Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1742 | 1743 | (Page 1744) | 1745 | 1746 | .... | 3278 | newer

  0 0
  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametoa wito kwa Baraza la Wauguzi na Wakunga la Zanzibar kusimamia vyema Sheria ya Baraza hilo sambamba na maadili kwa lengo la kuwahudumia vyema wananchi na kuzifanya huduma za afya zizidi kuimarika na kuendelea kuijengea sifa Zanzibar kama ilivyokuwa hapo siku za nyuma.

  Dk. Shein, aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Wajumbe wa Baraza la Wauguzi na Wakunga waliofika Ikulu mjini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha kwa Rais wakiwa wameongozana na uongozi wa Wizara ya Afya chini ya Waziri wa Wizara hiyo Mahmoud Thabit Kombo.

  Katika maelezo yake Dk. Shein aliwaeleza Wajumbe hao haja na umuhimu mkubwa wa kuipitia na kuisoma vyema vifungu vyote na hatimae kuifanyia kazi Sheria ya Baraza la Wauguzi na Wakunga la Zanzibar ya mwaka 2014 ili waweze kuliongoza vyema na kwa ufanisi zaidi Baraza hilo.

  Dk. Shein, alisema kuwa iwapo Sheria hiyo itasimamiwa vyema  fani ya Uuguzi itaendelea kuwa na mafanikio makubwa sana hapa Zanzibar.

  Alieleza matumaini yake makubwa kwa wajumbe hao ambao wamechaguliwa kutokana na kuwa kazi hiyo wanaiweza na kuwapongeza kwa kufanya mambo mengi tokea kuzinduliwa Baraza hilo lenye Wajumbe 13 Mrajis na wasaidizi wake wawili mmoja Pemba na mmoja Unguja mnamo mwezi June mwaka 2015.

  Aidha, Dk. Shein alisisitiza suala zima la maadili ambalo ndio jambo muhimu katika fani yoyote duniani na kueleza kuwa katika fani ya Uuguzi suala la maadili ndio jambo la kulipa kipaumbele ili kuweza kutoa huduma nzuri ya afya kwa jamii.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Na Tiganya Vincent

  Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri  ameziagiza Kamati za Ulinzi na Usalama kwa ngazi zote kuanza kuwasaka watu wanaopita pita katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuwatapeli wananchi kuwa wanaweza kuwapatia fursa za Kujiunga na Jeshi la Taifa kinyume cha utaratibu uliowekwa na Jeshi hilo.

  Bw. Mwanri alitoa kauli hiyo juzi Wilayani Tabora wakati akifunga mafunzo wa vijana  wa Jeshi la Kujenga Taifa Opereshi Magufuli katika Kikosi cha Jeshi cha 823 Msange JKT .

  Mkuu wa Mkoa wa Tabora alisema kuwa ni vema sasa Kamati hizo kutoka chini hadi juu kuangalia kwa ukaribu taratibu zinazotumika katika kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa ili kuwabaini matapeli ambao wamekuwa wakiwalaghai wananchi na kuwatoza pesa ili wawasaidie kujiunga na Jeshi hilo, jambo ambalo ni uongo.

  Awali Mkuu wa Bregedi ya 202 kundi la Vikosi vya Kanda ya Magharibi (FARU) Brigedia Jenerali Stephen Mkumbo alisema kuna haja ya viongozi wa Mkoa kushirikiana katika kutoa elimu kwa wananchi juu ya taratibu za kujiunga na JKT ili kuwasaidia wasije au wasiendelee kutapeliwa fedha zao.

  Alisema kuwa Makao Makuu ya  JKT wakitaka vijana wa kujiunga na Jeshi hilo wanaandika barua ya kuomba vijana na kujiunga na JKT ikiwa na masharti yanayotakiwa na kuipeleka kwenye Mikoa yote ambayo nao uandika barua ya aina ile ile na kuipeleka Wilayani nao wanashusha hadi ngazi za vijiji na sio vinginevyo.

