Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110019 articles
Browse latest View live

GREEN BIRD SCHOOL IN MWANGA, KILIMANJARO REGION, NOW ENROLLING


MUFTI WA TANZANIA AWASILI MKOANI KILIMANJARO KWA SWALA YA EID EL FITRI

$
0
0
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubery Ali amesema kwamba mwenye mamlaka ya kutangaza mwezi ni ya Mufti Mkuu baada ya kushauriana na Kamati ya Mwezi. Baada ya Mufti kujiridhisha ndipo Bakwata huutangazia Umma kuhusu kuandama kwa mwezi.  
Hivyo basi Mufti wa Tanzania amesema jana mjini Moshi kwamba leo Jumamosi Juni 24, 2017 kamati ya mwezi itaendelea kufuatilia kuandama kwa mwezi na ikiwa utaandama watautangazia umma kuwa Jumapili itakua Eid El Fitr na ikiwa hautoonekana basi itabidi kukamilisha siku 30 za mfungo wa Ramadhan na Eid kuswaliwa Jumatatu In Shaa Allah.

Mufti wa Tanzania,Sheakh Aboubakary Zubeiry Ali akiwa katika lango la kutokea eneo la watu mashuhuri (VIP) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) alipowasili jana mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya Swala ya Idd El- Fitr inayotaraji kufanika kitaifa mkoani humo.
Mufti wa Tanzania ,Sheakh Aboubakary Zubeiry Ali akiwa na viongozi pamoja na waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kuwasili mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya wanawake wa Dini ya Kiislamu walipofika kwa ajili ya kumpokea Mufti wa Tanzania,Sheikh Aboubakary Zubery Ali.
Mufti wa Tanzania Sheik Aboubakary Zubeiry Ali akiwasili katika mmoja wa misikiti iliyopo wilayani Hai kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la Msingi. 
Mufti wa Tanzania,Sheakh Aboubakary Zubeiry Ali  akifungua kitambaa katika kuweka jiwe la Msingi kuashiria kuendelea kwa ujenzi wa jengo hilo litakalotumika kama Madrasa.


VODACOM WATOA MSAADA KWA WAZEE NA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU ZANZIBAR

$
0
0
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais sharia, Utumishi wa Umma na Utawala bora Zanzibar, Khamis Juma Maalim(wapili kushoto) pamoja na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu(kushoto) wakiwakabidhi boksi la tende wazee wasiojiweza wa mjini Zanzibar ikiwa ni moja ya msaada na zawadi zilizotolewa na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya wazee hao pamoja na watoto yatima ili waweze kusherehekea sikukuu ya Ramadhani kesho kutwa,Mfuko huo wa kusaidia jamii ulitoa vyakula mbalimbali na mbuzi kwa wazee hao na watoto waishio katika mazingira magumu wa mjini humo jana.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais sharia, Utumishi wa Umma na Utawala bora  Zanzibar,Khamis Juma Maalim(kushoto) na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu (wapili kushoto) wakiwakabidhi mbuzi wazee wasiojiweza wa mjini Zanzibar ikiwa ni moja ya msaada na zawadi zilizotolewa na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya wazee hao pamoja na watoto yatima ili waweze kusherehekea sikukuu ya Ramadhani kesho kutwa, Mfuko huo wa kusaidia jamii ulitoa vyakula mbalimbali vya kula kwa wazee hao na watoto waishio katika mazingira magumu jana.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais sharia, Utumishi wa Umma na Utawala bora  Zanzibar,Khamis Juma Maalim (kushoto) akiwakabidhi mafuta ya kula  watoto waishio katika mazingira magumu wa mjini Zanzibar kwa niaba ya Vodacom Tanzania Foundation  ikiwa ni moja ya zawadi zilizotolewa na mfuko huo kwa ajili ya watoto hao pamoja na wazee kusherehekea sikuu ya Ramadhani kesho kutwa, Mfuko huo wa kusaidia jamii ulitoa vyakula mbalimbali  na mbuzi kwa wazee hao na watoto waishio katika mazingira magumu jana,Anaeshuhudia wapili toka kushoto ni na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu.
 Meneja biashara wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon akiwagawia mafuta ya kula baadhi ya watoto waishio katika mazingira magumu wa mjini Zanzibar kwa ajili ya sikukuu ya Ramadhani itakayofanyika kesho kutwa, Msaada huo ulitolewa na Vodacom Tanzania Foundation.
Mtoto aishio katika mazingira magumu wa mjini Zanzibar, Bakari Juma akipokea mafuta ya kula toka kwa mfanyakazi wa Vodacom Tanzania,Glory Mtui kwa ajili ya sikukuu ya Ramadhani itakayofanyika kesho kutwa, Mfuko wa kusaidia jamii wa kampuni hiyo”Vodacom Tanzania Foundation”ulitoa msaada wa vyakula mbalimbali kwa watoto hao na wazee wanaoshi katika mazingira magumu mjini humo jana.

