Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1765 | 1766 | (Page 1767) | 1768 | 1769 | .... | 3348 | newer

  0 0


  0 0
  0 0

   Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Richard Kwitega amekabidhi zawadi za Eid el Fitr kwa mahabusu ya watoto kwa niaba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. 
   Amesema: "Mheshimiwa Rais ametoa zawadi ya Mbuzi dume, mchele kilo 25 na mafuta ya kupikia lita 10. Vitu hivyo vitawasaidia watoto hao katika kusherekea sikukuu hiyo." 
   Aidha,amewapa salamu za Rais kwa kuwataka wajue mahali pale ni pa muda mfupi tu hivyo wakitoka wanatakiwa wakawe raia wema na wakujituma zaidi katika kazi na wale ambao ni wanafunzi wakakazane zaidi na shule. 
   Wakitoa shukrani zao watoto hao wamemshukuru sana katibu tawala kwa niaba ya Rais, na wamempongeza kwa kazi nzuri anayofanya katika kujenga taifa hili na wao wameaidi wakitoka hapo watakuwa raia wema. 
   Watoto hao wameiomba serikali kuwasaidia katika usikilizwaji wa kesi zao zisichukue mda mrefu sana na hivyo kupelekea wengi wao kukosa masomo yao ya shule.
   Mkurugenzi wa kituo hicho Musa Mapua, amesema tokea mwaka huu uanze ni watoto 48 wameshapita katika kituo hicho na kwa sasa wapo watoto 11 tu na wote ni wa kiume. 
   Amesema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo kituoni hapo ni ukosefu wa gari la kubeba watoto hao pale wanapoitajika kupelekwa mahakamani na ukosefu wa uzio kwa usalama wa watoto hao. Hivyo ameiomba serikali kukisaidia kituo hicho ili watoto hao wawe katika hali ya usalama zaidi. Kila mwaka Mheshimiwa Rais amekuwa akitoa zawadi mbalimbali za Eid katika maeneo mengi ya nchi kwa lengo la kushiriki na walengwa katika kusherekea sikukuu mbalimbali za kidini

  0 0  0 0


  0 0


  0 0


  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
  MBUNGE wa Jimbo la Hai na Kionozi wa Kambi rasmi Bungeni,Mh ,Freeman Mbowe ametunukiwa cheti cha heshima na jamii ya Waislamu katika wilaya ya Hai kutokana na jitihada zake zisizo na ukomo katika kuleta umoja katika Dini na Madhehebu mbalimbali.
  “Tunaamini katka Uhuru wa kuabudu na kujieleza ,malumbano ya hoja na mijadala ,Kuvumiliana na kusamehe, Vitisho ,ugandamizaji  na uonevu wa aina yoyote vinaweza kuendelea lakini havitaweza kushinda jamii yetu. Uhuru ni tunu ya sili tuliyopewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu” yalieleza maeno yaliyopo katika Cheti hiycho.
  Mh Mbowe alikabidhiwa cheti hicho na Mjumbe wa Baraza Kuu la Waisalmu (BAKWATA) Alhaji Habib Nasiwa , katika msikiti wa Lambo uliopo Machame wilayani muda mfupi baada ya kumalizika kwa hafla ya kushiriki futari iliyoandaliwa na mbunge huyo katika misikiti minne tofauti ya Modio ,Rundugai,Kibaoni na Lambo.
  Cheti hicho kilichosainiwa na Sheakh Mkuu wa wilaya ya Hai,Sheakh ,Omary Mahmoud ambaye pia ni katibu wa msikiti wa Kibaboni Bomangombe kimetolewa ikiwa ni ni ishara ya kutambua mchango mkubwa unatolewa na Mbunge huo kwa Waislamu.
  Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wakipata Futari katika msikiti wa Kibaoni wilayani Hai.
  Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akipata Futari na waumini wengine katika Msikiti wa Lambo uliopo Machame wilayani Hai baada ya kushiriki pia katika miskiti mingine mitatu .
  Mmoja wa viongozi wa Dini ya Kiislamu Mwl Mohamed Mbowe akizungumza wakati akimkaribisha Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe katika Msikiti wa Lambo .
  Mjumbe wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Alhaji ,Habib Nasiwa akikabidhi Cheti cha Heshima kwa Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe kwa jitihada zake za kuleta umoja katika Dini na Madhehebu mbalimbali katika wilaya hiyo.


  0 0

  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii 

  MKURUGENZI wa Kampuni ya Travel House Global, Sojan Varghese amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu tuhuma za kujipatia USD 88,012 kwa mahujaji.

  Imedaiwa kuwa, fedha hizo alipewa kwa ajili kuwakatia tiketi ya ndege mahujaji zaidi ya 119 wa Chama cha Karismatiki Katoliki Tanzania.