  Brigedia Jenerali huyo aliongeza kuwa mchujo uanzia ngazi za Kata na ndipo unaingia ngazi ya Wilaya na mwisho Mkoa ambapo Maafisa wa JKT uungana nao katika kuwasaili  vijana na ndipo upata wanaostahili kujiunga na Mafunzo ya Awali katika Kambi zao mbalimbali.

  Alisema kuwa matapeli hao wamekuwa wakiwaibia wananchi kwa kuwatoza kuanzia shilingi laki 5 hadi milioni moja kwa madai kuwa watawasaidia kupata fursa za kujiunga na JKT jambo ambalo ni uongo na sio utaratibu unaotakiwa.

  Brigedia Jenerali Mkumbo aliwaomba viongozi wa Mkoa wa Tabora kusaidia kutoa elimu juu ya utaratibu wa kujiunga na JKT ili wananchi wasaidie kuwafichua matapeli hao kwa ajili kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria .

  Akisoma risala ya wahitimu wenzake 870 wa mafunzo ya awali Fred Mashauri alitoa wito wa kuongezwa kwa idadi ya vijana wa kujitolewa ikiwemo walemavu ili nao wapate fursa za kupata mafunzo ya uzalishaji mali na stadi za maisha .

  Katika mafunzo hayo jumla ya wasichana 264 na wavulana 606 wametunukiwa vyeti vya kumaliza mafunzo ya awali kabla ya kwenda katika Kambi mbalimbali ili kujifunza stadi za maisha na ujarisiamali.

  0 0

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikian na DTBi wametoa mafunzo kwa walimu wa shule za msingi na sekondari ikiwa ni katika matayarisho yakufungua maabara ya kompyuta yanayotegemea kuzinduliwa mwezi huu.

  Mafunzo hayo yametolewa na walimu 6 toka katika Kituo cha Elimu cha Galway nchini Ireland kwa lengo la kuwapatia uwezo , mbinu na maarifa ya technoologia ya kompyuta ili kuweza kuwafundisha wanafunzi watakaojiunga na kutembelea maabara hiyo ujuzi utakaowawezeshaa kutengeneza program ndogo ndogo na baadaye kuweza kuvumbua program kubwa zenye kuleta suluhisho kwa mahitaji mbalimbali ya biashara na jamii.

  Maabara ya Airtel Fursa itatatoa fursa kwa vijana wenye malengo ya kujifunza masomo ya Tehama kuongeza ujuzi, na kutoa mwanga kwa vijana kuwa wabunifu kwa kuzindua application mbalimbali ambazo zitaweza kuwaingizia kipato.

  Akiongea wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), George Mulamula alisema “ kutokana na changamoto iliyopo kwa sasa ya wanafunzi wengi kutumia kompyuta kwa mara ya kwanza wanapoingia katika elimu ya chuo kikuu kumefanya kuwe na ufinyu katika ubunifu na kutumia technologia katika ujasiriamali. Tunaamini maabara ya Airtel Fursa yatatoa mwaya kwa vijana kujifunza masomo na kuvumbua mambo mengi wakiwa katika umri mdogo.

  Mafunzo haya kwa walimu tunayotoa leo ni uthibitisho wa dhamira yetu katika kuhakikisha tunakuwa na walimu bora watakaowasaidia wanafunzi kujikita kwenye technologia na kuwa wabunifu. Aliongeza Mulamula.

  Kwa upande wake Meneja huduma kwa jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayumi alisema “ tumejipanga kuwawezesha vijana kuzifikia ndoto zao kwa kuanzisha maabara hii yenye kompyuta za kujifunzia na kuwawezesha wanafunzi kujifunza mafunzo mbalimbali yatakayowawezesha kutanua wigo wao”.

