Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1743 | 1744 | (Page 1745) | 1746 | 1747 | .... | 3272 | newer

  0 0  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, itaingia kambini tena Juni 14, mwaka huu kujiandaa na michuano inayoratibiwa na Baraza la Soka la Kusini mwa Afrika (COSAFA).

  Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Juni 25, mwaka huu ambako Taifa Stars itakwenda Misri, Juni 20, mwaka huu.

  Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amepanga kufanya mabadiliko madogo ya kikosi cha Taifa Stars kitakaochokwenda kushiriki michuano hiyo.

  Kocha Mayanga amesema kesho atafanya uteuzi wa wachezaji wengine atakaowajumuisha kwenye kikosi chake, atafanya mabadiliko kidogo hivyo kesho atatangaza majina ya wachezaji ambao wataingia kambini kujiandaa na michuano hii ya Cosafa inayoanza Juni 25 huko Afrika Kusini.

  Wakati huo huo, awamu ya pili ya kozi ya Daraja A inayoendeshwa na Shirikisho la soka Afrika (CAF) imeanza leo kwenye ukumbi wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF).

  Kozi hiyo inahusisha makocha 20 ambao walishiriki kwenye kozi hiyo ya awamu ya kwanza iliyofanyika jijini Dar es Salaam Novemba, mwaka jana.

  Mkufunzi wa kozi hiyo ni Mtanzania Sunday Kayuni ambaye pia atakuwa na wataalam wa masuala ya Lishe, Masoko, Tiba, Habari, Bima pamoja na mtaalam wa masuala ya upingaji wa matumizi ya utumiaji wa dawa ả kuongeza nguvu michezoni.
  a


  Kocha wa Stars Salum Mayanga akiwa na Nahodha wa timu ya Taifa Mbwana Samatta.

  0 0


  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisalimiana na Balozi wa Iran hapa nchini Mousa Farhang alipokwenda kumpa pole kufuatia shambuliyo la Kigaidi katika Bunge la nchi hiyo ambapo watu 12 waliuwawa wakimeo Wabunge 6.
  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Iran kufuatia shambulizo la Kigaidi katika Bunge la nchi hiyo ambapo watu 12 waliuwawa wakimeo Wabunge 6. Kushoto ni Balozi wa Iran hapa nchini Mousa Farhang.
  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (katikati) akizungumza na Balozi wa Iran hapa nchini Mousa Farhang alipokwenda kumpa pole kufuatia shambulizo la Kigaidi katika Bunge la nchi hiyo ambapo watu 12 waliuwawa wakimeo Wabunge 6. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini Mhe. Dotto Biteko ambaye aliambatana na Mhe Spika na kushoto ni Mkalimani wa Balozi huyo.
  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akiagana na Balozi wa Iran hapa nchini Mousa Farhang mara baada ya kumpa pole kufuatia shambulizo la Kigaidi katika Bunge la nchi hiyo ambapo watu 12 waliuwawa wakimeo Wabunge 6.

  (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

  0 0


  Naibu waziri wa Kazi,Vijana ,Ajira na Watu wenye Ulemavu Ndg. Anthony Mavunde leo amefanya mazungumzo na Balozi wa Uswisi Mh Florence Mattli katika ofisi za Wizara ya Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu mjini Dodoma juu ya namna bora ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uswisi katika eneo la Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana kupitia mpango unaotekelezwa na Wizara.

  Balozi Mattli ameupongeza mpango wa Wizara wa utekelezaji wa Program ya Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana nchini kupitia mafunzo stadi ambayo yana lengo la kuwajengea Vijana wa Tanzania ujuzi stahiki na hivyo kuwawezesha kuwa na sifa za kuajiriwa,Kujiajiri na kuajiri Vijana wengine.

  Balozi Mattli ameahidi kushirikiana na Serikali katika kuunga mkono juhudi za Wizara katika uendeshaji wa Mafunzo ya Ufundi kwa Vijana kwa kufadhili kiasi cha Shilingi 34,000,000 USD kwa miaka 12 kwa ajili ya utekelezaji bora wa Mpango wa Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana nchini.

