Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1761 | 1762 | (Page 1763) | 1764 | 1765 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro (kushoto) akizungumza na maafisa wakuu wa Jeshi la Polisi alipofanya kikao na maafisa hao akiwa kwenye ziara ya kikazi visiwani Zanzibar kabla ya kwenda kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar mheshimiwa, Ali Mohamed Shein. Kulia ni Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Hamdani makame. Picha na Hassan Mndeme.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya zanzibar alipokwenda kufanya kikao na kamati hiyo akiwa kwenye ziara ya kikazi visiwani Zanzibar. IGP alikwenda pia kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar mheshimiwa, Dk Ali Mohamed Shein. 
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya zanzibar alipokwenda kufanya kikao na kamati hiyo akiwa kwenye ziara ya kikazi visiwani Zanzibar. IGP alikwenda pia kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar mheshimiwa, Dk Ali Mohamed Shein. Picha na Hassan Mndeme.

  0 0

  Mtaalamu  kutoka Timu ya Everton Bw. Shane Mcgeown (kushoto) akitoa maelekezo ya matumizi ya  mashine ya kushindilia na kutoa uchafu kwa ajili ya kusafishia uwanja  kwa uongozi na maafisa wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  leo Jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Taifa.
   Mtaalamu  kutoka Timu ya Everton Bw. Shane Mcgeown (kulia) akionyesha   mashine ya kukatia majani  na  kusafishia uwanja  kwa uongozi na maafisa wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  leo Jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Taifa.
  Mtaalamu  kutoka Timu ya Everton Bw. Shane Mcgeown (Mwenye kofia) akionyesha  mashine ya kubebea uchafu  katika ziara ya kukagua vifaa vinavyoyumika katika ukarabati wa uwanja  kwa uongozi na maafisa wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  leo Jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Taifa .
  Mkurungezi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Yussuph Singo (kulia) akimpa mkono wa shukrani Mtaalamu wa Uwanja kutoka Timu ya Everton Bw. Shane Mcgeown (kushoto) baada ya kutoa maelekezo ya vifaa mbalimbali vya kutunza mazingira ya Uwanja wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Lorietha Laurence WHUSM).

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akizungumza na mmoja wa wazee waliofika kupatiwa huduma katika viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo ofisi nzima ya Manispaa hiyo imehamia viwanjani hapo kwa ajili ya kuhudumia watu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma katika wilaya hiyo.
   Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala , Edward Mpogolo akiwa na Naibu Meya wa Manispaa hiyo Omary Kumbilamoto wakitoa huduma kwa wadau waliofika kutaka msaada juu ya mambo yanayowakabili . Ofisi za Manispaa hiyo zimahamia hapo kwa muda kwa ajili ya kuhudumia watu, ikiwa ni sehemu ya mahadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma katika wilaya hiyo.
   Afisa mkaguzi  Msaidiz wa jeshi la Zima Moto , akitoa maelezo kwa  Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema wakati wa maonyesho ya wiki ya utumishi wa Umma yaliyofanyika katika Viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam.
   Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akizungumza na baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Ilala ambo wanatoa huduma kwa wananchi katika Viwanja vya mnazi mmoja .Picha na Hamphrey Shao waa Globu ya Jamii.KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii .


  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, Mbunge wa Singida Mashariki kupitia tiketi ya Chadema, Tundu Lissu alikamatwa baada kutolewa kwa amri ya kufanyika hivyo kutoka kwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum (ZCO).  

  MKUU wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Wilaya (OCCID), Yustino Mgonja ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu MKazi Godfrey Mwambapa wakati akitoa ushahidi wake kama shahidi wa nne katika kesi ya kutumia lugha ya uchochezi inayomkabili Lissu ilipokuja kusikilizwa.

  Akiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi, Mgonja amedai kuwa Juni 28, mwaka jana, ZCO Wambura alimpa maelekezo ya kumkamata Lissu kwa kosa la kutoa lugha za uchochezi katika Viwanja vya mahakama hiyo.

  Amedai, Juni 29 mwaka jana, majira ya mchana alienda nyumbani kwa Lissu maeneo ya Tegeta wilayani Kinondoni ambapo alimkamata na kumfikisha katika Ofisi za ZCO na kumkabidhi.