  kupitia program ya Airtel Fursa tunayo application ya VSOMO iliyotengenezwa na kjana wakitanzania ambao leo hii inawawezesha maelfu ya watanzania kuipakuwa na kusoma masomo ya ufundi ya VETA kupitia simu zao za mkononi. Tunaamini maabara hii itakuvumbua na kukuza zipaji vingi na kuleta uvumbuzi katika Tehama. Aliongeza Bayumi.
  Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), George Mulamula (wa tatu kulia), akikabidhi cheti kwa Mwalimu wa Kompyuta wa Sekondari ya Loyola, Sista Maria Sany, baada ya kuhitimu Mafunzo ya Walimu katika fani ya sayansi kwa kutumia programu za kompyuta ili kuwawezesha kufundisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, yaliyofadhiliwa na Airtel Tanzania na kuwezeshwa na Kituo cha Elimu cha Galway cha Ireland, katika Shule ya Msingi Kijitonyama jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa nne kulia), Mkurugenzi wa Galway, Bernard Kirk (wa pili kulia) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Beatus Amri.
  Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), George Mulamula (wa tatu kulia), akikabidhi cheti kwa Mwalimu wa Sayansi wa Shule ya Msingi Kijitonyama, Magdalena Mtei, baada ya kuhitimu Mafunzo ya Walimu katika fani ya sayansi kwa kutumia programu za kompyuta ili kuwawezesha kufundisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, yaliyofadhiliwa na Airtel Tanzania na kuwezeshwa na Kituo cha Elimu cha Galway cha Ireland, yaliyofanyika shuleni hapo, jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa nne kulia), Mkurugenzi wa Galway, Bernard Kirk (wa pili kulia) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Beatus Amri.
  Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), George Mulamula (wa tatu kulia), akikabidhi cheti kwa Mwalimu wa Hisabati na Sayansi wa Shule ya Msingi Kijitonyama, Wilfred Ringo, baada ya kuhitimu Mafunzo ya Walimu katika fani ya sayansi kwa kutumia programu za kompyuta ili kuwawezesha kufundisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, yaliyofadhiliwa na Airtel Tanzania na kuwezeshwa na Kituo cha Elimu cha Galway cha Ireland, yaliyofanyika shuleni hapo, jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa nne kulia), Mkurugenzi wa Galway, Bernard Kirk (wa pili kulia) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Beatus Amri.

  0 0

   Mwenyekiti wa Kamati ya Pili ya Wachumi na Wanasheria iliyoundwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuchunguza Mchanga wa Madini unaosafirishwa kwenda nje ya nchi, Prof. Nehemia Osoro akiwasilisha Ripoti ya Kamati yake, mbele Rais Magufuli, Ikulu jijini Dar es salaam leo.


  0 0


  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza baada ya kupokea ripoti ya pili ya Kamati ya Wachumi na Wanasheria aliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza Mchanga wa Madini unaosafirishwa kwenda nje ya nchi, Ikulu jijini Dar es salaam leo. Katika ripoti hiyo iliyotolewa na Kamati imebaini kuwa Kampuni ya ACACIA MINE PLC haikusajiliwa nchini wala haina hati ya usajili na inafanya biashara ya madini nchini kinyume cha sheria, Pia Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Prof. Nehemia Osoro alisema kuwa Serikali imepoteza Kodi ya Mapato ya kiasi cha sh. trilioni 55 tangu mwaka 1998 hadi Machi 2017 katika usafirishaji wa makinikia, bilioni 94 Kodi ya Zuio ambayo Tanzania imepoteza tangu 1998 hadi Machi 2017 na kufanya Jumla ya thamani ya madini yaliyosafirishwa nje ya nchi kati ya 1998 hadi 2017 kwa Kiwango cha wastani ni trilioni 188.58.

  TAARIFA KAMILI ITAKUJIA BAADAE KIDOGO

  0 0

  RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KUPOKEA RIPOTI YA KAMATI YA PILI YA KUCHUNGUZA MADINI.


