Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1760 | 1761 | (Page 1762) | 1763 | 1764 | .... | 3278 | newer

  0 0


  0 0

  Na Tiganya Vincent.

  WAISLAMU Mkoani Tabora wametakiwa kuunga mkono juhudi zilizoanzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli za kupambana kikundi la watu wachache ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakinufaika na rasilimali ya nchi hii na kuwaacha watu wengi wakiwa maskini licha ya utajiri waliojariwa na Mungu.

  Kauli hiyo imetolewa jana mjini Tabora na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi wakati wa futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa huo Bw. Aggrey Mwanri.

  Alisema kuwa Rais Magufuli haipaswi kuachiwa pekee vita aliyoanzisha , bali anatakiwa kuungwa mkono na watu wote wenye mapenzi mema na nchi hii kwani kiongozi huyo amesaidia kuwafumbua macho na kuona kuwa wameibiwa sana na walikuwa wakiendelea kuibiwa na kikundi cha watu wachache kwa maslahi yao binafsi na sio ya watu wengi.

  Sheikh Mavumbi aliongeza kuwa Rais Magufuli ameonyesha mapenzi makubwa kwa nchi yake na wananchi wake na kukwerwa na umaskini wa wananchi wake uliosababishwa na tamaa ya watu wachache waliokuwa wakinufaika wakati nchi ikibaki na mashimo ambayo wakati mwingine yanaweza kusababisha vifo kwa watu kutumbukia ndani yake.

  Alisisitiza kuwa sio vizuri kupuuza juhudi kubwa anaozifanya Rais Magufuli kwa kushirikiana na viongozi wenzake za kusimamia rasilimali za nchi na kutetea haki za wanyonge ambao walikuwa wakidhulumiwa na watu wachache  kwa maslahi yao binafisi

  Sheikh Mavumbi aliongeza kuwa Rais Magufuli anataka kutupeleka ambapo kila raia wa nchini hii atakunufaika na utajiri wa nchi hii ambao wamejariwa na Mungu.


  0 0

  Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala Ofisi ya Makamu wa Rais, Samuel Mwashamba akimkaribisha Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais ili azungumze na Watumishi wa Ofisi ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais  Profesa Faustin Kamuzora (katikati) akiongea wakati wa mkutano wake na Watumishi wa Ofisi yake walioko Dar Es Salaam, ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma.
  Mmoja wa Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Aidan Mtuhi akichangia maoni yake wakati wa Mkutano huo.
  Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais waliohudhuria Mkutano huo wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (hayupo pichani).

  0 0


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge, Balozi wa India hapa Nchini Sandeep Arya, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo pamoja na Viongozi wengine wa Mkoa wa Pwani na Serikali akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mradi Mkubwa wa Maji wa Ruvu Juu Mlandizi Mkoani Pwani.
   Sehemu ya Mradi huo wa maji wa Ruvu juu Mlandizi Mkoani Pwani
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Mfuko wa sandarusi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo kabla ya kuzindua kiwanda cha Global Packing kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kiwanda cha kutengeneza  matrekta URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilijaribu Trekta mojawapo katika kiwanda cha kutengeneza  matrekta URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli   pamoja na viongozi wengine akifungua kiwanda hicho cha nondo.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 21 Juni, 2017 amefuturisha wananchi wa mkoa wa Pwani na kuwataka waumini wa dini ya Kiislam na madhehebu mengine kuendeleza umoja na mshikano uliopo kwa muda mrefu kwa lengo la kudumisha amani nchini.

  Mhe. Rais Magufuli amesema anaungana na waumini wa dini ya Kiislamu nchini katika kumi la mwisho la Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kuwaombea kumaliza kwa amani ibada ya Funga ya Ramadhani ikiwa ni kutekeleza nguzo ya nne kati ya nguzo tano ya dini ya kiislam.

  Amesema kwa mujibu wa dini ya Kiislamu ibada ya Funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni muhimu kwani ni njia sahihi ya kujirekebisha kuachana na matendo maovu yanayoweza kusababisha kutenda dhambi.