  Alidai kuwa, alipewa amri na ZCO kumkamata Lissu  na alifanya hivyo licha ya kuwa hakuwa na hati ya ukamataji kwa kuwa mamlaka yalikuwa yanamruhusu kufanya hivyo na kuwa mtu yoyote akifanya makosa ya jinai unaruhusiwa kukamata bila kuwa na hati. 

  Aliongeza kuwa, kumpinga Rais anapokosea sio kosa na kwamba tafsiri ya maneno aliyoyatoa ndio yamesababisha kukamatwa na kushitakiwa kwa kutumia lugha za kichochezi.

  Lissu anadaiwa kuwa Juni 28, mwaka huu, akiwa katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alitoa kauli za uchochezi kuwa, “Mamlaka ya Serikali mbovu ni ya kidikteta uchwara inahitaji kupingwa na kila Mtanzania kwa nguvu zote, “huyu diktekta uchwara lazima apingwe kila sehemu”. Kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi inaingia ndani ya giza nene.’’

  0 0

  Na Daudi Manongi, MAELEZO, DODOMA.

  Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu  imesema kuwa itaendelea kuelimisha jamii na wadau mbalimbali kuhusu mifumo,maudhui na taratibu za uridhiaji wa mikataba ili kufanya maandalizi stahiki kabla ya uridhiaji wa mikataba hiyo.

  Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi ,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde wakati akijibu Swali la Mhe.Ussi Pondeza Mbunge wa Chambani.
  “Nchi yetu inazo sheria mbalimbali zinazotambua na kusimamia maslahi ya wafanyakazi nchini wakiwemo wafanyakazi wa majumbani,wafanyakazi wa mahotelini na vyama vyao”,Aliongeza Mhe,Mavunde.

  Aidha Waziri Mavunde amewataka wafanyakazi nchini kutambua juhudi za Serikali za kulinda na kutetea haki na maslahi  ya wafanyakazi kupitia sheria,kanuni na taratibu zilizopo nchini.

  Amesema Serikali inaendelea kupitia kwa makini azimio lililofikiwa na Shirika la kazi la Umoja wa Mataifa mwaka 2011 linaotaka kila nchi mwanachama wa ILO kuwa na Sheria ya kuwalinda wafanyakazi wa Mahotelini na Majumbani.

  “Ni kweli kuwa Mwaka 2011,Nchi wanachama wa Shirika la Kazi Duniani ikiwemo Tanzania zilipitisha mkataba wa kimataifa kuhusu kazi za Staha kwa wafanyakazi wa Majumbani,ambapo hadi sasa nchi zilizoridhia ni 23 kati ya nchi 189 na kwa upande wa Afrika zimelizia nchi mbili tu kwa iyo bado tunaendelea kuupitia ili kufanya maandalizi ya kuridhia”,Aliongeza Mhe.Mavunde.

  Pamoja na hayo Waziri Mavunde amesisitiza kuwa Tanzania Bara ina sheria zake za kazi ambazo zinawahusu wafanyakazi wote  ikiwemo wafanyakazi wa mahotelini na majumbani ambazo zinalinda haki zao.

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi ,Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 22, 2017. 

  0 0


   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akipokea vitabu kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa kuondoa umasikini, Ndg. Mungwe Athman (katikati) kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tukio lililofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, wa pili kushoto ni Meneja wa Mtandao huo Ndg. Peter Yobwa na Wageni wengine ni Wajumbe wa tume ya Utumishi wa Bunge wakiongozwa na Mhe. Mussa Zungu(nyuma kulia).
   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akikata utepe ili aweze kufungua  boksi lenye vitabu alivyokabidhiwa na Mtandao wa kuondoa umasikini kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katikati ni Mwenyekiti wa Mtandao huo Ndg. Mungwe Athman, wa pili kushoto ni Meneja wa Mtandao huo Ndg. Peter Yobwa na wengine ni Wajumbe Mbali mbali wa tume ya utumishi wa Bunge wakiongozwa na Mhe. Mussa Zungu (nyuma kulia).
   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akionyesha moja ya kitabu alichokabidhiwa na Mtandao wa kuondoa umasikini, vitabu walivyokabidhi kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kushoto ni Mwenyekiti wa Mtandao huo Ndg. Mungwe Athman na kulia ni Mjumbe wa tume ya Utumishi ya Bunge Mhe. Peter Msigwa, nyuma yake pia ni Wajumbe wa tume ya utumishi wa Bunge ambao ni Mhe. Mussa Zungu na Mhe. Mary Chatanda.
   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza baada ya makabidhiano ya vitabu kwa Bunge  la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Msaada uliotolewa na Mtandao wa kuondoa umasikini, kulia kwake ni Mwenyekiti wa Mtandao huo Ndg. Mungwe Athman, tukio hilo pia lililouzuliwa na Wajumbe wa tume ya Utumishi wa Bunge katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akisalimiana na  Mwenyekiti wa Mtandao wa kuondoa umasikini, Ndg. Mungwe Athman (kushoto)kabla ya Makabidhiano ya vitabu kwa Bunge  la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , tukio lililofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

