Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHIMIZA USHIRIKIANO, UPENDO KWA DINI ZOTE TANZANIA

$
0
0
Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akitoa salamu za Shukurani kwa niaba ya Wabunge na wafanyakazi wa Bunge, kwa Spika wa Bunge Job Ndugai, kwa kuwafuturisha, June 20, 2017 katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma. Waziri Mkuu aliwaasa Watanzania wote kuwa na ushirikiano kwa dini zote na kupendana.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akibadilishana mawazo na Spika wa Bunge Job Ndugai katika Futari iliyoandaliwa na Spika kwa ajili ya Wabunge, Wafanyakazi wa Bunge na Wageni waalikwa katika viwanja vya Bunge Mjini Dododma, June 20, 2017
Baadhi ya Wabunge wakibadilishina mawazo wakati wa futari iliyo andaliwa na Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai , kutoka kulia, Mbunge wa Ilala Idd Zungu. katikati Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge .na kushoto ni Mbunge wa Mbarali Haroon Mulla .Futari hiyo ilifuturiwa katika viwanja vya Bunge June 20, 2017 Mjini Dodoma Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

MICHUZI TV: JPM afungua kiwanda cha kuunganishia matrekta cha URSUS, Tamco Kibaha leo

Tangazo la kifo cha BRIGEDIA mstaafu wa JWTZ

WAKAZI WA PWANI WAIFURAHIA HUDUMA YA UKARIMU YA VODACOM

$
0
0

Wakazi wa kanda ya Pwani wameipokea kwa furaha kubwa huduma mpya ya Ukarimu inayotolewa na Vodacom Tanzania wakati huu wa msimu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani inayolenga kutoa ushirika na utoaji.
Ukarimu huu wa Vodacom unakwenda sambamba na kuwapatia wateja kifurushi kinachowawezesha kupata Qaswida, Mawaidha, Hadith, Facebook yenye picha na kuzungumza usiku wanaposubiri daku BURE kabisa. Ili mteja aweze kunufaika na bando hili la Ukarimu anatakiwa kupiga *149*01# kisha kuchagua aina ya bando kulingana na uwezo wake wa kifedha. Lipo bando linalodumu kwa muda wa saa 24 na linalodumu kwa siku saba.

Kwa kiasi cha shilingi 1000, mteja atapata dakika 150 Vodacom kwenda Vodacom, dakika 10 kwenda mitandao yote, ujumbe mfupi wa maandishi wa maandhishi bila kikomo, simu kupitia mtandao pamoja na ujumbe wa didi bure.

Kwa mteja atakayenunua bando la shilingi 3000 atapata dakika 150 Vodacom kwenda Vodacom, dakika 30 kwenda mitandao mingine, ujumbe mfupi wa maandishi bila kikomo, simu za bure usiku Vodacom kwenda pamoja na ujumbe mfupi wa maandishi wa dini bure kwa siku saba.

Siku ya leo Vodacom wanaendelea na futurisha katika maeneo yafuatayo

Tangax
Nyako
Mtindiro Kwabeda
Korogwe mjini

Mtwara
Newala

Lindi
Kilwa somanga
Kilwa chumo
Ruangwa namungo

UTUMISHI YAWAAGA WATAALAM 14 WA KUJITOLEA KUTOKA NCHINI JAPAN WALIOKUJA KUTOA HUDUMA KATIKA MAENEO MBALIMBALI NCHINI

$
0
0
  Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bw.Hiroki TAMURA akielezea namna alivyofanya kazi katika Chuo cha Utalii Zanzibar, katika hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao iliyofanyika ukumbi wa UTUMISHI  leo.
  Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bi. Moemi Ikeda akielezea namna alivyofanya kazi katika Shule ya Msingi Lusanga-Morogoro, katika hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao iliyofanyika ukumbi wa UTUMISHI leo.
 Mwakilishi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw. Fundikira Ekerege (kulia) akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya elimu yaliyowasilishwa katika hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao iliyofanyika ukumbi wa UTUMISHI leo.
 Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi.Roxana Kijazi (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mtaalam wa kujitolea kutoka nchini Japan Bi. MIDORI MIYAZAKI  aliyemaliza muda wake wa kutoa huduma nchini  katika hafla ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika ukumbi wa UTUMISHI leo. 
 Mkurugenzi Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi.Roxana Kijazi (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mtaalam wa kujitolea kutoka nchini Japan Bw. Shota Yanagisawa aliyemaliza muda wake wa kutoa huduma nchini  katika hafla ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika ukumbi wa UTUMISHI leo. 
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi.Roxana Kijazi (wa tano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wataalam wa Kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini baada ya hafla ya kuwaaga iliyofanyika UTUMISHI leo.

