Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1770 | 1771 | (Page 1772) | 1773 | 1774 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Shizza Kichuya wa Taifa Stars akichuana na mlinzi wa Angola kwenye mchezo wao wa kundi A  uliomalizika kwa suluhu  ya 0-0 uwanja wa Royal Bafokeng  mjini Rustenburg Afrika Kusini 

  0 0
  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na watumishi wa iliyokuwa Presidential Delivery Bureau (PDB) waliokuwa wakisimamia utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRN alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata picha ya pamoja na na watumishi wa iliyokuwa Presidential Delivery Bureau (PDB) waliokuwa wakisimamia utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRNalipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na na watumishi wa iliyokuwa Presidential Delivery Bureau (PDB)waliokuwa wakisimamia utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRN baada ya kukutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na jopo la wataalam wa masuala ya umeme na ujenzi wa miundombinu ya mabwawa ya maji kwa ajili ya kuzalisha umeme na kujadiliana nao kuhusu utekelezaji wa mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Power Project) ambao una uwezo wa kuzalisha Megawatts 2,100 za umeme Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2017

  0 0  0 0

  Hivi ndivyo Ufukwe wa Coco (Coo Beach) ulivyofurika watu wa aina mbalimbali hapo jana jioni, katika kusherehekea sikukuu ya Iddi pili,Mabasi/Daladala kutoka kona kadhaa za jiji la Dar zilionekana zikishusha watu kwa wingi katika ufukwe huo ambao ulisheheni pia vyakula vya kila aina ikiwemo Mihogo,Chips mayai na wengine walikutwa na Camera ya Blogu ya jamii wakiwa wemebeba vyakula vyao na kujibweda kando kando ya ufukwe,ama kwa hakika ilikuwa burudani kwa wakazi wa jiji la Dar.Picha na Michuzi Jr.

  Kuhakikisha ulinzi na usalama wa kutosha unakuwepo,Jeshi la Polsi lilipiga kambi kabisa eneo hilo,kwa idadi ya watu ilikuwa ni kubwa.
  Sehemu za kupaki magari zikaonekana hazitoshi kabisa
  Foleni ya kuingia kando kando ya ufukwe nayo ilikuwa kubwa kiasi ambacho magari mengine yalipita kwa taabu kuendelea na safari zake.
  Chopa ya Jeshi la polisi nayo ilikuwa na kazi ya ziada kama hivi ya kukagua meneo mbalimbali yaliyokuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu,Pichani chini Chopa ikionekana kwa mbali ilipokuwa ikikatiza maeneo hayo.


  0 0

  MBUNGE wa Jimbo la Dodoma mjini, Anthony Mavunde leo amefanya ziara ya kutembelea maeneo ya katikati ya mji na kusikiliza kero zinazowakabili wananchi hasa wafanyabiashara ndogo ndogo.

  Hatua hiyo ya Mavunde imetokana na Ofisi yake ya Mbunge kuweka utaratibu wa kuwasikiliza wananchi kero zao na matatizo yao kila Alhamis(kero za Ardhi) na Ijumaa(Mambo ya kijamii).

  Hata hivyo kwa siku ya leo kutokana na mapumziko ya Sikukuu ya Eid El Fitr, Mavunde ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ameamua kutembea maeneo mbalimbali ya mjini katikati na kusikiliza kero za wananchi.

  Maeneo aliyotembelea ni pamoja na eneo la ‘One way’ ambalo kuna wafanyabiashara wengi wakubwa na wadogo na barabara ya sita ambako ni maarufu kwa maduka ya simu katika kata ya Madukani.

  Akizungumza mara baada ya kuwatembelea wananchi hao, Mavunde ameahidi kuzipatia ufumbuzi baadhi ya kero zinazowasibu wafanyabiashara hao.
  Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akiwasikiliza wafanyabiashara ndogo ndogo(machinga) katika eneo la ‘One way’.
  Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyabiashara katika maduka ya simu barabara ya sita.


