Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1741 | 1742 | (Page 1743) | 1744 | 1745 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto za utoaji wa elimu bora hapa nchini leo Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) wakishirikiana na ActionAid Tanzania wameandaa mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Lindi wilaya ya Kilwa kwa siku tatu ili kupanga mpango kazi wa utetezi na ushawishi wa masuala ya elimu yatakayoleta matokeo chanya kwenye masuala ya elimu hapa nchini.

  Mkutano huu ulikuwa ulingazia changamoto zinazoikabili elimu ya msingi hapa nchini ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa, upungufu wa ofisi za walimu, upungufu wa vyoo vya wanafunzi, uwiano usiokubalika kitaratibu wa mwalimu na wanafunzi, shule nyingine kukosa kabisa mwalimu wa kike, upungufu wa nyumba za walimu, kutokutosha kwa fedha za ruzuku, utegemezi wa bajeti ya nchi unaoathiri pia bajeti ya elimu na kusababisha Serikali kushindwa kugharimia kiufanisi utoaji wa elimu.

  Mgawanyo wa ruzuku usiozingatia mahitaji ya wenye uhitaji maalumu, jinsia na mahitaji ya kijiografia na pia shule changa na zile ambazo ni kongwe. Kuwa na mipango ya kibaguzi kwa shule inayofanya vizuri ndiyo inapewa fedha (payment for results- P4R) kutoka mpango wa BRN bila kujali mizania ya usawa wa mazingira kati ya shule na shule. Kukosekana kwa mafunzo kazini kwa walimu, kutopandishwa madaraja walimu na utolipwa kwa wakati stahiki za walimu wanaohamishwa/kustaafu mfano pesa ya usafiri.

  Katika majadiliano washiriki walichangia juu Upotevu wa kodi nchini hususani katika sekta ya madini na viwanda ndio chanzo cha kukosa fedha za kutosha kugharimia sekta ya elimu nchini.
  Afisa Mradi wa Elimu kutoka TENMET, Bi. Alistidia Kamugisha akifungua mafunzo ya siku tatu na kuelezea juu ya uhusiano wa ukusanyaji kodi na maendeleo katika sekta ya elimu nchini ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto za utoaji wa elimu bora hapa nchini kwenye mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.

   Afisa kutoka ActionAid Tanzania, Joyce John akitoa mada kuhusu utetezi wa haki za watoto maashuleni kwenye mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.
   Mwalimu Khamis Kikwajuni akichangia mada kuhusu haki za watoto mashuleni pamoja na Umuhimu wa ukusanyaji wa mapato ya ndani kuwekeza katika sekta ya elimu kwenye mafunzo yaliyoandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma.  Alimueleza balozi huyo kuwa Serikali imebaini na itakomesha ujanja unaofanywa na wafanyabiashara haramu wa kutakatisha fedha kwa kununua makundi makubwa ya mifugo na kuyachunga kwenye maeneo ya hifadhi nchini na baadae kuyauza kwa faida kwenye minada.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akifurahia jambo na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akimkabidhi Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke majarida mbalimbali enye taarifa za vivutio vya Tanzania ofisini kwake mjini Dodoma. (Picha na Hamza Temba - WMU)


  0 0


  0 0

  WATU tisa wamejeruhiwa na majambazi baada ya kuvamia machimbo mapya ya dhahabu yaliyopo katika kijiji cha Nyakivangala, Isimani wilayani Iringa mkoani Iringa na kupora zaidi ya Sh Milioni 81, dhahabu zaidi ya gramu 400, na baadhi ya mali za wafanyabiashara katika eneo. Akizungumza na wanahabari, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela anasema tukio hilo lililitokea majira ya saa nne usiku juzi.