Ziara ya TTB Israel yaleta mafanikio sekta ya utalii

$
0
0
BODI ya Utalii Israel imeahidi kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) katika kutangaza vivutio vilivyopo na kukuza sekta ya utalii nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bibi Devota Mdachi,  aliyeongozana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki, kuitembelea Israeli kwa siku tatu mwezi huu, amesema  ziara yao nchini Israel imeleta mafaikio katika sekta ya utalii  Tanzania.

Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni  kukutana na wadau wa sekta ya utalii wakiwemo mawakala wa utalii na sekta ya malazi.
“Israel imeonyesha shauku kubwa ya kushirikiana na sisi katika kuutangaza utalii wa Tanzania. Mwaka jana tulipata watalii 22,000 kutoka nchini humo ambapo wameahidi mwaka huu watakuja watalii wengi zaidi.

“Vilevile kupitia vyombo vyao vya habari tumeeleza namna vivutio vyetu vilivyo na mwonekano wa kipekee duniani, tumepokea maombi mengi ya kuja kutembelea fukwe na hifadhi za wanyamapori.”

Alieleza kuwa hifadhi zilizotajwa sana ni Katavi, Mahale, Ngorongoro na Zanzibar: “Tunafahamu Waisraeli wanapenda kuangalia wanyamapori.Nilipokuwa nikiwatajia wanayama tulio nao walionyesha kufurahi hasa nilipowaeleza kuwa faru Fausta (55) mwenye umri mkubwa kuliko wote barani Afrika yupo katika ardhi ya Tanzania walionyesha kuvutiwa zaidi.”

Bw. Nzuki aliuambia mkutano na wadau wa utalii nchini Israel katika Mji waTel Aviv, : “Tanzania kuna fursa nyingi katika uwekezaji,  upande wa hoteli za kitalii.  Ikiwa una kampuni ya kitalii pamoja nyumba ya wageni ya kisasa unajiwekea uhakika wa kupata wageni wengi.“Ukiwa tayari unaweza kuja na kufuata utaratibu wa kisheria katika mamlaka husika utapewa maelekezo. Tunawakaribisha kuwekeza katika utalii.”

Miongoni mwa wawekezaji wanaofanya shughuli za kitalii nchini , Bwana Alon Hovev anayemiliki kampuni ya utalii ya Sima Safari , ameuambia mkutano huo kuwa sababu zilizomfanya kuwekeza Tanzania ni hali ya hewa na watu wake.

“Watanzania ni wakarimu,  nimevutiwa na mtindo wao wa maisha, vilevile kuna maeneo mengi ya kuvutia ikiwemo pwani safi na mbuga za wanyama,” amesema Bw. Hovev ambaye ameoa raia wa Tanzania.Utalii ni miongoni mwa vyanzo vikubwa vya mapato nchini, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, ameliambia bunge la bajeti hivi karibuni na kueleza kuwa mwaka 2016 Tanzania ilipokea watalii  milioni 1.2 ikiwa ni ongezeko la asilimia 12.9 mwaka 2015 walipokuja watalii milioni 1.1.

