Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1757 | 1758 | (Page 1759) | 1760 | 1761 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Navy kenzo has released another music video for their Patoranking-assisted catchy afro pop song “Bajaj” which is the third from their album.

  The song is very inciting and the video will exhilarate you with the way Director Justin Campos used his eye of storytelling.

  The message is what arouses one's curiosity, it is spotlighted that women shouldn’t be treated like Bajaj. As matter of fact “Bajaj” is a prominent motorized tricycle in East Africa used a public transport and the song points a woman shouldn't treated like bajaj because usually whenever one hop off a bajaj never remembers the plate number or drivers name, and that’s when the value of bajaj goes down.

  The “Bajaj" music video premiere will proceed with a sneak peek on their NavyKenzoVEVO channel.

  According to Navykenzo, “Success is not built by power but mind and hard work”, apparently they are cooking up some new projects as much as they worked hard to come up with their idiosyncratic recipe. Stay tuned

  watch the video for BAJAJ here.

  0 0

   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi Hajat Mwanaisha Magambo mkuu wa kituo cha New Life Orphanage cha Boko Dawasco kwa niaba ya viongozi wa  vituo nane vya kulelea yatima na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu waliopewa vyakula kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja na sikukuu ya Eid el Fitr na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli  Ikulu  jijini Dar es salaam leo Juni 20, 2017. 

  Vituo vilivyopkea vyakula hivyo ni pamoja na New Life kilichopo Boko Dawasco chanye watoto 121, Charambe Islamic kilichopo Charambe (watoto 54), Mwandaliwa Centre kilichopo Mbweni (watoto 94) Al Madina Children Home cha Tandale ( watoto 65), Ijangozaidia Orphanage Centre kilichopo Sinza (watoto 1030, Azam Orphanage kilichopo Mbagala (watoto 51), Hiari Orphanage kilichopo Chang'ombe (watoto41) na CHAKUWAMA (watoto 64) kilichipo Sinza.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimsabahi mmoja wa yatima baada ya kumkabidhi vyakula Hajat Mwanaisha Magambo kutoka kituo cha New Life Orphanage cha Boko Dawasco kwa niaba ya viongozi wa  vituo nane vya kulelea yatima na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu waliopewa vyakula kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja na sikukuu ya Eid el Fitr na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli  Ikulu  jijini Dar es salaam leo Juni 20, 2017.
    Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na viongozi wa vituo nane vya kulelea yatima na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kabla ya kuwakabidhi vyakula kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja na sikukuu ya Eid el Fitr Ikulu  jijini Dar es salaam leo Juni 20, 2017.

  0 0

  WAENDESHAJI wa bahati nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku’ jana wamemkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wao Yahaya Ally Khamis, aliyeibuka na ushindi katika droo ya 15, iliyochezeshwa juzi Jumapili, huku akitokea wilayani Handeni, mkoani Tanga. 

  Makabidhiano hayo yamefanyika wilayani hapa katika tawi la benki ya NMB, wilayani Handeni, mkoani Tanga, tayari kwa kuziingiza katika matumizi ya kumkwamua kiuchumi.

  Akizungumza katika makabidhiano hayo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema mchezo wao ni rahisi kucheza na kushinda, tofauti na michezo mingine inayotumia akili nyingi pamoja na uzoefu wa kufuatilia mambo mengi ya kukuletea ushindi. Alisema Biko ili mtu ashinde ni kufanya muamala kwenye simu yake ya Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kwa kuanzia Sh 1,000 na kuendelea ambapo namba ya kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ikiwa ni 2456, huku mchezaji akiwa haulizwi swali lolote kwenye simu yake.

  “Biko hatuulizi mtu swali lolote na ndio maana zaidi ya mtu kufanya muamala ambao Sh 1,000 yake itampatia nafasi ya ushindi wa papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni 1,000,000 zinazolipwa kwenye simu mara baada ya kupokea ujumbe wa ushindi, huku nafasi nyingine ikiwa ni kuingia kwenye droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 20 ambayo Jumapili iliyopita tulimpata Khamis tuliyomkabidhi leo fedha zake.

  “Tumefarijika kuja Handeni kumpatia fedha zake mshindi wetu, huku tukiwaasa Watanzania wote kujitokeza kwa wingi kucheza Biko kwa sababu ni mchezo unaotoa ushindi mzuri na haraka, hivyo chezeni kwa wingi na mara nyingi zaidi ili mjiwekee mazingira mazuri ya ushindi,” Alisema Heaven.

  Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, kushoto akimkabidhi hundi ya Sh Milioni 20 Yahaya Ally Khamis, dakika chache kabla ya kuelekea katika tawi la benki ya NMB, wilayani Handeni walipomkabidhi pia kiasi cha fedha taslimu Sh Milioni 20 kama mshindi wa droo ya 15 ya Biko iliyochezeshwa Jumapili iliyopita. Wengine ni majirani na wadau wa Khamis, wilayani Handeni wakishuhudia wakati anakabidhiwa hundi hiyo.
  Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, akimkabidhi Sh Milioni 20 mshindi wao wa Handeni, mkoani Tanga, Yahaya Ally Khamis kulia. Makabidhiano hayo yalifanyika katika tawi la benki ya NMB, wilayani Handeni mkoani Tanga jana. Kushoto ni afisa wa NMB, wilayani Handeni akishuhudia makabidhiano hayo.


  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  *Ni zile korofi na zilizoharibiwa na mvua
  *Amkabidhi mhandisi wa manispaa mitambo ya kazi,lita 10,000 za dizeli

  Wilaya ya Kinondoni leo imezindua ukarabati wa barabara zenye urefu wa Kilomita 148 ambazo zimeharibiwa na mvua zilizonyesha katika msimu uliopita hali iliyosababisha adha ya usumbufu na foleni kwa wananchi.

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi ameeleza hayo wakati akizindua matengenezo hayo na kumkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni ambaye pia ni mhandisi wa manispaa hiyo Abdul Digaga mitambo ya ujenzi wa barabara na lita 10,000 za dizeli.

  Mafuta na mitambo hiyo inatokana na juhudi za Mkuu huyo wa Wilaya ya Kinondoni kwa kushirikiana na wadau wa kampuni za TOTAL TANZANIA na kampuni ya ujenzi GRAND TECH zilizotoa mitambo na mafuta ya dizeli kama sehemu ya mchango wao kwa DC Hapi kwa juhudi zake na za serikali ya awamu ya tano kwa ujumla katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Kinondoni.

  Barabara zitakazofanyiwa ukarabati ni barabara zote korofi na zilizoharibiwa na mvua katika kata zote 20 za manispaa ya Kinondoni.

  Aidha, DC Hapi ametembelea ujenzi wa barabara ya Nzasa KM 1.2 kwa kiwango cha lami unaofanywa na kampuni ya Esteem chini ya mradi wa Uboreshaji jiji la Dar es salaam (DMDP) ambapo chini ya mradi huo wilaya ya Kinondoni itanufaika na kiasi cha bilioni 22 huku Mfuko wa barabara ikiwa na bilioni 6 zilizoruhusiwa kutumika kukamilisha miradi iliyosimamishwa ya 2016/2017.

  "Mbali na juhudi hizi za wadau waliojitolea kunisaidia mafuta na mitambo ya kutengenezea barabara, tunazo bilioni 6 za Mfuko wa barabara na tutanufaika na bilioni 22 za mradi wa Uboreshaji wa jiji la Dar es Salaam.Hivyo wananchi msiwe na wasiwasi, mwaka huu ujao wa fedha ni mwaka wa barabara kwa Kinondoni." Alisema Hapi.

  DC Hapi aliwaomba wananchi waliojitokeza kuendelea kumuombea Rais Dr. John Magufuli na wasaidizi wake wote kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo nchini.

  Uzinduzi wa ukarabati huo wa barabara umefanyika katika kata ya Kijitonyama na kuhudhuriwa na wananchi wa eneo hilo.

  0 0


  Baraza la Michezo Tanzania (BMT), limebariki Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) likisema: “Tunaitakia TFF uchaguzi mwema wenye amani, upendo na utulivu.”

  Pamoja na baraka hizo, Baraza limeiagiza TFF kuwaelekeza wagombea wote kuzipitia sheria za Baraza la Michezo, Kanuni za Baraza na kanuni za Usajili, hususani kanuni ya 8 (1) na (2). 

  Kanuni hiyo ya 8 (1) na (2), inaagiza kuwa endapo wagombea wote watakaoshinda nafasi wanazowania kwa sasa ndani ya TFF, hawana budi kuachia nafasi mojawapo katika uongozi wa mpira kwa miguu katika ngazi ya wilaya au mkoa aliyoshinda awali.

  BMT imetoa agizo hilo ikiwa ni kukumbushana juu ya utii wa sheria na kuepuka kushika nyadhifa mbili kwa wakati mmoja.

  Katika barua yake iliyoandikwa Juni 19, mwaka huu na kusainiwa na Katibu Mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja, Baraza hilo limesema: “Uchaguzi huu usivuruge amani iliyopo nchini. Wagombea wakumbuke kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi.”

  Baraza limesisitiza kuwepo na haki katika mchakato mzima kuelekea kwenye uchaguzi. Uchaguzi na mchakato wake uwe huru na amani na usiwe ni kichocheo cha uvunjifu wa amani.

