Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 172 | 173 | (Page 174) | 175 | 176 | .... | 3284 | newer

  0 0

   Kelvin Msuya akitambulisha familia yake wakati wa mnuso wa kumeremeta kwao katika ukumbi wa Diamond Jubilee VIP hall jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo
   Maharusi wakiandaa keki kwa ajili ya kamati ya maandalizi kama shukrani yao kwa kazi nzuri


  0 0


  0 0

  Dear Tanzanians and Friends,
   
  I greet you all in the name of Jesus. I’m sure you all have heard the bombs that were detonated in Arusha, Tanzania that resulted in chaos and death of innocent civilians. Below you will see a message I sent out on June 19th that highlights the problem.
   
  In response to the chaotic situation in our country, I’m calling for an urgent prayer conference call to all Tanzanians residing in US and Canada and anywhere in the world. If you can’t join the conference call, please pray along.
   
  Day & Date: Tomorrow, Sunday, June 23, 2013
  Time: 9pm Eastern or 8pm Central, or 7pm Mountain or 6pm Pacific time. 
  Call in Number: (218) 548-1952
  Pass Code: 777999
   
  Focus of our prayer  will be to seek God in this and pray for peace and pray against the satanic and demonic conspiracy that is behind all the attacks. At this point we don’t know who is behind the attacks. Whether the attacks are politically motivated or not, brothers and sisters, let us say NO to this kind of behavior by few in our country! We speak peace, freedom and prosperity for Tanzania and its people.
   
  Unfortunately, it is a short notice. However, as Jesus’ foot soldiers, we need to be ready in short notice to intervene and intercede for the kingdom sake.
   
  See you all Sunday night!
   
  God’s blessings to you all,
   
  Evangelist Frank Mwakasisi, Ph.D.
  Founder and President
  Mighty Outreach International - "Helping Churches Reach More People for Christ"
  PO Box 1655
  Portage, MI 49081
  USA

  0 0

  Anna Nkinda – Maelezo, aliyekuwa Mbeya

  VIONGOZI wa Serikali, Dini na Vyama vya Siasa nchini wametakiwa kuondoa tofauti zao na kutumia majukwaa kuhubiri amani na upendo ili kudumisha mshikamano na utulivu ndani ya jamii.

  Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Mchungaji wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Ushirika wa Itiri Daniel Siame wakati wa ibada ya mazishi ya Ditective Sagenti Christopher Kyendesya aliyefariki Juni 19 mwaka huu wilayani Kisarawe mkoani Pwani kwa ajali ya Pikipiki.

  Mchungaji Siame alisema kuwa Serikali haina dini bali jamii ndiyo inadini mbalimbali zikiwemo za Ukristo, Uislamu na Upagani na kuwaomba viongozi hao pale wanapokutana na wananchi kuhubiri mambo yanayompendeza Mwenyezi Mungu.

  “Inawezekana kuwa ndani ya dini zetu kuna watu ambao wanamapokeo ya dini tu na siyo kumtangaza Mwenyezi Mungu hivyo basi sisi kama viongozi wa Serikali, Dini na Vyama vya siasa tunakazi kubwa ya kutangaza mambo ya kumpendeza Mwenyezi Mungu na amani na siyo mambo ya uchochezi”, alisema Mchungaji Siame.

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro alimshukuru mchungaji huyo kwa kuwahimiza watu wote wakiwemo viongozi na wananchi kuhusu umuhimu wa amani na upendo katika jamii.

  Kandoro alisema kuwa ni jukumu lao viongozi wa Serikali, Dini na wanasiasa kutumia lugha ya kuwajenga watanzania ili waone kuwa amani ni silaha ya maisha yao ya kila siku kwani ikivurugika msingi mkubwa wa maisha unaharibika na hakuna hata mmoja atakayefurahi kuona kuwa amani na upendo vinatoweka .

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ni miongoni mwa viongozi mbalimbali waliohudhuria mazishi hayo wakiwemo pia maofisa wa Jeshi la Polisi, wanasiasa, wasomi na watendaji wa Serikali.

  0 0


  Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Hamisi (katikati) akiwa na mwenyekiti wa UVCCM kilimanjaro, Fredrick Mushi (kulia) na Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Aluu Segamba katika Hafla ya kutunuku Vyeti kwa wanachama wa UVCCM vyuo vikuu Kilimanjaro.