Mwaka jana sekta ya utalii iliingiza kiasi cha Dola za Kimarekani bilioni 2 ikiwa ni sawa na Sh Trilioni 4, mwaka 2015 iliingiza Dola bilioni 1.9.
Kiwango hicho cha mapato kiliifanya sekta ya utalii kuchangia asilimia 17.5 ya pato la taifa katika bajeti ya mwaka 2016/17 pamoja na kuingiza asilimia 25 ya fedha za kigeni.
 Mkurugenzi  Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bibi. Devota Mdachi akitoa mada katika mkutano nchini Israel alipofanya ziara ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania na fursa za biashara kupitia sekta hiyo. Ziara ya siku tatu aliyoifanya nchini humo imeleta ushawishi kwa bodi ya utalii ya Israel kushirikiana na Tanzania katika sekta hii.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Aloyce Nzuki akichangia mada katika mkutano nchini Israel alipofanya ziara ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania na fursa za biashara kupitia sekta hiyo. Ziara ya siku tatu aliyoifanya nchini humo imeleta ushawishi kwa bodi ya utalii ya Israel kushirikiana na Tanzania katika sekta hii.
Mkurugenzi  Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bibi. Devota Mdachi akizungumza na waandishi   wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake jijini Dar es Salaam akitoa mrejesho kuhusiana na ziara yao iliyofanyika nchini Israel ikiwa na lengo la kutangaza utalii wa Tanzania iliyofanyika kuanzia Juni 11 hadi 15 mwaka huu.
Mkurugenzi  Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bibi. Devota Mdachi(wapili kushoto) katika picha ya pamoja na  Balozi wa Tanzania nchini Israel Job Massima (wapili kulia) mara baada ya kumaliza mkutano uliowakutanisha wadau wa sekta ya utalii wa nchini Israel kutambua fursa za utalii zilizopo Tanzania. Ziara ya siku tatu aliyoifanya nchini humo imeleta ushawishi kwa bodi ya utalii ya Israel kushirikiana na Tanzania katika sekta hii. Kulia ni Balozi mdogo wa Tanzania nchini Israel Kasbian Chirich na Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Aloyce Nzuki.

TPSC YAANZISHA MAFUNZO YA SHAHADA YA UHAZILI NA UTUNZAJI KUMBUKUMBU,TAARIFA NA NYARAKA

$
0
0
Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kwa mara ya kwanza kimeanzisha Masomo ya Shahada ya kwanza (Degree) katika fani za Uhazili na Utunzaji wa Kumbukumbu, Taarifa na Nyaraka.

Kufuatia kuanzishwa kwa masomo ya Shahada ya kwanza katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Mkuu wa Chuo Dkt. Henry Mambo ametoa wito kwa watumishi wa umma na Watanzania wenye sifa kuchangamkia nafasi hizo za masomo kwa manufaa yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

Dkt. Mambo alisema masomo hayo ya Shahada ya kwanza yataanza Mwezi Septemba,2017 katika Matawi ya Dar es Salaam na Tabora, nayo ni hatua kubwa kwa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania katika kuwaendeleza Watumishi na Watanzania Kitaaluma.

Kwa upande wa sifa za kujiunga na masomo hayo ya shahada ya kwanza, Dkt. Mambo alisema muombaji anatakiwa kuwa na elimu ya kidato cha sita pamoja na ufaulu katika masomo mawili au Diploma katika fani husika yenye ufaulu au GPA alama 3.

Mkuu wa Chuo pia aliendelea kufafanua kwamba Masomo hayo ya ngazi ya Shahada yameanzishwa ili kuhakikisha kwamba watumishi wa umma na Watanzania wenye sifa za kujiunga wanakabiliana na changamoto zinazojitokeza katika soko la ajira kufuatia mabadiliko ya teknolojia na mifumo mbalimbali ya utendaji kazi.“Kutokana na mabadiliko hayo ni vema Watumishi wa Umma na Watanzania wenye sifa kwa ujumla nao wakapata mafunzo ambayo yatawawezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali katika soko la ajira,”.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah Kairuki akijadiliana jambo na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dkt.Henry Mambo, katika moja ya hafla jijini Dar es Salaam hivi karibuni(Picha na Maktaba) .

MAALIM SEIF AONGOZA HARAMBEE YA MADRASSA MUUMINI KIWALANI KUWEZESHA KUPATIKANA MILIONI SABA

$
0
0
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto akikabidhi mchango wake wa shilingi laki tatu katika harambee ya kuchangia Madrassa ya Muumini Islamiya iIliyopo kiwalani Dar es Salaam
Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akikabidhi mchango wake kwa Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kwa ajili ya Muumini islamiya.
Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akiongoza harambee ya uchangiaji wa Madrasa Kiwalani Temeke jijini Dar es Salaam ambapo aliwezesha kupatika kwafedha zaidi ya Milioni 7 kwa ajili ya ununuzi wa kiwanja kipya cha Madrasa hiyo
Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akizungumza wakati alipokuwakitoa ahadi yake ya Milioni moja kwa ajili ya Madrasa hiyo na aliweza kuwasilisha shilingi laki tano papo hapo na kuongeza ahadi ya bati 70 na mifuko 50 ya Saruji.