  0 0

   Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Mwanza, akishuhudia mzani unaopima Pamba mara baada ya msimu wa Ununuzi kuanza
   Marobota ya Pamba yanayo subiri kuuzwa baada ya msimu kufunguliwa mkoani Simiyu
   Maafisa wa Wakala wa Vipimo Nchini, ukionesha Mizani iliyo kaguliwa na kukubaliwa kutumika katika msimu wa ununuzi wa Pamba kwa mwaka huu.
   Afisa wa wakala wa Vipimo, Bibi Rehema Michael akipima usahihi wa robota la Pamba kwakutumia mizani iliyohakikiwa na wakala wa Vipimo  mkoani Simiyu mara baada yakufunguliwa kwa Msimu (Picha zote na Wakala wa Vipimo)
  Mkulima wa Pamba Mkoani Shinyanga akipima Pamba yake katika mzani uliohakikiwa.

  0 0


   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimvalisha Jeremiah Nkondo kuwa Naibu Kamishina wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla hiyo
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimvalisha cheo Tusekile Mwaisabila kuwa Naibu Kamishina wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla hiyo 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimvalisha cheo, Afwililwe Mwakijungu kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla hiyo
   Manaibu Kamishina  wa Magereza wakisoma Tamko la Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma baada ya kuvalishwa vyeo na Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa aktika hafla fupi  iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. 

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa magereza aliowavalisha Vyeo kwa Niaba ya Rais John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni, 12, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Naibu waziri wa Kazi,Vijana ,Ajira na Watu wenye Ulemavu Ndg Anthony Mavunde leo amefanya mazungumzo na Balozi wa/  Uswisi Mh Florence Mattli katika ofisi za Wizara ya Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu mjini Dodoma juu ya namna bora ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uswisi katika eneo la Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana kupitia mpango unaotekelezwa na Wizara.
  Balozi Mattli ameupongeza mpango wa Wizara wa utekelezaji wa Program ya Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana nchini kupitia mafunzo stadi ambayo yana lengo la kuwajengea Vijana wa Tanzania ujuzi stahiki na hivyo kuwawezesha kuwa na sifa za kuajiriwa,Kujiajiri na kuajiri Vijana wengine.
  Balozi Mattli ameahidi kushirikiana na Serikali katika  kuunga mkono juhudi za Wizara katika uendeshaji wa Mafunzo ya Ufundi kwa Vijana kwa kufadhili kiasi cha Shilingi 34,000,000 USD kwa miaka 12 kwa ajili ya utekelezaji bora wa Mpango wa Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana nchini.
  Naibu waziri wa Kazi,Vijana ,Ajira na Watu wenye Ulemavu Ndg Anthony Mavunde akizungumza  na Balozi wa  Uswisi nchini Mh Florence Mattli katika ofisi za Wizara ya Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu mjini Dodoma

  0 0

   Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza na Vijana wa JUVICUF Tawi la chuo kikuu cha Dar es Salaam katika mkutano wao uliofanyika katika hoteli ya Vinna Jijini Dar es Salaam.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Chama cha Wananchi CUF , julius Mtatiro akizungumza na Vijana wa JUVCUF Tawi la Chuo Kikuu juu ya umuhimu wa kujenga chama
   Mbunge Viti Maalum CUF ,Sevelina Mwijage akizungumza na Vijana wa JUVCUF tawi la Mlimani mara baada ya kuchangia shilingi laki tano za ujenzi wa ofisi
  Vijana wa JUVCUF Tawi la Mlimani wakishangilia mara baada ya kuwasikiliza viongozi wa chama hicho katika mkutano wa mkuu uliofanyika katika ukumbi wa Vinna Hotel

  0 0


  0 0


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Nehemiah Osoro Ikulu jijini Dar es Salaam.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha Ripoti hiyo ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini mara baada ya kukabidhiwa Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakishuhudia.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Ripoti hiyo ya Kamati ya Pili ya Uchunguzi wa Madini Ikulu jijini Dar es Salaam.


  0 0


   Wafanyakazi wa Benki ya KCB Bank Tanzania leo wamechangia damu. Hii ni katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya uchangiaji damu (world blood donor day) ambayo itaadhimishwa dunia nzima jumatano wiki hii, tarehe 14 Juni.

  Akizungumza wakati wa zoezi hilo  ambalo lilihudhuriwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Ummy Mwalimu, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Cosmas Kimario alisema  kuwa mchango huo upo ndani ya vipaumbele vya benki katika uwekezaji  jamii kwa ajili ya kusaidia jamii zilizo na uhitaji.

