Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

BANDA AMALIZANA NA SIMBA, KUMWAGA WINO MUDA WOWOTE

$
0
0
Beki wa timu ya Taifa na klabu ya Simba Abdi Hassan Banda ameweka wazi msimamo wake wa kuendelea kuitumikia timu yake hiyo kwa mkataba wa miaka wa miaka miwili ila amewataka kuweka kipengele cha kumuachia iwapo atapata timu nyingine nje.

Ameyasema hayo wakati wa mazoezi ya timu ya Taifa kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya COASAFA inayotarajiwa kuanza Juni 25 nchini Afrika Kusini. Banda amekubali kusaini kandarasi na timu yake ya Simba huku akiwa amepatiwa dau la maana ambalo limeweza kumshawishi kuendelea kusalia kwa wana msimbazi hao.

Taifa Stars inayojiandaa na michuano ya COSAFA Castle nchini Afrika Kusini baadaye mwezi huu, Banda amesema kwamba wakati wowote, Meneja wake Abdul Bosnia atafika Dar es Salaam ili wasaini mkataba huo mpya na Simba.
“ Mkataba wangu na klabu ya Simba umesalia siku tano, lakini tumeshafikia makubaliano na nitaendelea nao baada ya kusaini mkataba huo inaweza kuwa  kabla sijaenda Afrika Kusini au baada ya kurejea kutoka huko,"amesema Banda.

Ameweka wazi kuwa,  mazungumzo baina yake na uongozi wa Simba umekuwa mzuri na wenyewe wanajua makubaliano yao ili aweze kuongeza mkataba na kuendelea kuitumikia klabu hiyo na zaidi anamsubiri meneja wake aje kumalizana nao.

Banda yumo kwenye kikosi cha Taifa Stars, kinachotarajiwa kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) Castle nchini Afrika Kusini kuanzia Juni 25, mwaka huu.

Taifa Stars iliyoweka kambi hoteli ya Urban Rose iliyopo iliyopo eneo la Kisutu, huku ikifanya mazoei Uwanja wa JMK Youth Centre, inatarajiwa kuondoka nchini Juni 22 kwenda Afrika Kusini kushiriki michuano ya COSAFA kama wa waalikwa kwa mwaka wa pili mfululizo na mara ya tatu kwa ujumla kihistoria.

Tanzania imepangwa kundi A pamoja na Mauritius, Malawi na Angola wakati Kundi B lina timu za Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe – na Botswana, Zambia, Namibia, Lesotho na Swaziland na wenyeji, Afrika Kusini zitacheza mechi maalumu za mchujo kuwania kuingia robo faina.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

TUMESHAKABIDHI RIPOTI KWA UONGOZI, TUNASUBIRI MAJIBU TUANZE KAMBI - KOCHA MTIBWA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

KOCHA msaidizi wa timu ya Mtibwa Zuberi Katwila amesema kuwa kwa sasa anasubiri maamuzi ya Mwenyekiti wa klabu hiyo baada ya kumkabidhi ripoti ya mwaka mzima ya kikosi hicho.

Akizugumza na Mtandao huu, Katwila amesema kuwa ameshakabidhi ripoti kwa Uongozi wa klabu hiyo  na wanatarajiwa kuanza maezoezi Julai mosi mwaka huu kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2017/18.

Katwila amesema, hawezi kuweka wazi ni wachezaji gani watakaoachwa ila ripoti nzima imeweka wazi wachezaji wanaohitajika kuachwa na sababu zao kwani kila mmoja amewekewa muda aliocheza na alicheza katika kiwango cha juu au chini.

"kila mchezaji ameainishwa katika ripoti katika vipengele tofauti kama aliweza kucheza kwa muda gani na kwa kiwango gani, mbali na hilo wapo ambao wameshindwa kuonyesha kiwango kikubwa na pia nao nimewaandikia sababu za kuachwa,"alisema Katwila.

Amesema, ukiachilia hilo pia katika ripoti yake ameweka wazi wachezaji anaowahitaji ila cha zaidi anasubiri majibu ya uongozi kuhusiana na wachezaji hao na iwapo watashindikana kupatikana hatua ya itakayofuata ni kuita wachezaji katika kufanya majaribio katika timu yao.