  ===================
  MWENYEKITI wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM), Sadifa Juma Hamisi, amepinga vikali kuwepo kwa mfumo wa serikali tatu kama inavyopendekeza rasimu ya katiba.

  Sadifa ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wasomi wa UVCCM kutoka katika vyuo vikuu mkoani kilimanjaro katika hafla ya kuwaaga wasomi hao na ambapo pia ametunuku vyeti vya uanachama kwa wanafunzi 312 pamoja na kuwakabidhi kadi za uanachama wanachama wapya.


  0 0

  Watch Full Program on PBS. See more from The Presidents Photographer.

  0 0

   Katibu wa Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Shy-Rose Bhanji akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu miswada mbalimbali iliyojadiliwa na bunge hilo kwa kipindi cha  mwaka mmoja. Kushoto ni mbunge wa bunge hilo, Abdullah Mwinyi. (Picha zote na Habari Mseto Blog)

   Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Abdullah Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari leo. Kulia ni Katibu wa wabunge wa Tanzania katika bunge hilo, Mhe. Shy-Rose Bhanji.
  KATIBU wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Shy-Rose Bhanji, amejivunia harakati chanya alizoshiriki katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kuanza kushiriki vikao vya bunge hilo Juni mwaka jana, huku akielezea kuvutiwa na miswada miwili inayosubiri baraka za Marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mhe. Shy-Rose Bhanji  alisema kuwa yeye kama mbunge amejifunza mengi katika miezi 12 ya uwapo wake bungeni, huku akiitaja miswada hiyo kuwa ni sheria ya Udhibiti wa Uzito wa Magari Barabarani ‘Vehicle Load Contol Bill’ na Punguzo la Vituo vya Ukaguzi Mipakani ‘One Stop Border Posts Bill.’
                                                                                                                                                                                                                                                 

  Aliongeza kuwa, bunge hilo limeijadili kwa kina miswada hiyo, ambayo kwa sasa inasubiri maamuzi ya Marais wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, huku akitoa wito kwa wafanyabiashara kutumia fursa za Kijiografia za Afrika Mashariki ili kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.


  Mhe Shy-Rose alisema kuwa, sheria hizo zitakuwa na tija kubwa kwa wananchi na mataifa yanayounda Jumuiya ya Afrika Mashariki, kutokana na ughali wa ujenzi wa miundombinu ya barabara kwa sasa, lakini pia urasimu ulioshamiri katika vituo vingi vya ukaguzi wa abiria na mizigo mipakani kwa wanaotoka nchi moja kwenda nyingine.


  “Uhai wa barabara zetu Afrika Mashariki unategemea matumizi sahihi, yanayozingatia uzito wa magari kwa barabara husika. ‘Vehicle Load Control Bill’ ina kila kanuni itakayowabana madereva kuhakikisha wanatumia barabara kwa uzito sahihi wa mzigo garini, ili kuzifanya zidumu kwa muda mrefu,” alisema Mhe. Shy-Rose.


  Aliongeza kuwa, mawasiliano ya barabara ndio mhimili wa maendeleo katika nchi yoyote na ili kudumisha barabara kuepuka ujenzi ghali wa mara kwa mara, sheria hiyo imependekeza uzito wa juu kabisa kwa magari yanayotumia barabara za Afrika Mashariki uwe ni tani 55 na sio zaidi.


  Alifafanua kuwa, muswada huo umezingatia mambo mengi, hasa kutokana na ukweli kuwa kabla ya hapo kila nchi ilikuwa na sheria yake ya uzito wa juu zaidi barabarani, huku nchi nyingine za Afrika Mashariki zikiwa hazina sheria hiyo na kuruhusu magari kubeba uzito wowote na kupita barabara yoyote.


  Kuhusu muswada wa ‘One Stop Border Posts Bill,’ Shy-Rose alisema kuwa, ni wazi kwamba jamii ya Wana-Afrika Mashariki, imechoshwa na urasimu mkubwa unaowakumba wanapohitaji kusafiri kutoka nchi moja kwenda nyingine, unaosababishwa na uwingi wa vituo vya ukaguzi wa abiria na mizigo yao, hivyo muswada huyo ni tiba ya kero hiyo.


