Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

Redds Miss Kanda ya Mashariki kufanyika Juni 29 mjini Morogoro

$
0
0
Na Mwandishi wetu

MASHINDANO ya Redds Miss Kanda ya Mashariki yatafanyika Juni 29 Nashera Hotel mkoani Morogoro kwa kushirikisha jumla ya warembo 14. 

Mkurugenzi wa kampuni ya Nikalex Ltd, Alex Nikitas aliwataja warembo hao ambapo wapo kambini hotel ya Starwing Hotel chini ya mkufunzi, Kudra Lupatu kuwa ni Muzne Abduly (19), Ummy Mohamed (21), Sabra Islam (19) na Diana Laizer ambao wote wanatoka Morogoro.

Warembo ambao wanatoka Mtwara kwa mujibu wa Nikitas ni Ivony Stephen (22), Purkeriah Ndovi (21), Zulfa Semboja (19) na wa Lindi ni Janeth Awet (19), Zainab Shaaban (23) na Sophia Mganga (21). Wanaotoka mkoa wa Pwani ni Elizabeth Perty (22), Suleiyah Abdi (22) na Easther Albert (20).

Nikitas alisema kuwa maandalizi ya mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Redds Original, Dodoma Wine, CXC Africa, Nyumbani Park, Usambara Safari Lodge, Michuzi Blog, Clouds Media Group, Chilakale Resorts, Nashera Hotel, Starwing Lodge, Simple car Rental, Big Solution na Mikocheni Resort Centre yamekwisha kamilika na warembo watatembelea sehemu mbali mbali mkoa wa Morogoro na kufanya kazi za jamii.

“Tumejiandaa vziuri na warembo kwa sasa wapo kambini wakijifua kwa ajili ya shindano hilo, warembo watatu wataiwakilisha kanda hiyo katika mashindano ya Redds Miss Tanzania ambayo yatafanyika mwezi Septemba,” alisema Nikitas.

Alisema kuwa wamejipanga vilivyo kwa ajili ya mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutoka kwa warembo wote.

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA) KANDA YA MASHARIKI WATOA SEMINA YA MAWASILIANO KWA WADAU WAO KATIKA WILAYA YA BAGAMOYO

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahamed Kibozi akihutubia wakati wa uzinduzi rasmi wa semina ya wadau wa huduma za Mawasiliano iliyowalenga wawakilishi wa jumuiya mbalimbali za vijiji na vitongoji vya Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.aliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzanizi(TCRA ) Kanda ya Mashariki hivi karibuni.Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma za Mawasiliano wa TCRA, Dk.Raynold Mfungahema na Kushoto ni Meneja wa Kanda ya Mashariki Mhandisi Oscar Mwanjesa.
Mkurugenzi wa Huduma za Mawasiliano Dk.Raynold Mfungahema akitoa mada ya Haki na wajibu wa watumiaji wa huduma za mawasiliano wakati wa semina ya watumiaji wa huduma za mawasiliano iliyofanyika katika chuo cha sanaa cha Bagamoyo kwa kuwashilikisha wawakilishi wa jumuiya mbalimbali za vijiji na vitongoji vya Wilaya ya hiyo.
Afisa wa Idara ya Posta wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA,Bi,Ccilia Sylvester,akitoa mada juu ya mfumo mpya wa anuani za posta semina ya wadau wa huduma za Mawasiliano iliyowalenga wawakilishi wa jumuiya mbalimbali za vijiji na vitongoji vya Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.aliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzanizi(TCRA ) Kanda ya Mashariki wakiwakatika foleni ya kujiandikisha wakati wakuingia katika semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha sanaa Bagamoyo.

SAFARI LAGER YAKABIDHI RUZUKU KWA WAJASILIAMALI KANDA YA KASKAZINI MKOANI ARUSHA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongella (wa pili kushoto) akimkabidhi mjasiliamali,Veronica Tarimo Mashine ya kusaga  vyakula vya kuku wakati wa hafla ya kukabidhi ruzuku za wajasiliwamali wa Safari Lager Wezeshwa  kanda ya Kaskazini ilifanyika katika viwanja vya General Tyre Arusha mwishoni mwa wiki.Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo na Meneja mauzo wa Kanda  ya Kaskazini, Wilderson Kitio.
Mjasiliamali,Judith Tarimo(kushoto) akiangalia zawadi yake mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongella(wa pili kulia) wakati wa hafla ya kukabidhi ruzuku za wajasiliwamali wa Safari Lager Wezeshwa  kanda ya Kaskazini ilifanyika katika viwanja vya General Tyre Arusha mwishoni mwa wiki.Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongella ( kushoto) akimkabidhi mjasiliamali,Joyce Mmali Mashine ya kusaga   wakati wa hafla ya kukabidhi ruzuku za wajasiliwamali wa Safari Lager Wezeshwa  kanda ya Kaskazini ilifanyika katika viwanja vya General Tyre Arusha mwishoni mwa wiki.Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo na Meneja mauzo wa Kanda  ya Kaskazini, Wilderson Kitio.