Waziri wa Habari akutana na Wasanii wa Filamu na Waandishi wa Habari wa AFm Dodoma leo

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akiwa na waandishi wa habari wa A Fm Radio walipomtembelea Bungeni leo.
 Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa Filamu, Ndg Nice Mtunze na Bi Lydia Mgaya walipowatembelea Bungeni leo.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakiwa katika picha ya pamoja waandishi wa habari wa A Fm Radio walipomtembelea Bungeni leo.

DK.SHEIN AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI TANZANIA SIMON SIRRO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na mgeni wake Inspekta Jenerali  wa Polisi Tanzania Simon Nyakoro Sirro alipofika Ikulu Mjini Unguja kujitambulisha kwa Rais.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na mgeni wake Inspekta Jenerali  wa Polisi Tanzania Simon Nyakoro Sirro alipofika Ikulu Mjini Unguja kujitambulisha kwa Rais. (Picha na Ikulu)

FUATILIA RAIS DKT MAGUFULI AKIZINDUA MTAMBO WA MRADI WA MAJI WA RUVU JUU -PWANI

MFANYABIASHARA WA KARIAKOO APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA NGUO ZA JESHI LA WANANCHI TANZANIA (JWTZ)

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

MFANYABIASHARA wa Kariakoo, Casto  Ngogo (35) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya kukutwa na nguo za jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) za milioni 50.

Ngogo ambaye ni Mkazi wa Tabata Segerea amefikishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa na kusomewa mashitaka yake na Inspekta msaidizi wa polisi Hamisi Saidi.

Imedaiwa kuwa, Juni 15, mwaka huu maeneo ya bandari kavu ya Galco iliyopo Chang'ombe wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, Ngogo alikutwa na suruali 5,000 za JWTZ kwenye kontena namba PCIU 82851 (5) zenye thamani ya Sh milioni 59 mali ya serikali bila kuwa na kibali.

Hata hivyo, mshtakiwa amekana mashtaka hayo na yuko nje kwa dhamana  baada ya kutimiza masharti ya dhamama.

Akisoma masharti hayo ya dhamana, Hakimu Nongwa amemtaka mshitakiwa  kuwasilisha fedha taslimu  milioni 30 au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo pamoja na wadhamini wawili watakaosaini ahadi ya milioni 10 kila mmoja.

Kesi imeahirishwa hadi Julai 17 mwaka huu itakapokuja kwa kutajwa. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi bado haujakamilika

TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA ALLY YANGA

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amepokea kwa mshtuko na majonzi makubwa taarifa ya kifo cha shabiki maarufu wa Young Africans, Ally Mohammed anayefahamika zaidi kwa jina la Ally Yanga, kilichotokea jana Jumanne Juni 20, 2017 kwa ajali ya gari iliyotokea mkoani Dodoma.

Katika salamu za rambirambi kwa uongozi wa Young Africans, familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Ally Yanga ambako Rais Malinzi amewaasa kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu kwao na kwa huzuni amewafariji akisema: “Sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake tutarejea.”

“Hakika nimeshtushwa na taarifa za kifo cha Ally Yanga ambaye nimejulishwa kuwa kilitokea katika ajali ya gari huko Dodoma. Kifo hiki kimefanya wanafamilia wa mpira wa miguu kupoteza hazina ya hamasa popote pale uwanjani,” amesema Rais Malinzi.

“Binafsi nilimjua Ally Yanga katika masuala ya mpira wa miguu hasa akishabikia Young Africans na timu zote za taifa bila kujali kuwa ni Twiga Stars (Timu ya taifa ya wanawake), Taifa Stars, Serengeti Boys au ile Ngorongoro Heroes,” amesema Malinzi.

“Hivyo, nawatumia Young Africans salamu zangu za rambirambi nikiwapa pole kwa kuondokewa na mmoja wa mashabiki mwenye mvuto wa kipekee katika hamasa uwanjani, lakini pia alikuwa akisapoti timu za taifa,” amesema Rais Malinzi.