  “Sheria hii ikipitishwa na kuridhiwa na Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, itamaliza hadha za usafiri zisizo za lazima, wanazokabiliana nazo wananchi, kiasi cha kuchelewesha safari zao na kjurudisha nyuma harakati chanya za kujiletea maendeleo yao na nchi zao kwa ujumla,” alisema Shy-Rose.


  Kwa upande wake, Mbunge mwingine wa bunge hilo, Mhe. Abdullah Mwinyi, alisema Jumuiya ya Afrika Mashariki imejikita kujiletea maendeleo kupitia nyanja tofauti, zikiwamo za Forodha, Soko Huria na Sarafu ya pamoja, ambapo Bunge hilo limejadili mengi yaliyo bora kuhusu Forodha na sasa wanaingia katika Soko Huria.


  “Soko Huria ndio kiini halisi cha mafanikio ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Dalili za mafanikio kupitia nyanja hiyo zimeanza kuonekana, ambapo bidhaa nyingi za Afrika Mashariki zilizokuwa zikiuzwa huko Afrika Magharibi, kwa sasa zinaingia rasmi kwenye mzunguko wa nchi wanachama wa Afrika Mashriki na kuchangia maendeleo ya pamoja,” alisema Mwinyi.


  Aidha, Wahe. Shy-Rose na Mwinyi wakatumia fursa hiyo kuwasilisha pole ya pamoja kati yao na wabunge wengine wa Bunge la Afrika Mashariki, kwa wahanga wa bomu jijini Arusha, ambako watu kadhaa walifariki dunia na wengine kujeruhiwa vibaya, huku wakilaani vikali shambulizi hilo lililoathiri watu wasio na hatia.


  “Tunaviomba vyombo vya dola kuhakikisha vinatumia kila njia kuwanasa waliohusika na kuwawajibisha kwa mujibu wa sheria. Tunawaomba wana Arusha na atanzania kwa ujumla kudumisha amani, upendo, utulivu na mshikamano miongoni mwa Watanzania,” walisisitiza wabunge hao.


  Kwa mujibu wa wabunge hao, vikao vijavyo vya bunge hilo vitafanyika kama ifuatavyo: Agosti 18 hadi 29, Oktoba 13 hadi 26 vikao vitakuwa jijini Arusha, huku Novemba 17 hadi Desemba 6 vikao vikiwa jijini Nairobi. Desemba 19 hadi 31, Januari 9 hadi Machi 22 na Mei 25 hadi Juni 6 mwakani vikao vyote vitafanyika jiji Arusha.

  0 0

  Dkt Frateline Mlashani Kashaga wa Helsinki,  Finland,  ni mdau wa siku nyingi wa blog ya jamii katika nchi hiyo ambayo Globu ya Jamii ilizaliwa mwaka 2005. Tangia April, 2008 mpaka mwaka huu 2013 amekuwa kwenye masomo ya PhD in Social Policy , University of Helsinki, Finland . Juzi tarehe 20th June, 2013 aliweza kutetea andiko lake la  PhD public defense katika Ukumbi wa Auditorium XII Main Building of the University of Helsinki. Globu ya Jamii inampongeza kwa fanaka hiyo. HONGERA SANA SANA!
   Picha ya kwanza, ni Mdau wa Helsinki, Mr. Dennis Londo akimpongeza Dr. Frateline Kashaga mara baada ya kumaliza kutetea nondozzz yake ya PhD  katika ukumbi wa chuo kikuu cha Helsinki Finland.
   Mdau FRATELINE MLASHANI KASHAGA (PhD) akipongezwa na mai waifu  wake kwenye ukumbi wa chuo kikuu cha Helsinki Finland.