Sheha aliekwagiwa Tindikali Zanzibar aanza kupatiwa matibabu nchini India

$
0
0
Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Miot Mjini Chenai Nchini India leo wanaanza kumfanyia huduma za matibabu Sheha wa shehia ya Tomondo Mohd Omar Said { Kidevu } baada ya kukamilisha uchunguzi wa matatizo yake kufuatia kumwagiwa Tindi kali karibu mwezi mmoja uliopita.

Sheha Kidevu aliyefika Nchini humo Tarahe 21 na kufanyiwa vipimo vyote vilivyohusika anaanza matibabu kwa hatua ya kupandikizwa ngozi katika sehemu zake alizoathirika kutokana na kuungua kwa maji ya Tindi kali hiyo.

Akizungumza kwa njia ya Simu Daktari aliyeambatana na Sheha huyo Dr. Said Ali Said { Mkarafuu } alieleza kwamba Madaktari wa India wameelezea kuridhishwa kwao na hatua kubwa iliyochukuliwa na Madaktari wa Zanzibar ya kumpatia tiba sahihi mgonjwa huyo.

Dr. Said alisema Madaktari hao Bingwa wa India wamekaririwa wakisema kwamba wamepata matumaini ya huduma hizo alizofanyiwa Zanzibar ambazo zinawapa hatua ya pili ya kuendelea na Tiba ya Sheha Kidevu.

“ Amefanyiwa uchunguzi wa vipimo vyote na kubainika kwamba jicho lake Sheha Kidevu ambalo liliwahi kupata athari kidogo limewahiwa na Madaktari wa Zanzibar wakiongozwa na Dr. Gang na Dr. Slim na hivi sasa liko katika hali ya kawaida “. Alifafanua Dr. Said Mkarafuu.

Alifahamisha kwamba Madaktari hao wa Hospitali ya Miot Mjini Chenai Nchini India wameelezea matarajio yao kwa mgonjwa huyo kuendelea na huduma za matibabu kwa haraka licha ya Madaktari hao kutokutaja huduma hizo zitamalizika katika kipindi gani.

Kabla Sheha Mohd Kidevu alikuwa akipatiwa huduma za matibabu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kwa takriban Mwezi Mmoja sasa kutokana na kuathirika sehemu ya kulia ya kifua chake, Bega pamoja na baadhi ya maeneo ya mapaja.

Sheha huyo wa Shehia ya Tomondo Mohd Omar Said Kidevu alipatwa na mtihani huo wa kumwagiwa Tindi kali { Acid } na mtu asiyejuilikana Usiku wa tarehe 22 Mei Mwaka huu wa 2013 akiwa katika harakati za kuteka Maji mara baada ya kurejea kwenye Ibada ya sala ya Ishaa.

Vitendo vya matumizi mabaya ya tindikali vinavyofanywa na baadhi ya watu vinaonekana kuanza kuwatia hofu wananchi na hasa baadhi ya Viongozi katika maeneo mbali mbali hapa Zanzibar.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
24/6/2013.

Prof. Tibaijuka azungumza na wakazi wa Makongo juu kuhusu uboreshaji wa mji huo

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka akizungumza na wakazi wa Makongo juu kuhusu uboreshaji wa mji huo kwa huduma muhimu za kimji. Kulia kwa Mhe. Tibaijuka ni Diwani wa Kata hiyo Bw. Deusdedit Mtiro na kushoto kwake ni Katibu wa mradi huo kutoka Wizarani bibi Neema Munuo.
Waziri wa Ardhi wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Makongo juu Bw. Joackim Shirima wakati akitoa maoni yake kuhusu uboreshaji wa mji huo.
Wakazi wa Makongo juu wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka (hayupo pichani) alipozungumza nao kuhusu uboreshaji wa mji huo. Miongoni mwa wakazi hao ni Waziri wa zamani katika Serikali zilizotangulia awamu ya sasa Bw. Ibrahimu Kaduma (wa pili kutoka kulia mstari wa mbele).
Wakazi wa Makongo juu wakiangalia michoro ya ramani inayoonesha mpango wa kuboresha mji huo wakati wa kikao kati yao na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka. (picha zote na Rehema Isango wa Wizara ya Ardhi)

Maandalizi tamasha Grand Malt Tanzania Open Film Festival yazidi kunoga

$
0
0

HUKU zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufanyika kwa Tamasha la Wazi la Filamu Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ ambalo litafanyika katika Viwanja vya Sahara jijini Mwanza, maandalizi yake yamezidi kupamba moto.

