Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

Swala ya eid El fitri kufanyika siku ya jumatatu viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar - Alhad Mussa Salum

$
0
0
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salum amewatangazia waumini wa dini ya kiislam kuwa Swala ya eid El fitri itaswaliwa mnamo siku ya jumatatu Juni 26, 2017 katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam, ikiwa ni baada ya kukamilika mfungo mtukufu wa mwezi wa Ramadhani.

Sheikh Salum aliyazungumza hayo jana wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari, na amewataka na kuwaasa waumini wa kiislam kuhakikisha wanatekeleza mema yote kama waliyokuwa wakiyafanya katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumzia siku ya ibada hiyo muhimu kwa waislam wote ulimwenguni, Sheikh Salum alimesema katika viwanja vya mnazi wageni mbali mbali wanatarajiwa kuwepo, lakini pia mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ali Hassan Mwinyi.

TAARIFA KUTOKA BARAZA KUU LA WAISLAM TANZANIA (BAKWATA).

KIJIJI CHA SHUJAAZ CHAFUNGULIWA KATIKA MASHINDANO YA EAC 2017 MJINI MOSHI

$
0
0
.
Baadhi ya Wageni wakijiandikisha kabla ya kuingia katika kijiji hicho ambako kumekuwa kukitolewa mafunzo mbalimbali hasa ya Kilimo .
Mratibu wa Tafiti wa Mradi wa Shujaaz,Winnie Nyato akitoa tiketi kwa mmoja wa watoto waliotembelea kijiji cha Shujaaz .
Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma ,Mohamed Kombo anayejishughulisha na Kilimo cha matunda akizungumza na vijana waliofika katika kijiji cha Shujaaz kuona namna gani wanaweza kuhamasika na kuingia katika shghuli za Kilimo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

UN Tanzania Chief visits projects in Zanzibar

$
0
0
Focus: Water and Sanitation projectsto ‘Leave No one Behind’ The UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative, Mr. Alvaro Rodriguez visits the island in a continuation and expansion of UNDP-supported projectsin Unguja and Pemba. Marking his tenth visit to Zanzibar, the UN Chief made several stops in Unguja, to seeseveral water-access projects as well as an environmental conservation project. Mr. Rodriguez is also expected to visit schools in both Pemba and Unguja to assess their facilities ahead of an upcomingwater and sanitation project which will involve ten schools. 
The three-day field visit in Zanzibar is part of UN efforts to monitor projects and meet beneficiaries in communities. In Unguja, Mr. Rodriguez visited a USD 90,000 water project in KijwajuniConstituency, Zanzibar Town, where the lives of over 25,000 people have improved through the project which facilitates access to clean water. 
He later visiteda USD 50,000 UNDP-supported Community Based Conservation Project in Kajengwa, Makunduchi. The conservation project has helped over 15,000 people, mostly women, who previously depended on firewood for cooking. They now have access to more efficient cooking stoves. The project supported the community in planting over 100,000 trees in the area and established 200 beehives which have helped improve nutrition and provide additional income. UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative, Alvaro Rodriguez (front right) and Deputy Minister of Home Affairs and founder of Tanzania Youth Icon, Hon. Hamad Masauni join local community members in listening to a presentation on the first phase of the UNDP water project.The water and the conservation projects have been running for several years and now that the first phase have been successfully implemented, both projects will be scaled-up. Each project is set to receive USD 50,000 this year through the UNDP Small Grants Programme to begin implementation of phase two. On Friday and Saturday, the UN Chief will also visit a number of schools where UN agencies, namely UNICEF and UNDP, are set to begin Water, Sanitation and Hygiene (WASH) projects later this year. These WASH projects will cover ten schools. Of these ten schools,the ones that will be visited include Mkwajuni Secondary School in Kaskazini, Unguja and Wingwi Primary School in Micheweni District, Pemba. 

KATIBU MKUU WA CCM APIGA MARUFUKU WAGOMBEA KUUZIWA FOMU.

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana amepiga marufuku uuzaji wa fomu za uchaguzi kwa ngazi zote za uongozi ndani ya Chama.

Taarifa iliyosainiwa na Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu Rodrick Mpogolo kwenda kwa Makatibu Wakuu wa Jumuiya imeeleza kuwa kwa mwanachama yeyote aliyeuziwa fomu arejeshewe pesa yake.

ASKOFU MTEULE BLASTON GAVILLE WA KKKT DAYOSISI YA IRINGA KUANZA KAZI RASMI

$
0
0
Na Fredy Mgunda, Iringa.