  0 0

  IMG_2565
  Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Tamko la Mount Meru la kuwalinda waandishi wa habari wakiwa kazini Afrika Mashariki, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Bw. Francis Stolla akizungumza machache wakati wa uzinduzi huo ambapo alisisitiza umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari katika kujenga Demokrasia na Utawala Bora katika Ukanda wa Afrika Mashariki na kati. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Misa-Tan Bw. Mohammed Tibanyendera (wa tatu kushoto), Mjumbe wa MCT Bw. Allan Lawa (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Abubakar Karsan ( wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa MISA-TAN Bw. Tumaini Mwailenge (kushoto).
  IMG_2504
  Mtangazaji wa Radio Clouds Fm Regina Mwalekwa akisoma Tamko rasmi la Mount Meru lililoandaliwa siku ya maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya habari Duniani yaliyofanyika Mei 3-4 mwaka huu jijini Arusha yaliyohudhuriwa na washiriki mbalimbali toka vyombo vya habari, redio za jamii, jumuiya mbalimbali za Kimataifa, Taasisi za mafunzo ya tasnia ya habari na mifuko ya Maendeleo ya Tasnia ya habari kutoka Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda.
  IMG_2519
  Mgeni rasmi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Bw. Francis Stolla (wa pili kulia) akizundua rasmi Tamko la Mount Meru linalozunngumzia vipengele mbalimbali vitakavyowalinda waandishi wa habari Afrika Mashariki.
  IMG_2533
  Mgeni rasmi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Bw. Francis Stolla akionyesha Tamko rasmi la Mount Meru la kutetea Uhuru wa Vyombo vya Habari kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.
  IMG_2543
  Mgeni rasmi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Bw. Francis Stolla akizindua rasmi CD ya wimbo ulioimbwa na Mjomba Band unaoitwa "Uhuru Wangu" uliopigwa kwa mara ya kwanza wakati maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika katika Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwenyekiti wa Misa-Tan Bw. Mohammed Tibanyendera ( wa pili kushoto), Mjumbe wa MCT Bw. Allan Lawa (kulia) na Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Abubakar Karsan (kushoto).
  IMG_2550
  Sasa umezinduliwa rasmi....Kaa tayari kuusikiliza katika radio mbalimbali na mitandao ya kijamii hapa nchini.
  IMG_2490
  Mjumbe wa MCT Bw. Allan Lawa akizungumza umuhimu wa waandishi wa habari kujali maslahi mapana ya taaluma ya uandishi wa habari katika mchakato wa kuandika Katiba mpya kupitia mabaraza ya Katiba ya Wilaya. Vile vile alisisitiza umuhimu wa waandishi wa habari kushiriki kikamilifu katika kujadili rasimu ya Katiba mpya iliyozinduliwa hivi karibuni na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal ili kuhakikisha Taifa linapata Katiba Mpya inayojali Uhuru wa vyombo vya Habari hapa nchini.
  IMG_2595
  Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Abubakar Karsan akifafanua jinsi Mfuko wa Mwangosi utakavyokuwa ukisaidia waandishi wa habari wanaopata majanga wakiwa kazini vile vile utaenda sambamba na Tuzo ya Mwandishi ambaye atakuwa amepata matatizo, misukosuko katika kutafuta habari za uchunguzi na Tuzo hiyo itakuwa ikitolewa kila mwaka Septemba 6 siku aliyokufa Daudi Mwangosi na mshindi atajinyakulia Milioni 10 zitakazotolewa na waendeshaji wa mfuko huu UTPC.
  IMG_2497
  Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania Jane Mihanji akiteta jambo na Usia Nkhoma Ledama wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) (Wa pili kushoto) na Bi. Rose Mwalimu kutoka UNESCO (wa pili kulia).