WAZIRI MWAKYEMBE ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MATENGEZO YA PITCH(SEHEMU YA KUCHEZEA) KATIKA UWANJA WA TAIFA.

$
0
0
Na Lorietha Laurence WHUSM.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe ameridhishwa na maendeleo ya ukarabati wa eneo la kuchezea mpira (picth) la Uwanja wa Taifa wakati wa ziara yake leo Jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza  katika ziara hiyo ya kukagua hatua iliyofikiwa katika matengenezo ya uwanja huo   Waziri  Mhe.Dkt.  Mwakyembe amesema kuwa amefurahishwa na hatua ya awali ya ukarabati na anatarajia mabadiliko makubwa  zaidi baada ya hatua zinazofuata kukamilika .

 “Nimefurahishwa na mabadiliko niliyoyaona katika hatua hii ya awali naamini ukarabati utakapokamilika milango itakuwa wazi kwa mechi za kimataifa ikiwemo mashindano ya AFCON yanayoratajiwa kufanyika nchini kwetu  mwaka 2019” alisema Dkt.Mwakyembe

Aidha aliongeza kwa kusema kuwa Serikali ipo katika mkakati wa kuhakikisha viwanja vingine vikiwemo vya mikoani  vinafanyiwa ukarabati ili kuboresha sekta ya michezo nchini.

Waziri Dkt. Mwakyembe ameushukuru uongozi wa SPORTPESA kwa kuonyesha ushirikiano wa karibu na Serikali katika kuhakikisha inaweka mchango wake  katika michezo kwa kukarabati sehemu ya kuchezea mpira (picth) ya Uwanja wa Taifa pamoja na vifaa mbalimbali vilivyotolewa katika kuhakikisha kazi hiyo inakamilika.

Naye Mkurugenzi wa Utawala Na Utekelezaji kutoka SPORTPESA Bw.Tarimba Abbas ameeleza kuwa kampuni yao imefanya hivyo ikiwa ni njia ya kuonyesha uzalendo wa kupenda na kuthamini vya nyumbani.
“Hatua hii ni ya awali baada ya mechi ya Everton na Gorimahiya mnamo Julai 13 mwaka huu  hatua itakayofuata ni ya   kuondoa nyasi zote  na kuotesha mpya ambazo zitachukuwa miezi mitatu kuwa sawa” alisema Bw.Tarimba.

Uwanja wa Taifa ulianza matengenezo ya eneo la kucheze (pitch) rasmi katikati wa mwezi wa sita lengo ni kuhakikisha nyasi zilizochakaa zinaondolewa na kuwekwa nyasi mpya zitazodumu zaidi ya miaka 10 .
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe(mwenye miwani) akisikiliza  maelekezo kutoka kwa  Mkurugenzi  Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo  Bw. Alex Nkenyenge (wa Tatu kulia) alipotembelea uwanja wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam. 
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (wa kwanza kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo  wa Wizara hiyo Bw. Alex Nkenyenge (katikati) alipokuwa akiwatambulisha vijana ambao ni Maafisa kilimo (wenye makoti)  leo Jijini Dar es Salaam , mwingine ni  Mkurugenzi wa Utawala  na Utekelezaji kutoka SPORTPESA Bw.Tarimba Abbas(mwenye shati jeupe).
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akipata maelekezo kuhusu mbegu za nyasi mpya kutoka kwa Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius  Mgaya leo Jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kutembelea uwanja huo.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akionyeshwa mashine zinazotumika katika ukarabati wa picth katika uwanja wa Taifa kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Alex Nkenyenge (aliyechuchumaa), katikati ni Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius  Mgaya na kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala  na Utekelezaji kutoka SPORTPESA Bw.Tarimba Abbas  leo Jijini Dar es Salaam .