  “Benki ya KCB Tanzania inadhamini uwajibikaji kwa jamii ambayo kwa kiwango kikubwa inalenga maeneo ya vipaumbele vya Afya, Elimu Mazingira, Ujasiriamali na malengo yake hasa ni kujikita katika masuala ya ubinadamu” alisema Kimario.

  Mkurugenzi huyo alisema kuwa swala la kuchangia damu ni la muhimu sana kwani kuna wagonjywa wengi wenye hitaji la damu hivyo elimu juu ya uchangiaji damu salama ni muhimu kutolewa kwa jamii ili kuifanya jamii kuwa na uelewa mpana juu ya zoezi hilo. 

  “Tumeamua kuandaa uchangiaji wa damu ili kuisaidia serikali katika sekta ya Afya hususani katika kupunguza vifo vinavyotokana na upungufu wa damu” aliongeza Kimario.

  Akizungumza katika zoezi hilo Waziri Ummy Mwalimu aliipongeza Benki ya KCB Tanzania kwa mchango wake huo na kutoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano wa ukarimu wa Benki hiyo, akibainisha kwamba serikali inahitaji kubwa la damu hivyo inawahamasisha na kuwakaribisha watanzania wengi zaidi kujitokeza kuchangia damu na kuokoa maisha kwa kuwa serikali haiwezi kufanikisha malengo peke yake.
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mh. Ummy Mwalimu (kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawamo pichani) kuhusiana na zoezi la uchangiaji damu salama na kuipongeza Benki ya KCB kwa kushiriki katika zoezi hilo lililofanyika Makao Makuu ya benki hyo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Bw. Cosmas Kimario.
    Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mh. Ummy Mwalimu (kushoto) akimpongeza mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya KCB Bi. Francisca Alphonce kwa kuwa mmoja wa watanzania waliojitokeza kuchangia damu salama
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mh. Ummy Mwalimu (wapili kushoto) kwenye picha ya pamoja na sehemu ya timu ya menejimenti ya Benki ya KCB Tanzania na baadhi ya wakilishi kutoka wizarani. Timu ya menejimenti ya Benki ya KCB, Wapili kulia ni Bw. Cosmass Kimario, wakwanza kulia ni Bw. Masika Mukule, wakwanza kushoto ni Bi. Christine Manyenye, wakwanza kushoto juu ni Bi. Joyce Wiki Mwashigadi na watatu kulia juu ni Bw. Rojas Mdoe.  0 0

             
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka maaafisa na makamanda wa Jeshi la Magereza nchini waendelee kusimamia haki na usawa wanapotimiza wajibu wao.

  Ametoa wito huo leo jioni (Jumatatu, Juni 12, 2017) wakati akizungumza na maafisa na makamanda wa jeshi hilo katika hafla ya kuwavisha vyeo maafisa 29 iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), Ukonga, jijini Dar es Salaam.

  Waziri Mkuu ambaye amefanya kazi hiyo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amewavisha vyeo maafisa watano kuwa Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) na maafisa 24 kuwa Kamishna Waandamizi Wasaidizi wa Magereza (SACP). Maaafisa hao walipandishwa vyeo Mei 25, mwaka huu.

  “Ninyi ni viongozi wakuu katika mikoa mnayotoka. Huko kuna makamanda walio chini yenu na jamii inayowazunguka. Endeleeni kuwahudumiana na kulitumikia Taifa hili kwa weledi mkubwa. Endeleeni kusimamia usawa na haki katika kazi zenu za kila siku,” amesema.

  Waziri Mkuu amesema hana shaka na utendaji kazi wa jeshi la Magereza kwani watumishi wake ni waadilifu. “Jeshi hili linayo nidhamu ya hali ya juu, mbali ya jukumu lenu la ulinzi, mnafanya kazi nidhamu, weledi na uadilifu mkubwa,” amesema.

  Amesema Serikali inatambua changamoto zinazowakabili katika utendaji wao wa kila siku na kwamba inajitahidi kuzishughulikia hasa baada ya kukamilisha zoezi la kuondoa watumishi hewa.

  Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuhutubia maafisa hao, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Yusuph Masauni amewataka maafisa waliovishwa vyeo wazingatie maadili ya kazi zao na uzalendo kama ambavyo wameapa kwenye kiapo cha maadili.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua gwaride katika hafla fupi ya kuwavalisha Vyeo Maafisa Magereza kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa mahaliwa alimwakisha Rais John Pombe Mgufuli katika hafla hiyo.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimvalisha Jeremiah Nkondo kuwa Naibu Kamishina wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017.  Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla  hiyo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimvalisha cheo Tusekile Mwaisabila kuwa Naibu Kamishina wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika  hafla hiyo . (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimvalisha cheo, Afwililwe Mwakijungu kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla hiyo . (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) 
  Manaibu Kamishina wa Magereza wakisoma Tamko la Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma baada ya kuvalishwa vyeo na Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa aktika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla hiyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .


  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  0 0


  0 0


  0 0

  Taifa Stars - Picha na Bin Zubeiry
  Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, itaingia kambini tena Juni 14, mwaka huu kujiandaa na michuano inayoratibiwa na Baraza la Soka la Kusini mwa Afrika (COSAFA).
  Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Juni 25, mwaka huu ambako Taifa Stars itakwenda Afrika Kusini, Juni 20, mwaka huu.Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amepanga kufanya mabadiliko madogo ya kikosi cha Taifa Stars kitakaochokwenda kushiriki michuano hiyo.
  Kocha kesho atafanya uteuzi wa wachezaji wengine atakaowajumuisha kwenye kikosi chake, atafanya mabadiliko kidogo hivyo  kesho atatangaza majina ya wachezaji ambao wataingia kambini kujiandaa na michuano hii ya Cosafa inayoanza Juni 25 huko Afrika Kusini.
  Wakati huo huo, awamu ya pili ya kozi ya Daraja A inayoendeshwa na Shirikisho la soka Afrika (CAF) imeanza leo kwenye ukumbi wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF).Kozi hiyo inahusisha makocha 20 ambao walishiriki kwenye kozi hiyo ya awamu ya kwanza iliyofanyika jijini Dar es Salaam Novemba, mwaka jana.
  Mkufunzi wa kozi hiyo ni Mtanzania Sunday Kayuni ambaye pia atakuwa na wataalam wa masuala ya Lishe, Masoko, Tiba, Habari, Bima pamoja na mtaalam wa masuala ya upingaji wa matumizi ya utumiaji wa dawa  kuongeza nguvu michezoni.
  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

  0 0


  0 0

  Na  Bashir  Yakub
  Kwa kutumia kigezo cha usajili, Tanzania tunazo aina kuu mbili za  kampuni. Kampuni za ndani(Local companies) na kampuni za kigeni ( foreign companies). 
  Kampuni za ndani ni zile  zote zilizoanzishwa  hapa nchini na kusajiliwa hapa nchini. Hata kama wanahisa wake wote ni raia wa kigeni kwasababu tu ya kuanzishwa hapa na kusajiliwa hapa zinakuwa ni kampuni  za ndani. 
  Kampuni ya kigeni ni ile iliyoanzishwa na kusajiliwa nje ya Tanzania lakini ikaanzisha ofisi/biashara/tawi hapa Tanzania. Sheria Na. 12 Sheria ya Makampuni kifungu cha 433 kinasema hivyo. Kampuni kama imeanzishwa nje hata kama wanahisa wake wote ni Watanzania, hapa kwetu hiyo bado ni kampuni ya kigeni. 
  Kampuni ya ndani inaposajiliwa hupatiwa cheti cha usajili kiitwacho "Certificate of Incorporation" kwa mujibu wa kifungu cha 15(2) Sheria ya Makampuni. Kampuni ya ndani inapopata cheti hiki basi usajili wake huwa umekamilika na inatambulika rasmi kama kampuni ya ndani. 
  Kampuni ya kigeni inaposajiliwa hapa Tanzania hupatiwa cheti kiitwacho "Certificate of  Compliance" kwa mujibu wa kifungu cha 435(1) Sheria ya Makampuni. Kampuni ya kigeni inapopata cheti hiki basi  usajili wake huwa umekamilika na hutambulika rasmi kama kampuni ya kigeni. 
  Acacia ni kampuni ya kigeni. Kwa maana kuwa ilianzishwa nje ya Tanzania na kufungua shughuli zake hapa nchini. Kwa hiyo ili ihesabike imesajiliwa Tanzania ilitakiwa kuwa na cheti kiitwacho"Certificate of Compliance". Kutokuwa na cheti hiki maana yake ni kuwa haijasajiliwa Tanzania na haitambuliki.   0 0
  NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewataka Wakuu wa wilaya kuacha historia katika utendaji wao (legacy) kwenye maeneo wanayoongoza.