  IMG_2585
  Mdau kutoka Chama cha waandishi wa habari Wanawake Tanzania (TAMWA) akitoa maoni yake juu ya tamko la Mount Meru kwenye uzinduzi uliofanyika leo jijini Dar katika Hoteli ya Peacock.
  IMG_2575
  Baadhi ya waandishi wa habari waandamizi nchini kutoka kushoto ni Shermax Ngehemera Mhariri wa The African, Hamis Mzee wa MCT na Mhariri wa zamani wa Mwanaspoti ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah.
  IMG_2495
  Wadau mbalimbali kutoka kwenye vyombo vya habari waliohudhuria uzinduzi wa tamko la Mount Meru.
  Kufuatia Mkutano wa Wadau wa Habari Afrika Mashariki waliadhimia yafuatayo;-
  1.Serikali zote nchi za Afrika Mashariki zihakikishe kuwa Katiba za nchi zao zinakuwa na vipengele kwa ajili ya:
  -Kuwa na tasnia ya habari ambayo ipo huru, salama na yenye kujitegemea ikijumuisha usalama wa wanahabari.
  -Sheria nyingine zote ziheshimu Katiba za nchi zikiendana na vyombo na mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu.
  2. Wamiliki wa vyombo vya habari wafanye marekebisho ya miundo ambayo itazingatia yafuatayo;
  - Uendeshaji bira- Ikiwa ni pamoja na masuala ya Ajira, Mishahara, Mikataba, Motisha na Marupurupu mengine ya kifedha.
  - Viendeshwe kwa kufuata na kuheshimu miiko ya Kitaaluma.
  -Kuhakikisha kuwa wanahabari wote wanakuwa na Bima.
  -Vyumba vya habari viongeze uwekezaji katika mitandao ya kijamii pamoja na utoajji elimu kwa wanahabari kuhusu mitandao binafsi yaani Blogs.
  3. Baraza la Habari lishirikiane na taasisi na vyama vya kitaaluma vya wanahabari ili kudumisha na kulinda ueledi na umoja katika tasnia ya habari.
  4. Wanahabari waanzishe vyama vya wafanyakazi ili kuwezesha na kuongeza mapatano na makubaliano ya hiari sehemu za kazi.
  5. Wamiliki wa vyombo vya habari walinde na kutetea usalama wa wanahabari na vyombo vyao kupitia
  -Wamiliki wa vyombo vya habari kuweka na kuzingatia taratibu za usalama sehemu za kazi
  -Wamiliki wa vyombo vya habari wahakikishe wanwapatia waandishi wa habari vifaa vya usalama au vya kujikingia na hatari na wawezeshe mafunzo juu ya taratibu za usalama.
  -Kujumuisha mitaala ya mafunzo ya usalama na ulinzi katika taasisi zote za mafunzo ya uandishi wa habari.
  - Wanahabari wao binafsi wachukue vipaumbele na tahadhari katika usalama wao binafsi.
  6. Jumuiya ya Afrika Mashariki lizitake nchi wanachama wake ambao walitia sahihi itifaki ya Udhibiti wa Tovuti wajiondoe katika Mkataba huo ikiwa ni njia moja wapo ya kudumisha utawala bora na uwajibikaji.
  7. Serikali za Afrika Mashariki zifanya juhudi katika kuwezesha uanzishwaji wa mfumo wa kisheria wa kuruhusu uendeshaji bora wa mitandao ya kijamii na wakati huo huo wakilinda uhuru wa wadhibiti ili kuboresha na kuendeleza uhuru wa mitandao ya kijamii katika eneo la Afrika Mashariki.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na waumuni wa kanisa katoliki Emaus Centre Ubungo Jijini Dar walioshiriki katika ibada ya kupanda mbegu hivi karibuni. Mkuu huyo wa Mkoa alialikwa kama mgeni rasmi kuongoza zoezi hilo la kupanda mbegu ambalo lilifanikiwa kukusanya Tsh. Milioni 41.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na waumuni wa kanisa katoliki Emaus Centre Ubungo Jijini Dar es Salaam  ambapo aliwaasa  juu ya umuhimu wa kutunza amani iliyopo nchini kwa kujiepusha na mambo madogomadogo yanayoweza kuondoa amani iliyopo ikiwemo mijadala ya kuchinja ambayo ilishaanza kufanya machafuko nchini. Hata hivyo aliwaomba waumini hao kuwaombea wanasiasa wafanye kazi zao vizuri kwa haki, usawa na uwajibikaji badala ya kuishia kuwatupia lawama ambazo hazijengi.