  0 0

  Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza na waandhi wa habari (hawapo pichani) kuhusu ushiriki wa Benki hiyo katika maonyesho ya Biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam maarufu kama “Maonyesho ya Sabasaba”, yanayotarajiwa kuanza Juni 28, 2017 mpaka Julai 08, 2017 katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Kurasini, Jijini Dar es Salaam.

  Benki ya CRDB imeahidi kushiriki kikamilifu na tutatoa huduma zote za kibenki kupitia “mobile branch” ambalo ni tawi kamili linalotembea na lenye uwezo wa kutoa huduma zote za kibenki za kutoa, kupokea na kutuma fedha, kununua fedha za kigeni na kupokea hundi, Hivyo Benki hiyo inawakaribisha wateja wake wote kutembelea tawi hilo.
  Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu .

  0 0

  Wasanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Harmorapa na Juma Nature (Sir Nature) watapamba tamasha la muziki Raha ya Rocky City lililopangwa kufanyika wakati wa sikukuu ya Eid El Fitr kwenye ukumbi wa Buzuruga Plaza.

  Mbali ya Sir Nature na Harmorapa ambao wanatamba na wimbo wa Kiboko ya Mabishoo, muandaaji nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, P-Funk naye atashiriki katika tamasha hilo lililoandaliwa na kituo cha redio nyota ya kanda ya Ziwa, 102.5 Lake FM.
  Mkurugenzi Mkuu wa 102.5 Lake FM, Doreen Noni amesema kuwa maandalizi ya tamasha hilo lililopangwa kuanza saa 12.00 jioni yamekamilika na mashabiki wa muziki wa kizazi kipya watarajie burudani safi kutoka kwa wasanii mbalimbali mbali ya Sir Nature na Harmorapa.

  Doreen alisema kuwa Nature na Harmorapa watafanya onyesho la kwanza ‘live’ kutambulisha wimbo wa Kiboko ya Mabishoo kwa mara ya kwanza kwa mashabiki wa muziki huo wa mkoa wa Mwanza na mikoa ya jirani.

  “Harmorapa pia atatambulisha nyimbo zake mbalimbali kama, Nundu, Usigawe Pasi wakati Nature atawakumbusha mashabiki wake wa zamani kwa nyimbo nyota za zamani kama Ugali, Hili Game, Utajiju, Naja, Hakuna Kulala, Inaniuma Sana, Ubinadamu Kazi, Kighetogheto na Mgambo.

  “Tamasha hili ni sehemu ya kuadhimisha sikukuu ya Eid El Fitr, tumeandaa burudani mbalimbali ambazo hazita wachosha mashabiki, lengo ni kuleta msisimko wa aina yake kwa mashabiki wa Kanda ya Ziwa,” alisema Doreen.

  Alifafanua kuwa Lake fm imedhamiria kutoa nafasi kwa wasanii wa mkoa wa Mwanza hivyo kutakuwa na wasanii mbalimbali wa Mwanza ambao nao ni moto wa kuotea mbali. Wasanii hao ni Jimmy Chansa, Future JNL, kundi la Lakezonia, Ngeta na Dogo D, Abu Mkali, vile vile kutakua na makundi ya kudans TYT na MCB pia jopo la warembo lukuki kutoka 21plus models na Blackfox models.

  Mbali na hayo, pia kutakuwa a burudani safi ya muziki kutoka Ma-DJ wa 102.5 Lake FM. Ma DJ hao deejays hao ni DJ Ten Ten, DJ Jabir, DJ Basta na DJ Steve wa Mitindo.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali haitarudi nyuma kamwe katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi nchini mpaka hapo vitendo hivyo vitakapokoma.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati anafungua Mkutano wa Kimataifa wa ngazi ya Juu wenye lengo la kubadilishana uzoefu katika mapambano dhidi ya Rushwa katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa vita ya kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi ni kipaumbele cha kwanza katika Serikali ya awamu ya Tano na wale wote wanaowezesha, kunufaika na kuhusika na vitendo hivyo wataendelea kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo nchini.