Aidha, Malinzi amesema: “Nawatumia pole wanachama wote wa Young Africans kwa kuondokewa na Shabiki mahiri Ally Yanga. Nawapa pole pia familia, ndugu, jamaa na marafiki ambao wamepoteza mhimili wao.

“Naungana nao katika msiba huu ambao pia ni msiba wetu sote wanafamilia ya mpira wa miguu. Naungana nao pia kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Ally Yanga. Amina.”

Inna Lillah wa Innalillah Rajaun.
……………………………………………………………………………………………….
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

RC WA TANGA MH MARTINE SHIGELLA AFUNGU MAFUNZO YA KUMALIZA MAFUNZO YA AWALI

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Tanga Mh. Martine Shigella amewataka wahitimu wa mafunzo  ya awali ya kijeshi ya vijana operasheni Magufuli awamu ya pili wa kujitolea kutumia mafunzo waliyoyapata kwa kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa niaba ya Taifa la Tanzania.

Hayo ameyazungumza wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya kumaliza mafunzo ya awali ya kijeshi ya vijana operesheni Magufuli awamu ya pili  wa kujitolea yaliyofanyika kwenye  Kituo namba  835KJ Mgambo JKT  kilichopo Kata ya Kabuku Wilayani Handeni.


Mkuu wa Mkoa amesema kuwa mafunzo ya ukakamavu wa mwili, uzalishaji mali, masuala mazima ya ulinzi na usalama na mafunzo ya kijeshi yatumike kwa uzalendo na kuwa mfano bora kwa jamii itanayowazunguka.


“ Nendeni mkawe mfano bora wa kuigwa  kwenye familia zenu na wazazi wenu wamekuja hapa kuwashuhudia, Sisi kama Serikali tunawaamini” alisema Shigella.


Ameongeza kuwa Mh. Rais alipoamua kurudisha mafunzo haya alitambua umuhimu mkubwa kwa Taifa letu sababu anajua mahitaji ya sasa na ya baadae wakati lengo kuu likiwa ni kuleta usawa na uzalendo kwa wasomi na wasio wasomi.


Amewataka wakatimize wajibu wao wa kuwa raia wema na kuwa walinzi wa Taifa kwa kupitia mafunzo ya ulinzi na usalama waliyoyapata huku akieleza kuwa Serikali inapambana na changamoto za kukabiliana na wahalifu  ambao hawataki kuwa kama wanadamu wengine.


 “ Nina imani kubwa na nyinyi kwamba mtaendelea kuwa waadilifu, waaminifu na kuendelea kupiga vita vitendo vya rushwa na ubadhilifu wa mali za umma na kwamba mtakuwa kimbilio la wanyonge na watu wenye matatizo makubwa” alisema Shigella. 
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh Martin Shigella akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo.
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akizungumza wakati wa kufunga Mafunzo hayo.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh Martin Shigella akitoka kukagua gwaride.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MWANZA AKIWA NJIANI KUELEKEA CHATO

$
0
0

WAZIRI MKUU AMUAGIZA MKURUGENZI WA MISUNGWI AITISHE KIKAO KESHO SAA 4    

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Bw. Eliud Mwaiteleke aitishe kikao na wananchi wa Kigongo na kutafuta ufumbuzi wa tatizo la eneo la kujenga soko. 

Ametoa agizo hilo leo jioni (Jumatano, Juni 21, 2017) wakati akizungumza na mamia ya wakazi na wajasiriamali wanaotumia kivuko cha feri cha Kigongo waliokuwa wakimsubiri avuke kwenda Busisi, wilayani Sengerema. 

"Mkurugenzi haya mambo ya mipango, mipango na kupanga hayaleti tija kwa wananchi. Hivi hamjui kuwa wananchi wanahitaji kuwa na soko katika eneo hili ili waweze kuuza mazao yao au samaki?"

"Ninakuagiza Mkurugenzi, kesho Alhamisi, saa 4 njoo na Afisa Biashara wako, Mwenyekiti wa kijiji na watu wako pamoja na Diwani wa hapa, itisheni kikao na muonyeshwe eneo la soko ili mliingize kwenye mipango yenu," alisema. 

Waziri Mkuu alisema Serikali ya awamu ya tano haitaki kusikia lugha za michakato wakati wananchi wanaendelea kuteseka.