  Baada ya viongozi kupatikana, watakula kiapo cha utii, na kujaza fomu Namba 5 ya BMT ya utekelezaji majukumu yao kama Kanuni ya 8 (4) inavyoeleza.

  Kadhalika, mara baada ya uchaguzi, Baraza limeagiza kuhusisha baadhi ya vifungu vya sheria ya Baraza ili viendane na katiba za TFF na wadau pamoja na kanuni zao.

  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

  0 0  0 0

  Na Veronica Simba - Dodoma .

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani amekutana na Ujumbe kutoka Kampuni ya Wind East Africa, yenye nia ya kuzalisha umeme kutokana na nguvu ya upepo mkoani Singida. 

  Ujumbe huo ulikutana na Naibu Waziri, hivi karibuni, Makao Makuu ya Wizara, mjini Dodoma.

  Katika Kikao hicho, Naibu Waziri aliuambia Ujumbe huo kuwa, Serikali inayo dhamira ya dhati kuwezesha jitihada na miradi mbalimbali ya umeme nchini; hivyo iko tayari pia kutoa ushirikiano kwa Kampuni husika ili iweze kuzalisha umeme wa upepo mkoani Singida.

  Hata hivyo, Dk. Kalemani aliutaka Ujumbe kutoka Kampuni hiyo, kuhakikisha wanakamilisha taratibu zote zinazostahili, ikiwa ni pamoja na kuwajibika kwa jamii inayozunguka Mradi husika, kwa kujenga mahusiano mazuri (Corporate Social Responsibility – CSR)

  Alimwagiza Kaimu Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kukaa na watendaji kutoka Kampuni husika na kukamilisha taratibu zote zinazotakiwa kwa mujibu wa sheria, ili Mradi uanze kutekelezwa mapema na hivyo kuwanufaisha wananchi wa Singida.

  Kampuni ya Wind East Africa, imedhamiria kuzalisha umeme wa megawati 100 kwa kutumia upepo, mkoani Singida.
   Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani (kushoto), akiwa katika kikao na Ujumbe kutoka Kampuni ya Wind East Africa (kulia). Wengine kushoto ni maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini na kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
   Kutoka kushoto ni Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga, Afisa Mwandamizi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi John Kabadi, Afisa kutoka TANESCO, Mhandisi Amos Kaihula na Afisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Christopher Bitesigirwe wakiwa katika kikao cha Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani na Ujumbe kutoka Kampuni ya Wind East Africa (Hawapo pichani).
  Ujumbe kutoka Kampuni ya Wind East Africa, wakiwa katika kikao na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani.

  0 0

  Wakazi wa Kijiji cha Ngulu kitongochi cha Mkongea wilaya ya Mwanga wamesema kuwa tatizo la maji limekuwa tatizo sugu kwa muda mrefu bila kutatuliwa hali inayosababisha ndoa nyingi kuvunjika. Mkazi wa kijiji hicho, Halima Miraji alisema kuwa tangu mwaka 2004 wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji ambapo kwa muda mrefu sasa maji yamekuwa yakitoka usiku wa manane tu.

  Halima alisema kuwa mfumo wa maji ulijengwa kwenye kijiji jirani cha Mgagani mwaka 1992 ambapo vijiji vyote viwili vilikuwa vikipata maji kutokea hapo. Hata hivyo, alisema wakati wa mafuriko, miundombinu iliharibika na hivyo kusababisha maji yapungue na ndipo viongozi wa vijiji hivyo viwili walipoamua kuwa maji yawe yanafunguliwa kwenye kijiji cha Ngulu nyakati ya mchana na kijiji cha Ngulu wakati wa usiku.

  “Kutokana na changamoto hiyo, wanawake tunalazimika kuamka usiku wa manane kuchota maji kwa kuwa kwa kawaida huwa yanakatika alfajiri,” alisema Halima. Alisema kwa kuwa wanawake ndio wanaochota maji usiku na badhi ya wanaume wachache ambao hawajaoa, kutokana na hilo alisema kuwa badhi ya wanawake walijikuta wakiianza uhusiano na wanaume jambo ambalo limefanya ndoa zao kuvunjika.

