Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 09.06.2017


MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JUNE 10,2017

RC TABORA ASEMA KUWEKA MAKUNDI KATIKA MABARAZA YANARUDISHA NYUMA MAENDELEO YA WANANCHI

$
0
0
Na Tiganya Vincent, NZEGA

Madiwani katika Halmashauri za  Mkoa wa Tabora  wametakiwa kuepuka kujenga makundi miongoni mwao ambayo yamekuwa yakisababisha wananchi waliowachagua kuchelewa kupata maendeleo kwa sababu ya muda mwingi kushughulikia migogoro badala ya kutatua matatizo mbalimbali ya wananchi.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri wakati akifunga mafunzo ya siku nne ya Madiwani na Watendaji wa Manispaa ya Tabora yaliyofanyika wilayani Nzega  kuhusu jitihada za jamii kupitia mbinu shirikishi jamii ya fursa na vikwazo kwa maendeleo (O&OD) iliyoboreshwa na usimamizi wa fedha za miradi ya maendeleo (LGDG)

Alisema makundi yatawafanya washindwe kuwajibika vizuri na kujikuta miaka mitano ya uongozi wao inakwisha bila kuwafanyia chochote wananachi zaidi ya kupigania kuondoana katika uongozi badala kukazania maslahi ya wananchi.

“Nyie ndio mliko zamu sasa mkiendekeza makundi na migogoro isiyokwisha, mtajikuta zamu zenu zinamalizika hamjawafanyia chochote wananchi waliowachagua badala yake kupambana kila mnapokutana katika vikao vyenu ….kila kikao itakuwa sisi hatumutaki fulani atuongoze au fulani fulani hatufai” alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.

Bw. Mwanri aliongeza kuwa wakimruhusu Shetani wa namna hiyo apite kati yao hakuna tena kazi wala maendeleo kwa wananchi wao waliowachagua.

SOMA ZAIDI HAPA

'KITIMOTO' MARUFUKU MAKAO MAKUU YA NCHI DODOMA

ENG. NGONYANI AKAGUA UJENZI WA BARABARA MBANDE- KONGWA KM 11.71

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. Deogratius Ndejembi (wa pili kushoto), pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakikagua barabara ya Hogoro - Kongwa KM 14.57 kwa kiwango cha changarawe wilayani humo, mkoani Dodoma jana.

Serikali imesisitiza nia yake ya kuhakikisha ujenzi wa barabara ya Mbande- Kongwa yenye urefu wa KM 11.71 inayojengwa kwa kiwango cha lami unakamilika kwa wakati.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amesema hayo mkoani Dodoma jana, mara baada ya kukagua sehemu ya mradi wa barabara ya Mbande-Kongwa- Mpwapwa yenye urefu wa KM 49.14 ambao ujenzi wake unaendelea na kumuagiza Kaimu Meneja Wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Dodoma Eng. Salome Kabunda kusimamia mradi huo kikamilifu.

"Tutahakikisha fedha za mradi huu zinapatikana kwa wakati ili mradi ukamilike mapema ikiwa ni mkakati wa kuifungua wilaya hii na kuhuisha fursa za kimaendeleo kwa wananchi wa Wilaya ya Kongwa na Mpwapwa", amesema Eng. Ngonyani.

Ameongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutafungua fursa za uwezekezaji katika maeneo hayo ikiwemo kurahisisha huduma za usafirishaji wa mazao kwa Wilaya hizo mkoani humo. Naye, Kaimu Meneja wa TANROADS, mkoa wa Dodoma Eng. Kabunda, amemhakikishia Naibu Waziri kuwa watamsimamia Mkandarasi anayejenga barabara hiyo kwa karibu ili ubora wa barabara hiyo uendane na thamani ya fedha.

Aidha, Eng. Kabunda amewataka wananchi wa Wilaya ya Kongwa kushirikiana na mkarandarasi ili kuwezesha ujenzi huo kwenda kwa haraka.

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. Deogratius Ndejembi ameishukuru Serikali kwa kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwani utachochea maendeleo wilayani humo.