KANISA la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa limesema maandalizi ya kumwingiza kazini askofu mteule litafanyika jumapili huku likimpongeza Rais Dkt John pombe Magufuli kwa utendaji kazi.

Katibu mkuu wa KKKT dayosisi ya Iringa Nayman Chavala ameyasema hayo leo
wakati akitoa taarifa Kwa wanahabari kuhusu maandalizi yaliyofikiwa ya sherehe kubwa ya kuwekwa wasifu kwa askofu mteule Mchungaji Blaston Gavile na msaidizi wake Mchungaji Himidi Saga.

Alisema kuwa sherehe za kumpa madaraka ya kuanza kufanya kazi kama askofu wa kanisa la KKT Jimbo la Iringa mchungaji Gavile na msaidizi wake Saga itafanyika jumapili ya june 25 mwaka huu majira ya saa 3 asubuhi kwenye viwanja vya shule ya msingi Gangilonga .

Kuwa ibada hiyo itaongozwa na askofu mkuu wa KKKT Dkt Frederick Shoo pamoja na askofu mstaafu Dkt Owdenburg Mdegella na kuwa kabla ya idaba kutakuwa na maandamano ya wachungaji na washarika yatakayoanzia usharika wa kanisa kuu hadi Gangilonga.

" Tunaomba wananchi wote na washarika kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo la kihistoria pia tunategemea kuwa na viongozi mbali mbali wa serikali na wageni mashuhuri kutoka ndani na nje ya Tanzania"

Chavala alisema maandalizi yote yamekamilika kwa ajili ya tukio hilo kubwa ambalo lilikuwa likisubiliwa kwa shauku kubwa .

Askofu Gavile amechukua nafasi ya aliyekuwa askofu wa kanisa hilo Dkt Mdegella ambaye alistaafu kwa heshima kubwa na kuacha heshima ya aina yake ndani ya KKKT .

Wakati huo huo Katibu huyo amempongeza Rais Dkt Magufuli kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya ya kuwatumikia watanzania kwa uadilifu mkubwa na kuwa kazi kubwa kwa watanzania ni kuendelea kumpa ushirikiano .

Kwani alisema kuwa hatua ya kuwabana wasio waadilifu pamoja na kupambana na wizi wa mchanga wa dhahabu (MAKINIKIA) ni hatua ya kupongezwa kwani suala hilo lilikuwa likiwanufaisha wachache huku Taifa likibaki patupu .

" Sisi kama kanisa tumekuwa tukimuombea kila wakati tena kwa kumtaja kwa jina na hatutachoka kuendelea kumuombea maana kazi anayoifanya ni ngumu ambayo silaha kubwa ni maombi "

Katibu mkuu KKKT dayosisi ya Iringa Nayman chavala akizungumza na wanahabari.

RAIS MAGUFULI ATOA MSAADA WA VITANDA,MAGODORO NA MASHUKA KATIKA HOSPITALI YA LEVOLOSI

$
0
0
Mbunge wa viti maalumu ccm Mkoa wa Arusha Catherine Magige akitoa nasaha mara tu baada ya kukabidhi msaada huo wa vitanda,magodoro na mashuka yaliyotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Picha ikionyesha wa kwanza kulia Mbunge wa viti maalum(CCM)Catherine Magige akikabidhi kwa niaba ya Rais John Magufuli msaada wa magodoro 25,mashuka 25 pamoja na vitanda 25 katika kituo cha afya cha Levolosi ,ambapo msaada wa vitu hivi umetolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni moja wapo ya ahadi zake alizozitoa katika kipindi cha kampeni ,katikati ni Mganga mkuu wa kituo cha Afya cha Levolosi Feksi Edward ,wa kwanza kushoto ni Mganga mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha Saimoni Chacha (picha na Woinde Shizza,Arusha)
Katibu wa UWT mkoa wa Arusha Fatuma Hassan akiwasalimia wananchi wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Fabian Daqarro akiongea na wananchi wa jiji la Arusha.