  Alisema kila mtu hulazimika kuweka ndo moja kwenye foleni ya maji iliyo na watu Zaidi ya hamsini kabla ya mzunguko kurudia mara ya pili, tatu na kadhalika jambo ambalo liliwafanya badhi ya wanawake kuingia kwenye vishawishi wakati wanasubiri kwenye foleni. Alisema kuwa changamoto nyingine, ni kuwa shughuli nyingi kama kilimo, biashara na kutunza familia zimekuwa zikizorota kwa kuwa wanakuwa wamechoka asubuhi baada ya kuchota bmaji usiku kucha.
  Mkuu wa Wilaya yaMwanga, mkoani Kilimanjaro, Aaron Mbogho.
  0 0  Afisa wa Kitengo cha Rasilimali watu Zantel, Maryam Khatri (kushoto) akitoa huduma ya chakula kwa Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Benoit Janin (kulia) katika tafrija ya futari iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Tafrija hiyo ilikuwa ni mahususi kwa ajili ya wafanyakazi na wadau wa kampuni hiyo.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Zantel wakijumuika kupata futari katika tafrija iliyoandaliwa na Kampuni hiyo katika kipindi hiki cha mfungo Mtukufu wa Ramadhani ambayo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akizungumza wakati wa tafrija ya futari maalumu iliyoandaliwa na Kampuni hiyo kwa ajili ya wafanyakazi na wadau mbalimbali katika kipindi hiki cha mfungo Mtukufu wa Ramadhani. Tafrija hiyo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu Zantel Joanitha Mrengo akizungumza wakati wa tafrija ya futari maalumu iliyoandaliwa na Kampuni hiyo kwa ajili ya wafanyakazi na wadau mbalimbali katika kipindi hiki cha mfungo Mtukufu wa Ramadhani. Tafrija hiyo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin (wa kwanza kushoto) akifurahia jambo na baadhi ya viongozi wa Kampuni hiyo wakati wa tafrija ya futari iliyoandaliwa na Zantel kwa ajili ya wafanyakazi na wadau mbalimbali katika kipindi hiki cha mfungo Mtukufu wa Ramadhani. Tafrija hiyo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam. 


  0 0


  Na Ripota wa Globu ya Jamii

  Zaidi ya wasanii kumi na mbili wa timu ya bongo fleva kusakata kabumbu na wadau wao wakubwa wa redio E-fm siku ya Jumamosi tarehe 25/06/2017 katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza katika mwendelezo wa kutambulisha masafa mapya ya EFM Radio ya 91.3 fm Mwanza.

  Kwa mujibu wa taharifa iliyotlewa na afisa uhisiano wa kituo hicho, Jesca Mwanyika amesema kuwa wakali hao wa bongo fleva na Efm redio watashiriki katika mtanange huo ili kuipa jamii hamasa katika kujikita kwenye michezo mbalimbali ili kuimarisha afya zao na kuepuka hatari ya kupata magojwa yasioambukizwa.

  “ mechi hii ni sehemu ya utaratibu wa E-fm ya kuwafikia wadau wao kama ilivyoada yao, vilevile kutoa wito kwa makampuni mbalimbali kuwekeza katika michezo ili kuhamasisha na kuvumbua vipaji vipya katika jamii” amesema Mwanyika .

  Mechi hiyo itaenda sambamba na mazoezi ya mbio za mwendo pole (jogging) zikiongozwa na Efm jogging club, Kubandika stika vyombo vya moto, na kuweka kifaa cha kuongeza masafa katika redio za daladala kwa madereva hamsini wa kwanza kufika uwanjani.

  0 0

  Wachezaji wa timu za taifa kutoka mataifa mbalimbali, wakishuka katika gari baada ya kuwasili katika lango la Lemosho kwa ajili ya kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuweka historia ya kucheza mchezo a kirafiki eneo la Kreta katika kilele cha Uhuru.
  Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania ,Twiga Stras ambaye kwa sasa anakipiga timu ya IFA Academy ya nchini Dubai,Rajvi Ladha akifurahia jambo na Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Geofrey Tengeneza.
  Wachezaji wa timu za Volcano fc na Gracier fc wakikamilisha taratibu kabla ya kuanza safari ya kupanda mlima Kilimanjaro kwa ajili ya mchezo wa kirafiki utakao pigwa June 26 mwaka huu katika kilele cha Uhuru.
  Afisa Uhusiano Mkuu wa TTB ,Geofrey Tengeneza akipata taswira ya pamoja na wachezaji hao.


  0 0

   Na Christina R. Mwangosi, MOHA 

  Jeshi la Magereza nchini ni moja kati ya Majeshi yaliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi yenye jukumu kubwa la msingi la kuwarekebishwa wafungwa wanaohukumiwa kwa makosa mbalimbali hapa nchini. 