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akishiriki kukusanya sadaka zilizokuwa zikitolewa na waumini wa kanisa katoliki Emaus Centre Ubungo Jijini Dar walioshiriki katika ibada ya kupanda mbegu hivi karibuni. Mkuu huyo wa Mkoa alialikwa kama mgeni rasmi kuongoza zoezi hilo la kupanda mbegu ambalo lilifanikiwa kukusanya Tsh. Milioni 41.

  Waumini wa kanisa katoliki kutoka sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam waliokuwa wamekusanyika "Emaus Centre" Ubungo kwa ajili ya ibada ya kupanda mbegu iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya hivi karibuni. Picha na Hamza Temba

  0 0

  RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodger Tenga anatarajia kuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa kozi ya makocha wa ngazi ya pili (Intermediate) itakayofanyika Jumanne kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa kuanzia saa tano asubuhi. 

  Kozi hiyo iliyodumu kwa wiki nne, ilifunguliwa rasmi Juni 3 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Harbours Club, uliopo Kurasini. Mkurugenzi wa Ufundi Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Joseph Kanakamfumu, alisema Rais Tenga ameridhia kufunga kozi hiyo baada kukosekana katika ufunguzi wa kozi hiyo kutokana na majukumu aliyokuwa nayo. 

  “Kozi yetu ya ngazi ya pili itafungwa Jumanne kwenye Uwanja wa Taifa kuanzia saa tano asubuhi na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodger Tenga ndiye atatufungia kozi yetu na ameridhia kuwa atakuwa nasi,” alisema Kanakamfumu. 

  Alisema kozi hiyo itakuwa chachu ya kupatikana kwa makocha watakaosaidia maendeleo ya mchezo huo katika Mkoa wa Dar es Salaam na Taifa kwa ujumla. Kozi hiyo ni ya kwanza kuendeshwa na DRFA tangu kuingia madarakani kwa uongozi mpya wa chama hicho Desemba 12, chini ya Mwenyekiti Almas Kassongo.

  0 0
 • 06/23/13--12:53: nyumba inauzwa
 • Nyumba iko Bunju karibu na shule ya Moga, Dar es salaam.
  Nyumba hii tayari ina title deed 
  Mawasiliano:0659 683771 au 0655227507 
  email add:misasophie@yahoo.com
  0 0


  Wajuzi wa mambo wanasema kisa cha kupopolewa kwa chupa wakati akiburudisha huko Dodoma usiku wa jana, ni kutokana na taarifa zilizoandikwa kwenye gazeti moja la udaku kuwa alimsema vibaya mwanamuziki mwenziye ambaye sasa ni marehemu, aliyefia nje ya nchi, kuwa aliaga dunia akiwa masikini na kutumia dawa za kulevya kutokana na msongo wa maisha yaliyomwendea kombo.
  Ingawaje mwenyewe alisema amenukuliwa vibaya na magazeti hayo yanalenga kuuza kwa habari za uzuri, aliomba samahani kwenye ukurasa wake wa Facebook na kuahidi kwenda nyumbani kwa wazazi wa marehemu kuwataka radhi.
  Lakini inaelekea jitihada zake hazikufanikiwa kiasi cha kupatwa na zahma asiyoitarajia usiku wa jana.
  Ikiwa ndivyo yaliyo, inaonesha ni kwa kiasi gani wananchi wanaamini na kutilia maanani vinavyoandikwa na kutangazwa kwenye vyombo vya habari.
  Laiti nguvu ii hii ya kuyapa kipaumbele masuala ya burudani ingewekwa katika kuyasaka maarifa thabiti ya elimu na kujiendeleza, pengine kila kaya na nchi ingekuwa iko katika hatua kubwa ya kimaendeleo.  0 0

   Watoto wakiwa na mishumaa wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha miaka 100 ya KKKT leo katika usharika wa Chuo Kikuu cha Tumaini,Makumira, Usa River, Arusha 
   Mkuu wa KKKT Askofu Alex Gehaz Malasusa.akiongoza maandamano
   Maaskofu katika maandamano

  Washarika na watu mbalimbali wamejumuika leo katika maadhimisho ya miaka hamsini tangu kuunganika kwa makanisa saba ya Kilutheri nchini na kuunda Kanisa moja la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

  Kilele cha maadhimisho hayo yaliyoanza jana kimeadhimishwa katika Dayosisi ya Kaskazini, usharika wa Chuo Kikuu cha Tumaini (TUMA - Tumaini University of Makumira), Makumira, Usa River, Arusha yakiongozwa na Mkuu wa KKKT Askofu Alex Gehaz Malasusa.

  Watu wapatao 5,000 wanatarajiwa kujumuila katika maadhimisho hayo.

  Wanahabari wa Redio Sauti ya Injili, Moshi Tanzania wakiripoti moja kwa moja kutoka katika viwanja hivyo, wanasema hali ya amani na utulivu vimetawala hadi sasa.

  KKKT inatokana na makanisa yaliyoanza kutekeleza utume wa kueneza Injili zaidi ya miaka 100 iliyopita nchini Tanzania. Mnamo tarehe 19 Jini 1963, makanisa yaliamua kiweka nbali tofauti zao na kuunganika na kuunda Sinodi na baadaye Dayosisi. Hadi Mei 26, mwaka huu, KKKT imefanikiwa kuwa na Dayosisi 22 na Misioni 20 zinazotoa huduma mbalimbali za kiroho kwa washarika wake na huduma za kijamii kwa wote kama vile mashule, vyuo vya mafunzo ya ufundi, Vyuo vya Elimu ya Juu, mabenki, mahoteli, mahospitali n.k.

