Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1738 | 1739 | (Page 1740) | 1741 | 1742 | .... | 3284 | newer

  0 0


  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuhukumu Mfanyabiashara Shabani Hussein (44) maarufu kama "Ndama mtoto ya Ng'ombe" kulipa faini ya milioni 200 au jela miaka mitano baada ya kukiri shtaka la sita la kutakatisha fedha ambazo ni dola za Marekani 540,000.


  Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi, Mkuu wa mahakama hiyo Victoria Nongwa.


  Kabla ya hukumu hiyo kusomwa, upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Christopher Msigwa alimsomea maelezo ya awali (PH), Ndama dhidi ya shtaka lake hilo na kukiri.

  Hatua hiyo ya Ndama kusomewa hukumu katika shtaka moja tu la utakatishaji wa fedha kati ya matano yanayomkabili limekuja baada ya wiki iliyopita kuomba kukumbushiwa mashtaka yake na kukiri shtaka hilo la utakatishaji wa fedha.

  Akisoma hukumu hiyo, hakimu Nongwa amesema mahakama imezingatia hoja za upande wa mashtaka na ule wa utetezi ambapo upande wa mashtaka uliiomba mahakama kwa mujibu wa sheria ya kutakatisha fedha kifungu cha 13 (a)cha Sheria ya kuzuia utakatishaji fedha, kumpa adhabu kali mshitakiwa kwa kuwa makosa hayo yanalenga kudidimiza uchumi wa nchi.

  Amesema, mshitakiwa anastahili faini kwa kuwa ameipunguzia garama mahakama kuhusu shughuli za uendeshaji wa kesi hiyo ikiwemo gharama za kuleta mashahidi katika shtaka hilo 

  Ameongeza kuwa, Sheria hiyo ipo kwa ajili ya kuonesha kuwa makosa kama hayo hayatakiwi kumnufaisha mkosaji hivyo, atatakiwa kulipa faini ya milioni 200 na asipolipa ataandikiwa hati ya kifungo cha miaka mitano jela.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Kocha Mkuu wa Stars, Salum Mayanga akiwa na Nahodha wa timu Mbwana Samatta wakati wa mahojiano na waandishi wa habari.


  Taifa Stars watawakaribisha Mamba kesho kuanzia Saa 2:00 usiku Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019.  Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limetangaza wamuzi wa mchezo kati ya Tanzania na Lesotho na kwa mujibu wa CAF, waamuzi hao ni Abdillah Mahamoud - atakayekuwa mwamuzi wa kati wakati wasaidizi wake ni Gamaladen Abdi na Farhan Bogoreth wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Twagirumukiza Abdoulkarim kutoka Rwanda huku Kamishna akiwa ni Amir Hassan wa Somalia

  Kocha Mkuu wa Stars, Salum Mayanga amesema kuwa  timu imemaliza salama mazoezi na wana imani kesho watafanya vizuri.


  “Timu imemaliza salama mazoezi leo asubuhi, hali za vijana ni nzuri na nina imani tutafanya vizuri na tutapata ushindi na tunaiheshimu Lesotho, kwa sababu ukiangalia mechi za nyuma zote wamefanya vizuri hivyo tutajitahidi kufanya vizuri kwenye mchezo wa kesho,”amesema Mayanga.


  Taifa Stars itaingia kwenye mchezo wa kesho ikitoka kwenye kambi ya wiki moja nchini Misri na kwa ujumla huio utakuwa mchezo wa tatu kwa Mayanga tangu arithi mikoba ya Charles Boniface Mkwasa baada ya Machi mwaka huu kushinda 2-0 dhidi ya Botswana na 2-1 dhidi ya Burundi.

  Nahodha  wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amesema kwamba kwa vyovyote vile kesho lazima washinde dhidi ya Lesotho.  Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji amesema; “Afe kipa, afe beki lazima tuifunge Lesotho kesho,”


  Jeuri ya Samatta kuwatangazia ubabe mapema Lesotho inatokana na maandalizi ya timu kwa ajili ya mchezo huo na zaidi anashukuru yeye kama Nahodha wa timu yuko vizuri kuelekea mchezo huo.

  “Nimejiandaa vizuri kwa mechi ya kesho dhidi ya Lesotho na wachezaji wenzangu wote wapo vizuri na nina uhakika kambi walioiweka nchini Misri wamefanya mazoezi ya kutosha na tutafanya vizuri japo mechezo huu hautakuwa mwepesi,”amesema.