  Katika taratibu za Urekebishaji wa wafungwa zipo stadi mbalimbali za kilimo, ufundi na uzalishaji ambazo zinatumika  kuwarekebisha  wafungwa ili hata pale wanapomaliza vifungo vyao na kurudi uraiani waweze kutumia ujuzi walioupata katika shughuli za uzalishaji na hivyo kujiletea maendeleo yao binafsi lakini kuchangia pia katika maendeleo ya nchi yetu.
   Mbali na jukumu hilo la msingi la Jeshi hilo, pia Jeshi hili limekuwa likijishughulisha na shughuli mbalimbali za uzalishaji mali ikiwemo shughuli za kilimo kwa ajili ya chakula kwa wafungwa, utengenezaji wa samani mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya ofisi na nyumbani, pamoja na utengenezaji wa viatu shughuli zinazofanyika katika Magereza yaliyopo hapa nchini.

  Aidha Jeshi la Magereza nchini lina fursa nyingi ambazo zikitumika vizuri zinaweza   kuwa na mchango mkubwa sana katika kukuza uchumi wa nchi yetu na hivyo kufikia malengo yetu ya kuwa na uchumi wa viwanda. Miongoni mwa fursa hizo ni pamoja na ardhi nyingi yenye rutuba inayofaa kutumika kwa kushughuli za kilimo na matumizi mengineyo ya uzalishaji vikiwemo viwanda.

  Kwa muda mrefu sasa jeshi la Magereza limekuwa likitumia kiwanda chake cha Utengenezaji wa Samani mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya Ofisi na hata nyumbani kilichopo katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam.
   Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza ambaye ndiye Mkuu wa Kiwanda cha Samani cha Ukonga cha Jeshi la Magereza nchini kilichopo jijini Dar es Salaam John Itambu anasema  kwa sasa kiwanda hicho kinafanya shughuli kubwa za aina mbili  ikwemo utengenezaji  wa samani mbalimbali  kwa ajili ya matumizi ya ofisini na nyumbani ikiwemo utengenezaji wa meza, viti, makabati,  vitanda,  meza za chakula na za ofisi,  pamoja na meza za chumbani maarufu kama ‘dressing table’.

  Kamishna Msaidizi Itambu anasema kiwanda hicho kinatengeneza samani hizo  kwa kutumia mbao za kawaida zile za asili zenye ubora wa kiwango cha juu na zile za henzerani yaani miti ya  minazi ambazo nazo pia zina mvuto wa hali ya juu pia ikiwemo ubora pia. 

  Anasema pamoja na utengenezaji wa samani kiwanda hicho pia kimekuwa kikijishughulisha na utengenezaji wa kazi za mikono ikiwemo mazulia, vikapu, ‘table mates’ pamoja na mazulia ya milangoni.
  Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza Itambu ambaye ndiye msimamizi wa shughuli za Kiwanda hicho anasema pamoja na kwamba Kiwanda cha Samani cha Magereza Ukonga kimekuwa kikitengeneza samani zenye ubora wa hali ya juu lakini siku zilizopita kulikuwa na changamoto ya ucheleweshaji wa ‘Oda’  ilikuwa mteja akiagiza samani za aina fulani inachukua muda mrefu kukamilishiwa mahitaji yake wakati mwingine na ubora unakuwa umepunguwa si kwa ubora aliokuwa ameuona kwenye shughuli za Maonyesho ya Sabasaba.

  Anasema kwa sasa Kiwanda hicho kimeondoa changamoto hiyo ya ucheleweshwaji na sasa  mteja anapoagiza mahitaji yake ya samani ziwe kwa matumizi ya Ofisi au nyumbani mteja anapata mahitaji yake kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu hakuna tofauti tena ya ubora anaotengenezewa  na ule aliouona kwenye Maonyesho ya SabaSaba.

  Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza John Itambu anasisitiza kuwa changamoto kubwa inayowakabili kwa sasa ni ile ya bei za mbao kwa ajili ya kutengeneza samani zao kupatikana kwa shida kwa kuwa mafundi wengi wa mitaani hununua mbao kwa kutumia fedha taslimu na bila kupewa risiti za EFD sasa pale Jeshi la Magereza linapofuata taratibu za kupewa risiti za EFD  wauzaji wa mbao hutoa kipaumbele kwa mafundi wale wa uraiani wenye fedha taslimu badala ya Magereza, hivyo ni muhimu kwa Mamlaka husika kuendelea kutoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kutumia mashine ama risiti za EFD.
  ‘‘Pamoja na kwamba mara nyingi wateja wanaona bei za bidhaa za kiwanda chetu cha samani ziko juu lakini wataalamu wetu wanachokiangalia ni kuzalisha bidhaa kwa kutumia mbao zenye ubora wa hali ya juu miti hasa ile ya asili, na ndio maana samani zetu zinadumu kwa muda mrefu huwezi kulinganisha ubora wake na bidhaa za mitaani’’ anasisitiza Mkuu wa Kiwanda hicho John Itambu.


  0 0

  Nteghenjwa Hosseah, Arusha.

