Benki ya CRDB ndio benki yenye huduma bora Tanzania kuliko benki nyingine yoyote, imeendeleo kuonyesha kuwajali Watanzania ambapo Menejmenti na Wafanyakazi wa CRDB Bank Tawi la Azikiwe Premier, la jijini Dar es Salaam, wameadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika, kwa kuwakumbuka watoto wanaoishi katika mazingira magumu, kwa kuwatembelea watoto wanaotunzwa katika kituo cha Jeshi la Wokovu kwa kuwapelekea zawadi mbalimbali za mahitaji muhimu, na kuwadhamini baadhi yao kwa kuwafungulia akaunti, kuwachangia, kugharimia elimu zao, na kugharimia mahitaji yao.
Wafanyakazi wa CRDB BANK, tawi la Azikiwe Premier, wakikabidhi zawadi mbalimbali kwa watoto wanaotunzwa katika kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ilioadhimishwa na benki hiyo kwa wiki nzima sasa.
Mfanyakazi wa CRDB BANK, tawi la Azikiwe Premier, akikabidhi zawadi mbalimbali kwa watoto wanaotunzwa katika kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ilioadhimishwa na benki hiyo kwa wiki nzima sasa.
Mkurugenzi na wafanyakazi wa CRDB Bank, Tawi la Azikiwe Premier, kwenye picha ya pamoja na mtoto Mariam Stephen Jackson, aliyekuwa akiishi katika mazingira magumu. Marriam pia amefunguliwa akauti maalum ya watoto ya benki hiyo iitwayo Junior Jumbo,ambayo wafanyakazi wa Tawi hilo la Azikiwe Premier, wananchangia kugharimia elimu yake. Sherehe hiyo imefanyika wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Africa ilioadhimishwa na benki hiyo kwa wiki nzima sasa.
Mkurugenzi na wafanyakazi wa CRDB Bank, Tawi la Azikiwe Premier, wakiwa na keki ya mtoto Mariam Stephen Jackson, aliyekuwa akiishi katika mazingira magumu. Marriam pia amefunguliwa akauti maalum ya watoto ya benki hiyo iitwayo Junior Jumbo,ambayo wafanyakazi wa Tawi hilo la Azikiwe Premier, wananchangia kugharimia elimu yake. Sherehe hiyo imefanyika wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Africa ilioadhimishwa na benki hiyo kwa wiki nzima sasa.
Mkurugenzi wa CRDB Bank, Tawi la Azikiwe Premier, Fabiola Musula, na wafanyakazi wa tawi hilo, na wateja, wakionyesha fedha walizomchangia mtoto Mariam Stephen Jackson, aliyekuwa akiishi katika mazingira magumu. Marriam pia amefunguliwa akauti maalum ya watoto ya benki hiyo iitwayo Junior Jumbo,ambayo wafanyakazi wa Tawi hilo la Azikiwe Premier, wananchangia kugharimia elimu yake. Sherehe hiyo imefanyika wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Africa ilioadhimishwa na benki hiyo kwa wiki nzima sasa.