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA YA KILWA YAFANYA ZIARA KATIKA KISIWA CHA SONGO SONGO

$
0
0
 Meneja Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi katika Kisiwa cha Songo Songo, Andrew Hooper (kulia) kutoka Kampuni ya Pan African Energy akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai (Wapili kushoto) walipotembelea mitambo ya Gesi Songas iliyopo katika kisiwa hicho juzi.
 Ofisa Usalama wa Kampuni ya Pan African Energy  inayochakata na kusafirisha Gesi kutoka Kisiwa cha Songo Songo, Baraka Melchiory (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai (kushoto) kuhusu hali ya usalama na namna ya kujikinga na majanga pindi itokeapo itilafu katika mradi huo. Mkuu wa Wilaya aliambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya katika ziara yake kutembelea mradi wa Songas juzi.
 Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai (Kushoto) akizungumza na Meneja Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi Songas katika kisiwa cha Songo Songo, Andrew Hooper (kulia) kutoka Kampuni ya Pan African Energy. Mkuu wa Wilaya ya Kilwa aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya katika ziara yake juzi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI KUHUSU SIKUKUU YA EID EL FITR

$
0
0
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Advera John Bulimba

Taswira ya mradi mkubwa wa mtambo wa maji wa Ruvu juu uliopo Mlandizi mkoa wa Pwani

$
0
0
Taswira ya Mradi wa Upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu na ulazaji wa mabomba makuu kutoka Mlandizi hadi uliozinduliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli June 22, 2017 katika siku yake ya pili ya ziara ya kikazi ya siku tatu  mkoani Pwani.
 Muonekano wa juu wa mradi huo mkubwa
 Muonekano wa juu wa mradi huo

HIVI NDIVYO UKARIMU WA VODACOM ULIVYOWAFIKIA WATANZANIA

$
0
0
Vodacom Tanzania imefanikiwa kufikia Watanzania zaidi ya 20,000 katika msimu huu wa Ramadhan unaoelekea ukingoni ambapo jumla ya tende tani 4 zimegawiwa pamoja na maji chupa 25,000. Kampeni hiyo yenye lengo la ukarimu, ushirika na utoaji katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan na katika maisha ya kila siku hadi sasa imewafikia wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi Mtwara, Tanga na Zanzibar. Ukarimu huu wa Vodacom unakwenda sambamba na kuwapatia wateja kifurushi kinachowawezesha kupata Qaswida, Mawaidha, Hadith, Facebook yenye picha na kuzungumza usiku wanaposubiri daku BURE kabisa. Huduma hii pia inawapatia muda wa maongezi, SMS na kuwawezesha kupiga simu BURE wakati wakisubiri muda wa kula daku, kugawa tende pamoja na maji. Pia huduma hiyo inawakumbusha muda wa kuswali na kuwapatia Mawaidha na Hadith. Ili kujiunga na huduma hii mteja anapiga *149*01# kisha anachagua aina ya bando kulingana na uwezo wake wa kifedha, kuna bando linalodumu kwa saa 24 na lingine linadumu kwa siku 7.

WAHAMIAJI HARAMU 45 WAKAMATWA WILAYANI MKINGA

$
0
0
IDARA ya Uhamiaji Mkoani Tanga imewakamata wahamiaji haramu 45 kutoka nchini Ethiopia katika Kijiji cha Horohoro wilayani Mkinga mkoani Tanga kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria wakiwa shambani kwa wananchi wanakula mahindi kabla ya kutiwa nguvuni. 

Licha ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu hao lakini pia idara hiyo inamshikilia raia mmoja kutoka nchini Kenya ambaye ndio alikuwa akiwaongoza wahamiaji haramu hapa. 
Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, Crispin Ngonyani alisema wahamiaji haramu hao walikamatwa June 18 mwaka huu katika kijiji hicho baada kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema wa eneo hilo. 

Alisema wahamiaji haramu hao walikamatwa wakiwa porini katika jiji hicho wakati wakisafiri kuelekea nchini Afrika Kusini ambapo waligunduliwa na wananchi baada ya kufika mashambani mwao wakawakuta wanakula mahindi ndio walipotoa taarifa kwa askari wa Polisi wa Horohoro na hivyo wakaenda kuwakamata.

Aliwataja wahamiaji haramu hao kuwa ni Melesa Manesha, Asaf Erisid, Ashnif Agide, Mulugeta Menano, Demek Sorebeto, Samal Latbo, Temesgen Tefera, Tememi Juheri, Mubarc Lamago, Temesa
Kibemo, Haftamu Tumiso, Teshum Assfe, Yohanness Ayano na Daniel Abbate. 

Aidha Ofisa Uhamiaji huyo aliwataka wengine walio kamatwa kuwa ni Kibmam Abab,Temesgzeen Ayele,Akilu Abraham,Pxirose Makore,Munyasha Lombaso,Berekei Cezenzeni ,Detebo Erikato, Ayele Kebamo,Tamrat Mamo. 