  Hivyo sasa Viingilio katika mchezo huo vitakuwa ni Sh 10,000 kwa Jukwaa Kuu wakati mzunguko itakuwa ni Sh 5,000.  0 0

  Serikali imetoa rai kwa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima nchini (TEWW) kuandaa mkakati wa kusaidia kupunguza idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika. 

  Rai hiyo imetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo wakati akifungua mkutano wa nane wa Baraza la Wafanyakazi la Taasisi hiyo.

  Akizungumza na wajumbe wa Baraza hilo, Dkt. Akwilapo aliitaka TEWW kuandaa utaratibu mzuri wa kuwafikia wananchi wengi ambao hawajui kusoma na kuandika ili waweze kupata elimu kupitia taasisi hiyo.

  “Ongezeko la wasiojua kusoma na kuandika linaelekea kuwa tatizo kubwa hapa nchini, hivyo natoa rai kwa taasisi hii kujadili namna ya kuendeleza kampeni za kisomo na kutoa mafunzo kwa wawezeshaji wa programu za kisomo ili kukabiliana na tatizo hilo.” Alisema Akwilapo.

  Sambamba na hilo Dkt. Akwilapo aliwasisitiza watumishi wa taasisi hiyo kufuata sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa shughuli zake ili kufikia malengo waliyojiwekea na kuleta matokeo chanya kwenye sekta ya elimu nchini.

  Aidha Katibu Mkuu huyo aliIshauri TEWW kuandaa utaratibu mzuri wa kuwasaidia kielimu wanafunzi wa kike walioshindwa kuendelea na masomo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kulazimishwa kuolewa au kupata ujauzito.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Dkt. Fidelis Mafumiko alisema kuwa taasisi hiyo inashirikiana na wadau mbalimbali katika kuendesha programu za elimu kwa vijana na watu wazima walikosa elimu kupitia mfumo rasmi.

  Alieleza kuwa program hizo ni pamoja na programu ya kuzuia ndoa za kulazimishwa za utotoni (Child Early and Forced Marriages) inayoendeshwa kwa kushirikiana na Taasisi ya Commonwealth of Learning ambayo imepanga kuwafikia walengwa 3000 katika mikoa ya Lindi, Rukwa na Dodoma.

  Pia Dkt. Mafumiko alisema kuwa TEWW kwa kushirikiana na UNICEF wanaandaa programu kwa ajili ya vijana walio nje ya mfumo rasmi wa shule ikilenga kuwafikia vijana wapatao laki tano ndani ya miaka mitatu katika mikoa ya Tabora, Katavi, Geita, Rukwa, Dodoma, Simiyu, Shinyanga, Singida, Lindi na Manyara. 

  Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ilianza mwaka 1975 na ipo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na ina jukumu la kutoa mafunzo kwa wataalamu wa Elimu ya Watu Wazima na kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya watu katika jamii wakiwemo waliokosa fursa ya kupata elimu katika mfumo rasmi.
  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa nane wa Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima uliofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Fidelis Mafumiko na Afisa Utumishi Bi. Mayasa Omary na kushoto ni viongozi wa vyama vya wafanyakazi.
  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Dkt. Fidelis Mafumiko akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi hiyo katika mkutano uliofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Kassim Nihuka na kulia ni watumishi wa taasisi hiyo.
  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima baada ya kufungua mkutano wa Baraza hilo jana Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Fatma Salum (MAELEZO)

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaelezea wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) umuhimu wa kupima afya zao mara kwa mara japo mara moja kwa mwaka wakati wafanyakazi hao walipofika katika Taasisi hiyo leo kwa ajili ya upimaji wa afya zao.
  Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Hesabu kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Fatuma Chillo akiuliza ni muda gani mzuri wa kupima shinikizo la damu mwilini (BP) wakati wafanyakazi wa shirika hilo walipofika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya upimaji wa afya zao. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Katibu wa NHC Martin Mdoe.
  Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Hesabu kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Fatuma Chillo akichukuliwa kipimo cha damu na Alex Onesmo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ikiwemo Moyo, figo na kisukari. Viongozi wa NHC walifika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwa ajili ya upimaji wa afya zao.


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  DROO ya makundi ya michuano ya Sports Extra Ndondo Cup imepangwa ambapo timu 32 zinatarajiwa kupambana katika kinyang'anyiro hicho. 