  0 0  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kushoto akimkabidhi cherehani cha kusonea nguo Aisha Mohamed wakati alipokwenda kuwakabidhi vifaa vyenye thamani ya sh.milioni 153 wasichana wajasiriamali 700 vilivyotolewa na Shirika la BRAC kwa wasichana waliopata mafunzo ya ujasiriamali na shirika hilo
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kushoto akimkabidhi mashine ya kukaushia nywele mwanafunzi Thabituwa Shabani wakati wa halfa hiyo kulia ni Meneja Mipango wa Elimu kutoka BRAC Tanzania Amina Shaban
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi katikati akikabidhi mabegi ya kike kwa wasichana 700 wa mkoa wa Tanga kushoto ni Meneja Mipango wa Elimu kutoka BRAC Tanzania Amina Shabani .


  0 0

   Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Benedict Wakulyamba akizungumza na waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda wilaya Muheza wakati wa  ufunguzi wa mpango wa kutoa elimu waendesha bodaboda mkoani hapa ambao ulihudhurwa na wadau mbalimbali ikiwemo madereva wa bodaboda kulia ni Kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani Mkoani Tanga (RTO) Nassoro Sisiwayah kushoto ni Kaimu Mkuu wa Polisi wilaya ya Muheza (OCD) ambapo aliwataka madereva wa bodaboda kuacha kutumika kuwabeba wahamiaji haramu na dawa za kulevya kwani watakaokamatwa hawatapona
   Kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani Mkoani Tanga (RTO) Nassoro Sisiwayah akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba na kulia ni Katibu wa Bodaboda wilayani Muheza,Fransic Gerald
   Kaimu Mkuu wa Polisi wilaya ya Muheza,(OCD) akizungumza katika kikao hicho kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa APEC Bahati Alex
   Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa APEC Bahati Alex akizungumza katika kikao hicho wa pili kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Benedict Wakulyamba kushoto mwenye miwani ni Kaimu Meneja wa Mfuko wa Mafao ya Wastaafu (GEPF) Erick Haule.


  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni(wa pili toka kulia) akiwaongoza kuimba wimbo wa Taifa la Tanzania Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC – Corrections/Prisons Sub Committee(hawapo pichani). Wa pili kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa, (wa kwanza kutoka kushoto) ni Mjumbe wa Sekretarieti ya SADC, Bw. Maemo Machete. Mkutano huo unafanyika kwa siku moja leo Juni 11, 2017 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa ambaye ni Mwenyekiti wa Mkutano huo wa Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC – Corrections/Prisons Sub Committee akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni kufungua rasmi mkutano huo wa siku moja.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni akitoa hotuba ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC – Corrections/Prisons Sub Committee uliofanyika leo Juni 11, 2017 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano huo toka nchi za SADC wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga.
  Mwenyekiti wa Mkutano wa Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC – Corrections/Prisons Sub Committee ambaye ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiongoza Kikao hicho kama inavyoonekana katika picha.


  0 0

  NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

  TAASISI ya Bilal Muslim Mission of Tanzania Kanda ya Ziwa imetoa msaada wa vyakula anuwai vya futari na daku kwa ajili ya kuwasaidia wafungwa na mahabusu 400 wa Gereza Kuu la Butimba Mwanza.

  Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi futari hiyo kwenye gereza hilo Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Kanda ya Ziwa Alhaji Sibtain Meghjee alisema msaada huo wa vyakula utawapa fursa ya kufunga na kuwajenga kiimani na hatimaye kuwa raia wema watakapomaliza kutumikia adhabu zao gerezani.

  Mbali na futari hiyo yenye thamani ya shilingi 3.5 milioni ambayo ni mchele kilo 500, sukari kilo 200, unga wa sembe kilo 400, mafuta ya kula lita 60 na kuni tani tatu pamoja na vitabu mbalimbali vya dini ya Kiislamu kwa ajili ya kujifunza masomo ya dini hiyo muda wote watakaokuwa gerezani.

  Alhaji Sibtain aliushukuru uongozi wa Gereza la Butimba akisema wataendelea kushirikiana na watakuwa tayari kupeleka masheikh wa kwenda kutoa mafundisho ya dini kwa wafungwa na mahabusu kwa gharama zao ili kuwajenga na watakaporudi uraiani wasirejee kufanya makosa.