Wengine waliokamatwa kuwa ni Saniel Wolde,Tomiot Deto Gem, Abeje Alemeyo, Ashenaf Waje,Tariko Dutamo,Birhanu Atso,Tesefaye Dena,Tekel Abush,Tesyfe Landu na Abdi Hassani. 

Kwa mujibu wa ofisa uhamiaji huyo aliwataja wengine kuwa ni Daafa Daimo,Getahun Zeleke,Yonas Liliso, Amanei Ashebo, Xesabo Womago,Isagay Tikie Mubarik Analo,Begaye Ganorem,Dawit Teso,Teshele Kemiso,Samweli Hyle na Tamasgen Sorsa. 

Alisema wahamiaji haramu hao wamefikishwa mahakamani jana kujibu tuhuma zinazowakabili akiwemo msindikizaji Mongela Kidhome ambaye ni Mkenya na mkazi wa mpakani mwa Kenya na Tanzania Horohoro. 

Hata hivyo aliwataka mawakala wa wahamiaji haramu kuacha mara moja vitendo vya kuwaingiza nchini kwani watakaobainika watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria kujibu tuhuma zinazowakabili.

SPIKA NDUGAI AKABIDHI VITABU VYA KUJIFUNZIA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI WILAYANI KONGWA

$
0
0
 Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza na wanafunzi wa Shule Secondari ya Banyibanyi iliyopo wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma, baada ya kuwapatia vitabu vilivyotolewa na Mtandao wa kuondoa umasikini.
 Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akimkabidhi vitabu Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Sejeli Ndg.Gerald Kagali ikiwa ni zawadi kwa Shule hiyo, Msaada uliotolewa na Mtandao wa kuondoa umasikini, tukio lililofanyika leo kijijini Mbande Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mtandao huo Ndg. Mungwe Athman.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya sekondari Banyibanyi  katika tukio lililofanyika leo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.

YALE YALEEE.......

MILIONI 110 ZATOLEWA KUSAIDIA HUDUMA YA MAJI KIKWAJUNI

$
0
0
 Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez,akifunga bomba la maji katika moja ya maeneo ambayo Mradi wa Maji Kikwajuni ushakamilika. UNDP wameahidi kuchangia   kiasi cha shilingi milioni 110 za kitanzania kufanikisha kukamilika kwa mradi huo katika maeneo yote ya jimbo hilo.
 Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez, akisadiana na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto), kumtwisha mkazi wa jimbo hilo ndoo ya maji wakati wa ziara ya ukaguzi wa maeneo ulikopitia Mradi wa Maji Kikwajuni. UNDP wameahidi kuchangia   kiasi cha shilingi milioni 110 za kitanzania kufanikisha kukamilika kwa mradi huo katika maeneo yote ya jimbo hilo.Kulia ni Katibu wa taasisi isiyo ya kiserikali ya TAYI inayosimamia mradi huo, Abdallah Ahmed Suleiman.
 Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez, akizungumza katika mkutano na wananchi wa eneo la Kikwajuni Mao, alipowatembelea baada ya kukagua maeneo unakopita Mradi wa Maji Kikwajuni ambapo aliahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 110 kupitia UNDP kukamilisha mradi huo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WIZARA YA AFYA YAKANUSHA TAARIFA ZA GAZETI LA HABARI LEO KUHUSU TAKWIMU ZA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

NEWS ALERT: aliyekuwa Mwanasheria Mkuu TBS ahukumiwa miaka mitano jela au faini ya Milioni 13.9

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Baada ya kuachiwa huru juzi na kukamatwa tena, leo aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Baptister Bitaho (54) amehukumiwa kulipa faini ya Sh milioni 13.9 au kifungo jela miaka mitano baada ya kusomewa upya mashtaka na kukiri.

Bitaho amefikishwa tena katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo asubuhi na kusomewa mashitaka nane likiwemo la kufanya kazi nchini bila kibali na kutoa taarifa za uongo.

Bitaho ambaye ni Raia wa Burundi, alifutiwa mashtaka yake, na baadae kukamatwa,  amesomewa hukumu hiyo,  na Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa.

Akisoma hukumu hiyo Nongwa amesema kuwa mahakama imesikiliza maombi ya pande zote mbili na kwamba katika kosa la kwanza hadi la saba mshitakiwa atatakiwa kulipa faini ya Sh laki tano au kifungo jela kuanzia miaka miwili hadi mitatu na kwamba kosa la nane mshitakiwa atatakiwa kulipa  faini ya Sh milioni 10 au kifungo jela miaka mitano.