  ‘’Ramadhani ni ibada muhimu kwa Waislaam kwani ndio mwezi ambao huchoma dhambi zao na kutenda matendo mema hivyo ni muhimu kwa ndugu Waislaam kuendeleza yote mema ambayo wanafanya katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani ikiwa ni pamoja na kuliombea Taifa.’’

  Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Aboubakar Zubeir Ali ametaka wananchi wa Tanzania bila kujali itikadi za kidini kuendelea kuliombea Taifa ili lizidi kuendelea kuwa na amani.

  Nae Kaimu Sheikh wa mkoa wa Pwani Sheikh Hamisi Mtupa amemshukuru Rais Magufuli kwa ukarimu wake wa kuwaaandalia futari wananchi wa mkoa wa Pwani ikiwa ni pamoja na makundi maalum ya watoto yatima wa kituo cha Bulome Foundation cha mjini Kibaha mkoani Pwani. 

  Jaffar Haniu

  Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

  Kibaha, Pwani

  21 Juni, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika foleni ya kunawa na kisha kuchukua chakula leo Jumatano Juni 21, 2017  katika futari aliyowaandalia wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha ambayo ilihudhuriwa pia na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali  pamoja na viongozi wengine wa dini, serikali, vyama na watoto wanaolelewa kwenye vituo mbalimbali vya yatima mkoani humo.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli (wa pili kulia) akichukua chakula leo Jumatano Juni 21, 2017 katika futali aliyowaandalia wananchi wa mkoa wa Pwani futari katika Ikulu ndogo ya Kibaha ambayo ilihudhuriwa pia na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali pamoja na viongozi wengine wa dini, serikali, vyama na watoto wanaolelewa kwenye vituo mbalimbali vya yatima mkoani humo.

   Kina mama wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaya Mhe. Asumpta Mshama wakichukua chakula wakati wa futari iliyoandaliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa neno la shukrani leo Jumatano Juni 21, 2017  wa waliohudhuria  futari aliyowaandalia wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha.
   Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali  akizungumza machache na kuomba dua baada ya futari iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha.

   Sehemu ya waalikwa wakiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali  baada ya   futari iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha.


  0 0
  0 0

  Wanachama wa majimaji wameandamana hadi ofisi ya mkuu wa mkoa wa ruvuma dkt bilinithi mahenge kwa lengo la kushinikiza uchaguzi katika klabu hiyo ambapo inadawai baadhi ya viongozi wameanda mchakato wa kubadilisha katiba ili viongozi walio salia waendelee kaubaki madarakani.

  0 0

  DONGE nono la Sh Milioni 20 la bahati nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, droo ya 16, leo limeenda kwa mshindi wao Ramadhan Juma Hussein, mwenye maskani yake mjini Dodoma, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Makao Makuu ya Nchi ya Tanzania kupata mshindi wake katika droo kubwa inayofanyika Jumatano na Jumapili.

  Ushindi wa Ramadhan umekuja siku chache baada ya kukabidhiwa fedha zake mshindi wa Handeni, mkoani Tanga, Yahaya Ally Khamis, aliyekabidhiwa pesa mapema wiki hii.

  Akizungumza katika droo hiyo leo mchana, Balozi wa Biko, Kajala Masanja alimpongeza Ramadhan kwa kuibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20, huku akiwataka Watanzania wote kucheza kwa wingi na mara nyingi ili wazoe mamilioni ya Biko.

  “Naomba kutangaza kwamba mshindi wetu wa Jumatano hii wa Sh Milioni 20 ni Ramadhan anayetokea mjini Dodoma, ambaye pia amekiri kucheza Biko mara kwa mara pamoja kuwahi kushinda zawadi za papo kwa hapo ambao zinatoka kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinatoka kila dakika kwa wale wanaocheza bahati nasibu yetu.