Awali, Waziri Mkuu alimwita Mkurugenzi huyo ili aeleze amejipanga vipi kwenye Halmashauri yake kutatua tatizo la soko kwa wananchi wa Kigongo. 

Akitoa majibu mbele ya Waziri Mkuu, Bw. Mwaiteleke alisema hawajawahi kupata mpango kutoka kwenye kata hiyo na kwa hiyo akawasihi wananchi waibue mpango huo na kuuwasilisha kwenye Halmashauri ili wao waweze kutenga fedha za kujenga soko.

Mapema, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kigongo, Bw. Sebastian Kisumo alimweleza Waziri Mkuu kwamba eneo hilo linakabiliwa na tatizo la soko pamoja na uhaba wa maji. 

Kuhusu maji, Waziri Mkuu alisema Serikali imetenga sh. bilioni 2.5 kwa ajili ya mradi wa maji wa kutoka Ziwa Victoria eneo la Itelele ambao utasambaza maji kwenda Misungi, Usagara hadi Kigongo Feri. 

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMATANO, JUNI 21, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Juni  21, 2017 akiwa njiani kueleakea Chato ambako atakuwa na ziara ya siku mbili. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


WADAU WA SHERIA WATAKIWA KUTOA MAONI KATIKA UTAFITI WA SHERIA YA HAKI JINAI

$
0
0

Na Munir Shemweta

Katibu Tawala MkoaTanga Bi. Zena Said amewataka wadau wa sheria kutumia fursa waliyonayo kuchangia kutoa maoni katika utafiti kuhusu taratibu zinazozuia haki jinai.Bi. Said alitoa rai hiyo wakati wa kufungua kikao cha wadau washeria mkoa wa Tanga juu ya utafiti kuhusu taratibu zinazozuia utoaji haki jinai kilichofanyika katika ofisi ya mkuu wa mkoa jijini Tanga.

Alisema, utoaji maoni yenye tija hususan kwa wadau wa mkoa wa Tanga siyotu utaisadia Tume ya KurekebishaSheria Tanzania katika mapitioya sharia hiyo bali kutaiwezesha nchi kuwa na mfumo wa sheria unaoendana na mabadilikoya jamii.

Kwa mujibu wa Katibu Tawala mkoa wa Tanga, mfumo wa utoaji haki jinai unakabiliwa na changamoto katika maeneo tofauti yanayohitaji kuangaliwa upya na kwa ukaribu ili kuhakikisha Tanzania inakuwa na sheria na taratibu zinazotoa haki kwa wananchi kwa wakati na haraka.

Awali Afisa Sheria Mkuu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Bi. Anjela Shila, aliwaeleza washiriki wa kikao hicho ambao ni Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo na Wilaya, maafisa Upelelezi wa polisi, Wanasheria wa Serikali, Mawakili wa Serikali na wa Kujitegemea , maafisa Magereza na Wanasheria kutoka Asasi za Kiraia zinazotetea haki za Jinai, Tume kwa sasa inaendesha utafiti kuhusu Mfumo wa Sheria ya Haki Jinai juu ya vipengele vinavyozuia haki.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Bi. Zena Said akifungua kikao cha Wadau wa sheria mkoa wa Tanga kutoa maoni juu ya utafiti kuhusu taratibu zinazozuia utoaji haki jinai kikao kilichofanyika ofisi za Mkuu wa mkoa jijini Tanga, kulia ni Afisa Sheria Mkuu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Bi. Anjela Shila.
Katibu Tawala Mkoa wa Tanga akizungumza na Afisa Sheria Mkuu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bi. Anjela Shila ofisini kwake kabla ya kufungua mkutano wa Wadau wa Sheria mkoa wa Tanga.
Mmoja wa wadau akiwasilisha maoni wakati wa Kikao.

NAIPENDA TANZANIA YANGU, NASIMAMA NA RAIS WANGU

$
0
0

Na Dkt. Hamisi Kigwangalla.

 Kila siku nashuhudia wananchi wenzangu wakikalamika. Natamani kujibu. Naacha. Natamani kuwakumbusha wananchi wenzangu. Naacha. Nasema mbona sisi ni wepesi kusahau? Natamani kuwakumbusha wabunge wenzangu. Naacha. Nasema na mimi sasa nipo kwenye Serikali. Ni mtunga sera, ni mfanya maamuzi, nikisema watasema huyu ni 'Naibu Waziri'. Lakini kiukweli nina hamu na shauku ya kuzungumza na wananchi wenzangu. Nami nitoe yangu ya moyoni. Kama mwananchi mwingine yeyote yule tu. 

