Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

MUONEKANO WA MWEZI MWANDAMO WA IDDI

$
0
0
Dk.  N. T. Jiwaji
ntjiwaji @ yahoo . com
Mwisho wa mwezi huu, watu watavutwa kuangalia angani jioni upande wa magharibi baada ya magharibi kutafuta Mwezi mwandamo ambao utakamilisha ibada ya kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani.  Wengine watavutiwa na sayari mbili ambazo pia zinang’aa angani mara baada ya giza kuingia.  Sayari hizo si zingine ila ni sayari maarufu za Mushtarii (Jupiter) na Zohali (Saturn). 
Mushtarii inang’aa vikali karibu na utosi, na Zohali inaonekana upande wa mashariki karibu na upeo.  ingawa Zohali siyo kali sana, mwanga wake unavuta na ni wa kutulia, mbali na nyota ambazo humeremeta.
Wanaoamka mapema kwa ajili ya sala ya alfajiri na kwenda kazini wanashangazwa na sayari nyingie inayong’aa kwa ukali sana jirani na upeo wa mashariki kabla ya Jua kuchomoza. Syari hiyo ni Zuhura (Venus) ambayo kwa sasa ina jina la Nyota ya Alfajiri, na baada ya miezi kadhaa sayari hiyo hiyo itakuwa Nyota ya Jioni itapohama nafasi na kuingia katika anga ya Jioni.
Kwa wakati huu Mwezi upo katika anga ya alfajiri jirani na upeo wa mashariki kabla ya Jua kuchomoza.  Kila mwezi, Mwezi husogea nyuzi 12 angani, kwa hiyo ifikapo tarehe 23 Juni, Mwezi utakuwa bado upo anga ya alfajiri upande wa mashariki  na hilali yake inatambulika ukiangalia vizuri.  Siku ya pili, yaani tarehe 24, Mwezi utakuwa umesogea kiasi cha kuhamia upande wa pili wa Jua na kuingia katika anga ya jioni.  

Wakati wa machweo jioni ya tarehe 24 Juni, Mwezi utakuwa mchanga sana, na hilali yake nyembamba kiasi cha asilimia 0.4% tu na nyuzi 7 jirani na upeo wa magharibi.  Pamoja na hiyo, kwa vile anga ya magharibi huwaka sana wakati wa machweo kwa hiyo hilali changa hufunikwa kabisa ndani ya uang’avu wa anga.  Kwa vile Mwezi unazidi kushuka upeoni muda unavyosogea ni vigumu sana kuuona Mwezi mwandamo siku hiyo.

Lakini jioni ya Jumapili tarehe 25 Mwezi utakuwa umesogea juu kwa nyuzi 12 zaidi, na kufikia nyuzi 20 juu ya upeo wa magharibi. Hilali ya Mwezi pia utatanuka kufikia asilimia 3.3% kwa hiyo kutakuwa na muda wa kutosha kabisa kuuona Mwezi hilali, mara giza litapoingia.

Kutafuta Mwezi mwandamo inabidi kuwa katika eneo lenye uwazi upande wa magharibi na kuanza kuangalia dakika kumi au kumi na tano baada ya magharibi ili kupata anga lenye giza ya kutosha.  Kwa Dar es Salaam muda mzuri ni kuanzia saa 12:30 jioni, na upande wa pili wa Tanzania, sehemu za Kigoma, itakuwa baada ya saa 1:15 jioni.