Mratibu wa Tamasha hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sophia Records, Musa Kissoky, alisema kwa sasa kila kitu kimekamilika na kinachosubiriwa ni kuanza kwa tamasha hilo Jumatatu ijayo.

Kissoky alisema, tamasha hilo ambalo litakuwa la bure kwa watu wote na kushirikisha mastaa wa filamu hapa nchini, litakuwa la aina yake kwani vitu vitakavyofanyika vitakuwa si vya kawaida.

“Kwa sasa maandalizi yamekamilika kwa asilimia 90, yaani tunaleta kitu tofauti ambacho watu watashangaa, ndio maana mpaka sasa wengi wanapigwa na bumbuwazi kuhusu kile tutakachofanya siku hiyo,” alisema.

Naye Meneja wa kinywaji cha Grand Malt walio wadhamini wakuu wa tamasha hilo, Consolata Adam, alisema wameamua kufanya kweli zaidi kwani wanataka kuona Watanzania wanapata kitu chenye uhakika.

“Tumejipanga katika hili na wala hatutanii kwani tunataka kuwawezesha wakazi wa Mwanza na maeneo ya jirani kuhudhuria tamasha hili kwa wingi . Tunawakaribisha watu wote wenye mapenzi na filamu zetu za Tanzania kufika na kushuhudia tamasha hili ambalo mwaka huu limeboreshwa zaidi,” alisema Consolata.

Naye Meneja Habari na Mawasiliano wa TBL, Edith Mushi, alisema, kutokana na ubora wa kinywaji cha Grand Malt hata tamasha hilo litakuwa la aina yake na litakaloiteka mikoa yote ya Kanda ya Ziwa.

“Tumeona jinsi wananchi wanavyozipenda filamu za Tanzania, maarufu kama ‘Bongo Movies’ na jinsi walivyo na kiu ya kuwaona wasanii wa filamu ana kwa ana, sasa kazi kwao kuwashuhudia na kuona tamasha bora zaidi,” alisema.

Tamasha la Filamu la Grand Malt linatarajiwa kuanza Julai 1-7, mwaka huu huku kukiwa na filamu mbalimbali zitakazooneshwa katika kipindi hicho. Filamu zote hizo ni kutoka Tanzania.

Wasanii wakali wa Bongo Muvi wakiwemo Aunty Ezekiel, Vicent Kigosi ‘Ray’, Jacqueline Wolper, Irene Uwoya, Jacob Steven ‘JB’, Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’na  Issa Mussa ‘Cloud’ ni baadhi ya wasanii walioahidi kufanya kweli pia katika tamasha hilo.


Tamasha hilo la filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

BALOZI WILFRED NGIRWA AANZA RASMI UENYEKITI WA BARAZA LA FAO

$
0
0
Leo asubuhi Balozi Wilfred Joseph Ngirwa amepokelewa kwa shangwe na bashasha alipoketi rasmi, kwa mara ya kwanza, kwenye kiti chake tayari kufungua na kuendesha Kikao cha 147 cha Baraza la FAO.

Balozi Ngirwa alianza kwa kuwashukuru wanachama wote wa FAO kwa kumchagua kwa asilimia 95 kwenye Mkutano Mkuu wa 38 wa FAO hapo tarehe 21 Juni, 2013 na baadaye kumteua rasmi kwenye nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa Baraza la FAO (Independent Chairperson of the FAO Council) hapo tarehe 22 Juni, 2013 kama taratibu na kanuni zinavyotaka.

Balozi Ngirwa aliahidi kuitumikia nafasi hiyo kwa uaminifu na kujituma, akiweka mbele maslahi na malengo ya FAO. Aidha, Balozi Ngirwa aliomba ushirikiano kutoka kwa Wajumbe wa Baraza, na nchi wanachama wote wa FAO kwa ujumla.

Katika mahojiano yetu awali, Balozi Ngirwa alimshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa imani kwake na hata kukubali Tanzania impendekeze, kama kanuni zinavyotaka, kama mgombea wa nafasi hiyo. 

Aidha, alimshukuru kwa dhati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Ben Membe (MP), na Wizara yake kwa ujumla, kwa kampeni nzuri na za mafanikio makubwa. Pia alimshukuru sana Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Eng. Christopher K. Chiza (MP), pamoja na Wizara yake kwa juhudi za hali na mali hadi kupatikana kwa ushindi.

