Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110133 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI JUMATATU KUPOKEA TAARIFA YA KAMATI YA PILI YA UCHUNGUZI WA MADINI KWENYE KONTENA


KONGAMANO LA PILI LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI LAFANYIKA MKOANI DODOMA LEO

$
0
0

 Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN), Dkt.  Jim Yonazi akijibu hoja mbalimbali ambazo ziliibuliwa katika kongamano la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika leo mjini Dodoma . TSNwalikuwa mmoja wa wadhamini. Dk Yonazi alisema kuwa ili kuwaezesha wananchi kiuchumi ni lazima jamii ihabarishwe juu ya fursa mbalimbali zilizopo, lakini pia muhimu wa sekta binafsi kuwa na ubunifu na mifumo ya kujitengenezea utajiri.

Afisa Mtendaji Mkuu wa MM Maxcom , Juma Rajab akielezea uzoefu wake na kusema kuwa inahitajika kuwawezesha wajasiriamali wote, wadogo, wa kati na wakubwa ili kufanikisha wananchi kuweza kuingia katika uchumi wa viwanda.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akitoa mada juu ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi ambapo alisema ni vyema viongozi na jamii ikawana na utaratibu wa kuchapa kazi ili iweze kufanikiwa katika suala la uwezeshaji wananchi kiuchumi.
.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala akisalimiana Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira walipokutana katika Kongamano la pili la  Uwezeshaji wananchi Kiuchumi mjini Dodoma.
 Dk. John Kyaruzi kutoka SAGGOT CTF akitoa mada na kuweka wazi kuwa taasisi hiyo iko vizuri kuwawezesha wananchi. Aidha alisema ni vyema sasa wananchi wakalazimishwa kulima kibiashara tofauti na ilivyo sasa. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA




Wakaazi wa Mbezi Beach na Mikocheni B jijini Dar es salaam wasafisha fukwe za bahari.

$
0
0
 Mjumbe wa Serikali za Mtaa wa Mikocheni B, Kamati ya Mazingira Moses Sanga pamoja na Victoria Kileo wa Nipe Fagio wakiwa wamebeba taka wakati wa zoezi la kufanya usafi katika fukwe za Mbezi Beach leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo limeshirikisha Marafiki wa Bahari, Nipe Fagio,Mbezi Beach Neighborhoods. 
 Delicia Mwanyika and Cindy Tibazarwa kutoka Mbezi beach Neighborhoods wakishirikiana kuokota taka sugu kama vile Plastiki, makopo, nguo, viatu, nyavu, mataili, sindano, vyupa na taka nyinginezo.
 Beatrice Steyn Muasisi wa Mbezi Beach Neighborhoods akizungumza na waandishi wa habari wakati wa  zoezi la kufanya usafi wa fukwe ya Mbezi Beach katika kuokoa Bahari ambapo alisisitiza ushirikiano kutoka Serikali, Viwanda, Taasisi mbalimbali pamoja na watu binafsi kuungana kwa pamoja kurudisha uhai wa bahari ambayo inaelekea kufa kama hakuna hatua itakayo chukuliwa sasa.

 Boss Brown Muasisi wa Marafiki wa Bahari kutoka Mikocheni B akiwa katika zoezi la kufanya usafi katika fukwe za Mbezi Beach leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo limeshirikisha Marafiki wa Bahari, Nipe Fagio,Mbezi Beach Neighborhoods
Washiriki wa zoezi la usafi wa fukwe wa Mbezi Beach wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kwa zoezi hilo leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi hiloni harakati za kuunga mkono kampeni ya kuiokoa Bahari ambalo limeshirikisha asasi za Nipe Fagio, Mbezi Beach na Friends Of Ocean kutoka Mikocheni B chini ya udhamini wa Nabaki Africa, Koncept Communication Pamoja na AFM 92.9 ya mjini Dodoma.

Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson awajulia hali watoto wanawaosubiri kufanyiwa upasuaji wa Moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimpokea  Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Tulia Ackson alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto  wanawaosubiri kufanyiwa upasuaji.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akieleza jinsi wanavyotoa  huduma za matibabu ya magonjwa ya Moyo kwa Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Tulia Ackson alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanawaosubiri kufanyiwa upasuaji.
.
  Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimbembeleza mtoto Venance  Christopher (14) aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kusubiri upasuaji wa  Moyo. Mhe. Dkt. Tulia alitembelea Taasisi hiyo   leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji.
 Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiongea jambo wakati akimjulia hali mtoto Rashid Kombo aliyelazwa katika  chumba cha uangalizi maalum (ICU) baada ya kufanyiwa upasuaji wa Moyo. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani akifuatiwa na  Daktari Bingwa wa Moyo kwa watoto na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo kwa Watoto Dkt. Sulende Kubhoja. 
Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimsikiliza Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa Watoto na Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto Godwin Sharau alipotembelea leo chumba cha upasuaji wa Moyo kilichopo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwetwe (JKCI). Picha na  Anna Nkinda wa JKCI.


J&M Virgo yatoa Punguzo la bei la karibu na Bure

$
0
0
Duka la viwalo vikali hapa mjini la J&M Virgo limetoa bonge la ofa la punguzo la bei ya bidhaa zake kwa wateja wake katika kipindi hiki cha Mwezi wa Ramadhan na kuelekea Sikukuu ya Idd El Fitr, hivyo kuwahi kwako mapema ndio kufaidi punguzo hilo, maana bei sasa ni karibu na bure kabisa. Hivyo watembelee Dukani kwao pale Mikocheni B usoni kabisa mwa Kiota cha Safari Canival karibu ya Daraja la Mlamakuwa au waweza kuwapigia simu kwa namba hii 0715 534 530, Pia uweza wafuate katika ukurasa wao KWA KUBOFYA HAPA

Bofya hicho kimshale hapo juu kuona Video hii.
Magauni ya mitoko.
 Skuna za haja.
 Moka za kisasa kwa kinaBaba.
 Mikoba.
Suti.

MRADI WA HIPZ WAANDAA MBIO ZA BASKELI KUKUSANYA FEDHA KWA AJILI YA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA HOSPITALI YA MAKUNDUCHI NA KIVUNGE

$
0
0


Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar

Mradi wa Kuimarisha huduma za Afya Zanzibar (HIPZ) unatarajia kukusanya zaidi ya dola za Marekani 25,000 kwa ajili ya kusaidia huduma za afya katika Hospitali ya Makunduchi na Kivunge ambazo wanazisaidia.
Fedha hizo zitapatikana kufuatia kuandaa resi za baiskeli za kilomita 300 (Bike Ride 2017) katika mikoa mitatu ya Unguja yatakayo dumu kwa muda wa siku sita kuanzia leo.

Akizungumza na waandishi wa habari Hoteli ya Tembo, Mratibu wa resi hizo Dkt. Jon Rees kutoka Uingereza  amesema jumla ya wapanda baiskeli 25 kutoka Ulaya na Zanzibar wanashiriki.

Amesema fedha hizo zitachangwa na makampuni ya ndani na nje ya nchi  na zitatumika kuimarisha huduma za afya hasa  afya ya mama na mtoto katika Hospitali za Kivunge na Makunduchi.

Amesema Resi hizo ambazo ni mara ya tatu kufanya  Zanzibar zilianzia Mji Mkongwe kuzunguka maeneo mbali mbali ya Mkoa Mjini Magharibi zitapitia Nungwi, Makunduchi, Kizimkazi na zitrejea Mji Mkongwe.

Dkt. Ress amewataka wananchi wa Zanzibar kuwaunga mkono na kuwatia hamasa wapanda baiskeli hao hasa katika sehemu watakazopita.Akizindua resi hizo, Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt. Fadhil Abdalla Mohd amesema Mradi wa HIPZ  umeleta mafanikio makubwa katika ubunifu wake wa kutafuta fedha kwa ajili ya  huduma za afya kwa kuanzisha mbio hizo.

Amesema pamoja na kukusanya fedha kwa ajili ya huduma za afya pia mbio hizo ni sehemu ya kuwashawishi vijana kufanya mazoezi ambayo ni moja ya njia ya kujikinga na maradhi yasiyoambukiza.