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akielezwa jambo kuhusu matumizi    mashine ya kuchorea mistari kutoka kwa Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius  Mgaya(aliyeinama) na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Alex Nkenyenge  leo Jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kutembelea uwanja huo. picha na Lorietha Laurence WHUSM).

WAZIRI KAIRUKI AFUNGUA SEMINA YA TAKWIMU HURIA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki akizungumza na wadau wa takwimu wakati wa semina ya Takwimu Huria iliyofanyika katika ukumbi wa COSTECH jijini Dar es Salaam. Semina hiyo iliandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Benki ya Dunia Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akizungumza na wadau wa takwimu wakati wa semina ya Takwimu Huria iliyofanyika katika ukumbi wa COSTECH jijini Dar es Salaam. Semina hiyo iliandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Benki ya Dunia Tanzania.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Huduma za Umma na Utendaji kutoka Benki ya Dunia Tanzania akizungumza na wadau wa takwimu wakati wa semina ya Takwimu Huria iliyofanyika katika ukumbi wa COSTECH jijini Dar es Salaam. Semina hiyo iliandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Benki ya Dunia Tanzania.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki akielezea umuhimu wa takwimu kwa waandishi wa habari mara baada ya kufungua semina ya Takwimu Huria iliyofanyika katika ukumbi wa COSTECH jijini Dar es Salaam. Semina hiyo iliandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Benki ya Dunia Tanzania.

MAFUNZO YA SIKU TANO KWA MADAKTARI YALIYOANDALIWA NA WCF YAFUNGWA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akimkabidhi Dkt.Kezia, cheti cha ushiriki wa mafunzo ya tathmini ya ajali na majeraha kwa mfanyakazi aliyeumia wakati akitekeleza majukumu yake mahala pa kazi, wakati wa kilele cha mafunzo ya siku tano kwa madaktari kutoka hospitali za umma na binafsi za jijini Dar es Salaam. Jumla ya madaktari 70 kutoka hospitali 35 walishiriki.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MAFUNZO ya siku tano kwa madaktari yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), ili kuwajengea uelewa wa namna ya kufanya tathmini ya ugonjwa na ajali kwa mfanyakazi aliyepata madhara mahala pa kazi yamemalizika kwa washiriki kutunukiwwa vyeti.

Mafunzo hayo yaliyofunhga na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba makao makuu ya Mfuko huo, jingo la GEPF barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam, Juni 23, 2017, yaliwaleta pamoja madaktari 70 kutoka hospitali mbalimbali za umma na binafsi jijini Dar es Salaam.

Mafunzo hayo yaliyogusa maeneo mbalimbali pia yaliwawezesha madaktari hao kujifunza Muongozo mpya unaohusu namna ya kufanya tahmini kabla ya kumlipa fidia stahiki Mfanyakazi aliepata madhara mahala pa kazi.

Akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw Masha Mshomba, alisema kuwa ni iani ya Mfuko kuwa Madaktari hao wamefaifika na mafunzo hayo na yatawezesha ufanisi katika kjutoa huduma hizo kwa wafanyakazi waliopata magonjwa au kuumia wakati wakiwa kazini.
Dkt.Benjamin Najimu Mohammed, akizungumz kwa niaba ya madaktari wenzake. "Nia ya mafunzo haya ni kwenda kuwasaidia watanzania wenzetu kwa niaba ya wenzangu napenda kuushukuru Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, kwa kutambua umuhimu wa ushiriki wetu katika mafunzo haya ili hatimaye kuwasaidia walengwa ambao ni watanzania wenetu." Alisema Dkt. Mohammed kutoka hospitali ya Kairuki ya Mikocheni jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