  Naibu Waziri Jafo aliyasema hayo mjini Morogoro alipokuwa akifungua semina kwa Wakuu wa wilaya ya kuwajengea uwezo katika usimamizi wa Miradi ya Maendeleo katika sekta ya Kilimo awamu ya pili(ASDPII) itakayotekelezwa kwa kipindi cha mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028.

  Akifungua semina hiyo, Jafo amewataka wakuu hao washindane katika kufanikisha Mipango ya maendeleo ya serikali ili kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. Kadhalika, amewataka wakurugenzi wa Halmashauri kuwapa taarifa za fedha za maendeleo ya miradi hiyo wakati wa utekelezaji ili wakuu hao wa wilaya waweze kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa Miradi hiyo.

  Jafo amesisitiza kwamba katika kipindi cha hichi ambacho kuelekea uchumi wa viwanda hapa nchini sekta ya kilimo ndio inategemewa kuzalisha malighafi za viwandani. Aidha amewataka wakuu hao wa wilaya kusimamia vyema sekta ya Kilimo ili Tanzania licha ya kutegemea mazao ya biashara kwa fedha za kigeni sasa Tanzania ijielekeze pia kuzalisha mazao mengi ya chakula.

  Amesema ukifanyika uzalishaji wa mazao ya chakula na ziada ya mazao hayo kuyauza nje ya nchi yataongeza fedha za kigeni nchini. “Tuna uwezo wa kufanya hivyo kutokana na uwepo wa ardhi ya kutosha yenye rutuba na vyanzo vingi vya Maji,”amesema Jafo

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya.

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi selemani Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa maendeleo pamoja waratibu wa ASDP II wa Ofisi ya Rais TAMISEMI na Ofisi ya Kilimo.

  0 0

  Na Fredy Mgunda, Mufindi.
  Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini mh Cosato Chumi amefanikiwa kutatua tatizo la vitanda katika shule ya sekondari Isalavanu iliyopo Kata ya Isalavanavu kwa kutoa vitanda 35 ikiwa lengo la kuendelea kuboresha na kuinua elimu ya shule hiyo.
  Akizungumza wakati wa kukabidhi vitanda hivyo alisema kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na ziara yake akiyofanya wiki kadhaa zilizopita wakati alipozitembelea shule mbalimbali za jimbo la Mafinga Mjini kujua changamoto na kuanza kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo.
  "Niligombea ubunge wa jimbo la Mafinga kwa lengo la kuleta maendeleo ndio maana Leo nipo hapa katika shule ya sekondari ya Isalavanu kuanza kuinua elimu ya shule hii kwa kuboresha miundombinu ya shule na baadae nitatu changamoto nyingine"alisema Chumi
  Chumi aliwataka wanafunzi wa shule ya Isalavanu kusoma kwa bidii ili kuleta matokeo chanya katika jimbo la Mafinga Mjini kwa lengo la kumuongezea kasi ya kutafuta wafadhili wa kusaidia kuleta maendeleo katika jimbo la Mafinga.
  " Kwa kweli najitahidi kutafuta wafadhili wa kusaidia kutatua changamoto za jimbo la Mafinga Mjini lakini wananchi wangu na ninyi wanafunzi mnatakiwa kunipa matokeo chanya na kufanya maendeleo yenu ya mtu moja moja na vikundi pia natamani siku moja kila sekta niwakute watu kutoka jimbo la mafinga Mjini" alisema Chumi

  Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini mh Cosato Chumi akimkabidhi vitanda 35  Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Mafinga ndg Charles Makoga kwa ajili ya kutatua changamoto zilizokuwa zinawakabili wanafunzi wa shule ya Isalavanu iliyopo katika Wilaya ya Mufindi
  Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiwa sambamba n wanafunzi wa shule ya sekondari y Isalavanu pamoja na Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga
  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1743 | 1744 | (Page 1745) | 1746 | 1747 | .... | 3272 | newer