Katwila amesema mpaka sasa hawajajua ni wapi wataweka kambi hiyo ya maandalizi ya ligi hadi pale watakapopata maelekezo kutoka kwa Uongozi kama watakaa Manungu au nje ya mkoa wa Morogoro.


Kikosi cha Mtibwa.

TAARIFA YA MSIBA

$
0
0
Familia ya Eng Deo Renati Masoy wa  Shirika la Nyumbu Kibaha anasikitika kutangaza kifo cha Baba yao Mzazi Mzee  Renati John Masoi .ambaye amefariki 19/Juni/2017 katika Hospitali ya Hindu Mandal

Mipango ya Mazishi inafanyika nyumbani kwa Mtoto wa Marehemu Eng Deo Masoy Kibaha kwa Mathias njia ya kwenda Nyumbu ,Habari ziwafikie Ukoo wote wa Masoy ,Ukoo wote wa Kombe Ndugu wa Marehemu Watoto wa   marehemu  Wajukuu waliopo ndani ya Nchi na Nnje ya Nchi , wwafanyakazi wa Shirika la Nyumbu  Pamoja na majirani wote.

BWANA AMETOA BWANA AMETWA JINA LAKE LIHIMIDIWE

MTOTO SHUKURU ARUHUSIWA MUHIMBILI , AFYA YAKE YAIMARIKA

$
0
0
Mtoto Shukuru Kisonga (16) ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) baada ya kupatiwa matibabu na afya yake kuimarika.
Mtoto Shukuru alifikishwa  katika  Hospitali ya Taifa Muhimbili Mei 16, mwaka huu akitokea Tunduru ambako aliripotiwa kuishi kwa kunywa mafuta , sukari na maziwa.

Baada ya kufikishwa MNH alifanyiwa uchunguzi na timu ya madaktari Bingwa  na kubaini kwamba ana ugonjwa wa Selimundu pamoja na upungufu wa madini ya chuma na kwamba upungufu wa madini hayo ulisababisha anywe mafuta, sukari na maziwa.

Kwa upande wake Mama mzazi wa mtoto Shukuru,  Mwanabibi Mtenje amesema amepata faraja kuona afya ya mtoto wake imeimarika na sasa anaweza kula chakula chochote.

“Kwakweli namshukuru Mungu, pia nawashukuru  sana madaktari na wauguzi wa Muhimbili  kwani  hali ya mwanangu ilikuwa mbaya, alikuwa hawezi kula chochote  zaidi ya kunywa mafuta, maziwa na sukari, lakini baada ya kupatiwa matibabu,  afya yake imeimarika na sasa anaweza kula vyakula vyote,’’ amesema Mama Shukuru.

Awali mtoto Shukuru  alipelekwa katika Hospitali ya Misheni Tunduru kwa ajili ya kupatiwa matibabu, lakini ugonjwa haukooneka na baadaye alipelekwa hospitali  Nyangao mkoani Lindi.
 Mtoto Shukuru Kisonga (16) akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako alifikishwa Mei 16, 2017 kwa ajili ya kupatiwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa na Selimundu na upungufu wa madini chuma. Mtoto huyo sasa anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu na madaktari wa hospitali hiyo.
Mtoto Shukuru Kisonga (16) ameruhusiwa baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako alikuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa selimundu na upungufu wa madini chuma.  Kushoto ni mama yake Shukuru, Mwanabibi Ntenje.

WAZIRI MWAKYEMBE ''MSIMAMO WA MWALIMU ULIOKOA MENGI YA NCHI HII''

HAKI ELIMU YAZINDUA KAMPENI YA KUMUWEZESHA MTOTO WA KIKE APATE ELIMU

$
0
0


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Haki Elimu Nchini , John Kalaghe akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuondoa Vikwazo kwa Mtoto wa Kike katika hafla iliyofanyika katika ofsi za Tasisi hiyo Upanga jijini Dar es Salaam,Kampeni hiyo itasaidia kuongeza uelewa kwa jamii kumpa fursa msichana hili aweze kupata mafanikio na kufikia maelengo yake
Msemaji kutoka TGNP, Grace Kisetu akichangia jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ondoa Vikwazo asome iliyofanyika katika ukumbi wa Haki Elimu Upanga Jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya Waandishi waliohudhuria kampeni ya ondoa Vikwazo asome iliyozinduliwa na Tasisi ya Haki elmu kwa kushilikiakana na mashirika mbalimbali ya kijamii.

