Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1736 | 1737 | (Page 1738) | 1739 | 1740 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanza usajili wa wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu, Wilayani Kasulu, mkoa wa Kigoma kwa lengo la kuwapatia watumishi wote vitambulisho.
   Watumishi wa NIDA wakisajili wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu walayani Kasulu mkoani Kigoma leo
  Watumishi wa NIDA wakiwapanga tayari kwa usajili wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu walayani Kasulu mkoani Kigoma leo

  0 0

  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika MasharikI, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akimsikiliza Afisa Mkuu wa Uhusiano wa Sekrearieti ya Jumuiya ya Afrika Mshariki, Bw. Otrhieno Richard Owora (kushoto). Katika mazungumzo hayo, wawili hao walizungumzia maandalizi ya uzinduzi wa mashindano ya kubuni nembo mpya ya EAC yatakayowahusisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vilivyopo kwenye nchi wanachama wa Jumuiya hiyo. Uzinduzi huo utafanyika kwenye Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam tarehe 09 Juni 2017. 
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kushoto), pamoja na Maafisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, wa kwanza kulia ni Bw. Ally Kondo pamoja na Robi Bwiru wakinukuu mambo yaliyokuwa yakizungumzwa na Balozi Mwinyi pamoja na Bw. Owora. 
  Mazungumzo yakiendelea. 
  Balozi Mwinyi akipokea kitabu chenye mwongozo wa namna ya kushiriki mashindano hayo. 
  Picha ya pamoja.   0 0

   Balozi wa Tanzania Nchini Burundi Mheshimiwa Rajabu Hassan Gamaha anayeangalia camera akizungumza na baadhi ya wajumbe wanaoshiriki Mkutano wa 8 wa Afrika Mashariki wa Sekta ya Petroli kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambao walifika katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania jijini Bujumbura, Burundi leo kwa mazungumzo yaliyolenga kuimarisha uhusiano mwema ulipo baina ya Burundi na Tanzania. Ujumbe huo uliongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana L. Pallangyo aliyevaa suti nyeupe.

  Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Bwana Felix Ngamlagosi akisisitiza jambo wakati akizungumza na Balozi Rajabu juu ya uhusiano wa Taasisi ya EWURA na Taasisi mpya iliyoanzishwa Nchini Burundi  yenye jukumu la Kudhibiti Nishati ya Mafuta na Maji, pembeni yake ni Mkurugenzi Msaidizi Miundombinu ya Kiuchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhandisi Abdillah Mataka.

  Balozi Rajabu na Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Mazungumzo hayo.

  0 0

  Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru , Amour Hamad Amour amewaasa watendaji mbalimbali nchini kuwajali vijana kwa kuwapa fursa mbalimbali pale inapotokea.

  Kiongozi huyo ameyasema leo wakati wa Mwenge wa Uhuru ulipopita katika mradi wa kituo cha watu walioathirika na Dawa za Kulevya Sober House Kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani,

  Amesema kuwa vijana ndio wamekuwa waathirika wakubwa katika matumizi ya dawa za kulevya ambao ndio nguvu kazi ya taifa.

  Nae Mkurugenzi Kituo hicho, Al –Karim Bhanji amesema vijana walioathirika na dawa za kulevya wanatakiwa kupewa upendo,kuwaacha kunaweza kukasababisha kurudi katika matumizi ya dawa za kulevya.

  Bhanji amesema malengo ya kituo hicho ni kuwa na walimu ambao watakuwa wanawafundisha waathirika hao ili kurudi kuendesha biashara zao kutokana na elimu itakayotolewa na kituo hicho.

  Amesema kuwa kutokana na kukua kwa sayansi na Teknolojia kituo kituo kitaanzisha darasa la kompyuta, ambapo waathirika watajifunza na wengine wanaweza kuwa na ujuzi tofauti.