  Kwa Upande wake Sheikh wa Bilal Muslim wa Mkoa wa Mwanza Sheikh Hashim Ramadhani alisema msaada huo utawapa fursa zaidi ya kuwafanya wawe karibu na Mwenyezi Mungu.

  Kiongozi wa wafungwa na mahabusu hao Yasin Said akitoa shukurani zake huku akinukuu aya na maandiko mbalimbali alisema wakati wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani aliye huru aanapaswa amkumbuke aliye kifungoni kwa kumtaja kwa wakubwa ili apewe taklififu (unafuu) bila kusahaulika.

  “Pamoja na Allah (S W T) pia kuna riziki za wafungwa ambazo hutolewa bila kutarajia kupata chochote bali radhi ya Allah.Waliokuchukizeni na kuwakwaza msilipize kisasi kwa jeuri na chuki, bali saidianeni nao katika kufunga, kuswali, kusoma, wema na kumcha Mungu na si katika dhambi na uadui,” alisema Said.

  Aliongeza kuwa msaada huo utawasaidia kuwafanya wawe watu wema zaidi na kufanya ibada za kufunga na kuswali.

  0 0

  Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE, Imepongezwa na kushukuriwa na watu wenye ulemavu wa kutoona, kwa  kuwakomboa kutoka walemavu omba omba, na kuwageuza kuwa ni wajasiliamali wanaojitegemea na kuchangia maendeleo ya Taifa.

  Pongezi hizo, zimetolewa na wahitimu wa kwanza, wa mafunzo ya kushona nguo kwa wasiona, yaliyofadhiliwa na TANTRADE na kuendeshwa na mtu asiyeona, Abdala Nyangarika,  wakati wa mahafali yaliyofanyika jana katika viwanja vya Tantrade, Kilwa Rd, jijini Dar es Salaam.

  Wahitimu hao, wamezitoa pongezi hizo katika risala yao, iliyosomwa na mmoja wao, Philemon Isaka, ambao kwanza waliishukuru na kuipongeza TANTRADE kwa  kuwathamini watu wenye ulemavu, kisha kujitolea kuwakomboa kwa kuwajengea uwezo, wa  kujitegemea,  hivyo kuwaepusha kugeuka omba omba. Ila pia wametoa wito kwa jamii, kuungana na TANTRADE kuwapatia vifaa ili waweze kujitegemea. TANTRADE imejitolea kuwapatia mafunzo tuu, lakini ili waweze kujitegemea, jamii imeombwa kuwapatia vyerehani na mitaji, ili ujuzi walioupata, uweze kuwasaidia kujitegemea na kuchangia maendeleo.
  Wahitimu wa mafunzo ya kushona nguo kwa wasiiona, wakiwa kwenye picha ya pamoja wakiwa na na nyuso za furaha, wakionyesha vyeti vyao vya kuhitimu mafunzo ya kushona kwa cherehani kwa watu wenye ulemavu wa kutoona, baada ya kuhitimu mafunzo haya ya miezi 6, , yaliyoendeshwa na mkufunzi mwenye ulemavu, Dr. Abdalah Nyangalio na kufadhiliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE. Wahitimu hao, wameomba jamii iwasaidie kupata cherehani ili waweze kuutumia ujuzi walioupata, kujitegemea badala ya kuendelea kuwa omba omba.

  Kwa Upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa TANTRADE, Edwin Rutageruka, baada ya TANTRADE kugundua kipaji cha  kushona cha Abdala Nyangalio, mwenye ulemavu wa kutoona, ilimpatia fursa kushiriki maonyesho ya sabasaba, na maonyesho mbalimbali ya nje ya nchi, ndipo ikaamua kuanzisha mafunzo hayo ili kuutumia utaalamu wa Nyangalilo kuwasaidia wasiona wengine wenye vipaji vya ushonaji bila kujijua.