  Mchezo huu unachezwa kwa kupitia ujumbe mfupi wa maandishi kwenye mitandao ya simu ya Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel, ambao huingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na ile ya kumbukumbu 2456, baada ya kufanya muamala kuanzia Sh 1,000 na kuendelea na kupata nafasi ya kuwania zawadi za papo kwa hapo bila kusahau kuingia kwenye droo kubwa ya Sh Milioni 20,” Alisema Kajala.

  Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema Biko imezidi kukolea baada ya kumpata mshindi wa Dodoma kwa mara ya kwanza tangu waanze kuchezesha bahati nasibu yao, huku akiwapongeza wote waliowahi kushinda donge nono la Biko kutoka kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania.

  “Ni furaha kubwa kuona Dodoma wameibuka na donge nono la Biko, huku nikiamini kuwa kucheza Biko ni rahisi pamoja na kuweza kuibuka na ushindi wa zawadi za papo hapo bila kusahau zawadi kubwa ya Sh Milioni 20 inayotoka mara mbili kwa wiki,” Alisema Heaven.

  Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akiwa kwenye tukio la kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 20 wa droo ya 16 ya Biko, ambapo bwana Ramadhan Hussein wa Dodoma aliibuka kidedea na kuzoa kiasi hicho cha pesa kutoka Biko. Kushoto ni mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amewataka wananchi wa kijiji cha Mwamagunguli kata ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga kuacha kuchanganya siasa kwenye masuala maendeleo kwani inakwamisha shughuli za maendeleo na kusababisha kero katika jamii.

  Matiro ameyasema hayo jana June 21,2017 baada ya kutatua mgogoro wa mradi wa maji ya kisima kirefu katika kijiji hicho ambapo viongozi wa eneo hilo kuanzia ngazi ya kitongoji hadi kata na wananchi walikuwa hawatumii maji hayo wakidai kuwa yana chumvi na hata yakitumika kupikia chakula yanakibadilisha na kuwa na rangi ya njano.

  Kufuatia utata huo wa mradi huo ambao ujenzi wake ulikamilika tangu Mwaka 2014 kwa gharama ya shilingi milioni 294.6,Mkuu huyo wa wilaya aliamua kufika katika kijiji hicho ili kubaini ukweli wa madai ya wananchi hao.

  Baada ya kufika katika kijiji hicho akiwa ameambatana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo pamoja na viongozi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga walizungumza na wananchi wa eneo hilo ambao walisisitiza kuwa maji hayo hayafai mbele ya mkuu wa wilaya.

  Mmoja wa wananchi hao,Shija Luhende aliuponda mradi huo wa maji mbele ya mkuu huyo wa wilaya akidai kuwa maji ya mradi huo wa kisima kirefu ukiyapikia kwenye ugali au wali chakula kinakuwa cha njano kutokana na kuzidi kwa chumvi hivyo hayafai kwa matumizi ya binadamu.

  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akiwa ameshikilia sahani yenye wali uliopikwa kwa maji yaliyokuwa yanadaiwa kuwa ukiyatumia kwa chakula,chakula kinabadilika na kuwa na rangi ya njano Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mwamagunguli.
  Wananchi wa kijiji hicho wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro 
  Mmoja wa wananchi hao Shija Luhende akiuponda mradi huo wa maji mbele ya mkuu huyo wa wilaya kuwa maji yake ukiyapikia kwenye ugali au wali chakula kina kuwa cha njano kutokana na kuzidi kwa chumvi na hayafai kwa matumizi ya binadamu.


  0 0

   Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (wa pili kulia), akifafanua jambo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi (kushoto) baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji ya Mkoa wa Singida kutoka kwa Katibu Tawala huyo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.
   Baadhi ya Watumishi wa Mkoa wa Singida wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kazi na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. 
   Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akiongea na watumishi wa Mkoa wa Singida wakati wa kikao kazi na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Kulia kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi.
   Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akipokea maoni na malalamiko yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya watumishi wa Mkoa wa Singida wakati wa kikao kazi na watumishi hao mkoani Singida ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Kulia kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi.


  0 0

  Mafunzo hayo ambayo yamekwisha kuanza katika kata ya Nguvumaliyanatarajiwa kuwafikia wanawake wajasiriamali 120 na baadae kuendeleakwenye maeneo mengine katika Jiji la Tanga.