  Michuano hiyo ambayo ambayo bingwa mtetezi ni Temeke Market itaanza Jumamosi ya Juni 17 ambapo timu za Makuburi FC itacheza na Stimtosha kwenye uwanja wa Kinesi katika mchezo wa ufunguzi. 

  Bingwa huyo mtetezi amepangwa kundi G pamoja na timu za Makuburi, Stimtosha na Dar Polisi College. 


  Makundi hayo yamepangwa kama ifuatavyo: 
  Kundi A
  Misosi FC
  Buguruni United
  Kibo Combine
  Mdandu Investment

  Kundi B

  Kibada One
  Madiba FC
  Burudani FC
  Twiga International


  Kundi C
  Tabata United
  Wauza Matairi
  Mpakani Combine
  Vijana Rangers


  Kundi D
  Boom FC
  Temeke Squard
  Tandavamba FC
  Vituka FC


  Kundi E
  Keko Furniture
  Mlalakuwa Rangers
  Black Six
  Goroka FC


  Kundi F
  Kigogo Combine
  Goms United
  Ukwamani 
  Kigoma Combine


  Kundi G
  Temeke Market
  Makuburi FC
  Stimtosha FC
  Dar Police College


  Kundi H
  Kauzu FC 
  Faru Jeuri
  Shelaton
  Miami FC

  0 0

  WAENDESHAJI wa Bahati Nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku, jana wamemkabidhi zawadi yake jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wao wa Arusha, Oscar Haule, huku wakijigamba kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwakwamua washiriki wao kwa kuwapa fedha zao haraka ili waziingize katika majukumu yao ya kiuchumi.

  Mbali na kumpa zawadi hiyo ya fedha taslimu mshindi huyo, Biko pia wametangaza kutoa jumla ya Sh Milioni 500 kwa washindi wao waliocheza Biko mwezi Mei.

  Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa Biko Tanzania, Charles Mgeta, alisema wanaamini kuwa kiasi cha pesa walichompa mshindi wao atazitumia vizuri katika kujiletea maendeleo kama ilivyokuwa dhamira ya kucheza Biko na kufikia kutoa Sh Milioni 500 kwa washindi wa mwezi Mei.

  “Tunampongeza Haule kwa kushinda donge nono la Sh Milioni 20 kutoka Biko katika droo iliyochezeshwa juzi Jumatano, sambamba na kuwapongeza wote wanaocheza mchezo huu kwa njia ya ujumbe wa maandishi kwa simu zao za Tigo, Vodacom na Airtel kwa kufanya miamala kwenye simu zao kwa kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na ile ya kumbukumbu ikiwa ni 2456,” Alisema Mgeta.


  Naye Balozi wa Biko, Kajala Masanja alisema mchezo wa Biko ni rahisi kucheza pamoja na kushinda, hivyo kila Mtanzania anapaswa kuanza kucheza ili aweze kuibuka na ushindi wa zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, huku zawadi nono ya droo kubwa ya Jumapili hii ikiwa ni Sh Milioni 20 kama ilivyokuwa Jumatano iliyopita.

  “Huu ni wakati wakutajirika kwa kupitia Biko Tanzania ambapo hakuna bahati nasibu inayolipa haraka kama Biko, hivyo Watanzania wanapaswa kutumia vyema fursa za uwapo wa bahati nasibu hii iliyojizolea umaarufu nchini,” Alisema Kajala.


  Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko Oscar Haule mwenye fulana nyekundu akipokea hundi yake ya ushindi kutoka kwa Balozi wa Biko, Kajala Masanja.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Biko Tanzania, Charles Mgeta kulia akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa Milioni 20 wa Biko droo ya Jumatano Oscar Haule wa jijini Arusha mwenye fulana nyekundu.  0 0


  Na Benny Mwaipaja-WFM, Dodoma

  SERIKALI imeendelea kupata neema kutokana na uwekezaji wake kwenye mashirika na taasisi mbalimbali yanayojiendesha kibiashara nchini ambapo leo Shirika la Bima la Taifa (NIC) limetoa gawiwo la Shilingi bilioni 1.707 baada ya kupata faida kiabishara mwaka 2016/2017.

  Kwa nyakati tofauti mwaka huu, Serikali ilipokea kiasi cha Shilingi bilioni 1.7 kutoka Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na kufuatiwa na NMB Bank Plc, iliyotoa kiasi cha Shilingi bilioni 16.5 hivi karibuni.