  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Madjid Mwanga amesema kuwa Mwenge umetoa hamasa kubwa na kupelekea kufungua miradi mbalimbali ,ambapo Sober House ni mradi ambao umeokoa vijana wengi waliotumbukia kwenye matumizi ya dawa za Kulevya.
  Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru , Amour Hamad Amour (aliesimama) akizungumza na katika kituo cha Sober House wakati mwenge huo ulivyopita katika kituo hicho leo Bagamoyo mkoani Pwani.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Madjid Mwanga (aliesimama) akizungumza wakati wa Mwenge wa Uhuru ulivyopita katika kituo hicho leo Bagamoyo mkoani Pwani.
  Mkurugenzi wa Kituo cha Sober House , Al –Karim Bhanji (katikati)akizungumza jinsi wanavyoendesha kituo hicho wakati mwenge huo ulivyopita katika kituo hicho leo Bagamoyo mkoani Pwani.kushoto ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2017, Amour Hamd na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Madjid Mwanga
  Mkurugenzi wa kituo hicho,Al –Karim Bhanji (katikati) akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru
  Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2017, Amour Hamd Amour akiwaaga viongozi na Watendaji wa Kituo hicho.
  Mwenge wa Uhuru


  0 0

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  ZAIDI ya wawakilishi 250 wa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu kutoka jijini Dar es Salaam wamejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia mpango wake wa uchangiaji wa hiari (PSS), baada ya kushiriki semina ya siku moja makao makuu ya Mfuko jijini Dar es Salaam Juni 8, 2017.

  Wanafunzi hao kutoka taasisi 20 za elimu ya juu, wamehudhuria semina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na PSPF kwa uratibu wa Taasisi ya Elimu ya Vyuo Vikuu Tanzania, (TAHILISO), ili kuwapatia elimu wanafunzi hao kuhusu shughuli za Mfuo na faida azipatazo mwanachama ikiwemo mafao mbalimbali.

  Kabla ya zoezi hilo la kujiunga na Mfuko, awali Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bi. Costantina Martin, aliwaasa wanafunzi hao kujijengea utamaduni wa kuweka akiba kwani manufaa yake huonekana katika kipindi kifupi.

  “Mimi nina mototo yuko chuo kikuu huwa ninampatia fedha kidogo za kujikimu lakini namueleza aweke akiba, ningependa kuwahamasisha vijana mjenge utamaduni wa kujiwekea akiba kidogo kidogo,zile posho mnazopata, na fedha kutoka kwa wazazi wenu, mnaweza kutenga sehemu ya fedha hizo na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima ili kujiwekea akiba.” Alsoema Bi. Costantina Martin, wakati akifungua semina hiyo.
  Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Neema Lowassa,(wapili kulia), na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali za wanavyuo wa elimu ya juu mkoa wa Dar es Salaam, wakionyesha vipeperushi vyenye melezo ya Mfuko huo, baada ya semina ya siku moja iliyoandaliwa na PSPF kuelimisha wanafunzi shughuli mbalimbali za Mfuko na fursa zilizopo. Semina hiyo imefanyika leo Juni 8, 2017.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bi. Costantina Martn, akifungua semina hiyo leo Juni 8, 2017
  Mwenyekiti wa TAHILISO, Bw.Stanslaus Peter Kadugalize,(aliyesimama), akifafanua baadhi ya mambo mwishoni mwa semina hiyo. Wengine kutoka kushoto, ni Katibu Mkuu wa TAHILISO, Bi. Zuhura A. Rashid, Afisa Mfawidhi wa PSPF mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Neema Lowassa, na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi.
  Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, akizunguzma na baadhi ya viongozi wa wanafunzi wa elimu ya juu, walipotembelea kuona jinsi utunzaji taarifa za wanachama wa Mfuko zinavyohifadhiwa. Hii ilikuwa ni sehemu ya semina waliyopewa viongozi hao na maafsia wa PSPF jijini Juni 8, 2017


  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akiagana na BALOZI WA Umoja wa Ulaya nchini mhe. Van De Geer Roeland baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na timu yake. Mazungumzo hayo yamefanyika ofisini kwa Katibu Mkuu Prof Mchome mjini Dodoma. Katika kikao hicho suala la upatikanaji wa haki kwa watu wote nchini hususan watu wasio na uwezo lilijadiliwa ikiwa ni pamoja na kuimarisha na kuboresha mahusiano mazuri baina ya Wizara na Umoja wa Ulaya.