  Akizungumza juzi wakati akifungua mafunzo hayo,Mstahiki Meya wa Jijila Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi alisema mpango huo utasaidiakuwakomboa wanawake kiuchumi lakini pia kuwaandaa na ujio wa miradimikubwa miwili mkoani hapa ikiwemo wa bomba la mafuta na kiwandakikubwa cha kuzalishia saruji.

  Alisema pia licha ya kuwapa uelewa masuala hayo lakini namna bora yakuzitumia kwa malengo yatakayokuwa na tija fedha wanazokopa kutokakwenye taasisi za kibenki kwani baadhi yao wanashindwa kutambuawazitumie vipi na kuzirejesha.

  “Utakuta wakina mama wajasiriamali wanakopa fedha kwenye taasisimbalimbali kwa malengo ya kufanya biashara lakini kutokana na kutokuwana elimu hivyo wanaishia kuzitumia kwenye mambo mengine na kusababishamadeni “Alisema.
    Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi akizungumza na wakina mama wajasiriamali kwenye kata ya Nguvumali wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo ambayo aliyaandaa kwa ajili ya kukabiliana na fursa mbalimbali za kujiwekeza kiuchum ambapo mafunzo hayo yatafika kwenye kata 27 za Jiji hilo
   Baadhi ya wanawake wajasiriamali katika Kata ya Nguvumali Jijini Tanga wakiwa kwenye mafunzo hayo
  WANAWAKE wajasiriamali Jiji la Tanga wanatarajiwa kunufaika na mafunzo ya kuwajengea uwezo katika utengenezaji na ubinifu wa bidhaa mbalimbali ili waweze kujikwamua kichumi jambo ambalo litasaidia kuondokana na utegemezi kwenye jamii.  0 0  0 0  0 0


  *Ahimiza nyumba za ibada zisitumiwe vibaya

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba waumini wa dini za Kiislamu na Kikristo nchini wahakikishe nyumba zao za ibada hazitumiki kuleta migogoro.

  Ametoa ombi hilo jana usiku (Jumatano, Juni 21, 2017) wakati akizungumza na mamia ya waumini wa dini za Kikristo na Kiislamu pamoja na viongozi wa dini walioshiriki ibada ya futari wilayani Chato, mkoani Geita.

  Akizungumza na waumini hao kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu alisema Mheshimiwa Rais alishapanga kufika Chato ili kushiriki nao ibada ya iftar lakini ametingwa na majukumu ya kitaifa akaona ni vema amtume yeye ili amwakilishe.

  “Mheshimiwa Rais alishapanga kuja Chato kufuturu pamoja na wana-Chato lakini kadri siku zinavyozidi kwenda anajikuta anabanwa na majukumu mengi ikiwemo kukutana na wageni wa kimataifa, kwa hiyo akaona ni vema nije kumwakilisha katika shughuli hii,” alisema.

  “Mheshimiwa Rais anawaombea heri katika siku zilizobakia za mfungo wa Ramadhan ili mmalize salama na Mungu akijalia muweze kusherehekea pamoja, na pia anawatakia heri wale watakaoendelea na sita tushawal.”

  Akisisitiza kuhusu amani na utulivu nchini, Waziri Mkuu alisema: “Hatupendi kusikia kuwa msikiti fulani wamechapana viboko kwa sababu ya kugombea uongozi au kwenye kanisa fulani waumini wamepigana wakigombea mchungaji wao.”