Amesema, kwa taratibu zilizopo, baada ya mshitakiwa kukutwa na hatia anatakiwa kupelekwa Uhamiaji na kurudishwa nchini kwao ili aombe uraia wa Tanzania upya.

Kabla hukumu hiyo kusomwa, Wakili wa utetezi,  Aloyce Komba amedai kuwa mshitakiwa hakuwahi kuvunja sheria  ya kijinai kwani alikuwa mwaminifu na hakuwahi kutoa siri ya nchi licha ya ukimbizi wake.

Komba pia ameongeza kuwa, tangu mteja wake apate kashfa hiyo, ameathirika kiuchumi kwa kuwa alitakiwa kustaafu miaka sita ijayo  lakini sasa anakosa mapato yake.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Jafo akitaka kikundi cha DOYODO kuongeza ubunifu

$
0
0
Naibu Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (TAMISEMI)Mhe.Selemani Jafo amewataka vijana wa Taasisi ya Maendeleo ya Vijana Dodoma(DOYODO) kuongeza ubunifu ili waweze kuwa washindani katika soko la biashara kwa kutumia fursa ya  wahamiaji wanaokuja Dodoma.

Mhe.Jafo aliyazungumza hayo alipokuwa anakagua miradi mbalimbali ya taasisi hiyo mapema leo na kuwataka kuwekeza kwenye kilimo  kwa kuwa   wanafikilia kupata eneo lao wenyenye ni vyema  kupata hekari moja kwa ajili ya kilimo cha mboga mboga na matunda kwani kinalipa.

’’Kumekuwa na tabia ya vijana kuchagua kazi na baadhi yao kusubiri kupata ajira kutoka Serikalini lakini nyie mmetoa mfano badala ya kutegemea ajira, mmejiajiri na ntahakikisha baadhi ya wabunge wanakuwa wa kwanza kuja kununua matofali hasa kwa wale wanaojenga Dodoma ’’

“Nitaongea na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma ili mpatiwe milioni moja kutoka mfuko wa 5% ya makusanyo ya Manispaa ya Mapato ya vijana na milioni kumi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na mimi nachangia  kwa kununua matofali mia tano “Mhe.Jafo aliahidi.

Naye Afisa Mipango na Muhasibu wa DOYODO Elias Mbogo amesema taasisi inajipatia kipato chake kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo ada ya uanachama,tozo,miradi yao na misaada kutoka kwa wadau wa Taasisi. 

Taasisi ya DOYODO imesajiliwa kisheria mwaka 2002 na kuanza kufanya shughuli zake rasmi toka 2015 na miradi waliyonayo ni mradi wa matofali,tuition(elimu),ufundi chelehani na kukodisha ukumbi kwa ajili ya semina na sherehe mbalimbali.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari akiwataka vijana wa taasisi ya DOYODO kuwa mfano wa kuigwa Dodoma na nchi nzima katika kampeni yao ya kujiajiri wenyewe.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akiwasha mtambo wa kufyatulia matofali.
 Naibu Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akizungumza na Wanafunzi waliokuwa wanafundishwa masomo ya ziada(tution) katika ofisi ya DOYODO.


 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa taasisi ya DOYODO na Afisa Vijana kutoka Manispaa ya Dodoma alipokuwa anakagua miradi mbalimbali mapema leo ofisini kwao mjini Dodoma.

Mkono wa Iddi kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro

$
0
0
Katika kuelekea kusherehekea sikukuu ya eid El Fitri, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imetoa zawadi ya vyakula mbali mbali na vifaa vya elimu vyenye thamani ya takriban shilingi milion kumi na nne kwa vituo vinavyotunza na kulea watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Pichani Naibu Mhifadhi wa Ngorongoro Dr. Maurus Msuha akikabidhi zawadi hizo kwa vituo vya Shalom orphanage centre, Mwema Street Children na Imani Focus Foundation vilivyomo pembezoni mwa Hifadhi ya Ngorongoro katika Wilaya ya Karatu.

IGP SIRRO AZUNGUMZA NA WANANCHI WA MJI WA MOMBO MKOANI TANGA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akizungumza na wananchi wa Mombo mkoani Tanga jana wakati akiwa njiani kuelekea Mkoani Kilimanjaro. IGP amewataka wananchi wa mombo kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kudumisha amani na utulivu nchini. Picha na hassan mndeme-jeshi la polisi

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images