  0 0

   Beki wa Yanga, Juma Abdul, (kulia) akiruka kuwania mpira na beki wa AFC Leopards Abwao Marcus, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo. Katika mchezo huo AFC Leopards wameibuka na uwashinda wa mikwaju ya penati 4-2 baada ya kumalizika dakika 90 kwa sare ya 0-0.
   Mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi (kulia) akiwania mpira na Kiungo wa AFC Leopards, Alan Katerega, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
   Mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi (kulia) akimtoka mpira na beki wa AFC Leopards, Abdallah Salim, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
   Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa, akijiandaa kupiga shuti huku akizongwa na mabeki wa AFC Leopards, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
   Mshambuliaji wa Yanga Yusuph Mhilu (kushoto) akimtoka beki wa AFC Leopards, Abwao Marcus, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam

  0 0


  0 0
  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wauguzi na Wakunga la Zanzibar walipofika Ikulu Mjini Zanzibar.
  Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wauguzi na Wakunga la Zanzibar walipokuwa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipozungumza nao leo walipofika Ikulu Mjini Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wauguzi na Wakunga la Zanzibar pamoja na Viongozi wengine baada ya mazungumzo yalitofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar. Picha na Ikulu

  0 0

   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo akiwasili ukumbini kuendesha kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Misenyi, Mabalozi, viongozi wa Jumuia za CCM na watendaji wa Serikali katika Wilaya hiyo mkoani Kagera.
   Wajumbe wakihamasika kwenye kikao hicho
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na wajumbe wakati wa kikao hicho.


  0 0

   Kaimu Hakimu Mkazi-Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi-Njombe, Mhe. Paul Kapokolo akiwa ofisini kwake mkoani Njombe, Mhe. Kapokolo ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Wilaya Njombe amesema Mahakama mkoani Njombe imejiwekea mikakati ya kushughulikia mashauri kwa wakati ikiwa ni pamoja na kufanya vikao vya kusukuma mashauri (case flow management) ili kupata ufumbuzi kwa mashauri yanayoonekana kukwama, kuhimiza Waendesha Mashitaka/Polisi kuleta mashahidi kwa kila tarehe wanayopangiwa kusikiliza mashauri n.k
   Mtendaji, Mahakama ya Hakimu Mkazi-Njombe, Bi. Maria Francis Itala, Bi. Itala alisema kuwa Mahakama mkoani Njombe wanakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa Watumishi wa Kada mbalimbali, alisema kwa sasa Mkoa huo una jumla ya Watumishi 78 na uhitaji wa Watumishi ili kutekeleza Majukumu tofauti tofauti ni 359, na hivyo kufanya kuwa na upungufu wa Watumishi 28.
   Mhe. Isaya, wa kwanza kulia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Mwanzo-Kalenga, wa kwanza kushoto ni Hakimu Mkazi Mfawidhi-Mahakama ya Mwanzo-Kalenga, Mhe. Magdalena Malaba.

  Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Wilaya-Iringa, Mhe. Isaya Godfrey akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Kalenga mara baada ya kukamilisha shughuli ya ukaguzi iliyompeleka katika Mahakama hiyo. (Picha na Mary Gwera, Mahakama)
  0 0


  0 0
  0 0
 • 06/09/17--03:00: Article 0


 • 0 0

  · Waunga mkono kampeini ya kitaifa ya usafi wa mazingira

  Mashirika ya kimataifa yanayounga mkono juhudi za serikali kuwezesha upatikanaji wa maji safi na salama leo kwa pamoja yameunga mkono kampeni ya kitaifa ya usafi ijulikanayo kama Niko Tayari inayoendeshwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

  Mashirika hayo ni UNICEF (Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto), Benki ya Dunia, Shirika la misaada la Uingereza (DFID), Shirika la Miradi la Ujerumani (GIZ) na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA). Wawakilishi wa mashirika hayo walikutana kwenye ukumbi wa mikutano, Ubungo Maji, jijini Dar es salaam leo.

  Mashirika hayo ya maendeleo yamekubali kuunga mkono kampeini hiyo ilizinduliwa mwezi uliopita mjini Dodoma ikiwa na lengo la kuhamisha usafi wa mazingira kwa kila Mtanzania hasa kuwa na choo katika kila familia na kujenga utamaduni wa kunawa mikono baada ya matumizi yake. Kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza vifo hivyo kusaidia ukuaji wa uchumi nchini.

  Akiongea na waandishi wa habari, Mratibu wa kampeini ya Nipo Tayari Anyitike Mwakitalima kutoka Wizara ya Afya alisema ili kuwa na huduma bora ya maji, usafi wa mazingira ni muhimu kuzingatiwa. ‘Kwa kujitokeza wadau wetu wa Maendeleo na kuunga mkono kampeini yetu ni kitu cha kupogezwa sana na pia niishara kwamba malengo yetu ya kuwa na mazingira salama yatafanikwa’, alisema Mwakitalima. 

  Zaidi ya mashirika 10 ya maendeleo ya kimataifa yamejitokeza kuunga mkono kampeini hiyo inayojumuisha mikoa yote Tanzania Bara.