  Akipokea Hundi kifani ya kiasi hicho cha Shilingi 1.707 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa, Bw. Sam Kamanga, Waziri wa Fedha na Mipango, amelipongeza shirika hilo kwa kuonesha maendeleo makubwa katika kipindi kifupi tangu azindue Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo mwishoni mwa mwaka uliopita.

  “Nilipozindua Bodi yenu ya Wakurugenzi uliniahidi Mkurugenzi Mtendaji kuwa mtafanyakazi kwa bidii na kuanza kutoa gawiwo Serikalini, ninajisikia furaha sana kwa niaba ya watanzania kuona kuwa mnatimiza ahadi hiyo kwa kutoa asilimia 15 ya pato ghafi la mapato yenu. Nawapongezeni sana” alisisitiza Dkt. Mpango.

  Alizitaka taasisi nyingine za umma zilizochini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina zinazofikia 260 kuanza kutumia huduma za bima kupitia Shirika la Bima la Taifa.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw. Sam Kamanga, akizungumza jambo wakati wa tukio la Shirika hilo kukabidhi gawiwo kwa Serikali, kiasi cha Sh. Bil. 1.7, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha, mjini Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (MB) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Sam Kamanga, katika hafla ya makabidhiano ya gawiwo la Sh. Bil.1.7 liyofanyika mjini Dodoma.
  Viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakishiriki tukio la Shirika la Bima la Taifa (NIC) kuikabidhi Serikali gawiwo la Sh. Bil. 1.7 baada ya Shirika hilo kufanya vizuri kibiashara katika Mwaka wa Fedha 2016/2017, tukio lililofanyika makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, mjini Dodom
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika, akifurahia jambo wakati wa tukio la Shirika la Bima la Taifa (NIC) kuikabidhi Serikali gawiwo la Sh. Bil. 1.7 baada ya Shirika hilo kupata faida katika mwaka wa fedha 2016/2017
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akisisitiza jambo wakati wa tukio la Shirika la Bima la Taifa (NIC) kukabidhi Serikalini gawiwo la Sh. bil. 1.7, baada ya Shirika hilo kupata faida kibiashara katika mwaka wa Fedha 2016/2017, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Mjini Dodoma
  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akitoa neno la Shukrani kwa uongozi Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwa ubunifu na uwajibikaji wao ulioliwezesha Shirika hilo kupata faida na kutoa gawiwo kwa Serikali, Mjini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango).


  0 0


  Serikali Mtandao inarahisisha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma. Usikose kuangalia kipindi hiki cha Seikali Mtandao katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) uone jinsi wanavyotumia mifumo mbalimbali ya TEHAMA katika kazi zao za kila siku.

  0 0  0 0

  Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kulia) akizungumza na viongozi wa Tanzania Media Fund (TMF) walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma kuzungumza masuala mbalimbali yahusuyo Taasisi hiyo Kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi.
  Meneja Huduma kutoka Tanzania Media Fund (TMF) Bw. Alex Kanyambo akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (hayupo pichani) wakati viongozi wa Tanzania Media Fund (TMF) walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma kuzungumza masuala mbalimbali yahusuyo Taasisi hiyo.
  Mtendaji Mkuu wa Tanzania Media Fund (TMF) Bw. Alex Kanyambo(kulia) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (hayupo pichani) wakati viongozi wa Tanzania Media Fund (TMF) walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma kuzungumza masuala mbalimbali yahusuyo Taasisi hiyo.
  Mtendaji Mkuu wa Tanzania Media Fund (TMF) Bw. Alex Kanyambo(kushoto) akijadilana jambo na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura(katikati) pamoja na Mkurugenzi Idara ya Hbabari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) wakati viongozi wa Tanzania Media Fund (TMF) walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma kuzungumza masuala mbalimbali yahusuyo Taasisi hiyo.
  Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Tanzania Media Fund (TMF) walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma wa pili kulia ni Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi.

  Picha zote na Octavian Kimario MAELEZO DODOMA 

  0 0

  Wananchi wakiwa katika dirisha la malipo katika Kituo cha Afya cha Nyamagana.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua utekelezaji wa maagizo katika Kituo cha Afya Nyamagana Jijini Mwanza
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika dirisha la malipo kukagua matumizi ya mfumo wa kielektroniki kama umefungwa katika Kituo cha Afya Nyamagana Jijini Mwanza
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua utekelezaji wa maagizo katika Kituo cha Afya Nyamagana Jijini Mwanza
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya Umiseta yaliyozinduliwa na Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu jana Jijini Mwanza.