Pamoja na shukrani kwa wengine wengi, Balozi Ngirwa alimshukuru Balozi na Watumishi wote wa Ubalozi wa Tanzania Roma kwa kujitolea kwa dhati kufanya kampeni pevu katika anga za kidiplomasia kwa kipindi chote cha miezi 14 tangu jina lake lilipopendekezwa kwa mara ya kwanza katika duru za FAO na kufungua mlango wa kuungwa mkono na makundi yote, kuanzia na kundi la Africa (FAO Regional Group for Africa) kwenye Mkutano uliofanyika huko Congo-Brazzaville mwezi April, 2012.

Aliahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa Ubalozi katika kipindi chote cha uwepo wake kwenye nafasi hiyo, pia akitegemea ushirikiano wa Ubalozi wa Tanzania Roma kumwezesha kutekeleza vyema majukumu yake.

Balozi Ngirwa anakuwa mwafrika wa pili kuchukua nafasi hiyo tangu mwaka 1945 wakati lilipoanzishwa Shirika hili la Chakula la Umoja wa Mataifa. Balozi Ngirwa, mtaalam wa masuala ya kilimo na chakula, ana uzoefu mkubwa kupitia utumishi wake uliomfikisha hadi ngazi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Tanzania. Baadaye aliteuliwa na Mhe. Rais kuja Roma kama mwakilishi wetu wa kudumu kwenye mashirika ya chakula ya Umoja wa Mataifa, ambapo alipata pia uzoefu mkubwa katika diplomasia kwa miaka 6, hadi alipostaafu mwezi Machi, 2012.

Ni matumaini yetu kuwa Watanzania tutampa ushirikiano na kumsaidia kuiwezesha Tanzania kufaidika na kuendeleza vyema maslahi yake katika mashirikiano na mashirika haya ya Umoja wa Mataifa jijini Roma.
Balozi Ngirwa akiendesha Mkutano wa 147 wa Baraza la FAO uliofunguliwa leo asubuhi. Pembeni yake ni Katibu Mkuu wa Baraza na Mkutano Mkuu wa FAO.
Wajumbe na wahudhuriaji (observers) wa kikao cha 147 cha Baraza la FAO leo asubuhi katika Red Room, makao Makuu ya FAO.
Balozi Eng. Dr. James Alex Msekela (wa pili kulia walioketi) akiwa na Mwambata Kilimo na msaidizi wake Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo Roma, Bw. Ayoub Mndeme, wakishiriki kwenye kikao cha 147 cha Baraza la FAO leo asubuhi.

MAVETERANI WANOGESHA BONANZA LA MBUNGE UKONGA

$
0
0
BONANZA la Maveterani jimbo la Ukonga limefanyika mwishoni mwa wiki na kushuhudia maveterani waalikwa kutoka Sinza timu yenye Star wengi wa zamani ya Golden Bush wakiibuka mabingwa wa mchezo wa Soka.

Bonanza hilo lililoandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo Eugene Mwaiposa lilizikutanisha timu zipatazo kumi za jimbo hilo na timu mbili zilialikwa kwenye Bonanza hilo.

Ushindani kwenye michuano hiyo ulikuwa mkali ambapo wenyeji wa mashindano hayo timu ya Pugu ilitinga fainali na kupambana na timu ya Golden Bush ya Sinza iliyojaza nyota kama Salum Sued Kusi, Abuu Mtiro na Amani Simba.

Hata hivyo haikuwa kazi rahisi kwa mastaa hao kupata ubingwa huo kwa vijana wa pugu hadi pale ilipofikia changamoto ya mikwaju ya Penalt 5, ambapo Golden Bush walipata Penalt saba kwa 6, kutokana na kumaliza muda wote wa mchezo bila kufungana.

Kivutio kikubwa kwenye bonanza hilo kulikuwa kwa mwanamuziki wa kizazi kipya KR Mulla, alipoingia kwa upande wa timu ya Golden Bush na kufanikiwa kuunganisha kross kali na kupiga bao ambapo alishangalia kwa Staili ya mapanga Shaa! na kurusha miguu juu.
Mbunge wa jimbo la Ukonga Eugene Mwaiposa akimkabidhi jezi kapteni wa timu ya vijana wa CCM wa jimbo hilo Abubakari (fulana ya bluu) wakati walipoalikwa kwenye bonanza la maveterani wa jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga Eugene Mwaiposa akikagua timu za Kigogofresh na Tumaini kabla ya kuanza kwa mpambano wao kwenye bonanza la Maveterani lililoandaliwa na mbunge huyo mwishoni mwa wiki eneo la Pugu Kajiungeni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, matokeo ya mchezo huo Kigogo ilishinda 2 kwa 1.
Wazee wakichuana vikali kumkimbiza kuku.
Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Bombani Pugu akishangilia mara baada ya kukamata kuku aliyeshindaniwa na Wazee wa eneo hilo ikiwa ni miongoni mwa michezo iliyofanyika kwenye bonanza lililoandaliwa na mbunge wa jimbo la Ukonga Eugene Mwaiposa mwishoni mwa wiki.


