Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

Sherehe za kuapishwa Skauti Mkuu wa Chama cha Maskauti Tanzania

$
0
0
 Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania mteule Mhe. Mwantumu Mahiza akisubiri kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijiandaa kuvishwa skafu na skauti kabla ya kumuapisha Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza akisubiri kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akivishwa skafu na skauti kabla ya kumuapisha Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza akisubiri kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha  Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza akisubiri kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi baada ya kumuapisha Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi vitendea kazi Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013.

Article 0

$
0
0
Dear Friend,
Cheka Tuesdays is on AGAIN, at Evans Bukuku's Comedy Club!! Kama Kawaida on every LAST Tuesday of the month!! It's Tuesday 25th June from 8pm, NDANI YA EAST 24 Bar & Grill, Mikocheni, (Former ARCADE)!!

FACT: Those who laugh more. . . .LIVE LONGER!! So come laugh the night away with Enika, Dogo Pepe, Side Story, Maganiko, Ray & Evans Bukuku!! Not forgetting a GUEST comedian - Saganda!! (Wimbo wa Rafaeli: "Ni namna gani, ni jinsi gani tutawini maishani mpaka siku tunasema buriani.. . . ."

All this for only Tshs 10,000/- PLUS you get a chance to win some DODOMA WINE during the OPEN MIC SESSION. KAZI NI KWAKO!!
 
Please find poster attached and feel free to forward.

Best Regards,
Evans Bukuku.

Jacline Walper atamba kwenye Filamu

$
0
0
WASANII mbalimbali watakaoshiriki katika Tamasha la Tamasha la Wazi la Filamu Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ ambalo litafanyika katika Viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza, wameanza kutoa tambo zao.
Tamasha hilo linatarajiwa kuanza Jumatatu ijayo, ambapo kutakuwa na maonyesho mbalimbali ya filamu pamoja na burudani za muziki kutoka bendi ya Extra Bongo, pamoja na ngoma za asili. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wasanii hao walisema tamasha hilo litawafungua macho wengi ikiwa pamoja na kupata kujua kile ambacho wanakifanya wakati wakirekodi sinema zao.
Msanii mahiri wa filamu, Aunty Ezekiel alisema atakuwepo Mwanza kipindi chote cha tamasha hilo na akataka mashabiki wafike kwa wingi kushuhudia filamu kali zaidi ambazo amezicheza katika siku za karibuni, ambazo zitaonyeshwa bure.
“Mimi ndiye mkali wao, Watanzania waje kushuhudia kile ambacho tumekifanya,” alisema Aunty Ezekiel, kauli ambayo iliungwa mkono na Jacqueline Wolper aliyedai naye atakuwepo, ila ndiye pia anayejiamini ni ‘mzuri’ zaidi katika mambo ya filamu.
Irene Uwoya alitamba atafunika wengi katika tamasha hilo, huku Vicent Kigosi ‘ray’ na Jacob Steven ‘JB’ nao wakijinasibu watafanya vitu adimu zaidi katika tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi wa filamu hapa nchini.
Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki alitamba watafanya kweli zaidi siku ya uzinduzi kwani watapiga vibao vipya na kutoa shoo mpya kwa mashabiki watakaojitokeza kipindi chote cha tamasha hilo. “Tumejiandaa vya kutosha, tuna shoo mpya na ya aina yake, ambayo si ya kukosa. Waje tu waone Extra Bongo itakachofanya ni nini,” alisema Choki.
Mratibu wa Tamasha hilo aliye pia Mkurugenzi wa Sophia Records, Musa Kissoky, alisema kwa sasa kinachosubiriwa ni siku ya tamasha tu na kusema wasanii wengi wa filamu watakuwepo hapo. “Kwa sasa maandalizi yamekamilika kwa asilimia 90, yaani tunaleta kitu tofauti ambacho watu watashangaa, ndio maana mpaka sasa wengi wanapigwa na bumbuwazi kuhusu kile tutakachofanya siku hiyo,” alisema.
Naye Meneja wa kinywaji cha Grand Malt walio wadhamini wakuu wa tamasha hilo, Consolata Adam, alisema wameamua kufanya kweli zaidi kwani wanataka kuona Watanzania wanapata kitu chenye uhakika. “Tumejipanga katika hili na wala hatutanii kwani tunataka kuwawezesha wakazi wa Mwanza na maeneo ya jirani kuhudhuria tamasha hili kwa wingi . Tunawakaribisha watu wote wenye mapenzi na filamu zetu za Tanzania kufika na kushuhudia tamasha hili ambalo mwaka huu limeboreshwa zaidi,” alisema Consolata.
Tamasha la Filamu la Grand Malt linatarajiwa kuanza Julai 1-7, mwaka huu huku kukiwa na filamu mbalimbali zitakazooneshwa katika kipindi hicho. Filamu zote hizo ni kutoka Tanzania.
Tamasha hilo la filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana vyema na ISAMILO LODGE ya Mwanza