  ……………………


  NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amempongeza Mbunge wa Nyamagana na Viongozi wote wa Wilaya ya Nyamagana kwa kutekeleza maagizo ya serikali kwa maslahi mapana ya wananchi.

  Mnamo mwezi Februari, mwaka huu Jafo alitembelea wilaya ya Nyamagana ambapo licha ya kuongea na watumishi alitembelea pia miradi ya maendeleo na kutoa maagizo mbalimbali.

  Miongoni mwa miradi hiyo ni ujenzi wa barabara za lami zinazojengwa chini ya ufadhili wa Benki ya dunia pamoja na kukagua miundombinu na utoaji wa huduma katika kituo cha afya cha Nyamagana.

  Katika ziara yake, alitoa maagizo mbalimbali ambayo alitaka yatekelezwe Kabla ya mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.

  Hata hivyo, jana baada ya kufanikisha zoezi la ufunguzi wa mashindano ya UMISETA yaliyozinduliwa rasmi na Makamu wa Rais mama Samia Suluhu Hassan, Jafo amefuatilia utekelezaji wa maagizo hayo na kukuta viongozi na watendaji wa jiji la Mwanza wametekeleza kwa kiwango cha kuridhisha.

  Katika ujenzi wa barabara ijulikanayo kwa jina la Tilapia road, Jafo amekuta barabara ya lami imekamilika na kubakia maeneo madogo sana ya kuweka taa za barabarani.

  Katika Kituo cha Afya cha Nyamagana, Naibu Waziri Jafo amekuta agizo la kuwekwa kwa mifumo ya kukusanya mapato kwa njia ya kielektroniki ukiwa umekamilika na mapato yameanza kuongezeka kutoka sh. milion 4 hadi Sh.milioni 10 kwa mwezi.

  Mbali na hilo, pia amekuta wamekamilisha kutenga eneo Maalum kwa wagonjwa wa bima ambapo katika eneo hilo la bima mapato yameongezeka kutoka wastani wa Sh.milioni 6 hadi zaidi ya Sh.milioni 10 kwa mwezi.

  Kufuatia utekelezaji huo, Jafo amewapongeza viongozi wote wa Nyamagana akiwemo Mkuu wa wilaya, Mbunge, madiwani pamoja na timu ya watendaji wa jiji la Mwanza huku akiwataka

  watendaji hao kuchapa kazi ili kuleta maendeleo kwa wananchi.

  0 0
  0 0
  0 0

  Wananchi wa Manispaa ya Iringa, Mkoani Iringa wamejitokeza kwa wingi kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa, baada ya zoezi hilo kumalizika katika Wilaya ya Mufindi iliyokuwa na Kata 36 na kuanza rasmi Manispaa ya Iringa. 

  Katibu Tawala wa Manispaa ya Iringa ndugu Joseph Chitinka amefanya ziara kukagua maendeleo ya zoezi hilo na kushuhudia mamia ya wananchi waliofurika katika vituo vya Usajili wakijaza fomu za maombi ya Usajili pamoja na kuchukuliwa Picha, alama za vidole na saini ya Kielektroniki. 

  Amesema kama viongozi wamefarijika sana kwa namna wananchi walivyojitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo. 

  “ Sisi kama Manispaa tumefarijika sana kwa namna wananchi walivyotuunga mkono kwenye zoezi hili kwa kujitokeza kwa wingi na kuacha shughuli zao kuja kusajiliwa. Hii inaonyesha ni kwa namna gani wananchi wanatambua umuhimu mkubwa wa zoezi hili” alisisitiza. 

  Zoezi la Usajili na Utambuzi katika Manispaa ya Iringa limeanza rasmi tangu tarehe 08 Juni 2017 kwa wananchi wa Kata za Kitwiru, Ruaha , Igumbilo, Mshindo, Kitanzini, Mivinjeni na Mlandege. Zoezi la Usajili katika Manispaa ya Iringa limepangwa kumalizika tarehe 30 Juni 2017 kabla ya kuanza Usajili katika Halmashauri ya Iringa. 