  0 0

  Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii asubuhi hii inaeleza kuwa, Rais wa Shirikisho la Soka nchini, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa wanashikirikia na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na wapo katika Kituo cha Polisi Salander Bridge ili kupisha uchunguzi dhidi yao. hilo limethibitisha na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Takukuru, Mussa Misalaba alipokuwa akihojiwa na kituo cha Radio EFM leo. Misalaba amesema ni kweli wanawashikilia na taarifa zaidi wataitoa baada ya kumaliza uchunguzi wao, kwa sasa ifahamike kuwa viongozi hao wanawashikilia.

  0 0
 • 06/27/17--23:17: MAPOROMOKO YA MAJI MWALALO.
 • Ni maporomoko yanayopatikana katika safu za milima ya LIVINGSTONE karibu na kingo za ziwa Nyasa (MATEMA BEACH), kijiji cha Matema, wilaya ya Kyela mkoani Mbeya. Mto huu humwaga maji yake ziwa Nyasa.

  Maporomoko haya yapo sehemu ambayo ni nzuri kwa (ku hike) ambapo huchukua takribani saa 1 (1hr) kutembea kwa mwendo wa kawaida (kwa miguu) kutoka katika kijiji cha Matema.

  Ni nzuri kutembelea eneo hilo kwa muda wa ziada pale unapotembelea fukwe za ziwa Nyasa kwaajili ya mapumziko au sababu za kitalii kwa ajili ya zoezi la mwili, moja kati ya interesting moment ni pale katika kakilima ka mwisho kanakohitaji kupanda kwa kujivuta katika kamba.

  Eneo lina sifa ya muonekano mzuri hasa wa rangi nyeupe ya maji yanayoporomoka katika miamba ya rangi ya mvuto ya kijivu.

  Maporomoko haya yametengeneza bwawa zuri na la asili katikati ya miamba (mawe) ambacho ni kizuri kwa kuogelea, na kupigia picha

  Ungependa kufika mahali hapa? Wasiliana na UYOLE CULTURAL TOURISM ENTERPRISE
  Simu 0783545464,
  Barua pepe: uyolecte@gmail.com

  0 0

  BBC Swahili launched on 27th June 1957 and will be celebrating its Diamond Jubilee this week. Special programming will be available throughout the week to recognise this impressive milestone.

  Celebration editions of AMKA na BBC (radio) and Dira ya Dunia (TV and radio) will look at how far BBC Swahili has come over its long history.  This will include the growth of the Kiswahili media industry, the impact of democracy and how BBC Swahili has touched listener’s lives. The service will also look at entertainment from the region over the years - in particular Swahili Beats. Past BBC presenters will be popping up to reflect on how things have changed since the first broadcast from London.

  As well as these treats there will be a one-off debate in Dar es Salaam today, the exact date the first Swahili program went on air. Entitled : ‘’My Swahili’’ it will look at how the language - widely spoken in East Africa - has evolved, including the different dialects and how people are embracing Swahili.  There will be a panel of special guests representing BBC Swahili audiences and locals taking part.

  There will be a host of online content for Swahili- speaking audiences across the world to access at their convenience, including fun fact videos with BBC reporters and presenters; a comparison of the old and the new through the eyes of ex-BBC Swahili staff and a newbie to the service; a day in the life of a Swahili digital fan and an informative chronicle of key milestones for the service.

  BBC Swahili has evolved from a radio station to a broadcaster offering a breadth of multimedia content, with daily television programming, a comprehensive online news website and popular social media feeds.

  Caroline Karobia, Editor BBC Swahili says “We are so proud of our great broadcasting history and hope we can carry on improving and serving our audiences for many years to come.  We are excited by the possibilities opened up by new technology to engage even more closely with our audience in the future. ”

  0 0


  150+ business leaders engage in panel discussion on solutions for ‘off-grid societies’.

  Dar es Salaam, Tanzania: Dalberg Group, The Africa List and the CEO Roundtable hosted an Iftar dinner to celebrate Dalberg’s 10 years in Africa by launching the book “17 Big Bets for a Better World”. The purpose of the launch was to kick off a discussion on Tanzania’s future and the role that the private sector plays in building the economy while addressing issues that affect Tanzanians.