  0 0

  Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed (left), with some invited guests during an iftar hosted by the bank to its customers in Dar es Salaam. On his left are; former MD, Rished Bade, Acting Board Chairman, Simon Mponji, Retail and Business Banking Director, Kumaran Pather and CEO’s Roundtable Chairman, Ali Mufuruki. 
   Barclays Bank Tanzania Acting Board Chairman, Simon Mponji (right), with some invited guests during an iftar hosted by the bank to its customers in Dar es Salaam at the weekend.
   Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed (left) talking to former Barclays MD, Rished Bade (centre) during an iftar hosted by the bank to its customers in Dar es Salaam at the weekend. Looking on is BBT Acting Board Chairman, Simon Mponji.
   Barclays Bank Marketing and Communications Manager, Joe Bendera (left), welcomes Sheikh Said Mpeta from the National Muslim Council of Tanzania (BAKWATA) at an iftar hosted by the bank to its customers in Dar es Salaam. BBT Citizenship Manager, Hellen Siria looks on.
   Barclays Bank Tanzania Retail and Business Banking Director,  Kumaran Pather (second right), exchanging views with some guests during an iftar hosted by the bank to its customers in Dar es Salaam recently.

  0 0

  Wakulima wa zao la tumbaku nchini wanatarajia kufaika na ulimaji wa zao hilo baada ya kampuni yaPhilp Morris Tanzania Limited kuwekeza zaid ya Sh. Bilioni 60 kwenye ujenzi wa kiwanda kipya, eneo la Kingolwira katika Halmashauri ya Morogoro mjini. 

  Kampuni ya Philip Morris ambayo imekuwa ni mnunuzi mkubwa zaid wa tumbaku inayolimwa zaidi hapa nchini ikiwa inanunua zaidi ya asilimia 40, inatarajiwa kuongeza ununuzi wake baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda.

  Akiongea wakati wa kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho, kiongozi wa kitaifa wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour amesema amefurahisha na uamuzi wa kampuni ya Philip Morris Tanzania kuamua kujenge kiwanda hapa nchini kwani mbali na kuongeza ununuzi wa zao la tumbaku na kuongeza kipato kwa wakulima wetu, lakini pia kitatoa ajira kwa watanzania na pia kuongeza na kukuza uchumi wa taifa.

  ‘Nimepata taarifa kuwa kampuni hii imekuwa ndio inaongoza kwa kununua tumbaku ya Tanzania na sasa mmeamua kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda. Nawapongeza sana kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ambapo kauli mbiu yake ni Tanzania ya viwanda. 
  Lakini pia serikali imekuwa kwa muda mrefu ikitaka makampuni kuwekeza kwenye viwada na hasa vya mazao ya kilimo kwa kunaongeza thamani ya mazao yetu na kuongeza kipato kwa wakulima wetu,’ alisema Amour huku akiongeza kuwa makampuni mingine yanayonunua bidhaa za mkulima ni muhimu wakawekeza kwenye viwanda ili kupata bidhaa za mwisho zinazotengenezwa hapa nchi.

  Serikali imekuwa msitari wa mbele kuunga juhudi zozote za kuinua kipato cha wakulima wetu. Hii imejidhiirisha baada ya budget ya mwaka kufuta baadhi ya kodi ambazo zimekuwa ni changamoto kwa wakulima. Hii yote inaonyesha ni jinsi ngani tumekuwa msitari wa mbele kukuza sekta hii kwa vyovyote mwekezaji yeyote inakuja na kuwekeza kwenye kilimo ni wa kupongezwa, aliongeza Amour.


  Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Philip Morris Tanzania Ltd Dagmara Piasecka akipokea mbio za mwenge wa Uhuru baada ya kuzindua ujenzi wa kiwanda mjini Morogoro Jumamosi .
  Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi wa kiwanda cha Philip Morris Tanzania jana mjini Morogoro. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro. Ujenzi wa kiwanda hicho ambao utagharimu zaidi ya 60bn/- utawaongezea faida wakulima wa zao la tumbaku hapa nchini.
  Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akizungumza baada ya uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa kiwanda cha Philip Morris Tanzania jana mjini Morogoro. Kulia ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour na kushoto ni mkurugenzi wa kampuni Dagmara Piasecka. 
  Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akizungumza baada ya uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa kiwanda cha Philip Morris Tanzania jana mjini Morogoro. Kulia ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour na kushoto ni mkurugenzi wa kampuni Dagmara Piasecka.