SSRA yaadhimisha wiki ya utumishi wa umma kwa kutoa elimu kwa wadau

$
0
0
Mkurugenzi wa uhusiano na uhamasishaji Bi Sarah Kibonde Msika akiwasikisha maada ya hifadhi ya jamii wakati wa kikao  kwenye wiki ya utumishi wa umma kilichofanyika jana katika Ofisi za SSRA jijini Dar es Salaam.
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) wamekutana na maafisa Habari wa serikali katika maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma ili kuwaongezea ujuzi ili kuongeza ufanisi kwenye kazi zao.
Baadhi ya maafisa Habari wa serikali pamoja na wadau mbalimbali wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) wakifuatilia mada wakati wa maadhimisho ya wiki ya utumishi.
                      Mkurugenzi wa uhusiano na uhamasishaji Bi Sarah Kibonde Msika (kushoto aliyekaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa Habari wa serikali pamoja na wadau mbalimbali wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA)  baada kumaliza semina ya wiki ya utumishi wa umma.

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA YA KILWA YAFANYA ZIARA KATIKA KISIWA CHA SONGO SONGO

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai (Kushoto) akizungumza na Meneja Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi Songas katika kisiwa cha Songo Songo, Andrew Hooper (kulia) kutoka Kampuni ya Pan African Energy. Mkuu wa Wilaya ya Kilwa aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya katika ziara yake juzi. 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Zablon Bugingo akizungumza na Meneja Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi Songas kutoka Kampuni ya Pan African Energy, Andrew Hooper wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama walipotembelea Kisiwa cha Songo Songo kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hizo kijijini hapo.
Meneja Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi katika Kisiwa cha Songo Songo, Andrew Hooper (katikati) kutoka Kampuni ya Pan African Energy akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai namna mitambo ya kuchakata Gesi inavyofanya kazi wakati wa ziara yao walipotembelea chumba maalumu (Control room) katika mitambo ya Gesi Songas iliyopo katika kisiwa hicho juzi. 

MAVUNDE ATOA RAI KWA BENKI NA TAASISI ZA FEDHA KUSOGEZA HUDUMA ZAO VIJIJINI ILI KUWAHUDUMIA WAKULIMA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde, akizungumza wakati wa uzinduzi wa benki ya Microfinance Bank PLC katika kata ya Mngeta,Wilaya ya Kilombero,Mkoani Morogoro.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde, wa kushoto  akiwa katika uzinduzi wa benki ya Microfinance Bank PLC katika kata ya Mngeta,Wilaya ya Kilombero,Mkoani Morogoro.


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde amezitaka benki na Taasisi za Fedha kusogeza huduma zao katika maeneo ya Vijijini ili kuwafikia watanzania wengi ambao wanajihusisha na shughuli za uzalishaji mali kama vile kilimo na Ufugaji.


Mavunde alitoa rai hiyo jana wakati wa uzinduzi wa benki ya Yetu Microfinance Bank PLC katika kata ya Mngeta,Wilaya ya Kilombero,Mkoani Morogoro kwa kuzitaka Taasisi hizo za fedha zisaidie katika utoaji wa mikopo nafuu kwa wakulima ikiwemo mikopo ya fedha taslimu,mikopo ya zana za kilimo na mashine za uchakataji wa mazao kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali kupitia uchumi wa Viwanda.


Mavunde amewataka wananchi wa kata ya Mngeta kuitumia hiyo fursa kuboresha kilimo chao kwa kulima kwa njia za kisasa na pia kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya uchakataji mazao.


Aidha,Mkurugenzi Mtendaji wa Benki Bwana Millinga alimuelezea Naibu waziri kwamba wameshaanza mchakato wa kuwakopesha wakulima mashine za uchakataji wa mazao na watatanua wigo zaidi ili kuwafikia wakulima wengi zaidi.