  The event was attended by more than 150 business leaders in Tanzania representing a diverse range of sectors including finance and banking, telecoms, agribusiness and manufacturing. Reflecting on the launch in the Tanzanian context, Dalberg Group’s Executive Director - James Mwangi - remarked, “The book presents 17 bold and innovative ideas to reduce global poverty and improve lives. 

  It tackles the types of questions that Dalberg has been addressing in Tanzania and the rest of Africa for the past decade. The private sector is a major driving force in developing our economies and a key partner in the type of work we do – working on the most pressing development challenges.”

  In the book, some of the world’s most renowned thought leaders detail how we collectively can reach the global goals (Sustainable Development Goals) set forth by the UN last year. From a bank president and a Nobel Peace Prize winner to an artist and Michelin-chef, contributors include Amina Mohammed – current Deputy Secretary-General of the United Nations and a former Minister of Environment of Nigeria, Ashish J. Thakkar – the founder of the Mara Group and Mara Foundation, James Mwangi – Managing Director and CEO of Equity Bank among others.

  The book presents fresh and credible solutions to the challenges humanity faces through 17 transformational ideas for positive change. Reviews of 17 Big Bets Ban Ki-moon, Secretary General, United Nations.

  Ruge Mutahaba, Co-founder Clouds Media Group (right) speaking during the panel discussion on solutions for ‘off-grid societies’ during the launch of the book ’17 Big Bets for a Better World’. Also in the panel is, Chief Executive Officer of Benjamin Mkapa Foundation, Dr Ellen Mkondya- Senkoro (left) and Executive Director of the Dalberg Group, James Mwangi (middle) moderating the panel discussion
  Executive Director of the Dalberg Group, James Mwangi (middle) moderating the panel discussion on solutions for ‘off-grid societies’ during the launch of the book ’17 Big Bets for a Better World’. Also in the panel is, Chief Executive Officer of Benjamin Mkapa Foundation, Dr Ellen Mkondya- Senkoro (left) and Ruge Mutahaba, Co-founder Clouds Media Group.
  Guests following the panel discussion on solutions for ‘off-grid societies’ during the launch of the book ’17 Big Bets for a Better World’. 


  0 0
 • 06/28/17--01:05: TANZIA
 • Mchambuzi mahiri wa muziki wa Charanga Zerno Andrew Lucas, aliyefahamika zaidi kwa jina Brother Zeno, amefariki dunia jana asubuhi katika hospitali ya Temeke, Brother Zeno aliyekuwa akishirikiana na 'Mzee wa Macharanga' Charles Hillary enzi hizo Radio One, alikuwa na ufahamu mkubwa wa muziki wa kutoka Cuba na hivyo kuwa mpenzi mkubwa wa watu waliopenda muziki huo. 

  Brother Zeno amesumbuliwa karibu mwaka mzima na tatizo la moyo na katika siku zake chache za mwisho alikuwa akipumua kwa msaada wa mashine, alitegemewa angepata nafuu na kuhamishiwa Muhimbili kwa matibabu zaidi lakini Mungu amekuwa na mipango mingine. 

  Msiba wa Mzee utakuwa nyumbani kwake Mbagala Kibonde Maji na mazishi yatakuwa leo 28/6/2017 saa kumi hukohuko Mbagala

  0 0

  MKOA wa Singida umebuni mkakati wa kuanzisha dawati la sekta binafsi litakalokuwa chini ya afisa Maendeleo ya jamii wa Mkoa litakalotambua takwimu, mahali, aina ya shughuli na hali ya uzalishaji ili kuhakikisha ushiriki mtambuka unaowajibika ipasavyo kwa kumjulisha afisa ugani kuhusu uhitaji wa huduma za ugani kwa wajasiriamali.

  Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi alitoa kauli hiyo katika Kijiji cha Sanza wilayani hapa wakati alipokuwa akitoa salamu za Mkoa kwa Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka huu, Amour Hamad Amour.
  Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa mwaka ahuu 2017,Bwana Amour Hamad Amour(wa tatu kutoka kushoto) akijiandaa kuukabidhi mwenge huo kwa kaimu Mkuu wa wilaya ya Manyoni, Miraji Mtaturu (hayupo pichani).

