ya E-fm radio, Adam Melele ( Swebe Santana) akimkabidhi mshindi wa kwanza Vaileth Rumishael Shayo kitita cha shilingi milioni moja.
   Adam Melele (Swebe Santana) akizungumza jambo na moja ya washindi wa saka saka Bw. Aibu Msomba
   Afisa Uhusiano na mawasiliano wa Efm radio akimkabidhi Bw. Munir Hamidu moja wa washindi wa saka saka shilingi elfu hamsini.
  Bi. Khadia Selemani akikabidhiwa kiasi cha shilingi laki moja baada ya kuibuka mshindi kwa kile alichokisaka kuwa sahihi na kinatoka E-Fm radio.

  0 0


   Mkuu wa Jeshi la Polisi nchi IGP Simon Sirro akikagua gwaride la maofisa wa uhamiaji wakati wa sherehe za kumaliza kozi namba moja kwa maofisa hao, sherehe zimefanyika leo chuo cha polisi moshi CCP. Kozi hiyo ilihusisha warakibu wasaidizi (ASP), wakaguzi wasaidizi, meja, sajenti na koplo.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchi IGP Simon Sirro akiwa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji CGI Dkt. Anna Peter Makakala wakati wa sherehe za kumaliza kozi namba moja kwa maofisa hao. Sherehe zimefanyika leo Chuo cha Polisi Moshi (CCP). Kozi hiyo ilihusisha warakibu wasaidizi (ASP), wakaguzi wasaidizi, meja, sajenti na koplo.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro akimvisha cheo Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Hadija Masoud Ali wakati wa sherehe za kumaliza kozi namba moja kwa maofisa hao. Sherehe zimefanyika leo Chuo cha Polisi Moshi (CCP). 


  Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro akihutubia wakati wa sherehe za kumaliza kozi namba moja kwa maofisa hao katika Chuo cha Polisi Moshi (CCP). Kozi hiyo ilihusisha warakibu wasaidizi (ASP), wakaguzi wasaidizi, meja, sajenti na koplo. Picha na Hassan Mndeme wa Jeshi la Polisi

  0 0
  0 0

  Sheikh Shariff Majini siku ya Jumamosi tarehe 24-06-2017 alifanya Dua nzito katika ukumbi wa Star Light Hotel uliopo Jijini Dar. 
   Dua ya Sheikh Shariff ilianza saa moja asubuhi na kumalizika saa saa saba mchana.. Mara baada ya dua Sheikh amesafiri mpaka Arusha tayari kwa kufanya Dua maalum la kumaliza mwezi mtukufu mara baada ya kuombwa sana kupitia simu ilo arudi. 
   Sheikh atafanya Dua kwa siku mbili mfululizo Eid Pili na Eid Tatu katika viwanja vya soko la Kilombero stendi ya vi hiace Jijini Arusha kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi na mbili jioni.
  Sheikh Shariff Majini akifanya dua siku ya Jumamosi  katika ukumbi wa Star Light Hotel uliopo Jijini Dar es salaam. 
  Sehemu ya umati mkubwa uliohudhuria wakati Sheikh Shariff Majini akifanya dua siku ya Jumamosi  katika ukumbi wa Star Light Hotel uliopo Jijini Dar es salaam. 
  Sheikh Shariff Majini akiendelea na dua siku ya Jumamosi  katika ukumbi wa Star Light Hotel uliopo Jijini Dar es salaam. 

  0 0

  Ebby mwenye jezi nyeusi akiwatambulisha baadhi ya vijana wenzake wa Marafiki Charity kwa mmoja wa walezi wa kituo cha CHAKUWAMA wakati walipowasili hapo jana Juni 24.2017 katika tukio hilo la kuwafuturisha watoto hao wanaolelewa kituoni hapo.
  Baadhi ya wanaumoja wa Marafiki Charity wakiwa kwenye pozi tofauti, akiwemo Devotha, Leah Mushi aliyembeba mtoto Malaika Ebby, Munira Hussen, Esther Namuhisa,na Pendo
  Watoto hao wanaolelewa na kituo hicho cha CHAKUWAMA wakiwa kwenye foleni ya kupata futari hiyo maalum iliyoandaliwa na MARAFIKI CHARITY
  Watoto hao wanaolelewa na kituo hicho cha CHAKUWAMA wakiwa kwenye foleni ya kupata futari hiyo maalum iliyoandaliwa na MARAFIKI CHARITY

  Watoto hao wanaolelewa na kituo hicho cha CHAKUWAMA wakiwa kwenye foleni ya kupata futari hiyo maalum iliyoandaliwa na MARAFIKI CHARITY.  0 0