  “Kupambana na rushwa ni jambo la msingi na muhimu kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo endelevu katika nchi yeyote Duniani,” Amesisitiza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya awamu Tano chini ya Uongozi Shupavu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli inaendelea kukaza kamba katika mapambano dhidi ya rushwa ambayo kwa muda mrefu sasa yamechangia kurudisha nyuma juhudi za Serikali za kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

  Amesema Serikali ya Tanzania inalenga kufikia kipato cha kati na kuimarisha uchumi wa viwanda hadi ifikapo mwaka 2015 hivyo malengo hayo yatafanikiwa haraka iwapo tu vitendo vya rushwa vitakomeshwa katika ngazi zote nchini.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa zamani wa nchi ya Georgia Mhe. Mikheil Saakshvili akihutubia na kutoa uzoefu wa nchi yake dhidi ya mapambano dhidi ya rushwa wakati wa ufunguzi Mkutano wa Kimataifa wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu  Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassanakiangalia kitabu kinachoelezea mapambano dhidi ya rushwa na Rais wa zamani wa nchi ya Georgia Mhe. Mikheil Saakshvili (kushoto) wakati Ufunguzi Mkutano wa Kimataifa wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa , Rais huyo wa zamani alitoa uzoefu wake na wa nchi yake katika kupambana na rushwa.
  Sehemu ya Wajumbe waliohudhuria ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa , Rais huyo wa zamani alitoa uzoefu wake na wa nchi yake katika kupambana na rushwa.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI 

  0 0

   Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akikabidhi zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori kwa Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 Julai, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Waziri Maghembe alimshukuru Balozi huyo kwa ushirikiano na misaada mbalimbali aliyoitoa, yeye binafsi na nchi yake katika kusaidia kuendeleza sekta ya uhifadhi nchini.
  Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (katikati) akifurahia zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori alivyopewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 Julai, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi.  Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akikabidhi zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori kwa Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 Julai, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAWA, Martin Loibooki.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro amewataka viongozi na watumishi wote nchini kuzingatia nidhamu kama msingi wao wa utendaji kazi pamoja na kanuni na maadili ya utumishi wa umma ili utumishi wao uweze kuwa mzuri.

  Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo alipokutana na watumishi Mkoani Singida na kusikiliza matatizo, kero, changamoto pamoja na kupata maoni ya namna ya kuboresha utumishi wa umma kama sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma nchini.

  Amesema kila mtumishi anapaswa kufanya kazi kwa bidii na kwa nidhamu ya hali huku akiwasisitiza viongozi hasa wa watumishi wa umma kuwasikiliza watumishi wao pale wanapotoa maoni yao bila kuyapuuzia au kuwakatisha tamaa kwa vitisho.

  “Ukiwa kiongozi unapaswa uweze kuishi na kila aina ya mtu, kuna watumishi wengine hawawezi kufichaficha mambo ukikosea wanakusema bila kupepesa maneno, wengine ni waoga hawawezi kukueleza wazi ila wanatumia mbinu mbali mbali, ukiwa kama kiongozi uwe tayari kupokea ushauri ili uweze kuboresha utendaji wako”, amesisitiza Dkt Ndumbaro.

  Dkt Ndumbaro amewaasa viongozi hao kuwapongeza watumishi wanaofanya kazi kwa bidii na wenye nidhamu ili iwe motisha kwa wale wavivu huku akiwataka kuwachukulia hatua wale wazembe na ambao hawataki kufuata kanuni na maadili ya utumishi wa umma.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida (hawapo pichani) kama sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma.
   Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro alipowatembelea katika kuadhimisha wiki ya utumishi umma.
   Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Singida Mwalimu Eva Mosha akitoa maoni yake kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro aliwapotembelea watumishi wa Mkoa wa Singida katika kuadhimisha wiki ya Utumshi wa Umma.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja Mama Salma Kikwete (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Norman Sigala, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga, Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete , Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM Hamphrey Polepole pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine wa Kiserikali na Wabunge, akivuta kitambaa kuashiria jiwe la ufunguzi wa  Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kuweka jiwe la ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani.
  Sehemu ya barabara ya Bagamoyo-Makofia –Msata kama inavyoonekana pichani.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa TANROADS mkoa wa Pwani na Dar es Salaam mara baada ya kufungua barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo, Mama Salama Kikwete, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Norman Sigala, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM Hamphrey Polepole pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0