HIVI NDIVYO KIJIWE CHA UGHAIBUNI KILIVYOANZA

maandalizi ya sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na Tamasha la utamaduni wa kiswahili Marekani

$
0
0
Afisa Ubalozi Suleiman Saleh (kushoto) akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Idd Sandaly wakati akiwakaribisha kamati ya maandalizi ya sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na Tamasha la utamaduni wa kiswahili Marekani Ubalozini kwenye kikao cha maandalizi ya mwisho mwisho ya sherehe ya Vijimambo pamoja na mambo mengi yaliyojadiliwa, ulinzi na kuhofiwa watu kuwa wengi ndiyo maswala yaliyochukua muda mrefu kuyajadili na kushauriwa watu kuwahi mapema na kwa sababu kutakua na zoezi la kukaguliwa kabla ya kuingia ukumbini na nafasi za kukaa kwenye ukumbi ni watu 500 kwa kuepuka usumbufu wa msururu mrefu jaribu kufika mapema milango itakua wazi kuanzia saa 3 asubuhi.
Mwenyekiti wa kamati Bwn. Baraka Daudi akitia saini kitabu cha wageni.
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn Idd Sandaly akitia saini kitabu cha wageni.
Katibu msaidizi wa kamati Julius Katanga akitia saini kitabu cha wageni.
Kaimu Balozi Mama Lily Munanka (kati) akiongoza kikao cha kamati ya maandalizi kilichofanyika Ubalozi wa Tanzania Washington, DC Jumatatu June 24, 2013 wengine katika picha kutoka kushoto ni Bwn. Idd Sandaly, Bwn. Baraka Daudi, Afisa Ubalozi Suleiman Saleh na Dj Luke.
Kutoka kushoto ni Afisa Ubalozi Edward Masanja, Idd Sandaly, Baraka Daudi, Kaimu Balozi Mama Lily Munanka, Afisa Ubalozi Suleiman Saleh Dj Luke na Julius Katanga.
Kamati na maofisa Ubalozi wakimsubili Kaimu Balozi mama Lily Munanka (hayupo pichani).
Bwn. Idd Sandaly, Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV(kushoto) wakiwa kwenye kikao cha kamati ya maandalizi na maafisa Ubalozi wakiongozwa na kaimu Balozi mama Lily Munanka katika kujadili maandalizi ya miaka 3 ya sherehe ya Vijimambo na Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili.
Afisa Habari wa Ubalozi Mindi Kasiga akichangia jambo

mpiganaji nelly mtema wa daily news afiwa na mumewe

$
0
0
Habari wadau, 
Naomba kuwajulisha kuwa mwanachama mwenzetu wa TASWA, ambaye ni mwandishi wa habari wa gazeti la Daily News, Nelly Mtema amefiwa na mumewe usiku wa kuamkia jana. Msiba upo nyumbani kwake Kimara Matangini jijini Dar es salaam. Tutaendelea kupeana taarifa ya msiba huo.
Ahsanteni.
Katibu Mkuu TASWA

MAMBO YALIVYONOGA TBL'S FAMILY DAY DAR

$
0
0
 Mkurugenzi wa Fedha wa TBL, Kelvin (kulia), akimkabidhi George Magombeka zawadi ya saa ya ukutani baada ya kuwa mshindi wa riadha katika bonanza hilo la kukata na shoka lililofanyika Kunduchi, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Oriyo (kulia) akimkabidhi zawadi  .Mbwana Milanzi baada ya kuwa mshindi wa kwanza wa mbio za magunia katika hafla ya Siku ya wafanyakazi wa TBL kufurahi na familia zao kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi, Kunduchi Dar es Salaam
 Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakifurahi na familia zao kwa kucheza kushindana kuvuta kamba katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, Kunduchi Dar es Salaam, wakati wa sherehe 'Tbl's Family Day'.
 Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakifurahi na familia zao kwa kucheza soka katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, Kunduchi Dar es Salaam juzi, wakati wa sherehe 'Tbl's Family Day'.