  Wadaiwa sugu wa Kodi ya Majengo katika Jiji la Arusha watafikishwa Mahakamani mwanzoni mwa mwezi Julai endapo wataendelea kukaidi kutolipa Kodi hiyo katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka wa Fedha 2016/2017 unaomalizika Juni 30.

  Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo katika kikao chake na waandishi wa habari kuwukumbusha wananchi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi hiyo mapema kabla ya hatua kazi hazijachukuliwa wale ambao hawajalipa.

  Alisema wamiliki wote wa majengo wanatakiwa kulipa Kodi hiyo kwa mujibu wa Sheria lakini hali hairidhishi kwani wengi wao hawajajitokeza kulipa wakati Serikali inategemea Fedha hizo kwa ajili ya Kutekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo.

  Aliongeza kuwa muda uliowekwa kwa ajili ya malipo hayo unaelekea ukikongoni:  Juni 30 itakua ni mwisho na baada ya hapo Sheria kali za Kisheria zitaanza kuchukuliwa kwa wote watakaobainika kuiibia Serikali kwa kutolipa mapato ya majengo wanayoyamiliki.

  “Haiwezekani unamiliki nyumba halafu hutaki kuchangia kodi, ninatoa rai kwa wote kulipa kwa hiari kwa sababu baada ya hapo ni Faini ambayo ni mara tano ya kiasi kile ambacho ungetakiwa kulipa kwa sasa au kupelekwa Mahakami kwa mujibu wa Sheria.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo katika kikao kazi cha kuhamasisha ulipaji wa Kodi ya Majengo.
  Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Arusha Ndg. Apili Mbarouk akizungumza katika kikao na wanahabari cha kuwakumbusha wananchi kuhusu ulipaji wa Kodi ya Majengo.

  Baadhi ya wataalam waliohudhuria katika Kikao cha Mkuu wa Mkoa kuhamasisha uhamasishaji wa Kodi ya Majengo.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akizungumza na mkuu wa chuo cha ulinzi cha Taifa cha Rwanda Kamishina wa Polisi wa Rwanda Felix Namhoranye ofisini kwake makao makuu ya Jeshi la Polisi. Kamishina Namhoranye ni kiongozi wa msafara wa maafisa mbalimbali kutoka chuo cha ulinzi cha Taifa cha Rwanda ambao wapo nchini kwa ziara ya mafunzo. Picha na Hassan Mndeme – Jeshi la Polisi.

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akizungumza na maofisa wa polisi kutoka nchi mbalimbali za Afrika mashariki na Afrika magharibi ambapo wanasoma chuo cha ulinzi cha Taifa cha Rwanda hawapo picha. Kushoto ni mkuu wa chuo cha ulinzi cha Taifa cha Rwanda, Kamishina Felix Namhoranye na kulia ni Kamishina wa Polisi Jamii , Mussa Alli Mussa – picha na Hassan Mndeme – Jeshi la Polisi.

  Baadhi ya maafisa wa Polisi kutoka nchi mbalimbali za afrika mashariki na magharibi wanaosoma chuo cha ulinzi wa taifa cha Rwanda wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Tanzania makao makuu ya Jeshi la ( hayupo picha ) wakati wa ziara yao ya mafunzo hapa nchini. Picha na Hassan Mndeme – Jeshi la Polisi.

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Polisi kutoka nchi mbalimbali wanaosoma chuo cha ulinzi wa taifa cha Rwanda. Ujumbe huo unaohusisha maofisa wa Polisi kutoka nchi za Afarika mashariki na Afrika magharibi unaongozwa na Kamishina wa Polisi wa Rwanda Felix Namhoranye ambaye ndiye mkuu wa chuo cha ulinzi cha ulinzi cha Rwanda wapo nchini Tanzania kwa ziara ya kijifunza namna taasisi mbalimbali zinavyoendeshwa hapa Tanzania. Picha Hassan Mndeme – Jeshi la Polisi.

  0 0


  · Airtel wazindua vocha ya kiwango cha chini kabisa kwa wateja wa simu za mkononi

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua vocha mpya ya muda wa maongezi kwa wateja wake wa malipo ya awali nchini itakayowaongezea wateja wake TABASAMU pale wanapopiga simu au kuitumia kwa matumizi yoyote ya kuwasiliana au kujiunganisha kwenye vifurushi vya gharama nafuu.