  “Tutumie nyumba zetu za ibada kudumisha amani na mshikamano wetu. Napenda niwahakikishie kuwa Serikali yenu chini ya Rais John Pombe Magufuli itaendelea kuheshimu dini zote.”
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akishiriki  katika swala ya magaharibi katika  futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu mjini  Chato, mkoani Geita, Juni 21, 2017.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifuturu pamoja na Askofu Mussa Magwesera wa Kanisa la African Inland Church (AIC)  Dayosisi ya Geita (kushoto) na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Geita, Alhaj Yusuph Kabaju(kulia) katika futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu kwa niaba ya Rais John Pombe Magufuli, mjini  Chato, mkoani Geita  Juni 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mussa Magwesera wa Kanisa la African Inland Church (AIC), Dayosisi ya Geita katika futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu kwa Niaba ya Rais John Pombe Magufuli  mjini  Chato mkoani Geita  Juni 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza  na wananchi wa eneo la Kigongo feri Wilaya ya Misungwi, wakati aliposimama kwa muda akiwa njiani kuelekea Chato kwa ziara ya siku mbili  Juni 21, 2017.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu,  Ezekiel Kyunga wakati alipowasili mjini Chato mkoani Geita  Juni 21, 2017 kwa ziara ya siku mbili mkoani humo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

  The Ngorongoro District Authorities, in collaboration with the UNESCO Dar es Salaam Office, will welcome the Permanent Secretary of the Ministry of Health (MoHCDGEC), Dr. Mpoki Ulisubisya, the Vice-Chancellor of the Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS), Prof. Ephata Kaaya and the UNESCO Representative, Ms. Zulmira Rodrigues on 23 June 2017 for a visit to the first Tele-health Centre in the country. The mission is taking place in the context of the preparations of the handover from UNESCO to Government of this innovative model for provision of specialised health care to remote rural populations. 

  The Tele-Clinic is part of a UNESCO/Samsung Digital Village programme in a remote Maasai village in Ngorongoro, Arusha. It is an innovation platform, testing health services provision in maternal and infant care, dental and Ear, Nose and Throat (ENT) services that utilizes connectivity and smart technologies. It will be the first tele-health pilot to connect all levels of the Tanzanian healthcare system reaching out to the remotest communities. The pilot is in the initial service trial phase, focusing first on the operationalization of remote maternal consultations. The Digital Village is a pioneering example that demonstrates how remote communities can be empowered by modern technology improving their access to quality health and education services and build capacities to generate decent income. 

  UNESCO’s innovation approach is unique in its focus on incorporating the cultural specifics in the programme by working in close collaboration with the local community, traditional leaders and healers and by building on traditional Maasai livelihoods such as Maasai crafts to tap into the opportunities for sustained development of the Northern Circuit. The visitors will also be introduced to other Digital Village programme components including e-learning, livelihoods development and cultural tourism development activities.

  0 0

   Wanawake wakichagua nguo za watoto wao wa kike  kwa ajili ya maandalizi ya sikuu ya Eid  El Fitri kama walivyokutwa na Camera yetu katika mtaa wa Congo Soko Kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam
   Mzazi akimjaribisha nguo mtoto wake wa kiume kutoka kwa wamachinga wa soko la Kariakoo kwa ajili ya maandalizi ya sikuu ya Eid el Fitri
   Wanawake wakiwa wanachgua  viatu vya kuvaa  kwa ajili ya maandalizi ya sikuu ya Eid el Fitri
  Sehemu ya umatai wa watu uliofurika katika mtaa wa Congo katika soko kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam 

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge pamoja na watendaji wake kuhakikisha Mji wa Kisarawe uliopo mkoani Pwani unapata huduma ya maji safi na salama.

  Rais Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo jana mkoani Pwani wakati akizindua Mradi wa upanuzi wa Mtambo wa  maji wa Ruvu Juu na ulazaji wa Mabomba Makuu kutoka Mlandizi kwenda Jijini Dar es Salaam.

  Mh. Magufuli amesema kuwa Mkoa wa Pwani umefanya kazi kubwa ya kutunza miundombinu ya maji ambayo imewezesha kuhudumia wananchi wa Dar es Salaam hivyo ni haki kwa wananchi wa Mkoa huo kufaidika na maji wanayoyatunza kwa muda mrefu.