  Mpango wa usajili katika Manispaa hiyo umepangwa kwa Kata ambapo kila Kata imepangiwa kati ya siku tatu hadi tano za Usajili kutegemeana na idadi ya Watu. 
   Wananchi wa Mtaa wa Kibwabwa A na B Manispaa ya Iringa wakiendelea na hatua za kujaza fomu za Maombi ya Vitambulisho vya Taifa, wakati Usajili wa Vitambulisho cha Taifa ukiendelea katika Manispaa hiyo. Wananchi mbali na kujaza fomu za maombi papo hapo wanapigwa picha, kuchukuliwa alama za vidole na saini ya kielektroniki ili kukamilisha Usajili wao.
   Baadhi ya wananchi wa Kata ya Kitwilu wakiwa katika kituo cha Usajili wakisubiri kusajiliwa wakati wa zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa.
   Mtendeji wa Kata ya Kitwilu Ndg. Simba Mansul Nyunza akitoa maelezo ya namna zoezi la Usajili linavyoendeshwa katika Kata yake wakati wa ziara ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa Ndg. Joseph Chitinka.
   Watumishi wa NIDA wakiendelea na zoezi
   Mtendeji wa Kata ya Kitwilu Ndg. Simba Mansul Nyunza akitoa maelezo ya namna zoezi la Usajili linavyoendeshwa katika Kata yake wakati wa ziara ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa Ndg. Joseph Chitinka. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akisalimiana na Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Kilimanjaro alipofika nyumbani kwa Marehemu Dkt Philemoni Ndesamburo kutoa pole kwa familia.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akisalimiana na mtoto wa Marehemu Dkt Philemoni Ndesamburo Bw. Sindato Ndesamburo alipotembelea nyumbani kwa marehemu kutoa pole kwa familia.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akitia saini katika kitabu cha waombolezaji mara baada ya kufika nyumbani kwa Marehemu Dkt Ndesamburo kutoa salamu za pole kwa familia.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro  Mhe. Anna Mghwira akizungumza jambo na mjane wa Marehemu Dkt Ndesamburo  Mama Ndehorio Ndesamburo alipofika nyumbani kutoa salamu za pole kwa familia. Picha na Daily News blog.

  0 0


  0 0

  Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo 

  RAIS mstaafu wa awamu ya Nne ambae pia ni mkulima wa tunda la mnanasi ,dk.Jakaya Kikwete,amewataka wamiliki wa viwanda vya matunda kuacha kuwakandamiza wakulima kwa kununua matunda kwa gharama ya chini .

  Amesema viwanda hivyo vinasaidia kupatikana kwa masoko ya ndani lakini vimekuwa havina uwiano wa gharama zinazolingana na maumivu anayoyapata mkulima.Aidha dk. Kikwete ameeleza kumekuwa na changamoto ya kushuka kwa soko kwa wakati mwingine hali inayokuwa ikisababisha wakulima kupata hasara kwa matunda kuoza yakiwa mashambani .

  Akitoa taarifa ya shamba lake la mananasi lililipo Bago-Kiwangwa wilayani Bagamoyo ,wakati Mwenge wa Uhuru ulipokwenda kutembelea shamba hilo ,alisema kilimo cha matunda kina tija endapo utalima kisasa na kuwa na soko la uhakika .

  Kikwete alieleza ,viwanda vya usindikaji matunda mbalimbali ,vinapaswa kumjali mkulima ambae amekuwa akipata shida na kutumia gharama kubwa kuandaa shamba .“Wakati utafika watakosa matunda ,kutokana na gharama yao hailipi ,wakulima wa matunda tushindwa kukubali kuuza kwa bei ya chini ambayo hailipi ” alifafanua .
  Rais mstaafu wa awamu ya nne dk .Jakaya Kikwete akishika Mwenge wa Uhuru uliopita kutembelea shamba lake la mananasi lililopo Bago -Kiwangwa Bagamoyo .(Picha na Mwamvua Mwiny.
  Rais mstaafu wa awamu ya nne dk .Jakaya Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakikimbiza Mwenge wa Uhuru uliopita kutembelea shamba lake la mananasi lililopo Bago -Kiwangwa Bagamoyo .
   
  Kongozi wa mbio za mwenge kitaifa Amor Hamad ,akizungumza baada ya kupata taarifa ya ujenzi ,wa kiwanda cha kusindika matunda cha sayona kilichopo Mboga – Msoga Chalinze ,kutoka kwa afisa uhusiano wa kampuni mama ya MMI ,Abubakar Mlawa.