MOTO WAATHIRI MIUNDOMBINU YA UMEME MKOANI RUKWA

$
0
0
NA MWANDISHI WA K-VIS BLOG
WATU wasiojulikana wamechoma msitu wa Kirando wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa ambao umeunguza miundombinu ya umeme ya Shirika la umeme Nchini TANESCO.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jioni hii Juni 24, 2017 na Kaimu Meneja Uhusinao wa TANESCO makao Makuu, Bi. Leila Muhaji, imesema, uharibifu huo mkubwa wa miundombinu umeathiri upatikanaji wa umeme kwa wateja wa maeneo ya Kirando na Kipili wanaopata huduma ya umeme ya njia ya msongo mkubwa wa umeme unaopita kwenye maeneo hayo.
“Mafundi wa TANESCO waliofika kwenye eneo hilo, wameshuhudia uharibifu mkubwa ambapo miundombinu ya umeme imeungua na kusababisha hasara kubwa.” Alisema Bi Leila katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Bi Leila amesema TANESCO inawaomba wananchi wote waishio kwenye maeneo hayo kutoa taarifa kwenye ofisi za TANESCO au kituo cha polisi kilicho karibu ili kuokoa miundombinu ya umeme kwa manufaa ya taifa.
Amesema, tayari vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na TANESCO wameanza msako ili kuwabaini wahusika ili sheria ichukue mondo wake.

Uharibifu mkubwa ambapo miundombinu ya umeme imeungua na kusababisha hasara kubwa na kuathiri upatikanaji wa umeme kwa wateja wa maeneo ya Kirando na Kipili wilayani Nkasi, mkoa wa Rukwa
 Afisa wa polisi akiwa eneo la tukio huku akishuhudia jinsi moto huo ulivyoathiri nguzo za umeme
Uharibifu mkubwa ambapo miundombinu ya umeme imeungua na kusababisha hasara kubwa wilayani Nkasi, mkoa wa Rukwa

YALIYOJIRI KATIKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI LEO June 24, 2017

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassa Azindua Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS)

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea kitabu cha picha kutoka kwa Kamishna wa Utalii Zanzibar Javed Jafferji wakati wa hafla ya futari iliyoambatana na uzinduzi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) jana Jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha kitabu cha picha alichokabidhiwa na Kamishna wa Utalii Zanzibar Javed Jafferji (kulia) wakati wa hafla ya futari iliyoambatana na uzinduzi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) jana Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ambaye pia alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue. 
 Mwanzilishi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS), Bw. Abdulsamad Abdulrahim akitoa maelezo kuhusu malengo ya jumuiya hiyo mbele ya mgeni rasmi Makamu Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, wakati wa hafla ya futari iliyoambatana na uzinduzi rasmi wa Jumuiya hiyo jana Jijini Dar es Salaam. Mwanzilishi huyo alitoa mchango wa shilingi milioni 25 kama mtaji wa kuanzia wa ATOGS. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiomba dua wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) jana Jijini Dar es Salaam, Mwanzilishi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS).Kutoka kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage na Mwanzilishi wa Jumuiya hiyo Bw. Abdulsamad Abdulrahim.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Jumuiya ya Watoa Huduma ya Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) mara baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliyoambatana na uzinduzi wa Jumuiya hiyo jana Jijini Dar es Salaam. Lengo la Jumuiya hiyo ni kushirikiana na Serikali katika kuwahamasisha wazawa kujihusisha na masuala ya gesi na mafuta ili kuongeza mnyororo wa katika sekta hiyo. Picha na Frank Shija - MAELEZO

MAGIC FM BAMIZA TOP 20 COUNT DOWN JUNE 24TH 2017

NMB yafuturu pamoja na wateja wake waliofunga mkoani Mbeya

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (tatu kushoto) akiteteta jambo na Shekh wa Mkoa wa Mbeya, Mohamed Ally Mwansasu wa (pili kulia)wakati wa hafla ya futari iliyo andaliwa na Benki ya NMB kwa ajili ya wateja wa NMB walio katika Mfungo wa Ramadhani Mkoa wa Mbeya. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Tughimbe mwishoni mwa wiki. Wengine katika picha ni maofisa wa Benki ya NMB. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker ( pili kulia) akitetea jambo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhairi Kidavashari mara baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliyo andaliwa na Benki ya NMB kwa ajili ya wateja wa NMB walio katika Mfungo wa Ramadhani Mkoa wa Mbeya. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Tughimbe mwishoni mwa wiki. Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa (kwanza kulia) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker wa (kwanza kushoto) wakati wa hafla ya futari iliyo andaliwa na benki ya NMB kwa ajili wateja wa NMB walio katika Mfungo wa Ramadhani Mkoa wa Mbeya. Hafla hii ilifanyika katika Ukumbi wa Tughimbe mwishoni mwa wiki. Katikati ni mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi NMB, Margaret Ikongo. Kaimu Mkurugenzi wa Wateja wadogo na wakati NMB, Abdulmagid Nsekela (pili kushoto) akiteta jambo na Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini –Badru Idd, wakati wa hafla ya futari iliyo andaliwa na benki ya NMB kwa ajili wateja wa NMB walio katika Mfungo wa Ramadhani Mkoa wa Mbeya. Hafla hii ilifanyika katika Ukumbi wa Tughimbe mwishoni mwa wiki.