  Varghese anadaiwa kuchukua fedha hizo kutoka kwa John Ngotty kwa ajili ya usafiri wa mahujaji hao waliokuwa wakitaka kusafiri kuelekea nchi za Roma, Italia na Israeli kwa ajili ya hija.

  Mwendesha mashtaka, wakili wa serikali, Adolph Mkini amedai Desemba 23, 2016 ofisi za Kampuni hiyo zilizopo mtaa wa Jamhuri, mshitakiwa alijipatia USD 7,012 kutoka kwa Ngotty fedha ambazo ni kwa ajili ya nauli ya kupata tiketi ya ndege kwa Wakarismatiki 119 kutoka Dar es Salaam kwenda Roma na Israeli.

  Desemba 23, mwaka jana mshitakiwa huyo alijipatia USD 9,500 kupitia hundi namba 000005 kutoka kwa Ngotty kwa ajili ya kuwakatia tiketi ya ndege.

  Mbele ya Hakimu Mkazi,Wilbard Mashauri imedaiwa kuwa, Januari 11, Varghese alijipatia USD 9,500 kutoka kwa Ngotty kwa lengo la kutumika kununulia tiketi za ndege kwa mahujaji hao

  Aidha mshtakiwa anadaiwa kujipatia USD 9,500 kwa hundi namba 000008 kutoka kwa Ngotty.

  Januari 31, mwaka huu, Varghese alijipatia USD 37,500 kutoka kwa Ngotty na Aprili 12, pia alijipatia USD 15,000 kwa ajili ya nauli ya tiketi ya ndege kwa wanachama 199 wa Karismatiki.

  Mshitakiwa amekana mashitaka yote na amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

  Mahakama ilimtaka mshitakiwa kuwasilisha Sh milioni 100 au hati ya mali yenye thamani hiyo pamoja na wadhamini wawili wanaotambulika kisheria.

  Pia alimtaka mshitakiwa kuwasilisha pasi yake ya kusafiria na kwamba haruhusiwi kutoka nje ya Mkoa wa Dar es Salaam.

  Kesi hiyo itatajwa tena Julai 6 mwaka huu.

  0 0


  ASALAM ALEIKUM,
   SHUGHULI YA AROBAINI YA MAREHEMU BABA YETU MPENDWA, ABDUL CISCO OMAR MTIRO ITAFANYIKA TAREHE 15 JULAI 2017 NYUMBANI MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM BAADA YA SWALAH YA ADHUHOUR.
  ITATANGULIWA NA MKESHA USIKU WA 14 JULAI 2017 INSHALLAH.
   KUFIKA KWAKO NDIO UKAMILIFU WA SHUGHULI HII.
  TAFADHALI UKIPATA UJUMBE HUU MJULISHE NA MWENZAKO

  Wa Bilah Toufik,
  Omar Mtiro

  0 0


  MKURUGENZI wa Kampuni ya Travel House Global, Sojan Varghese amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu tuhuma za kujipatia USD 88,012 kwa mahujaji. Imedaiwa kuwa, fedha hizo alipewa kwa ajili kuwakatia tiketi ya ndege mahujaji zaidi ya 119 wa Chama cha Karismatiki Katoliki Tanzania.
  Varghese anadaiwa kuchukua fedha hizo kutoka kwa John Ngotty kwa ajili ya usafiri wa mahujaji hao waliokuwa wakitaka kusafiri kuelekea nchi za Roma, Italia  na Israeli kwa ajili ya hija.
  Mwendesha mashtaka, wakili wa serikali, Adolph Mkini amedai Desemba 23, 2016 ofisi za Kampuni hiyo zilizopo mtaa wa Jamhuri, mshitakiwa alijipatia USD 7,012 kutoka kwa Ngotty fedha ambazo ni kwa ajili ya nauli ya kupata tiketi ya ndege kwa Wakarismatiki 119 kutoka Dar es Salaam kwenda Roma na Israeli. Desemba 23, mwaka jana mshitakiwa huyo alijipatia USD 9,500 kupitia hundi namba 000005 kutoka kwa Ngotty kwa ajili ya kuwakatia tiketi ya ndege.
  Mbele ya Hakimu Mkazi,Wilbard Mashauri imedaiwa kuwa, Januari 11, Varghese alijipatia USD 9,500 kutoka kwa Ngotty kwa lengo la kutumika kununulia tiketi za ndege kwa mahujaji hao. Aidha mshtakiwa anadaiwa kujipatia USD 9,500 kwa hundi namba 000008 kutoka kwa Ngotty. Januari 31, mwaka huu, Varghese alijipatia USD 37,500 kutoka kwa Ngotty na Aprili 12, pia alijipatia USD 15,000 kwa ajili ya nauli ya tiketi ya ndege kwa wanachama 199 wa Karismatiki.
  Mshitakiwa amekana mashitaka yote na amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
  Mahakama ilimtaka mshitakiwa kuwasilisha Sh milioni 100 au hati ya mali yenye thamani hiyo pamoja na wadhamini wawili wanaotambulika kisheria.Pia alimtaka mshitakiwa kuwasilisha pasi yake ya kusafiria na kwamba haruhusiwi kutoka nje ya Mkoa wa Dar es Salaam.