  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oriflame Afrika Mashariki, Piyush Chandra akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kusheherekea miaka 50 ya kampuni hiyo katika utoaji huduma na uuzaji wa bidhaa za vipodozi Duniani. Wapili kushoto ni Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Katarina Rangnitt, Mtaalamu wa masuala ya siasa na biashara kutoka ubalozini, Ludvig Bontell na Meneja Masoko wa Oriflame Afrika Mashariki, Mary Riungu.

   Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Katarina Rangnitt (wapili kushoto) akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kutimiza miaka 50 ya kampuni hiyo katika utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa za vipodozi Duniani. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oriflame Afrika Mashariki, Piyush Chandra,Mtaalamu wa masuala ya siasa na biashara kutoka ubalozini, Ludvig Bontell na Meneja Masoko wa Oriflame Afrika Mashariki, Mary Riungu. 

   Meneja Masoko wa Oriflame Afrika Mashariki, Mary Riungu jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kutimiza miaka 50 ya kampuni hiyo katika utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa za vipodozi Duniani. Wapili Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oriflame Afrika Mashariki, Piyush Chandra, Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Katarina. 
   Balozi wa bidhaa za Oriflame Tanzania, Missie Popular akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya kutambulishwa na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo katika nchi za Afrika Mashariki, Mary Riungu wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa za vipodozi Duniani.


  Baadhi ya wadau waliohudhuria katika maadhimisho ya miaka 50 ya utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa za Oriflame, wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na viongozi wakuu wa Kampuni hiyo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 
  PICHA ZOTE NA VENANCE NESTORY

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

   katika viwanja vya Airwing Ukonga Dar es salaam kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni kuzipata timu nne zitakazoingia nane bora.
  Mratibu wa Mashindano hayo Basilisa Basike amesema kuwa  kutakuwa na mechi nne zitakazochezwa kesho kuanzia saa 2 asubuhi na mechi zingine zitakuwa wikiendi ijayo ili kuzipata timu zingine zitakazoingia katika hatua ya nane bora.
  Wikiendi iliyopita, mashindano hayo yalianza kwa timu 52 kuumana katika viwanja vya JMK Park na kupatikana kwa timu 18 ikiwa ni hatua ya pili.


  0 0

  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

  Kampuni ya uuzaji wa vifaa vya Michezo ya ,Speshoz Tanzania imeingia mkataba wa kutoa vifaa vya Michezo  kwa timu ya Soka ya Lipuli ya Iringa ambayo imepanda kucheza ligi kuu ya Vodacom Tanzania.

  Akizungumza wakati wa kusaini mkataba wa timu hiyo mkurugenzi wa Speshoz Tanzania,Jeffrey Jessey amesema mkataba huo ambao ni wa zaidi ya Milioni 30 utawawezesha kuuza jezi za Lipuli na kuwagawia vifaa vyote vya mazoezi.

  “mkataba huu utaweza kuisadia timu hii kuwa na vifaa vya uhakika na vya kisasa ambavyo vitasaidia timu hiyo kuwa na morali na kuhimili ushindani na timu mkubwa” Amesema Jessey.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa timu ya Lipuli, Abu Changawa amesema kuwa mkataba huo ni moja ya vitu ambavyo vitasaidia timu hiyo kuwa na vifaa vya uhakika.

  Amesema kuwa kampuni hiyo imewapa masharti kuwa timu hiyo ikifanikiwa kubaki sita bora basi wataongeza udhamini katika msimu ujao.

  Changawa amesema  ni vyema makampuni mengine yakajitokeza kusaidia timu hiyo kwa upande wa udhamini hili iweze kufanya vizuri. 
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Speshoz Tanzania Jeffrey Jessey akizungumza na Waandishi wa habari juu ya Mkataba wake na timu ya soka ya Lipuli ya Mkoani Iringa

   Mkurugenzi wa Kampuni ya Speshoz Tanzania ,Jeffrey Jessey  na  Mwenyekiti wa Lipuli Abu Changawa  wakisaini Mkataba wa Vifaa vya Michezo
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Speshoz Tanzania ,Jeffrey Jessey  na  Mwenyekiti wa Lipuli Abu Changawa  wakipeana mikono baada ya kusaini Mkataba wa Vifaa vya Michezo


older | 1 | .... | 1738 | 1739 | (Page 1740) | 1741 | 1742 | .... | 3284 | newer