Wananchi wa Tarafa ya Pande Wilayani Kilwa Walia na Mbunge wao kwa kutohudhuria Vikao vya Bunge mara kwa mara

$
0
0
Katibu Mtendaji wa Asasi isiyo ya Kiserikali wilayani Kilwa,Omary Mkuwili akitoa maelezo mafupi kuhusiana na Mdahalo huo wa Uwajibikaji wa Viongozi wa Serikali za Mitaa Chini ya Ufadhili wa The Foundation na kufanyika jana katika Tarafa ya Pande wilayani Kilwa.
Baadhi ya wadau mbalimbali waliohudhuria Mdahalo Huo wakichangia mada

Na Abdulaziz Video,Kilwa

Wananchi wa kata ya Pande, wilayani Kilwa,mkoani Lindi wanakerwa na tabia ya mbunge wao wa Jimbo la Kilwa Kusini, Selemani Bungala Bwege ya kukwepa kushiriki kwenye vikao vya Bunge la Jamhuri la muungano kwa muda Mwingi na hasa bunge la bajeti.

Wakizungumza kwenye mdahalo Unaohusu uwazi na uwajibikaji wa Viongozi na watendaji wa serikali za mitaa kwa maendeleo ya wananchi ulioandaliwa na Mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali wilaya ya Kilwa,(KINGONET) kwa ufadhili wa The foundation for civil socitey na kufanyika katika shule ya Msingi ya Pande, wananchi hao, Akiwemo Bw Anan Nahoda, Saidi Athumani Kifuku na Mariamu Kajoka walisema kuwa muda wote wa kipindi cha mikutano ya bunge huko Dodoma mbunge huyo uwa hanaonekana mitaani akifanya mikutano ya kuhamamsisha wananchi wagomee malipo ya pili ya korosho badala ya kuwa bungeni.

Anan Nahoda mkazi wa Pande alisema kuwa,kitendo cha Mbunge wao kukwepa vikao vya bunge vinawaumiza kwani moja kati ya kazi ya mbunge ni kuwakilisha mawazo ya wananchi kwenye mikutano ya bunge na kitendo cha mbunge wao kutokuwepo huko inaonyesha hatimizi wajibu wake ambao wapiga kura walimchagua hawatekelezewi.

“Kinachotusikitisha sisi tuliomchagua ni kumwona mbunge wetu muda wote wa bunge yupo nje ya bunge tena kama kuondoka ni leo kwani hata jana alikuwepo hii inafanya tusiwe na mwakilishi kule bungeni hii si halali kwani hata akiwepo huku hashughuliki na masuala ya maendeleo badala yake anaendesha mikutano ya ndani ya kushawishi wananchi wagomee malipo ya korosho”alisema Anan.

Aidha Anan alilalamikia tabia ya mbunge huyo kutotembelea na kutofanya mikutano na wananchi ili kukusanya kero na maoni mbalimbali na kuyasemea akiwa bungeni na kudai kuwa tangu achaguliwa hajafanya mkutano wowote wa hadhara unaojumuhisha wananchi licha ya kufanya mikutano ya ndani.

Saidi Athuman alisema kuwa, tatizo la viongozi wengi waliochaguliwa ni kutofahamu vyema mfumo wa vyama vingi kwani badala ya kushughulikia matatizo ya wananchi hujikuta wakishughulikia maslahi ya vyama vyao vilivyowawezesha kuwa madarakani hali ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya nchi na kusababisha uvunjifu wa amani na kuwataka wajue majukumu yao kwa wananchi waliowachagua.