BINTI WA MBARAKA MWINSHEHE, MUHTAJI, AKIWA MSANII MWALIKWA TWANGA PEPETA


RAIS MAGUFULI ATOA MKONO WA IDD KWA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA MALAIKA KIDS

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani Mhe. Filberto H. Sanga akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi ya sikukuu ya Idd El Fitri  kwa niaba ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Malaika Kids kilichopo Mkuranga leo.Kutoka kushoto ni Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Utawala na Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abdullrahaman Mdimu na Afisa Tarafa ya Mkuranga Clement Muya.
 Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Utawala na Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bw. Abdullrahaman Mdimu akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi ya sikukuu ya Idd El Fitri  kwa niaba ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Malaika Kids kilichopo Mkuranga leo. Mhe. Rais ametoa zawadi ya mchele kilo 150, mbuzi pamoja na mafuta ya kupikia lita ndoo mbili.Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria kutoka Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Mohamed Magati, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto H.Sanga na Afisa Tarafa ya Mkuranga Clement Muya.

 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, Filberto H. Sanga akimkabidhi zawadi ya shilingi elfu kumi mmoja wa watoto wanaolelea katika Kituo cha Malaika Kids wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi ya sikukuu ya Idd El Fitri  kwa niaba ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kilichopo Mkuranga leo. Mtoto huyo amepewa zawadi hiyo kufuatia kujibu swali la Mkuu wa Wilaya huyo lililotaka kufahamu watoto hao wanataka kuwa wakina nani katika maisha yao ambapo mtoto huyo alisema anataka kuwa Rais. Anayeshuhudia ni Meneja maarufu kama Baba Mlezi wa Kituo hicho James Kallinga.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, Filberto H. Sanga akiwakabidhi watoto wa Kituo cha Malaika Kids kilichopo Mkuranga zawadi ya sikukuu ya Idd El Fitri  kwa niaba ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo. Mhe. Rais ametoa zawadi ya mchele kilo 150, mbuzi pamoja na mafuta ya kupikia lita ndoo mbili.
 Mkuu wa Kituo cha Kulelea watoto cha Malaika Kids kilichopo Mkuranga, Pwani James Kallinga akitoa neon la shukrani kwa niaba ya watoto wa kituo hiyo mara baada ya kukabidhiwa zawadi za Idd El Fitri zilizotolewa na na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kituo hicho leo.  Kutoka kulia ni Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Utawala na Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bw. Abdullrahaman Mdimu, Afisa Tarafa ya Mkuranga Clement Muya na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, Filberto H. Sanga. Picha zote na Frank Shija – MAELEZO, Mkuranga.


MASHAURI 18 YA MADAI YA KODI YA ARDHI YENYE THAMANI YA BILIONI 1.1 YAWASILISHWAKWENYE BARAZA LA ARDHI NA NYUMBA WILAYA YA TANGA