Nina haki hiyo. Na mimi haki yangu inalindwa na katiba na sheria za nchi yetu. Leo nimeona acha nipumue kidogo. Niseme. Niuvue userikali wangu. Niseme kama mwananchi mwingine yeyote yule. Nianze kwa kuweka wazi kabisa hapa, kwamba; haya ni yangu. Si ya Serikali. Serikali ni ya Rais Magufuli, tumempa dhamana, ndiyo. Hili halibishaniwi. Tumempa kazi, ndiyo. 

Hili pia halibishaniwi. Lakini kazi hii anaifanyaje? Tunazijua changamoto anazokumbana nazo? Je, ana nia ya kuzitatua? Ni maswali ambayo yanastahili majibu. Kwenye makala hii nitajaribu kuyafafanua kidogo kwa mtazamo wangu kadri nitakavyojaaliwa. Pamoja na kumpa dhamana Rais wetu, ni lazima tufahamu kuwa na sisi tuna wajibu wa kutimiza kwa Taifa letu. 

Tuna kazi ya kufanya kumsaidia Rais wetu kubeba mzigo wa kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kijamii kwenye Taifa letu. Tusimuachie huu mzigo peke yake. Tuubebe sote. Nchi ina changamoto nyingi sana, siyo kwamba Rais ama Serikali yake haizifahamu ama haina nia ya kuzitatua, ama Rais Magufuli amesinzia, ama anastarehe; kila siku anahangaika kukuna kichwa, usiku na mchana kuzitafutia ufumbuzi. Nadhani hili halina ubishani sana kwa mpenda kweli. 

Binafsi, sina shaka kabisa juu ya uwepo wa nia thabiti ya kuleta mapinduzi. Sina. Kwenye biashara ya kujenga nchi changamoto haziishi siku moja. Ukimaliza moja, nyingine inaibuka, na nyingine zinazaliwa kutokana na majawabu ya changamoto uliyoitatua. Juzi juzi hapa nilisema kuhusu mfumo wa afya wa nchi kubwa kama ya Marekani kuwa na changamoto ya kuwabagua watu maskini na wale wa tabaka la kati na kwamba unajenga matabaka makubwa sana yanayowanyima fursa sawa baadhi ya watu kwenye Jamii. 


Mwanasheria ya TBS huru, akamatwa tena.

$
0
0
Na Karama Kenyunko blogu ya jamii


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia kesi mwanasheria Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Baptister Marco Bitaho (54) baada ya upande wa mashtaka kuomba kufanya hivyo.

Bitaho alikuwa akikabiliwa na mashtaka matatu likiwamo la kuishi na kufanya kazi nchini Tanzania bila kuwa na kibali. 

Mashtaka hayo yamefutwa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa baada ya Mwendesha Mashtaka kutoka Uhamiaji, Method Kagoma kuiomba mahakama imfutie mwanasheria huyo mashtaka yake chini ya kifungu cha 98(a)cha sharia ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (CPA).

Hata hivyo baada ya mshtakiwa huyo kuachiwa huru alikamatwa tena na yupo katika Idara ya Uhamijai kwa ajili ya mahojiano. 

Mapema mwezi huu, ilidaiwa kuwa Mei 19,2017 huko Kinondoni katika ofisi ya uhamiaji, Bitaho akiwa raia wa Burundi alikutwa akiishi nchini bila ya kuwa na kibali.

Ilidaiwa kuwa siku hiyo, Bitaho alikutwa akifanya kazi kama mwanasheria Mkuu wa TBS bila ya kuwa na kibali kinachomruhusu kufanya kazi hapa nchini.



Iliongezwa kuwa, Julai 6 mwaka 2011 katika ofisi ya Uhamiaji ya Dar es Salaam iliyopo wilaya ya Ilala, mshtakiwa huyo akiwa raia wa Burundi alitoa taarifa za uongo kuhusu maelezo yake binafsi wakati akijaza fomu ya kuomba hati ya kusafiria namba CT (5)(Ai).