  Kesi hiyo itatajwa tena Julai 6 mwaka huu.

  0 0
  0 0


  0 0
 • 06/24/17--00:45: Article 13


 • 0 0

  Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma 

  Serikali imewashauri wakazi wa Wilaya ya Malinyi mkoa wa Morogoro, kutumia njia mbadala kupata huduma za kibenki ikiwemo kupitia simu za mkononi yaani (simbanking) ya CRDB na Banking on the Wheel ya NMB iliyoko Mlimba kwa kipindi hiki ambacho mchakato wa kufungua matawi rasmi ya benki unaendelea. 

  Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Malinyi Dkt. Hadji Hussein Mponda (CCM), aliyetaka kujua ni lini huduma rasmi za kibenki zitaanzishwa katika wilaya ya Malinyi ama kama kulikuwa na mpango wa taasisi za fedha kuanzisha huduma za matawi ya benki yanayohamishika (mobile banking) wilayani humo.

  Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa, wilaya ya Malinyi ni moja ya wilaya ambazo zinanufaika na mfumo wa utoaji huduma kupitia mawakala wa Fahari Huduma (Malinyi SACCOS na Zidua Waziri Shop) zinazoendeshwa na benki ya ‘CRDB Bank’ ambapo wateja wanapata huduma za kibenki ikiwemo kufungua akaunti, kuweka na kuchukua fedha, kuomba mikopo na kupata ushauri wa huduma za kifedha. 

  “Gharama za kuanzisha na kuendesha tawi kuwa kubwa Benki ya NMB na CRDB zinaendelea na upembuzi yakinifu kwa ajili ya kufungua tawi katika wilaya ya Malinyi utakaotoa mwelekeo wa kufungua tawi au la, kwa sababu Tawi linatakiwa liwe endelevu na kujiendesha kwa faida”. Alisema Dkt. Kijaji.

  Dkt. Kijaji aliongeza kuwa Serikali inatambua umuhimu wa wananchi wa Tanzania kupata huduma za kibenki karibu na maeneo yao na kwamba huduma hizo lazima ziwe na faida kwa pande zote yaani kwa mabenki na wateja pia. 


  0 0

   Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti ,Omary Kumbilamoto akizungumza wakati akiwakaribisha wakazi wa kijiji cha Kauzeni Wilaya ya Kisarawe  katika Dua na futari aliyoiandaa kwa ajili ya wana kijiji hao katika kipindi cha mwezi hu mtukufu wa Ramdhani
   Bondia wa Zamani na Bingwa wa Dunia katika uzito wa kati ,Rashid Matumla akizungumza na wakazi wa kijiji cha Kauzeni kabla ya futari  iliyoandaliw ana Naibu Meya wa Manispaa Ilala.

   Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Kauzeni akisoma majina wakati wa Dua ya kuwasomea ndugu zao waliotangulia mebele ya haki
   Wazee na viongozi wa dini wa kijiji cha Kauzeni Wilayani Kisarawe wakioma dua kabla ya futari iliyoandaliwa na Naibu Meya wa jiji Omary Kumbilamoto
   Sehemu ya Wanakijiji wa kijiji cha Kauzeni wakipata futari ya pamoja na iliyoandaliw ana Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala.

  0 0

  Mkuu wa utafiti wa Kampuni ya Well Told Story, Dkt Anastasia Mirzoyants akitoa maelezo kwa washiriki wa Warsha iliyoandaliwa na  Mradi wa Shujaaz  iliyofanyika Hotel ya Uhuru mjini Moshi.
  Baadhi ya Vijana waliofanikiwa kuingia katika Kijiji cha Shujaaz wakionesha umahiri wao katika uimbaji ambapo pia walipata zawadi kutoka Shujaaz.
  Timu za watoto chini ya miaka 13 za Msimamo na Right to Play kutoka Dar es Salaam zikichuana katika mashindano ya East Africa Cup 2017 yanayofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya Moshi Ufundi.
  Katika Kijiji cha Shujaaz wakishiriki michezo mbalimbali ikiwemo ya kukimbia huku wakiwa ndani ya magunia.
  Kijiji cha Shujaaz kimekuwa kivutio kikubwa kwa vijana wanaoshiriki mashindano ya East Africa Cup 2017.
  0 0

  Taarifa tulizopokea hivi punde zinaeleza kwamba mmoja wa wanamuziki nguli nchini, Shaaban Dede, amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kupatiwa matibabu.