  Rutageruka ametoa wito kwa Jamii kujitokeza kununua bidhaa za walemavu hawa, ili kuwaunga mkono, na kwa upande wake, amesema TANTRADE  itaendelea kuwafungulia fursa, watu wenye ulemavu, ili kuvitumia vipaji vyao mbalimbali kuzalisha mali,  kwa kuwaunganisha  na masoko kupitia maonyesho ya Saba Sana, na kuwapeleka soko la Afrika ya Mashariki hatimaye kuzitumia fursa za soko la AGOA.

  Mgeni rasmi  ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, aliyewakilishwa na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, Mafuku Kabeya, ameipongeza TANTRADE kwa kuanzisha mafunzo hayo, na kutoa wito kwa  jamii na taasisi ziunge mkono juhudi za TANTRADE  ili kutanua wigo wa mafunzo hayo kuwafikia  walemavu wengine mbalimbali wenye vipaji, kuwafundisha wengine kujitegemea na kuchangia maendeleo ya taifa.
  Mkufunzi wa mafunzo ya kushona kwa wasiiona, ambaye yeye mwenyewe haoni, Dr. Abdalah Nyangalio akimuonyesha Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke Mafuku Kabeya, (katikati), nguo zilizoshonwa na watu wenye ulemavu wa kutoona, walizoshona kwa cherehani, baada ya kuhitimu mafunzo haya ya miezi 6, yaliyo fadhiliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, Tantrade. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa TANTRADE, Edwin Rutageruka. Wahitimu hao, wameomba jamii iwasaidie kupata cherehani ili waweze kuutumia ujuzi walioupata, kujitegemea badala ya kuendelea kuwa omba omba.

  Mwenyekiti wa Chama cha Wasiona cha Mkoa wa Dar es Salaam,Alex Lwimbo, ameiomba jamii na taasisi kujitolea  kusaidia uwezeshaji ya watu wenye ulemavu, ili waweze kujitegemea, kwa hoja kuwa walemavu wakiwezeshwa, wanaweza.


  0 0

  Na Editha Karlo,wa blog ya jamii,Kigoma.

  HATIMAYE aliyekuwa Shekhe wa mkoa Kigoma kwa zaidi ya miaka 30,  Taufiq Malilo amezikwa huku sehemu kubwa ya wananchi wa mkoa Kigoma wakijitokeza kuhudhuria mazishi hayo.

  Shekhe Malilo ambaye alifariki Ijumaa jioni ya wiki iliyopita kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya kisukari na moyo amezikwa juzi jioni katika makaburi ya Kazaroho Ujiji mjini Kigoma.

  Katika mazishi hayo yaliyofanyika majira ya saa 11 jioni yaliacha vilio na simanzi kwa mamia ya waislam waliohudhuria msiba huo, wengi wakikumbwa mafundisho ya dini ya kislam katika kuishi maisha ya kumcha Mwenyezi Mungu.

  Akisoma Wasifu wa marehemu Katibu wa BAKWATA wilaya ya Kigoma vijijini ,Sheikh Yassin Kabunguru alisema kuwa Alhaji Malilo alichaguliwa kuwa Sheikh wa mkoa Kigoma mwaka 1979 hadi mauti yalipomfika akiwa pia Ulamaa wa Taifa.

  Sheikh Kabunguru alisema kuwa katika uhai wake Alhaji Malilo alifundisha dini na kutembelea misikiti zaidi ya 600 mkoani Kigoma akiweka kambi kwa ajili ya kufundisha dini na kufungua shule mbalimbali za kiislam mkoani Kigoma kwa juhudi kubwa ambayo aliifanya binafsi.