  0 0

  Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Andrew Chenge akiongoza kikao cha 45 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 12, 2017.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha 45 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 12, 2017.
  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Joyce Ndalichako akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha 45 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 12, 2017.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha 45 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 12, 2017.
  Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha 45 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 12, 2017.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Taswira kabla ya kuanza kwa usafi wa fukwe ya Mbezi Beach ambapo ni fukwe inayotumiwa na wakazi wa Mbezi Beach na maeneo ya jirani , lakini kuna uchafu mwingi uliokusanyika pembeni hapo na kuleta kero kwa wakazi hao wanaotumia fukwe hii kwa mapumziko . 
  Wadau na marafiki wa bahari wakiendelea kufanya usafi katika maeneo ya fukwe hii ya Mbezi Beach ikiwa ni moja ya juhudi za kuweka mazingira safi ya bahari ikiambatana na kuunga kampeni ya kimataifa ya kutunza fukwe na mazingira ya bahari kuelekea kutimiza Agenda ya mwaka 2030 ya mpango wa maendeleo ya Umoja wa mataifa .Kampeni hiyo inaratabiwa na kampuni ya KONCEPT ,Nipe Fagio na Marafiki wa Bahari na usafi huo ulifanyika mapema mwisho wa wiki iliyopita. 
  Baadhi ya sindano zilizopatikana wakati wa usafi wa fukwe ya Mbezi Beach uliofanyika mapema mwishoni wa wiki iliyopita ,Sindano hizi ni hatari kwa watumiaji wa fukwe hasa kwa watoto wanaocheza bila kuwa na tahadhari. 
  Taswira ya Fukwe ya Mbezi Beach wakati wa usafi ukiendelea .


  0 0


  0 0

  Timu ya  Madaktari kutoka nchini Japan kwa kushirikiana na watalaam wa afya wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na MUHAS wanatarajia kuwafanyia upasuaji wagojwa 30 wenye matatizo ya mtoto wa jicho.

  Akipokea msaada wa kifaa cha utakasaji (Sterilizing instruments ) pamoja na vifaa mbalimbali vitakavyotumika wakati wa upasuaji huo (Consumables) kutoka kwa timu ya wataalam wa afya wa nchini Japan, Mkuruenzi Mtendaji  wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru amesema zoezi hilo la upasuaji litafanyika kesho na keshokutwa .

  ‘’Tumekua na ushirikiano mzuri na wataalam hawa  kwa muda wa miaka 12 sasa na niamini ushirikiano huu utaendelea, lakini pia  uwepo wa Madaktari  hawa utusaidia kuwajengea uwezo watalaam wetu hapa Muhimbili,” . Amesema Profesa Museru.

  Profesa Museru amesema msaada huo umekuja wakati muafaka ambapo MNH ina mahitaji ya vifaa mbalimbali  vya  vifaa tiba kwa ajili ya kuwahudumia  wagonjwa .

  Kwa upande wake Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida amesema nchi yake itaendelea kushirikiana na MNH katika kuboresha huduma za afya na kudumisha ushirikinao huo wa kihistoria.
   Mkurungezi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru (wa tatu kutoka kushoto) akipokea kifaa cha sterilizing kutoka kwa Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida (kulia).  Kutoka Kushosho ni Mkuu wa Idara ya Macho Muhimbili, Dk Mtemi Baruani na Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Muhimbili, Dk Julieth Magandi. Kutoka Kulia ni Mkurugenzi wa Kliniki ya Yamasaki Eye, Dk Takashi Yamasaki na Kenji Takeuchi wa Take Opht Medical Corporatio. Kifaa hicho kitatumika wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa wenye matatizo ya macho.
   Mkurungezi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akimshukuru Balozi wa Japan, Masaharu Yoshida baada ya kuupokea Leo.
   Mmoja wa wataalamu wa Afya kutoka Japan, Chika Yoshinda akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa kifaa hicho, jinsi ya kikutumia na kukitunza.
   Baadhi ya wataalamu wa afya kutoka Muhimbili na Serikali ya Japan wakimsikiliza, Chika Yoshinda.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


  MASHINDANO ya Sprite BBall Kings yameendelea tena jana kwa michezo minne kupigwa katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Airwing.  Ikiwa ni hatua ya pili ya mashindano hayo baada ya wiki iliyopita kupatikana kwa timu 18 zilizoingia baada ya kupigwa michezo takribani 26.