Kiwanda cha nywele cha Darling Hair chatakiwa kupigwa kufuli

$
0
0
 Barua toka kwa Mganga mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke iliyopelewa kwa Uongozi wa Kiwanda hicho.
 Mgambo wa Manispaa ya Temeke wakisubiri kufunguliwa kwa Geti la Kiwanda cha nywele cha Darling Hair kilichopo Maeneo ya Pugu Road,jijini Dar.
Sehemu ya Wafanyakazi wa kiwanda hicho wakiendelea na kazi wakati wengine walikuwa wakitolewa nje kwa kuzidiwa na hewa nzito iliopo ndani ya kiwanda hicho.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kiwanda hicho wakiwa wamembeba mwenzao aliekuwa amepoteza fahamu kutokana na kukosa hewa wakati akiwa anaendelea na kazi ndani ya kiwanda hicho.

Vodacom kukabidhi zawadi ligi kuu Julai 3

$
0
0
Meneja Uhusiano wa nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim, Akizungumza na waandishi wa habari ( Hawapo pichani) Wakati akitangaza tarehe ya utoaji wa zawadi za ligi kuu ya Vodacom zitakazo tolewa julai 3 jijini Dar es Salaam, Zawadi hizo ni za jumla ya shilingi Milioni 200 zitakazotolewa kwa vipengele mbalimbali kwa timu za ligi hiyo.
Waandishi wa habari wakimsikiliza meneja Uhusiano wa nje wa kampuni ya Vodacom Tanzania Salum Mwalim ( Hayupo pichani) Wakati akitangaza tarehe ya utoaji wa zawadi za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara zitakazo tolewa julai 3 jijini Dar es Salaam. 

Wadhamini wakuu wa Ligi kuu soka Tanzania Bara Kampuni ya Vodacom imetangaza kuwa itakabidhi zawadi kwa washindi wa ligi hiyo Julai 3 jijini Dar es salaam.

Vodacom imekuwa ikisubiri kumalizika kwa hekaheka za timu ya taifa - Taifa Stars za kusaka nafasi ya kushiriki fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil hali iliyochelewesha tukio la kukabidhi zawadi hizo kwa mabingwa pamoja na wote waliofanya vema katika msimu wa 2012/2013 "Tulikuwa tukisbiri wakati muafaka wa kufanya hivyo kwani tangu kumalizika kwa ligi mwezi uliopita mwelekeo wa taifa ulikuwa ni kuipa ari na nguvu timu yetu ya taifa katika kusaka tiketi ya kufuzu kushiriki fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil." Alisema Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.

Mwalim amesema maandalizi yote ya zoezi hilo yamekamilika kwani hakukuwa na sababu nyingine ya kutokabidhi zawadi mara tu baada ya ligi kumalizika zaidi ya timu ya taifa - taifa stars.

Mwalim amesema hafla ya utoaji wa zawadi inahitaji ushiriki wa wadau mbalimbali wa soka nchini wakiwemo wachezaji wa vilabu ambao miongoni mwao wamo kwenye kikosi cha Stars, viongozi wa TFF na walimu wa timu ya taifa ambao wote hao kwa pamoja walikuwa na jukumu moja tu la kuhakikisha Stars inafuzu kwenda Brazil na hivyo isngekuwa vema kuingiza maandalizi ya jambo jingine katikati ya juhudi hizo.

Mwalim ametumia nafasi hiyo kuvishukuru vilabu pamoja na Shirikisho la Soka - TFF na kamati ya ligi kwa uvumulivu wao wakati wote ambapo Vodacom ikisubiri kupatikana kwa muda mufaka wa kukabidhi zawadi.

"Tendo la kukabidhiwa zawadi ni moja ya matendo makuu kabisa kwa yeyote anaeshinda, tumeona uvumilivu mkubwa na wenzetu walituelewa wakati tulipowashauri kutoa nafasi kwa Stars bila kuharibu concetratiuon ya taifa. Tumeonesha umoja wetu."

Mbali ya mabingwa timu ya Yanga ambayo watakabidhiwa kitita cha fedha cha Sh 70 Milioni zinahusisha pia zawadi za wachezaji na wadau wengine mmoja mmoja walioonesha umahiri kwenye maeneo yao.

Vodacom itakabidhi zawadi za fedha taslimu takribani Sh. 200 Milioni kwa mabingwa Yanga na Azam, Simba na Kagera Sugar zilizoshika nafsi ya pili hadi ya nne.