MCHEZAJI WA KIKAPU ANAYEKIPIGA MAREKANI ATOA MAFUNZO KWA VIJANA NCHINI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mchezaji wa Mpira wa Kikapu wa Nchini Marekani wa ligi ya Chuo cha New Brunswick Alphaeus Kisusi  amedhamiria kuinua mchezo wa kikapu nchini kwa kuanza kuwafundisha vijana wa kuanzia miaka 12 katika viwanja vya  JMK PARK.
Kikusi aliweza kuondoka nchini mwaka 2012 na kwenda nchini Canada na kuendeleza kipaji chake cha mpira wa kikapu.
Kliniki  hiyo kwa vijana wa kike na kiume na itakuwa ni kwa siku tatu na inajulikana kama 'Shoes For Tanzania' ilianza jana na itamalizika kesho katika viwanja vya JMK Park.
Mchezaji wa Mpira wa Kikapu wa Nchini Marekani wa ligi ya Chuo cha New Brunswick Alphaeus Kisusi akiwa katika picha ya pamoja na vijana waliopo katika Kliniki ya mpira wa Kikapu inayoendelea katika viwanja vya JMK Park.\
Mchezaji wa Mpira wa Kikapu wa Nchini Marekani wa ligi ya Chuo cha New Brunswick Alphaeus Kisusi akitoa maelezo mbalimbali kwa vijana vijana waliopo katika Kliniki ya mpira wa Kikapu inayoendelea katika viwanja vya JMK Park.
Mchezaji wa Mpira wa Kikapu wa Nchini Marekani wa ligi ya Chuo cha New Brunswick Alphaeus Kisusi akitoa maelezo mbalimbali kwa vijana vijana waliopo katika Kliniki ya mpira wa Kikapu inayoendelea katika viwanja vya JMK Park. Picha na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.





UKUTANAPO ANA KWA ANA NA TEMBO MBUGANI, TULIA TULI.....

TANGAZO RASMI LA EID EL-FITRI KUTOKA BAKWATA

Jokate atoa zawadi ya Eid El Fitr kwa wajane na yatima wa taasisi ya Ahbaabul Khairiya ya mwanyamala B

$
0
0
Mwanamitindo maarufu nchini, Jokate Mwegelo akikabidhi misaada kwa Mwenyekiti wa Taasisi inayoshughulikia masuala mbalimbali ya Wajane na Watoto Yatima ijulikanayo kwa jina la Ahbaabul Khairiya, Ahmed Chebe ya Mwanayamala B jijini Dar es Salaam. Jokate ambaye pia ni Kaimu Katibu Hamasa na Chipukizi wa Umoja wa Vijana Tanzania (UVCCM) amebidhi kilo 250 za unga na mchele, mbuzi wawili, mafuta ya kupikia, nguo za watoto wa kike na wa kiume, mafuta yakupikia na nguo za watu wazima kwa ajili ya kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitr kwa faraja zaidi.

Mwanamitindo, Miss Tanzania namba mbili 2006 na mbunifu wa mavazi, Jokate Mwegelo ametoa sadaka ya sikukuu ya Eid El Fitr kwa taasisi ya wanawake wajane na watoto yatima ilijulikanayo kwa jina la Ahbaabul Khairiya cha Mwanayamala B jijini Dar es Salaam. Jokate ametoa zawadi hiyo kwa kituo hicho chenye jumla ya wajane 32 na watoto yatima 41 kama sehemu ya kuwafanya wajane na yatima hao kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitr kwa faraja zaidi.

Mrembo huyo ambaye pia ni Kaimu Katibu Hamasa na Chipukizi wa Umoja wa Vijana Tanzania (UVCCM) amebidhi kilo 250 za unga na mchele, Mbuzi wawili, mafuta ya kupikia, nguo za watoto wa kike na wa kiume, mafuta yakupikia na  nguo za watu wazima.

Amesema kuwa ameguswa na changamoto za kituo hicho ambacho kimefanya kazi kubwa kujua changamoto mbalimbali za wajane na watoto yatima wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

“Nimegushwa sana na kuamua kidogo nilichonacho kugawana na ninyi, sikukuu ya Eid El Fitr inakaribia na natarajia kila mmoja wetu atasheherekea kwa faraja zaidi, naomba mpokee msaada huu na matarajio yangu ni kuendelea kuwasaidia pindi ninapata nafasi,” alisema Jokate.