$
0
0
 Mashauri 18 ya madai ya kodi ya ardhi yenye thamani ya shilingi bilioni 1.1 yamewasilishwa katika Baraza  la ardhi na nyumba  wilaya ya Tanga ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kuwabana wamiliki wa viwanja wanao kwepa kulipa kodi.
Akizungumza mara baada ya kuwasilishwa kwa mashuari hayo mwakilishi wa afisa ardhi msaidizi kanda ya kazikazini Thadeus Riziki amesema hatua ya kuwafikisha mahakamani wamiliki wa viwanja  hivyo ni kupata kibali kitakacho wezesha wizara kulipwa makusanyo ya madeni.
Amesema baada ya halmashauri kuwapelekea wamiliki hati ya madai na kushindwa kulipa hatua inayofuata ni kuwafikisha mahakamani ili kupata ridhaa ya kisheria ya kukamata mali za wadaiwa.
Kwa upande wake afisa ardhi mteule Halmashauri ya jiji  la Tanga Straton Thobias amesema katika mwaka wa fedha wa 2016/7 halmashauri imeweka lengo la  kukusanya kodi ya ardhi kiasi cha shilingi bilioni 2.5 ambapo hadi sasaimefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 2.3
Akizungumzia zoezi hilo mwanasheria ofisi ya kamishina wa ardhi  Rosemery Mshana amesema wamiliki wa ardhi wanatakiwa kilipa kodi bila shuruti na kwamba kinyume chake watafikishwa mahakamani  mujibu wa kifungu cha  50  cha sheria ardhi namba nne(4). H
abari kwa hisani ya blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
Mwakilishi wa Kamishna wa Ardhi Msaidizi Kanda ya
Kaskazini, Ardhi Mwandamizi Thadeus Riziki akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu Baraza la Ardhi Mkoani Tanga kupokeamashauri 18 yenye thamani ya Bilon 1.1 ambayo yamefikishwa kutokanawamiliki wa nyumba ,makazi na viwanda  kushindwa kulipa kodi ya ardhikwa wakati

 Afisa Ardhi Mteule Halmashauri ya jiji  la Tanga Straton Thobias akielezra mkakati wa  mwaka wa fedha wa 2016/7 halmashauri imeweka lengo la  kukusanya kodi ya ardhi kiasi cha shilingi bilioni 2.5 ambapo hadi sasaimefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 2.3
Mwanasheria wa  Ofisi ya Kamishina wa Ardhi Kanda ya Kaskazini  Rosemery Mshana akiwataka wamiliki wa ardhi wanatakiwa kilipa kodi bila shuruti na kwamba kinyume chake watafikishwa mahakamani  mujibu wa kifungu cha  50  cha sheria ardhi namba 4.

MICHUZI TV: WAKAZI WA MTAA WA MPAKANI MAGOMENI KAGERA WAOMBA WADAU KUSAIDIA UJENZI WA DARAJA

$
0
0
 Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mpakani Magomeni Kagera kata ya Ndugumbi, Shaaban Kawambwa akiwa amembeba mmoja wa watoto wakati akiwavusha kwenye daraja la mpakani lilalounganisha eneo la Kagera Ndugumbi na Tandale ambalo usalama wake ni mdogo kwa wavukaji hasa watoto wadogo, kama alivyokutwa na kamera yetu leo Jijini Dar es salaam.
 Mjumbe wa Mtaa huo akiendelea la zoezi hilo la kuwavusha watoto kama alivyokutwa na Kamera yetu leo.
Mmoja wa wakazi wa maeneo la Mpakani na Tandale akivuka kwenye daraja hilo kwa uangalifu na umakini mkubwa.