Dkt. Fadhil amesema wakati serikali ipo katika mpango wa kuzipandisha daraja Hospitali ya Makunduchi na Kivunge kuwa za Mkoa, fedha hizo zitatumika kuanzisha majengo mapya na kuimarisha huduma za afya.
MBI1
Mratibu wa resi za baskeli (Bike Ride 2017) Dkt. Jon Rees akizungumza na waandishi wa habari kuhusu dhamira ya mbio hizo Zanzibar ikiwa ni mara yake ya tatu.
MBI2
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Abdalla Mohd akizungumza na washiriki wa resi za baskeli kabla ya kuanza rasmi  zikiwa na lengo la kuimarisha huduma za afya Hospitali ya Kivunge na Makunduchi.
MBI3
Picha ya pamoja ya washiriki wa Bike Ride 2017 wakifurahia mbio hizo kabla ya kuanza rasmi.
MBI5
Washiriki wa resi za baskeli (Bike Ride 2017) wakikata maeneo ya  viwanja vya Maisra kuendelea na safari yao itakayochukua sita sita.
Picha na Makame Mshenga.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNE 11,2017

KISOMO CHA DUA YA KUMWOMBEA AUNTY REHEMA CHAFANYIKA DMV

$
0
0
Aunty Rehema (kati) akiwa katika picha ya pamoja na Mr and Mrs Gao siku ya Jumamosi June 10, 2017 Silver Spring, Maryland nchini Marekani siku akina dada DMV wakitaribiwa na TAMCO walipomfanyia dua.

Aunty Rehema akijipakulia futari  siku ya Jumamosi June 10, 2017 Silver Spring, Maryland nchini Marekani siku akina dada DMV wakitaribishwa na TAMCO walipomanyia dua la kumwombea.

Wakina dada wa DMV waandaaji huku wakiwa wameratibiwa na TAMCO wakiwa katika picha ya pamoja na Aunty Rehema.

Kushoto ni Ustadh Gadafi pamoja na Miki wakiongoza dua la kumwombea Aunty Rehema. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

RAIS DKT MAGUFULI KUPOKEA RIPOTI YA PILI YA MCHANGA WA MADINI KESHO

BREAKING NEWZZZZ: WAZIRI MKUU AMSIMAMISHA KAZI BOSI WA EWURA

Introducing new hit "ORUGAMBO" by Saida Karoli

MICHEZO NI AFYA, AJIRA, BURUDANI - EFM 73.7

$
0
0
Wakazi wa mwanza wameaswa kuendelea na utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara pamoja na kujiunga katika vikundi mbalimbali vinavyohusiana na michezo  kwa manufaa ya afya zao. Wito huo umetolewa na Afisa utawala wa wilaya ya Ilemela Mr. Saidi Kitinga katika uzinduzi wa  kikundi cha EFM jogging Mwanza, uliofanyika siku ya Jumamosi tarehe 10/06/2017 katika kiwanja cha Furahisha.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na vikundi mbalimbali vya mbio za mwendo pole (Jogging) za mkoa huo pamoja na maafisa kutoka katika ngazi ya wilaya na mkoa.
Efm redio kupitia kikundi chake cha Jogging inatarajia kuhamasisha jamii umuhimu wa mazoezi katika kila mkoa ambao redio itafika, na kuhakikisha jamii inanufaika kupitia mazoezi.
 Wakaazi wa mkoa wa Mwanza wakiongozwa na Kikundi cha Efm katika mbio za mwendo pole
 Wakaazi wa mkoa wa Mwanza wakiongozwa na Kikundi cha Efm katika mbio za mwendo pole
 Mazoezi ya viungo katika uwanja wa Furahisha – Mwanza
Kulia ni Meneja Mkuu wa Efm redio Dennis Busulwa pamoja na Maulid Kitenge Mtangazaji wa Efm redio kipindi cha michezo
Meneja Mkuu Efm redio Dennis Busulwa katika picha ya pamoja na maofisa kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza.