  Mchezo wa kwanza uliwakutanisha timu za Dream Chaser na Land Force na timu ya Dream Chaser kuibuka na ushindi wa vikapu 92 dhidi ya 72 za Land Force.

  Mechi ya pili iliwakutanisha Kurasini Heat ambaye alitoka na ushindi mnono wa vikapu 124 dhidi ya Bongo Hits aliyepata vikapu 14, The Fighters wakaumana na Chanika Legends na kufanikiwa kushinda kwa vikapu 93 dhidi ya vikapu 16.

  Mechi ya mwisho iliwakutanisha TMT na God With Us na kuhitimisha mechi ya nne kwa TMT kuibuka na ushindi wa vikapu 72 dhidi ya 23 huku kukisubiriwa mechi zingine zitakazopigwa wiki ijayo kuwapata washindi wa jumla watakaoingia hatua ya tatu ya mashindano hayo.

  Mratibu wa Mashindano hayo ya Sprite BBall Kings Basilisa Biseko amesema kuwa baada ya kumalizika kwa mechi za wiki ijayo timu zilizopata alama nyingi ndiyo zitafanikiwa kuingia hatua inayofuata.

  "Timu zilizopata alama nyingi katika michezo ya leo na katika michezo ya wiki ijayo ndiyo watakaofanikiwa kuingia hatua inayofuata ya michuano ya Sprite BBall Kings,"amesema Basilisa.

  Michuano hiyo inayodhaminiwa na Sprite kwa kushirikiana na East Africa Tv na Redio inaendelea tena wiki ijayo katika viwanja vya Chuo cha Bandari na mshindi kamili ataondoka na kitita cha shiling milion 15

  Timu ya Land Force wakiumana na Dream Chaser katika mechi ya hatua ya pili ya mashindano ya Sprite Bball Kings jana katika Viwanja vya Airwing.
  Timu ya Mpira wa Kikapu Dream Chaser.
  Mchezaji wa Dream Chaser akifunga kwa mtindo wa kudanki katika mchezo wa hatua ya pili ya mashindano ya Sprite BBall Kings.

  0 0

   Mkurugenzi Ajira kutoka Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Ameir Ali Ameir akitoa hotuba ya kumkaribisha mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo kwa watafutaji kazi kuhusu mfumo wa Taarifa za soko la ajira kwa Wilaya ya Mjini yaliofanyika katika Ukumbi wa Hospitali ya Wagonjwa wa akili Zanzibar.
   Mkuu wa Wilaya ya Mjini Marina Joel Thomas akitoa hotuba ya ufunguzi katika mafunzo kwa watafutaji kazi kuhusu mfumo wa Taarifa za soko la ajira kwa Wilaya ya Mjini yaliofanyika katika Ukumbi wa Hospitali ya Wagonjwa wa akili Zanzibar.
   Baadhi ya washiriki wa mafunzo kwa watafutaji kazi kuhusu mfumo wa Taarifa za soko la ajira kwa Wilaya ya Mjini wakimsikiliza Mgeni rasmi hayupo pichani katika ufunguzi wa mafunzo hayo aliofanyika katika Ukumbi wa Hospitali ya Wagonjwa wa akili Zanzibar.
   Baadhi ya washiriki wa mafunzo kwa watafutaji kazi kuhusu mfumo wa Taarifa za soko la ajira kwa Wilaya ya Mjini wakimsikiliza Mgeni rasmi hayupo pichani katika ufunguzi wa mafunzo hayo aliofanyika katika Ukumbi wa Hospitali ya Wagonjwa wa akili Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (kulia) akihimiza jambo kwa washiriki wa Mafunzo ya Awali ya Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo. Mafunzo hayo ya siku sita yanafanyika kati ya TADB, NABAD na MIVARF, yanaendelea katika Hoteli ya Beach Comber, Dar es Salaam.