  Aidha Mkuu wa Mkoa huyo wa Singida hata hivyo alizitaja shughuli zitakazovyafanywa na dawati hilo kuwa ni pamoja na kumjulisha Afisa ugani kuhusu uhitaji wa huduma za ugani kwa wajasiriamali pamoja na kutoa taarifa ya soko kwa mazao mbali mbali. Shughuli zingine kwa mujibu wa Dk.Nchimbi ni pamoja na kuwajulisha wafugaji tahadhari ya mlipuko wa magonjwa  na kufikisha kwa wanufaika fursa za kiuchumi zilizopo na hivyo kuifanya serikali kuwa bega kwa bega na sekta binafsi.

  Hata hivyo Dk.Nchimbi aliweka bayana kwamba lengo la Mkoa ni kuwa na pikipiki zaidi ya saba kabla ya kilele cha mbio za Mwenge Oktoba, 2017 wataakuwa wamepata pikipiki hizo na kumuahidi kiongozi huyo mkuu wa mwenge kwamba atamtumia taarifa ya uthibitisho popote atakapokuwa.
   
  Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliutaja mkakati wa pili katika ubunifu huo wa Mkoa kuwa ni kuwapa mizinga ya nyuki kwa shughuli mbadala kwa wachoma mkaa. “Wachoma mkaa hawa wanakiri kuwa kufuga nyuki siyo tu kunaokoa mazingira na raslimali bali ni hakikisho la wao kushiriki vema katika kukuza uchumi wa viwanda na maendeleo ya Mkoa na nchi kwa ujumla”alifafanua. Hata hivyo aliweka bayana kwamba mizinga wanayopewa itaambatana na elimu ya mara kwa mara na kwamba mradi wa kuashiria mkakati huo wa “ACHIA SHOKA KAMATA MZINGA” utakutwa wilaya ya Mkalama.

  Naye Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka huu wa 2017, Amour Hamoud Amour akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Singida wakati alipokuwa akiuaga msafara wa mbio za mwenge wa uhuru kutoka Mkoa wa Dodoma, alionyesha kuridhishwa na jinsi watendaji pamoja na wananchi wa Mkoa wa Dodoma kwa namna walivyouenzi mwenge huo. 

  Mwenge  wa uhuru kitaifa mwaka huu wa 2017 wenye kauli mbiu isemayo “SHIRIKI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA VYA NCHI YETU”umeanza mbio zake Mkoani Singida baada ya kumaliza mbio zake Mkoani Dodoma ambapo utakapokuwa mkoani Singida,miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 21.9,ikiwemo miradi 14 itafunguliwa,utazindua miradi 8,utaweka mawe ya msingi miradi 13 na utatembelea miradi 10.
  baadhi ya viongozi wa chama na serikali wa wilaya ya Manyoni wakijiandaa kupokea mwenge wa uhuru kutoka kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka huu wa 2017, Amour Hamad Amour.

  0 0


  0 0

  Muonekano wa picha kwenye Tamasha la Kids Circus Carnival. Benki ya NMB ilikuwa ni mmoja wa makampuni wadhamini.

  BENKI ya NMB Tanzania jana iliungana na Watanzania nchini kusherehekea Siku Kuu ya Eid El Fitr kwa kuwa mmoja wa makampuni wadhamini wa tamasha lililoandaliwa na kampuni ya Azam la Kids Circus Carnival ambalo limehusisha watu wa aina mbalimbali kuanzia watoto na hata watu wazima kufurahi kwa pamoja. 

  Tamasha hilo ambalo linafanyika kwa siku mbili mfululizo yaani Eid Mosi (Juni, 26) na Eid Pili (Juni, 27) linafanyika katika viwanja vya Kenyatta (Kenyatta Ground) vilivyopo Osterbay, jijini Dar es Salaam. 

  Katika tamasha hilo lililokuwa na michezo anuai lilijumuisha huduma mbalimbali ambazo zinazotolewa na Benki ya NMB ambapo watu waliohudhuria tamasha walipata nafasi ya kujua huduma zinazotolewa na NMB, na pia kupata nafasi ya kufungua akaunti. 