Article 0

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA MRADI WA PROGAMU YA KITAIFA YA KUKUZA UJUZI WA NGUVU KAZI, MKOANI IRINGA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu(sera, bunge, kazi, vijana, na watu wenye ulemavu), Mhe Jenista Mhagama, akiwa na Naibu Waziri Mhe Anthony Mavunde wakikagua karakana na baadhi ya kazi zinazofanywa na Taasisi ya Don Bosco wanaotekeleza mradi wa Programu ya kitaifa ya kukuza ujuzi wa nguvu kazi wa stadi za maisha ya Taifa kwa vijana, Mkoani Iringa mpango ambao utawanufaisha vijana elfu tatu mianne 3,400 mpango unaogharamiwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu(sera, bunge, kazi, vijana, na watu wenye ulemavu), Mhe Jenista Mhagama amezindua Programu ya kitaifa ya kukuza ujuzi wa nguvu kazi wa stadi za maisha ya Taifa kwa vijana, Mkoani Iringa mpango ambao utawanufaisha vijana elfu tatu mianne 3,400 mpango  unaogharamiwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli.

Mhe Mhagama amesema mpango huu ni sehemu ya kuwaandaa vijana ambao watashiriki katika mapinduzi ya viwanda nchi Tanzania na utasaidia kutoa fursa kwa vijana kujiajiri na kuajiriwa kupitia mafunzo ya Uanagenzi, katika nyanja za ujenzi, tehama, ufundi magari, na ushonaji nguo katika mikoa yote nchini Tanzania.

Katika awamu hii ya kwanza, mpango huu unaendeshwa kwa pamoja baina ya Serikali ya Tanzania na taasisi ya Wasalesiani wa Don Bosco Tanzania.

Uzinduzi huo umeshuhudiwa na Naibu waziri Mhe Anthony Mavunde, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina Masenza, Wabunge kutoka mkoa wa Iringa, na Njombe na Mkuu wa Shirika la Wasalesiani wa Don Bosco Africa Mashariki Fr. Simon Asira.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu(sera, bunge, kazi, vijana, na watu wenye ulemavu), Mhe Jenista Mhagama akiangalia baadhi ya bidhaa katika moja ya mabanda baada ya kuzindua Programu ya kitaifa ya kukuza ujuzi wa nguvu kazi wa stadi za maisha ya Taifa kwa vijana, Mkoani Iringa. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Anthony Mavunde.
Picha ya Pamoja.

GOR MAHIA MABINGWA WA SPORTPESA SUPER CUP 2017, WAWATANDIKA FC LEOPARDS BAO 3-0

$
0
0
 Mabingwa ma Mashindabo ya SportPesa Super Cup 2017, Timu ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya wakishangilia ushindi wao na Kombe la Ubingwa huo, baada ya kuwatandika wapinzani wao FC Leopards Mabao 3-0 katika mchezo uliomalizika hivi punde katika Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam.
 Mabingwa ma Mashindabo ya SportPesa Super Cup 2017, Timu ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya wakishuhudia Nahodha wao akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Dola elfu 30, baada ya kutwaa Ubingwa wa Mashindano hayo kwa kuwatandika wapinzani wao FC Leopards Mabao 3-0 katika mchezo uliomalizika hivi punde katika Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam. 

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Timu ya Gor Mahia ya Kenya imetwaa ubingwa wa kwanza wa mashindano ya SportPesa Super Cup baada ya kuwasambaratisha wapinzani wao, AFC Leopards kwa mabao 3-0 kwenye uwanja wa Uhuru.

Kwa ushindi huo, Gor Mahia imepata nafasi ya kupambana na timu maarufu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Everton FC  Julai 13 kwenye uwanja wa Taifa jijini.

Kwa ushindi huo, Gor Mahia ilizawadiwa Sh milioni 62 za Tanzania huku AFC Leopards ikiambulia Shilingi Milioni 22 kwa kushika nafasi ya pili.

Mabao ya Timotho Otieno katika dakika ya 60, OliverMaloba katika dakika ya 76 na John Ndirangu katika muda wa nyongeza yalitosha kuinyamazisha AFC Leopards kwenye fainali hiyo iliyokuwa ya kusisimua.

Dalili za ushindi kwa Gor Mahia zilionekana tokea mwanzoni  mwa mchezo huo ambapo mshambuliaji wake hatari, Medie Kagere alikosa baola wazi baada ya pasi nzuri ya GeorgeOdhiambo.