  Na mwandishi wetu,
  Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kushirikiana na  Benki ya Taifa ya Kilimo na Maendeleo Vijijini India (NABAD) na Programu ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani Mazao na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) zimeanza kutoa Mafunzo ya Awali ya Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo.

  Mafunzo hayo ya siku sita (6) yanalenga kuwajengea uwezo watoa huduma hasa kutoka mabenki na taasisi za kifedha nchini kuweza kutoa huduma kwa wakulima kwa wakati na kuzingatia tija wakulima nchini ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

  Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi wa TADB alisema kuwa katika kuunga mkono kwa vitendo juhudi za serikali kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania, TADB imeamua kuwajengea uwezo wadau kutoka mabenki na taasisi za kifedha nchini kwa kushirikiana na  NABAD na MIVARF ili kuweza kutoa huduma kwa uhakika ili kuwakomboa wakulima nchini.

  “Mafunzo haya yanalenga kuunga mkono juhudi za Serikali ili kuharakisha  mapinduzi na maendeleo katika Sekta ya Kilimo, ambayo inaajiri zaidi ya asilimia 75 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi nchini na pia kutoa kiasi cha zaidi ya  asilimia 65 cha mali ghafi kwa ajili ya viwanda vya nchi,” alisema.

  Bw. Assenga aliongeza kuwa TADB imedhamiria na kujizatiti kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika  kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa kusaidia kuyajengea uwezo mabenki na taasisi za kifedha ili kuchagiza upatikanaji na utoaji wa fedha ili kusaidia maendeleo ya kilimo nchini.

  Kwa upande wao wakufunzi wa mafunzo hayo kutoka NABAD, walisema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo watoa huduma watoaji wa mikopo kwa upande wa kilimo kufahamu kwa undani vigezo vya kuzingatia wakati wa utoaji wa mikopo hiyo.
   Meneja Msaidizi wa Mafunzo kutoka NABAD, Dkt. R.S. Reddy akizungumza kuhusu mafunzo hayo. Mafunzo hayo ya siku sita yanaendeshwa kwa pamoja kati ya TADB, NABAD na MIVARF.
   Meneja Msaidizi wa Mafunzo kutoka NABAD, Bw. M.R. Gopal akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Mafunzo ya Awali ya Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo. Mafunzo hayo ya siku sita yanaendeshwa kwa pamoja kati ya TADB, NABAD na MIVARF.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Nehemiah Osoro Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakiangalia Ripoti hiyo ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini wakati ikifunguliwa kwenye kabrasha.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha Ripoti hiyo ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini mara baada ya kukabidhiwa Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakishuhudia.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Ripoti hiyo ya Kamati ya pili ya Uchunguzi Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli  mara baada ya kumkabidhi Ripoti hiyo ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF), imetangaza Uchaguzi Mkuu wa shirikisho hilo utakafanyika Agosti 12, mwaka huu mjini Dodoma.

  “Napenda kuwatangazia wadau wote wa mpira wa miguu kuwa mnakaribishwa kugombea nafasi zilizo orodheshwa hapo chini kwa kuchukua fomu Ofisi za TFF Karume Ilala na pia unaweza kuzipata katika tovuti ya TFF: www.tff.or.tz,” amesema Kuuli.

  Akitangaza tarehe hiyo mbele ya wanahabari, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Wakili Revocatus Kuuli, amesema kwamba kamati yake haitakuwa na huruma kwa ishara yoyote ya rushwa katika kipindi chote cha uchaguzi.

   Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Wakili Revocatus Kuuli (Katikati) akiwa pamoja na wajumbe wengine wa kamati hiyo.

  Wakili Kuuli amesema kamati yake itandesha uchaguzi huo kwa Uhuru na Haki na kuzingatia taratibu, kanuni na sheria zote zilizopo.

  Kuuli, amesema Kamati yake itafanya kazi na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na jeshi la Polisi kuhakikisha uchaguzi huo hautakuwa na vitendo vya rushwa.