Mmoja wa wasanii wa luninga nchini, Juma Chikoka ambaye alikuwa katika makabidhiano hayo alitoa wito kwa jamii kuunga mkono juhudi za Jokate za kutatua changamoto mbalimbali katika jamii. Mwenyekiti (Amiri) wa Taasisi hiyo, Ahmed Shebe alimshukuru Jokate kwa msaada huo na kuomba wadau mbalimbali kujitokeza kutatua changamoto hizo.

“Taasisi inahudumia wajane wa mikoa ya Pwani na Dar es Salaam, wapo wengine Chalinze na Bagamoyo mbali ya hapa wa jijini, tunajitahidi kutafuta michango sehemu mbalimbali ili kuweza kuondoa changamoto hizi, hata hivyo bado hatujafikia lengo, tunahitaji msaada kwa wasamaria ili kuwapa faraja zaidi,”

“Kuna wajane wanaosaidiwa kulipia kodi yay a nyumba na watoto yatima wanaolipiwa ada, hatuna uwezo mkubwa wa kufanya hivyo na zaidi fedha za msaada zinatokana na michango yetu,” alsema Shebe.
Mmoja wa wajane wa Taasisi ya Ahbaabul Khairiya, Nawili Saidi akibeba nguo mbalimbali zilizotolewa na Mwanamitindo, Jokate Mwegelo kwa ajili ya kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitr.
Jokate akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kituo cha Ahbaabul Khairiya pamoja na wajane na yatima.
Wanawake wajane wakimshukuru Jokate mara baada ya kutoa msaada katika kituo hicho.

DAR CONSTRUCTION EXPO 2017 # SAVE THE DATE

$
0
0

Our team distributing our "Save the Date Fliers" for the Dar Construction Exhibition Expo and East Africa Building Summit 2017 which will take place on the 17th and 18th of August along the Furniture Expo 2017. Almost 2000 of our fliers have been distributed all over Dar es Salaam! Do not plan to miss this one! GET YOUR TICKET NOW!
http://construction.mikonoexpogroup.com/index.php

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0

SIMU.TV: Wadau wa zao la tumbaku mkoani Tabora wameshauri kutonunuliwa kwa tumbaku inayozalishwa katika mashamba yanayo tumikisha watoto wadogo. https://youtu.be/b1I7Tse_JqI

SIMU.TV: Wakazi wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida wameipongeza serikali kwa jitihada inayochukua kutatua kero za wananchi wilayani humo. https://youtu.be/z-Ze93BPHbA

SIMU.TV: Watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu mkoani Iringa wamemshukuru rais Dr John Pombe Magufuli kwa kuwapa zawadi ya sikukuu ya Idd. https://youtu.be/tfBxLLvgwYY

SIMU.TV: Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam limesema litaimairisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya jiji siku ya sikukuu ya Idd ili kukabiliana na uhalifu wa aina yeyote. https://youtu.be/UTKV7hho8AA


SIMU.TV: Mkurugenzi mkuu wa shirika la utangazaji TBC Dr. Ayoub Rioba amekutana na kufanya mazungumzo na balozi wa jamhuri ya watu wa Korea ya Kusini yenye lengo la kujenga mahusiano ya masuala mbalimbali. https://youtu.be/VMMEtxxi4RI

SIMU.TV: Kikosi cha jeshi la kujenga taifa JKT wilayani Mlale kimeanza ujenzi wa kiwanda kipya cha kusindika mahindi kinachotarajiwa kutumia zaidi ya shilingi milioni 250. https://youtu.be/mnAvTgHrDlE

SIMU.TV: Wahitimu wa mafunzo ya jeshi la kujenga taifa JKT operesheni Magufuli Makuyuni Mkoani Arusha wametakiwa kulienzi jina hilo kwa kufanya yale anayotekeleza Rais Magufuli ikiwemo kulinda rasilimali za taifa. https://youtu.be/A9WkRe9tlko