  Akitoa mawaidha kabla ya kuelekea makaburi Sheikh Uwesu Mohamed alisema kuwa Alhaji Malilo aliishi katika misingi sita ya kiislam ambayo ilimfanya kuwa mcha Mungu,mnyenyekevu anayewapenda wengine,asiye na tamaa wala kujilimbikizia mali na kwamba Marehemu amekufa akiwa hana hata gari kutokana na sehemu kubwa ya kipato chake kutumia kuendeleza masuala ya dini.
   Waumin wa dini ya Kiislam wakisalia mwili wa Marehemu Sheikh Taufiq Malilo aliyekuwa Sheikh wa mkoa Kigoma kabla ya mwili huo kupelekwa makaburi ya Kazaroho kwa mazishi.
   Mamia ya waumini wa dini ya kiislam na wananchi wa mkoa Kigoma waliojitokeza nyumbani kwa Marehemu Taufiq Malilo aliyekuwa Shekhe wa mkoa Kigoma Muda mfupi kabla ya mwili kuzikwa
   Mamia ya waumini wa dini ya kiislam na wananchi wa mkoa Kigoma waliojitokeza nyumbani kwa Marehemu Taufiq Malilo aliyekuwa Shekhe wa mkoa Kigoma Muda mfupi kabla ya mwili kuzikwa


  0 0


  0 0

  Na Bashir Nkoromo

  Hatimaye Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi na Mbunge wa Kuteulia na Rais Alhaj Abdallah Bulembo, amemaliza ziara yake ya Kichama akiwa amefanikiwa kutembelea mikoa saba na jumla ya Wilaya 47 za mikoa hiyo.

  Katika ziara hiyo ambayo alianza May 26, 2017, aliihitimisha jana, Juni 10, 2017 katika mkoa wa Geita, ziara ikiwa imechukua zaidi ya wiki mbili, ambapo mkoa wa kwanza kufanya ziara hizo uliuwa Dar es Salam na badaye kuendelea katika mikoa ya Dodoma, Manyara, Tabora, Kigoma, Kagera na Geita ambao ndio mkoa aliomalizia.

  Alhaj Bulembo katika ziara hiyo ambayo haikuhusu Jumuia yake ya Wazazi Tanzania, bali ya Kichama zaidi ilikuwa mahsusi kwa kuagizwa na Bosi wake, Mwenyekiti wa CCM Rais John Magufuli, kwa lengo la kutoa shukrani kwa wana CCM kufuatia kura nyingi walizompa hadi kukipatia Chama Cha Mapinduzi kura nyingi wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 2015.

  Hata hivyo Bulembo anasema, Shukrani hizo, ni za awali kwa kuwa Mwenyekiti Mwenyewe Rais Dk. John Magufuli atafanya ziara rasmi kutoa shukrani.
  Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akisiriki kuapa wakati wanachama wapya waliohamia CCM kutoka Chadema walipokuwa wakiapa na kuungwa mkono na wanachama wote katika kiapo hicho
  Wanachama wapya wa CCM wakiapa
  Wanachama wa CCM wapya wakiapa huku wakiungwa mkono na wanachama wote waliokuwa ukumbini, kula kiapo hicho
  Alhaj Bulembo akimvalisha kofia mmoja wa wanachama hao wapya


  0 0


  0 0

  Na Jumbe Ismailly, Singida

  MKUU wa Mkoa wa Singida, Dk.Rehema Nchimbi ameahidi kuvifuta vyama vya msingi vya wakulima wa zao la Tumbaku pamoja na Bodi ya Tumbaku ya Mkoa wa tumbaku Manyoni endapo wakulima wa zao hilo watakosa soka la kuuzia tumbaku yao waliyolima kwa mwaka 2016/2017.

  Akifungua soko la zao la tumbaku kwa msimu wa kilimo wa 2016/2017 uliofanyika katika Chama cha Ushirika cha Msingi Isingiwe LTD Mitundu,Mkuu huyo wa Mkoa alisisitiza kwamba endapo wananchi hao watabaki na zao la tumbaku ndani ya nyumba zao,mwenyekiti wa Bodi ya tumbaku ndiyo itakuwa mwisho wa kuitumikia nafasi hiyo.

  “Wananchi hawa wakibaki na tumbaku ndani nasema kabisa Bodi ya tumbaku hapa Mwenyekiti ujue kabisa uenyekiti wako haupo,ndiyo, kabisa kwa hiyo hii risala mliyonisomea hii tena mngesema afadhali tusingesoma na kuongeza….. 
  Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk.Rehema Nchimbi (mwenye kufunga kitambaa kichwani) akipokea taarifa ya uteuzi wa madaraja ya tumbaku kutoka kwa mteuzi wa zao hilo,Bwana Charles Kizighaaliyevaa sare ya bluu).