  Vocha hiyo mpya ya TABASAMU kwa shilingi 200 inapatikana kwa wachuuzi wote wa vocha za Airtel na kuwawezesha wateja wa Airtel na watanzania wote watakaojiunga na Airtel kumudu gharama za mawasiliano wakati wowote kwa gharama nafuu zaidi

  Akiongea wakati wa uzinduzi, Meneja Masoko wa Airtel , Bi Aneth Muga alisema “ Leo tunajisikia fahari kuzindua na kuitambulisha sokoni vocha ya muda wa maongezi ya shilingi 200 itakayowapatia wateja Tabasamu na uhuru wa kuwasiliana na ndugu jamaa marafiki au wale wajasiliamali kuweza kuitumia kupanga mipango yao wakati wowote mahali popote kwa gharama nafuu”

  “Tunatambua mawasiliano ya simu ni muhimu katika kuendesha shughuli zetu za kila siku na hivyo kuboreshwa kwa viwango vya vocha kutasaidia sana kuchochea upatikanaji wa huduma ya mawasiliano kwa wote. Tunataka kuendelea kutoa huduma bora za kibunifu na zenye kukidhi mahitaji ya wateja wetu huku tukiwawezesha kutatua changamoto zao za kila siku”. Alieleza Bi, Muga

  “Tunaamini kwa kuwezesha upatikanaji wa vocha za shilingi 200 sokoni tumewawezesha zaidi ya watanzania milioni 10 kuunganishwa na huduma za mawasiliano na kufurahia ofa mbalimbal zinazotolewa na Airtel. Aliongeza muga

  Ili kuingia vocha ya muda wa maongezi mteja atapiga *104* kisha kuingiza namba zilizokwanguliwa na kubonyesha alama ya reli # na kisha OK. Vocha hiyo itaingia moja kwa moja kwenye Salio lake la kupiga simu na mteja ataamua kuitumia kwa kupiga simu au kujiunga na kifurushi cha shilingi 200 kwa kupiga *149*99#.
  Meneja Masoko ya Airtel, Anethy Muga (kulia) na Meneja wa chapa wa Airtel, Arnold Madale (kushoto) wakionyesha vocha mpya ya Airtel Tabasamu itakayouzwa kwa bei ya shilingi mia mbili tu. Katikati  ni Meneja  Uhusiano wa Airtel , Jackson Mmbando .
  Meneja Masoko ya Airtel , Anethy Muga( kulia) akiongea wakati wa uzinduzi wa vocha mpya ya Airtel Tabasamu ambayo ni maalumu kwa wateja wa Airtel wa malipo ya awali nchini. (kushoto) Meneja wa chapa wa Airtel , Arnold Madale na (katikati) Meneja Uhusiano wa Airtel , Jackson Mmbando . Vocha hiyo itapatikana kuanzia sasa kupitia maduka yote ya Airtel , wakala na wachuuzi wa vocha za Airtel nchi nzima.

  Meneja Uhusiano wa Airtel , Jackson Mmbando (kati) akitoa ufafanuzi juu ya vocha mpya ya Airtel Tabasamu ambayo ni maalumu kwa wateja wake wa malipo ya awali nchini. (kushoto) Meneja wa chapa wa Airtel , Arnold Madale na Meneja Masoko ya Airtel , Anethy Muga (kulia). Vocha hiyo itapatikana kuanzia sasa kupitia maduka yote ya Airtel , wakala na wachuuzi wa vocha za Airtel nchi nzima.

  0 0

  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Kiongozi wa Msafara na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kutoka Bunge la Msumbiji, Mhe. Lucas Jeremias (katikati) pale ugeni kutoka kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kutoka Bunge la Msumbiji ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, kulia ni Mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Beatriz Chaguala.
    Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akisisitiza jambo mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kutoka Bunge la Msumbiji uliomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, katikati ni Kiongozi wa Msafara na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kutoka Bunge la Msumbiji, Mhe. Lucas Jeremias na kulia ni Mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Beatriz Chagula.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akizungumza  mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kutoka Bunge la Msumbiji ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, wa pili kushoto ni Kiongozi wa Msafara na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kutoka Bunge la Msumbiji, Mhe. Lucas Jeremias.

  (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

  0 0

  Rais Dkt. John Pombe Magufuli.


  0 0

  Globu ya Jamii imepokea taarifa ya kifo cha shabiki maarufu wa timu ya Yanga Ally Mohamed almaarufu kwa jina la Ally Yanga. Taarifa zinaeleza kuwa Ally Yanga amefariki Dunia mapema leo katika ajali ya gari eneo la kijiji cha Chipogoro wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.  Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi-Amin.

  UPDATES. 

  Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa amethibitisha kifo cha aliyekuwa shabiki maarufu wa klabu ya soka ya Yanga Ally Yanga kilichotokea leo katika ajali ya gari aina ya Rav4 eneo la Chipogolo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.