Baada ya kosa kosa hiyo, AFC Leopards ilikuja juu na kukosa nafasi tatu za kufunga kupitia kwa Gilbert Fiamenyo, Allan Katerega na Mangoli Benard. Mshambuliaji hatari wa Gor Mahia,Medie Kagere aliibuka  kuwa mfungaji bora wa mashindano hayo kwa kufunga mabao manne.





WATANZANIA WATAKIWA KUBADILI FIKRA KUFIKIA UCHUMI WA VIWANDA

$
0
0
Watanzania wametakiwa kubadili fikra za kimtanzamo na kila mtu kutimiza wajibu wake kwa lengo la kuunga mkono dhamira ya serikali ya  awamu ya tano ili kujenga uchumi wa viwanda na kuboresha ustawi wa jamii.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama alisema hayo wakati alipokuwa akifungua Kongamano la Pili la  Uwezeshaji Watanzania Kiuchumi, kuwa watanzania wanatakiwa kubadili fikra za kimtanzamo ili kuweza kufikia uchumi wa viwanda, na kuboresha ustawi wa jamii.

“ Nchi yetu imeamua kubadilisha mwelekeo wa uchumi wa nchi yetu na sisi tunawajibu wa kubadili fikra za kimtanzano ili kufikia uchumi wa viwanda,” aliongeza kusema Bi. Mhagama, ambaye alifungua kongamano hilo kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Pia aliwataka washiriki wa kongamano kwenda kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha suala la uchumi wa wananchi unakuzwa. Na aliwasisitiza watumishi wa umma kuwa mfano katika kuchochea dhamira hiyo kwa kufanya kazi kwa vitendo.

Alisema serikali imeweka mikakati kabambe ya kuandaa nguvu kazi yenye ujuzi  inayoendana na soko la ajira kupitia program mbalimbali ikiwemo ya kuwafundisha vijana ujuzi waweze kutumika katika nguvu kazi. Na aliwataka wakuu wa mikoa yote kuainisha fursa za kiuchumi na kumpatia waziri mkuu ili zifanyiwe kazi.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama kushoto  akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Dk. John Jingu (katikati) na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo,  Bi. Beng Issa kulia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la  Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama kushoto  akikata utepe(ribbon) kuashiria kuzindua wa taarifa ya utekelezaji wa sera ya taifa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ya Julai 2015 mpaka April 2017 wakati wa Kongamano la Pili la  Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi,(katikati) Mwenyekiti wa Bodi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Dk. John Jingu na kulia ni  Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Bi. Beng’i Issa.  
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama kushoto  akionyesha kitabu cha taarifa ya utekelezaji wa sera ya taifa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ya Julai 2015 mpaka April 2017 mara baada ya kuzindua taarifa hiyo wakati wa Kongamano la Pili la  Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi,(katikati) Mwenyekiti wa Bodi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Dk. John Jingu na kulia ni  Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Bi. Beng’i Issa.  
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama kushoto  akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Bw. Joel Bendera  taarifa ya utekelezaji wa sera ya taifa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ya Julai 2015 mpaka April 2017 mara baada ya kuzindua taarifa hiyo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la  Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng Issa.

KUSOMA ZAIDI BOPFYA HAPA

Mbunge AMINA MOLLEL awakumbuka Watoto Wenye Mahitaji Maalum, Shinyanga

$
0
0
 
Mbunge wa Viti Maalumu Bi Amina Mollel, akiwakabidhi msaada wa vitu Mbalimbali Wanafunzi wenye mahitaji Maalumu wa Shule ya Msingi Buhangija iliyopo mkoani Shinyanga, Sambamba na Msaada huo aliweza Kukabidhi Kadi za Bima ya Afya Kwa ajili ya Matibabu. 
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Buhangija Wakiwa wameketi, Wakati Mbunge wa Viti Maalum Bi Amina Mollel alipofika Kwenye Kituo hicho Kukabidhi Misaada ya Vitu Mbalimbali Ikiwemo Chakula na Kadi ya Bima ya Afya Kwa ajili ya Matibabu Kwa Watoto hao. 
Mbunge wa Viti Maalum Bi Amina Mollel akipata Maelezo Mbalimbali Kutoka Mmoja wa Viongozi wa Kituo cha Buhangija Kinachohudumia Watoto wenye Mahitaji Maalum.