  “Ninafahamu Mji wa Kibaha kwa sasa hauna shida ya maji, shida iliyopo ni kuzidi kwa presha ya maji ambayo sio tatizo la DAWASA wala DAWASCO hivyo ili kutatua tatizo hilo ni jukumu la Wizara husika na watendaji wake kujipanga na wahandisi wa maji kuunganisha bomba kutoka Wilaya ya Kibaha hadi Kisarawe ambapo kuna changamoto ya maji safi na salama,” alisema Rais Magufuli.

  Akiongelea utunzaji wa miundombinu ya maji, Rais Dkt. Magufuli amewataka watendaji wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji kuhakikisha wanashughulikia maji yanayopotea kwa kurekebisha miundombinu ambayo imeharibika na kuweka miundo mbinu mipya inayoweza kuhimili wingi wa maji.

  Aidha, Rais Magufuli ameishukuru Serikali ya India kwa kutoa trilioni 1.3 kwa ajili ya kuendeleza miradi ya maji kwa Miji 16 nchini ambayo ikikamilika itawezesha wananchi wengi kupata maji safi na salama hivyo amewaahidi kudumisha ushirikiano uliopo katika sekta ya maji baina ya nchi hizo mbili.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt. John Pombe Magufuli

  0 0

   Mtakwimu, Jovitha Rugemalila akiwa na Mkutubi wa Nilam Mgassa kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakitoa elimu kwa wadau  wa Takwimu waliotembelea maonesho ya wiki ya utumishi wa Umma yaliyofanyika nje ya ofisi ya Taifa ya Takwimu jijini Dar es Salaam, ambapo ofsi hiyo hutoa elimu kwa wadau na wakazi wote wa jiji ambao hupata fursa ya kukutana na wataalam mbalimbali kutoka ofsi hiyo.Picha na Humphrey Shao wa Globu ya Jamii.
   Mtakwimu, Jovitha Rugemalila akiwa na Mkutubi wa Nilam Mgassa kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakitoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Royola ya Jijini Dar es Salaam ambao walifika katika eneo hilo kwa ajili ya kujifunza masuala ya takwimu.
  Mtakwimu, Jovitha Rugemalila , akitoa elimu ya masuala ya Takwimu kwa mmoja wa wadau wa Takwimu waliofika kujifunza katika maenesho ya wiki ya Utumishi wa Umma ynayofanyika mbele ya ofisi hiyo iliopo barabara ya kivukoni Jijini Dar es Salaam

  0 0

  Loveluck Mwasha, a midwife and lecturer at The Aga Khan University (AKU) School of Nursing and Midwifery – Tanzania has received the coveted Midwife for Life Award 2017.

  Amina Sultani of Afghanistan also received a similar Award presented by Save the Children, and the International Confederation of Midwives (ICM) at the ICM 31st Triennial Congress in Toronto, Canada.

  The midwives have been awarded for their outstanding roles in developing the profession in their countries despite all odds. ICM President Frances Day-Stirk and Save the Children President and Chief Executive Officer Patricia Erb jointly presented the awards.

  Mwasha who has practiced midwifery for 30 years is a staunch advocate for the midwifery profession, midwives’ improved working conditions and improved health for mothers and new-borns in Tanzania.

  She has also been a “steadfast advocate for and mentor” to midwives through her work on the board of the Tanzania Nursing and Midwifery Council and at The Aga Khan Hospital and AKU School of Nursing and Midwifery.

  “My work is an opportunity to advocate for better support and training of midwives,” Mwasha said. “We work with stakeholders to help them appreciate midwives’ role in supporting women’s reproductive health, from community groups to members of parliament.”

  In Tanzania, 257 women and their babies die due to complications of pregnancy or childbirth which means 93,800 deaths each year, 70 percent or more of which are preventable with proven and effective interventions.

  Midwives are seen as the single most important cadre for preventing maternal and new-born deaths and stillbirths.

  Especially in humanitarian contexts and for poor or hard-to-reach populations, midwives provide the majority of immediate care to mothers and new-borns, often without support, materials, training, or recognition.

  FOR MORE NEWS CLICK HERE

older | 1 | .... | 1760 | 1761 | (Page 1762) | 1763 | 1764 | .... | 3278 | newer