  Kwa mujibu wa msemaji wa Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA), Dede amelazwa wodi ya Mwaisela Namba 5 kitanda namba moj, ambapo wadau wa muziki wameombwa kwenda kumjulia hali huku wakimuombea apate nafuu haraka. Taarifa hiyo haikumesema Dede anasumbuliwa na matatizo gani.


  Shaaban Dede ni mwanamuziki mkongwe ambaye anajulikana kwa sauti yake tamu pamoja na tungo zilizosheheni kila aina ya ladha.


  Kwa ufupi Dede alizaliwa Mkoa wa Kagera mwaka 1954 ambako alianza kupenda muzikiakiwa bado mdogo kabisa na bendi yake ya kwanza kujiunga nayo ilikuwa ni ya TANU ambayo makazi yake yalikuwa Biharamulo, mjini Bukoba.
  “Mwaka 1974 alijiunga na Bendi ya Polisi na mwaka 1975 akajiunga na Tabora Jazz ambako alikaa kidogo kabla ya kuhamia 1976 nilihamia Dodoma Internationl Band mwaka 1976  ambako alidumu kwa miaka mitatu.

  Mnamo mwaka 1979 alijiunga na bendi ya Msondo wakati huo ikijulikana kama JUWATA JAZZ  ambako alidumu  mpaka mwaka 1982 alipoahamia Mlimani Park Orchestra wana SIKINDE ambako alikaa kwa mwaka mmoja kabla ya kujiunga na Bendi ya Bima a.k.a BIMA LEE. Mnamo  mwaka 1987 Deded alirudi tena Msondo ambako alikaa  kidogo na baadaye akahamia tena Sikinde. Hata hivyo mwaka 20111 akarejea tena Msondo ambako yuko hadi hii leo.

  Globu ya Jamii inamtakia apate nafuu haraka gwiji wa muziki Shaaban Dede. Tutaendelea kuwaletea taarifa za maendeleo yake kila zitapopatikana.
  0 0

   Mkuu wa Jeshi la Polisi nchi IGP Simon Sirro akikagua gwaride la maofisa wa uhamiaji wakati wa sherehe za kumaliza kozi namba moja kwa maofisa hao, sherehe zimefanyika leo chuo cha polisi moshi CCP. Kozi hiyo ilihusisha warakibu wasaidizi (ASP), wakaguzi wasaidizi, meja, sajenti na koplo.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchi IGP Simon Sirro akiwa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji CGI Dkt. Anna Peter Makakala wakati wa sherehe za kumaliza kozi namba moja kwa maofisa hao. Sherehe zimefanyika leo Chuo cha Polisi Moshi (CCP). Kozi hiyo ilihusisha warakibu wasaidizi (ASP), wakaguzi wasaidizi, meja, sajenti na koplo.

  0 0


  0 0

  Katika kuelekea sikukuu ya Eid el-Fitri, E-FM Radio imetoa zawadi kwa wasikillizaji wake kama ilivyo tamaduni yake ya kutoa kwa jamii, ambapo wasikilizaji 10 kutoka jijini Dare s salaam waliofanikiwa kusikiliza redio na kujibu maswali kuhusu kampeni ya Kapu la sikukuu wameondoka na makapu yalioyo sheheni vitu mbalimbali ikiwemo vyakula muhimu  kwa ajili ya  sikukuu hiyo. 
  Tukio hilo limefanyika leo siku ya Jumamosi ya tarehe 24/06/2017 katika ofisi zao zilizopo Kawe – beach.DSTV nao waliongezea nakshi kwenye kapu kwa kuwazawadia washindi wa makapu ya sikukuu ving`amuzi vyao na kuwapa kifurush cha mwenzi moja bure. Zoezi hili litaendeshwa pia kwa washindi kutoka jijini Mwanza ambako EFM Radio inasikika kupitia masafa ya 91.3. washindi hao watajipatia zawadi zao za Kapu la sikukuu siku ya Jumapili tarehe 25/06/217 kwenye ofisi za DSTV Kenyata road Mwanza.
  Washindi wa makapu katika picha ya pamoja wakisubiria kukabidhiwa makapu yao
  Makapu ya Eid el-Fitri yakiwa yamesheheni vyakula mbalimbali
  Washindi wa makapu katika picha ya pamoja wakisubiria kukabidhiwa makapu yao
  Mwigizaji mashuhuri  Riyama Ally ambaye ni balozi wa Dstv akimkabidhi mshindi Benjamin n osha kapu lake la Eid el-Fitri’

  Meneja wa vipindi wa Efm radio Dickson Mponela akimkabidhi moja ya washindi Rebeca Lukule kapu lake la Eid Al Fitri

older | 1 | .... | 1765 | 1766 | (Page 1767) | 1768 | 1769 | .... | 3348 | newer