  Kampeini hiyo ya usafi wa mazingira na matumizi bora ya choo (NikoTayari) inatarajiwa kuwa chachu ya upatikanaji wa maji safi na salama na kuboresha afya za Watanzania wote, mijini na vijijini.   Afisa Afya Mkoa wa Pwani Emmanuel Mwandepa akitoa ishara ya Nipo Tayari kuunga mkono kampeni ya taifa ya usafi wa mazingira wakati wa mkutano wa wadau wa maji uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo iko chini ya Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii ikiwa na lengo la kuhamasisha usafi wa mazingira na matumizi ya choo bora.


  Mwakilishi wa TAMISEMI, Idara ya Afya, Mwajina Lipina akitoa ishara ya Nipo Tayari kuunga mkono kampeini ya Taifa ya usafi wa mazingira wakati wa mkutano wa wadau wa maji uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo iko chini ya Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii ikiwa na lengo la kuhamasisha usafi wa mazingira na matumizi ya choo bora.

  Mratibu wa huduma ya maji na usafi wa mazingira shule kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Technolojia Theresia Kuiwipe akitoa ishara ya Nipo Tayari kuunga mkono kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira wakati wa mkutano wa wadau wa maji uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo iko chini ya Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii ikiwa na lengo la kuhamasisha usafi wa mazingira na matumizi ya choo bora. 

  0 0

  Na Frank Mvungi-Maelezo

  Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imetoa mafunzo kwa wasindikaji wadogo wa vyakula 1287 tangu mwaka 2013 ili waweze kusindika vyaklula vyenye ubora kwa mujibu wa sheria na kanuni za uzalishaji na kuhimili ushindani wa soko.

  Akifungua mafunzo ya wasindikaji wadogo wapatao 60 wa vyakula yaliyoratibiwa na Mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Hiiti Sillo, Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula Bw. Raymond Wigenge, amesema dhamira ya Serikali ni kuwawezesha wajasiriamali wadogo hapa nchini.

  “Kukua kwa viwanda hivi kutakuwa na mchango mkubwa katika kuongeza ajira na kipato katika ngazi ya kaya, kukuza kilimo cha mazao ya chakula kutokana na kuwepo kwa soko la mazao ya vyakula”. Alisisitiza Wigenge.

  Akifafanua Wigenge amesema Serikali inatambua kuwa viwanda vidogo vina nafasi kubwa ya kuchangia pato la Taifa hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali inasisitiza ujenzi wa uchumi wa Viwanda.

  Alieleza kuwa Mamlaka hiyo imeingia mkataba wa maridhiano (MOU) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambapo mchango wa taasisi hizo mbili utatambuliwa katika tasnia ya ujasiriamali wa bidhaa zinazodhibitiwa na Mamlaka.

  Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Raymond Wigenge akifungua mafunzo ya wasindikaji wadogo wa vyakula (hawapo pichani) ambayo yaliatibiwa na Mamlaka hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
  Meneja wa Ukaguzi na Ufuatiliaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Justin Makisi akitoa ufafanuzi kuhusu umuhimu wa mafunzo kwa wasindikaji wadogo wa vyakula.
  Mwenyekiti wa Chama cha Kuweka na Kukopa Wajasiriamali Wadogo Tanzania (TASWE) na muwakilishi wa wanawake wajasiriamali Bi. Anna Matinde akipongeza juhudi za Serikali katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo hapa nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa Mamlaka hiyo Bw. Raymond Wigenge na kushoto ni Afisa Udhibiti Ubora Bi. Prisca Kuela
  Baadhi ya wajasiriamali wakifuatilia mafunzo yaliyoratibiwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini (TFDA) kwa wasindikaji wadogo wa vyakula .
  Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Raymond Wigenge akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Hiiti Sillo wakati wa mafunzo ya wasindikaji wadogo wa vyakula.(Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo)

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akizungumza na baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi alipotembelea ofisi za chama hicho kujitamburisha .kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro Idd Juma ,na anayefuatia ni Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi,Aisha Amour.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akitia saini katika kitabu cha waombolezaji mara baada ya kufika nyumbani kwa Marehemu Dkt Ndesamburo kutoa salamu za pole kwa familia.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna mngwira akizungumza jambo na mjane wa Marehemu Dkt Ndesamburo ,Ndehorio Ndesamburo alipofika nyumbani kutoa salamu za pole kwa familia.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,akitembelea kaburi ulipolazwa mwili wa marehemu Dkt Philemoni Ndesamburo alipofika nyumbani kutoa salamu za pole kwa familia.