SIMU.TV: Kituo cha uwekezaji nchini TIC kitaanza kutoa vibali vya uwekezaji ndani ya siku tatu kuanzia mwezi julai ili kuharakisha uwekezaji wa viwanda nchini. https://youtu.be/09uRr5YVnvE

SIMU.TV: Waziri wa nchi ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Angela Kairuki amezitaka taaisi za umma kutangaza takwimu zao ili wananchi waweze kuzifuatilia. https://youtu.be/6mRLGRhXWzQ

SIMU.TV: Waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo Dr Haryson Mwakyembe amemtembelea nahodha wa Serengeti Boys Isa Abdi nyumbani kwao mjini Dodoma na kueleza kuridhishwa na maendeleo ya afya yake. https://youtu.be/Y2zj__BebXM

SIMU.TV: Klabu ya Yanga imesema inawarudisha wachezaji wake wote waliomaliza mikataba yao na timu hiyo kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao. https://youtu.be/gKf-g4R2AOk

TRA YAFUNGIA MADUKA YA WAFANYABIASHARA WASIOTUMIA MASHINE ZA EFD KARIAKOO

$
0
0
Maafisa wa Mamalaka ya Mapato Nchini (TRA) wameendelea  kufanya zoezi la ukaguzi wa maduka ya wafanyabiashara wanaouza bidhaa zao pasipo kuwapatia risiti za mashine za Kielektroniki (Efd) jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo imeendelea kufanyika katika eneo la Kibiashara la Kariakoo na itakuwa endelevu kuhakikisha wafanya biashara wanazingatia sheria, kanuni na taratibu za biashara katika mauzo ya bidhaa zao. 
Afisa wa Kampuni ya Yono Auction Mart na askari polisi wakisimamia zoezi la kuingiza ndani bidhaa za wafanya biashara walikutwa wakiendelea kutoa huduma ilhali awali walikutwa wakiuza bidhaa hizo pasipo kutoa risiti ya kielektoniki licha ya kuwa na mashine. Hatua ya ukamatwaji kwa wafanya biashara hao inatokana na kitendo cha kutokuitikia wito wa mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) wa kwenda kulipa faini baada kufanya kosa hilo. Kwa kosa hilo watalazimika kulipa kati ya shilingi milioni 3 mpaka 4 na nusu ili waruhusiwe kuendelea na biashara. 
Afisa wa Kampuni ya Yono Auction Mart (kulia) na mmoja wa wafanya biashara wakifunga makofuli kwenye duka la madera katika mtaa wa Congo Kariakoo Dar es Salaam Juni 22 2017 baada ya kukutwa duka hilo likiendelea kutoa huduma ilhali awali walishakutwa wakiuza bidhaa hizo pasipo kutoa risiti ya kielektoniki licha ya kuwa na mashine ya risiti za kieletroniki (Efd). Hatua ya kuwakamata wafanyabiashara wa jinsi hiyo ilitokana na kitendo cha kutokuitikia wito wa mamlaka ya Mapato Nchini wa kwenda kulipa faini baada kufanya kosa hilo. Kwa kosa hilo watalazimika kulipa kati ya shilingi milioni 3 mpaka 4 na nusu ili waruhusiwe kuendelea na biashara.
Wafanya biashara waliokamatwa eneo la Kariakoo Mtaa wa Congo Dar es Salaam, kwa kosa la kutoitikia wito wa mamlaka hiyo kwenda kulipia faini ya utoaji wa huduma pasipo kutoa risiti za kielektoniki licha ya kuwa na mashine wakifunga duka lao walipokamatwa na maofisa wa TRA Juni 22 2017. Kwa mujibu wa sheria za nchi wafanyabiashara hao watatakiwa kulipa kati ya shilingi milioni 3 mpaka 4 na nusu ili waruhusiwe kuendelea na biashara. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA


WAZIRI MWAKYEMBE AMKABIDHI WAZIRI SIMBACHAWENE KAMUSI KUU YA KISWAHILI LEO MJINI DODOMA

WAZIRI MWAKYEMBE AMTEMBELEA NA KUMJULIA HALI NAHODHA WA SERENGETI BOYS

KAMBI YA VIJANA NA WATOTO 'ARIEL CAMP 2017' YAFUNGWA JIJINI MWANZA

$
0
0
Keki maalum kwa ajili ya washiriki wa kambi ya Ariel mwaka 2017.
Mgeni rasmi,Dk. Silas Wambura,Mkurugenzi wa Miradi AGPAHI, Dk. Safila Telatela na watoto walioshiriki Kambi ya Ariel wakikata keki.
Mgeni rasmi / Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Dk. Silas Wambura akimlisha keki mtoto.
Picha ya pamoja: Mgeni rasmi na wafanyakazi wa AGPAHI.
Picha ya pamoja: Mgeni rasmi na watumishi wa afya waliombatana na watoto na vijana kutoka mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Geita.


BALOZI ADADI AWAFUTURISHA WAKAAZI WA JIMBONI KWAKE

$
0
0


Mbunge wa Jimbo la Muheza  Balozi Adadi Rajabu (kushoto) akiwa na wageni waalikwa wakipiga dua kabla ya kuanza kufuturu katika futari aliyoandaa nyumbani kwake.
Mbunge wa Jimbo la Muheza(CCM) Balozi Adadi Rajabu akiwa na wananchi wa Jimbo lake wakipata futari
 Mwandishi wa AZAM TV mkoani Tang,Mariam Shedafa kulia na Anna Peter wakipata futari. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

DG WA PPF WILLIAM ERIO AUNGANA NA WAFANYAKAZI KUHUDUMIA WAWANACHAMA WA MFUKO KWENYE KILELE CHA WIKI YA UTUMISHI

$
0
0

 Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (kushoto), akismikiliza Mwanachama wa Mfuko huo, Bw.Clemence Munisi, aliyefika kitengo cha huduma kwa wateja ili kuhudumiwa wakati wa kilele cha wiki ya utumishi Makao Makuu ya PPF Barabara za Samora/Morogoro jijini Dar es Salaam, Ijumaa Juni 23, 2017.


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio, aliiacha ofisi yake na kujiunga na kitengo cha Huduma kwa Wateja cha Mfuko huo Makao Makuu ya PPF barabara ya Samora na Morogoro jijini Dar es Salaam ambapo alifanya kazi ya kuwahudumia wateja.
 Bw. Erio akizungumza na baadhi ya wanachama waliofika kitengo cha huduma kwa wateja cha Mfuko huo ili kupaiwa huduma.

WAZIRI KAIRUKI AKIZUNGUMZA MARA BAADA YA KUFUNGA MKUTANO WA KIMATAIFA KUHUSU VITA DHIDI YA RUSHWA

WANAWAKE WAJITOKEZA UCHAGUZI TWFA, WAPITISHWA

$
0
0
Wanawake wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Chama cha Mpira wa Miguu Wanawake (TWFA) katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Julai 8, mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Msomi Wakili George Mushumba leo Juni 23, aliongoza kikao cha Kamati ya Uchaguzi kupitia majina ya wagombea walioomba kugombea nafasi mbalimbali.
Mara baada ya kikao hicho, amewataja wanaowania nafasi mbalimbali kwenye mabano kuwa ni Amina Karuma (Nafasi ya Uenyekiti); Rose Kissiwa (Makamu Mwenyekiti); Somoe Ng’itu (Katibu) na Theresia Mung’ong’o (Katibu Msaidizi ).
Nafasi ya Mweka Hazina, kwa mujibu wa Mushumba inawaniwa na Hilda Masanche ilihali nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu TFF, inawaniwa na Salma Wajesso na Zena Chande huku Ujumbe wa Kamati ya Utendaji TWFA waliopitishwa ni Triphonia Temba, Jasmine Badar, Chichi Mwidege na Mwamvita Kiyogomo.
Musumba ametangaza majina hayo ya wagombea waliostahili au waliotimiza taratibu za uchaguzi kwa mujibu wa katiba na kanuni za uchaguzi za TWFA. 
Kinachofuata kwa sasa ni kwamba Juni 26 na 27, 2017- Kupokea pingamizi kati ya saa 4:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni katika ofisi za TFF.