WAZIRI MKUU -SERIKALI INATAMBUA UMUHIMU WA KISWAHILI

Article 6

$
0
0
Sasa tabasamu kwa SH 200 tu uchonge na uwapendao. Vocha ya Sh 200 imetua mtaani kwako, Fika duka lolote karibu na wewe ujinyakulie vocha ya Tabasamu kwa Sh 200 sasa, hii ndio njia sahihi ya maisha  #TabasamuKwa200 FOLLOW: @airtel_tanzania

WATANZANIA WANG'ARA MAREKANI.

$
0
0
 Wanafunzi watatu wa shule ya sekondari ya FEZA BOYS Dar es Salaam wamenyakua medali za dhahabu huko Marekani katika mashindano ya uwezo wa kitaaluma ya GENIUS OLYMPIAD yaliyoshirikisha nchi 63 Duniani. Walionyakua medali hizo ni wanafunzi Abdulrazak Juma Mkamia,Rashid Jakaya Kikwete na Abdallah Rubeya

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA CHAMA CHA ASKARI WASTAAFU WA VITA KUU YA PILI YA DUNIA LEO OFISINI KWAKE MJINI DODOMA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akipokea Barua ya kujitambulisha na kuomba msaada wa mchango kwa ajili ya kufanya Mkutano Mkuu wa Chama cha Askari wastaafu kwa Vita kuu ya pili ya dunia waliopigana Mwaka 1939 – 1945 kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama hicho ambae ni Ndg. Bakari Ngonja, katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akutana na kufanya mazungumzo na Chama cha Askari wastaafu wa Vita kuu ya pili ya dunia waliopigana Mwaka 1939 -1945 katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akisisitiza jambo pale alipokutana na kufanya mazungumzo na Chama cha Askari wastaafu wa Vita kuu ya pili ya dunia waliopigana Mwaka 1939 -1945 katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

MICHUZI TV: WADAIWA WA KODI YA MAJENGO KUBURUZWA MAHAKAMANI - RC GAMBO

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA WANANCHI WA KIBAHA MKOA WA PWANI

$
0
0


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Kibaha Maili moja katika viwanja vya Bondeni Mkoani Pwani katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu
Mkoani humo.
 Mmoja wa Wananchi akionesha hisia zake wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia Wananchi wa Kibaha Maili moja katika Viwanja vya Bondeni Mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha wageni  mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Bondeni Mjini Kibaha kwa ajili ya kuwahutubia wananchi wa Mkoa wa Pwani.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza katika mkutano huo.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNE 21,2017

DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI JUNI 20, 2017

Wajasiliamali wawezeshwa kuzikabili changamoto

$
0
0
Na. Frank Mvungi - Maelezo

Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imeandaa mkakati wa kuwasaidia wajasiriamali nchini kukabiriana na changamoto zinazokwamisha maendeleo yao ili waweze kuchangia juhudi za Serikali katika kujenga uchumi wa viwanda.

Mkurugenzi wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo ameeleza hivi karibuni kuwa miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiliamali kwa kushirikiana na taasisi zingine ambazo kwa njia moja au nyingine zinagusa shughuli za wajasiliamali nchini.

Alizitaja taasisi hizo kuwa ni Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) na GS1, ambazo kwa pamoja zitakuwa zikitoa mafunzo ya namna ya kuboresha bidhaa za wajasiriamali ili ziendande na mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.

“Changamoto zinazowakabili wajasiriamali ni mtambuka na zinahitaji mikakati ya pamoja ya sekta na wadau katika kukabiliana nazo”. Alisisitiza Sillo wakati wa kikao cha pamoja na taasisi hizo.

Ametaja mkakati mwingine ni kuundwa kwa Kamati ya wataalam nane ambayo itaratibu namna ya kutekeleza mikakati ya kuondoa changamoto zinazowakabili wajasiriamali kote nchini. Kamati hiyo itajumuisha wajumbe wawili kutoka kila taasisi.

Pia Bw. Sillo amezishauri TanTrade na SIDO kufuatilia katika halmashauri zote nchini upatikanaji wa maeneo ya uzalishaji yatakayotumiwa na wajasiriamali hao ili kutekeleza dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa vitendo.