Kufuatia malalamiko hayo,Mtandao ulimtafuta Mbunge Huyo kwa njia ya Simu ili kutoa ufafanuzi wa tuhuma hizo Ambapo Bungala alikanusha tuhuma za kutofanya mikutano kwenye kijiji na kubainisha kuwa tangu amechaguliwa amefanya mikutano saba ambapo alikutana na wananchi mbalimbali kupokea kero zao,na kuhusu la kutohudhuria bunge alikiri kutokwepa vikao vya bunge na kuwa hivi karibuni alionekana jimboni kwake na kudai kuwa alikuwa kwenye shughuli za uchaguzi ndogo ulizofanyika hivi karibuni wilayani Nachingwea ambapo alikwenda ili kusaidiana na viongozi wenzake kumnadi mgombea wa chama chake(CUF).

“Ni kweli sikuwepo kwani nilikuwa kwenye kampeni ya uchaguzi mdogo huku Nachingwea ili kuhakikisha mgombea wetu anashinda na sasa hivi naelekea bungeni….hoja ya kutoonekana muda mwingi bungeni hiyo si kweli na ili la kutofanya mikutano si kweli labda huyo aliyelalamika hakuwepo…. kwani nimefanya mikutano mingi hapo na wa mwisho ni wa mwezi wa pili mwaka huu”alisema Bungala.

WATANZANIA WALIVYOSHIRIKI MATEMBEZI YA HIARI YA SIKU YA UTUMISHI WA UMMA AFRIKA HUKO NCHINI GHANA

$
0
0
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Bi. Ingiahedi Mduma akiwa na washiriki wa nchi mbalimbali wakati wa matembezi ya hiari wakati wa kukamilisha maonesho ya wiki ya utumishi wa umma nchini Ghana.
Watanzania wakiwa kwenye matembezi ya hiari pamoja na washiriki wa nchi zingine wakati wa kukamilisha maonyesho ya wiki ya utumishi wa umma Nchini Ghana.
Washiriki wa Tanzania na washiriki wa nchi zingine wakisubiri kuanza kwa matembezi ya hiari wakati wa kuadhimisha maonesho ya wiki ya utumishi wa umma Nchini Ghana.

Article 13

Sifa United yaiadhibu Mtakuja 5-2 Airtel Rising Stars

$
0
0
Mshambuliaji wa Sifa United Haruna Athuman (kushoto) akichuana na Alex Simenga wa Mtakuja Beach wakati wa mechi ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, iliyochezwa kwenye uwanja wa Mwanamanyala Shule ya Msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 24, 2013. Sifa United walishinda 5-2.
Alphonce Shabani wa Mtakuja Beach (kulia) akimtoka Haruna Athuman waf Sifa United wakati wa mechi ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, iliyochezwa kwenye uwanja wa Mwanamanyala Shule ya Msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 24, 2013. Sifa United walishinda 5-2.
Abdulazizi Haruna wa Mtakuja Beach na Hamir Sheh wa Sifa United wakiwania mpira wa juu wakati wa mechi ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, iliyochezwa kwenye uwanja wa Mwanamanyala Shule ya Msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 24, 2013. Sifa United walishinda 5-2.

MAANDALIZI YA MAONYESHO YA 37 YA SABA SABA 2013 YAENDELEA KWA KASI .

$
0
0

Pichani juu ni maandalizi ya maonyesho ya 37 ya saba saba  yatakayoanza hivi karibuni  katika viwanja vya Mwalimu nyerere vilivyopo kilwa road jijini  Dar es salaam.Maonyesha hayo ya 37  yameelezwa kuwa  ni maonyesho makubwa ya kimataifa na ya kipekee kufanyika jijini Dar es salaam ikilinganishwa na maonyesho ya miaka mingine iliopita, kwani maonyesho haya yatashirikisha nchi nyingi zaidi  kuliko miaka  yote.Imeelezwa kuwa nchi zitakazoshirkia katika maonyesho ya mwaka huu  zimeongezeka kutoka nchi 11 zilizoshiriki mwaka jana na kufikia nchi 32  ambazo zitashiriki katika maonyesho hayo mwaka huu.
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

MKURABITA KULETA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA KWA VITENDO

$
0
0
Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania, MKURABITA, unaendelea na utekelezaji kwa vitendo, wa awamu ya kwanza ya kuwapatia “Maisha Bora kwa Kila Mtanzania” kwa kuendelea kugawa hati miliki za kimila kwa wanavijini mbali mbali, ili kwanza kuwamilikisha rasilimali, kasha ndipo kuwaelimisha jinsi ya kuzitumia rasilimali hizo kujiletea maendeleo ambayo ndiyo yatakayo leta maisha bora kwa kila Mtanzania.