  Pamoja na hilo pia kulikuwa na michezo mbalimbali ya watoto na maonesho ya wanyama mbalimbali wakiwepo simba, chui, mamba, farasi, sungura na wengine wengi. Zifuatazo ni picha mbalimbali za tamasha hilo. Watoto mbalimbali wakifurahia huduma kwenye Tamasha la Kids Circus Carnival.
  Watu mbalimbali wakifurahia huduma kwenye Tamasha la Kids Circus Carnival Watoto mbalimbali wakifurahia huduma kwenye Tamasha la Kids Circus Carnival. Baadhi ya michezo kwenye Tamasha la Kids Circus Carnival.


  0 0

  Shimo lililokua likichimbwa mchanga zamani likionekana kujaa maji machafu ambayo hutiririka kwenye kiwanja maalum cha kusherehekea sikukuu mbalimbalinkatika kijiji cha Kianga na kusababisha kushindwa kufanyika sherehe hizo.
  Kiwanja cha mpira cha Kianga Mento ambacho wananchi wanakitumia kwa sherehe za Iddi kikiwa kimejaa maji yanayotiririka kutoka kwenye shimo lililopo pembezoni mwa uwanja huo na kupelekea kushindwa kufanyika sherehe hizo mwaka huu. Picha na Abdalla Omar, Zanzibar.

  0 0

  Karibu katika mahojiano kati ya Mubelwa Bandio na Mkuu wa Mawasiliano wa Diaspora kutoka KCB Bank Shose Kombe.
  Mahojiano haya yalifanyika ndani ya Kilimanjaro Studio iliyopo Beltsville, Maryland nchini Marekani


  0 0

  Wakati uhalifu wa mtandao ukionekana kushika kasi duniani, Jamii imetakiwa kuzitumia simu za mkononi katika kulisaidia jeshi la polisi kubainisha watu wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kama sehemu ya kutekeleza haki yao ya kikatiba

  Wito huo ulitolewa na Mkaguzi wa Polisi Merkiad Makumba jana kwa niaba ya Kamanda wa Polisi wa wilaya ya Korogwe , wakati akizindua duka la Kisasa la kampuni ya simu za mkononi la Airtel katika wilaya hiyo mkoani Tanga. Hatua hiyo itasaidia kukabiliana na vitendo vya namna hiyo ambavyo vinahatarisha ustawi wa raia na mali zao…alisema Mkaguzi Makumba.

  “ Wahalifu wengi wanatumia mawasiliano ya simu za mkononi na wamekuwa wakiwasiliana nanyi,iwapo mtazitumia simu kwa nia njema Tanzania itakuwa sehemu salama ya kuishi” alisema Mkaguzi Mkumba. Meneja mauzo wa Airtel Tang, Habibu Kiango alisema duka hilo limewarahisishia wateja kupata huduma za Airtel kwa urahisi zaidi blia ya kwenda umbali mrefu kufuata huduma za mawasiliano . natoa wito kwa wakazi wa hapa na maeneo ya karibu kutumia fursa hii katika kukuza na kuendeleza biashara zao.

  Kiango aliongeza kwa kusema duka hili litatoa huduma nyingi pamoja na kusajili line, kutoa huduma za kifedha za Airtel Money, kuunganisha wateja na huduma za intaneti na nyingine nyingi , aidha alitumia fursa hilo kuwakaribisha wakazi wa Korogwe kulitembelea duka hilo.

  Mpaka sasa Airtel imeshazindua maduka mengine kama hili katika mikoa ya Shinyanga, Dodoma, Arusha , Manyara , Dar na Morogoro. Mpango huo wa kuzindua maduka ya kutoa hudma kwa wateja unalenga kupanua na kusogeza huduma za AIRTEL karibu na jamii hivyo kurahisisha upatikanaji wa huduma hizi muhimu na kutatua changamoto za wateja kwa urahisi na haraka zaidi. Mpaka ifikapo mwisho wa mwaka Airtel itazindua zaidi ya maduka 2000 nchini
  Mkaguzi wa Polisi wa wilaya ya Korogwe, Merkiad Makumba akikata utepe wakati wa kuzindua duka la Airtel katika wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, akishuhudia ni Afisa wa wateja wa Airtel Korogwe, Bi Elen na Meneja mauzo wa Airtel Tanga, Habibu Kiango.