Kwa upande wa bidhaa hatarishi (high risk food products), Mkurugenzi wa TFDA amesisiza bidhaa hizo zisizalishwe bila kuwa na vibali kutoka TFDA ili kulinda afya ya mlaji na mamlaka hiyo kufanya marejeo ya kanuni ya ada na tozo ni mkakati wa kuweka unafuu kwa wajasiriamali. Kuanzia mwaka 2013/14 hadi 2016/17, TFDA imetoa mafunzo kwa wajasiliamali katika mikoa 16 ambayo ni Dar es Slaam, Pwani, Mwanza, Arusha, Mbeya, Dodoma na Rukwa.

Mikoa mingine ni Manyara, Lindi, Mtwara, Tanga, Singida, Iringa, Kigoma, Kilimanjaro na Morogoro. Aidha jumla ya wajasiriamali 1,287 wameisha pewa mafunzo mapaka kufikia mwezi June, 2017 ambapo kwa sasa mafunzo hayo yatafanyika kwa kushirikisha taasisi zote zenye jukumu la kuwahudumia wajasiriamali hapa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) bw. Hiiti Sillo akizungumza wakati wa Kikao cha pamoja kati kati ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS),SIDO,TANTRADE kilichofanyika hivi karibuni kikilenga kuweka mikakati ya pamoja itakayosaidia kutatua changamoto zinazowakabili wajasiriamali hapa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) bw. Hiiti Sillo wakwanza kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Mhandisi Agnes Kiwelu (katikati) na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Prof. Sylvester Mpanduji na mwisho kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE Bw. Edwin Rutagarika. (Picha na TFDA).

FATILIA HAPA MOJA KWA MOJA ZIARA YA RAIS DKT. MAGUFULI MKOANI PWANI LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Kibaha Maili moja katika viwanja vya Bondeni Mkoani Pwani jana, wakati akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu Mkoani humo. leo Rais Magufuli anaendelea na ziara yake mkoani humo ambapo atazindua viwanda vitatu pamoja na mradi wa maji wa Ruvu na baadae kuongea na wananchi.

AGPAHI YAENDELEA KUTOA HUDUMA ZA KISAIKOLOJIA KWA WATOTO NA VIJANA

$
0
0
Jumla ya watoto 8,615 kutoka mikoa ya Tanga, Mara, Mwanza,Geita, Simiyu na Shinyanga wamepatiwa huduma za Virusi vya Ukimwi na Ukimwi ikiwemo kupatiwa dawa za kupunguza makali ya VVU (ARVs) katika kipindi cha kuanzia mwaka 2011 hadi mwezi Machi 2017. 

Huduma hizo zimetolewa na shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi kwa kushirikiana na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto. 

Takwimu hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Miradi kutoka AGPAHI,Dk. Safila Telatela wakati wa kufungua Kambi ya Ariel 'Ariel Camp' ya siku tano inayokutanisha watoto na vijana wenye umri kuanzia miaka 10 mpaka 17 kutoka mikoa ya Shinyanga,Geita na Mwanza inayofanyika katika Hotel ya Lesa Garden jijini Mwanza. 
Mkurugenzi wa Miradi kutoka shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) Dk. Safila Telatela akizungumza wakati wa kufungua Ariel Camp (Kambi ya Ariel) ya siku tano kuanzia June 19,2017 - June 23,2017 iliyokutanisha watoto na vijana 50 kutoka mikoa ya Shinyanga,Mwanza na Geita jijini Mwanza.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog 

Dk. Telatela alisema watoto hao ni sawa na asilimia 5 kutoka jumla ya watu 189,806 waliopatiwa huduma na shirika hilo katika kipindi hicho na shirika linaendelea na kazi ya kutoa matunzo na tiba za VVU katika vituo 553 katika mikoa hiyo sita. 

Alisema pia wanafanya kazi ya kutokomeza maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto katika vituo 631. Aidha Dk. Telatela alisema wamefanikiwa kuunda vikundi zaidi ya 65 vya watoto na vijana katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu ambapo takribani watoto 2640 wamenufaika na vikundi hivyo. 