Juni 28, 2017- Kamati ya Uchaguzi kupitia pingamizi kama zimewasilishwa.

Juni 29, 2017-  Kamati kutoa majumuisho ya pingamizi kama ziliwasilishwa na wadau.

Juni 30, 2017-  Usaili kwa wagombea waliotangazwa.

Julai 01, 2017- Kutangaza majina ya wagombea waliopitishwa

Julai 02, 2017-Kamati kupokea rufaa

Julai 03, 2017-  Kamati kupitia rufaa kama zimewasilishwa.

Julai 04, 2017   Kamati kutangaza orodha ya mwisho ya wagombea.

Julai 04 hadi 07, 2017 - Wagombea kufanya kampeni kwa kuzingatia maadili.

Julai 08, 2017- Uchaguzi Mkuu wa TWFA
.……………………………………………………………………………………………..
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO NA CHAMA CHA MAWAKALA WA FORODHA TANZANIA WAZINDUA RASMI KONGAMANO LA GLOBAL LOGISTICS SUMMIT –TANZANIA 2017

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (katikati) akiongea katika mkutano na waandishi wa habari kuelezea Tanzania itakavyokuwa wenyeji wa kuandaa Kongamano la ‘Global Logistics Summit 2017’ linalotarajia kufanyika Agost 23-26, 2017 jijini Dar es Salaam. Kulia ni Rais wa Chama cha Wakala wa Forodha Tanzania (Taffa), Stephen Ngatunga na kushono ni makamu wa Rais wa Chama cha Wakala wa Forodha Tanzania (Taffa), Edward Urio.
Kwa habari kamili BOFYA HAPA

WAZIRI MWAKYEMBE AMKABIDHI KAMUSI KUU YA KISWAHILI WAZIRI SIMBACHAWENE LEO MJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dk.Harrison Mwakyembe akitia saini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ofisi za TAMISEMI mjini Dodoma.Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe.George Simbachawene.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dk Harrison Mwakyembe akimkabidhi Kamusi kuu ya Kiswahili  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe.George Simbachawene leo Mjini Dodoma. 
Picha na Daudi Manongi - MAELEZO,DODOMA.

Kwa Simu Toka London: WAAFRIKA TUACHE KUWANYANYAPAA WENYE ULEMAVU

$
0
0
Na Freddy Macha
Mshindi wa picha bora duniani ya wenye hali ya Mtindio wa Ubongo (Down Syndrome) , Samwel Mwanyika alikuwa London mwezi Juni 2017 kupokea tuzo ya "Stephen Thomas Award". 
Baada ya sherehe kijana alikaribishwa na kutunukwa pia na Balozi wetu Dk Asha Rose Migiro. Siku moja kabla ya kurudi nyumbani , akiwa mitaani, alipiga piano, St Pancras, Kings Cross,... na hapo tukazungumza naye na Mama yake. Hebu sikiliza uone kazi waliyo nayo wazazi kupambana kuendeleza maisha ya watu wenye hali hii, Afrika.