  Wanabaki na tumbaku hawa wananchi bila kupata soko vyama vya msingi hamna kazi,hamna kazii,lakini najua Mrajisi msaidizi ambaye ndiyo mlinzi na mlezi wa vyama hivi utahakikisha unasimama kwamba vyama hivi vikae vizuri na viendeleze heshima yake”alisisitiza.

  Hata hivyo Dk.Nchimbi aliwataka watendaji,hususani maafisa ugani katika Halmashauri ya Itigi kujenga utamaduni wa kuishi na wakulima wa zao la tumbaku badala ya kuwatembelea pale tu wanapohitaji michango ya shughuli mbali mbali za mandeleo.
  Marobota ya tumbaku yakiwa kwenye ghala la kuhifadhia tumbaku kabla ya kufanyiwa uteuzi wa madaraja na mteuzi wa zao hilo kutoka katika Bodi ya Tumbaku.

  Katika risala ya wakulima wa zao la tumbaku wa vyama vitano iliyosomwa kwenye sherehe na Mwenyekiti wa Chama Cha Ushirika cha Isingiwe,Daud Ngayaula imevitaja vyama vitano vilivyolima zao la tumbaku kwa msimu wa kilimo wa 2016/2017 kuwa ni pamoja na IsingiweAmcos,Manyanya Amcos,Idodoma Amcos,Mtakuja Amcos na Umoja Amcos.

  Aidha Mwenyekiti huyo wa Isingiwe Amcos alibainisha kwamba vyama hivyo vinatarajia kuzalisha kilogramu 295,000 ambazo iwapo zitanunuliwa zote kwa wastani wa bei ya kitaifa ya dola mbili za kimarekani kwa kilo,vyama hivyo vitapata dola 590,000 za zenye thamani ya shilingi 1,298,000,000/= za kitanzania.
  baadhi ya wakulima wa zao la tumbaku kutoka katika vyama vitano vinavyolima tumbaku katika kata ya Mitundu,tarafa ya Itigi,wilayani Manyoni.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).

  Hata hivyo Ngayaula hakusita kuzitaja baadhi ya changamoto zinazovikabili vyama hivyo kuwa ni kupewa uzalishaji mdogo wa Makampuni na kujitoa kwa Kampuni ya AOTTL kutonunua zao la tumbaku kwa msimu wa kilimo wa 2017/2018.

  Naye Mteuzi wa zao hilo kutoka Bodi ya tumbaku,Charles Kizigha alisema katika siku ya kwanza ya ufunguzi huo wa soko tumbaku iliyonunuliwa ina thamani ya dola za kimarekani 575.786 sawa na shilingi za kitanzania milioni 1,281,085.13 kwa bei ya shilingi 2,225. 

  0 0


  0 0

  Duka la viwalo vikali hapa mjini la J&M Virgo limetoa bonge la ofa la punguzo la bei ya bidhaa zake kwa wateja wake katika kipindi hiki cha Mwezi wa Ramadhan na kuelekea Sikukuu ya Idd El Fitr, hivyo kuwahi kwako mapema ndio kufaidi punguzo hilo, maana bei sasa ni karibu na bure kabisa. Hivyo watembelee Dukani kwao pale Mikocheni B usoni kabisa mwa Kiota cha Safari Canival karibu ya Daraja la Mlamakuwa au waweza kuwapigia simu kwa namba hii 0715 534 530, Pia uweza wafuate katika ukurasa wao KWA KUBOFYA HAPA

  Bofya hicho kimshale hapo juu kuona Video hii.
  Magauni ya mitoko.
   Skuna za haja.
   Moka za kisasa kwa kinaBaba.
   Mikoba.
  Suti.

  0 0  Mchezaji soka wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Sammata ameihakikishia kampuni ya Bia ya Serengeti ambayo ni wadhamini wa timu ya taifa Taifa Stars kwamba wachezaji wa timu hiyo watajituma ili kuhakikisha kuwa wanashinda mechi zote walizopangiwa kwenye ratiba.