Takribani shilingi Bilioni 7.5 zinatarajiwa kutumika katika sehemu ya kwanza ya mradi huo wa Mbande-Kongwa ambapo KM 5 zitajengwa na zinatarajiwa kumalizika ndani ya miezi nane.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto), akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. Deogratius Ndejembi (kulia), wakati alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mbande - Kongwa KM 11.71 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma jana.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. Deogratius Ndejembi (kulia), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto), mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mbande - Kongwa KM 11.71 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma jana.
Sehemu ya barabara ya Mbande - Kongwa yenye urefu wa KM 11.71 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma jana.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kulia), akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Dodoma Eng. Salome Kabunda (kushoto), wakati alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mbande - Kongwa KM 11.71 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma jana.

DMF YATOA "KAPU LA RAMADHAN" KWA WANANCHI WA KIJIJI CHA HOYOYO, MKURANGA MKOANI PWANI

$
0
0
 Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Taasisi ya Doris Mollel, Erick Kajahurwa akiwa katika maandalizi ya kugawa vikapu vya vyakula mbali mbali kwa wananchi wa Kijiji cha Hoyoyo, Mkuranga Mkoani Pwani, ikiwa ni sadaka inayotolewa na Taasisi hiyo kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kupitia kampeni yake ya KAPU LA RAMADHAN.
 Mratibu wa Matukio ya Kijamii wa Taasisi ya Doris Mollel, Alice Mwakatika (kushoto) akikabidhi sehemu ya vyakula kwa familia ya Mzee Seif Maruyo ambao ni wakazi wa Kijiji cha Hoyoyo, Mkuranga Mkoani Pwani, ikiwa ni sadaka inayotolewa na Taasisi hiyo kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kupitia kampeni yake ya KAPU LA RAMADHAN.
 Mratibu wa Matukio ya Kijamii wa Taasisi ya Doris Mollel, Alice Mwakatika (wa pili kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Taasisi hiyo, Erick Kajahurwa (kushoto) wakimsikiliza Bw. Shamte Ndikayi ambaye ni mlemavu wa macho, walipomtembelea nyumbani kwake Kijijini Hoyoyo, Mkuranga Mkoani Pwani, baada ya kukabidhi vyakula mbalimbali ikiwa ni sadaka inayotolewa na Taasisi hiyo kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kupitia kampeni yake ya KAPU LA RAMADHAN.

KATIBU MKUU BI SIHABA NKINGA KATIKA MAKAZI YA WAZEE YA NJORO MOSHI NA MAGUGU BABATI

taswira ya mawio huko Lufilyo

$
0
0
 Taswira ya mawio kutoka nyumba ya Profesa Mark Mwandosya huko Lufilyo, Busokelo, wilayani Rungwe mkoani Mbeya kama ilivyonaswa na yeye mwenyewe alipojilawakufanya mazoezi


'KITIMOTO' MARUFUKU DODOMA KUTOKANA NA MLIPUKO WA HOMA YA NGURUWE

Kamati ya Pili ya Mchanga wa Madini kuwasilisha ripoti yake kwa Rais Magufuli Jumatatu 12 Juni, 2017

TPA WASAINI MKATABA WA UPANUZI WA BANDARI YA DAR ES SALAAM.

$
0
0
Benjamin Sawe-Maelezo

Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), imesaini mkataba wa upanuzi na uongezaji wa kina cha bandari utakaowezesha bandari ya Dar es Salaam kupokea meli kubwa za mizigo na kushindana na bandari nyingine katika pwani ya bahari ya hindi.

Upanuzi huo utakaofanywa na kampuni ya China Harbor Construction ya China utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 336 na utadumu kwa miezi 36, ambapo utahusisha uongezaji wa kina cha lango la bandari na uongezaji wa kina cha maji kati ya gati namba 0, 1 hadi 7.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba huo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema hatua hiyo inalenga kuifufua upya bandari ya Dar es Salaam ili ifanye kazi kwa ushindani na kuhudumia wateja wengi kuliko ilivyo sasa. 

“ Kukamilika kwa upanuzi na uongezaji wa kina cha maji katika gati namba 1 hadi 7 kutoka mita 8 hadi 15 kutawezesha meli kubwa na za kisasa zenye uwezo wa kubeba hadi makontena elfu kumi na tisa kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam na kuongeza ufanisi na kukuza uchumi wa Tanzania”, amesema Prof. Mbarawa.