  Na Frank Shija-MAELEZO

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali yake haitoruhusu mwanafunzi aliyepata ujauzito kuendelea na masomo kama ambayo baadhi ya Asasi za Kiraia zinavyopiga kampeni kuruhusu wanafunzi kuendelea na masomo mara baada ya kujifungua.

  Kauli hiyo imetolewa leo Wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani na Mhe. Rais alipokuwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Barabara ya Bagamoyo–Makofia-Msata, yenye urefu wa kilomita 64

  “Nataka niwaambie ndani ya utawala wangu hakuna mwanafunzi mwenye mimba atakaye rudi shuleni, hayo ndiyo maisha aliyoyachagua, akalee huyo mtoto. Hata hivyo anaweza akaanza maisha mengine akaenda Veta, akajifunza kushona au kuchukua mkopo na kujiingiza katika kilimo cha kisasa,” alisema Rais Magufuli

  Rais Magufuli aliongeza kuwa Serikali haiwezi kulipeleka taifa hili katika maadili ambayo hayapo katika jamii ya Kitanzania, hivyo kuruhusu watoto wa kike waliopata ujauzito kuendelea na masomo ni kuharibu maadili ya Kitanzania.

  Rais Magufuli amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha watoto wanapata elimu ndiyo maana alianzisha sera ya kutoa elimu bure, hivyo wanaopiga kelele kuwa watoto wa kike wanaopata ujauzito wapewe nafasi ya kuendelea na masomo wanataka kurudisha nyuma nidhamu ya wanafunzi.

  Katika hatua nyingine Rais Magufuli alimpongeza Mke wa Rais Mstaaafu wa Awamu ya Nne na Mbunge wa Kuteuliwa, Mama Salma Kikwete kwa juhudi zake za kupigania haki ya watoto wa kike kwa kupinga jambo hilo ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloendelea.

  Aidha Rais Magufuli alisisitiza kuwa kamwe Serikali haiwezi kufanya maamuzi kwa kuzingatia matakwa ya Asasi za Kiraia na kuzishauri asasi hizo kuwa badala ya kuishawishi Serikali ichukue uamuzi wa kuwaruhusu watoto wa kike wanaopata ujauzito kuendelea na masomo ni bora asasi hizo zikaanzisha shule zitakazotoa fursa hiyo.

  Rais Magufuli amesema kuwa Sera ya Serikali ni kumsomesha mtoto bure na siyo kumfundisha azae na kwamba suala hilo halikubaliki katika Serikali yake na kusisitiza kuwa hakuna mwanafunzi mwenye mtoto atakaye ruhusiwa kuendelea masomo.


  Hivi karibuni kumekuwa na mijadala bungeni na katika asasi za kiraia kuhamasisha Serikali iharakishe mchakato wa kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo katika shule za msingi na sekondari mara baada ya kujifungua.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne na Mbunge wa Kuteuliwa, Mama Salma Kikwete wakati wa hafla ya uzinduzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia-Msata yenye urefu wa kilomita 64, leo Wilayani Bagamoyo, Pwani. Mama Salma amekuwa mstari wa mbele kupinga mwanafunzi wa kike kuendelea na masomo mara baada ya kujifungua. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhwani Kikwete.


  0 0

  Picha na Habari za Freddy Macha 
   Baadhi yetu huwaita wenye hali hii “taahira” – neno la asili ya Kiarabu  lenye maana “mtu asiye sawa” (wazimu, chizi, bwege, nk).  Sahihi ni “mtindio ubongo” – kwa Kiingereza “Down Syndrome”....

  Baadhi ya taswira zake ni : kufikiri na kuzungumza taratibu, kigugumizi,  mwili mfupi,  utofauti wa tambo la kichwa,vidole vya mikono na miguu,nk.

  Mbali na kuwanyanyapaa,  jamii zetu Afrika bado hazitambui umuhimu wa kuendeleza wenye ulemavu.