“Kuanzia mwezi Oktoba 2016, shirika letu limeongeza wigo wa kutoa huduma kutoka mikoa miwili ya Shinyanga na Simiyu na sasa imekuwa sita na tunafanya kazi ya kutoa matunzo na tiba za VVU katika vituo 553 kwenye mikoa hii sita”,alieleza Dk. Telatela. 
Mratibu wa Ukimwi wa Mkoa wa Mwanza Dk. Pius Maselle akifungua kambi ya watoto na vijana 'Ariel Camp' katika hotel ya Lesa Garden jijini Mwanza.Wa kwanza kushoto ni Mratibu wa Miradi AGPAHI mkoa wa Shinyanga,Dk. Gastor Njau akifuatiwa na Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Geita Dk. Joseph Odero. Wa kwanza kulia ni Mratibu wa Miradi AGPAHI mkoa wa Mwanza, Olympia Laswai akifuatiwa na Mkurugenzi wa Miradi AGPAHI, Dk. Safila Telatela. 


“Shirika letu limekuwa likiandaa kambi kwa ajili ya watoto na vijana kwa lengo la kuwakutanisha ili kujifunza mambo mbalimbali kuhusu afya, stadi za maisha, kupata ushauri wa kisaikolojia kutokana na changamoto wanazokutana nazo na pia huduma za kitabibu kutoka kwa daktari wa watoto katika kipindi chote cha kambi na kuwafanya kuwa mabalozi wa huduma za watoto katika jamii zao”,aliongeza. 

Naye Mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kambi hiyo, Mratibu wa Ukimwi wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Pius Maselle alitoa rai kwa mikoa mipya ya AGPAHI (Geita,Tanga,Mara na Mwanza) kufanya jitihada za ziada katika uundaji wa vikundi vya watoto na vijana ili idadi ya watoto watakaonufaika na huduma za kisaikolojia iwe kubwa. 

Aidha Dk. Maselle alitoa shukrani kwa shirika la AGPAHI kwa jitihada mbalimbali linazofanya katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi nchini kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia shirika la Centres for Disease Control and Preventation (CDC),mfuko wa kusaidia Watoto wenye VVU Kwa hisani ya watu wa Uingereza (CIFF) na Shirika la Development Aid From People to People (ADPP - Mozambique). 

Mbunge wa Ruangwa akabidhi msaada wa bajaj kwa mlemavu mjasiliamali

$
0
0
Katibu Tawala Wilaya ya Ruangwa (DAS), Twaha Mpembenwe (katikati) akimkabidhi kadi ya Bajaji Rashidi Makolelo (mlemavu wa miguu) Mkazi wa mpume kata ya Nkowe wilayani Ruangwa kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Ruangwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliyoahidi kumpatia siku kadhaa zilizopita.
Rashidi Makolelo (mlemavu wa miguu) Mkazi wa mpume kata ya Nkowe wilayani Ruangwa akiwa ndani ya Bajaj hiyo, baada ya kukabidhiwa.
Rashidi Makolelo (mlemavu wa miguu) Mkazi wa mpume kata ya Nkowe wilayani Ruangwa akisikiliza maelekezo kabla ya kukabidhiwa Bajaji aliyosaidiwa na Mbunge wa Jimbo la Ruangwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliyoahidiwa na sasa kutimia kwa ahadi hiyo.

MICHUZI TV: RAIS DKT. MAGUFULI AKITEMBELEA KIWANDA CHA GLOBAL PACKIGING BAADA YA KUKIZUNDUA MJINI KIBAHA ASUBUHI HII

BAJETI KUU YA SERIKALI YAPITISHWA KWA KISHINDO MJINI DODOMA

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), pamoja na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), pamoja na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb), wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Bustani kilichoko wilayani Kondoa mkoani Dodoma, walipotembelea bungeni mjini Dodoma, siku ambayo Bunge limepitisha kwa kishindo Bajeti ya Sh. trilioni 31.7 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akimshukuru na kumpongeza Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), kwa ushirikiano mkubwa aliompatia hadi kufanikisha kazi kubwa ya kuandaa na kusimamia Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 31.7 iliyopitishwa na Bunge kwa kishindo mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akiteta jambo na maafisa waandamizi wa Wizara yake nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, baada ya Bunge kupitisha kwa kishindo Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 31.7

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images