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Mkurabita, Bibi. Seraphia Mgembe, wakati akitoa tathmini ya zoezi la kuwakabidhi hati miliki za kimila, kwa wakulima wa zao la chai wa wilaya ya Mbinga, Mufindi na Njombe, lililohotimishwa hivi karibuni.

Bibi Mgembe amesema, maisha bora kwa kila Mtanzania, haya patikana kwa wananchi kubweteka na kuisubiria serikali ndio ifanye kila kitu, bali ni kwa serikali kujenga mazingira ya uzalishaji mali, ikiwemo kuwamilikisha wananchi rasilimali zao, na maendeleo ya kweli, yatapatikana kwa wananchi kuelimishwa na kujibiidisha katika kutumia rasilimali hizo kama dhamana za kupatia mitaji ya kujiletea maendeleo.

Bibi Mgembe amesema, huku zoezi la kuwamilikisha wananchi rasilimali zao likiendelea, MKURABITA inayapitia tena yale maeneo ambayo tayari wananchi wake wameisha kabidhiwa hati miliki, ili kuwajengea uwezo wananchi hao, jinsi ya kuzitumia hati miliki hizo kama dhamana na kukopa katika mabenki ili kutumia fedha za mkopo kujiletea maendeleo.

Bibi Mgembe amesisitiza, maendeleo ya kweli na endelevu, ni yale yanayotokana na matumizi ya rasilimali zilizowazungunguka wananchi husika, nan i kwa kulitambua hilo, ndio maana MKURABITA imekuwa ikizishirikisha taasisi za kifedha, ili kuwaelimisha wananchi fursa mbalimbali za mikopo ya kibiashara na kimaendeleo zinazoweza kupatikana kwa kutumia dhamana za hati miliki zao.

Kwa upande wao, Wakuu wa wilaya za Njombe, Bi. Sarah Dumba na Mkuu wa Mufindi, Bi. Evarista Kalalu, waliipongeza MKURABITA kwa juhudi zake za kuhakikisha wakulima wa chai sasa wanayamiliki rasmi mashamba yao ya chai, ambapo mwanzo walikuwa na utajiri ambao hauwafaidii chochote zaidi ya kulima na kuuza mazao yao, lakini sasa, sio tuu ni wamiliki wa mashamba hayo, bali wanaweza kuzitumia hati miliki zao, kukopa mikopo mikubwa ya kimaendeleo.

Jumla ya hati miliki za kimila zaidi ya 2000 zilikabidhiwa kwa wakulima wa chai.
Wananchi wa Njombe, wakifurahia kukabidhiwa hati miliki za kimila, kulikofanywa na MKURABITA hivi karibuni.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Sarah Dumba, akimkabidhi hati miliki ya kimila, Mwanakijiji wa kijiji cha Matembwe, Bw. Solomon Matunasa wakati wa hafla fupi ya MKURABITA kukabidhi hati miliki za kimila kwa wakulima wa chai wa Rungwe, Mfindi na Njombe hivi karibuni. Katikati ni Mratibu wa MKURABITA, Bibi Seraphia Mgembe.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Sarah Dumba, akimkabidhi hati miliki ya kimila, Mwanakijiji wa kijiji cha Iwafi, Bw. Eneas Paruasi wakati wa hafla fupi ya MKURABITA kukabidhi hati miliki za kimila kwa wakulima wa chai wa Rungwe, Mfindi na Njombe hivi karibuni. Katikati ni Mratibu wa MKURABITA, Bibi Seraphia Mgembe.

Mapitio ya magazeti leo

Yupi ni Dereva Bora kati ya Hawa??,Angalia kwa Makini Picha hizi


WANAFUNZI WALIOSOMA SHULE ZA KATA MPAKA VYUO VIKUU WATOA SHUKRANI ZAO KWA MH. LOWASSA

$
0
0

Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowasa akisalimiana na wanafunzi wa chuo kikuu cha UDOM waliotoka shule za sekondari za kata, wakati walipofika nyumbani kwake mkoani Dodoma kutoa shukrani zao kwa hatua waliyofikia kielimu.