  Samatta ambaye ni nahodha wa timu hiyo ya taifa alitoa hakikisho hilo jijini Dar es Salaam jana katika mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) na kuhudhuriwa na Meneja Masoko wa SBL, Nicholus Machugu. Mkutano huo ulijadili mechi kati ya Taifa Stars na Lesotho timu ambayo Stars inatarajiwa kucheza nayo katika mashindano yajayo.Alithibitisha kuwa timu hiyo haitaiangusha SBL katika mechi zake kwa kuwa kampuni hiyo imeonesha kuithamini kutokana na udhamini wake kwa timu hiyo.

  Aidha alitoa wito kwa wachezaji wenzake kuhakikisha kuwa wanajiweka vizuri kkwa ajili ya mechi hizo ili waweze kuingia na kutambuliwa katika ramani ya soka barani Afrika.

  Samatta ambaye hivi sasa anafanya shughuli zake kama mchezji wa kulipwa nchini Ubeljiji aliinga jijini Dar es Salaam Jumatano ya wiki hii ili kuungana na wachezaji wenzake wa timu ya taifa kwa ajili ya mechi ya duru ya kwanza ya kufuzu mashindano Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON). Duru ya pili ya mashindano hayo itafanyika Januari 2018 na mechi ya fainali inatarajiwa kufanyika kufanyika Cameroon mwka 2019.

  Kwa upande wake Kocha wa Timu hiyo Salum Mayanga alisema kwamba timu yake imejitayarisha sawasawa kwa ajili ya mechi zote na kuongeza kuwa mazoezi ya timu hiyo iliyoyafanya walipokuwa Alexandria, Misri walikokuwa hivi karibuni hivi karibuni yaliwapa mwanga na ana matarajio makubw kwamba timu hiyo itashinda mechi zote.

  Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ni mashindano ni mashindano makubwa ya kimatiafa barani Afrika. Mashindano hayo yalianzishwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), na yalifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1957.

  Kuanzia mwaka 1967, yamekuwa yakifanyika kila baada ya miaka miwili. Wanachama wa Mashirikisho ya Soka ya FIFA ndio walio na sifa za kushiriki mashindano hayo.

  Mchezaji soka wa kimataifa wa Tanzania na Nahodha wa Taifa stars Mbwana Sammata akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema m mwishoni wa wiki iliyopita kuhusu maandalizi yao ya kucheza na Lesotho katika mkutano na waandishi uliofanyika katika makao makuu ya TFF .

  Waandishi wa habari wakichukua matukio katika mkutano huo uliofanyika mapema mwishoni mwa wiki iliyopita. 

  0 0

  Wanaharakati walioshiriki changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro wakiimba na kucheza wakati wakishuka kutoka Mlima Kilimanjaro.
  Timu ya Wanaharakati 86 kutoka taasisi na kampuni mbalimbali walioshiriki changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia mapambano dhidi ya Ukimwi wakishuka kutoka katika kilele cha Uhuru.  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Geita ,Herman Kapufi aliyeshiriki Changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za mapambano ya Ukimwi.Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi ,TACAIDS ,Dkt Leonard Maboko akizungumza katika hafla fupi ya kuwapokea wanaharakati hao. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akitoa hotuba yake ya kwanza wakati w hafla fupi ya kuwapokea wanaharakati hao.
  Wanaharakati katika changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za mapambano ya Ukimwi kupitia kampeni ya Kili Challange inayoratibiwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mngwira.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.