  “Tunawatahadharisha wagombea woye kukaa mbali na vitendo vya rushwa…, kamati yetu haitakubali vitendo hivyo na tutafanya kazi na mamlaka za Serikali kuhakikisha yeyote atakayehusika na vitendo hivi anachukuliwa hatua, Takukuru wataufuatilia kwa karibu uchaguzi huu,” alisema Kuuli.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika Job Ndugai,  Kaimu Jaji Mkuu Profesa Ibrahim wakiwa katika picha na kamati ya Rais ya pili ya kuchunguza makinikia na mustakabali wa sekta ya madini nchini baada ya kupokea ripoti yao Ikulu Dar es salaam leo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika Job Ndugai,  Kaimu Jaji Mkuu Profesa Ibrahim wakiwa katika picha na kamati ya Rais ya pili ya kuchunguza makinikia na mustakabali wa sekta ya madini nchini na vingozi wa vikosi vya Ulinzi na Usalama baada ya kupokea ripoti yao Ikulu Dar es salaam leo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika Job Ndugai,  Kaimu Jaji Mkuu Profesa Ibrahim wakiwa katika picha na kamati ya Rais ya pili ya kuchunguza makinikia na mustakabali wa sekta ya madini nchini na vingozi wa vikosi vya Ulinzi na Usalama na baadhi ya wanahabari baada ya kupokea ripoti yao Ikulu Dar es salaam leo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika Job Ndugai,  Kaimu Jaji Mkuu Profesa Ibrahim wakiwa katika picha na kamati ya Rais ya pili ya kuchunguza makinikia na mustakabali wa sekta ya madini nchini na viongozi wa dini baada ya kupokea ripoti yao Ikulu Dar es salaam leo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika Job Ndugai,  Kaimu Jaji Mkuu Profesa Ibrahim wakiwa katika picha na kamati ya Rais ya pili ya kuchunguza makinikia na mustakabali wa sekta ya madini nchini na wakuu wa Mikoa baada ya kupokea ripoti yao Ikulu Dar es salaam leo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika Job Ndugai,  Kaimu Jaji Mkuu Profesa Ibrahim wakiwa katika picha na kamati ya Rais ya pili ya kuchunguza makinikia na mustakabali wa sekta ya madini nchini na viongozi wa vyama vya siasa baada ya kupokea ripoti yao Ikulu Dar es salaam leo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika Job Ndugai,  Kaimu Jaji Mkuu Profesa Ibrahim wakiwa katika picha na kamati ya Rais ya pili ya kuchunguza makinikia na mustakabali wa sekta ya madini nchini na wabunge baada ya kupokea ripoti yao Ikulu Dar es salaam leo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika Job Ndugai,  Kaimu Jaji Mkuu Profesa Ibrahim wakiwa katika picha na kamati ya Rais ya pili ya kuchunguza makinikia na mustakabali wa sekta ya madini nchini na wazee wa jiji baada ya kupokea ripoti yao Ikulu Dar es salaam leo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika Job Ndugai,  Kaimu Jaji Mkuu Profesa Ibrahim wakiwa katika picha na kamati ya Rais ya pili ya kuchunguza makinikia na mustakabali wa sekta ya madini nchini na wawakilishi wa Sekta binafsi baada ya kupokea ripoti yao Ikulu Dar es salaam leo.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika Job Ndugai,  Kaimu Jaji Mkuu Profesa Ibrahim wakiwa katika picha na kamati ya Rais ya pili ya kuchunguza makinikia na mustakabali wa sekta ya madini nchini kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Dar es salaam baada ya kupokea ripoti yao Ikulu leo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika Job Ndugai,  Kaimu Jaji Mkuu Profesa Ibrahim wakiwa katika picha na kamati ya Rais ya pili ya kuchunguza makinikia na mustakabali wa sekta ya madini nchini na wasanii wa Tanzania All stars baada ya kupokea ripoti yao Ikulu Dar es salaam leo.

  0 0older | 1 | .... | 1742 | 1743 | (Page 1744) | 1745 | 1746 | .... | 3278 | newer