Hamida Salum mwanafunzi wa mwaka wa kwanza UDOM, akizungumza kwenye hafla hiyo Juni 25, 2013


Mh. Lowasa katikati, Dkt. Mahanga (Kulia) na Parseko Korne wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi hao.


Na Father Kidevu Blog, Dodoma


Wanafunzi wa Chuo Kikuu ch DODOMA, maarufu kama UDOM, ambao walifika hapo wakitokea zile shule za makabwela (Shule za Kata), wamemtaka Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowasa, achukue fomu za kugombea urais 2015 muda utakapowadia.


Pia wameahidi kujichangisha fedha kwa ajili ya malipo ya fomu hizo endapo italazimika.



Kauli hiyo ya kwanza kutoka kwa makundi na watu wasiokuwemo ndani ya siasa, ilitolewa Jumatatu usiku nyumbani kwa Lowasa mjini Dodoma, wakati kundi la wanafunzi hao walipofika kutoa shukrani zao kwa hatua waliyofikia ikiwa ni matunda ya shule hizo, ambazo muasisi wake ni mbunge huyo wa Monduli.


“Mimi ninayofuraha kusimama hapa leo hii, nikiwa mtu tofauti, kwa maana ninayesoma elimu ya juu, baada ya kufanikiwa ,kuendelea na elimu ya sekondari kupitia shule za kata pale Kiluvya Dar es Salaam” anasema Hamida Salum ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza hapo UDOM.


“Wewe ni jembe, kama uliweza kusimamia ujenzi wa shule za kata kwa kipindi kifupi cha miaka 2, ninahakika unaweza kufanya men gi zaidi endapo utakuwa rais wan chi hii” mwanafunzi mwingine wa mwaka wa kwanza, Clementina Ophoro alisema, kwenye salamu za mwanafunzi mmoja mmoja wakati wa utoaji shukrani kwa Lowasa.


Lowasa wakati akiwa waziri mkuu wa Tanzania, kwenye mwanzoni mwa awamu ya n ne ya utawala wa rais Jakaya Kikwete, aliweza kusimamia ujenzi wa shule za kata kote nchini, ili kutoa nafasi zaidi za wanafunzi wa makabwela, walioishindwa kendelea na masomo kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhaba wa madarasa.



Kwa sasa shule hizo zimekuwa zikibezwa na watu mbalimbali kwa maelezo kuwa hazina walimu wa kutosha na uhaba wa vifaa vya kufundishia ikiwemo vyumba vya maabara.


“Mimi ninawashangaa watu wanaosema kuwa eti shule za kata hazifai, kwa vile hazina walimu na vifaa. Haya maneno ni ya kupuuzwa, kwani binadamu hupaswi kukwepa changamoto za maisha” alisema mwanafunzi mwingine Victor Mafuru pia wa mwaka wa kwanza.


Wanafunzi hao wa UDOM waliotoka kwenye shule za sekondari za kata, wameamua kuanzisha umoja wao kote nchini, ili kuendeleza ndoto za kuhakikisha kila mwanafunzi wa mtu masikini anapata elimu.


Kwa kuanzia wanafunzi hao wapatao 600, wameahidi kufundisha bure kwenye shule za umma, wawapo likizo baadaye mwishoni mwa mwezi huu wa Juni.


Kwa upande wake, Lowasa ambaye alikuwa pamoja na naibu waziri wa kazi na ajira, Dkt. Makongoro Mahanga, mbunge wa Kigoma mjini, Peter Serukamba, na mkuu wa mkoa wa Singida, Parseko Kone, aliwapongeza wanafunzi hao kwa moyo wao wa shukrani na kuwataka wasikatishwe tama na maneno yanayotolewa juu ya ubora wa shule hizo, kwani yeye binafsi anajivunia juhudi zake kupitia sera za chama cha Mapinduzi, zimeweza an galau kutoa wanafunzi wengi kutoka shule hizo kujiunga na vyuo vikuu.