  Mwaka huu kijana wa miaka 18, Samwel Mwanyika, mwenye “Mtindio Ubongo “  (Down Syndrome) alikuwa mshindi wa kimataifa wa upigaji picha.

  Balozi wetu Uingereza Mheshimiwa Asha-RoseMigiro akaeleza:

  “Wametoka vijana wengi kwenye nchi  zilizoendelea, wengine wamemzidi umri...tena wenzetu huwa na mipango maalum ya kuwapa mbinu mbalimbali,...sasa huyu wa familia ya kawaida tu ya Kitanzania ambapo bado hatujaweka miundo mbinu kama walivyoweka huku,  picha yake imeshinda...”

  Mwasisi wa kujitolea  wa shirika la Mtindio Ubongo (Pearl of People with Down Syndrome) , Mony Teri Pettite  na wazazi wake Samwel, Philip Mwanyika na Sophie Mshangama, walikutana na Balozi  Migiro na kupongezwa Ijumaa iliyopita. Afisa Utawala Ubalozini, Rose Kitandula , pia alikuwepo.

   Picha ya  Samwel Mwanyika iliyonyakua  tuzo la kimataifa la Stephen Thomas, mjini London.
   Samwel Mwanyika na picha iliyonyakua  tuzo la kimataifa la Stephen Thomas, mjini London.

  Balozi Migiro akimvika Samwel Mwanyika bendera ya taifa, alipowakaribisha na familia ofisini kwake, Ijumaa 16, Juni 2017.


  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
  KAMPUNI ya Bima ya Jubilee Insurance imezindua kampeni ya ISHI HURU kwa watoto wa darasa la tatu lililoanza Juni 12 na litamalizika rasmi tarehe 30 Juni mwaka huu ikizihusisha shule zote za Serikali.
  Katika shindano hili, mwanafunzi wa darasa la tatu atatakiwa kuchora picha zinazoelezea na kuonesha mtazamo wake kuhusu nini maana ya neno ‘ishi huru’ (live free).
  Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya Bima ya Jubilee, Mhasibu Mkuu Hellena Mzena amesema kuwa Jubilee imeandaa shindano liitwalo  hilo la ‘Ishi Huru’  ambalo washiriki watakuwa ni wanafunzi wa darasa la tatu wa shule zote za msingi za serikali.
  Hellena amesema washindi wa Tano watakaopatikana watazawadiwa Bima ya Elimu yaani “Jubilee Career Life Cover” watakayoipata watakapojiunga na elimu ya sekondari na kila shule itakayotoa mshindi itapata zawadi ya kikombe na cheti cha kutambua ushindi huo.
  Mgeni Rasmi Kamishna wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania , Dr. Baghayo Saqware akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Bima ya Jubilee baada ya kuzindua kampeni ya 'Ishi Huru' itakayomalizika Juni 30 mwaka huu pamoja na Mkuu wa Shule ya Madenge Lissy Kaluvya, Diwani na Naibu Meya wa Temeke Feisal ....
  Mgeni Rasmi Kamishna wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania , Dr. Baghayo Saqware pamoha na Mkuu wa Shule ya Madenge Lissy Kaluvya wakizindua shindano la 'Ishi Huru' uliofanyika katika shule hiyo leo Jijini Dar es salaam.
  Mkurugezi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Jubilee Life Insurance; Mr. Karim Jamal akizungumza na kuwashukuru Shule ya ,Msingi ya Madenge kwa kuweza kukubali kukarabati shule yao.
  Mhasibu Mkuu kampuni ya Bima ya Jubilee Hellena Mzena akisoma risala kwa Mgeni rasmi kuhusiana na kampuni yao ya Jubilee pamoja na jitihada wanazozifanya katika kuhakikisha wanasaidia jamii.