Aidha Prof. Mbarawa amesisitiza kuwa pamoja na upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam Serikali inaendelea na ujenzi wa miundombinu wezeshi ya reli na barabara ili kuhakikisha mizigo haikai muda mrefu bandarini.

“Ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge toka Dare s Salaam hadi Kanda ya Ziwa na Kigoma na ufufuaji wa reli ya Tazara kutawezesha bandari ya Dar e s Salaam kufanya kazi kwa ufanisi na kuvutia wafanyabiashara wengi hivyo nawataka wafanyakazi wote wa bandari kufanyakazi kwa bidii na uadilifu”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eng. Deusdedit Kakoko amesema kiasi cha dola za Marekani milioni 421, kitapatikana kwaajili ya ujenzi huo ambapo kati ya fedha hizo Benki ya Dunia itatoa mkopo wa masharti nafuu wa dola milioni 345.

Kukamilika kwa ujenzi huo kutaondoa adha ya baadhi ya meli kusubiri kwa muda mrefu kupata nafasi ya kutia nanga na kutaongeza hadhi ya bandari ya Dar es salaam na kuvutia wasafirishaji wengi kutoka ndani na nje ya nchi.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Prof: Makame Mbarawa (katikati) akishuhudia makabidhiano ya mkataba wa upanuzi na uongezaji wa kina cha Bandari kati ya Serikali na Kampuni ya China Harbour Engineering. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania (TPA). Mhandisi Deusdedit Kakoko na kushoto ni Mtedaji Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. XU XINPEI. (Picha na Benjamin Sawe- Maelezo).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania (TPA). Mhandisi Deusdedit Kakoko kulia na Mtedaji Mkuu wa Kampuni ya China Harbour Engineering Bw. XU XINPEI wakionyesha mkataba wa makubaliano ya upanuzi na uongezaji wa kina cha Bandari kwa wadau wa sekta ya usafirishaji baada zoezi la utiaji saini wa mkataba huo kukamilika. (Picha na Benjamin Sawe- Maelezo).

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Prof: Makame Mbarawa akiongea na wadau wa sekta ya usafirishaji kabla ya zoezi la utiaji saini wa mkataba wa upanuzi na uongezaji wa kina cha Bandari kati ya Serikali na Kampuni ya China Harbour Engineering. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania (TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko na kushoto ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari Bw. Mkinga Mkinga. (Picha na Benjamin Sawe- Maelezo).

AJALI YA MOTO

$
0
0

Basi la BATCO lenye namba za usajili T192DHW likiteketea kwa moto hii leo katika eneo la Kirumi kata ya Bukabwa Wilayani Butama Mkoani Mara, gari hilo lilikuwa linafanya safari zake kutoka Tarime-Sirari na Mwanza.Chanzo cha Moto huo bado hakijafahamika,taarifa za awali kutoka kwa baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo pamoja na abiria wameeleza kuwa baadhi ya mali za abiria zimeketea kwa moto,hakuna mtu aliyepoteza maisha..PICHA NA CLEO 24 NEWS

HABARI KAMILI TUTAENDELEA KUKUFAAMISHA



MBUNGE WA VITI MAALUM MKOANI RUVUMA, AZUNGUMZIA MAMBO MANNE ANAYOPAMBANA NAYO

$
0
0
Dakika mbili za Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Ruvuma kupitia chama cha mapinduzi (CCM ) Mhe. Sikudhani Chikambo, akizungumzia mambo manne anayopambana nayo katika mkoa wa Ruvuma.

AFC LEOPARDS USO KWA USO NA GOR MAHIA KWENYE MECHI YA FAINALI YA SPORTPESA SUPER CUP- USHEMEJI POPOTE

$
0
0
Na Zainab Nyamka-Globu ya Jamii.

Washindi wa nusu fainali za SportPesa Super Cup zilizofanyika Juni 08, 2017 Jijini Dar es Salaam, wanatarajiwa kukutana uso kwa uso kwenye mechi ya fainali ya kuwania kombe la michuano ya SportPesa Super Cup siku ya Jumapili ya tarehe 11, Juni 2017 itakayochezwa kwenye dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katika mechi za nusu fainali, AFC Leopards walipambana na mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara, Klabu ya Yanga na kuwang’oa kwa mikwaju ya penati 4-2 huku Gor Mahia kwa upande wao wakiifungasha virago timu ya Nakuru All Stars FC kufuatia ushindi wa magoli 2-0 ambayo yalitiwa kimiani na mshambuliaji Medie Kagere na George Odhiambo.     