Wakazi wa kanda ya ziwa wajipanga kumpokea mfalme Costa Siboka

$
0
0
Wakazi wa kanda ya ziwa katika kumpokea mfalme Costa Siboka wameendelea kuonyesha ushirikiano mkubwa katika kubandika matangazo kwenye nyumba zao za kuishi magari, maduka, na stationary, nyumba za kulala wageni na katika mabar kumekua na matangazo mengi kwa sehemu wanazofanya shoo alhamisi tarehe 27/ 6/ 2013 atakuwa Ramadi V.I.P Club siku ya Ijumaa tarehe 28/6/2013 atakuwa Bunda mjini katika ukumbi wa Diamond Pub Jumamosi tarehe 29/6/2013 atakuwa nyumbani kwao katika kisiwa cha maraha UK na atafanya Bonge ya ufunguzi rasmi ndani ya ukumbi mpya wa Afro beach Club mbali na hivyo viatu vya mfalme vimekuwa kivutio kikubwa sana kwa mashabiki wake vilevile kila anakopita muda mwingi ameonekana akipenda watoto kwa kuwapa hi na kupiga nao misosi hii inaonesha ni jinsi gani mfalme anavyokubalika kanda ya ziwa na watu wa lika zote. ziara hiyo inadhaminiwa na KONYAGI, BALIMI EXTRA LAGER. CXC AFRIKA NA MICHUZI BLOG.

PPF YAONGEZA MUDA WA KUSOMESHA WATOTO MPAKA KIDATO CHA SITA

$
0
0
Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bi. Lulu Mengele akielezea kuhusu miaka 35 tangu kuanzishwa kwa PPF mwaka 1978 wakati wa mkutano na wanahabari leo katika Ofisi za PPF Makao Makuu. Mkutano huo ulielezea mafanikio Mbali mbali ya Mfuko pamoja na PPF kuoongeza muda wa kuwasomesha watoto wa wanachama kutoka kidato cha nne mpaka cha sita. Vilevile katika kusheherekea miaka 35 PPF itakuwa na wiki ya huduma kwa wateja kuanzia tarehe 1 Julai mpaka tarehe 5 Julai 2013 ambapo wanachama wanaombwa kufika kwa wingi kwenye ofisi za Mkoa wa Dar es salaam ili kuweza kuendelea kujua shughuli mbalimbali zitolewazo na Mfuko wiki, hiyo itaenda sambamba na maonyesho ya sabasaba ambapo Mfuko wa PPF utakuwa na banda katika viwanja vivyo. Sherehe za miaka 35 zitafikia kilele katika Mkutano wa 23 wa wanachama na wadau utakaofanyika mwezi wa 10 mwaka huu. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Bw. Nsajigwa Mwandwani na Kushoto ni Meneja Huduma kwa Wanachama Bw. Godfrey Mollel

Judgment in the matter of Urban Mkandawire v. the Republic of Malawi

NEWS ALERT: POLISI JIJINI DAR WAKAMATA WATU WAWILI WAKIWA NA BASTOLA KATIKA PIKIPIKI

$
0
0
Askari kanzu (kulia) akiwa ameshika bastola aliyokutwa nayo mtu mmoja aliyekuwa amepakiwa katika pikipiki aina ya Boxer yenye namba za usaji T 961 CJW katika mtaa wa Makunganya jirani kabisa na benki ya Posta jijini Dar es Salaam mchana huu. Kutokana na kuongezeka kwa matukio ya ujambazi wa kutumia pikipiki Polisi wameimarisha ulinzi na hasa katika maeneo ya mabenki. 
Asklari kanzu akiwa na bastola alikamatwa nayo mtu mmoja aliyekuwa amepakiwa katika pikipiki aina ya Boxer.
 Watu waliokamatwa wakijaribu kuwasiliana na ndugu zao.
 Neno kwenye Pikipiki waliyokuwa wakitumia hao. 
 Ofisa wa Polisi akijaribu bastola waliyokutwa nayo watu wawiliwaliokuwa katika Pikipiki Posta Mpya jirani na Benki ya Posta leo.
 Heee ina risasi!
 Mtu aliyekutwa  na bastola hiyo, ambaye alijitambulisha kama mfanyabiashara.
 Polisi wakifanya mawasiliano na wenzao wa doria kuomba msaada wa gari.
 Mtuhumiwa aliyekutwa na bastola akihojiwa na kuchukuliwa maelezo.
 Dereva wa Pikipiki naye akichukuliwa maelezo yake.
 Unaitwa nani, unaishi wapi, unafanya kazi gani, kabili gani, Ofisa wa Polisi akimuhoji mtuhumiwa.
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images