Wengine watakaonufaika na zawadi za fedha ni Mlinda mlango bora, mwamuzi bora, mwalimu bora, timu iliyoonyesha nidhamu na mfungaji bora.

Vodacom imekuwa ikiidhamini ligi kuu ya soka ya Tanzania bara kwa zaidi ya misimu mitano sasa huku ikiiwezesha ligi hiyo kuimarika na kuwa ya ushindani kadri miaka inavyosonga mbele.

TFF YATOA RAMBIRAMBI MSIBA WA MATHIAS KISSA

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mchezaji wa zamani wa timu za Cosmopolitan na Taifa Stars, Mathias Kissa (84) kilichotokea leo alfajiri (Juni 24 mwaka huu) kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

Msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani enzi zake, Kissa akiwa na timu ya Tabora alitamba katika michuano ya Kombe la Taifa wakati huo ikiitwa Sunlight Cup. Alikuwa akicheza katika nafasi ya ulinzi.

Baadaye alijiunga na Cosmoplitan ya Dar es Salaam, na pia kuwa mchezaji wa timu ya Taifa ambapo enzi zake akiwa na wachezaji kama Yunge Mwanansali wakiiwakilisha Tanganyika na baadaye Tanzania Bara walitamba katika michuano ya Kombe la Chalenji wakati huo ikiitwa Gossage, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.

Kissa ambaye alipata tuzo ya mchezaji bora wa karne kwa upande wa Tanzania, tuzo inayotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) alikuwa ndiye mchezaji msomi kupita wote wakati akichezea timu ya Taifa akiwa amehitimu elimu ya Darasa la Kumi.

Kwa mujibu wa binti yake, Erica, marehemu ambaye pia aliwahi kuwa mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi (stroke) alioupata miaka mitano iliyopita, na kisukari. Baadaye alipata kidonda ambacho ndicho kilichosababisha kifo chake.

Msiba uko nyumbani kwa marahemu, Masaki, Mtaa wa Ruvu karibu na Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST). Maziko yatafanyika keshokutwa, Jumatano (Juni 26 mwaka huu) kwenye makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Kisa, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na klabu ya Cosmopolitan na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Mungu aiweke roho ya marehemu Kisa mahali pema peponi. Amina

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

MH. ZITTO KABWE KUHUDHURIA TAMASHA LA ASPEN IDEAS 2013 NCHINI MAREKANI

$
0
0

MBUNGE WA Kigoma Kaskazini, Ndugu Zitto Z. Kabwe amealikwa kuhudhuria tamasha la tisa la Aspen la mwaka huu huko Marekani. Tamasha hilo linawaleta pamoja watu mashuhuri kutoka nyanja mbalimbali duniani.


Lengo kubwa la tamasha ni kuwawezesha washiriki kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali ambayo wana uzoefu nayo.

Ushiriki katika tamasha hilo utamwezesha Zitto kukutana na kubadilishana mawazo na magwiji wa masuaka mbalimbali duniani. Ratiba iliyotolewa na waandaaji inaonyesha kuwa tamasha hilo litakaloendeshwa kwa muda wa wiki moja kuanzia Juni 26, limegawanyika katika sehemu mbili.

Kama ilivyo kwa miaka iliyopita, tamasha hilo litahusisha majadiliano ya pamoja, ya vikundi pamoja na ya mtu mmoja mmoja. Pia washiriki watakuwa na fursa ya kukutana na wabunifu na wataalamu wa nyanja mbalimbali na kubadilishana nao mawazo.

Mijadala itahusu mambo ya kijamii, siasa, mahusiano ya kimataifa, watoto na vijana pamoja na namna ya kukabiliana na changamoto kubwa zinazoikabili dunia hivi sasa.

Vile vile kutakuwa na maonyesho ya vitabu pamoja na mikutano na waandishi wa habari maarufu kutoka Marekani. Washiriki pia watapata fursa ya kujifunza kupitia filamu na michezo ya kuigiza. “Nimefurahi kupata mwaliko huu na nimekubali kushiriki kwa sababu kwangu mimi hii ni nafasi adhimu sana na kupanua uelewa wangu wa masuala mbalimbali, pia ni fursa kubwa ya kueleza maoni yangu kwa waalikwa mbali mbali.

Nina uhakika kuwa watu nitakaokutana na kubadilishana nao mawazo na uzoefu watasaidia kupanua uelewa wangu wa masuala kadhaa”, alisema Zitto alipotakiwa kufafanua umuhimu wa tamasha hilo kwa vijana.