  0 0


  0 0

  Serikali imesema imeridhishwa na Utendaji kazi wa Mamalaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) katika kutekeleza miradi mikubwa ya maji kwa kuzingatia Sheria na Kanuni hali inayoongeza tija katika mamlaka hiyo.

  Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na DAWASA katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo amesema moja ya miradi hiyo ni ule wa kupanua na kusambaza maji katika mji wa Chalinze utakaonufaisha wakazi zaidi ya laki mbili.
  Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo akikagua moja ya mitambo katika chanzo cha maji ruvu juu,kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA Romanus Mwangi’ngo.

  “Kwa ujumla naridhishwa na kazi inayofanywa na DAWASA katika kutekeleza miradi ya maji nawatia moyo muendelee kufanya kazi hii kwa bidii ili azma ya Serikali kuwafikishia wananchi huduma ya maji kwa wakati itimie” Alisisitiza Prof. Mkumbo.

  Akifafanua Prof. Mkumbo amesema katika ziara yake amejionea na kukagua miundo mbinu ya kusambaza maji,ujenzi wa matanki ya kuhifadhi maji na miundo mbinu yote katika chanzo cha maji Wami kinachopanuliwa ili kukidhi mahitaji ya wakazi wa Chalinze .
  Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo akikagua miundo mbinu ya chanzo cha maji ruvu juu wakati wa ziara yake ya kukagua miradi inayotekelezwa na DAWASA.

  “Wananchi wajenge utamaduni wa kutunza rasilimali zilizopo ikiwemo miundo mbinu ya maji mbayo inajengwa kwa gharama kubwa ili iweze kuwanufaisha Wananchi wote na kuchochea maendeleo” Alisisitiza Prof. Mkumbo Mradi mwingine uliotembelewa ni ule wa uchimbaji visima vyenye urefu wa mita 600 kila kimoja vipatavyo 20 na kati ya hivyo 17 vimekamilika hivyo kuongeza upatikanaji wa maji ambao utachochea maendeleo na ukuaji wa sekta ya Viwanda.

  Visima hivyo vitawezesha kuzalishwa kwa lita milioni 260 za maji kwa siku zitakazotumika katika Wilaya ya Kigamboni na Jiji la Dar es Salaam. Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA mhandisi Romanus Mwangi’ngo amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa vyanzo vya maji Ruvu Juu na Ruvu Chini na Visima vya Kimbiji na Mpera vitasaidia kufikisha kiwango cha maji yanayozalishwa kufikia lita milioni 756 zitakazosaidia katika kuondoa tatizo la maji katika Jiji la Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo (katikati) akisisitiza jambo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi inayotekelezwa na DAWASA.Kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA Romanus Mwangi’ngo na kushoto ni Meneja wa Kituo cha uzalishaji maji Ruvu Juu Bw. Emmanuel Makusa.

  Aliongeza kuwa kwa upande wa mradi wa Chalinze vituo vya kusambaza maji takribani 236 vimeshajengwa kati ya 351 vilivyopangwa hali inayoonyesha kuwa mradi huo unaendelea kutekelezwa kama ilivyopangwa na utakamilika mwezi oktoba 2017.

  Ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji na umwagiliaji kukagua miradi inayotelezwa na DAWASA katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani imehusisha vyanzo vya maji vya Ruvu Juu,Mradi wa uchimbaji Visima virefu Kimbiji na Mpera,Chanzo cha maji Wami unakotekelezwa mradi mkubwa wa upanuzi na ulazaji mabomba, ujenzi wa vituo vya kusambazia maji na matanki ya kuhifadhi maji Chalinze.
  Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo akioneshwa ramani ya mradi huo na hatua iliyofikiwa katika ulazaji wa mabomba kutoka kwa meneja wa mradi huo unaoanzia katika chanzo cha mto wami,mradi unaotekelezwa na Kampuni ya WAPCOS ya India chini ya usimamizi wa DAWASA.


  0 0
 • 06/28/17--03:33: Article 4


older | 1 | .... | 1770 | 1771 | (Page 1772) | 1773 | 1774 | .... | 3282 | newer