  Viongozi wakuu walioiongoza KKKT hadi sasa ni:

  1. Askofu Stefano Ruben Moshi (1963 - 1976)
  2. Askofu Dk Sebastian Kolowa (1976 - 1992)
  3. Askofu Samson Mushemba (1992 - 2007)
  4. Askofu Dk Alex Gehaz Malasusa ( 2007 hadi sasa)


  Maaskofu Moshi na Kolowa ni marehemu. 
  Askofu Mushemba ni mstaafu  .  0 0

  JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) LINAWATANGAZIA VIJANA WALIOMALIZA KIDATO CHA SITA 2013 NA KUCHAGULIWA KUJIUNGA NA JKT KATIKA MAKAMBI YARUVU PWANI, MGAMBO TANGA, MSANGE TABORA, BULOMBORA KIGOMA, MARAMBA TANGA, RWAMKOMA MARA, MLALE RUVUMA NA KANEMBWA KIGOMA KURIPOTI KATIKA MAKAMBI HAYO TAREHE 24 JUNI 2013 KAMA ILIVYOTANGAZWA AWALI.

  VIJANA HAO WARIPOTI KATIKA MAKAMBI WALIYOPANGIWA KAMA ILIVYOONYESHA KATIKA TOVUTI YA JKT WWW.JKT.GO.TZ. ATAKAYERIPOTI KAMBI AMBAYO HAKUPANGIWA HATAPOKELEWA. VIJANA HAO WALIPOTI WAKIWA NA VYETI VYA LEAVING VYA KIDATO CHA NNE AU CHA SITA KWA UTHIBITISHO

  INASISITIZWA KUWA KUJIUNGA NA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA NI LAZIMA, ATAKAYESHINDWA KURIPOTI ATAKUWA AMEVUNJA SHERIA NA ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA

  VIJANA WATUNZE TIKETI ZAO WALIZOTUMIA KWENDA KATIKA MAKAMBI YA JKT. NAULI ZAO ZITAREJESHWA NA JKT WATAKAPORIPOTI KAMBINI.

  VIJANA WALIOCHAGULIWA KATIKA AWAMU YA PILI NI WALE WALIOFAURU KWA DIVISIONI, II NA BAADHI YA DIVISION III MCHEPUO WA SAYANSI.

  VIJANA WA KIDATO CHA SITA 2013 AMBAO MAJINA YAO HAYAKUORODHESHWA KATIKA TOVUTI HIYO, WATAJIUNGA NA JKT AWAMU YA TATU MWEZI SEPTEMBA 2013.

  0 0
 • 06/23/13--14:50: mambo ya gado
 • The Nile: Egypt Vs the Rest


  0 0

  Mwishoni mwa wiki AAR imetoa huduma ya bure ya mafunzo kwa wafanyakazi wa nyumbani kwa wafanyakazi wa CRDB . Programu hii iliandaliwa na kutolewa na idara ya huduma ya washauri wa kampuni ya bima ya Afya ya AAR (AAR Employees Wellness Program) kwa nia ya kusaidia vijana hawa kuweza kujitambua, kujithamini na kufahamu jinsi ya kumudu majukumu yao kwa vizuri wanayopewa na waajiri wao. 
   “Tunawashukuru sana AAR kwa kutoa huduma hii kwa wahudumu wetu wa nyumbani, kwani vijana hawa ndio wana muda mwingi wa kukaa na nyumba pamoja na malezi ya watoto wetu kwa muda wote tunapokua kazini , natumai mafunzo haya yatakua na faida kwao na sisi pia kuwa na imani hata tuwapo makazini”. Alisema Meneja Mafunzo wa CRDB,  Agnes Robert. 
  Mafunzo haya yalihusika na mambo mengi mbalimbali, baadhi ikiwa ni pamoja na kujitambua na kujithamini, heshima nyumbani, jinsi ya kulea watoto kiuangalifu na kuwahudumia endapo wapatapo matatizo ya kiafya na mengineyo, vitu muhimu vya kuzingatia ndani ya nyumba ,Vitu visivyopaswa kufatwa. 
   “Kwakweli leo tumefurahi sana kuja hapa CRDB nakupewa mafunzo na kampuni ya AAR , kwanza kabsa tumepanuka kimawazo, mambo mengi tulikua hatuyajui, na mengine hatukua tunadhani yana umuhimu lakini leo tunashukuru AAR kwa kutusaidia kuyaelewa na pia kujithamini, kujikubali na kupenda kazi zetu..." alisema mmoja kati ya wafanyakazi wa nyumbani hao,  Mariam Kayege.
    Programu hii inategemea kufanyika tena kwa mara nyingine kwenye makao makuu ya CRDB, na hapo baadae pia kwa makampuni na mashirika mengine mbali mbali nchini.
  Wakufunzi wa AAR wakiwa na wafanyakazi wa ndani wa ndani kabla ya kuanza darasa
  Mkufunzi wa AAR Josephine Tesha akitoa somo
  Bw John Ngonyani AAR akitoa somo
  Dkt Kissah wa AAR akitoa mafunzo kwa mifano halisi
  Wafanyakazi wa ndani waliohudhuria mafunzo hayo ya AAR