 
Watoto wenye Albnism Wanaosoma Shule ya Msingi Buhangija iliyopo Mkoani Shinyanga Wakimsikiliza Mbunge wa Viti Maalum Bi Amina Mollel, aliyefika Kwenye Kituo Hicho Kuwapatia Msaada wa Vitu Mbalimbali ikiwemo Kadi za Bima ya Afya Katika Mwezi Huu Mtukufu wa Ramadhani.

 
Mbunge wa Viti Maalum Bi Amina Mollel akizungumza na Baadhi ya Viongozi pamoja na Walimu Katika Shule ya Msingi ya Buhangija iliyopo Mkoani Shinyanga, Baada ya Kukabidhi Msaada wa Vitu Mbalimbali pamoja na Kadi za Bima ya Afya Kwa ajili ya Matibabu Kwa Watoto wenye Mahitaji Maalum. 

Walimu wa Shule ya Msingi ya Buhangija Wakiwa Katika Picha ya Pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Bi Amina Mollel ambae alifika Kwenye Shule hiyo Kwa ajili ya Kutoa Msaada Kwa Watoto wenye Mahitaji Maalum.

Picha kwa Hisani ya www.habari360.co.tz

Amani Kabuku wa Dar es Salaam aibuka kidedea Milioni 20 za Biko

$
0
0
DROO ya 13 ya Biko waendeshaji wa mchezo wa kubahatisha Tanzania maarufu kama ‘Ijue Nguvu ya Buku’, imefanyika leo asubuhi, huku mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaa, Amani Kabuku, mwenye miaka 23, akifanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa Sh milioni 20.

Mshindi huyo ameibuka katika droo iliyochezeshwa jana jijini Dar es Salaam na Balozi wa Biko, Kajala Masanja, kwa kushirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.

Akizungumza katika droo hiyo leo asubuhi, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, alisema ni wakati wa kutajirika kwa kupitia mchezo wao wa Biko uliozidi kujizolea umaarufu katika kipindi kifupi tangu kuanzishwa kwake nchini Tanzania.

Alisema anaamini washindi wao wanaoendelea kujipatia fedha mbalimbali kupitia mchezo wao, huku akiwataka Watanzania waendelee kucheza kwa kufanya miamala ya fedha kwenye simu zao za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kwa kuanzia Sh 1,000, ambapo namna ya kucheza ni kuweka namba ya kampuni ambayo ni 505050 na ile ya kumbukumbu 2456.

“Wanachotakiwa kufanya ni kucheza mara nyingi zaidi ili wajiwekee mazingira mazuri yaushindi wa zawadi mbalimbali kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, huku zikilipwa moja kwa moja kupitia simu zao za mikononi walizotumia kuchezea Biko,” Alisema Grace.
Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja kulia akiwa kwenye majukumu ya kumtafuta mshindi wa droo ya 13 ya Biko ambapo kijana mwenye miaka 23 mkazi wa Mbezi Makonde, jijini Dar es Salaam, Amani Kabuku, alifanikiwa kuibuka na zawadi nono ya Sh Milioni 20. Kushoto ni mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.

Kajala Masanja kulia akizungumza huku akionyesha namba ya mshindi wa Sh Milioni 20 kutoka Mbezi Makonde, jijini Dar es Salaam baada ya kutangazwa mshindi katika droo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, huku akishuhudiwa na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MTOTO WA MIAKA 12 AIBUKA KIDEDEA MASHINDANO YA KUHIFADHI QURAN

$
0
0

*Waziri Mkuu amuagiza Meya wa Temeke kesho atoe maamuzi ya kiwanja

MTOTO wa miaka 12 kutoka Somalia, Mohammed Abdullahi Aden ameibuka kidedea na kitita cha dola za Marekani 7,000 (sawa na sh. milioni 15.75) katika mashindano ya 18 ya Afrika ya kuhifadhi Quran kwenye kundi la washiriki wa juzuu 30.