  0 0
  0 0


  Mwenyekiti wa TAMCO (Jumuiya ya Waislamu DMV) Bwn Ally Mohamed akitoa salamuza Eid El Fitr kwa Waislam na marafiki zao DMV kwenye sherehe ya Eid El Fitr iliyofanyika siku ya Jumapili June 25, 2017 Silver Spring, Maryland.Picha na Vijimambo Blog na Kwanza production.
  Kushoto ni Balozi Mustafa Nyang"anyi akijumuika kwenye sherehe ya Eid El Fitr na Watanzania DMV.
  Balozi Mustafa Nyang"anyi akifuatilia sherehe ya Eid El Fitr iliyofanyika Sliver Spring, Maryland siku ya Jumapili June 25, 2017, kulia ni Seif Ameir.
  Watanzania DMV wakijumuika pamoja katika sherehe ya Eid El Fitr iliyofanyika Silver Spring, Maryland siku ya Jumapili June 25, 2017.


  0 0


  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wananchi mbali mbali baada ya Swala ya Eidd Fitri iliyoswaliwa leo katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja katika kusherekekea kumalizika kwa Mfungo wa MweziMtukufu wa Ramadhan.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wananchi mbali mbali baada ya Swala ya ElIdd Fitri iliyoswaliwa leo katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja katika kusherekekea kumalizika kwa Mfungo wa MweziMtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.
   Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga   alipokuwa akitoa khutba baada ya Swala ya El Idd elfitri iliyoswaliwa katika Uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja katika kusherehekea Sikukuu ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan aliyohudhuriwa na Viongozi  wa Kitaifa na Waislamu mbali mbali wa Mkoa wa Mjini Magharibi  leo.
   Waislamu wanawake wakiwa katika Swala ya Eid  el fitri iliyoongozwa na Sheikh Fadhil Soraga katika Uwanja wa Maisara Suleiman Mjni Unguja leo katika Mkoa wa Mjini Magharibi ambapo  Viongozi  wa Kitaifa na Waislamu mbali mbali walihudhuria [Picha na Ikulu.] 26/06/2017.
   Baadhi ya waislamu wanaume waliohudhuria katika swala ya EId elfitri wakimsikiliza  Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar  Sheikh Fadhil Soraga aklipokuwa akitoa khutba ya Swala ya El Idd elfitri iliyoswaliwa katika Uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja katika kusherehekea Sikukuu ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.

  0 0

  Rais mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi akitoa Salamu za Eid el Fitr kwa waislam baada ya Swala ya Eid el Fitr katika viwanja vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam, mapema leo
  Pichani kulia ni Rais mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi sambamba na waumini wengine wakiswali swala ya sikukuu ya Eid El Fitr iliyofanyika mapema leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja,jijini Dar es Salaam.
  Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum akitoa mawaidha yake wakati wa Swala ya Eid El Fitr katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Waumini wa dini ya Kiislamu wakifuatilia mawaidha mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa katika Swala ya Eid El Fitr,iliyofanyika kwenye viwanja vya mnazi mmoja mapema,leo jijini Dar. 
  Swala ya Eid El Fitr ikiendelea mapema leo asubuhi.
  Waumini wa dini ya Kiislamu wakiswali swala ya Eid El Fitr,katika viwanja vya mnazi mmoja mapema,leo jijini Dar.
  Waumini wa dini ya Kiislamu wakiwa wamejumika pamoja katika swala ya Eid El Fitr,katika viwanja vya mnazi mmoja mapema,leo jijini Dar.
  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Dkt Hussein Mwinyi akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Mhe.Salum Hapi mara baada ya kuwasili katika Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika mapema leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,Pichani kati ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Al Had Mussa Salum .
  Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Mhe.Salum Hapi mara baada ya kuwasili katika Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika mapema leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Pichani kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha CUF,Prof Haroun Lipumba na waumini wengine wakiwasili katika viwanja vya Mnazi mmoja kwa ajili ya kushiriki swala ya Eid El Fitr jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim akiongozwa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Al Had Mussa Salum pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Mhe.Salum Hapi kushiriki kwenye swala ya sikukuu ya 
  Eid El Fitr iliyofanyika mapema leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja,jijini Dar es Salaam.


  0 0


  0 0  0 0

  Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma, akizungumza kwenye mkutano uliofanyika jana, Kata ya Bugarama Msalala. Wabunge wanaotoka maeneo jirani yenye wawekezaji wa madini pia walihudhuria mkutano huo.
  Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma, amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuacha tabia ya kuwazuia wananchi wanaounga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli za kupambana na wezi wa raslimali za taifa ikiwemo madini.