Baadhi ya watu maarufu watakaotoa mada katika tamasha hilo ni pamoja na Majaji washiriki wa Mahakama Kuu ya Marekani Stephen Breyer na Elena Kagan, Mwakilishi Eric Cantor, Rais wa Kituo cha Brady Dan Gross, Rais wa Chama cha Wamiliki wa Bunduki Marekani David Keene, Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Susan Rice; Rais wa Taasisi ya Taasisi ya Kulinda Rasilimali, Frances Beinecke; Mkurugenzi mwenza wa Boies, Schiller & Flexner LLP David Boies, Waziri wa kazi wa zamani Elaine Chao, Waziri wa Usafirishaji Ray LaHood, Meya wa New Orleans Mitch Landrieu, Waziri wa Fedha wa zamani Hank Paulson, Gavana wa zamani wa Minnesota Tim Pawlenty, Mshauri wa Chama cha Republican Karl Rove na Rais wa Shirikisho la Walimu Marekani Randi Weingarten.

Taasisi ya Aspen inajihusisha na masuala ya elimu na sera ambayo ina makao makuu katika jiji la Washington, Marekani. Lengo lake kuu ni kuendeleza maadili ya kiuongozi. Pia taasisi hii ni kama kituo cha kuwezesha kutafuta ufumbuzi wa masuala magumu.

Taasisi ina matawi kadhaa baadhi yakiwa huko Aspen, Colorado na Wye River huko Maryland. Pia Taasisi ina ofisi katika jiji la New York. Pia taasisi ina mtandao mkubwa wa washiriki duniani kote.

KUMBUKUMBU

$
0
0
Ilikuwa tarehe kama ya leo mwaka 2009 na sasa umetimiza miaka minne haupo nasi kimwili lakini kiroho tupo pamoja nawe Steven (jr). unakumbukwa na Dada zako Doreen na Doris pamoja na Kaka yako David.
 
Mungu alitoa na Mungu alitwaa, jina lake libarikiwe.

KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa mkuranga na Waziri wa Kilimo na Ushirika, Adam Malima, Bungeni mjini Dodoa Juni 24, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na wabunge, Bungeni Mjini Dodoma 24,2013.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiteta na Wabunge Mary Chatanda wa Viti Maalum (kushoo) na Mbunge wa Sumbawanga, Aeshi Hillaly kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 24, 2013.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (kushoto) kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 24, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimsaidia kurekebisha tai Mbunge wa Ileje,Aliko Kibona kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 24,2013. Katikati ni Mbunge wa Kuteuliwa James Mbatia.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta Mbunge wa Ileje,Aliko Kibona (kushoto) kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 24,2013. Katikati ni Mbunge wa Kuteuliwa James Mbatia.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

mzee wa feva akichukua taswirazzz

$
0
0
Kamera ya Globu ya Jamii ilifanikiwa kupata taswira hii ya afande aliekuwa akirekodi spidi za magari yaliyokuwa yakipita katika barabara kuu ya Dodoma - Morogoro kwa kutumia kifaa maalum,hii ni katika kuhakikisha Sheria na taratibu za usalama barabarani zinafuatwa.

WAZIRI MKUU PINDA AFUNGUA MKUTANO WA MADC, MARC NA MARAS MKOANI DODOMA LEO

$
0
0
Waziri Mkuu MizengoPinda akihutubia wakati alipofungua Mafunzo ya Kujenga Uwezo kwa Wakuu wa Wilaya , Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Mikoa kwenye ukumbi wa Hoteli ya New Dodoma mjini Dodoma Juni 24,2013.
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakinukuu maelekezo ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipofungua Mafunzo ya Kujenga Uwezo kwa Wakuu wa Wilaya , Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Mikoa kwenye ukumbi wa Hoteli ya New Dodoma mjini Dodoma Juni 24,2013.
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipofungua Mafunzo ya Kujenga Uwezo kwa Wakuu wa Wilaya , Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Mikoa kwenye ukumbi wa Hoteli ya New Dodoma mjini Dodoma Juni 24,2013.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

JESHI LA POLISI MKOANI RUVUMA LAKAMATA MENO 18 YA TEMBO

$
0
0
Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma  Deusdedit Nsimeki akipanga maneno ya tembo kulingana na uneno /uzito kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

-------------------------------------------------- 

JESHI  la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kukamata meno ya Tembo  18 yenye uzito wa kilo 84 yenye  thamani ya Tsh216,000,000/ambapo meno hayo 18 ni sawa na dola 15 elfu za kimarekani pia ni sawa na Tembo tisa waliouwawa .
 
 Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo Kamanda wa polisi mkoani Ruvuma  Deusdedit Nsimeki amesema kuwa tukio hilo la kukamata meno hayo lilitokea Juni 20 Mwaka huu majira ya saa 3.00 usiku  katika kijiji cha Majala kata ya Nandembo iliyopo wilaya  ya Tunduru mkoani Ruvuma .
  
 Kamanda Nsimeki amesema kuwa  tukio hilo la kukamatwa kwa meno hayo ya tembo lilitokea  baada ya askari polisi wa wilaya hiyo kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema ndipo wao waliweka mtego wa kuwanasa watuhumiwa hao lakini bahati mbaya watuhumiwa hao walikurupuka na kuacha mizigo ya meno hayo iliyokuwa imefungwa kwenye mifuko tofauti tofauti.
   
 Alisema kuwa watuhumiwa waliokurupuka walikuwa wanne huku kila mmoja na baiskeli ambazo walikuwa wamebebea meno hayo na kwa upande wa watuhumiwa wa meno ya tembo kukurupuka bila kutiwa mbaroni na jeshi hilo limekuwa ni tukio la pili la kwanza  lilitokea katika kijiji  cha Hanga wilayani Namtumbo na la pili ndiyo hilo la wilaya ya Tunduru zote za mkoani Ruvuma .
  
 Aidha kamanda alisema kuwa jeshi la polisi linajitahidi kuwasaka watu ambao wamejificha na wanajihusha na matukio hayo ya ujangili kwa wanyama  na hasa tembo.
             
Pia ametoa wito kwa wananchi uendelea kushirikiana jeshi la polisi mkoani Ruvuma kwa kutoa taarifa za siri zitakazowezesha kukamatwa kwa wahusika wa vitendo vya uhalifu wa aina yoyote kwa sababu suala la ulinzi ni kila mmoja hivyo kunasoaswa kuwepo kwa ushirikiano wa karibu baina ya polisi na wananchi.

Picha na habari kwa hisani ya Demashonews.blogspot.com

MTANGAZAJI JOYCE KIRIA AMTAFUTA MUMEWE KWA MABANGO

$
0
0
1a
Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake ndani ya Kituo cha Televisheni cha EATV,Joyce Kiria akiwa amewashikilia watoto wake Lingatone Kileo (kulia) na Lincorn wakati alipozungumza na waandishi wa habari nje ya Jengo la Idara ya Habari Maelezo iliopo katika mtaa wa Samora,jijini Dar huku akipaza sauti kuomba msaada kwa Rais Jakaya Kikwete na watanzania kwa ujumla ili kusaidiwa na kujua aliko mume wake,Bw. Henry Kileo ambaye inadaiwa kuwa anashikiriwa na Jeshi la Polisi, Joyce Kiria amesema mpaka sasa hajaambiwa kama mume wake yuko wapi hivyo hata kama ana makosa anaomba afahamishwe kwani hajui kinachoendelea mpaka sasa.
3
Joyce Kiria akifafanua mambo mbalimbali mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo huku akiwa amewabeba watoto wake na ndugu zake wengine wakiwa na mambongo yenye ujumbe mbalimbali.
4

Joyce Kiria akendelea kujibu maswali kadhaa ya wanahabari wakati akizungumza nao leo jijini dar es salaam.Picha kwa hisani ya FullshangweBlog.

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI YAHAMIA OFISI MPYA

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawajulisha wadau wake wote kuwa Ofisi yake ya Makao Makuu inahama kutoka Jengo la TIRDO, Barabara ya Kimweri, Msasani kwenda Kiwanja Na.. 8, Kitalu Na. 46, Barabara ya Sam Nujoma, Mwenge, Dar es Salaam kufikia Juni 30, 2013.

Katika kipindi cha kuhama, Bodi itahakikisha huduma zinarejea katika hali ya kawaida ndani ya siku chache.

Aidha uombaji wa mikopo kwa njia ta mtandao upo kama kawaida, na hivyo waombaji wa mikopo wanaweza kuendelea na utaratibu wa kuomba mikopo. Hata hivyo, huduma ya simu kwa waombaji wa mikopo imesitishwa kwa muda wakati mitambo ikifungwa na huduma itaendelea kama kawaida kuanzia Jumanne Juni 25, 2013.

Bodi inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaotokea wakati ikijiweka sawa katika makazi mapya.

Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
Kiwanja Na.. 8, Kitalu Na.. 46, Barabara ya Sam
Nujoma, Mwenge
S.L.P. 76068, Dar es Salaam, Tanzania.
Simu: +255 22 2669036/2669037 Faksi: +255 22 2669039
Barua pepe: info@heslb.go.tz
Tovuti : www.heslb.go.tz

MIMI NA TANZANIA - JEREMIAH MTOBESYA NA HAKI YA ELIAS

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images