  0 0

   Katibu wa taasisi ya vijana ya Tanzania Youth Icon (TAYI), Abdallah Ahmed Suleiman akimuonyesha Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN)nchini,  Alvaro Rodriguez (wakwanza kushoto),ramani ya mpango wa uboreshaji huduma ya maji katika jimbo la Kikwajuni.Mratibu huyo amefika jimboni hapo ikiwa ni juhudi za Mbunge wa Jimbo hilo,Mhandisi Hamad Masauni(watatu kushoto) katika juhudi zake za kutatua changamoto za  huduma ya maji kwa wananchi.
   Mkurugenzi Uzalishaji Maji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Mhandisi Mohamed Elyas, akitoa maelezo ya Mradi wa Maji Kikwajuni kwa Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Alvaro Rodriguez alipotembelea mradi huo uliopo katika jimbo la Kikwajuni,Zanzibar.
   Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN)nchini,  Alvaro Rodrigues, akiangalia moja ya mabomba yanayotumika kusafirisha maji kwenda kwenye maeneo mbalimbali jimboni Kikwajuni ikiwa ni sehemu ya ushirikiano na Mbunge wa Jimbo hilo,Mhandisi Hamad Masauni katika kuhakikisha anamaliza tatizo la upungufu wa maji jimboni hapo.
  Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Loveluck Mwasha, a midwife and lecturer at The Aga Khan University (AKU) School of Nursing and Midwifery – Tanzania has received the coveted Midwife for Life Award 2017.

  Amina Sultani of Afghanistan also received a similar Award presented by Save the Children, and the International Confederation of Midwives (ICM)at the ICM 31st Triennial Congress in Toronto, Canada.

  The midwives have been awarded for their outstanding roles in developing the profession in their countries despite all odds. ICM President Frances Day-Stirk and Save the Children President and Chief Executive Officer Patricia Erb jointly presented the awards.


  Mwasha who has practiced midwifery for 30 years is a staunch advocate for the midwifery profession, midwives’ improved working conditions and improved health for mothers and new-borns in Tanzania.

  She has also been a “steadfast advocate for and mentor” to midwives through her work on the board of the Tanzania Nursing and Midwifery Council and at The Aga Khan Hospital and AKU School of Nursing and Midwifery.

  “My work is an opportunity to advocate for better support and training of midwives,” Mwasha said. “We work with stakeholders to help them appreciate midwives’ role in supporting women’s reproductive health, from community groups to members of parliament.”

  In Tanzania, 257 women and their babies die due to complications of pregnancy or childbirth which means 93,800 deaths each year, 70 percent or more of which are preventable with proven and effective interventions.

  0 0


  Kikosi cha wachezaji 22 wa timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kimeondoka leo Alhamisi Juni 22, 2017 kwenda Afrika Kusini katika michuano ya kuwania Kombe la Castle Cosafa.
  Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, ilikuwa kambini Hoteli ya Urban Rose, iliyoko Mtaa wa Jamhuri katikati ya jiji la Dar es Salaam, tangu Jumapili Juni 18, mwaka huu.
  Taifa Stars imeandaliwa kwa michuano hiyo iliyoandaliwa na Baraza la Mpira wa Miguu la nchi za Kusini mwa Afrika. Tanzania si mwanachama wa Cosafa, lakini imealikwa katika mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza Juni 25, mwaka huu.
  Taifa Stars imepangwa kundi A na timu za Mauritius, Malawi na Angola wakati Kundi B ni Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe. Timu za Botswana, Zambia na Afrika Kusini kadhalika Namibia, Lesotho na Swaziland zitakuwa na mechi maalumu (play off) ili kuingia robo fainali.
  Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga, kikosi kinachoondoka leo ni makipa Aishi Salum Manula  (Azam FC), Benno David Kakolanya  (Young Africans SC) na Said Mohammed Said (Mtibwa Sugar FC).
   Walinzi wa pembeni upande wa kulia ni Shomari Salum Kapombe    (Azam FC) na Hassan Hamis Ramadhan ‘Kessy’ (Young Africans SC) wakati upande wa kushoto wapo Gadiel Michael (Azam FC) na Amim Abdulkarim (Toto Africans FC).
  Walinzi wa kati ni Erasto Nyoni  (Azam FC), Salim Hassan Abdallah (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Nurdin Chona (Tanzania Prisons) wakati viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao (Azam FC) na Salmin Hoza wa Mbao FC.
  Kadhalika wako viungo wa kushambulia ambao ni Mzamiru Yassin Selembe (Simba), Simon Happygod Msuva (Young Africans SC), Raphael Daudi (Mbeya City) na Shizza Ramadhani Kichuya (Simba SC).
  Katika safu ya ushambuliaji wamo Thomas Emmanuel Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden), Mbaraka Abeid Yusufu (Kagera Sugar), Stamili Mbonde, Elius Maguli (Dhofar SC) na Shabani Idd Chilunda (Azam FC).

older | 1 | .... | 1761 | 1762 | (Page 1763) | 1764 | 1765 | .... | 3272 | newer