  0 0  Katika kutekeleza Sera ya Diplomasia ya Uchumi, Ubalozi wa Tanzania kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uholanzi uliopo Tanzania, Wizara ya Masuala ya Uchumi na Wizara ya Mambo ya Nje za Uholanzi na Taasisi ya Netherlands–African Business Council (NABC)kwa pamoja ziliandaa Kongamano la Biashara na Uwekezaji lililofanyika hapa The Hague, Uholanzi tarehe 31 Mei 2017. 

  Lengo kuu la Kongamamo hilo, pamoja na kuendeleza na kukuza uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Uholanzi, nikutangaza fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji zilizopo nchini Tanzania hususan katika Sekta za Kilimo, Ufugaji, Uvuvi na Miundombinu ya Kilimo. 

  Aidha, Kongamano hilo lililohudhuriwa na Wawakilishi wa Makampuni takriban mia moja (100) ni mwendelezo wa utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kwenye Mkataba kati ya Tanzania na Uholanzi kuhusu Uingizwaji wa Mbegu za Viazi kutoka Uholanzi uliosainiwa kwenye ziara ya Mhe. Martijn Van Dam, Waziri wa Kilimo wa Uholanzi nchini Tanzania tarehe 16 Juni 2016. 

  Aidha, Kongamano hii lilitanguliwa na ziara ya ujumbe kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo mashamba yanayomilikiwa na wakulima na wafugaji binafsi nchini Tanzania pamoja na kupata fursa za kusikiliza mada mbalimbali zilizotolewa na wakulima/wafugaji na wakufunzi wa Chuo Kikuu cha Wageningen kinachohusika na kufanya tafiti za Kilimo na Ufugaji.

  Ujumbe kutoka Tanzania uliongozwa na Mhe.Eng. Mathew Mtigumwe, Katibu Mkuu anayeshughulikia Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi, akimwakilisha Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

  Uwekaji saini wa makubaliano (letter of intent) ya kuanzishwa kwa kituo cha kuendeleza zao la viazi Tanzania .
  Picha ya Pamoja ya Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania na Uhoalnzi na Makatibu Wakuu wa Kilimo na Uvuvi na Mkurugenzi wa TAHA. 

  0 0


  NA TIGANYA VINCENT,TABORA.

  SERIKALI ya mkoa wa Tabora imesema haitasita kuchukua hatua za kisheria kwa mtu yoyote atakayebainika kuendesha vitendo vya uharibifu wa ardhioevu kwa kuendesha shughuli za kibinadamu kama kilimo, ufugaji mifugo, uchomaji mkaa na uchomaji moto hovyo kwenye vyanzo vya maji na hifadhi za misitu.

  Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri mara baada ya kushiriki kampeni ya upandaji na umwagiliaji wa miti ambalo ziliendeshwa na vijana 600 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Msange ambao wametekeleza agizo la Makamu wa Rais kwa vitendo .

  Alisema kuwa viongozi wote wanatakiwa kushirikiana na wananchi katika kuwabaini wote wanaoendesha shughuli hizo ovu katika mistu mkoani hapo kwa kuwa wanahatarisha wakazi wa Tabora na mikoa jirani.

  Mkuu huyo wa Mkoa aliwashukuru vijana hao wa JKT waliomba kushiriki katika zoezi la kupanda miti kabla ya kumaliza mafunzo yao Jumamosi ili iwe alama ya uwepo wao katika eneo hilo.

  Alisema kuwa kitendo walichoufanyia vijana hao kimeonyesha jinsi walifundishwa vizuri juu ya kuwa wazalendo kwa Taifa lao na kitabaki katika kumbukumbu za Mkoa huo na majina yao yataandikwa.


  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri akizungumza na waandishi wa habari jana kabla ya kuanza zoezi la kuondoa magugu katika miti iliyopandwa katika Manispaa ya Tabora juzi.
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri akishirikiana na askari wa Kujenga Taifa(JKT) Msange wanaohitimu mafunzo yao Jumamosi wakati wa zoezi la kuondoa magugu katika miti iliyopandwa katika Manispaa ya Tabora juzi.Picha na Tiganya Vincent-RS -Tabora

older | 1 | .... | 1736 | 1737 | (Page 1738) | 1739 | 1740 | .... | 3278 | newer