Timu za Yanga na Nakuru All Stars FC ambazo ziling’olewa kwenye hatua ya nusu fainali, zilikabidhiwa medali za shaba na kiasi cha dola za kimarekani 5000 wakati wenzao (Gor Mahia na AFC Leopards) ambao wamefuzu kucheza fainali wakiwania kiasi cha dola za kimarekani 30,000.

Akizungumzia mshindano ya SportPesa Super Cup kwa ujumla, Mkurungezi wa Utawala na Utekelezaji SportPesa Tanzania Ndugu Abbas Tarimba alisema; “Michuano ilikuwa migumu ingawa timu zetu za Tanzania zimeaga katika hatua za awali lakini ni nafasi nzuri kwetu kama Tanzania kujipanga vizuri zaidi ili kuboresha sekta ya michezo na kufanya timu zetu kushika nafasi za juu maana kwa sasa tumeweza kutambua changamoto mbalimbali na jinsi ya kuzikabili.

SportPesa ni kampuni nguli ya michezo ya kubashiri inayojulikana kimataifa yenye makao yake makuu nchini Kenya ambayo imeanza rasmi shughuli zake nchini Tanzania Mei 9 mwaka huu na mpaka sasa imeshaingia makubaliano rasmi ya udhamini na vilabu vya Simba, Yanga na Singida United ikiwa imejidhatiti katika kuinua ba kuendeleza sekta ya michezo nchini.

TFF YATOA UFAFANUZI KUHUSU SERENGETI BOYS

$
0
0
Kuna taarifa zimekuwa zikienea na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii, zikidai kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewatelekeza wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17.

Wadai kwamba eti hawakulipwa posho na kushutumu viongozi wa juu wa shirikisho kuhusu jambo hilo. Hizi taarifa si za kweli.

Aidha, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linapenda kuwajulisha wazazi na umma kwa ujumla kwamba vijana wetu walilipwa posho zao zote wakiwa kambini Morocco na Cameroon na zile za mashindano ya AFCON nchini Gabon.

Vilevile, Shirikisho linafanya taratibu za kupeleka maombi kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (Football Development Fund FDF) ili kuweza kuwalipa vijana na benchi la ufundi sehemu ya posho zilizokuwa bado hazijakamilishwa wakati wa michuano ya kufuzu kwa AFCON 2017.

Tumeshtushwa na taarifa hizo ambazo tafsiri yake ni kuharibu uhusiano mwema kati ya shirikisho, wazazi na wachezaji ambao wanatarajiwa  kuitumikia timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka  20 maarufu kama Ngorongoro Heroes.

Shirikisho linaendelea kuwatambua vijana wa Serengeti Boys kwani bado ni sehemu ya kikosi cha Ngorongoro Heroes na hivyo ukifika wakati wataitwa kambini kwa ajili ya michezo ya kimataifa ya U-20.

TFF inazidi kuushukuru umma ambao umeendelea kuchangia Mfuko wa FDF ambao kimsingi kazi yake ni kutafuta rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya mpira.

Tunaomba michango iendelee kwani bado tuna changamoto za mashindano mbalimbali kwa timu za wanawake na vijana ikiwemo fainali za wanawake Afrika zitakazofanyika Ghana hapo mwakani kwa timu ya Twiga Stars na AFCON 2019 kwa Serengeti Boys ambayo itakuwa mwenyeji.

Mfuko wa Maendeleo ya Mpira - FDF ulianzishwa kwa lengo la kutafuta rasilimali za maendeleo ya mpira wa miguu hasa kwa wanawake na vijana pamoja na miundombinu ya mchezo huo.

Mfuko huo uko chini ya Mwenyekiti Bw. Tido Mhando anayeongoza Bodi na Mtendaji Mkuu (CEO) ni Bw. Dereck Murusuri anayesimamia sekretarieti.