  Dr. Kissah wa AAR akiwapa somo wafanyakazi wa ndani namna ya kuhudumia watoto

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu(kulia)akimwelezea Bi.Tumu Saidi ambae ni mkazi wa Mbagala,Dar es Salaam manufaa na faida za kujiunga na Promosheni ya Cheka Nao inayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kupiga simu kwa bei nafuu kwenda mtandao wowote na kujishindia shilingi milioni 2 kwa mwezi,ili kujiunga na kufaidika nayo piga *149*01#,Wanaoshuhudia kushoto ni Meneja wa kanda ya Mbagala Idd Mawe.
  Ofisa wa Vodacom Tanzania bi.Rehema William(alieketi)akimwelezea jambo mkazi wa mbagala Dar es Salaam,wakati Promosheni ya Cheka Nao iliyofanyika mbagala hapo jana inayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kupiga simu kwa bei nafuu kwa mitandao yote nchini na kujishindia shilingi milioni 2 kwa mwezi,ili kujiunga na kufaidika nayo piga *149*01#.
  Ofisa wa Vodacom Tanzania Alfani Mdachi(katikati)akimwandikisha Mustafa Mustafa mkazi wa Mbagala ili kumpatia kadi ya simu tayari kwa matumizi halali zoezi hilo lilifanyika wakati wa kampeni ya Cheka Nao inayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kupiga simu kwa bei nafuu kwenda mitandao yote nchini na kujishindia shilingi milioni 2 kwa mwezi,ili kujiunga na kufaidika nayo piga *149*01#.Anaeshuhudia ni Meneja wa kanda ya Mbagala Idd Mawe.


  0 0
 • 06/24/13--00:10: Article 23


 • 0 0

  MWANAMKE mkazi wa kijiji cha Ikandamoyo, wilayani Katavi, Veronica Saleh ‘Mama Kaela’ (50), amefanya uamuzi adimu wa kuolewa na wanaume wawili ambao anaishi nao kijijini hapo.

  Kijiji hicho kipo umbali wa takribani kilometa 30 kutoka mjini hapa katika Jimbo la Katavi linalowakilishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

  Pamoja na ndoa hiyo iliyowezeshwa na mume mkubwa kukubali kuishi na mume mdogo, imeelezwa kuwa mwanamke huyo ndiye ‘aliyewaoa’ wanaume hao kwa zaidi ya miaka saba sasa, huku akiwa na amri kuu katika nyumba, kama ilivyo katika ndoa za kawaida.

  Wanaume hao ni Paulo Sabuni ‘Baba Kaela’ (60) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (45) ambaye ni mume mdogo.

  Taarifa za kuwapo kwa ndoa hiyo ya aina yake, ziliifikia Globu ya Jamii na kufanyiwa uchunguzi kwa zaidi ya wiki tatu, na hatimaye katikati ya wiki hii, wahusika walikubali wao wenyewe kuzungumzia suala hilo. Kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo ambaye alionekana kuwa msemaji wa familia hiyo, yeye na mumewe mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita, wakitoka kijiji cha Usumbwa mpakani mwa Chunya, Mbeya na Tabora.


older | 1 | .... | 172 | 173 | (Page 174) | 175 | 176 | .... | 3284 | newer