  Msukuma aliyasema hayo baada ya polisi katika wilaya ya kipolisi Msalala, kuzuia maandamano ya amani na mkutano wa hadhara yaliyoandaliwa na mbunge wa Msalala mkoani Shinyanga, jana jumamosi katika eneo la Kakola.

  Hata hivyo polisi walitoa idhini ya mkutano wa hadhara kufanyika katika uwanja wa Bugarama badala ya Kakola kwa madai kwamba walipata taarifa za uvunjifu wa amani katika eneo la Kakola.

  Naye mbunge wa Msalala Ezekiel Maige alisema bado ataandaa mkutano mwingine utakaofanyika Kakola ili kutoa fursa ya wananchi wengi kujitokeza kutoa pongezi kwa Rais Magufuli pamoja na kero zao baada ya wengi wao kushindwa kufika katika mkutano wa jana kutokana na umbali wa kwenda Bugarama.

  Alisema halmashauri ya Msalala inaidai migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu takribani shilingi tilioni mbili ambazo atahakikisha zinalipwa ili kusaidia maendeleo ya jimbo lake ikiwemo ujenzi wa barabara ya lami ya Kahama-Geita.

  Katika mkutano huo, bado kilio cha wakazi wa Kakola kilikuwa ni kuutaka mgoni wa Bulyanhulu kuwalipa fidia zao za ardhi na zile za baadhi ya wafanyakazi kuumia na kuachishwa kazi huku baadhi yao wakikumbushia machungu ya ndugu zao kufukiwa mashimoni wakati wakihamishwa ili kupisha shughuli za mgodi ambapo nao wanashinikiza kulipwa fidia.
  Mbunge wa jimbo la Msalala, Ezekiel Maige, akizungumza kwenye mkutano huo.
  Viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Shinyanga, Azza Hamad (kushoto), diwani wa Kata ya Bulyanhlu, John Kiganga (katikati).
  Wakazi wa Msalala wakiwa kwenye mkutano huo

  0 0

  Kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa Malaria kilichopo Kibaha, Mkoani Pwani.
  Tarehe 22 June 2017, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilipia VIUADUDU vya kutokomeza Mbu wa Malaria lita 100,000 na kuagiza vigawanywe kwenye Halmashauri zote nchini.
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu anapenda kuwatanganzia Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuwa VIUADUDU hivi vitaanza kugawiwa leo kwa Halmashauri za Mikoa 14 yenye kiwango kikubwa cha Maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria. 

  Mikoa hii (na kiwango cha maambukizi ya malaria kimeonyeshwa kwenye mabano) ni;- Kagera (41%), Geita (38%), Kigoma (38%), Ruvuma (23%), Tabora (20%), Mtwara (20%), Mara (19%), Morogoro (14%), Shinyanga (17%), Lindi (17%), Pwani (15%), Mwanza (15%), Katavi (14%) na Simiyu (13%).

  Mikoa mingine ambayo haijatajwa itagawia Viuadudu katika Awamu ijayo. Idadi ya Lita zitakazogawanywa kwa kila Halmashauri zilizo katika Mikoa  hii tayari imeshaainishwa.

  Wizara inawakumbusha Waganga Wakuu wa Mikoa/Wilaya kufanya Upuliziaji wa Viuadudu kwa kuzingatia Miongozo ya Wizara ya Afya. Hii itawezesha kupata matokeo tarajiwa ya kutokomeza mbu ili kudhibiti ugonjwa wa Malaria nchini. 
  Aidha, Wizara ya Afya inapenda kumshukuru kwa dhati na kumpongeza Mhe.Rais Dkt. Magufuli kwa kuongeza chachu katika Mapambano dhidi ya Malaria Nchini. 

  Imetolewa na;
  Catherine Sungura
  Kaimu Msemaji- Idara Kuu  Afya
  26 June 2017

  0 0

  Na Jumia Travel Tanzania
  Inastaajabisha kuona watu wa mataifa ya nje wanajua vitu vingi zaidi vinavyopatikana Tanzania kuliko watanzania wenyewe. Sijui ni ile hulka ya kutopenda kufuatilia mambo au ni dhana kwamba waache wageni waje kushangaa maana hivyo vitu vitaendelea kuwepo tu.