ZANZIBAR WATAHADHARISHWA NA KIPINDUPINDU WAKATI WA KUSHEREHEKEA EID EL-FITRI

$
0
0

Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar           
Wananchi Zanzibar wameshauriwa kuchukua tahadhari kubwa zaidi wakati wa sherehe za Edd el Fitri katika kujikinga na maradhi ya kipindupindu ili kuhakikisha maradhi hayo hayaongezeki na kuleta athari zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi Mmoja, Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt. Fadhil Mohamed Abdallah ametaka tahadhari zaidi iwe ni kuwadhibiti watoto ili kuhakikisha hawali ovyo hasa katika kumbi na viwanja vya Sikukuu.
Aliwanasihi wananchi wasiwe tayari kukigeuza kipindi cha sikukuu kuwa cha madhara kwao na kuwashauri wafanyabiashara kuwa wazalendo kwa wananchi wenzao kwa kuacha kufanya biashara za vyakula vilivyopikwa na juisi katika sehemu zisizoruhusiwa.
Alisema Wizara ya Afya imetoa mwongozo kuhusu biashara za vyakula vinavyoruhusiwa kuuzwa katika viwanja vya sikukuu ambazo ni bidhaa zilizotengenezwa viwandani.
Aidha alitaka familia ambazo zitapenda kuandaa chakula na kula nje ya nyumba zao katika sehemu za wazi kuhakikisha wanafuata masharti yote ya  afya ikiwemo kunawa mikono kwa sabuni kabla ya kuanza kula.
Akizungumzia hali halisi ya kipindupindu Zanzibar tokea kilipoanza wiki tatu zilizopita, Dkt Fadhil alisema wagonjwa 303 wamelazwa katika kambi ya Chimbuni na Gamba iliyopo Wilaya Kaskazini A ambapo wanne kati yao wamefariki.
Alisema hivi sasa kambi ya Chumbuni imebakiwa na wagonjwa nane wa kipindupindu na kambi ya Gamba haina mgonjwa hata mmoja kuanzia tarehe 8 mwezi huu.
Alitaja sababu kubwa ya vifo hivyo vya watu wanne vilitokana na upungufu mkubwa wa maji mwilini na chanzo chake ni kucheleweshwa kupelekwa katika kituo cha afya.
 Dkt. Fadhil alikiri kuwa hali bado haijawa ya kutisha hadi hivi sasa lakini kumejitokeza ongezeko la wagonjwa wa kipindupindu katika vijiji vya Bambi na Mpapa Wilaya ya Kati na wanafikiria kufungua kambi wakati wowote katika maeneo hayo iwapo hali  itaendelea kuwa hivyo.
Aliwasisitiza wananchi kuendelea kufuata masharti ya afya katika kupambana na Kipindupindu ikiwa ni pamoja na kuyatibu maji ama kuyachemsha kabla ya kunywa na kuhakikisha wanatumia vyoo na kukosha vizuri mboga za majani na matunda kabla ya kula.

DMF YATOA MKONO WA EID EL FITR KWA WAKAZI WA MAGOMENI KAGERA JIJINI DAR

$
0
0
Mratibu wa Matukio ya Kijamii wa Taasisi ya Doris Mollel, Alice Mwakatika (kulia) pamoja na Mkuu Msaidizi wa Kitengo cha Elimu wa taasisi hiyo, Rahma Amoud (wa pili kulia) wakikabidhi sehemu ya vyakula kwa Bi. Aisha Mohamed (kushoto) mkazi wa eneo la Mpakani Kata ya Ndugumbi, Magomeni Kagera jijini Dar es salaam ikiwa ni mkono wa Eid el Fitr kutoka Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Rehema, iliyofanyika leo Juni 24, 2017. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mpakani, Saleh Kawambwa.
Mkuu Msaidizi wa Kitengo cha Elimu wa Taasisi ya Doris Mollel, Rahma Amoud akikabidhi sehemu ya vyakula kwa wakazi wa eneo la Mpakani Kata ya Ndugumbi, Magomeni Kagera jijini Dar es salaam ikiwa ni mkono wa Eid el Fitr kutoka Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Rehema, iliyofanyika leo Juni 24, 2017. 
Mkuu Msaidizi wa Kitengo cha Elimu wa Taasisi ya Doris Mollel, Rahma Amoud akikabidhi sehemu ya vyakula kwa Bi. Ashura Nassor mkazi wa eneo la Mpakani Kata ya Ndugumbi, Magomeni Kagera jijini Dar es salaam ikiwa ni mkono wa Eid el Fitr kutoka Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Rehema, iliyofanyika leo Juni 24, 2017. Katikati ni Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mpakani, Shaban Kawambwa.
Mratibu wa Matukio ya Kijamii wa Taasisi ya Doris Mollel, Alice Mwakatika akimkabidhi mfuko wa sandarusi wenye vyakula mbalimbali Mtoto Biatha Shembilu (14)  ambaye ni mgonjwa wa moyo mkazi wa eneo la Mpakani Kata ya Ndugumbi, Magomeni Kagera jijini Dar es salaam ikiwa ni mkono wa Eid el Fitr kutoka Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Rehema, leo Juni 24, 2017.
Viewing all 110019 articles
Browse latest View live




Latest Images