  Ally Yanga ambaye pia ni mkereketwa wa Mwenge wa Uhuru alikutwa na mauti akiwa katika gari la kampuni ya Faidika ambalo lilikuwa kwenye shughuli zake za promosheni na SIO KWAMBA alikuwa kwenye msafara wa Mwenge kama inavyoenezwa.

  Ally aliyezaliwa mkoani Shinyanga Machi 1, mwaka 1984 katika familia ya watoto sita, kabla ya umauti wake inafahamika alikuwa anaishi Yombo Vituka, Dar es Salaam.


  Lakini tangu baada ya uchaguzi Mkuu Novemba 2015, Ally Yanga ameadimika viwanja vya soka kutokana na kujikita zaidi kwenye shughuli za Chama cha Mapinduzi CCM.
  Pichani juu na chini ni gari iliyopelekea kifo cha Shabiki huyo wa Yanga,Ally yanga


  0 0

   Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

  Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni na mfanyabiashara wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka manne ya kuomba na kupokea rushwa.

  Mwendesha Mashtaka kutoka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Emmanuel Jacob amewataja washtakiwa hao kuwa ni  Omary Mohammed Abdallah ambaye ni Hakimu na mfanyabiashara George Joseph Barongo.

  Wakisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Respicious Mwijage, imedaiwa kuwa, kati ya January na Februari 12/ 2017 hakimu Omary alitenda kosa.

  Imedaiwa kuwa, siku hiyo Omary akiwa muajiriwa wa Mahakama ya Mwanzo Kinondoni aliiomba rushwa  ya sh. 205,000 kutoka kwa Agnes Nyenza kwa ajili ya kumsaidia kwenye kesi yake ya mirathi ya namba 570/2016 ambayo ilikuwa mbele yake.

  Katika shtaka la pili Hakimu Omary anadaiwa kupokea rushwa ya kiasi hicho cha fedha Kutoka kwa Nyenza ili aweze kumsaidia katika kesi hiyo.

  Mahakama imeendelea kuambiwa kuwa, kati ya Februari na Machi mwaka huu, jijini Dar es salaam, Hakimu Omary akiwa na mfanyabiashara Barongo waliomba rushwa ya sh. Milioni moja kutoka kwa Nyenza kwa ajili ya kumsaidia katika kesi hiyo ya mirathi.

  Wakili wa Takukuru aliendelea kuieleza mahakama kuwa, siku na mahali hapo watuhumiwa hao wote kwa pamoja walipokea rushwa ya sh. 500,000 kwa ajili ya kumsaidia Agnes Nyenza kwenye kesi yake ya mirathi ambayo iko mbele ya hakimu huyo Omary Mohammed wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni.

  Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na wako nje kwa dhamana hadi Julai 4 mwaka huu.

  0 0

       Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amezindua zoezi la ugawaji wa mabeseni yenye vifaa tiba 200 yaliyotolewa na Ubalozi wa Kuwait nchini kwa ajili ya wanawake wajawazito katika hospitali ya Mbagala Rangi Tatu  na Kituo cha Afya cha Mbagala Round Table katika wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam.


  Lengo la mpango huo ni kutoa mabeseni hayo zaidi ya 1,000 kwa wanawake wajawazito wasio na uwezo kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar kama hatua ya kukabiliana na vifo vya watoto na wanawake wajawazito nchini.


  Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa vifaa tiba hivyo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa mpango huo utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kupambana na vifo vya watoto na wanawake wajawazito kwa kukosa vifaa tiba kutokana na umaskini unaowakabili.


  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kwa maeneo yaliyopatiwa mabeseni yenye vifaa tiba yahakikishe vifaa hivyo vinatolewa kwa wanawake wajawazito ambao baadhi yao wanakata tamaa kwenda kujifungulia kwenye hospitali au kwenye vituo vya afya  kwa kukosa vifaa hivyo kwa sababu ya umaskini.


  Amesema mkakati uliopo wa Serikali ni kuhakikisha huduma za afya nchini zinaendelea kuboreshwa hasa huduma ya mama na mtoto ambapo kutokana na umuhimu wa sekta ya afya Serikali imetenga fedha za kutoka katika bajeti ya mwaka 2017/2018.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania wakiangalia mbabeseni yanya vifaa vya kusaidia wakina mama kujifungua yaliotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100.

   Baadhi ya mabeseni yenye vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati wa kujifungua
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Bi.Arafa Nurdin wakati alipotembelea wodi ya wazazi ya hospitali ya Mbagala Rangi 3 kabla uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mbagala Rangi Dkt. Joseph Kiani wakati alipotembelea wodi ya wazazi ya hospitali ya Mbagala Rangi 3 kabla uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100.


older | 1 | .... | 1757 | 1758 | (Page 1759) | 1760 | 1761 | .... | 3348 | newer