  Nchi yetu imebarikiwa na inaendelea kubarikiwa kugunduliwa kwa mambo mengi zaidi ya kustaajabisha ambayo hayapatikani kwingineko duniani. Jumia Travel ingependa kukufumbua macho kwamba yafuatayo ni baadhi tu ya mambo yanayopatikana na unaweza kuyashuhudia ukiwa nchini Tanzania. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Naibu  Katibu Mkuu wa  Muungano wa Makanisa ya Pentekoste katika Tanzania wa Umoja wa Wanawake (UW-MMPT), Loveness Maiko akizungumza katika Kongamano la Kitaifa la Wanawake wa kanisa hilo la mwaka huu wa 2017 lililofikia tamati jana Misheni ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
   Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Kitaifa, Erasto Makalla akitoa mahubiri ya kufunga kongamano hilo.
   Askofu Methusela John Mpera akiongoza maombi ya kufunga kongamano hilo.
   Hii ni kamati nzima iliyofanikisha kongamano hilo.
  Naibu  Katibu Mkuu wa  Muungano wa Makanisa ya Pentekoste katika Tanzania wa Umoja wa Wanawake (UW-MMPT), Loveness Maiko akizungumza katika Kongamano la Kitaifa la Wanawake wa kanisa hilo la mwaka huu wa 2017 lililofikia tamati jana Misheni ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
   Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Kitaifa, Erasto Makalla akitoa mahubiri ya kufunga kongamano hilo.
   Askofu Methusela John Mpera akiongoza maombi ya kufunga kongamano hilo.
   Hii ni kamati nzima iliyofanikisha kongamano hilo.
  Naibu  Katibu Mkuu wa  Muungano wa Makanisa ya Pentekoste katika Tanzania wa Umoja wa Wanawake (UW-MMPT), Loveness Maiko akizungumza katika Kongamano la Kitaifa la Wanawake wa kanisa hilo la mwaka huu wa 2017 lililofikia tamati jana Misheni ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
   Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Kitaifa, Erasto Makalla akitoa mahubiri ya kufunga kongamano hilo.
   Askofu Methusela John Mpera akiongoza maombi ya kufunga kongamano hilo.
   Hii ni kamati nzima iliyofanikisha kongamano hilo.
   Taswira ya kongamano hilo. Hawa ni wanawake walioshiriki kutoka mikoa mbalimbali. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA
  0 0


  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein ametanabaisha na kusisitiza juu ya umakini mkubwa unaohitajika katika kuandaa, kusimamia na kufuatilia Mikataba ya Mafuta na Gesi ili kuepuka ubabaishaji kwani rasilimali hizo ni za Wazanzibari wote. 
  Alhaj Dk. Shein aliyasema hayo leo katika hotuba yake aliyoitoa katika Baraza la Idd El Fitri lililofanyika huko katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi, Kikwajuni Mjini Zanzibar. 
  Alisisitiza kuwa mikataba ya Mafuta na Gesi Asilia isitoe mwanya wa kuwanufaisha watu wachache na makampuni yao kwa njia za kijanja, dhulma na mambo ya ubabaishaji na kutaka kujifunza kwa waliotangulia katika biashara ya aina hiyo. 
  Katika hotuba yake, Dk. Shein alisema kuwa baada ya kukamilika kwa kazi ya kutunga Sheria ya Mafuta na Gesi Asilia, kuanzisha Mamlaka ya Kusimamia na kuratibu shughuli za Mafuta na Gesi na kuanzisha Kampuni ya Mafuta, hatua muhimu inayofuatana ni kuandaa Mikataba ya Mafuta na Gesi Asilia.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Dini na Mashekhe wa Dini ya Kiislamu waliofika  Ikulu Mjini Unguja   leo kumtakia  Rais Sikukuu njema baada ya kumalizika kwa  Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein  pampja na Viongozi mbali mbali wa Dini na Mashekhe wa Dini ya Kiislamu waliofika  Ikulu Mjini Unguja   leo kumtakia  Rais Sikukuu njema baada ya kumalizika kwa  Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,wakiitikia Dua Iliyoombwa na Mufti Mkuu wa Zanzibae Sheikh Saleh Omar Kabi
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)alipokuwa akitoa Sikukuu kwa Mzee Juma Kesi (kulia) alipojumuika na Wazee mbali mbali waliofika katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja  kupokea mkono Eid el Fitri katika kusherehekea Sikukuu ya  Eid el Fitri iliyoanza leo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,


   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) aliopokuwa akitoa hutuba yake kwa Wananchi na Waislamu mbali mbali katika Sherehe za Baraza la Eid el fitri lililofanyika   katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi, Kikwajuni Mjini Unguja katika   kusherehekea Sikukuu ya  Eid el Fitri iliyoanza leo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan
   Baadhi ya Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi na Wananchi mbali mbali wakisikiliza Hutuba ya sherehe za  Baraza la Eid el fitri iliyosomwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani )  katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi, Kikwajuni Mjini Unguja katika   kusherehekea Sikukuu ya  Eid el Fitri iliyoanza leo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA


older | 1 | .... | 1768 | 1769 | (Page 1770) | 1771 | 1772 | .... | 3348 | newer