Sheikh Shariff majini atikisa jiji la Tanga

$
0
0
Katika siku yake ya kwanza leo Jumamosi Tarehe 10 Juni 2017 Jijini Tanga, Sheikh Shariff Majini  ametikisa jiji hilo kwa mkutano uliokusanya watu wengi katika ukumbi wa Community centre uliopo kitongojini Makorora.
Mkutano wa mwisho wa Sheikh Shariff utafanyika kesho Jumapili tarehe 11 Juni 2017 katika Ukumbi wa Xommunity Centre uliopo Makorora.
Mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo Sheikh Shariff anataraji kurudi Dar es salaam tayari kwa kongamano la kina mama litakalofanyika ukumbi wa Star Light siku ya Jumamosi tarehe 24 Juni 2017.
 Sheikh Shariff Majini akihutubia umati wa kinamama katika  kongamano lake kwenye ukumbi wa Community centre uliopo kitongojini Makorora.
 Sheikh Shariff Majini akiendelea na kongamano lake katika  ukumbi wa Community centre uliopo kitongojini Makorora.
 Sehemu ya umati wa kinamama katika kongamano la Sheikh Shariff Majani kwenye ukumbi wa Community centre uliopo kitongojini Makorora.
Sehemu ya umati wa kinamama katika kongamano la Sheikh Shariff Majani kwenye ukumbi wa Community centre uliopo kitongojini Makorora.

BAMIZA TOP 20 MUSIC CHART 10th JUNE, 2017)

MASHINDANO YA QUR'AN YA AISHA SURURU FOUNDATION 2017

$
0
0
IMG-20170610-WA0116
Masheikh wa dini ya Kiislam na viongozi wakubwa akiwamo Sheikh Basaleh na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad, kwenye mashindano ya Qur'an yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
.
IMG-20170610-WA0114
Mgeni wa heshma, Mke wa Makamu wa Rais Mstaafu, Mama Gharib Bilal, akitoa nasaha kwa waumini wa dini ya Kiislam waliohudhuria katika mashindano ya Qur'an yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
IMG-20170610-WA0115
Mwanaharakati wa kijamii, Mwenyekiti na Mlezi wa Mashindano ya Qur'an ya Aisha Sururu Foundation, Bi Aisha Sururu, akitoa nasaha kwa waumini wa dini ya Kiislam waliohudhuria katika mashindano ya Qur'an yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
IMG-20170610-WA0111
Baadhi ya waumini wa Kiislam waliohudhuria kwenye mashindano ya Qur'an kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
IMG-20170610-WA0103
Baadhi ya waumini wa Kiislam waliohudhuria kwenye mashindano ya Qur'an kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

MICHUZI TV: IGP SIRRO AYASEMA HAYA AKIWA MKOANI MOROGORO LEO

WAZIRI MKUU APOKEA TAARIFA YA UCHUNGUZI WA SALFA

$
0
0
*Ni ya makontena 211 yaliyokuwa bandarini Dar
*Yabainika kuwa inafaa kwa matumizi ya kilimo
*Asisitiza wakulima waanze kupulizia mikorosho

       WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema salfa iliyoingizwa nchini kwenye makontena 211 haina kasoro na inafaa kwa matumizi ya kupulizia kwenye mikorosho.
Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Juni 10, 2017) wakati akizungumza na wajumbe wa kamati maalum, waagizaji wa salfa na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Korosho nchini (CBT) kwenye kikao alichokiitisha kwenye makazi yake, Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
“Bodi kaandaeni taratibu za kawaida kusambaza salfa kwa wakulima ili waanze kupuliza dawa hiyo. Wasichelewe kupuliza kwa sababu msimu umeshaanza,” amesema.
Juni 4, mwaka huu Waziri Mkuu alimuagiza Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samuel Manyele aende kuchunguza mzigo wa salfa ulioko bandari ya Dar es Salaam baada ya kutokea mkanganyiko uliosababishwa na ripoti ya TPRI kuwa ya salfa iliyoingizwa nchini na kampuni ya ETG Inputs Ltd kwa niaba ya Bodi ya Korosho haijakidhi viwango.

  Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele akiwasilisha ripoti ya uchunguzi wa salfa kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Juni 10, 2017. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt Mathew Mtigumwe. Kulia ni  Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti wa Ubora wa Bidhaa, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Daniel Ndiyo  
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza ripoti ya Mkemia Mkuu wa Serikali ,  Samwel Manyele (kulia) ya chunguzi  wa Salfa  kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Juni 10, 2017.   Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt, Mathew Mtigumwe. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images