Ilidaiwa kuwa, kitendo hicho cha kutoa taarifa za uongo kilimuwezesha Bitaho kupata hati ya kusafiria ya Tanzania yenye namba AB 474856 huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za nchi.

OBASANJO PRAISES PRESIDENT MAGUFULI AND TELLS AFRICAN LEADERS TO EMULATE HIM

$
0
0
Nigeria retired President Olusegun Obasanjo has hailed President United Republic of Tanzania Dr. John Pombe Magufuli for being exemplary leader in Africa in spearheading the country’s economic development and safeguarding national interests.

Mr. Obasanjo, one of the prominent African leaders, made those remarks today when he paid a courtesy call to President Magufuli at the state house.
Mr. Obasanjo lauded President Magufuli’s efforts to attract investors from all corners of the world and praised his determination and desire to make sure the country is adequately benefiting from those investments. 
        
“President Magufuli’s efforts to make sure foreign investments benefiting the country is a crucial one and should be emulated by other African leaders because it is the only way that the continent can make economic headways” said Mr. Obasanjo.

According to the statement from state house signed by the Director of Presidential Communications, Mr. Gerson Msigwa quoted former president of Nigeria saying that he was impressed by the state of the economy Tanzania’s which he said it is on “the right track”.   
        
“I have visited various countries including Mozambique, Malawi and now I am in Tanzania. In all those countries, my discussions are focused on economic development and most importantly how our countries can sufficiently benefit from investments in various areas of the economy” Mr. Obasanjo noted.

He added that Africa can no longer afford to let foreign investors rip off the continent resources and left African with very little to share.

BENKI YA KCB TANZANIA YAFUTURU NA WATEJA WAKE MWANZA

$
0
0
Benki ya KCB Tanzania imefuturisha wateja wake wa Mwanza katika hoteli ya JB Belmont. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Bw. Ahmed Msangi, wajumbe wa bodi ya huduma za kiislamu wa benki ya KCB, wafanyakazi na wateja wa benki hiyo. 

Akizungumza wakati wa futari hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Cosmas Kimario alisema kuwa futari hiyo ipo ndani ya vipaumbele vya benki kuwekeza katika jamii na kuboresha uhusiano na wateja wake.

“Benki ya KCB Tanzania inadhamini uwajibikaji kwa jamii ambayo kwa kiwango kikubwa inalenga maeneo ya vipaumbele vya Elimu, Afya, Mazingira, Ujasiriamali na malengo yake hasa ni kujikita katika masuala ya ubinadamu”, Kimario alisema na kubainisha kwamba tangu ilipofunguliwa hapa Tanzania mwaka 1997, benki hiyo imekuwa ikijikita katika kuisadia jamii.

“Mwezi huu mtukufu unaamrisha watu kujirudi, kuutambua na kuuheshimu uwepo wa Mungu. Pia unatukumbusha kufanya yale yampendezayo Mungu na ndio maana benki ya KCB tumeona umuhimu wa kukutana hapa jioni hii ili kufuturu pamoja” alisema Kimario.

Bw. Kimario alieleza kuwa, benki ya KCB inakitengo maalumu kwa ajili ya huduma za Kiislamu inayoitwa “Sahl Banking” na huduma hiyo hupatikana katika matawi yote 14 ya benki hiyo. “Benki ya KCB ndio ya kwanza kuanzisha huduma zinazozingatia shari’ah hapa nchini na inazidi kuimarisha huduma hizo kwa kuzingatia muongozo husika. Huduma hizo bora ni akaunti za biashara kwa watu binafsi na taasisi mbalimbali, jamii (community account), akiba (savings account), watoto, hijja n.k.

Alimaliza kwa kuwataka wale ambao bado hawajajiunga na benki ya KCB kujiunga leo na kupata huduma za kibenki kwa haraka, usalama na bila usumbufu.

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB, Bw. Cosmas Kimario (wapili kulia) akipata futari pamoja na wateja wa benki hiyo. Hafla hiyo ya futari iliandaliwa na benki ya KCB kwa ajili ya wateja wake Jijini Mwanza. 
Baadhi ya wateja wa Benki ya KCB walio kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani Jijini Mwanza wakiwa kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo. 
Baadhi ya wateja wa Benki ya KCB walio kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani Jijini Mwanza wakiwa kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo. 


PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images