  0 0

  Na Ripota wetu
  Watalii wanaokuja Tanzania na kuelekea moja kwa moja kwenye hifadhi za taifa za Serengeti, Kilimanjaro au Ngorongoro inamaanisha nini? Ni kwamba wanakuwa wamekwishaambiwa kuwa ukifika Tanzania sehemu pekee za kutembelea ni hizo tu? Je tunawezaje kukabiliana na hali hii ambayo kwa namna moja ama nyingine inaweza kufifisha vivutio vilivyopo maeneo mengine nchini kutotembelewa?
  Hakuna anayeweza kubisha kwamba sehemu ya Kaskazini mwa Tanzania imebarikiwa kwa kiasi kikubwa kuwa na vivutio visivyopatikana duniani kote. Vivutio kama hifadhi za kitaifa za Serengeti, bonge la Ngorongoro, Mlima Kilimanjaro na hivi karibuni mti mrefu zaidi barani Afrika uligunduliwa.

  Tunapenda kukufahamisha kwamba tangu mwaka huu wa 2017 uanze nchi yetu imeshuhudia watu mbalimbali maarufu duniani wakifurika nyanda za Kaskazini wakiwemo Waziri Mkuu mstaafu wa Israel, Bw. Ehud Barak, muigizaji wa filamu kutokea Hollywood nchini Marekani, Will Smith na familia yake.

  Kama hiyo haitoshi hazijapita hata wiki mbili tangu aliyekuwa nguli wa kusakata kabumbu nchini Uigereza, David Beckham ambaye aliwahi kuvichezea vilabu vya Manchester United, Real Madrid, LA Galaxy na PSG naye kutembelea hifadhi ya mbuga ya Serengeti akiwa na familia yake.

  Huyo hakuwa mchezeji pekee kutokea bara la Ulaya kufanya hivyo kwani nyota anayechezea kwa mkopo katika klabu ya Crystal Palace inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza akitokea Liverpool, Mamadou Sakho naye pamoja na mkewe na watoto wake wa kike wawili wameonekana wakifurahi mapumziko yao katika hifadhi ya mbuga ya wanyama ya Serengeti.

  Jambo la msingi la kujiuliza hapa ni kwanini watu hao wote mashuhuri pindi tu watuapo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Nyerere hubadilisha ndege na kuelekea moja kwa moja uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro ambapo kutokea pale ni rahisi kwenda hifadhi za kitaifa za Serengeti, Ngorongoro na Mlima Kilimanjaro?

  Tunafahamu kwamba suala la watalii kutembelea sehemu wanazozitaka wanapofika nchini Tanzania ni maamuzi yao na pia huchangiwa na sababu kadhaa kama vile vivutio miundombinu kama vile usafiri, hoteli zenye hadhi na kuvutia lakini pia na hali ya hewa kinaweza kuwa kigezo kingine.

  Kwa kuzingatia sababu za miundombinu na huduma bora za malazi na zenye viwango vya kimataifa, hakuna ubishi kwamba nyanda za Kaskazini zimejitahidi kwa kiasi kikubwa kukidhi mahitaji ya watalii. Lakini linapokuja suala la vivutio vya kitalii na hali ya hewa bado Tanzania tumejaaliwa vivutio vya kila aina na hali ya hewa nzuri karibuni kila mikoa ya nchi hii.


  0 0  Fundi Sanifu Mkuu Bonde la Pangani Bw. Vendelin Basso akionesha namna ya kusoma vifaa vya kupima kina cha maji kwa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu (bajeti) Bi. Grace Mosha
  Muonekano wa Vifaa vya kisasa vya kupima kina cha maji vilivyofungwa na mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari katika mto Kikuletwa Kijiji cha Kikwe Meru ambavyo husaidia katika taarifa za utabiri wa hali ya hewa na kuchukua tahadhari ya mafuriko. 

  Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari Bw.Daniel Alfei akizungumza na baadhi ya wanufaika wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari (hawapo pichani) walipotembelea kufanya tathimini ya utekelezaji wa mradi huo Wilayani Arumeru Juni 09, 2017. 
  Baadhi ya wakazi wa Vijiji vya Mbuguni Wilayani Arumeru wakimsikiliza Mratibu Taifa wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari Bw.Daniel Alfei (hayupo pichani) wakati wa tathimini ya utekelezaji wa mradi huo iliyofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu 09Juni, 2017.


older | 1 | .... | 1741 | 1742 | (Page 1743) | 1744 | 1745 | .... | 3283 | newer