INTRODUCING KENNEDY ENTERTAINMENT kampuni ya KITANZANIA ya sanaa na burudani Sweden

Mkutano wa Sita wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar waahirishwa

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  ameonya kwamba kuanzia sasa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitowavumilia Madaktari wanaofanya uzembe wakati wa kutoa huduma za Afya kwa Wananchi wanafika Hospitalini kupata huduma za matibabu.
Alisema Serikali haitosita kumfukuza kazi mara moja Daktari ye yote atakayebainika kufanya uzembe  wa makusudi bila ya kujali jina au sifa alizonazo Daktari husika.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa onyo hilo wakati akitoa hoja ya kuahirisha Mkutano wa Sita wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar lililojadili Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 2017/2018 kwenye ukumbi wa Baraza hilo Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Alisema dhamira ya Serikali kupitiA Wizara husika ya Afya ni kutoa huduma bora  yaliyobainishwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakati wakichangia Hotuba ya Wizara ya Afya.
Balozi alisema yapo malalamikombali mbali ya kiutendaji hasa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja yaliyojitokeza  ambayo huleta kero na maudhi kwa Wananchi wanaofika kupata huduma za matibabu.
Alitanabahisha wazi kwamba  baadhi ya Madaktari wamekuwa na tabia sugu ya kutotekeleza wajibu na majukumu yao wakati wengine wakipenda kutumia lugha chafu zinazowavunja moyo wagonjwa.
Alisema hatua hiyo inakera na kuchukiza Wananchi kutokana na kufikia huduma zinazotolewa kamwe hazilingani na fedha nyingi zinazotolewa na kugharamiwa na Serikali kwa kila Mwezi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitahadharisha kwamba vipo vifaa kufanyia uchunguzi kwa wagonjwa ambavyo kufanyiwa hujuma kwa makusudi ili wahusika wawaelekeze wagonjwa  kwenda kwenye Hospitali zao au zile wanazopewa baghshishi.
Alisema kitendo hicho kisichokubalika si cha haki kufanyiwa wagonjwa ambao wengi wao ni maskini na baadhi yao hutoka masafa ya mbali kama Vijijini kufuata huduma za matibabu Hospitali za rufaa.
Akizungumzia migogoro ya ardhi  Zanzibar licha ya Serikali kuanzisha Kamisheni ya  ardhi kwa lengo la kuodnosha migogoro hiyo kupitia Mamlaka ya Ardhi Balozi Seif alisema bado tatizo hilo halijapatiwa ufumbuzi kutokana na baadhi ya Watu hawajali kufuata sheria.
Alisema hivi sasa Kamisheni ya Ardhi ipo katika hatua za kutayarisha Sera mpya ya Ardhi, kuweka usimamizi imara wa Ardhi pamoja na upangaji wa matumizi bora ya Ardhi.
Balozi Seif alieleza kwamba Serikali kufuta maeneo yote ya Ardhi ili yarudi Serikalini na kupangwa upya.
Alifahamisha kwamba kuanzia sasa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitomvumilia mtu ye yote ambae atasababisha migogoro ya Ardhi hata kama ni Kiongozi au Mwananchi wa kawaida.
Baraza la Wawakilishi limeahirishwa hadi asubuhi ya Jumatano ya Tarehe 27 Septemba Mwaka huu wa 2017.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiufunga Mkutano wa Sitai wa Baraza la Tisa laWawakilishi Zanzibar uliokuwa ukijadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2017/2018 katika Ukumbi wa Baraza hilo uliopo Chukwani nje kidogo ya Kusini mwa Mji wa Zanzibar.
 Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Baadhi ya Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia Hotuaba ya Balozi Seif  katika Baraza la Wawakilishi Chukwani.
 Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakichukuwa dondoo kwenye  Hotuba ya kufungwa kwa  Mkutano wa Sita wa Baraza la Tisa la Wawakilishi iliyotolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani.

 Wa kwanza kulia ni  Mh. Simai Mohammed Said Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu. Mh.Suleiman Sarahan Said Mwakilishi wa Jimbo la Chake chake na Mwakilishi wa Kuteuliwa Ikulu Mheshimiwa  Ahmeda Abdulwakil.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zuberi Ali Maulid akitoka  barazani baada ya kuahirishwa Mkutano wa Sita wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar lililojadili Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 2017/2018 kwenye ukumbi wa Baraza hilo Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images