Mohammed ambaye ni miongoni mwa washiriki wadogo zaidi wawili kuliko wote (mwenzake anatoka Burundi), amejishindia pia IPAD, cheti, kompyuta iliyotolewa na Balozi wa Kuwait, ahadi ya sh. milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na ahadi ya kwenda nchi yoyote aitakayo kutoka kwa kampuni ya Sky Bus Travel Agency ya jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na maelfu ya waumini na Watanzania waliofurika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo mchana (Jumapili, Juni 11, 2017), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa waandaaji wa mashindano hayo ambayo ni Taasisi ya Al-Hikma waangalie uwezekano wa kuboresha zawadi kwa kutoa scholarships (udhamini) kwa washindi au washiriki, hususan kwa washiriki wa Tanzania.

“Ongeeni na nchi marafiki kama Saudi Arabia, waone uwezekano wa kutoa zawadi za ufadhili kwenye masomo ya sekta za kimkakati kama vile mafuta na gesi, ili kuongeza hamasa na chachu ya vijana walioko kwenye sekondari zetu nao waone fursa hii na kuichangamkia, badala ya mashindano kujikita kwenye madrasa peke yake,” amesema.

Waziri Mkuu amewataka wazazi wafuatilie nyendo za vijana wao ili wasijiingize kwenye matumizi ya dawa za kulevya na vitendo vingine viovu vinavyoweza kuhatarisha maisha yao na ustawi wa nchi yetu lakini akasisitiza pia waisaidie Serikali katika mapambano yake dhidi ya rushwa na ufisadi.

  Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa akizungumza katika kilele cha Mashindano  ya 11 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. 
Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa akizungumza katika kilele cha Mashindano ya 11 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi , Mohammed Abdullah Aden (12) wa Somalia hundi ya shilingi milioni 15, 750,000/= mshindi wa kwaza wa mashindano ya 18 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi , Mohammed Abdullah Aden (12) wa Somalia hundi ya shilingi milioni 15, 750,000/= mshindi wa kwaza wa mashindano ya 18 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akizungumza katika mashindano hayo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo. 
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili na Mlezi wa Taasisi ya Al- Hikma Foundation, Alhaj Ali Hassan Mwinyi akizungumza katika kilele cha Mashindano ya 18 ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally (kulia) na Sheikh Sharif Abduqadir Mohamed Ahmed Al Ahdar ambaye ni Rais wa Taasisi ya Al – Hikima Foundation na Mlezi Mwenza wa Taasisi hiyo , katika Mashindano ya 18 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mufti na Sheikh Sharif Abduqadir Mohamed Ahmed Al Ahdar ambaye ni Rais wa Taasisi ya Al – Hikma Foundation na Mlezi Mwenza wa Taasisi hiyo, katika Mashindano ya 18 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


PROF. JUMMANE MAGHEMBE ATEMBELEA JAMII YA WAHADZABE, KABILA AMBALO BADO WANAISHI KWA KUWINDA NA KUCHUMA VYAKULA BILA UZALISHAJI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jummane Maghembe akishuhudia jamii ya Wahadzabe wakitengeneza chakula cha mchana ambao ni unga utokanao na ubuyu. Kabila la Wahadzabe ni moja ya jamii za wawindaji na wakusanyaji wanaopatikana Tanzania ambao chakula chao kikuu ni nyama, matunda, mizizi na asali
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jummane Maghembe akionja unga wa ubuyu ambao ndiyo chakula maarufu cha jamii ya Wahadzabe.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jummane Maghembe akipewa maelezo kuhusu nyumba maarufu za jamii ya Wahadzabe
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jummane Maghembe akipewa maelezo ya matumizi ya mshale katika jamii ya Wahadzabe
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jummane Maghembe akichezewa ngoma maarufu ya jamii ya Wahadzabe ambayo huchezwa wakati wakimpokea Mgeni mwenye hadhi katika jamii.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jummane Maghembe akisaini kitabu cha Wageni mara alipowasilia katika kijiji cha Yaeda chini wilayani Mbulu mkoani Manyara.
Mkurugenzi wa Rasilimali Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)Bw. Zawadi Mbwambo (katikati) akisikiliza kwa makini risala iliyosomwa na Wawakilishi wa Jamii ya Wahadzabe kwa Mgeni rasmi
Viewing all 110133 articles
Browse latest View live




Latest Images